ibra87
R I P
- Jul 22, 2015
- 5,614
- 5,360
- Thread starter
- #601
******NITAKUFA NA WEWE*******
*******SEHEMU YA 080*******
Wakati Akielekea barabarani ili kuangalia usafiri wa kumpeleka bunju.. Akashtuliwa na msururu wa magari yakija na usawa ule aliyosimama Yeye... Kabla hajajua kipi akifanye akashangazwa na Mtindo wa kikomando kutoka kwa Askari wale. Walikuwa wakishuka katika aina fulani ambayo ungekuwa mtu wa kitengo ungefurahi Kuutazama ule mtindo. Kila askari Aliyekuwa Akishuka Ndani ya Gari alikuwa Akichupa katika aina fulani na hata walipokuwa wakitua chini walikuwa wakiruka tena katika aina fulani ambayo ilimuweka Jenifer katika Woga, woga ambao hakuutarajia kumjia katika Hali ile.. Makomandoo wale wenye kofia Nyekundu huku wakiwa na Alama ya Bawa kwenye mavazi Yao walimtisha kwa Mara ya kwanza na kumfanya atamani kujisalimisha, lakini kila alipokumbuka vifo vya Wazazi Wake alipuuza mpango wa kujisalimisha. Chuki ikaongezeka na Nguvu kumjia kwa nguvu upya... Mkono wake uliokuwa Ukivuja damu Haukumzuia Kufanya kitu kibaya kwa Makomandoo wale... Akaupeleka mkono wake katika kiuno chake alipomuhifadhi mwanawe, mwanawe ambaye alipenda kumtumia katika mikasa mizito kama Huu... Akaishika bastola Sawa sawia katika Mikono yake..... Kisha akaanza kukimbia kuelekea kwenye mashimo ya michanga huku masikio yake yakiwa yananusa kila Aina ya Michakato Hata kama ni ya wadudu...
Alijua maisha yake yapo mikononi mwake hivyo alikuwa makini katika kuruhusu mtu kumuona au kumgundua... Akaendelea kukimbia huku wakati mwingine akilazimika kutambaa kwa kwa tumbo yote ikiwa ni Kukwepa kuingia mikononi kwa Wanajeshi wale na Makachero Wengine. Akiwa amebakisha hatua kama tatu Kukifikia kibarabara ambacho kilikuwa kikitumiwa na Wakazi wa maeneo ya Ununio... Mara Akasikia Mngurumo Wa Pikipiki.. Mngurumo Ambao haukuchukua Muda ukanyamaza,.. Wakati Akiwa Ametulia kusikiliza kile kitakachotokea pale, mara Akasikia Mazungumzo Ya Kunong'ona... Akajiinua taratibu na kunyata mpaka karibu na iliposimama Ile Pikipiki ambapo aliendelea kuwasikiliza Watu wale waliokuwa wakiongea kwa kunong'ona. Sasa akawafikia karibu, ni ukaribu Huo Uliyomfanya akipeleke kidole chake kwenye kitufe cha kuruhusu risasi... Bastola Ikakohoa mara mbili... Risasi kutoka kwenye Bastola Zikaifanya kazi ambayo Zilitumwa. Miili ya Watu wawili akatambarajika Chini katika namna fulani Ilitia Raha kuitazama... Akasogea katika namna ya kipekee huku bastola Akiwa imetazama mbele katika kumziba mdomo Yoyote Ambaye Angeleta Fyoko fyoko......
Akaifikia Ile miili ya Watu Wale, akashangaa kukutana na Miili ya watu wawili ambao mmoja alikuwa mwanamke na mwingine mwanaume... Wote walikuwa wamelaliana wakiwa katikati ya dimbwi la damu... Akaumia sana katika Maisha Yake hakupenda kuua watu wasio na hatia lakini hutokea kufanya Hivyo kwa kutaka ama kuokoa maisha yake au kupoteza Ushahidi..
Hakutaka kuupoteza Muda, Alichokifanya ni Kuiendea ile pikipiki na kupanda kisha kuiondoa Eneo lile katika Mwendo wa Kasi Sana... Ni mwendo na Mngurumo wa Pikipiki ile Kuliko wagutusha makomandoo na Maofisa usalama waliokuwa wamezagaa Katika Eneo lote la Mbweni Jkt.... Mpaka Wanaifikia Sehemu ulipoanzia Mngurumo wa pikipiki... Jenifer Alikuwa Hayupo pale na Alikuwa Tayari Ameshafika mbali...
Wakabaki wakiitazama Miili ya Watu wale wawili Waliolala katika Dimbwi la Damu Huku Vichwa vyao vikiwa vimefumuliwa kwa risasi....
Wote wakaangaliana na Kutikisa Kichwa, Walikuwa wameachwa kwa Mara Nyingine na Jenifer.. Ilikuwa Dharau Kubwa kwa Makomandoo wale... Sasa Wakaamua Kulichukua wao lile Jukumu la Kumsaka Jenifer... Iwe mchana au Usiku, asubuhi au Jioni mpaka pale atakapopatikana.... Wanaume Wakakoki Silaha zao wakaingia Kazini Huku wakisema Ama Zake Ama Zetu.....
UKIITAKA HII UTAIPATA KWA BEI YA 5000 KUPITIA WHATSAP NA KWINGINEKO