Riwaya: Nitakupata tu

Riwaya: Nitakupata tu

NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 060

Alikuwa Masimba katikati ya watu wale. Watu ambao walikuwa wakiwachunguza na kuwafuatilia. Wakati akilifikiria hilo akaliona jingine likitokea katika uharaka ambao hakuutarajia na kuutegemea. Watu waliokuwa wameongozana na masimba wakikimbia kwa pamoja sekunde mbili nyuma, sekunde hii walikuwa wakianguka chini katika namna ya kushangaza. Matundu mawili kwenye miili ya watu wawili ilitosha kubwambia na kumjulisha mwanadada yule kuwa hapakuwa na uhai katika miili iliyotambalajika pale chini. Miili ya hawa watu wawili waliokuwa katika uchunguzi. Hata pale Masimba alipogeuka na kumwangalia mwanamke yule kisha kutabasamu, mwanadada yule ndio kwanza alikuwa akigundua kuwa masimba alikuwa amewagundua hila zao katika kuwafuatilia watu hawa. Akaruhusu macho yake yamtizama masimba alivyokuwa akitembea katika aina imvutiayo, Akahisi labda Alikuwa akimtizama Willy Gamba. Akaliacha hilo lipite katika aina ya kuuburudisha moyo na hata moyo wake. Alikiwa akimtizama masimba kanakwamba alikuwa akilitizama tunda tamu kutoka juu ya mti mbichi. Hakujua ni saa ngapi alifika sehemu ya tukio. Mbele ya macho yake mwili wa mtoto mzuri ulikuwa umelala chini ya mchanga damu zikichuruzika. Amanda, Abby na Queen walikuwa wakilia pasipo mpangilio. Masimba alikuwa chini ya mwili wa Vicky wakati wanausalama wengine walikuwa wamemkinga kwa kumuweka katikati. Macho yao yakitizama Huku na Huko. Vicky hakuwa akipumua tena, alikuwa ametulia Juu Ya mchanga akiwa tayari ni Marehemu. Hilo lilionekana kama ndoto kichwani kwa Masimba. Ndoto ambayo asingependa kuiota katika maisha yake. Ni vipi atamwambia Teddy kuhusu hili? Huo ulikuwa mtihani mkubwa sana. Akainuka pale chini safari akiwaendea watoto wale waliokuwa wakilia. Alipowafikia aliwakumbatia kwa pamoja kabla ya kuondoka nao huku akilindwa na Wana usalama sambamba na wanajeshi wa Jeshi la wananchi wa Tanzania kitengo cha mizinga ambao kambi yao ilipakana na ufukwe ule. Aliongozwa mpaka kwenye gari ambayo ilikuja na wanausalama wale. Akawapandisha watoto kisha naye kujipakia. Kabla ya kuondoka akamvuta mwana usalama mmoja na kuongea naye kitu. Baada ya hapo akawasha gari na kuondoka akipishana na Gari zaidi ya tano za polisi zikielekea Sehemu ya tukio. Aliendesha gari huku kichwa chake kimevurugika. Kitendo cha vicky kupigwa Risasi huku yeye yupo hapo hapo kilikuwa kitu cha aibu sana. Ni jana tu usiku alipoipata taarifa ya Vicky kupigiwa simu. Ni yeye aliyemruhusu Vicky akutane na watu hao waliompigia simu licha ya hapo mwanzo kukataa, licha ya Teddy kuukataa huo mpango , lakini Masimba alimhakikishia usalama wa Vicky kuwa kitakachotokea Atakibeba yeye. Leo hii hapa Vicky alikuwa amelala akiwa hana uhai. Atamwambia nini Teddy? Lilikuwa swali lililomkoroga na kumvuruga. Alitambua kosa lake kubwa ni kushindwa kumlinda Vicky mpaka kupelekea kuuawa. Ingawa hakujua wapi alipofeli, lakini moyoni alijikuta akimsifu muuaji aliyeifyatua Risasi na kumuua vicky. Alimsifu kwa vitu vitatu, vitu ambayo hata yeye mwenyewe alishindwa kuvitambua. Cha kwanza ni Usiri wa mtu huyu aliyemuua Vicky. Usiri wakuingia mahala pasipokuonekana. Kitu cha pili ni ufyatuaji wake wa Risasi katika kadamnasi ile. Ufyatuaji wa aina ile hufanywa na watu wataalam katika taaluma ile. Kuiruhusu risasi kumfikia mlengwa akiwa amezungukwa na umati wa watu ilionyesha mtu huyu alivyo hatari.

Kitu cha tatu niuondokaji wa mtu huyu eneo lile baada ya kufanya mauaji. Hakumuona akiondoka katika eneo lile la fukwe. Hakumuona akisimama na hata kukimbia katikati ya umati. Hilo kwa Kwake lilikuwa suala jingine, suala ambalo lilimpa uhakika kuwa kazi ile ilikuwa ngumu sana na ilifanywa na mtu mwenye utaalam wa hali ya juu. Kumuua mtu katikati ya umati kisha kuondoka katika namna ya kutokuonekana ni wazi kuwa muuaji alikuwa Jasusi wa kutupwa. Akayatoa mawazo yake huko sasa alikuwa akiwafikiria watu wale wawili ambao aliwaua. Hawa ndio watu pekee ambao aliwahisi kuwa ndio waliompigia simu Vicky.. hakutambua kuhusu uwepo wa mtu wa tatu licha ya kuwahi kwake mapema kufika sehemu ya ahadi. Damu ya vicky ilikuwa mikononi mwake, damu ya vicky ni damu ambayo ilitakiwa kulipwa kwa mikono yake. Hali ilishakuwa katika kuhitaji umakini sana. Alipofikiria taarifa hii itakapomfikia Teddy, kipi kitafuata, hakujua lakini aliuona mwisho wake katika mahusiano yao. Teddy alimpenda Sana Vicky, alimpenda kupita uwezo. Nini ambacho kitatokea Masimba atakapompa taarifa? Haikuwa Rahisi sana kuipokea hiyo. Akapiga moyo konde na kuelekea huko.

******

Alikuwa amejilaza kitandani akiisubiri kwa hamu taarifa ya kukutana kwa vicky na watu hao waliompigia simu. Muda wote alikuwa amejilaza akimuwaza mdogo wake, lakini kitu kimoja ambacho kilianza kumshangaza tokea asubuhi ni kuhusu moyo wake kupiga kila pale alipolitaja au kukumbuka ahadi ya vicky na watu hao. Alijua vicky hakuwa na ujuzi wowote katika kupambana na hata kutumia Silaha. Alijua ni rahisi sana watu kumuondoa kama wataamua. Hata pale alipomkataza kukacha wito huo, alijua mdogo wake hawezi kuwakwepa watu hao. Aliendelea kusubiri huku wasiwasi ukizidi. Hata mlango ulivyofunguliwa kisha mtu kuingia, Teddy hakuinuka bali aliinua macho na kutizama. Akajikuta akiangaliana na tukio ambalo lilimpa baridi. Alikuwa akiwatizama wadogo zake wote watatu wakiwa wanamuangalia Huku wakilia. Macho yake yakatua kwenye mavazi waliovaa. "Damu" ndio kitu alichokiona. Punde alikuwa amechupa pale kitandani akaelekea waliposimama Wadogo zake. "Sweet Yuko wapi Vicky? Aliuliza Teddy akimtingisha mdogo wake kwa nguvu.

"Samahani Mpenzi, Ujinga wangu umesababisha kumpoteza Vicky. Vicky hatupo naye tena." Ilikuwa sauti kutoka mlangoni. Sauti ambayo haikusikika vizuri masikioni kwa Teddy.

"Una Semaje Masimba? Unasemaje wewe? Namtaka vicky wangu akiwa Hai hapa. Sitakusikiliza kwa chochote." Aliongea Teddy safari hiii akiinuka kumfuata Masimba. Bastola yake mkononi akimuendea kwa shari. Machozi yalikuwa yakishuka mashavuni. "Namhitaji mdogo wangu akiwa hai.. la sivyo nitakuua au kuviua vifaranga wako wale wawili." Aliongea Teddy akionyesha kutokuwa na utani kabisa. Alikuwa akimaaanisha kile alichokuwa akisema. Masimba bado alitulia akimuangalia Kwa umakini. Sio kwamba hakuumizwa na kifo cha Vicky, sio kwamba hakuwa na maumivu juu ya kilichotokea. Alikuwa na maumivu sana moyoni. Lakini maneno ya Teddy kuwa atawaua watoto wake hakuwa amelitegemea kabisa. Awaue wanawe France na Yaseer? Kilikuwa kitu ambacho hakukitegemea. "Unataka kuwaua wanangu kwa sababu ya kilichotokea? Wanangu wanahusika nini katika hili? Niue mimi mwenyewe ili ufurahi.. waache watoto wangu. Aliongea masimba huku akiushika mkono wa Teddy ulioshika bastola na kuinua Juu usawa wa kichwa chake. "Naomba Uniue mimi, Yaseer na France naomba uniachie. Mbona wewe ulisababisha kuuawa kwaa mama lakini sikutaka kulipa kisasi? Mbona mwanangu Yasser mpaka leo yupo hospitalini kwa sababu yake, lakini sikulipa kisasi kwa hao? UNADHANI SIKUUMIA
 
Vicky amesahau kuwa yote haya yanatikea Kwa ujinga wake?
 
NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 061

Wewe Mbona umesababisha kifo cha mama yangu, uliona nikienda kulipa kisasi? Mwanangu Yasser mpaka leo yupo hospitalini sababu yako, uliniona nikienda kuwagusa Amanda na Abby? Au kuna siku umeniona nimemgusa sweet na hata patra? Unadhani mimi siumii? Unadhani sijaumia kumfukia mama kwa upuuzi wako? Ningetaka kukuua mpaka sasa ungekuwa marehemu. Lakini kwa kuwa umeona kitu kilichofanyika ni makusudi, ruhusu risasi yako iniondoe Hapa Duniani. Mtu badala utulie tuangalie tunapambana vipi na watu hawa wewe unapayuka payuka tu. Piga hiyo risasi yako sasa. Aliongea Masimba huku akiutingisha mkono wa Teddy. Teddy akaganda kama sanamu huku mdomo wa bastola ukiwa kwenye paji la uso wa Masimba. Punde akaishusha bastola kisha kuwafuata wadogo zake na kutoka nao ndani ya Nyumba huku akimuacha Masimba akiwa ametulia akimuangalia. Kichwa chake bado hakikutulia kutokana na kifo cha Vicky. Hakuna kitu kilichomkosesha amani katika kazi yake hii kama kuzudiwa akili na watu. Alipenda siku zote kuibuka mshindi katika kila kitu anachokianzisha. Lakini leo hii alikuwa amezidiwa ujanja na mtu mmoja. Ujanja na mtu ambaye hakujua alikuwa ni nani. Aliondoka pale aliposimama na kuelekea kitandani kwake. Uso wake ulionyesha kuchoka sambamba na mwili wake. Hakupenda kilichotokea kimtoe kwenye njia ya kuimaliza hii kazi. Hakupenda kilichotokea kiharibu mipango yake. Ni kweli vicky amekufa lakini kufa kwake hakutufanyi sisi tukakata tamaaa. Hilo likamuamsha hapo kitandani mpaka bafuni. Maji yakamiminika mwilini kisha sabuni kupita juu. Alipotoka hapo akaingia chumbani na kuchagua mavazi fulani. Punde alikuwa akitoka akiwa mtu mwingine. Mawazo yake aliamua kurudi sehemu ya tukio. Alitaka kurudi Ufukwe wa Bahari ya Hindi sehemu alipouawa Vicky. Alitaka kurudi kwa mara hii akiwa kwenye utimamu. Utimamu wa akili sambamba na mwili. Lakini aliamua kupita hoteli zote ambazo aliambiwa kuwa walifikia wageni hawa ambao wawili kati yao ndio wale waliouawa Jana. Alitaka kwenda kuuliza kama kuna chochote kimenuswa hasa baada ya tukio la jana pale ufukweni. Alifika hotelini na kupokelewa na 'wahudumu' kwa bashasha na ukaribu. Akachagua sehemu ya pembeni kabisa mwa hoteli ile. Akakaa hapi na kuagiza Chakula. Mhudumu mrembo aliyevalia kinadhifu akatokea mbele yake akiwa na sahani ya chakula na matunda mkononi. Kufika kwenye meza ya masimba akainama na kukitua kile chakula pale mezani. Baada ya kukitua hapo akaondoka katika namna ya kuvutia. Baada ya mhudumu yule kuweka chakula pale na kuondoka, masimba akaiinua kidogo sahani ya chakula, akakutana na bahasha ndogo ya kaki. Akaiangalia kwa umakini kidogo, baadae akafanya kama kupuuzi na kuendelea na chakula. Baada yakumaliza kula akatoka ndani ya hoteli na kutembea kwa mguu kuelekea sehemu yenye kijiwe cha tax. Muda wote alikuwa akitembea huku macho yake yakizunguka huku na huko. Alichokifanya na kuamua kukutembea ili kuw ni mbinu moja wapo ya kutaka kujua kama anafuatia ama lah.

Mpaka anafika kwenye kituo cha tax hakuona mtu yoyote aliyekuwa akimfuatilia hata kumtilia mashaka. Akaingia kwenye tax kisha kuamuru dereva ampeleeke kigamboni.

Kitendo cha dereva kutajiwa jina la sehemu husika anayotakiwa kwenda hakuficha mshangao wake. Akatamani kuuliza, lakini kabla yakuuliza akaamua kumtizama abiria wake huyu anayetaka kupelekwa huko ufukweni. Macho ya mtu huyu yalimfanya Dereva anyamaze. Hakutaka tena kuuliza. Akakanyaga mafuta na muda mfupi walikuwa wakivuka pantoni wakielekea Ufukwe wa mikadi. Muda wote huko hakutaka kuifungua bahasha aliyopewa. Alitaka kwanza kufika eneo la tukio ndipo hapo angepata muda wa kuifungua bahasha.

******
Ufukwe ulimlaki katika utulivu wa hali ya juu wakati huo ikikaribia kufika saa moja za usiku. Ukimya wa ajabu ulimpokea aliposhuka kwenye tax na kuongoza ndani. Utepe wa rangi ya manjano sambamba na Askari wenye silaha nzito walimpokea katika namna ya kumuangalia. Mwili wa Vicky haukuwepo tena kuonyesha kuwa ulikuwa umepelekwa chumba cha kuhifadhia maiti. Aliongoza na kuwapita askari wale kisha kuongoza sehemu ile ambayo alikuwa amekaa mchana ule kabla ya kifo cha vicky. Alitulia pale akiangaza macho huku na huko. Kanakwamba angeweza kumuona muuaji. Mawazo yake yakaishia kwenye bahasha ndogo ambayo alipewa na wanausalama pale hotelini. Akaichukua kutoka kwenye koti lake na kuishika mkononi. Wakati akitaka kuanza kuifungua akaisikia michakato ya miguu kama ya mtu. Sekunde moja mkono wake ulikuwa juu ya bastola yake tayari kwa kufanya lolote. Lakini alijikuta akitizamana na mwana usalama yule aliyemuacha pale ufukweni wakati wa tukio. "Kuwa makini kijana unapoingia anga hizi katika namna hiyo." Aliongea Masimba huku akimpa ishara ya kijana yule kukaaa.

"Sorry mkuu imenibidi nitumie njia hii kukwepa macho ya watu. Watu tunaopambana ni hatari sana. Kama tumeweza kuambulia patupu mchana na kumpoteza msichana yule, basi tutambue watu ni Hatari zaidi." Aliongea kijana yule akikaa chini. "Nikweli usemayo, maana kwa Jinsi muuaji alivyotuacha katika umati ule. Nilazima tuwe makini. Vipi una kitu chochote umekinasa baada ya mimi kuondoka? Akauliza Masimba. "Yeah kuna kitu nimekipata mkuu. Baada ya taharuki ile na ule mkanyagano wa watu kuna kitu ambacho nilikiona wakati wewe ukiondoka." Akajibu mtu yule. "Kitu Gani? Aliuliza Masimba. "Mwanamke mwenye mtoto mdogo." Akajibu kijana yule.

"Mwanamke mwenye mtoto? Akauliza Masimba kwa Utulivu. "Yeah mwenye mtoto mdogo, alikuwa mtu wa mwisho kutoka humu ufukweni baada ya taharuki. Utokaji wake na hata uangaliaji wake, haukua wa kawaida. Nilipolishtukia hilo nikaamia kumfuatilia kwa siri bila mwenyewe kugundua. Lakini wakati tunafika pale feri, mwanamke yule alinipotea katika mazingira ya kutatanisha. Na sikumuona tena licha ya kuwasiliana na wenzetu." Alijibu kijana yule. "Mwanamke mwenye mtoto mdogo? Lilikuwa swali lililojengeka kichwani kwa masimba. Taswira ya mwanamke mwenye mtoto aliyemuona kwenye jengo la benki ya taifa ya biashara ilimjia usoni kwake. Lakini mwanamke yule mbona aliuawa? Hilo pia likamchanganya. Huyu mtoto alikuwa nani? Na kwa nini anatembea na watu hawa? Hawa wanawake ni wakina nani? Kama yule aliuawa huyu wa leo ni nani?. Yalikuwa maswali yaliokiumiza kichwa cha masimba. Akauona ni muda wa kuifungua ile bahasha. Akaifungua kisha kukitoa kitu kilichokuwa ndani yake. Ikajikuta akitizamana na picha, picha ya mwanamke akiwa na mtoto mdogo wa kiume. Chini kulikuwa na maandishi madogo "Mwananyamala A". Baada ya kusoma maandishi yale akaunyoosha mkono wake kumpa kijana yule aitizame ile picha. "Mtu wetu ndio huyu, huyu ndiye nilimuona hapa ufukweni muda mfupi uliopita." Aliongea yule kijana akiirudisha picha ile mikononi kwa Masimba. "Tuondoke hapa twende mwananyamala, nataka nikapate maelezo kutoka kwa mwanamke huyu." Aliongea masima akiinuka tayari kwa kuianza safari kuelekea mwananyamala.

******

Kama ilivyo wilaya ya kinondoni ifikapo usiku, ndicho walichokutana nacho masimba na kijana yule waliposhuka pale mwananyamala. Madada poa walikuwa wengi wakiwaiita na kuwaonyesha biashara yao ya kuuza sukari guru. Kila mmoja alikuwa akipandisha nguo yake na kuwaonyesha kile kitu. Masimba na kijana yule hawakuonyesha kulishangaa hilo. Wakaingia kwenye uchochoro fulani uliowapeleka mpaka uwanja wa ccm mwinjuma. Wakapita pembeni mwa kituo kidogo cha polisi. Walipoingia katika uchochoro mwingine wakajikuta wakitizamana na Nyumba husika.
 
SITAKUSAHAU RUKIA

SEHEMU YA 022

Na Ibrahim Masimba

Nilitupa macho yangu kitandani na kupokewa na kitu cha kuvutia. Rukia alikuwa amelala kifudifudi kitandani huku akiwa hana hata kipande cha nguo mwilini. Alikuwa kama alivyotoka tumboni kwa mama yake. Ngozi yake ilikuwa ikiwaka na kuvutia kuitizama kwa muda wote. Ulikuwa ulalaji uliovuruga kichwa changu na moyo wangu, damu zilisimama na moyo kushindwa kudunda kwa usahihi. Nilikuwa nikimuangalia mwanamke mrembo akiwa amelala kihasara. Mwanamke mwenye mvuto mubashara. Macho yakatamani kutizama zaidi huku mikono ikitetemeka ikihitaji kwenda kuushika mlima ule. Mlima uliotukuka katika matumizi sahihi ya kutafunwa kama sio kuchemshwa. Miguu ikahitaji kupiga hatua kuelekea pale kitandani. Alifanana kabisa na Kim kardashian ule muinuko wa upande wa pili. Mate yakajaa mdomoni na uchu kuongezeka. Sikuweza kumkumbuka tena Dalillah Adam, sikuweza kumkumbuka kwa wakati ule. Licha ya kutokumkumbuka lakini hilo halikunifanya nipige hatua nielekee pale kitandani, bado nilikuwa nimesimama nikitafakari. Mara nikaliona tukio jingine ambalo lilinishtua na kunifanya nianze kutetemeka. Rukia alijigeuza na kuiachanisha miguu yake huku na huko. Hapo ndipo nilipohisi kuwa ulikuwa mtego, mtego wa kunivuta na kunikamata kabisa. Sikuwa na ujanja zaidi ya kuangalia ule uumbwaji uliotukuka. Uumbwaji ambao haukukosewa hata kidogo. Nikatamani kuuvamia ule uumbwaji lakini niliogopa kwa kuwa Rukia Bado alikuwa ana mshono, bado hakuhitaji kukutana na mtu kimwili. Licha ya kupita miezi tisa lakini bado nilikuwa nikiogopa hilo. Nikasogea taratibu pale kitandani, hofu moyoni tamaa machoni. Mlalo wa rukia haukuwa katika kiwango cha Masters ulikuwa mlalo ambao ulipitiliza. Nikakifikia kitanda kisha nikakaa pembeni yake. Hapo ndipo nilipochanganyikiwa kabisa, hapo ndipo nilipochanganyikiwa nikashindwa pakuanzia. Ni mwanaume gani lijali angeuacha urembo huu? Ni mwanaume gani aliekamilika atakaemuacha Rukia? Hilo lilikuwa gumu kwangu, hilo lilikuwa gumu kwa kuwa nilitambua Rukia Bado anaomshono. Nikaendelea kukaa pale kitandani nikimuangalia kwa matumaini ya kuanguka dhambini. Nam, ilikuwa ni lazima katika hilo. Nikajilaza kitandani nikitizama pembeni, sikutaka kumuangalia tena. Nilitamani kufanya lakini nilihofia kwanza. Sikujua ni muda gani nilipitiwa na usingizi, lakini nilijikuta nikimshtuka saa kumi za usiku tena kwa kuamshwa na Rukia.

Niliinuka huku nikimuuliza kulikoni, lakini bado hakunijibu, bado aliiniangalia usoni mwangu. Bado hakuinua mdomo kunijibu. Alionekana kutafuta maneno ya kusema lakini hakuonyesha kama ameyapata. Nikaendelea kumsubiri aongee, aongee kile ambacho alitaka kukisema.

"Ibu Hivi mimi ni dada yako? Hatimaye aliuliza. Hapo nikahisi uwepo wa tatizo.

"Hapana, wewe sio dada yangu." Nikamjibu.

"Kama unalijua hilo kwa nini unanitendea hivi? Hujui hata mimi nina hisia? Akanipa maswali tena magumu sana. Sauti yake haikuonyesha utani.

"Najua Rukia lakini huoni kama bado wewe ni mgonjwa? Huoni kuwa tunaweza kutafuta tatizo jingine? Nami nilimjibu lakini kwa namna ya kuuliza. Maswali yangu yalimfanya rukia aniangalie usoni kwa muda mrefu bila kuongea kitu. Licha ya Kuniangalia lakini pia mikunjo ya hasira ikatokea usoni.

"Hivi Ibu, wewe na Daktari nani anautaalam kuliko mwenzie? Akauliza.

"Ni daktari. Nikajibu.

"Kama ni Daktari, kwa nini wewe useme sijapona wakati Dk Hamza Kibirige amesema Nipo safi na nina uwezo wa kukutana na mwanaume? Lilikuwa swali ambalo sikupata majibu yake. Nikabaki kimya nikimuangalia tu Rukia. Nilijua nikipi ambacho alikuwa akihitaji.

"Sikiliza Ibrah, hata mimi nina hisia, mwili wangu unahitaji kumbatio. Nimekwambia wewe kwa kuwa tunaishi wote. Lakini kama unaona sikufai niache nikatafute mwanaume mwingine. Wapo wanaume wanapigana vikumbo kwa ajili yangu. Wapo wanaume wanaokosa usingizi kwa ajili yangu. Ninachofanya nikukuheshimu na pia kwa kuwa nimeamua kulipa fadhila kwa kukuonyesha penzi la kweli. Lakini kama hutaki acha nitafute mwanaume tena mwanaume ambaye nitakuja naye hapa ili umuone na nikutambulishe. Naona mimi na wewe tumeshakuwa kaka na dada kwahiyo acha nikuonyeshe shemeji yako." Alipoongea hilo akajilaza kitandani na kujifunika shuka gubigubi. Akaniacha nikianza kutafakari maneno yake, maneno ambayo yaliufanya moyo Wangu Ukose amani. Atamleta mwanaume hapa anitambulishe kwa kuwa mimi ni kaka yake, inawezekana kweli hii? Hapo nikauona wivu ukijaa moyoni. Nikabaki kumuangalia pale alipolala. Wakati mimi nikihangaika mwenzangu ndio kwanza alikuwa akijigeuza huku na huko akionyesha kufurahishwa na maamuzi yake.

******
Ilikuwa wiki ngumu sana kwangu, wiki ambayo haikuwa na kumbukumbu nzuri kwangu. Ilikuwa ni siku ya jumamosi nikiwa nimetulia nyumbani nikijisomea kitabu changu kiitwacho Kikosi cha Kisasi kilichotungwa na kuandikwa na mwandishi nguli wa vitabu vya kipelelezi Hayati ELVIS MUSIBA. Nikausikia mlango ukigongwa huku ukisindikizwa na sauti ya mtu. Kabla sijainuka hapo nikamuona Rukia akiinuka na kuuende mlango kisha kuufungua. Punde nikawaona wazee wawili wakiingia. Walikuwa wamevalia kanzu zao maridadi sana. Nilikiacha kitabu nilichokuwa nikikisoma nikawakaribisha ndani wazee wale. Ulikuwa ni ugeni ambao sikuutegemea. Ulikuwa ugeni ambao ulinipa mashaka sana. Mawazo yangu nikadhani labda ni wazazi wa Dalilah Adam. Lakini nilipoiona ile pilikapilika ya Rukia nikaanza kuhisi uwepo wa kitu. Lakini nikavumilia ili kuuona mwisho wake.

"Samahani Sana bwana Ibrahim, sisi ni washenga tumetumwa hapa kuleta posa kuhusu mdogo wako huyu. Tulipanga tujetokea jumatato lakini kutokana na majukumu mengine tukashindwa na ndio maana tumekuja leo.""alimaliza kuongea mzee mmoja.

Kwanza nilikosa maneno ya kuongea, nikabaki kushikwa na bumbuwazi. Wivu ukanishika kama sio kunishika. Jasho likaanza kunitoka huku mishipa ya hasira ikionekana. Nikaangalia wale washenga kwa muda nikitamani kuwaambia posa hakuna. Lakini watanielewaje...

NIKABAKI KIMYA NIKIUGULIA WIVU MOYONI

******

UKIITAKA YOTE UTATUMIWA KWA BEI NAFUA 3000 YOTE MPAKA MWISHO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom