NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 047
Teddy ametoroka na mtoto na inasemekana wameelekea Arusha. Lakini tulipowasiliana na watu wetu kule hawakumuona Teddy popote pale licha ya kupekuwa viwanja vyote vya ndege sambamba na kuangaliwa kwa umakini kwa kila gari ambayo ilikuwa ikiingia arusha na kutoka. Hivyo basi Jimmy na Ben wameelekea huko kumtafuta Teddy ili wamuue ili wamchukue mtoto wako iwe chamba cha kukufanya wewe urudishe mzigo uliouchukua." Aliongea salha akimtizama masimba kwa umakini. Alitaka kugundua nini ambacho angekishuhudia machoni kwake. Lakini hakukutana na chochote kile, hakukiona alichokuwa anakitafuta. Licha ya masimba kutokushtuka kwa taarifa ile, lakini moyoni na kichwani hakuwa katika usawa. Hakuwa katika utimamu wa kiakili na hata kimwili. Alimuwaza france, alimuwaza mwanaye aliempenda sana. Hakutaka kukubali mwanawe kupotezwa. Alinhitaji mwanawe akiwa hai. Alimuhitaji france akiwa kwenye tabasamu lake alilolizoea. Lakini alipofikiria kuhusu Teddy kutoroka bado mwanamke huyu aliiyumbisha akili yake. Bado mwanamke huyu hakueleweka upi msimamo wake. Alifanya mauaji na usaliti wote sababu ya Kundi lao. Hata kuuawa kwa mama yake, Teddy alikuwa nyuma ya kifo cha mama yake. Lakini leo hii tena Teddy alikuwa akisakwa na Jimmy, teddy leo alikuwa ametoroka tena akiwa kwepa Jimmy na Kundi lake. Kwa nini amekimbia? Kipi kimemfanya akimbie Tena akiwa na france. Akaiona Hatari mbele yake endapo atamuacha Jimmy amfikie Teddy. Alitambua ungekuwa nwisho wake sambamba na mwanawe france. Hapo akaamua kufanya kitu. Akarudisha macho kwa Salha. Wakaangaliana kwa mara nyingine. Kila mmoja akisoma kilicho ndani ya macho ya Mwingine. Kila mmoja alijua yupo na nani. Licha ya salha kudanganya kuwa ni mfanyakazi wa kawaida haikuwa hivyo. Huyu alikuwa Jasusi. Alisomeka na Masimba alilitambua hilo. "Naelekea Arusha kumrudisha Teddy na France, nina kisasi na teddy na nitapenda kumuua kwa mikono yangu. Naomba tuondoke hapa nikakuache sehemu salama. Lakini kukuacha huko itabidi ufumbe na usiufumbue Mdomo wako. Ukifanya hivyo nilichomfanya mwamvita Muda mfupi uliopita ndio nitakachokifanya kwako." Alinguruma masimba huku akianza kutembea kuelekea Nje. Licha ya Masimba kutembea kuelekea nje, lakini Salha bado alikuwa amekaa. Alionyesha kupigwa na bumbuwazi. Maneno yaliyotamkwa na Masimba yalimuingia sawasawa. Kwamba mwamvita amekufa? Kwamba mwanamke yule katili ameuawa? Kilikuwa kitu kigumu kukiamini. Alijikuta akiwa kondoo mbele ya Masimba. Alimfuata kwa nyuma akihitaji kukijua kile alichokisia. Hata alipomkaribia Masimba bado aliilazimisha miguu yake kutembea. Akamuangalia Tena masimba. Lakini kabla hajaongea chochote simu yake ikaonyesha uhai. Kuna mtu alikuwa akimpigia. Akaitoa simu na Kuitizama. Jimmy,neno pekee lililosomeka Juu ya kioo. Akasita kisha kumuangalia Tena Masimba. Kuangaliwa kule akatambua kulikuwa kuna kitu. "Jimmy anapiga.!! Ilikuwa sauti iliyomvuta Masimba karibu na Salha. "Pokea, harafu muulize yuko wapi na wamefikia wapi." Ilikuwa amri kutoka kwa Masimba, amri ambayo ilitekelezwa muda ule ule.
********
Alikuwa juu ya kaburi la mama yake Masimba akilia kwa uchungu katika usiku ule. Moyo wake ulikuwa umepondekapondeka. Alikuwa akijuta na hata kulia kwa sauti. Hakuna baya ambalo alifanyiwa na huyu mama. Siku zote alimpenda kuliko hata mwanawe Masimba. Alikuwa akisuluhisha migogoro yao kwa upendo mkubwa. "Nisamehe mama yangu, bila ujinga wangu leo hii nisingekupoteza. Tamaa ya pesa imenifanya niusahau utu wako. Imenifanya nisahau mapenzi yangu kwako. Nikafanya kitu ambacho sasa nakiwaza. Mama nipo hapa nikishindwa kujua wapi nitakwenda. Masimba ananisaka aniue mama. Masimba anitafuta anilete huko, sina uwezo na ujasiri wa kusimama mbele yake kumuomba msamaha. Sina ujasiri hata wa kumuangalia Machoni. Mama nakisubiri kifo changu hapa hapa Juu ya kaburi lako. Nataka Risasi ya Masimba Inilipue nikiwa hapa. Nitamwambiaje mama na hata baba yangu? Vicky atanielewaje katika hili niliofanya? Ataniacha? Vipi mwanangu patra? Hapana Nastahili kufa." Yalikuwa maneno aliyotamka Teddy akiwa juu ya kaburi. Alikuwa Tanga badala ya Arusha. Alitambua asingeweza kufika arusha bila kutiwa nguvuni. Kitu alichoona ni kushinda juu ya kaburi ya mama yake Masimba. Alishinda hapo huku france akimuacha nyumbani kwao kibugumo Nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
*****
Alishuka Handeni Usiku wa Saa sita kwa Usafiri wa kukodi. Baada ya kushuka hapo akaongoza Moja kwa moja mpaka nyumbani kwao ambapo bado watu walikuwa wanalala Matanga. Aliwakuta wengi wa watu wakiwa wamelala huku wachache tu ndio waliokuwa wakiota moto. Aliwasalimia wachache waliokuwepo na kuanza kuongea nao. Kufika hapo akakutana na vilio kutoka nyumbani kwa mzee First wazo,. Hapo akagundua kuwa tayari taarifa za kifo cha Dee Plus zilikuwa zimefika hapo kijijini. Wakaongea mpaka asubuhi kulipokucha. Watu wakajiandaa kwa sababu ya kwenda kuchimba kaburi la kumhifadhi Dee plus. Wakiwa bado wanajiandaa wakalisikia yowe kutoka kwa mmoja wa watoto ambaye alipita karibu na makaburi. Watu waliokuwepo msibani wakageuka na kutizama huko. Wengine walishaanza kukimbia kuelekea kule wengine wakibeba silaha tayari kwa lolote. Masimba ndio aliyekuwa wa kwanza kufika pale makaburini. Macho yake yakatembea katika sekunde ile ile. Macho yake yakatua juu ya kaburi la mama yake. Akamuona mtu akiwa amelala juu akionyesha kudhoofika mwili. Hakushangazwa na kule kudhoofika, bali alishangazwa na mtu aliyejuu ya kaburi. Teddy alikuwa juu ya kaburi la mama yake. Kaburi la mwanamke ambaye alihusika katika kumuondoa duniani. Alikuwa amelala na alikuwa akionyesha kuchoka sana. Wakati huo watu wengine nao walikuwa wameshafika. Kila mmoja alikuwa akikiangalia kile kinachoendelea pale. Mwanamke wanayemjua alikuwa akilia, akilia juu ya kaburi la mama wa masimba. Kaka yake Masimba aitwaye Samwebondo ndiye aliyepiga hatua kuelekea pale kaburini. Dada zake masimba naye wakaungana naye kuelekea pale. Sekunde hii walikuwa wakimbeba Teddy akiendelea kulia. Licha ya ndugu wote kufanya hivyo lakini kwa Masimba haikuwa hivyo. Bado alisimama akimuangalia Teddy Hasira zikimchemka. Alitamani kuchomoa bastola yake na kumlipua. Alitamani kumuendea pale na kufanya lolote. Lakini hakuweza hilo, kwa kuwa macho ya watu yakaanza kumtizama na minong'ono kuanza taratibu. Watu walianza kuhoji katika hili. Walianza kuhoji ulipo utu wa masimba. Wakamlaumu tena na tena. Masimba hakuwasikiliza. Akaondoka pale akiwaza na kuwazua. Alitaka kumuua Teddy, hakutaka alione Juaa la kesho, lakini angemuuaje wakati tayari teddy alikuwa mikono mwa ndugu zake tena akiwa mwenyewe pasipo mtoto wake? Kwa nini hakuelekea arusha na kuamua kuja huku? Inamaana tokea majuzi alikuwa pale juu ya kaburi. Alijiuliza huku akijilazimisha kutembea kurudi nyumbani. Hapo akakutana na kitu kingine. Dada zake walikuwa wamembadili nguo na sasa walikuwa wakimpeleka bafuni kwa minajili ya kumuogesha. Hapo akatamani kuwaambia ukweli. Alitamani kupaza sauti lakini hakuweza. Hawakuweza kwa kuwa dada zake walimpenda na Hawakujua kama alikuwa nyuma ya kifo cha mama yao. LAITI WANGEJUAA!!@@@??? SIDHANI KAMA KUNGEKUWA NA HATA MMOJA ANGEMGUSA.
ITAENDELEA