NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 043
Mwili wa tejayule ulikuwa umelala kanakwamba alikuwa kwenye usingizi wakawaida, ukimuangalia juu juu unaweza kudhani alikuwa usingizini lakini michirizi YA damu pembeni mwa ule Mwili ndio kitu kilichomwambia masimba kuwa mtu yule alikuwa ameshasafirishwa kwenda kuzimu. akaufungua mlango akaingia ndani nakuurudisha mlango akabaki ndani akiutizama Mwili wa kijana yule. kisu kidogo kikiwa kifuani kwa kijana huyu. kwa mara nyingine alikuwa amewahiwa na watu wale. watu ambao walianza kumtia hofu nakujua kuwa alikuwa akionekana kila mahala alipokuwa akipita . akasogea mpaka kitandani alipo mwili wa kijana yule. wakati akitembea taratibu ndani ya chumba, macho yakagota kwenye pazia la dirisha. hapo akauona uwazi ambao aliutilia mashaka. uwazi uliokuwepo ulikuwa na uwezo wa kupitisha mdomo wa bastola . akasimama kwanza akikitizama hicho. baada ya kutizama sana akageuza macho kuuangalia tena mwili wa kijana. hapo akakiona kitu kilichofanya kengele za hatari kugonga kichwani Kwake. usawa wa kusimamia mtu endapo atataka kuuchunguza mwili ndio usawa ambao uliachwa uwazi. masimba hakuwa mjinga kiasi hicho. aliujua mtego, aliujua kwa kuwa kama angesogea mbele zaidi basi risasi kutoka kwa mtu ambaye alihisi kuwepo kwake kwa nje ya chumba kile. alichokifanya nI kurudi nyuma nakuizima taa kisha kuondoka taratibu bila kupiga kelele. akatokea sebuleni na kuondoka kwa kutokea mlango wa mbele. hiyo ilikuwa mbinu ya kijasusi, siku zote unapoingia sehemu ukakuta kuna tukio la kutisha kisha ukaiona hila fulani ndani yake, unachotakiwa kufanya ni kutoka hapo kwa kutokea mlango ulioingilia kwanI kwa mazingira ya kifo kilichotokea watu wanaweza kukutengenezea "mlango" wa kifo kwa kutumia kifo kilekile kilichotokea. aliujua akipita mlango wa uani unaweza kuwa mtego kwake kwa kuwekewa mazingira ya kupigwa Risasi. Alitembea taratibu safari hii akiamua kuwatafuta Teddy Harry na mwamvita kwa sabab ya kuwaondoa hapa chinI ya jua. bado tukio la kupigwa risasi kwa mama yake na kuuawa kwa Dee Plus lilikuwa likikisumbua kichwa chake. alitembea usiku ule akihitaji kuelekea mbezi beach anapoishi mwamvita alitambua kuwa Angeweza kumpata kwa wakati ule. alikuwa MakinI kwa kila hatua, alikuwa akitembea na damu ya watu nane mikono mwake. Alihitaji kuilipa damu iliyomwagwa kwa mikono yake. alikuwa pekee Katika HilI. Alitakiwa kulimaliza pasipokuimwaga damu ya mtu mwingine. Hakutaka kumshirikisha mtu katika hili. Hakumuamini mtu kabisa. Kwa alichotendewa na Teddy hakutaka kumuamini tena mtu. Alumpenda teddy, akamthamini kutoka ndani ya moyo wake. Lakini Teddy hakuliona hilo. Akafanya usaliti na kuja kumuua mama yake mzazi. Akaona haitoshi akawajeruhi watoto ambao hawakuwa wakijua chochote kilichokuwa kikiendelea. Alitaka kuutumia usiku ule kuichukua roho ya mwamvita. Hii ilikuwa mission ngumu kwake, mission ambayo haikuwa na msaidizi. Hakutaka kumtafuta msaadizi kutoka idara nyeti ya usalama. Mama yake alikuws amelala na hata Dee plus hakuwa macho tena. Mara hii alikuwa akipita pale Lugalo military Base usiku ule. Alikuwa akiiangalia kambi ile. Kambi iliyompokea kwa mara ya kwanza wakati alipotoka kwenye mafunzo ya awali. Kambi ambayo ilimpa ujasiri na nguvu ambazo ziliwafanya wakuu wake wamhamishie Idara ya usalama wa Taifa. Aliitizama kambi ile kwa makini sana. Akamkumbuka major general Hayati Imran Hussein kombe, ambaye alikuja kuwa mkurugenzi wa Idara ya usalama wa Taifa. Ndio huyu aliyekuja kuuawa na polisi walipomhisi kuwa alikuwa mwizi wa magari. Licha ya kujitambulisha kwake lakini polisi wale walimpiga risasi mbele ya mkewe. Mkewe pekee ndiye aliyepona baada ya kutoroka kupitia kwenye mashamba ya mahindi. Hata pale wauaji walipohukumiwa kifungo cha kunyongwa lakini walikuja kuachiwa huru pasipo maelezo yoyote. Kuliwaza hilo likamtoa machozi.. Punde alikuwa akiipita lugalo na kukipandisha kilima cha kuifikia Mbezi. Baada ya kufika tangi bovu, akamuomba Dereva yule amshushe hapo. Dereva akaegesha pembeni kisha kumruhusu masimba kushuka. Baada ya kushuka alimuacha yule dereva aondoke, kisha naye akaondoka pale akitembea kwa miguu.
Ulikuwa usiku wa malipo na usiku wa kupeleka tiketi na hata usafiri. Mbezi yote ilikuwa kimya sauti za pekee zikisikika. Hapakuwa na sauti ya mkazi ama mpita njia yoyote yule isipokuwa magari machache tu yaliokuwa yakipita barabarani.. alitembea na kivuli cha miti wakati mwingine akikwepa taa za magari mpaka alipoifikia Africana. Kufika hapo akaangalia huku na huko lakini leo hapakuwa na watu, kwani hata ile bar ambayo jana aliikuta wazi. Leo ilikuwa imefungwa na hapakuwa na kitu chochote. Wakati akiendelea kuchunguza hiki na kile, mara akauona mwanga wa taa za gari zikusogea maeneo yale. Akajibanza kwenye jumba fulani bovu, hapo akaliona gari ya kifahari ikipita. Aliitizama kwa sekunde kazaa akaondoka pale akiifuata nyuma nyuma. Alikuwa akihama hapa na kuhama pale. Alikuwa akitembea kama mcheza sinema. Mpaka gari ile inasimama Nje ya geti la jumba analoishi Mwamvita, masimba naye alikuwa umbali wa hatua tatu tu. Mlango ukafunguliwa akashuka mwamvita akiwa sambamba na watu wawili. Kati ya hao mmoja tu ndiye aliyemtambua. Alikuwa yule mwanamke alikuja ofisini kwa chief mchana ule na ndiye aliyehusika na kifo cha yule teja. Wote wakaingia ndani pasipokuacha mtu yeyote nje. Ulikuwa muda wa sekunde mbili zilizotumiwa na Masimba kuifunua buti ya gari na kujitupa ndani yake. Akatulia kama Dakika mbili akawasikia watu wakirudi wakiongea.
"Huyu Teddy itabidi itafutwe popote na kuuawa. Hawezi kujiondoa katika mpango huu. Ni lazima mzigo tuupate na lazima Masimba na Teddy tuwasafirishe kuzimu. Nimejisikia raha sana kumuua Dee kwa mkono wangu. Ndio maana hata mama wa masimba alipoleta ujinga sikumkopesa. Teddy atafutwe popote sambamba na yule mtoto." Alijitapa mwamvita bila kujua maneno yake yalikuwa yakimchoma Masimba. Alitamani kufungya buti na kutoka. Lakini kitendo cha kusikia teddy haonekani, kilimpa faraja ya kutambua kuwa France alikuwa hai.
"Teddy tutampata nyie msijali. Tunachotakiwa kufanya ni kuendelea kumlaghai Chief aweze kuitisha Mkutano na Wana Habari ili aionyeshe ile video inayomuonyesha Masimba akimuua waziri. Tukilifanikidha hilo tutakuwa tayari." Akaongea mwanamke mwingine huku wakiingia kwenye gari na muda mfupi akaliona gari likitembea. Hakujua wapi walipokuwa wakielekea. Na pia hakuwa akiyasikia tena mazungumzo ya watu wale. Muda wote alikuwa akifikiria jinsi ya kulimaliza hili. Ilikuwa ni lazima azuie chief kuitisha mkutano na waandishi wa habari na pia alitakiwa kuizuia hiyo video ama aipate na iwe mikononi mwake. Alikuwa lazima afanye hivyo huku akiamini kuwa angemsaka Teddy hata pale atakapo wamaliza hawa. Gari ilitembea kwa dakika kama Ishirini na tano ama thelathini. Ghafla akasikia likipunguza mwendo na kupiga honi kadhaaa. Mara lango likafunguliwa akahisi gari ikiingizwa ndani. Punde gari ilikuwa ikisimama. Akaisikia milango ikifunguliwa kisha akasikia hatua za watu zikitembea kuelekea ndani. Baada ya ukimya fulani kutawala, akafunua buti na kuchungulia kwa nje. Hapo akauona uwazi wa kuweza kutoka. Sekunde ya pili alikuwa akiangukia pembeni na kuchupa tena mpaka sehemu fulani ambayo ilikuwa na mbaombao. Akatulia hapo kwa muda akitazama kila kitu kinachoendelea mle ndani. Alikaa hapo kwa muda wa kama dakika tano akawaona watu walewale wakitoka. Wanne kati yao wakajipakia ndani ya gari lakini Mwamvita hakufanya Hivyo. Baada ya maongezi Mawili matatu gari ile ikaondoka huku mwamvita yeye akirudi ndani. Baada ya mwamvita kuingia Masimba naye aliianza kutambaa kwenye ukuta mpaka penbeni mwa jumba lile. Kufika hapo akaliona dirisha Moja la kioo likiwa wazi. Akasogea mpaka hapo na alipolifikia akachungulia kwa ndani. Macho yake yakakutana na mwamvita akiwa hana hata nguo maungoni mwake. Alikuwa akielekea bafuni kuoga. Baada ya Mwamvita kutoka mle chumbani Masimba akasogeza kioo na kujitumbukiza ndani tayari kumsubiri mwamvita. Akachepuka mpaka kando ya mlango na kutulia hapo. Akatulia hapo kwa Dakika Tano. Punde akasikia nyayo za mtu zikisogea pale mlangoni. Punde akamuona mwamvita akiingia akiwa mtupu vile vile.
NAAM TUKUTANE KESHO.
MICHANGO YENU BADO NI MUHIMU SANA