NITAKUPATA TU
SEHEMU YA O51
*******
Zilikuwa sura za watu ambao aliwafahamu kabisa. Walikuwa watu kutoka kikosi maalum cha kuwalinda viongozi. Hawa huendeshwa ama kuagizwa na Rais, makamu, waziri mkuu sambamba na mkurugezi wa idara ya ujasusi. Hawa wawili walikuwa vijana wale ambao walimkanata na kumpeleka kule kuzimu. Lakini leo hii wameingia ofisi ya waziri mkuu na kuichukua simu ambayo ingeweza kumsaidia yeye kwenye kazi yake. Hilo hakuwa amelitegemea kwa kuwa hapo mwanzo alidhani Simu ipo mikononi mwa Wana usalama. Akaziangalia zile sura kwa muda kisha akageuka tena kumuangalia yule Mama. Akili yake haikuwa pale kabisa. Bado aliuona utata katika kuupata ushahidi wa kuuthitishia ulimwengu kuhusu ubaya wa waziri. "Kuna kingine Mama unachojua ukiondoa hivi vichache.? aliuliza Masimba. Mama yule hakumjibu kwa maneno bali akaondoka pale na kuingia katika kichumba kingine. Akatoka na mfano wa bahasha na kumkabidhi masimba. "unachokitafuta kuhusu waziri vyote viko humo ndani. Humo ndio utamjua waziri. Nimekupa hiyo bahasha nikiwa najua nina hatarisha maisha yangu. Lakini siogopi, hata nikifa leo najua nimekufa sababu ya Nchi yangu." Aliongea mama yule huku tabasamu lake likiyeyuka Usoni. Sasa alikuwa katika Uso wa Hofu. Hofu juu ya kifo, hofu juu ya kutoa siri ambayo hakutakiwa kuijua ama kuitoa. Masimba akamuangalia mwanamke huyu kwa muda mrefu. Alimuona ni kama malaika aliyetumwa kwake. "Mama naitwa Masimba, nadhani ushawahi kunisoma mahala ama kunisikia sehemu nikitajwa. Kama nikiwa hai hakuna ambaye atakugusa." Aliongea masimba akimpiga piga yule mama mgongoni. Mama aliganda kwa mshangao, mshangao wa kutokuamini maneno kutoka kwa kijana yule. Masimba ni Huyu? Anawezekana vipi kuwa huyu? Mbona hafanani na sifa anazopewa? Hapana huyu sio masimba. Huyu ni muongo..!! Yalikuwa maswali yalitiririka kichwani kwake. Hakuamini kuwa mtu yule ni masimba. Ni hapo akataka kurudisha macho kumuangalia tena Usoni. Lakini akaendelea kupigwa na butwaa baada ya kujikuta yuko peke yake. Masimba hakuwepo lakini kilichomshangaza Zaidi milango Ilikuwa bado imefungwa. Atakuwa amepitia wapi? Alijiuliza mama yule akiangaza huku na kule. Bado hakumuona Masimba. Bado hakumuona kijana huyu aliyekuwa akizisikia sifa zake. Akatoka ofisini mle haraka hadi pale alipowaacha wenzake. Akawakuta wamejiinamia wakionyesha kuanza kuchoka . "Amepita hapa, lilikuwa swali la kwanza Bi Nina baada ya kutokea pale. "Nani? Wenzake wote wakamuuliza wakimtizama kwa mshangao. "Yule kijana niliyekuwa naye ndani." Akajibu Huku akipepesa macho yake huku na kule. "Hatuja muona mtu hapa." Nao wakajibu wakitizamana.
*****
Wakati kule ofisi ya waziri mkuu wakimtafuta masimba, yeye ndio kwanza alikuwa anavuka Hotel ya kilimanjaro akielekea posta. Alikuwa akitembea kwa miguu kwa umakini wa hali ya juu. Aliijua sasa vita ndio ilikuwa imeiva. Alitambua wakati huo alikuwa akisakwa na kutafutwa. Lakini hilo halikumtisha wala kumuogopesha. Alijua kucheza na watu hawa, na ukitaka kucheza nao ni lazima uwe muwazi na usiwaogope. Hilo ndilo lililomfanya atembea mpaka ilipo benki ya taifa ya biashara. Wakati anaukaribia mlango akawasikia polisi wawili wakiongea kwa sauti ya chini kuhusu tukio la kuuawa kwa mbunge. Ingawa walikuwa wakiongea kwa sauti ya chini lakini kwenye masikio ya Masimba ilikuwa ni sauti kubwa. Moyoni akajua tayari teddy ameshaianza kazi. Akatawapita huku akitabasamu akiuendea mlango wa kuingia ndani ya Jengo lile lenye Benki. Baada ya masimba kuingia, haikupita dakika gari moja alionekana ikipaki pembezoni mwa Benki ile. Kisha wakashuka wasichana wawili na mvulana mmoja sambamba na mtoto wa kiume mwenye umri wa Miaka Saba. Baada ya kushuka kwa wanawake wale, wakaangaza kidogo kisha akaonekana yule mwenye mtoto wa kiume akiuendea mlango Huku wale wawili wakionyesha kumsubiri. Msichana yule aliingia ndani kisha kuchukua karatasi ya kujaza tayari kwa kutoa pesa. Lakini wakati akijazajaza ile karatasi alionekana akigeuka huku na huko katika aina fulani ambayo kama umtu wa kawaida usingeweza kugundua.
Baada ya masimba kuondoka pale Ofisi ya waziri mkuu, alijua kabisa kuwa lazima alikuwa akifuatiliwa na watu mahali fulani. Hakuwa na wazo la kuingia pale Benki, lakini ilikuhakikisha hisia zake kama ni za kweli ndipo alipoamua kuingia hapo benki. Na hata alipoingia alipanda mpaka ghorofa ya tatu sehemu ambayo ilikuwa na chumba cha kuongozea Camera za usalama ndani ya Jengo lile. Akajitambulisha kisha kuomba kuangalia gari zinazoingia sambamba na watu. Wataalam wakamkaribisha. Ni hapo alipoishuhudia gari ile ikiegeshwa kisha kushuka kw watu watatu sambamba na mtoto mdogo wa kiume. Mwanzo walitaka kumpoteza kutokana na kutowatilia mashaka. Lakini kuingia ndani ya benki kwa mmoja kati ya watu wale walioingia sambamba na mtoto mdogo, kuliyafanya maamuzi yake kubadilika ghafla. Uangaliaji na ugeukaji wa mwanamke yule ilikuwa ni majibu tosha kwamba aliyeingia pale licha ya kuwa na mtoto mdogo, alikuwa mmoja kati yao. Alikuwa mtu wa fani kama yake. Yaani alikuwa ni Shushushu. Akavutiwa na hilo. Macho yake yakaendelea kumtizama mwanadada huyu katika namna ya mshangao. Jimmy alikuwa na watu wangapi nyuma ya biashara hii? Swali hilo likamfanya amkumbuke mwandani wake Teddy. Akamtafuta katika namba yake ya kifucho. Licha ya simu kusikika kuita lakini haikupokewa. Akapiga tena na tena lakini hali ilikuwa ni vile vile. Hakuhisi chochote kile katika hilo. Bali aliamini Teddy alikuwa sehemu akifanya kitu. Akageuza macho kwa tetere huyu, tetere aliyekuja na kifaranga chake. Akaiona hamu na kiu, kiu ambayo ilihitaji glass ama kikombe cha maji katika wakati huu. Huyu alikuwa masimba na alikuwa jasusi. Bado alipendezwa na ule utizamaji na hata uangaliaji wa watu wale. Sasa akaamua kuinuka akiondoka katika chumba kile. Akashuka ngazi mpaka chini kabisa sehemu ya wateja. Hapo akajifanya kuongea na watu wawili wa tatu. Akaiendea karatasi kisha kuijaza na kuelekea kwenye foleni. Sasa alikuwa amesimama nyuma ya msichana yule mrembo. Walitenganishwa kwa umbali wa nusu Hatua tu. Walikuwa wakipumuliana na kila mmoja kuisikia pumzi ya mwenzake. Hilo likaileta Raha katika roho ya masimba. Raha ambayo ilikuja pale yule mtoto mdogo alipokuja na kumkumbatia miguu. Hilo akalipenda. Mikono yake ikashuka na kumuinua mtoto na kumbeba kwa mikono yake. Sasa walikuwa wakicheza na kutaniana katoto kale. Katoto ambako kalitokea kumzoea kabakwamba kalishawahi kumuona mahala fulani. Hapo ndipo alipomuona mwanadada yule akitamani kugeuka. Alitaka kumuangalia masimba, wakati mwingine mikono yake ilikuwa akienda uelekeo ambao masimba alikuwa akiu0na. Zamu ikatembea hatimaye ikafika zamu ya msichana yule. Akasogea kwa mwendo wake wa madawa. Alijikaza asionekane kama anatetemeka, lakini hilo aliliona machoni mwake. Baada ya binti kuhudumiwa na kumaliza shida yake ndipo alipogeuka ili kumchukua mtoto. Wakakutanisha macho yao, wakaangaliana na kuangaliana. Wakajuana na kutambuana. "Nenda kwa mama. Mwambie mama tutaonana siku nyingine. Nitamtafuta kwa muda wangu." Aliongea masimba akimshusha mtoto ili kumruhusu aende kwa mama yake.
*******
Kama lilivyoeneo lote la Oystebay mchana huwa kimya sana. Hata leo hii lilikuwa kimya sana kutokana na wakazi wengi wanaoishi eneo hilo kuwa makazini ama wengine kuwa ndani ya majumba yao. Teddy alikuwa mtu pekee ambaye alionekana akitembea katika barabara moja yenye utulivu. Alionekana kutulia sana katika utembeaji wake. Macho yake madogo hayakuacha kutizama kila upande katika namna impendezayo mtu yoyote yule. Hakuuonyesha wasiwasi na wala hakuonyesha kwamba alikuwa akikifuata kitu. Alitulia na kutulia. Alikuwa njiani kupeleka tiketi ya kifo kwa mkurugenzi fulani wa Shirika la kigeni. Muda wote alikuwa akitabasamu. Na hata pale alipolifikia geti la jumba analoishi mkurugenzi yule akalakiwa na mlinzi wake. Na kwakuwa walikuwa wakifahamiana, waliongea maneno mawili matatu, kisha akalisukuma geti na kuingia ndani. Mlinzi hakujua nini ambacho kinaendelea. Akamfuata Teddy kwa Nyuma. Lakini hatua yake ya tatu akahisi kitu kikipenya kifuani. Ulikuwa kama ubaridi fulani hivi. Lakini punde akaelemewa na kuupiga mweleka. Damu zilikuwa zikishuka kifuani. Teddy hakugeuka nyuma, alikuwa akitembea kuingia ndani ya jumba. Nyuma akiiacha maiti ya mlinzi yule ikiwa imelala pasipokuwepo na Uhai. Baada ya kuufikia mlango wa kuingilia ndani ya Jumba lile, akaibonyeza kengele ya mlangoni. Zilipita sekunde kumi bila mlango kufunguliwa. Akausukuma mlango kujaribu kama uko wazi. Naam! Mlango ulikuwa wazi na mbaya zaidi alipokelewa na dimbwi la damu iliyotapakaa pale sebuleni. Vitu vilikuwa vimetupwa ovyo kuonyesha kwamba kulikuwa na vurugu zilizofanyika. Teddy akaingia sasa akiwa tayari kwa chochote. Akaufunga mlango kwa ndani sasa akiitizama ile damu. Bado ilikuwa mbichi kabisa kuonyesha aliyefanya tukio hilo amelifanya katika muda ule. Lakini mpaka muda ule hakujua nani ambaye aliuawa katika damu ile iliyosambaa. Teddy akaongeza umakini zaidi na zaidi. Hatua kumi mbele juu ya ngazi akaukuta mwili wa mzungu yule ukiwa umelala kifudifudi huku KISU KIKUBWA KIKIWA KIMESIMAMA KATIKATI YA MGONGO.
TEDDY AKAPATWA NA BUMBUWAZI. Nani huyu amefanya hivi? Ni swali pekee alilojiuliza ambalo hakupata JIBU KWA MUDA ULE.