Riwaya: Nitakupata tu

Riwaya: Nitakupata tu

Kwa sasa nmejifunza kitu, mpka riwaya ikifika mwisho ndiyo naanza kusoma, lege amenifundisha hvyo,

Walao kidogo the bold yy unapay unasoma.... Ila lege ni shida....
 
Jamani mumvumilie amesema simu yake inasumbua mpaka either jioni au mpaka kesho.amenijulisha
 
Jaman kisukari we unampataje Ibra maana no. yake haipatikani!!!!!
 
[4/12, 15:43] ‪+255 717 808 444‬: Nitakupata tu

Sehemu ya 030.

Chumba kizima kilikuwa kimya, kila mmoja akiwa amejiinamia chini akiwaza na kuwazua.hakuna aliyeamini taarifa kwamba waziri amekufa. Tena amekufa kwa kupigwa risasi. Ameuawa vipi? Na nani? Teddy? Ama ni nani? Yalikuwa maswali tata, yalikuwa maswali ambayo yalikosa majibu. Wao ndio walikuwa na waziri, wao ndio waliokwenda na waziri kule magomeni. Wakamuacha na teddy pale hotelini kwa pendekezo lake. Alitaka kumuonja teddy autambue utamu wake, alipanga atakapofanikisha hilo basi atamuua Teddy kwa mikono yake. Lakini kinyume chake waziri ameuawa yeye huku akiachwa peke yake. Hakuna mlinzi aliyemshuhudia teddy au muuaji akitoka chumbani kwa waziri. Hicho kilikuwa kitendawili, kitendawili ambacho hakikupata mtenguaji. Hakuna ambaye haujui ulinzi wa viongozi wa nchi. Hakuna asiyejua wanausalama wanavyokuwa makini katika kazi yao. Lakini Usiku wa Jana walinzi hao hawakutenda kilichozoeleka. Hapo wakauona mwisho wao, mwisho wa maovu yote waliokuea wakitenda. Waliishi kifahari na kufanya kila kitu wakilindwa na mtu ambaye Leo hii alikuwa hayati. Wakiliwaza hilo punde wakauona mlango ukisukumwa kisha sura ya mwanadada akijipenyeza hapo ndani. Alikuwa mwamvita akitembea akionyesha kuchoka. Hata yeye sasa alikuwa akiona muda unakwenda ndivyo sivyo. Yalikuwa mmoja kati ya watu waliotumwa kwenda kunusa kilichopo nyumba ya kifo cha mfadhili wao. Mkononi alikuwa amekamatia kitu mfano wa karatasi. Baada ya kusogea mpaka karibu na watu wale akabwaga kitu alichokishika mkononi. Watu wale wakasogea kila mmoja akielekeza Hicho lake pale mezani. Macho yao yakajikuta yakiangalia picha mbaya. Wasichana wawili tofauti walikuwa wameuawa katika staili mbili tofauti. Wakati mmoja akionyesha kulala katikati ya dimbwi la damu, huyu wa pili alionekana amewekwa ndani ya pila, lakini kitu kilichowasisimua zaidi, ni pale kugundua kila marehemu alikuwa na matundu ya risasi upande wa kushoto wa kifua. Hilo likawafanya kwanza wawe kimya wakimtizama Mwamvita Usoni. Bado hawakuijua sababu ya kuwaletea zile picha. Lakini baada ya kuangaliana kwa mda huku macho ya mwamvita yakiongea, wakarudisha macho pale chini. Jimmy akaziangalia sura za marehemu wale kwa sekunde tano tu, akawakumbuka. Aliwakumbuka wote kwa pamoja. Mmoja alikuwa mhudumu wa hoteli yalikofanyika mauaji, na mwingine alikuwa ni changudoa, Naye alikuwa akifanyia biashara pale pale travertine magomeni. Hapo akaunganisha picha na kupata jibu kwa nini picha zilikuwa pale.

"Wamesafirishwa kama kufumbwa midomo. Hawa ndio wangetupa majibu juu ya kilichotokea. Ni wakati wa kufanyakazi bila kumtegemea mtu. Tukae tukijua kuwa hata sisi tutachunguzwa. Tutaanza kufuatiliwa na tutanuswa kila tutakapo pita. Jimmy nadhani wewe utahojiwa, nadhani utafuatiliwa kuliko sisi. Unatakiwa makini zaidi. Kama teddy yupo salama mpaka mud huu ni lazima atataka kulipiza kwa kilichotokea. Naadhani mapambano yameanza sasa." Aliongea mwamvita huku akiendelea kutizama zile picha. Wrote mle ndani wakaafiki. Ilikuwa lazima wamsake Teddy.

****
Ofisi za idara ya usalama wa taifa zilikuwa katika hekaheka kubwa. Vijana walikuwa mtaani wakinusa na kutafuta chochote. Shinikizo kutoka kwa rais ndio kitu kilichokuwa kikiivuruga akili ya mkurugenzi wa usalama wa Taifa Mr Godliving Kimaro. Muda wote alikuwa akipakipigiwa simuakiulizwa hili na lile. Hasa akiulizwa wapi amefikia katika suala hili. Kichwa chake kilikuwa kimevurugika, hakuwa akijua wapi pa kuanzia na hata kumalizia. Taarifa za kwamba mhudumu wa Zamu katika hoteli alimouawa WazirWaziri naye ameuawa katika aina ya kuufumba mdomo asiongee chochote. Changudoa aliyesemekana kwamba ameonekana akiwa na mwanaume anayetuhumiwa kufanya unyama huo naye ameuawa. Tena wote wakiuawa katika staili moja kwakupigwa risasi kifuani. "Alikuwa kijana aliyejengeka kimazoezi mwenye muonekano kama mcheza sinema. Begani alimbeba msichana aliyeonekana kupoteza fahamu" alikuwa akiirudia taarifa aliyotumiwa na vijana wake. Taarifa ambayo bado haikumfumbua na kumtoa gizani katika sakati hili. Kilikuwa ni lazima ajue na atambue nani alionekana na waziri kabla ya kifo chake. Hakuchelewa katika hilo, muda mfupi baadae simu yake ilikuwa sikioni akiipiga namba Fulani.
[4/12, 16:11] ibrahim: Simu ilikuwa sikioni akiongea na namba Fulani. Alikuwa akitoa maelekezo ya nini kifanyike katika muda ule. Wana usalama hawakuwa wametulia, kila sehemu walijaa. Mpaka inafika jioni bado hapakuwa na chochote cha maana kilichofanyika. Kila mmoja alikuwa akihisi na kuongea hiki. Ni katika hao mmoja peke take ndiye alikaribia kufahamu ukweli. Suala kwamba aliyeua alikuwa Masimba hilo hakuwa na shaka nalo, lakini angemuaminisha vipi mkurugenzi? Akaona huu ulikuwa wakati wakuliondoa suala hili katika kutuhumiwa kina jimmy na kulihamishia mikononi kwa Masimba. Alitambua kama likiachwa kisha lijekugundulika kwamba waziri alikuwa nyuma ya biashara haramu hata wao wasingepona. Akainuka na kuuendea mlango wa chumba chake. Akaufungua mlango na kutoka nje. Alihitaji kwenda kumuona mkurugenzi wa usalama. Huyu alikuwa mmoja kati ya wale waliompa kazi masimba
[4/12, 17:48] ‪+255 717 808 444‬: Alikuwa ni yule aliyempa masimba kazi ya kufuatilia mzigo wao. Kazi ambayo ndio iliyomfanya masimba kuingia katika matatizo haya , matatizo yakuweka rehani maisha yake kwa kunusurika kulipuliwa pale alipotegewa Bomu kwenye gari. Lakini Leo alikuwa ameamua kuukandamiza msumali wa moto katika kidonda kibichi. Gari yake ya kifahari ikatembea kwa mwendo wa taratibu katika barabara za hili jiji. Mawazo ilikuwa ni kujivua katika hili ambalo kama lingefanikiwa basi wangekuwa sehemu nyingine. Lakini kwa kuwa halikufanikiwa basi aliamua kulitenda hili taratibu na akiwa peke yake. Hakupenda kuwaambia wala kuwashilikisha wenzake. Gari ikaenda kuegeshwa kwenye maegesho ya magari katikati ya jiji la dar es salaam. Akatembea kwa miguu akielekea katikati ya jengo moja ambalo hutumiwa sana na Idara ya usalama wa Taifa. Muda wote aliokuwa akitembea hakuacha kuangalia nyuma, alikuwa akihofu kuwa alikuwa akifuatiliwa. Hata alipogeuka hakumuona yeyote, wala kuona macho yanayomtazama kwa hila. Akaufikia mlango wa jengo hilo , vijana waliokuwa pembeni wakamuangalia sekunde kadhaa kisha wakaonyesha kumuacha aendelee na safari yake. Hawakumuacha tu kwa kumuacha Bali ilikuwa amri kutoka ndani. Akaufungua mlango kisha kuuruhusu mwili wake uingie.. Miguu ikitembea kuelekea ndani kabisa. Macho machache yalimtizama na mengine mengi kumpuuza. Aliamua kufanya hivyo, aliamua kuusema ukweli ili ijulikane nani amehusika kuisafirisha roho ya Waziri.

*****

Mdomo wa bastola ulikuwa ukimtizame Teddy. Sura ya mtu asiye na masihara ilikuwa mbele yake. Alimjua masimba kwa mda mrefu, lakini hakuwahi kumuona akiwa katika hali hii. Hasira, chuki, na neno kifo ndio kitu pekee kilichosomeka kwenye USO wa mtu huyu. Macho yake yakashuhudia vidole vikishuka taratibu katika kitufe cha kufyatulia risasi. Teddy akatamani kuongea kitu. Mdomo haukufumbuka na wala maneno hayakutoka. Akabaki kumuangalia masimba katika sina ya upole na kutia huruma. Alikuwa ni mwenye majuto. Hakuweza kuvuta hata sekunde alishuhudia Risasi Ikipita pembeni kidogo ya kichwa chake na kwenda kuchimba ukutani. Teddy Hakuamini Macho yake, Akaporomoka chinu akiuomba msamaha, lakini Masimba hakuwepo pale. Alishaondoka mbele yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom