Riwaya:Mtuhumiwa

Kabla ya kuanza kusoma imebidi niangalie mwenendo ukoje,urosto sio poa
 
Nimepitia kona nyingi hii Riwaya inaishia episode 48 nafikiri mpka tupate kitabu chake tu
 
Anatunyanyasa sana
Hiyo riwaya ina kibali cha kuiuza na kuisambaza, ukiileta huku uwe na kibali la si hivyo ukishtakiwa na ukatiwa ndani itakutoka si chini ya milioni tano.

Mwandishi wa riwaya hiyo alipenda sana kuandika mitandaoni humu, ndiyo maana alifungua ukurasa facebook wenye kuitwa Kona Ya Riwaya. Tena watu wakawa wanajisomea bure kwa siku riwaya tatu tofauti.

Ila hamu ya kuwafanyia watu wema huo tena halipai ulimwisha, akaacha kupost. Chanzo kikiwa ni watu kama mleta huu uzi, anaicopy na kuileta humu au mitandao mingine ilihali hairuhusiwi. Wengine hadi wanauza kabisa, mwishowe mwandishi akaacha kupost riwaya zake. Anaharibu kazi za watu, aandike yake na kuipost aachane na kazi za watu

Huyu mtoa post pia hana yote hii riwaya, ndiyo maana anajifanya maringo akijua pa kupost kumeisha sasa anatafuta sababu ilimradi aache. Na hata kama anayo ataishia jela huyu akifuatiluwa,
 
Riwaya hii ipo mtandaoni kuanzia sehemu ya kwanza hadi 49!! Hivyo basi ni kosa la jinai kupost bila ruhusa ya mwandishi kuanzia sehemu hiyo ya 49!

Nimekujibu ili uone ya kuwa kusitishwa kupostiwa hapa ni sababu maalumu lakini pia nikukumbushe kitu kimoja usipende kuwajaji watu bila kuwauliza ama kuona wametoka nje ya mipaka ya umiliki wa kazi za wengine...
Nina access ya Uwaridi na ni mwanachama wa Uwaridi pia nina hard-copy ya kitabu hiki lakini pia kuwa na nidhamu ya maneno usipende kujionesha kama mkerereketwa wa umiliki wa kazi ikiwa hata leo hii ukienda Kona ya Riwaya kuna post hadi hapa ilipofikia na ndipo iliishia....

Hizi nguvu ungewekeza kumshitaki yule jamaa wa blog ya riwaya mwenye kujaza riwaya za watu bila taarifa ningekuona wa maana sana.

Jiheshimu nawe utaheshimiwa na nimeamua kukujibu kwa sababu mtu wa kwanza kuanza kuipost hapa IAmShedeOne hayupo karibu na ni member hai wa UWARIDI na ndie hupost humu riwaya zote za UWARIDI na hazimalizagi kwa sababu ya haki miliki na kuvuta watu zaidi waipakue App ya Uwaridi.

Nimekujibu kwa sababu nimegundua hujui unachokifanya yani ungelijitambua basi ungeliwambia watu kama kina kulubule waende kule UWARIDI APP wakidhi kiu zao kwa bei ya Tsh 6000/=

jaribu kuwa muungwana hakuna asie jua ugumu wa kazi za kalamu
Mimi ni mwanachama wa UWARIDI pia ni mwandishi wa ndani ya UWARIDI. Ninaongea ninachokijua, usitetee uozo wa huyo jamaa kwa usichokijua. Hiyo screenshot ni Hussein Tuwa mwenyewe wakati namwambia kuhusu uzi huu, nadhani umeona alichokiandika hapo.

Usijifanye unajua kuongea sana ilihali humo ndani ya UWARIDI, jana mwenyewe kasema alushakataza. Maana yake mmiliki akishakataa huna mamlaka ya kuipeleka popote, hata kuiona bure mtandaoni. Hiyo ni intellectual property ina copyright, mwenye kuruhusu ni mwenye hiyo hakimiliki. Keshakataa sasa, unalazimisha nini?

Hakuna kupost kuanzia sehemu ya 49 ndiyo ruhusa wala nini, keshakataa.

Screenshot_20180712-135902.jpg
 
Tangu jana ulipoweka post hii sikutaka kukujibu nikasubir labda IAmShedeOne atajitokeza ila naona kimya basi nakupa mfano wa hii screensho kutoka pm kwangu
Siku nyingine acha kubwabwaja kitu Usichokijua, eti mwanachama wa Uwaridi katiba umeisoma hadi uje kubwabwaja hayo?
Yaani unajipindisha taratibu mbele yangu mimi niliyepo ndani ya Uwaridi, siku nyingine usiongee usichokijua
 
Kaka naona unanivunjia heshima sasa kuwa muungwana kidogo kuwa ndani ya group la Uwaridi sio kujulisha basi walionje si member lakini kikubwa kuwa Uwaridi sio sifa basi ukionekana huko utakuwa milionea

Sina sababu ya kukuwekea vithibitisho eti kisa tu tunabishana
Lakini kubwa naona hauna staha hivyo naomba tuishie hapa as nimekukwaza nisamehe
Chief
Heshima ungeichunga kwa kukaa kimya na kuacha usichokijua na si kuja kuongea mambo ambayo huna ujuzi nayo humu.

Kuwa Uwaridi sijasema ni sifa, nimejitaja baada ya kusema wewe upo humo na ni mwanachama. Maana yake umesajiliwa, huwezi kuwa mwanachama bila usajili. Kibaya zaidi wewe unayejinadi mwanachama unaonesha hujui lolote kuhusu umoja ule, laiti usingeingilia usipopajua basi usingejua mimi ni mwandishi mmojawapo aliyepo ndani ya Uwaridi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom