CHADEMA na Udikteta Makao Makuu

Na hapa unamsema Mkjj kuwa amefanya nini so far. Huo upuuzi unaoutaja hapa ni upi? Ametetea nini kwenye hili so far zaidi ya kuuliza maswali ambayo sio wewe wala wana ccm hapa na wapambe wao wameshindwa kujibu?

Mbona unajichanganya mkuu! Kuwa wazi sio kutoa madai na kuita watu wapuuzi kwa kitu ambacho kinakuonyesha kuwa labda wewe ndio unaweza kuwa kwenye upuuzi zaidi!

tumeshindwa kuelewana sikuwa na maana kuwa mkjj ametetea CHADEMA kwenye hii thread nimemtolea mfano kwa sababu wanamlaumu sana kuwa ni mtetezi wa CHADEMA kama KADA anavyolaumiwa kwa CCM, pole kwa hilo
 
Katika hili nitakujibu hata kama connection yangu hapa nilipo sio nzuri sana. Hebu wewe ambaye unaweza kujua watu ni wa mkoa gani kwa kuangalia majina sema hilo na wala usikwepe hapa.

MwK,
Sitakwambia ukafanye reserch mwenyewe kama ulivyofanya hapo awali, lakini jaribu tu kutembelea hizi page uone hiyo distribution ya madaraka na maeneo watokayo.
http://www.chadema.net/uongozi/sekreta.php
http://www.chadema.net/uongozi/wabunge.php

Taja majina kisha useme unafikiria kuwa wanatoka mkoa gani na kisha tufanye uchunguzi tujue kama kweli hao watu wanatoka mkoa wa kilimanjaro na sio Dar Es Salaam like most of us here as far as I know.

Hapa naona umewadanganya wanaukumbi. Chadema walionyesha matumizi yao ya 2005 tu. Hivi sasa kuna malalamiko kutoka kwa wanachama wao na wameshindwa kuchapisha matumizi yao. This is very unfortunate. Waangalie kwenye hiyo link yao. Ni vema wakaweka wazi zaidi mambo yao, hasa kunapokuwa na utata, kama tunavyokubaliana hivi sasa.
http://www.chadema.net/uchaguzi/gharama.php

MwK, It was a nice debate and hope you took some of my views with you. Cheers

hapa wewe ndiye unadaganya kwa kusema kuwa Chadema hawaweki wazi matumizi yao na kuwaita kuwa wao ni sawa na ccm na kisha wewe mwenyewe unadai kuwa wameweka mapato yao na matumizi ya mwaka 2005. Hii ni tofauti kubwa kabisa na ccm ambao hakuna mtu wa nje ya mtandao anajua mapato yao na matumizi yao. Kwa hili umedanganya na mimi bado niko right.

Zaidi sana nakusubiria utoe majina na useme wanatoka mkoa gani hao wateuliwa wa Chadema. Masaa mengi sana yamepita kuanzia nitoe hili ombi?

Mwafrika wa Kike,
Hebu acha uvivu kidogo na usome hizo pages nilizokupatia. Maeneo ya kila mhusika anakotoka yameandikwa. Kweli waafrika tunachukia kusoma.

Halafu kama posting ya matumizi ya Chadema ya mwaka 2005, tena yenye nia tu ya kuwaumbua CCM, ni valid kwa matumizi ya 2008 na inatatua manung'uniko na makunyanzi ndani ya chama, basi nafikiri hakuna sababu ya kuchapisha tena matumizi yao, milele na milele. CCM kama waliwahi kuchapisha hata kama ni wakati chama kikitwa TANU, basi inatosha hadi leo. Hii argument yako inafurahisha sana.
 
You are making some good points and can even feel your anger/pain. It is true that there are much bigger issues to discuss than what is going on in Chadema, but I think some how tuwe mult-dimensional, tusiache lolote nyuma kwa kukabiliana na moja tu linalotuumiza zaidi.

Mkuu KJ,

Point yako nimeigusa kuwa kama the idea ni ku-balance ishus, basi ziwe ishu za uhakika, tuache uvivu wa kutafuta ishus na kutegemea internent, tuende tutafute real ishus against Chadema, so far sijaiona ya maana ya kuweza kuiweka meza moja na za CCM,

Seif, Lipumba, na Mrema hata wangekuwepo bungeni leo wasingefanya kitu maana wote walishapitwa na wakati, wote walishashika nafasi nzito sana serikalini na CCM, hebu onyesha one thing walichofanya kinachoweza kumshawishi mwananchi kuwa wanafaa? Nothing! Hao nao wajitoe ili kina Duni waingie huko CUF na kuleta akili mpya,

Maneno yako ni kweli, lakini tatizo ni kwamba ishu mnazowashambulia nazo upinzani ni weak sana the matter of fact ni completely none ishus kwa taifa letu, especially at this time, kwa hiyo fanyeni basi home work nzito, otherwise turudi kwenye kumkoma nyani wakuu, kuanzia juzi tumepiga kelele kuhusu Chenge, si umeona leo CCM wajikanyaga, kwa hiyo tuendelee kumkoma nyani wakuu taifa liko njia panda!

Lakini tafuteni ishu za kweli na nzito, hizi za viongozi njaa waliotemwa huko ni none ishus kwa taifa, maana hata kina Tambwe nao walisema hizo hizo, motive yake ni nothing but njaaa ya binafsi, sio ya taifa!
 
MwK,

Tarime inayoshikiliwa na Chadema, imejaa watu wa Tarime, like wise kule Rombo iliyo ya CCM imejaa wa Warombo, au ya Mkoani, Pemba iliyo ya CUF wote ni wapemba na waislamu. Hii ni kutokana na asili ya wakazi walio wengi wa eneo husika.

Lakini kufungia macho kero za wapiga kura kuwa 70% kitaifa ya wabunge wa kuteuliwa, au sekretarieti n.k., n.k. hutokea eneo moja, kuwa sio kasoro ni kujidanganya. Tanzania tumepiga hatua kwenye mambo ya kiukabila lakini sio kuwa tumeyamaliza kabisa. Tribalism is a serious allegation that Chadema has to explain or tackle head on, and not just sweep under the carpet hoping for them to disappear, especially malalamiko yanapokuwapo kwa muda mrefu hadi magazetini.

Ruzuku iliyochapishwa ni ya matumizi ya uchaguzi mkuu 2005 tu, kama ilivyo kwenye http://www.chadema.net/uchaguzi/gharama.php. Uchapishwaji wenyewe unaonekana zaidi kuwa na nia ya kuwaumbua CCM waliokuwa 'allergedly', wametumia $40 billioni, kitu ambacho nafikiri ilikuwa ni kizuri kwa Chadema kufanya. Lakini wasingeishia hapo, ingekuwa rahisi kabisa kwa Chadema kuwakata ngebe wanaolalamika kwa kuweka wazi mtandaoni mgao wa ruzuku wanayopata kila mwaka, ili kila mtu auone unavyotumika. What is wrong with that?? It is transparency that is missing in CCM, and Chadema should capitalise on the CCM's mess instead of joining them.

Unaona sasa. Jitahidi uwe unasoma. Umesema ruzuku iliyochapishwa ni ya matumizi ya 2010 tu? Mbona hii hapa ya 2008 nayo imesemwa?
"Kwa msingi huo tunapenda kuwataarifu watanzania kuwa CHADEMA katika uchaguzi huu tumetumia shilingi milioni 48, milioni 15 ikiwa ni mchango wa chama na milioni 33 ikiwa ni michango ya wanachama"

Halafu ujue kwamba hizi ni za uchaguzi. Kila Kamati Kuu CHADEMA inatoa taarifa ya matumizi. Na mara mbili kila mwaka kwa Baraza Kuu. Jiunge na CHADEMA kama mwanachama utapata? Sasa jiulize lini Chama Cha Mafisadi kimewaeleza wanachama wake matumizi? Halafu soma pia sheria inavitaka vyama kufanya nini.

Ama kwa madai yako ya UKABILA nimekwambia utoa ushahidi wa kwamba sekretariati imejaa wachagga, na kwamba wabunge wa viti maalum wote ni wakilimanjaro. Links ulizozitoa zote zimeonyesha sivyo. Ukweli ni kuwa ukitazama majina ya watendaji makao makuu; wasukuma ni wengi zaidi. Tumbo, Mnyika, Sabula, Shija, Kafulila nk. Na kwenye viti maalum, ni kweli watu wenye asili ya uchagga ni wengi lakini si wote. Wako sita; wenye asili ya kilimanjaro ni wanne, na wawili wana asili tofauti kabisa. Na hata hao wanne wenye asili ya uchagga, aliyetokea kilimanjaro ni mmoja tu; wengine watatu wameteuliwa kutoka Dar es salaam na wanajulikana kabisa kuwa ni wakazi wa DSM miaka na miaka. Inasemekana wawili kati yao hata kichaga hawakijui kabisa

Asha
 
Si kweli kwamba CHADEMA imejaa Wachagga!

Kwa akili za kawaida, shutuma kwamba CHADEMA imejaa wachaga maana yake ni kwamba CHADEMA ina viongozi na wanachama wengi wachagga kuliko kabila lolote hapa Tanzania. Je ni kwa kiasi gani kauli hiyo ina ukweli?.

Katika safu ya juu ya uongozi wa kitaifa wa CHADEMA yenye viongozi sita: wenyeviti na makatibu mchaga ni mmoja tu-Mwenyekiti wa chama Taifa, Freeman Mbowe. Viongozi wengine wanatoka makabila mengine kama MuIraq, Myao, Mpemba na Mu-Unguja.

Aidha katika sekretariati ya chama taifa ambacho ndio chombo kinachosimamia utekelezaji wa kila siku wa shughuli za chama kikiwa na kurugenzi 9, kati ya wakurugenzi wake mchaga ni mmoja tu. Na wasukuma ni watatu. Kwa nini hawasemi kwamba CHADEMA ni chama cha wasukuma?

Kadhalika mpaka sasa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameteua wajumbe wanne wa Kamati Kuu, kati yao hakuna mchaga hata mmoja na kati yao wawili ni wahaya, Profesa Mwesiga Baregu na Balozi Ngaiza. Kwa nini hawakusema kwamba CHADEMA ni chama cha wahaya?

Kwa upande mwingine kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi uliopita, jimbo ambalo CHADEMA iliongoza kwa uwingi mkubwa zaidi wa kura ni Tarime ikiwa asilimia zaidi ya 64. Kama CHADEMA ni chama cha wachaga kwa nini jimbo la kwanza lisingekuwa la mkoa wa Kilimanjaro?

Kati ya majimbo kumi ambayo CHADEMA ilifanya vizuri zaidi, jimbo la Kilimanjaro ni moja tu la Moshi mjini huku mikoa kama Kigoma, Rukwa ikiwa na majimbo mawili ambayo CHADEMA imefanya vizuri zaidi.

Kama CHADEMA ingekuwa chama cha wachaga si ingefanya vizuri zaidi katika majimbo ya Kilimanjaro?

Je, wanataka kutuambia kuwa Mara, Kigoma, Rukwa na mikoa mingine ambayo CHADEMA imefanya vizuri kote kumejaa wachaga?

Kwa mantiki hiyo basi, si kweli kwamba CHADEMA ni chama kilichojaa wachaga. CHADEMA ni chama cha kitaifa. Kinachojumuisha wanachama na wapenzi wa asili na hali mbalimbali.

Soma zaidi hapa:http://www.chadema.net/tamko/2007/mwanri.php
 
Asha,
Inaelekea wewe ni mndani kabisa wa Chadema, jambo ambalo ni zuri na litasaidia kufikisha haya malalamiko.

KJ

Umesema vyama vilipoanzishwa vimeanzishwa kwa malengo ya kikabila, kimajimbo na kidini- PROVE KAMA CHADEMA ilianzishwa kikabila.

PROVE kwamba CHADEMA ilianza na misingi mibaya tofauti na katiba yake.

Hapa nakuletea makala ya Mzee Mtei aliyoiandika mwaka 2005, itakupa historia kiasi ya kuanzishwa kwa CHADEMA.
CHADEMA NI NINI NA NI NANI

Nikiwa Muasisi na Mwenyekiti (Taifa) Mstaafu wa Kwanza wa CHADEMA naona ninawajibika kujibu makala ilioandikwa na H. Nesario iliyokuwa na kichwa cha habari kama hapo juu, na kuchapishwa katika Toleo la Mtanzania Jumapili tarehe 4 Desemba, 2005.

Kuanzishwa kwa Chadema
Ni kweli kwamba wastaafu kadhaa walikuwa miongoni mwa watu waliojiunga nasi kuanzisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo mwaka wa 1992. Lakini kulikuwa na wananchi wa kila rika, taaluma na kazi. Kulikuwa na wanasiasa kama Mheshimiwa Edward Barongo ambaye aliungana na mimi hata kutia saini katika Fomu ya Maombi ya kusajiliwa kwa awali na Mama Mary Kabigi, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania, Mkoa wa Dar es Salaam. Wafanya biashara kama Bwana Medard Mutungi na Kanali Mstaafu Geofrey Marealle walituunga mkono. Wana-ushirika kama Brown Ngwilulupi walijiunga siku zile za mwanzo. Mameneja wa makampuni kama Victor Kimesera, Michael Shang’a na Alphonse Maskini. Vijana kama Freeman Mbowe pamoja na kundi kubwa la wanazuoni kama Lenny Kassoga walishiriki kubuni katiba ya awali. Wanasheria pia walikuwepo, mmoja wao akiwa Bob Makani ambaye alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa kwanza na Mwanaidi Majaar ambaye alikuwa mmoja wa wadhamini wa mwanzo. Wakulima na wafanyakazi, wake kwa waume, walituunga mkono mara tu ilipojulikana kwamba tulikuwa na mpango wa kuanzisha Chama kipya cha siasa sheria itakaporuhusu. Kwa hiyo si kweli kwamba CHADEMA kilianzishwa tu na wastaafu.

Asili ya Misimamo ya Chama
Ni sahihi pia kwamba mimi binafsi nilibahatika kushika nyadhifa za kiserikali kuanzia wakati tulipopata Uhuru, zikiwepo Chief Establishment Officer, mwaka wa 1962, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha 1964, Gavana mwanzilishi wa Benki Kuu, 1966, Katibu Mkuu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, 1974 na mwishowe, Waziri wa Fedha na Mipango. Wadhifa wa uwaziri niliushika mara baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki 1977, nikaendelea hadi wakati wa vita dhidi nduli Idi Amin wa Uganda.

Baada ya vita nilikuwa na msimamo tofauti na ule wa bosi wangu, Rais Mwalimu Julius Nyerere. Tofauti hizi zilihusiana na mikakati ya kufufua uchumi ambao uliathirika sana wakati wa (na hasa kutokana na) harakati za kumfukuza adui kutoka nchi yetu. Uchumi ulidorora pia kutokana na miradi na mashirika mengi ya umma kuanzishwa kisiasa bila uchambuzi yakinifu na kuendeshwa kwa hasara na kutegemea ruzuku kutoka Hazina. Kwa maoni yangu haya yote yalihitaji kurekebishwa kimuundo na kimenejimenti.

Kutokana na mlipuko mkubwa wa bei uliosababishwa na sera zetu za kuendesha serikali na mashirika ya umma, na uzalishaji duni wa bidhaa, thamani ya sarafu ya Tanzania ilikuwa imeshuka sana. Nilikubaliana na ushauri wa I.M.F. na Benki ya Dunia wakati huo kuwa tulihitaji kurekebisha thamani hiyo, pamoja na kutathmini uendeshaji wa miradi na mashirika kadhaa ya umma. Rais Nyerere alikataa kata kata kwamba hawezi kukubali ushauri huo na hata akaamuru ujumbe wa I.M.F. uliokuwa nchini ufukuzwe. Kwa vile niliona msimamo wa bosi wangu ulitokana na watu waliokuwa wanapotosha mambo na haungesaidia kutatua matatizo yaliyokuwa yanakabili taifa letu, nilimwandikia kumuomba ateuwe Mtanzania mwingine ambaye angeweza kuendesha naye uchumi wa nchi yetu. Rais alikubali kujiuzulu kwangu na ndipo nikaacha uwaziri, nikahamia Arusha kuwa mkulima kuanzia 1980.

Kwa hiyo ni hisia za Bwana H. Nesario tu kwamba eti mimi nilikuwa natetea au kusimamia haki za wenye mitaji, ambapo Mwalimu alikuwa anatetea haki za Watanzania masikini. Najiuliza kuendelea kuyapa ruzuku kutoka Hazina mashirika muflisi ni kutetea haki za Watanzania masikini? Huko ni kutoelewa menejimenti fanisi au uchumi! Nesario anahitaji kufunzwa uchumi na menejimenti yenye tija, licha ya kwamba alifanya kazi serikalini mpaka akastaafu. Alikuwa na cheo gani alipostaafu?

Historia ya nchi yetu kuanzia wakati nilipojiuzulu, mwisho wa 1979 imedhihirisha kwamba kama ushauri wangu ungekubaliwa, mambo yangeendelea kwa unafuu zaidi. Nimkumbushe Nesario na wengine wanaoonekana kusahau, kwamba kuanzia mwanzo wa 1980 bidhaa muhimu kwa matumizi ya wananchi wa kawaida zilikuwa adimu sana na Watanzania hasa wa kipato cha kawaida na cha chini, waliteseka sana. Ni wale wakubwa tu waliosafiri nje ya nchi ndiyo walioweza kuleta na kukidhi mahitaji yao.

Sijui Bwana Nesario alikuwa anaishi wapi wakati huu, lakini sabuni, sukari, mafuta ya kupikia, nguo, viatu, karatasi, unga wa sembe na wa ngano, mchele, mafuta ya taa na karibu kila aina ya bidhaa ilikuwa inauzwa kwa kibali au kwa bei ya juu sana. Hata baadhi ya wananchi mashambani walilazimika kuvaa mifuko mitupu ya saruji au ya mbolea! Ilifikia mtu akitoka nyumbani akaona foleni ya watu mbele ya duka alikuwa anajiunga nayo akitarajia mwisho wake angeweza kununua chochote kilichokuwa kinauzwa. Wenye magari hawakuwa wanaruhusiwa kuendesha Jumapili jioni, na petroli ilikuwa inauzwa kwa kibali na kwa bei ya kuruka. Nahisi Nesario alikuwa nje ya Tanzania ndiyo maana anajizungumzia tu bila kuona adha au taabu tuliokuwa tunapata.

Fursa ya kuunda chama mbadala kwa Chama cha Mapinduzi ilitulazimisha tubuni filosofia na sera ambazo zingeepusha taifa kurudia makosa ya zama za ujamaa zenye sera zisizo na tija na uendeshaji wa kiimla. Wananchi ni lazima waweze kuamua mambo yahusuyo maendeleo ya taifa lao kwa uhuru kamilifu, ujasiri na bila ya woga na kuepuka utawala wa kiimla. Rasilimali za nchi ni lazima zitumike kunufaisha wananchi. Serikali ina wajibu wa kuweka mazingira yanayowezesha mitaji kuingia nchini. Uhuru wa soko ndiyo njia endelevu ya kuvutia mitaji ili raslimali za nchi ziweze kutumika kikamilifu, lakini papo hapo lazima umma wote ufaidike na mazingira yawekwe kuhakikisha wananchi wanajituma kwa kadri iwezekanavyo kupata kipato chao wenyewe. Wasiojiweza na ambao hawakupata ajira watadhaminiwa na umma. Miundombinu ya kiuchumi na ya kijamii itamilikiwa na umma na kuendeshwa kisayansi, kuhakikisha ni endelevu na ina tija. Miradi ya umma itabuniwa na kuendeshwa bila pupa za kisiasa. Misimamo kama hii ni ya social democrats na ilitangazwa mapema na CHADEMA. Kama Bwana Nesario aliisoma au kuisikia hangeweza kusema eti kwamba chama hiki kinasimamia mabepari na wenye mitaji. Najisikia mshindi kwamba licha ya CCM kujidai eti ni chama cha ujamaa, wameiga sana misimamo ya CHADEMA kama tulivyoitangaza hapo awali.

Itakumbukwa kwamba licha ya matamshi ya Mwalimu Nyerere wakati wa kukataa ushauri wangu (na wa I.M.F) kwamba hatageuka kutazama nyuma kwani angekuwa “jiwe la chumvi kama mke wa Loti”, sisi CHADEMA tulimpelekea kijitabu cha Sera na Misimamo yetu mwanzoni mwa mwaka 1994. Mwalimu alizisoma na baadaye alitamka hadharani alipokuwa huko Mbeya kwamba sera zetu zilikuwa safi na zingeweza kuwaondolea Watanzania kero zao. Maneno ya Mwalimu yalikuwa “Heri Mtei, Bwana”! Hizo ndizo sera za CHADEMA kimsingi.

Viongozi ni Wanafamilia?

Kuhusu madai ya Bw. Nesario kwamba CHADEMA ni kikundi cha familia ya viongozi, naweza kusema ni uzushi mtupu usiokuwa na msingi wowote. Kama kulikuwa na watu walioniunga mkono ambao wana uhusiano wa karibu na mimi, hii ni kutokana na kwamba wananifahamu kwa kina na walielewa mapema umakini wangu katika upendo wa nchi yetu na uzalendo wangu. Si ajabu kwamba wanaweza kuwa wa karibu kijamii. Hata Baba wa Taifa, ndugu zake wa karibu kama mdogo wake, Joseph Nyerere aliongoza TANU Youth League, shemeji yake, Lawrence Gama alikuwa Katibu Mkuu wa CCM. Kuna ajabu gani kama ndugu wa karibu anaafikiana na kiongozi na kujiunga na Chama chake? Nesario anafahamu kwamba Rais wa sasa wa Zanzibar alilelewa na Hayati Abeid Amani Karume, Rais wa kwanza wa Zanzibar? Mbona hata mwanae Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ni kiongozi katika serikali ya CCM?

Jambo la msingi na muhimu la kuzingatia kama kiongozi ananuia kwa dhati kuwa na chama cha kitaifa kweli kweli, ni lazima ahakikishe uongozi una mtandao wa kitaifa na kwamba yeyote anayechaguliwa au kuteuliwa awe ni yule mwenye uwezo wa kutekeleza majukumu yake. Kama ni uchaguzi uwe ni wa uwazi na wa kidemokrasia. Naweza kujivunia kwamba viongozi wakuu wa CHADEMA wakati nikiwa Mwenyekiti walitoka kona zote za Tanzania Bara: Makamu wangu akiwa Brown Ngwilulupi toka Mbeya, Katibu Mkuu, Bob Makani akitoka Shinyanga, Makamu wake akitokea Mtwara na Mkuu wa Kitengo cha Wanawake akitokea Mbeya. Mwenyekiti wa Vijana alikuwa Freeman Mbowe. Kamati Kuu ilikuwa na wajumbe kutoka mikoa yote. Nasisitiza kwamba kiongozi makini hawezi kubagua watu wenye uwezo na kuwazuia wasichaguliwe eti kwa vile wana uhusiano naye wa karibu.

Mapato ya Chama
Miongoni mwa viongozi wakuu wa Chama kulikuwa na waliokuwa na uwezo kifedha ambao walikifadhili. Mmoja wa hawa ni Bwana Philemon Ndesamburo ambaye sio tu alisaidia sana Mkoa wa Kilimanjaro kama Mwenyekiti, bali hata Dar es Salaam aliweza kutupa ofisi tuliotumia kama Makao Makuu kwa miaka ya mwanzo. Mimi mwenyewe nilikaa Dar es Salaam kwa miaka yote sita nikiwa Mwenye Kiti, bila kulipwa hata senti moja kama mshahara, au kulipiwa kodi ya nyumba. Mara nyingi nilitumia magari yangu binafsi kwa mashughuli ya Chama nikinunua petroli au dizeli bila CHADEMA kunirudishia.

Viongozi karibu wote walijitolea magari yao kwa ajili ya safari za Chama mikoani, mara nyingi bila hata Chama kulipia gharama za petroli. Samani za awali ofisini zilitolewa kama zawadi na wanachama, na hata magari ya kwanza, mengi yakiwa sio mapya yalitolewa kama zawadi na wapenzi wa Chama, miongoni mwao wakiwa ndugu zangu wa karibu. Kama Makao Makuu yalionekana kwamba yanaendeshwa kwa kubana matumizi sana ni lazima ieleweke kwamba mapato yalikuwa finyu kwa vile ada za uanachama hazingeweza kukidhi mahitaji, hasa kwa vile tulitarajia kukua kwa kasi. Pale mwanzo ilikuwa ni lazima kila mwisho wa nwezi kukutanisha Wajumbe wa Kamati Kuu ili kutoa michango kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Chama ambao hawakuwa na kipato kingine.

Licha ya kwamba CHADEMA kimeweza kupata ruzuku kidogo miaka hii ya karibuni, mapato mengi ya Chama yameendelea kuja kutokana na wanachama kujitolea kibinafsi kwa vile ada za uanachama ni kidogo. Kwa hiyo ni lazima kudhibiti matumizi ili wafadhili wa ndani na wa nje waendelee kuwa na imani kwetu. Bwana Nesario anasema kuendesha Chama namna hiyo ni kukiendesha kama kampuni binafsi. Kama kudhibiti matumizi ni kuendesha Chama kama kampuni, basi hilo lilikuwa lengo letu. Anayetaka pesa za dezo na takrima abaki au aende CCM. Tunahitaji wazalendo walio tayari kujitolea kujenga chama mbadala kwa CCM.

Kueneza Chama Nchini
Licha ya unyonge wetu, kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 1995, tuliweza kuwa na matawi katika kila wilaya, na mimi nikiwa Mwenyekiti niliweza kutembelea wilaya zote Tanzania Bara isipokuwa Ukerewe, Ngara na Makete. Itakumbukwa pia kwamba, kabla ya Bwana Augustine Mrema kuingia upinzani, CHADEMA kilikuwa ndicho Chama cha upinzani kilichoongoza kwa ukubwa na wingi wa wanachama. Itakumbukwa pia kwamba CHADEMA kilishindwa tu kuchukua kiti cha Ubunge cha Kigoma-Ujiji katika uchaguzi mdogo wa 1994 kutokana na mbinu chafu za CCM. Mahakama ya Rufaa ilibatilisha uchaguzi wa Azim Premji wa CCM na jimbo hilo lilibaki wazi mpaka Mhe Aman Walid Kabourou wa CHADEMA alipochaguliwa katika uchaguzi mkuu wa 1995.

Uamuzi ambao uliathiri mtandao wa CHADEMA kitaifa ni ule wa kumuunga mkono Augustine Mrema wa NCCR-Mageuzi mwaka 1995 na kumpigia debe ili awe Rais. Makubaliano baina ya CHADEMA na NCCR-Mageuzi ya kuachiana majimbo yalipuuzwa na Mrema na alifanya kampeni nchi nzima akisema yeye alikuwa “shoka” na NCCR-Mageuzi walikuwa “mpini”, kwa hiyo Mbunge wake lazima awe mwana-NCCR-Mageuzi. Matokeo yake wana-Chadema waliopania sana kuwa wabunge walihamia NCCR katika dakika za mwisho wakitazamia kwamba kimbunga cha Mrema kingewavusha. Baadhi yao waliweza kuwa Wabunge, lakini kwa tiketi ya NCCR.

Wale tulioamini katika misimamo ya CHADEMA tulipania kukiimarisha baada ya ule Uchaguzi ambao ulitutupa katika nafasi ya tatu. Kuna rafiki yangu ameniambia kwamba kosa langu kuu la kisiasa ni lile la kumuunga Augustine Lyatonga Mrema mkono mwaka wa 1995. Nakubaliana na huyu rafiki, lakini pia mimi ni mtu ninayeheshimu maamuzi ya wengi, na ni CHADEMA waliamua kwa kura nyingi kidemokrasia na kwa uwazi kumuunga mkono Mrema.

Mrema hakudumu NCCR-Mageuzi, na baadhi ya wana-CHADEMA waliohamia NCCR walirejea chamani kwetu na wengine wakamfuata T.L.P. Hao wataangamia naye kisiasa kwa vile mahali alipo Mrema mihadi haiheshimiwi. Uchambuzi wa Bwana H.Nesario kuhusu chaguzi za 1995 na 2000, na waliochaguliwa Rombo, Vunjo, Moshi Vijijini, Moshi Mjini, Hai, Siha n.k. haukugusia uvurugaji wa mtandao wetu wa viongozi kutokana na Mrema kutojali makubaliano. Hata hivyo, naamini kwamba wazalendo walio makini wamejiunga sasa na CHADEMA na kwamba wanasiasa wengi wazalendo wa kweli wanaonuia kwa dhati kuboresha maendeleo ya nchi yetu, wataendelea kuimarisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika safari yake ya kuwa Chama tawala.

Kuimarisha mtandao wa CHADEMA nchi nzima ulianza tena kwa ari mpya mwaka 2004, hasa baada ya Bwana Freeman Mbowe kuchaguliwa Mwenyekiti na Dkt. Willibroad Slaa kuwa Katibu Mkuu. Wakishirikiana na Wabunge wengine wa CHADEMA wameweza kuweka mtandao imara na tumeweza kuweka wagombea wengi katika majimbo ya ubunge na udiwani kuliko wakati wote wa historia yetu pamoja na Freema Mbowe mwenyewe kama Mgombea wa kiti cha Urais.

Kuhusu Mgombea Mwenza

Kukerwa kwa Bw. Nesario na uteuzi wa Mama Anna Komu kuwa Mgombea Mwenza kwa maoni yangu kunaonyesha mawazo ya Mfumo Dume wa kizamani na uliopitwa na wakati. Hakuna mtu anayeweza kusema Mama Komu si mzaliwa wa Zanzibar. Kwa hiyo kisheria na kikatiba ana haki ya kugombea. Eti kwa vile ameolewa na mwananchi wa Tanzania Bara, basi anyimwe haki yake. Mbona hata Bwana Salmin Amour alioana na mwanamke wa Bara? Kuna mtu ameweza hata kutaja kwamba hakustahili kuwa Rais wa Zanzibar? Mbona Mama Magimbi aliyekuwa kiongozi wa Upinzani kati ya 1995 na 2000 alikuwa mzaliwa wa Zanzibar lakini ameolewa na Mtanzania wa Bara? Kuna yeyote isipokuwa Nesario ambaye angeweza kusema eti Mama Maghimbi hangestahili kuwa Makamu wa Rais endapo chama chake kingemteua na kikashinda? Mantiki za akina Nesario ni za ufinyu.

Uwakilishi wa Wanawake

Sio kweli kwamba ni mtu mmoja alichagua na kuandaa orodha ya Wakina mama wa CHADEMA watakaoingia Bungeni kwa uwiano wa kura. Mimi niliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa jopo la wanachana waliochambua sifa za kila aliyeomba na tulitumia vigezo vya kisayansi kufikia orodha hiyo. Sijui huyu Nesario alipata wapi uvumi huo kuwa ni mtu mmoja alitayarisha hiyo orodha.

Kuhusu Kampeni za Sasa

Nafajirika sana na jinsi kampeni za sasa zilivyoendeshwa kwa ubunifu wa hali ya juu na kwa uchambuzi wa kina wa matatizo yanayolikabili taifa letu. Hii iliwakera wakina Nesario mpaka wakalaumu Mtei na Ndesamburo kwa kuchangia. Nesario hata kaota ndoto kwamba ninaye mwanangu huko Marekani ambaye anasaidia kukusanya misaada na kuipelekea CHADEMA. Kwa wale watu wanaofadhaika na kukosa usingizi kutokana na CHADEMA kuwa tishio kwa CCM, mimi sina mtoto anayeishi Marekani. Wanangu niliowaacha Marekani kumalizia masomo baada ya kazi yangu kama Mkurugenzi wa I.M.F. wamerudi nyumbani; wa mwisho akiwa amerudi miaka saba iliyopita. Swali la kujiuliza ni kwa nini Nesario ameamua kuwa mzushi?

Edwin I. M. Mtei
P.O. Box 967
ARUSHA
 
Bi. Asha pole sana, majibu uliyotoa yametolewa hapa mwaka mmoja na ninakuhakikishia miezi michache ijayo atakuja mwingine na madai yale yale. Sasa utachoka wangu, next time ni bora kuwapatia link tu maana wengine ni wavivu hata kubonyeza keyboard kutafuta majibu wao wenyewe. Ukiwaambia nenda kwenye tovuti inakuwa kama umewatumia kisimani kuchota maji!
 
Unaona sasa. Jitahidi uwe unasoma. Umesema ruzuku iliyochapishwa ni ya matumizi ya 2010 tu? Mbona hii hapa ya 2008 nayo imesemwa?
"Kwa msingi huo tunapenda kuwataarifu watanzania kuwa CHADEMA katika uchaguzi huu tumetumia shilingi milioni 48, milioni 15 ikiwa ni mchango wa chama na milioni 33 ikiwa ni michango ya wanachama"

Halafu ujue kwamba hizi ni za uchaguzi. Kila Kamati Kuu CHADEMA inatoa taarifa ya matumizi. Na mara mbili kila mwaka kwa Baraza Kuu. Jiunge na CHADEMA kama mwanachama utapata? Sasa jiulize lini Chama Cha Mafisadi kimewaeleza wanachama wake matumizi? Halafu soma pia sheria inavitaka vyama kufanya nini.

Ama kwa madai yako ya UKABILA nimekwambia utoa ushahidi wa kwamba sekretariati imejaa wachagga, na kwamba wabunge wa viti maalum wote ni wakilimanjaro. Links ulizozitoa zote zimeonyesha sivyo. Ukweli ni kuwa ukitazama majina ya watendaji makao makuu; wasukuma ni wengi zaidi. Tumbo, Mnyika, Sabula, Shija, Kafulila nk. Na kwenye viti maalum, ni kweli watu wenye asili ya uchagga ni wengi lakini si wote. Wako sita; wenye asili ya kilimanjaro ni wanne, na wawili wana asili tofauti kabisa. Na hata hao wanne wenye asili ya uchagga, aliyetokea kilimanjaro ni mmoja tu; wengine watatu wameteuliwa kutoka Dar es salaam na wanajulikana kabisa kuwa ni wakazi wa DSM miaka na miaka. Inasemekana wawili kati yao hata kichaga hawakijui kabisa

Asha

Heshima Mbele Asha,

Nashukuru kwa maelezo yako ingawa hata hivyo bado hayatatui madukuduku yaliyomo ndani ya baadhi ya wanachama na wapenzi wa Chadema. Naomba uelewe haya mawili;
  1. Hakuna matumizi yoyote yaliyopo kwenye www ya Chadema zaidi ya yale ya uchaguzi wa mwaka 2005 ambayo yaliwekwa zaidi kuiumbua CCM. Kama yapo nipe link ili tumalizane. Malalamiko yaliyotolewa ni kuwa, mikoani hawapati ruzuku ukilinganisha na makao makuu. Hili ndio la kujibu. Kama matumizi ni uchaguzi tu, basi Chadema hawatashinda hata siku moja, maana mpiga kura huandaliwa mikoani kabla ya uchaguzi.
  2. Kuhusu ukabila, hili liko wazi na ndio maana linapigiwa kelele mwaka hadi mwaka. Kama Chadema wanataka kulifumbia macho, ni juu yao, lakini lipo. Wewe mwenyewe unakiri kuwa kati ya wabunge 6 wa kuteuliwa, 4 wanatokea ya Kilimanjaro, kwa hiyo kama huoni kuwa hili ni doa, basi huwezi kuona mengine. Si unajua tena ukipenda hata chongo inakuwa ni kengeza.
Mwanakijiji amesema vema, ingawa alikuwa na nia ya kukutetea lakini badala yake ameelezea yanayokusibu, kuwa kila wakati haya masuala yatakuzukia, kwa sababu moja tu, hayajarekebishwa. Mzee Mtei atasema asemalo, lakini ukweli utabaki pale pale kuwa, wakati wake Chadema kilikuwa ni chama cha kikabila zaidi na ngome yake ilikuwa Kilimanjaro tu, mpaka Kaborou alipoigombea Kigoma.

Muhimu ni kuwa, ikubalike tu kuwa tatizo lipo na linahitaji ufumbuzi. Chadema ni chama kichanga na isingekuwa rahisi kikawa a national party over night, hili linaeleweka. TZ ilikubikwa na msululu wa vyama wakati vilipoanzishwa kwani waanzilishi hawakuweza kukubaliana kutofautiana. Walichoweka mbele ni ubinafsi wao kwanza, huku wakipeperusha makaratasi ya Demokrasia. Ndio maana vyama vikuu vyote, isipokuwa NCCR kabla ya Mrema, vilikuwa identified na makundi fulani, kijimbo na kidini.

Bahati nzuri ni kuwa, hii awamu ya pili ya viongozi ambao wengi wao wamevikuta hivi vyama na hawafungwi sana na ubinafsi wa waanzilishi labda ndio watakaoviokoa hivi vyama. Lakini hii haina maana kuwa mizizi na ushawishi wa waasisi haupo, la hasha, bado upo na ndio maana unaona kunakuwa na mapungufu hayo yaliyorithiwa tokea awali.

Asha, kama unaiombea mema Chadema, basi pigia debe ili hayo yanayopigiwa kelele yatatuliwe badala ya kujitahidi kuyakingia kifua, kinyume na hapo, yatarudi kulalamikiwa kila kukicha maana wanachama nao wana macho na masikio. Tunahitaji Chadema ya kutukomboa, sio Chadema ya kutugawa zaidi.
 
Heshima Mbele Asha,

Nashukuru kwa maelezo yako ingawa hata hivyo bado hayatatui madukuduku yaliyomo ndani ya baadhi ya wanachama na wapenzi wa Chadema. Naomba uelewe haya mawili;

Hakuna matumizi yoyote yaliyopo kwenye www ya Chadema zaidi ya yale ya uchaguzi wa mwaka 2005 ambayo yaliwekwa zaidi kuiumbua CCM. Kama yapo nipe link ili tumalizane.

Hii statement kwenye red ndiyo inakuonyesha jinsi usivyo na hoja bali viroja. Yaani wewe CHADEMA kuweka mapato na matumizi yake kwenye mtandao ni kuiumbua CCM na sio kuwa wazi.

Kwa hili umeonyesha ni mtu wa namna gani so keep exploding maana umenipa sababu ya kukamata chupa nyingine ya pepsi!

Malalamiko yaliyotolewa ni kuwa, mikoani hawapati ruzuku ukilinganisha na makao makuu. Hili ndio la kujibu. Kama matumizi ni uchaguzi tu, basi Chadema hawatashinda hata siku moja, maana mpiga kura huandaliwa mikoani kabla ya uchaguzi.

Hao watu wa Tarime na Kigoma walishinda vipi? Kwa argument yako basi CHADEMA ingeshida Dar na sio mikoani? Mkuu unaaibisha hadi inatia huruma!

Kuhusu ukabila, hili liko wazi na ndio maana linapigiwa kelele mwaka hadi mwaka. Kama Chadema wanataka kulifumbia macho, ni juu yao, lakini lipo. Wewe mwenyewe unakiri kuwa kati ya wabunge 6 wa kuteuliwa, 4 wanatokea ya Kilimanjaro, kwa hiyo kama huoni kuwa hili ni doa, basi huwezi kuona mengine. Si unajua tena ukipenda hata chongo inakuwa ni kengeza. Mwanakijiji amesema vema, ingawa alikuwa na nia ya kukutetea lakini badala yake ameelezea yanayokusibu, kuwa kila wakati haya masuala yatakuzukia, kwa sababu moja tu, hayajarekebishwa.

Hili limekuonyesha ulivyo na chuki za kikabila na vikorosho vya ubaguzi. Jana nilikuuliza uweke majina unayosema kuwa ni ya mkoa wa Kilimanjaro na hukufanya hivyo. Hivi unawezaje kujua kabila la mtu kwa kuona jina lake?

Mbona hao waliotajwa ni watu waliokulia Dar es salaam na wote wanajulikana zaidi kama wana darisalama kuliko hiyo mikoa wewe unayotaka kuwapandikizia.

Babu punguza chuki za kikabila utakuwa na maisha marefu kidogo!

Mzee Mtei atasema asemalo, lakini ukweli utabaki pale pale kuwa, wakati wake Chadema kilikuwa ni chama cha kikabila zaidi na ngome yake ilikuwa Kilimanjaro tu, mpaka Kaborou alipoigombea Kigoma.

Katika hili umekamatwa ukidanganya mchana kweupe na sasa wewe mwenyewe umejithibitishia jinsi usivyo na data. Poor guy, mwaka 1995, Bob Makani aligombea jimbo la Shinyanga mjini. The last time I checked, yeye ni miongoni wa viongozi wa mwanzo wa Chama na pia kati ya waliokieneza chama mikoani kuchuana na NCCR.

Get your facts utaabika hapa mzee!

Muhimu ni kuwa, ikubalike tu kuwa tatizo lipo na linahitaji ufumbuzi. Chadema ni chama kichanga na isingekuwa rahisi kikawa a national party over night, hili linaeleweka. TZ ilikubikwa na msululu wa vyama wakati vilipoanzishwa kwani waanzilishi hawakuweza kukubaliana kutofautiana. Walichoweka mbele ni ubinafsi wao kwanza, huku wakipeperusha makaratasi ya Demokrasia. Ndio maana vyama vikuu vyote, isipokuwa NCCR kabla ya Mrema, vilikuwa identified na makundi fulani, kijimbo na kidini.

Hizi statement zinakuabisha mzee bora utulie tuli maana ni wewe tu waliokuwa paranoidi huko ccm ndio mnajaribu kuleta issue kuwa chadema ni chama cha wachaga huku facts zikionyesha vinginevyo. Na kama kawaida ya JF, utafunuliwa hadi moyo wako wenye chuki za kikabila na uongo wenye udaku ndani yake uwekwe hapa kwa kila mtu kuona!

Bahati nzuri ni kuwa, hii awamu ya pili ya viongozi ambao wengi wao wamevikuta hivi vyama na hawafungwi sana na ubinafsi wa waanzilishi labda ndio watakaoviokoa hivi vyama. Lakini hii haina maana kuwa mizizi na ushawishi wa waasisi haupo, la hasha, bado upo na ndio maana unaona kunakuwa na mapungufu hayo yaliyorithiwa tokea awali.

Asha, kama unaiombea mema Chadema, basi pigia debe ili hayo yanayopigiwa kelele yatatuliwe badala ya kujitahidi kuyakingia kifua, kinyume na hapo, yatarudi kulalamikiwa kila kukicha maana wanachama nao wana macho na masikio. Tunahitaji Chadema ya kutukomboa, sio Chadema ya kutugawa zaidi.

Wewe na chuki zako za kikabila ishia huko huko ccm kwenye wizi na ufisadi huku mkitafuta namna ya kuwagawa watanzania kama vile ilivyofanyika kwa Dr Salim Ahmed Salim!

Katika hili, ushauri wako wa kinafiki unafutwa na chuki zote zile ulizozionyesha hapo juu!

Next ........
 
Heshima Mbele Asha,

Nashukuru kwa maelezo yako ingawa hata hivyo bado hayatatui madukuduku yaliyomo ndani ya baadhi ya wanachama na wapenzi wa Chadema. Naomba uelewe haya mawili;
  1. Hakuna matumizi yoyote yaliyopo kwenye www ya Chadema zaidi ya yale ya uchaguzi wa mwaka 2005 ambayo yaliwekwa zaidi kuiumbua CCM. Kama yapo nipe link ili tumalizane. Malalamiko yaliyotolewa ni kuwa, mikoani hawapati ruzuku ukilinganisha na makao makuu. Hili ndio la kujibu. Kama matumizi ni uchaguzi tu, basi Chadema hawatashinda hata siku moja, maana mpiga kura huandaliwa mikoani kabla ya uchaguzi.
  2. Kuhusu ukabila, hili liko wazi na ndio maana linapigiwa kelele mwaka hadi mwaka. Kama Chadema wanataka kulifumbia macho, ni juu yao, lakini lipo. Wewe mwenyewe unakiri kuwa kati ya wabunge 6 wa kuteuliwa, 4 wanatokea ya Kilimanjaro, kwa hiyo kama huoni kuwa hili ni doa, basi huwezi kuona mengine. Si unajua tena ukipenda hata chongo inakuwa ni kengeza.
Mwanakijiji amesema vema, ingawa alikuwa na nia ya kukutetea lakini badala yake ameelezea yanayokusibu, kuwa kila wakati haya masuala yatakuzukia, kwa sababu moja tu, hayajarekebishwa. Mzee Mtei atasema asemalo, lakini ukweli utabaki pale pale kuwa, wakati wake Chadema kilikuwa ni chama cha kikabila zaidi na ngome yake ilikuwa Kilimanjaro tu, mpaka Kaborou alipoigombea Kigoma.

Muhimu ni kuwa, ikubalike tu kuwa tatizo lipo na linahitaji ufumbuzi. Chadema ni chama kichanga na isingekuwa rahisi kikawa a national party over night, hili linaeleweka. TZ ilikubikwa na msululu wa vyama wakati vilipoanzishwa kwani waanzilishi hawakuweza kukubaliana kutofautiana. Walichoweka mbele ni ubinafsi wao kwanza, huku wakipeperusha makaratasi ya Demokrasia. Ndio maana vyama vikuu vyote, isipokuwa NCCR kabla ya Mrema, vilikuwa identified na makundi fulani, kijimbo na kidini.

Bahati nzuri ni kuwa, hii awamu ya pili ya viongozi ambao wengi wao wamevikuta hivi vyama na hawafungwi sana na ubinafsi wa waanzilishi labda ndio watakaoviokoa hivi vyama. Lakini hii haina maana kuwa mizizi na ushawishi wa waasisi haupo, la hasha, bado upo na ndio maana unaona kunakuwa na mapungufu hayo yaliyorithiwa tokea awali.

Asha, kama unaiombea mema Chadema, basi pigia debe ili hayo yanayopigiwa kelele yatatuliwe badala ya kujitahidi kuyakingia kifua, kinyume na hapo, yatarudi kulalamikiwa kila kukicha maana wanachama nao wana macho na masikio. Tunahitaji Chadema ya kutukomboa, sio Chadema ya kutugawa zaidi.

MwK,
Hebu punguza jazba kidogo na kusoma tena ujumbe wangu kwa uangalifu ili ujibu hoja badala ya kuendeleza mayowe. Mimi ni Mdanganyika, sishabikii chama chochote kama mwenzangu ambaye umemchagua Mrema. Kama uteuzi wenye ratio ya 4 out of 6 kiukabila sio controversial basi tunaweza ku-ignore wanaolalamika, otherwise Chadema ni vema wakarekebisha hiyo hali. Halafu narudia tena kuwa, matumizi yaliyotangazwa na Chadema ni ya mwaka 2005 tu. Kingine cha muhimu ni kuangalia statement ya mwisho kabisa kwenye hiyo page ya matumizi, kuhusu CCM, ili uelewe kwa nini matumizi hayo yaliwekwa na pengine kwa nini mengine hayajawekwa wazi hadi leo ambapo wanachama mikoani wanalalamika.

Gharama za Kampeni Uchaguzi Mkuu 2005 - Chadema
http://www.chadema.net/uchaguzi/gharama.php

Mapato
1. Ruzuku kutoka Serikalini 22,770,712
Agosti mpaka Novemba
2. Michango ya Wanachama na Wapenzi wa Ndani 246,723,543
3. Michango ya Wahisani wa Nje ya Nchi 83,500,000
Conservative Party
4. Mikopo ya Wanachama na Wapenzi wa Ndani 399,574,543
Jumla 752,568,798

Matumizi
1. Gharama za Helikopta 223,030,726
Kukodisha helikopta 186,500,800
Mafuta ya helikopta 31,057,786
Vibali, Kodi viwanja vya ndege, Uendeshaji n.k. 5,472,140
2. Kampeni kupitia vyombo vya habari 60,576,450
Malazi, chakula na posho za waandishi wa habari 21,186,050
Matangazo kwenye luninga, radio na magazeti 39,390,400
3. Nyenzo za Kampeni 61,363,660
Machapisho - mabango, vipeperushi 51,113,500
Nyenzo za kampeni - bendera, fulana 8,580,000
Gharama za uchapishaji Makao Makuu 1,670,160
4. Gharama za Vikao vya Uteuzi 87,386,659
Kura za awali (Primaries) 43,490,959
Kamati Kuu, Baraza Kuu & Mkutano Mkuu 43,895,700
5. Misaada ya fedha taslim kwa Wagombea Ubunge 59,250,000
6. Gharama za Usafiri 160,558,084
Kukodisha magari 35,580,000
Kununua magari 79,200,000
Matengenezo ya magari 15,867,850
Mafuta ya magari 26,725,234
Usafiri wa ndege 3,185,000
7. Uendeshaji wa Makao Makuu kipindi cha Kampeni 17,500,000
8. Gharama za kuendesha mikutano 68,615,000
Kukodisha vipaza sauti 44,095,000
Kununua Majenereta kwa ajili ya mikutano 17,720,000
Kununua vipaza sauti kwa Wagombea Ubunge 6,800,000
9. Gharama za Simu/Mawasiliano 1,112,000
10. Gharama za Mazishi 1,300,000
11. Posho za Watendaji wa Kampeni 7,780,000
12. Malazi na chakula kwa Watendaji wa kampeni 5,021,826
13. Gharama nyinginezo 292,100
Jumla 753,786,505

Chama cha Mapinduzi kimepata kigugumizi na kimeshindwa kukanusha tuhuma kwamba kilitumia zaidi ya shilingi bilioni 40 (40,000,000,000,000) katika kampeni za Uchaguzi wa 2005. Aidha, Chama cha Mapinduzi kimekuwa kikipinga kwa nguvu zake zote mabadiliko yeyote kwenye sheria za uchaguzi ambayo yataweka ukomo wa matumizi ya fedha katika kampeni. Huu ni mkakati wa makusudi kabisa wa chama hiki cha mafisadi wakuendelea kung'ang'ania madaraka kwa kuhakikisha uchaguzi hauwi wa huru na haki.

Sasa ulichohakikisha hapa ni nini hasa?

Nimekushauri uachane na chuki ya kikabila na utareason zaidi ya kutoa mambo ambayo sio tu yanakanusha unachosema, bali pia yanakufunua zaidi ulivyo - unataka kuanzisha issue out of nothing!

Next ......
 
Mzee Halimoja ni mtetezi wa miaka mingi wa Chadema lakini kwa kuuweka ukweli huu imekuwa ni msaliti anatumiwa na Rostam au Ccm naona pia huyu mzee ndio Mswahili,Kada Mpinzani au Chinga.

Kitila na Mwanakijiji.

huyu mzee mnadharau leo wakati katoa mchango mkubwa sana kwenye NGO ya mzee Mtei, kuliko nyinyi ambao mmefuata Wallet ya Mbowe.

lazima mje kutetea ujinga wenu hapa kwa mfano pesa alizopewa Mwanakijiji kufungua website na karedio kake ni Ruzuku ya chama inayozungumzwa na Mzee Halimoja.

mnataka kutuambia kuwa Mbowe au Mtei ni malaika?

Inajulikana na tumesema sana humu kuwa Chadema ni chama cha kichagga kilianzishwa na wachagga waliokufukuzwa BOT hata Trustees waasisi wanaonesha wazi kuwa ni chama cha kikabila.

Mbowe kapewa uenyekiti na baba mkwe wake mzee Mtei baada ya kumuoa Lilian Mtei.

Mnyika anatoka kilimanjaro si Iringa ni single parent wa kipare.

kuna wakurugenzi wa JF bwana Kitila na Mwanakijiji wanalipwa ruzuku hizo hizo, ndio maana wamekuwa wakali kwa hili la Mzee Halimoja na limeelezwa sana humu.

mzee Ndesamburo (mchagga) kalazimisha mtoto wake apewe ubunge wa viti maalum kupitia Chadema ilihali si mpenzi wa siasa, alichokifanya Ndesamburo ni sawa alivyofanya Mtei kulazimisha mkwe wake(Mbowe) awe mwenyekiti.

maneno ya ubaguzi wa kikabila kayasema sana Wangwe nae katumwa na RA?

Huwezi kusema uongo kuwa Msafiri Mtemelwa ana sauti sawa na Ndesamburo, Mbowe au Mtei.

lazima watakuja juu kutetea ujinga huo kwani wengi wao wanaishi kwa ruzuku ya Chadema mfano Mwanakijiji na Kitila bila kumsahau Ngurumo, wanajua kuwa pesa wanazopewa na MBOWE ni jasho la Chadema hili ndio fungu la makao makuu linalolalamikiwa.
Mnyika amekuwa akipeleka Invoice feki huo ndio uhuni wa genge la makao makuu ya Chadema.

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=10807&page=22

Ukisikia bangi na kuhishiwa hoja kwa ccm soma kinachoandikwa hapa na mswahili!
 
Poa tu yote maisha ulitaka niwe wapi? au ulitaka nile ruzuku za makao makuu ambazo wewe unapata?

Ulirudishwa kwa ufisadi sasa utakoma kuringa maana kesi dhidi yako inaandaliwa! Watu kama wewe mnatumainiwa na serikali na kuwekwa nchi za nje kisha mnaaibisha watanzania.... grrrrr
 
Sasa ulichohakikisha hapa ni nini hasa?

Nimekushauri uachane na chuki ya kikabila na utareason zaidi ya kutoa mambo ambayo sio tu yanakanusha unachosema, bali pia yanakufunua zaidi ulivyo - unataka kuanzisha issue out of nothing!

Next ......

MwK,
Nashukuru sana kwa kunifahamisha kuwa kuhubiri usawa ni chuki ya kikabila. I hope huo ni msimamo binafsi na sio wa Mh. Mrema na TLP kwa ujumla. Ila sitabadilisha msimamo wangu kuwa kuteua wabunge wanne (4) kati ya sita (6) kutoka mkoa mmoja ni upendeleo na sio Demokrasia. Hii ina maana kuwa kati ya hao wabunge 6 wa kuteuliwa, Kilimanjaro ina wawakilishi (4) na the rest of the country inawakilishwa na wawili (2) tu. MwK tuwe wakweli na kuacha ushabiki wa kitoto.
 
Mimi nimekuuliza swali rahisi sana lakini naona unakimbia kama vile sijui nini. Nimekuomba utaje majina ya wabunge wa kuteuliwa wa CHADEMA, kisha utaje mikoa au makabila yao maana mimi sina utaalamu huo wa kujua hili.

Simple and clear
 
Mkuu KJ,

Point yako nimeigusa kuwa kama the idea ni ku-balance ishus, basi ziwe ishu za uhakika, tuache uvivu wa kutafuta ishus na kutegemea internent, tuende tutafute real ishus against Chadema, so far sijaiona ya maana ya kuweza kuiweka meza moja na za CCM,

Seif, Lipumba, na Mrema hata wangekuwepo bungeni leo wasingefanya kitu maana wote walishapitwa na wakati, wote walishashika nafasi nzito sana serikalini na CCM, hebu onyesha one thing walichofanya kinachoweza kumshawishi mwananchi kuwa wanafaa? Nothing! Hao nao wajitoe ili kina Duni waingie huko CUF na kuleta akili mpya,

Maneno yako ni kweli, lakini tatizo ni kwamba ishu mnazowashambulia nazo upinzani ni weak sana the matter of fact ni completely none ishus kwa taifa letu, especially at this time, kwa hiyo fanyeni basi home work nzito, otherwise turudi kwenye kumkoma nyani wakuu, kuanzia juzi tumepiga kelele kuhusu Chenge, si umeona leo CCM wajikanyaga, kwa hiyo tuendelee kumkoma nyani wakuu taifa liko njia panda!

Lakini tafuteni ishu za kweli na nzito, hizi za viongozi njaa waliotemwa huko ni none ishus kwa taifa, maana hata kina Tambwe nao walisema hizo hizo, motive yake ni nothing but njaaa ya binafsi, sio ya taifa!

Good points, bado CHADEMA hawajashika usukani kwa hiyo issue zao sio nzito kama zile zilizoibuliwa na Slaa, Zito na wengine. Vile vile sio guarantee kwamba watashinda uchaguzi ujao.

Tatizo ni hawa vibaka ambao wanakula pesa ya walipa kodi kwa ridhaa ya CCM.
 
Back
Top Bottom