Riwaya: Mke wa Rais

Riwaya: Mke wa Rais

MKE WA RAIS

SEHEMU YA 44

Mwanamke Mweupe akatokea mbele yake tabasamu mdomoni.. Huyu hakuwa mwingine bali Inspekta Ummu Sammy. Alikuwa akisogea kwa mwendo wake wa Madaha.. Alipomfikia Mudy Wakasalimiana kwa kupeana mikono kisha wakaongozana mpaka sehemu ambayo ilikuwa maalumu kwa Maongezi.. Muda wote macho ya Mudy hayakutulia sehemu moja.. Yalikuwa yakitambaa na kuangalia kila kona ya chumba kile. Uwepo wa waziri wa mambo ya ndani kulimpa wasiwasi mkubwa kwa kuwa alifahamu kuwa alikuwa mmoja kati ya wanaopanga mkakati wa kufanya mapinduzi.. Kwahiyo kila alipokuwa akiongea na Inspekta Ummu Sammy macho yake yalikuwa yakitizama kwa hila katika kila dirisha na kila kona.. Alihitaji kufanya mAongezi na Afande Ummu Sammy lakini kila alipokuwa akitizama mazingira hayakumpa Ujasiri wa kufanya hivyo kwa kuwa hapakuwa Salama Zaidi... Wakati akiendelea kuongea hiki na kile bila kuonyesha Chochote cha maana mara simu Ya Inspecta Ummu Samy ikaita kuonyesha kuwa kulikuwa na Sms imeingia.. Mudy Bado alikuwa akiendelea kutizama nje Huku akimtupia jicho la chati Inspekta. Akamuona Inspekta Ummu Akiifungua simu yake na kuanza kuusoma ujumbe Ulioingia.. Punde uso wake ukapoteza Ile furaha.. Alionyesha kuwa na Wasiwasi katika macho Yake... Ingawa alijitahidi sana kujikaza, lakini alikuwa ameshachelewa kwani MUDY tayari alikwisha kigundua kitu kutoka kwake... Lakini Kabla hajaongea naye, akamuona Ummu Sammy akiinuka na kuufungua mlango Kisha kutoka Nje ya Chumba kile.. Mudy akaduwaa karibia dakika moja.. Mabadiliko katika Sura ya Afande Ummu Sammy yalimshangaza.. Hakuwahi kumuona Ummu akiwa na Wasiwasi na Yeye.. Hata walipokutana kule Cuba katika Mafunzo Ya Kijasusi hawakuwahi kufichana kitu, lakini hiki kilichotokea Muda Mfupi uliyopita kilimpa mashaka makubwa sana.

Akainuka na kuchungulia Huku na Huko.. Kwa mbali akamuona Ummu akiongea na Vijana wawili ambao walionyesha kuwa na wasiwasi Sana Huku Ummu Akigeuka kila wakati kutizama ndani Ya Ofisi Zao alipomuacha Mohamedi.. Mudy hakutaka kuchelewa kutoka ndani Ya Chumba kile.. Alichokifanya nikuinuka na kuuendea mlango, akaufungua kisha akatoka nje taratibu kwa kupitia Mlango wa Nyuma Ya Jengo.. Alipotoka Nje akawapita Askari Wawili Watatu kisha akapita uchochoro Huu na Ule Muda Mfupi baadae alikuwa ameshatoweka maeneo Ya polisi.

Alitembea kwa miguu safari hii akitaka kufanya Uchunguzi wake kuhusu kile ambacho kimewaleta Arusha.. Lakini kabla ya kufanya hivyo alichoamua ni Kuelekea Sanawari Eneo ambalo alikuwa akiishi mtu fulani ambaye alimjua Sana Mohamedi huku Mohamedi Akishindwa kumjua ni nani hasa. Hakuna kitu ambacho Mudy alikipenda kama kuitwa Sehemu na mtu ambaye hakumfahamu... Michezo ya Hatari kwake kilikuwa ni kitu cha kawaida na hata ikitokea Akaumizwa basi Yeye Huchukulia kama Bahati Mbaya kazini. Alijikagua hapa na pale.. Bastola Zake Mbili Zilikuwa zimetulia Sehemu husika huku upande Wa pili kukiwa na kisu Chake kikubwa ambacho alipenda sana kukitumia. Aliporidhika kuwa Yupo na kila kitu Chake akaianza Safari kuelekea Sanawari.

*****

upepo mwanana ulikuwa ukivuma na Kuwaburudisha watu waliokuwa wameketi sehemu wakipata moja moto moja Baridi.. Walikuwa watu wachache sana katika ukumbi ule lakini machoni kwa Jenifer Ulionekana ni Ukumbi wenye watu wengi sana.. Aliingia pale akiwa kama wateja Wengine. Leo hii alikuwa katika Jeans Matata Sana iliyoubana mwili wake, huku juu akitupia Tshirt Nyeupe pamoja na Raba nyeupe miguuni. Alipoingia alikwenda kukaa sehemu, akaagiza mishkaki mitano pamoja na Chupa kubwa ya Maji kisha akaomba aletewe na Ugali kidogo. Wakati akiendelea kusubiri Oda yake iletwe.. Akawaona wanaume wawili Wakiingia pale ukumbini.. Walikuwa ni Wanaume Aliyowajua sana.. Wanaume wale walipoingia waliangaza Huku na huko walipoonyesha kuridhika na Alichokuwa wakikitizama.. Wakaamua kuvuta viti na kukaa.. Ingawa walikuwa wamekaa lakini walikuwa hawaonyeshi Utulivu wa Macho yao.. Kila wakati walikuwa wakiangalia upande Fulani Huku wakati mikono Yao ikiwa Mifukoni.. Jenifer akavutiwa na Kilichokuwa kikitokea kwa watu wale.. Kila walipokuwa wakiangalia kule, Jenifer Naye alikuwa akipeleka Macho Yake Kwa Chati... Kila walichokuwa wakikifanya Jenifer alikuwa akitizama lakini muda wote hakufanikiwa kukiona kilichokuwa kikiangaliwa. Akiwa na Shauku ya kuona chochote, akashangaa Kumuona Mohamedy Akiingia akiwa Ametangulizana na Mwanadada Mrembo sana.. Akahamisha Macho Yake kumtizama Mohamedi.. Macho Yao Yakakutana! Wote wakatabasamu, lilikuwa tabasamu na Ishara fulani... Mudy Akazuga kutomuona Jenifer.. Akaendelea na Safari Yake.. Punde walikuwa wakivuta viti na kutaka kukaa lakini kabla hawajafanya Hivyo wakaingia Askari Wakiwa na Bunduki na kuongoza mpaka aliposimama Mohamedi..

'''Unahitajika kituoni Mohamedi, tunaomba tuongozane Muda huu na Usijaribu kufanya lolote kwa kuwa hutaweza Kurudi Dar es salaam Ukiwa hai'' ilikuwa Sauti Ya Inspekta Ummu Akimwambia Mohamedi.. Mohamedi Alimtizama Askari Yule kwa Muda kisha Kwa Kujiamini akamwambia.. NeNda nitakuja
Endeleaa baba kukiwashaaa
 
TE="Blaki Womani, post: 17523457, member: 38228"]Nimesoma hapo kwenye DIMBWI LA DAMU nikamkumbuka nameless girl 😀
Upo Na mumewe hapa kwahiyo usishangae,nimeachiwa na mkwe wangu BEN MTOBWA[/QUOTE]

urithi mzuri huo.......toeni kitabu pamoja na wife kitakuwa bomba sana
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 42

Mbele Ya macho Yake karibu na mlango wa kutokea akamuona mtu aliyemfahamu sana.. Alikuwa mtu ambaye alimshangaza kwa muonekano wake.. Hakuwa kusikia popote kuwa ameugua wala hawakuwa kumuona akiwa kichaa.. Sasa mbona huyu ni kichaa? Kengele Ya tahadhali ikagonga katika kichwa Chake. Akaendelea kutembea huku akimwangalia kijana Yule.. Kijana Ambaye Alikuwa kichaa wa kutupwa. Alipomfikia karibu Mudy akampita kwa kumtupia Jicho.. Macho Yao yakakutana.. Mudy Akauona mshtuko kutoka kwa kijana Yule.. Lakini hakumpa nafasi zaidi ya kumshangaa.. Mudy akapotea mfano wa kivuli kwenye chochoro Za Mji wa Arusha. Akaibukia katika meza ya muuza magazeti, akachukua magazeti kadhaa kisha akaondoka na Kurudi Zake Hotelini.. Aliupitia Ufunguo kwa mhudumu yule kisha kuongoza moja kwa moja kuelekea Chumbani kwake. Kitendo cha kukutana na vijana kadhaa kutoka Usalama Wa Taifa wakiwa wamezagaa kwenye jiji la Arusha kulimpa picha kuwa tayari mambo yamekucha hasa kutokana na Mauaji yaliyotokea Usiku Uliyopita. Akafungua mlango na kuingia chumbani kwake.. Alipoingia tu akahisi kuwa chumba chake kiliingiliwa na mtu kwani alikikuta kikiwa kimepekuliwa kwa Utaalam Wa Hali ya Juu, ambao kwa mtu wa kawaida Asingeweza kuligundua hilo. Akachunguza huku na Kule aliporidhika kuwa mpekuaji HakuChukua chochote, akatulia kitandani na kuanza kusoma vichwa vya habari vya Magazeti Yale...

******

alifumbua macho yake kutoka katika usingizi mzito.. Usingizi ambao hakuwahi kulala hata Siku moja.. Baada ya kufumbua macho yake akaanza kutizama Huku na Huko.. Akajikuta Yupo sehemu ngeni machoni mwake.. Sehemu ambayo hakuwahi kufika. Taratibu akaanza kuangalia Huku na Huko.. Alikuwa akitizama ili kukumbuka pale alipo... Alikuwa akitizama kuangalia uwezekano wa kuondoka.. Lakini hapakuonyesha ubaya, wala hapakuonyesha kile ambacho alikitegemea labda. Bado hakuwa katika kukumbuka vizuri.. Hapa niko wapi? Hatimaye akajiuliza.. Alitarajia kuziona pingu mikononi mwake, lakini hakuliona hilo.. Badala Yake alijishangaa baada ya Kujikuta yu Uchi wa Mnyama akiwa kitandani.. Akajikagua sehemu Zake kuangalia kama hajaingiliwa.. Alipokuta kila kitu kipo salama, sasa Akaanza kuvuta kumbukumbu Ya kilichotokea.. Akajaribu kuinua kichwa lakini maumivu Aliyojisikia kutoka nyuma ya kichwa chake Yakaanza kumpa kumbukumbu.. Kumbukumbu Ya kilichotokea katika Ukumbi Ule.. Ghafla mwili ukamsisimka baada ya kulikumbuka pigo alilopigwa wakati pale taa za ukumbi ule Zilipozimwa... Akakumbuka alipokuwa akitizamana na Mdomo wa bastola.. Mwisho akakumbuka pale alipoamshwa na Mtu.. Mtu Ambaye Alimtajua Wakati ule... Mtu ambaye kwa Wakati huu bafo hakuwa Akimkumbuka tena.. Akainuka na Kusimama katikati Ya kioo na kujitizama huku na huko.. Hakuwa mwingine, alikuwa ni Jenifer akiamka kutoka katika Usingizi Mzito.. Akasogea mpaka Sehemu fulani katika nyumba Aliyolazwa.. Akavikuta vitendea kazi Vyake Vyote Vikiwa vipo sawa sawia.. Bastola zake mbili.. Zilikuwa Zimetulia kabisa. Akaichukua na kuitizama.. Ilikuwa bado na Risasi Zake kamili.. Punde Mlango Ukagongwa...

Ulikuwa ukigongaji ambao aliutambua.. Akalitwaa taulo ambalo lilkuwa pale kitandani.. Akalitwaa na Kulitupia Maungoni Mwake.. Akapiga hatua kuelekea Mlangoni huku umbo lake matata likiruka na Kucheza cheza.. Basyola Yake Ilikuwa Imetangulia Mbele Kama Tai... Akaungiza ufunguo mahala pake.. Mlango Ukatii kwa kufunguka.. Akakutana na tabasamu la Mohamedi... Hakujali kama alikuwa na taulo kiunoni wala hakujali kuwa ndani hakuwa na Nguo Yoyote.. Aliufungua mlango Zaidi na Kuruhusu Mudy Kuingia ndani... Baada Ya Mudy Kuingia, Jenifer Aliufunga mlango na Kusogea mpaka karibu na Mohamed. Akasimama huku akinuangalia Mudy kwa Macho Yenye maswali Mengi... Mudy akaendelea kutabasamu huku wakiangaliana. Yalikuwa Macho Ya kazi.. Macho Ambayo Yaliongea kila kitu ambacho kilitokea Usiku Wa Jana.

*****

Kanali jamila na luteni Sevenlee walikuwa ni kati ya wapelelezi ambao walikuja Arusha kwa sababu ya kumdhibiti Mudy.. Wao hawakuwa katika Kile kikosi kilichotumwa kutoka Dar es salaam Ili kuongeza nguvu katika kukabiliana na mauaji ambayo yalianza kuutikisa Mji Wa Arusha..
Kutokana na Hilo na kuogopa kuonekana walikuwa wakijaribu kila wakati Kujibadilisha. Kujibadilisha kwao kulitokana na ukweli kuwa hawakutaka kuonekana wala Kujulikana na wanausalama wenzao.. Muda Mwingi walikuwa wakiutumia kwa kuvaa Sura Za bandia. Mchana Huu Uliwakuta wakiwa katika Hoteli Moja Ya kifahari wakionekana ni Watu tofauti na waliokutana hapo kwa ahadi Zao. Walikuwa wakiongea huku kila wakati Macho Yao yakizunguka katika eneo la Hoteli.. Wana usalama waliozagaa katika Hotel Zote kuliwapa Tahadhali Kubwa Sana.. Hivyo walikuwa wakiishi kwa kuhakikisha kuwa hawashtukiwi kwa Muda wote Ambao watautumia kuwepo Arusha. Lakini Wakati Wakilizungumza na Kulipanga Hilo.. Wakamuona Mudy Akiingia pale Hotelini... Alikuwa peke yake.. Akaongoza Moja kwa Moja mpaka Sehemu Ya Chakula.. Wao wakainuka na kutoweka lakini punde wakarud
Story nzuri ibra
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 44

Mwanamke Mweupe akatokea mbele yake tabasamu mdomoni.. Huyu hakuwa mwingine bali Inspekta Ummu Sammy. Alikuwa akisogea kwa mwendo wake wa Madaha.. Alipomfikia Mudy Wakasalimiana kwa kupeana mikono kisha wakaongozana mpaka sehemu ambayo ilikuwa maalumu kwa Maongezi.. Muda wote macho ya Mudy hayakutulia sehemu moja.. Yalikuwa yakitambaa na kuangalia kila kona ya chumba kile. Uwepo wa waziri wa mambo ya ndani kulimpa wasiwasi mkubwa kwa kuwa alifahamu kuwa alikuwa mmoja kati ya wanaopanga mkakati wa kufanya mapinduzi.. Kwahiyo kila alipokuwa akiongea na Inspekta Ummu Sammy macho yake yalikuwa yakitizama kwa hila katika kila dirisha na kila kona.. Alihitaji kufanya mAongezi na Afande Ummu Sammy lakini kila alipokuwa akitizama mazingira hayakumpa Ujasiri wa kufanya hivyo kwa kuwa hapakuwa Salama Zaidi... Wakati akiendelea kuongea hiki na kile bila kuonyesha Chochote cha maana mara simu Ya Inspecta Ummu Samy ikaita kuonyesha kuwa kulikuwa na Sms imeingia.. Mudy Bado alikuwa akiendelea kutizama nje Huku akimtupia jicho la chati Inspekta. Akamuona Inspekta Ummu Akiifungua simu yake na kuanza kuusoma ujumbe Ulioingia.. Punde uso wake ukapoteza Ile furaha.. Alionyesha kuwa na Wasiwasi katika macho Yake... Ingawa alijitahidi sana kujikaza, lakini alikuwa ameshachelewa kwani MUDY tayari alikwisha kigundua kitu kutoka kwake... Lakini Kabla hajaongea naye, akamuona Ummu Sammy akiinuka na kuufungua mlango Kisha kutoka Nje ya Chumba kile.. Mudy akaduwaa karibia dakika moja.. Mabadiliko katika Sura ya Afande Ummu Sammy yalimshangaza.. Hakuwahi kumuona Ummu akiwa na Wasiwasi na Yeye.. Hata walipokutana kule Cuba katika Mafunzo Ya Kijasusi hawakuwahi kufichana kitu, lakini hiki kilichotokea Muda Mfupi uliyopita kilimpa mashaka makubwa sana.

Akainuka na kuchungulia Huku na Huko.. Kwa mbali akamuona Ummu akiongea na Vijana wawili ambao walionyesha kuwa na wasiwasi Sana Huku Ummu Akigeuka kila wakati kutizama ndani Ya Ofisi Zao alipomuacha Mohamedi.. Mudy hakutaka kuchelewa kutoka ndani Ya Chumba kile.. Alichokifanya nikuinuka na kuuendea mlango, akaufungua kisha akatoka nje taratibu kwa kupitia Mlango wa Nyuma Ya Jengo.. Alipotoka Nje akawapita Askari Wawili Watatu kisha akapita uchochoro Huu na Ule Muda Mfupi baadae alikuwa ameshatoweka maeneo Ya polisi.

Alitembea kwa miguu safari hii akitaka kufanya Uchunguzi wake kuhusu kile ambacho kimewaleta Arusha.. Lakini kabla ya kufanya hivyo alichoamua ni Kuelekea Sanawari Eneo ambalo alikuwa akiishi mtu fulani ambaye alimjua Sana Mohamedi huku Mohamedi Akishindwa kumjua ni nani hasa. Hakuna kitu ambacho Mudy alikipenda kama kuitwa Sehemu na mtu ambaye hakumfahamu... Michezo ya Hatari kwake kilikuwa ni kitu cha kawaida na hata ikitokea Akaumizwa basi Yeye Huchukulia kama Bahati Mbaya kazini. Alijikagua hapa na pale.. Bastola Zake Mbili Zilikuwa zimetulia Sehemu husika huku upande Wa pili kukiwa na kisu Chake kikubwa ambacho alipenda sana kukitumia. Aliporidhika kuwa Yupo na kila kitu Chake akaianza Safari kuelekea Sanawari.

*****

upepo mwanana ulikuwa ukivuma na Kuwaburudisha watu waliokuwa wameketi sehemu wakipata moja moto moja Baridi.. Walikuwa watu wachache sana katika ukumbi ule lakini machoni kwa Jenifer Ulionekana ni Ukumbi wenye watu wengi sana.. Aliingia pale akiwa kama wateja Wengine. Leo hii alikuwa katika Jeans Matata Sana iliyoubana mwili wake, huku juu akitupia Tshirt Nyeupe pamoja na Raba nyeupe miguuni. Alipoingia alikwenda kukaa sehemu, akaagiza mishkaki mitano pamoja na Chupa kubwa ya Maji kisha akaomba aletewe na Ugali kidogo. Wakati akiendelea kusubiri Oda yake iletwe.. Akawaona wanaume wawili Wakiingia pale ukumbini.. Walikuwa ni Wanaume Aliyowajua sana.. Wanaume wale walipoingia waliangaza Huku na huko walipoonyesha kuridhika na Alichokuwa wakikitizama.. Wakaamua kuvuta viti na kukaa.. Ingawa walikuwa wamekaa lakini walikuwa hawaonyeshi Utulivu wa Macho yao.. Kila wakati walikuwa wakiangalia upande Fulani Huku wakati mikono Yao ikiwa Mifukoni.. Jenifer akavutiwa na Kilichokuwa kikitokea kwa watu wale.. Kila walipokuwa wakiangalia kule, Jenifer Naye alikuwa akipeleka Macho Yake Kwa Chati... Kila walichokuwa wakikifanya Jenifer alikuwa akitizama lakini muda wote hakufanikiwa kukiona kilichokuwa kikiangaliwa. Akiwa na Shauku ya kuona chochote, akashangaa Kumuona Mohamedy Akiingia akiwa Ametangulizana na Mwanadada Mrembo sana.. Akahamisha Macho Yake kumtizama Mohamedi.. Macho Yao Yakakutana! Wote wakatabasamu, lilikuwa tabasamu na Ishara fulani... Mudy Akazuga kutomuona Jenifer.. Akaendelea na Safari Yake.. Punde walikuwa wakivuta viti na kutaka kukaa lakini kabla hawajafanya Hivyo wakaingia Askari Wakiwa na Bunduki na kuongoza mpaka aliposimama Mohamedi..

'''Unahitajika kituoni Mohamedi, tunaomba tuongozane Muda huu na Usijaribu kufanya lolote kwa kuwa hutaweza Kurudi Dar es salaam Ukiwa hai'' ilikuwa Sauti Ya Inspekta Ummu Akimwambia Mohamedi.. Mohamedi Alimtizama Askari Yule kwa Muda kisha Kwa Kujiamini akamwambia.. NeNda nitakuja
Mudy jamaan sijui atatoka
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 47

Mudy akatabasamu, kisha akainuka na kuongoza kuelekea alipoambiwa. Alikuwa akitembea bila wasiwasi wowote.. Licha ya kujua kuwa anafuatiliwa lakini bado aliupa ubongo wake Utulivu.. Utulivu ambao aliuhitaji sana katika kazi yake ya Hatari. Akauvuka mlango wa kuelekea ndani Ya hoteli ile.. Alipouvuka akaongoza moja kwa moja mpaka sehemu husika.. Alianza kuhesabu chumba kimoja baada ya kingine. Alipokifikia Chumba namba 14 B akakipita kama hakuwa na umuhimu nacho. Akaendelea na Safari kuelekea upande Mwingine.. Wakati akiumaliza upande wa chumba kile, akahisi kusikia vishindo vya mtu.. Hakujipa kazi Ya kugeuka bali aliongoza kama hakuhisi kitu. Kila alipokuwa Akisonga ndivyo vile vishindo vilivyozidi kusikika.. Mudy Akageuka kwa Silika Ya Aina Yake bastola ikiwa tayari Mkononi kulipua.. Macho yake yakagota kwenye mguu wa mtu uliyokuwa ukipotelea kwenye kona.. Mguu ambao alihisi ulikuwa wa mwanamke.. Akarudi na kuendelea na safari.. Tayari kengere ya Hatari zilikuwa zikigonga ovyo katika kichwa chake.. Alitambua uwepo wa mtu sehemu Husika.. Alijua kuhusu kufuatwa kwake na uwepo wa mtu nyuma yake.. Licha Ya kulifahamu Hilo hakuwa na Wasiwasi.. Hakuwa na wasiwasi kwa kuwa alikuwa akitembea huku akijuwa kuwa kulikuwa na watu au Mtu akimfuatilia kutoka mahala fulani..

Mwisho wa safari yake ilikuwa ni katika Vyoo vya Hoteli Ile.. Akaviendea Vyoo vya wanaume.. Akakichagua kimoja na kuingia ndani. Baada ya kuhakikisha hapakuwa na Mtu, akazichomoa bastola Zake mbili na kuziangalia.. Punde akaisikia miguu ya mtu ikisogea pale nje ya Vyoo... Akatega sikio Zaidi.. Bado Mtu Yule aliendelea kusimama pale nje... Mudy akajiandaa kwa Hadaa.. Akaufungua mlango kwa kasi Ya Ajabu huku bastola Mkononi. Lakini kile ambacho alikitarajia hakukiona.. Nje hapakuwa na mtu wala kiumbe Chochote.. Akashangaa kwanza na akili kuhama kwa umbali fulani.. Alikuwa akichezewa mchezo.. Alikuwa akichezewa na mtu ambaye alikuwa na uhakika alimfahamu yeye.. Ni wakati akiwa amezubaa akitizama Mbele Akahisi uwepo wa Mtu mbele Yake.. Akageuka tena kwa Kasi.. Lakini mara hii Hakufanya alichotegemea... Akiwa amegeuka akiwa ameshikilia Bastola Mkononi akajikuta akikutana na Mapigo mawili ambayo Yalitua mkononi kwa Mudy, Bastola Zote Zikaanguka Chini.. Mudy akajiweka sawa Tayari kwa mapambano, mapambano Ambayo hakujua anapambana na Yupi... Akainua macho Yake kumwangalia kiumbe anayetaka kupambana naye.. Macho Yake yakakutana na macho Ya mwanamke.. Alikuwa mwanamke haswa kwa muonekano.. Lakini Macho yao yalipokutana na kuangaliana kwa muda kila mmoja akamsoma Mwenzake.. Kila mtu aliisoma fani Ya mwenzake kupitia Macho Yake.. Kila mmoja alimtambua mwenzake kuwa yu mwalimu katika mapambano ya kutumia mikono na ni mtaalamu katika mapambano Ya kutumia Silaha.

Mudy Alikuwa akitazamana na Revina Michael.. Mwanadada kutoka Shirika la Kijasusi la Rwanda.. Alikuwa ni Mtulivu akimuangalia Mohamedi katika namna ya kumlazimisha kukisoma kitu katika Macho Yake.. Naam, Mudy akakisoma na kukiona kile kilichondani Yake. Hakuogopa wala kuhofia.. Alichokifanya ni kutabasamu.. Tabasamu ambalo lilikuwa kipimo cha mwisho Cha hasira. Kilichofuatia hapo yalikuwa mapigano, mapigano ambayo yalikuwa na ufundi wa hali ya Juu.. Kila mmoja alikuwa akionyesha yeye ni nani katika medani Ya sanaa ya kimapigano.. Zikapita dakika mbili kila mmoja akiwa hajaruhusu kuguswa na Mwenzake.. Mudy hakuwa Mjinga wa kutumia kila alichonacho.. Alichokifanya ni kuchanganya mapigo fulani ya Kirusi na Kimarekani ambayo yalionyesha kupanguliwa kiustadi na Mwanadada Yule.. Akaona Muda wake Ukipotea Bure.. Akabadilisha mapigo na kuanza kutumia Martial Combart.. Yalikuwa mapigo Yenye mchanganyiko wa kijeshi hasa yakitumiwa sana na Makomandoo wa Kirusi, kimarekani na hata Majasusi Wa CIA na wale wa FBI... Ni Mapigo matano Yaliyoweza kumlevya na kumuangusha REVINA MICHAEL..akabaki akitweta pale Chini akimuangalia Mohamedi..

Ni wakati Huo wakitizamana mvua ya Risasi ikavurumishwa kuelekea pale walipo.. Mudy alikuwa amechupa huku na Revina alikuwa amechupa kule.. Hapo ndipo Mudy aliposhuhudia Shabaha na Utaalam Kutoka kwa mwanadada Yule.. Alikuwa akirusha risasi kwa utaalamu wa kipekee, alikuwa akirusha Risasi akizunguka hewani.. Na hata Alipokuja kutua Chini hapakuonekana kuwa na binadamu Aliye hai.. Wote walikuwa wapo chini wametambarajika katikati Ya madimbwi Ya damu... Mohamedi akatabasamu na kumpa Dole Gumba, Revina naye akafanya hivyo... Wote wakainuka na Kuondoka katika Namna ya kila mmoja na Njia Yake. Mudy hakutaka kurudi pale Hotelini bali aliondoka kupitia Mlango wa Nyuma huku Revina Akirudi Chumbani kwake kwa maandalizi fulani ambayo alitaka kuyafanya kabla Hajaondoka kwenda Kwao Rwanda Ndani Ya Siku Inayofuata. Ulikuwa Muda wa Mapambano, Ulikuwa Muda ambao alitamani Kumwambia Mohamedi Ukweli Wote.. Muda ambao alitamani kurudi kwao Rwanda.. Akafungua mlango wa Chumba chake na kuzama ndani. Mbele ya Macho yake akawaona watu wawili
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 48

Akaufungua mlango na kuzama ndani.. Macho yake yakakutana na watu wawili waliokaa kitandani.. Walikuwa mwanaume na mwanamke.. Wote wakimtizama huku mikono yao ikiwa imekamatia bastola.. Revina akaonyesha kutokuwa na mashaka, akaingia kisha kuufunga mlango kwa ndani. Hakuonyesha kuogopa wala kuhofia.. Hofu kwake haikuwepo kabisa. Tabasamu tamu la mtoto wa kinywaranda liliupamba uso wke kana kwamba limetengenezwa mahususi. Akatembea kwa mwendo waKe wa kawaida.. Alionekana kuufurahia ugeni uliyomtembelea Chumbani kwake katika mtindo wa kumfumania. Bado watu wale walikuwa wakimtizama. Bado walikuwa wakiusoma uso na Macho Ya Revina.. Kile ambacho walidhani watakiona kwenye macho yake ndicho ambacho walikutana nacho. Macho yake mazuri kwa kuyatizama hayakuficha kuonyesha kuwa yeye alikuwa ni nani katika Dunia hii.. Hayakuficha kuuonyesha utaalam wake na pia hayakuficha kuwaambia watu wanaomchunguza kuwa yeye hakuwa mtu Wa kuogopa. Revina Akasogea tena na Tena.. Akawafikia karibu watu wale.. Wakajitahidi kutizamana hapa na pale.. Punde mlango ukasukumwa kwa nguvu mtu mmoja akaingia akipiga sarakasi na kuwahi kuizima taa.. Chumba chote kikawa giza.. Kila mmoja alikuwa ameruka na kuangukia upande Wake..

Ukimya wa Ajabu ukajitokeza ndani ya Chumba kile.. Ukimya ambao haukuwapa watu hata nafasi ya kupumua. Kila mmoja alikuwa sehemu yake, alikuwa akiwaza kuondoka pale.. Uingiaji wa kiumbe kile ulioendana na tukio la kuzimwa kwa taa za chumbani kilimduwaza kila mmoja huku Revina akionekana kuduwaa Zaidi. Alijua Mudy alishatoweka katika eneo lile, sasa ni nani aliyeingia chumbani mwake Ukiondoa watu wawili waliokuwemo mwanzo? Ni swali lake hilo ambalo lilimpa Hamu ya kumjua kiumbe Aliyeingia pale ndani.. Lakini hakujua njia gani atumie kumfikia mtu Huyo.. Akaona avute Subira, Subira Ambayo mwisho wake Ungekuwa kuondoka pale. Bado akiwa kwenye lindi la mawazo Huku macho yake yakiangaza kuitafuta nafasi yakuondoka pale. Akausikia mlango ukisukumwa.. Punde akamuona mtu mfano wa kivuli akiingia.. Uingiaji wa Mtu huyu wa pili kulimburudisha Sana Revina.. Uingiaji ambao hakuwahi kuuona hapo kabla. Ingawa kulikuwa na giza na uingiaji wake kuwa mfano wa kivuli, lakini katika macho Ya Revina alimtambua mtu Yule kwa Mapema Sana.. Alimtambua kutokana na kutambua kuwa hakuna mwingine Mtaalam Zaidi Yake.. Alikuwa Mohamedi, Alikuwa Mudy Akiwa amerudi kivingine. Hakuonekana kuwa na papara wala kuhofia kitu. Alionyesha kuingia kanakwamba anaingia Chumbani kwake. Kwanini aingie mfano huu na watu waliopo humu ndani wasimshuti? Kwa nini Arudi hapa Chumbani kwangu wakati Alishaondoka? Wakati akiwaza hilo kukatokea kile ambacho kiliendelea kumsisimua na Kumshangaza.. Mudy Akamuita Revina Kisha kumuita Jenifer.. Hapo ndipo alipogundua kuwa Mohamedi alikuwa na Watu wengine tofauti wanaomsaidia bila kujulikana. Hapo ndipo alipojua kwa nini alipoingia mwanzo watu wale hawakuonyesha matamanio Ya kupambana.. Wakati akiendelea kushangazwa na kinachotokea , taa ikawashwa na Chumba chote kuwa Cheupe. Revina akajikuta Akitizamana na Watu wanne.

Alikuwa Mudy, Jenifer, na Vijana wengine wawili ambao walikuwa ni wasaidizi waliotumwa na Rais kuja kumsaidia Mohamedi. Kati Ya hawa vijana wawili mmoja alikuwa ni Yule aliyekuwa akizozana na Jenifer katika Ukumbu fulani katika kutengeneza mazingira Ya Kumuondoa Mohamed, alipozungukwa na Maadui.

Baada ya wote kutambuana na kupeana mikono.. Wakatakiwa wotoke pale bila kuonekana. Wa kwanza kutoka alikuwa MOHAMED akifuatiwa na Kijana wake.. Akafuatia Jenifer na Mwisho kabisa Alikuwa Revina Na kijana Mwingine.

******

wakati Mohamed Akiondoka katika Hoteli hii pamoja na watu wake, upande wa pili kulikuwa na kikao kizito katika Hoteli fulani katikati ya Jijini la Arusha. Ulikuwa mkutano Uliohudhuriwa na Watu wate wazito katika masuala yao. Mkutano ulikuwa chini ya ulinzi mkali kupindukia. Hakukuwa na mtu yoyote kupita na Hata ulipopita ni lazima uwe Umepekuliwa na wapekuaji kuridhika. Kila aliyekuwa akipita alikuwa ni lazima akaguliwe na kuhojiwa.

Vigogo wengi waliopo kwenye mpango wa kupanga mapinduzi walikuwa kimya katika ukumbi huku kila mmoja akifikiria la kwake katika Moyo Wake. Wengine walikuwa katika Hofu kubwa kutokana na kilichokuwa kikifanywa na Mohamedi. Na Wengine walikuwa katika taharuki hasa kutokana na Mohamedi Kuwaua wenzao ndani Ya Makao Makuu Ya Polisi Mkoa Wa Arusha. Ukumbi ulikuwa Umetulia kila mmoja akimsubiria Mkuu wao. Punde wakasikia sauti Za Viatu virefu Vikiingia. Kila mjumbe akageuza shingo Kuangalia mlangoni.. Wote wakamuona Mwanamke Mrembo akiingia.. Hakuwa Yeye tu, bali alikuwa Amefuatana Mwanamke Mwingine Mrembo Kupindukia. Mmoja walimtambua kuwa ni Mmoja wao, Lakini Mwingine Hawakumtambua. Wote wakamkazia Macho kumwangalia msichana Yule mgeni katika kikao chao.. Kila mmoja alionyesha kuwa na Shauku Ya Kumjua na Kumtambua Mgeni Yule.
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 49

Wajumbe wote wakageuza shingo zao kumtizama mwanadada yule akiingia pale ukumbini. Wote walionekana kujenga maswali katika vichwa vyao.. Hawakuwahi kutambulishwa wala kuambiwa Uwepo wa Mtu huyu.. Mtu ambaye ameingia katika kikao kile kiliosheheni viongozi waandamizi Wa Serikali.. Msichana ambaye hakuonyesha uhatari Wowote katika kumuangalia kwao. Kwanini ameletwa hapa? Na kwanini hatuwahi kuambiwa uwepo wake? Huyu ni nani? Yalikuwa maswali mfululizo yaliosumbua vichwa vya Wajumbe wa Kikao kile. Kila mmoja alikuwa na Shauku ya kumtambua na kumjua alikuwa nani katika kikao hiki nyeti kama Kile. Majibu Yote yalikuwa yakimsubiri mwenyekiti Wa Kikao.. Punde kidogo Mwenye kiti akaingia ukumbini.. Wajumbe wote wakasimama katika kuonyesha heshima kwa kiongozi Wao, lakini mtu mmoja hakuwa amenyanyuka na hakuwa akipiga makofi wala kusalimia kama Wajumbe wengine.. Huyu Alikuwa amekaa akitabasamu.. Na hata wajumbe wote walipokaa bado hakuonyesha kujali. Mwenyekiti akatembea kwa Mwendo wake wa kikakamavu.. Mwendo ambao aliupenda sana tokea alipokuwa Afisa wa ngazi Za Juu katika Jeshi la Wananchi.. Alikuwa mwanajeshi aliyefikia Cheo Cha Uluteni General.. Cheo ambacho kilimfanya kuwa Chini Ya Mkuu Wa Majeshi. Alipofika sehemu alipokaa yule mwanamke, Wakatizamana kwa Muda kisha Wajumbe wote wakashuhudia Mwanamke Yule Akisimama na kutoa Heshima ya kijeshi kisha kukaa tena.

Lilikuwa tukio lililowaburudisha Wajumbe wengi, ile shauku ya kumjua Huyu ni nani ikaongezeka. Kila mmoja alikuwa akiusubiri Utambulisho wa Mwanadada Yule kuliko hata walivyo usubiri Mkutano wao. Baada ya Utaratibu Wote kuwekwa sawa, mwenyekiti alisimama na kuanza kuelezea kila kitu kuhusu kilichotokea Huku akianza na Utamburisho.

'''Ndugu Zangu wajumbe wa kikao hiki. Nadhani kila mmoja anajua kwanini tumeamua kukutana hapa kwa muda huu. Nadhani kila Mmoja anatambua ni Ipi mipango Yetu iliyotufanya Wote tukutane hapa usiku Huu. Lakini kabla Sijaanza kuelezea kile kilichotokea hapa Arusha, kwanza naomba nimtambulishe kwenu Mpiganaji Wetu. Najua Wengini hamumjui mwanadada Huyu lakini hilo sio tatizo.. Huyu mwanadada Anaitwa Revina Michael. Ni mwanadada kutoka katika Shirika la Kijasusi la Rwanda. Huyu ni mwanamke mwenye record katika mapambano Ya kutumia Silaha, mikono na hata Yale ya Ana kwa ana. Ameshiriki mission nyingi za ukombozi wa afrika na Hata kufikia kutunukiwa Tuzo Ya Ushujaa na mshindi wa Tuzo Ya Nobel Kwa Afrika Askofu Desmond Tutu. Kwahiyo nadhani Huyu atakuwa bega kwa bega katika kusaidiana na Vijana wetu kuhakikisha kuwa Mohamed hafiki popote na Lengo letu la kuipindua Serikali hii linafanikiwa.

Tukiachana na Suala la mwanadada Huyu ambaye naweza kumuita shujaa Wa Afrika. Kingine kilichotukutanisha hapa ni kuzungumzia kuhusu mipango Yetu na Wapi ambapo tumefikia kwa nchi wahisani kutuongezea pesa Zaidi ili tuweze kufanyakazi Yetu Vizuri. Wote tunatambua kuwa Tupo katikati ya Mipango Yetu na nchi Nyingi za Ulaya Zimeonyesha kutuunga mkono katika mpango huu. Kwa kutambua hili, kila mjumbe ambaye Ni Kiongozi katika Serikali hii anatakiwa kuwa makini na kunusa kila neno ambalo litaonyesha kuwa na ukakasi katika Safari Hii Ya kimapambano.

Natambua wote tupo katika nia moja, nguvu moja na lenge moja.. Nilazima tusimame tupambane. Ni lazima tuhakikishe Mohamedi Anazuiwa na Kufutiliwa Mbali katika Uso wa dunia Hii.. Ahsanteni kwa kunisikiliza. Nawatakia Mapambano mema na Mipango thabiti katika kulipigania Hili.'' Alimaliza mwanaume Yule kisha akasimama na Kuanza kutoka Nje.

*****
wakati Viongozi wale wakiwa katika kikao katikati Ya Mji wa Arusha.. Huku Upande Wa Pili Mohamed Alikuwa yupo hatua kadhaa kutoka Jengo ambalo lilikuwa likifanyikia Kikao kile. Alikuwa amesimama Sehemu ambayo ilikuwa vigumu kuonekana na mtu kutokana na mavazi ambayo amevaa.. Sauti Kutoka ndani Ya kikao kile alikuwa akiisikia kwa ukaribu zaidi kutokana Na Revina Kuingia Kikaoni Akiwa na vinasa Sauti vidogo mfano wa sindano za kushonea nguo. Sauti ya muongeaji mkuu katika kikao kile haikuwa ngeni masikioni Mwake. Ilikuwa Sauti ambayo alikuwa akiisikia kila siku.. Sauti ya KiongozI Ambaye alikuwa na Dhamana kubwa Katika nchi.. Ilikuwa Sauti Ya Waziri Mkuu. Mohamedi bado hakutaka kuliamini lile.. Akataka kupata Uthibitisho kutoka kwa Jasusi Mwenzake:. Jasusi ambaye alionekana kukubaliwa upande wa pili. Kuisikia Sauti Ya Waziri Mkuu Katika kikao chenye malengo ya hatari kama kile, kilimpa hamu Mohamedi ya kukutana na Waziri mkuu kwa Njia Yoyote. Akaondoka katika Eneo lile katika Uondokaji wa Aina yake.. Alitembea kama babu wa miaka themanini.. Alikuwa amekamata Mkongoja huku Akionekana kutembea kwa Shida kubwa.. Wajumbe wachache Waliokuwa wakitoka hawa kumtupia macho na Hata kama wangemtupia bado Wasingemtambua kutokana na Mavazi Yake. Akaendelea kutembea katika Aina ile ile.. Wakati anataka kuupita uchochoro fulani, akajikuta akivamiwa na WATU, Ghafla Akausikia Ubaridi Wa Mdomo Wa Bastola Ukimgusa kichwani.. TULIA MPUUZI WEWE!
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 50

Akahisi kitu cha baridi kikimgusa kwenye paji lake la uso.. Ulikuwa mdomo wa bastola. Akasikia sauti nzito ikinguruma kutoka nyuma kwake.. TULIA MPUUZI WEWE..

Mohamedi akatulia, alitulia katika namna ya kumpa nafasi aliyemshikia bastola aamini kuwa Hakukuwa na madhara. Ndicho kilichotokea... Watu wale waliamini hakuwa mtu hatari kwao kwa kule kujilegeza na kutii kwake.. Wakalegeza mikono yao.. Wakajisahau kuwa waliambiwa wasimuamini mtu katika Eneo hilo. Wakasahau kuwa waliambiwa wamshuti kila mtu ambaye atapita eneo lile. Wakamuacha kumpa nafasi, walijua ni mzee asiye na madhara.. Hakuwajua kuwa walikuwa wakicheza na kifo.. Hawakujua kuwa walikuwa wakicheza na mdomo wa Mauti.. Hawakujua kuwa Alikuwa Mohamedi, Mohamedi anayesakwa na kutafutwa na kamati ya mapinduzi.. Wakamuweka sawa kutaka kuhoji kwa nini yuko pale.. Hawakuipata nafasi hiyo, hawakupata muda wa kuwa tayari.. Wote walishangaa walipomuona mzee akipaa hewani mithili Ya chui, mshangao wao hawakuumaliza.. Wakajikuta wote wakipiga mweleka baada ya mapigo kadhaa kutoka kwa Mohamedi Kuwaingia sawia.. Hawakuweza kuamka kwa wakati kila mmoja alikuwa chini akiugulia maumivu.. Maumivu ya pigo moja takatifu kutoka kwa Mohamedi.. Hakuwapata nafasi hiyo.. Bastola yake ikakohoa mara nne.. Kikohozi ambacho kiliondoa roho za watu.. Alipomaliza kazi Hakusubiri washtuke, alichokifanya nikuondoke Eneo la tukio kwa kupitia njia ambazo Zisingekuwa Rahisi kugundulika. Akatokomea Mtaani huku akiwa na furaha ya kugundua nani alikuwa nani Nyuma ya Mauaji ya mke Wa Rais na Mpango wa kufanya mapinduzi..

Kwa mara ya kwanza alikuwa amepiga hatua kubwa sana.. Akatabasamu na kucheka kisha kutoweka kabisa tayari kwa maandalizi ya kazi Ya kufa na kupona.

******
wakati Mohamedi akipambana huku, Jenifer na kijana kutoka makao makuu DIDAS RUGIMBANA walikuwa katika mitaa ya jiji la Arusha wakiitafuta Nyumba yenye namba ambazo walipewa na Kepteni George kabla ya Kuuawa. Walikuwa wakitembea huku na huko kama wafanyavyo wapenzi.. Walikuwa wakishikana viuno na wakati mwingine hata kushikana mikono na kubusiana. Kila aliyewaona ama kukutana nao alihisi ni wapenzi.. Wapenzi ambao wanapendana sana. Licha ya kile ambacho walikuwa wakikifanya, lakini bado macho Yao hayakuchoka kutizama kila Jengo lililopo mbele yao.. Wakiwa umbali mfupi kutoka Ulipo ukumbi wa Triple A macho Yao yakakiona kitu ambacho walikuwa wakikitafuta. Ilikuwa Nyumba yenye namba husika. Lilikuwa jumba kubwa sana, jumba ambalo lilizungushiwa ukuta mkubwa ulionakshiwa na Marumaru zenye mfano wa Madini Ya Tanzanite. Ukiondoa hilo, jumba lote lilikuwa limepandwa miti mirefu ambayo ilisababisha uwepo wa Giza Nje ya Jumba lile na ndani Yake.

Nje hapakuonekana na mlinzi au walinzi wa aina yoyote.. Sehemu yote ilikuwa kimya kupindukia. Sehemu yote hapakuonyesha dalili ya kuwepo kwa watu na hata kuishi kwa watu sehemu ile. Jenifer na Rugimbana wakaendelea kuliangalia jumba lile kwa namna ya kutokuwa na Hofu huku wakati Mwingine wakiendelea kukifanya kile walichokuwa wanakifanya ili kuwapoteza Maboya watu ambao wangewahisi ama kuwashtukia. Wakiwa wamelipita jumba lile wakiendelea na safari Yao, mara waKayaona magari Mawili yakitoka katika Jumba lile na kuwapita kwa Mwendo wa kasi Huku ndani Yake wakionekana Watu kibao ambao kwa kuwaangalia tu mavazi Yao, ungejua tu wale ni Special Force.. Lakini Kwa nini wametoka katika jumba lile? Wanahusika vipi na Jumba Hili? Ni mawazo Yaliyopita katika vichwa vyao na kusababisha kupatwa na Hamu kubwa ya kukijua kile ambacho George alikiona mpaka kufikia kuwatuma Wao... Jenifer Akamuangalia Rugimbana kwa Mara Moja, Rugimbana naye Akafanya Hivyo.. Punde kila Mmoja akaingia Upande wake.. Wote walikuwa wakirudi katika jumba lile... Jumba ambalo lilionyesha kuwa na Siri kubwa. Kila mmoja alikuwa ameishikilia bastola yake Mkononi.. Wakati Jenifer akinyata kuelekea kwenye Uzio Wa Jumba lile, kwa mbali Macho yake yakawaona watu wawili wakiwa wamelala Chini.

Ulalaji wao haukuonyesha uhai kabisa.. Akawasogelea watu wale kwa tahadhali Kubwa.. Alipowafikia alishangaa akiwaona wakivuja damu huku wakiwa na matundu Ya Risasi vichwani mwao.. Jenifer akainama na kuugusa mwili wa Marehemu mmoja.. Akaukuta mwili ukiwa Wa Moto Kuonyesha kuwa Muuaji hakuwa mbali na Sehemu Ile. Akaongeza Umakini na kuzidi kutambaa kuelekea kule.. Hatua kumi mbele alikutana na Maiti Wengine wawili.. Hawa walionekana kuvunjwa Shingo. Hisia kuwa Mohamed ndio aliyeifanya kazi ile Zikaanza kumjia Jenifer.. Aliutambua Uuaji wa Mohamed.. Lakini hakuwa na uhakika wa hilo. Akaongeza Umakini huku akiendelea kutembea Nyuma ya Uzia Wa lile Jumba. Mbele kidogo akamuona mtu.. Mtu ambaye alimfahamu sana... Mtu ambaye alikuwa akiuruka ukuta wa jumba Lile.. Ukuta ambao ulionekana kuwa na Nyaya Nyingi na Hatari Sana Za Umeme.. Hakuwa Mwingine Bali alikuwa Mohamedi.. Tabasamu likachanua Usoni kwa Jenifer hasa pale aliposhuhudia maiti Nyingi Zikiwa Zimelaliana..
 
Back
Top Bottom