ibra87
R I P
- Jul 22, 2015
- 5,614
- 5,360
- Thread starter
- #81
MKE WA RAIS
SEHEMU YA 37
Alikuwa na Uwezo wa kuwaua kwa Risasi, lakini Mudy hakupenda kufanya hivyo... Kupita kwa kanali Jamila na luteni Sevenlee.. Kuliirudisha kumbukumbu Mbaya ya kifo cha George katika Kichwa Chake... Akakumbuka kiapo alichokiweka Juu Ya waliohusika na Mauaji ya George. Licha ya kiapo hicho lakini hakutaka kufanya haraka katika kukabiliana na watu wale. Baada ya kupitwa bila kuonekana Mudy alimshika Jenifer Mkono wakaondoka kuelekea katika Hoteli ile ile ambayo walitoka Sevenlee Pamoja na Jamila. Ilikuwa ni faida kubwa sana kupanga sehemu ambayo unajua kabisa Yupo adui yako.. Lakini hapo hapo adui akiwa hafahamu Uwepo Wako. Wakaingia Hotelin kama babu na bibi.. Kufika kwao mapokezi Wakapokewa na mwanadada ambaye hakusita kuonyesha mshangao wake hasa kwa watu ambao alikuwa akiwapokea kwenye Hoteli Yake. Muda mfupi uliyopita alitoka kuwapokea Vikongwe Wawili.. Na muda huu huu tena alikuwa akiwapokea vikongwe wengine tena wakiwa kwenye mavazi kama ya wateja walioingia punde tu.. Hilo lilimshangaza sana.. Lakini mshangao wake haukuwa wake tu, bali ulikuwa mshangao uliogundulika machoni kwa Jenifer na Mohamedi.. Mshtuko ambao hawakuuacha Uende kama ulivyokuja.. Walihitaji kuujua ulikuwa una nini na ulikuja kwa sababu gani... '''vipi mjukuu wangu mbona umeonyesha mshangao baada ya kutuona hapa? Au hatukutakiwa kufika hapa? Lilikuwa swali la Mtego kutoka kwa Mudy...
Mhudumu Yule akamuangalia Mudy Usoni kisha kwa sauti Yake Ya Uchangamfu akajibu.
''Hapana babu, tunawapenda sana watu kama Nyie.. Lakini kuna kitu kimenishangaza na kunishtua Siku Ya leo.''
Mudy akavutiwa na maneno yale .. Akazuga Kuuliza..
''kipi hicho kimekushangaza?''
Mhudumu akacheka tena lakini ndani ya kicheko hicho akanema kitu ambacho kilimvutia Mudy..
''siku ya leo nimepokea wageni wa aina yenu kama sita hivi.. Lakini hawa waliokuja hapa muda mfupi uliyopita ndio walionishangaza''
''Kuku shangaza kivipi mjukuu wangu!?'' hatimaye kwa Mara ya kwanza Jenifer akauliza.
''walikuwa wakionekana kama vijana licha ya mindevu na Mvi walizonazo hasa Yule mwanaume'' akajibu mhudumu wa ile hoteli.
Mudy na Jenifer wakaangaliana kwa sekunde, kisha Jenifer akamshukuru na kumwambia kuwa ilikuwa ni baraka kutembelewa na wazee kama Wao. Baada ya kuupata huo ukweli kutoka kwa Mhudumu yule.. Wakapewa Funguo na kuongozwa mpaka kilipochumba walichochagua.. Wakaingia ndani kwa kuongozwa na Mhudumu.. Baada Ya mhudumu kuondoka Mudy Na Jenifer wakaufunga mlango kisha wakakaa katika sofa ambayo ulikuwa katika chumba kile. Muda mfupi wa kukaa pale.. MUDY akatoa makablasha fulani ambayo alipewa na Mheshimiwa Rais akamkabidhi Jenifer ili ayatazame. Huku Jenifer Akitizama makablasha Yale, Mudy alikuwa ameichomoa simu Aliyopewa na Yule Marehemu kule kibaha. Akaitizama kwa Muda kisha kuiwasha... Muda Mfupi alikuwa akiipekua Simu hapa na pale.. Macho yake yalikuwa Yakiuzingatia Kila Ujumbe anaokutana nao.. Kulikuwa Ujumbe Mwingi Sana kutoka sehemu mbali mbali lakini katika Ujumbe Wote huo alivutiwa na Ujumbe mmoja kutoka kwa Mtu ambaye alikuwa akitumia Jina ambalo kwa kuliangalia tu halikuwa jina Sahihi... Ulikuwa Ujumbe wa kulazimisha kuuawa na kutekwa kwa Baadhi ya Mawaziri Ambao walikuwa wakipinga mpango fulani... Mtumaji Ujumbe Huyo alionekana kuwa na Taarifa nyingi Za Siri..
Hata kuondoka kwa Rais katika makazi Yake na kufichwa sehemu alikuwa akifahamu. Hapo ndipo ambapo Mudy alikuwa na Mashaka napo na pia kuwa na Mashaka na Usalama Wa Rais.. Kila alipokuwa akiendelea kuipekuwa Simu alizidi kukutana na ujumbe ambao uliandikwa kimafumbo.. Mudy hakuwa mgeni wa Maandishi Ya Kijasusi.. Alisoma kama kawaida. Baada ya kumaliza kusoma na Kuridhika Akaizima tena Simu.. Hapo ndipo alipokumbuka kuwa Chumbani mle alikuwa na Jenifer.. Akageuza Shingo kumtizama cha ajabu hakumuona Jenifer.. Alikuwa ametoka bila kumshtua Mohamedi.. Akafika kwenye meza ambapo alikaa Jenifer.. Akakutana na Ujumbe Ulioandikwa.. '''Nimetoka kidogo, nisiporejea tutaonana kesho''' Ulikuwa ni Ujumbe uliyomaanisha kitu.. Kitu ambacho Mohamedi Alikitambua Mapema... Akatabasamu kisha akajisemea Mwenyewe.. Kazi Imeanza... Muda mfupi nae alikuwa akikiacha kile Chumba.. Simu Aliyoipekuwa ilimpa wapi pa kuanzia.. Akatembea kuelekea Mlango wa Nyuma Wa Hotel ile. Hakutaka kusumbuka kuufungua.. Alichokifanya ni kuuruka Ule uzia na kutokea Mtaani.. Akatembea kukifuata kijiwe cha Madereva Wa tax.. Akaingia Kisha Akaomba Apelekwe Triple A... Aliamua kwenda kumsaka Mwanadada Ambaye alihisi atakuwa anaujua ukweli Wote Juu ya mpango wa kumpindua Rais na Yupi mfadhili wa mpango huyo.. Wakati tax ikiendelea kukata Mbuga ndipo akaikumbuka Simu Yake kuwa alitumiwa Sms kipindi alipovamiwa chumbani kwake.. Akaukuta Ujumbe .. Akaufungua na Kuusoma... Kuusoma Ujumbe ule kutoka kusikojulikana kukamfanya Atabasamu.. Ulikuwa Ujumbe Kutoka kwa mwanamke Anayejiita Revina Michael... Akahitaji Kuonana na Mohamedi Katika Hotel Ya Arusha Star Hotel. Mudy akatabasamu.. Gari Ikageuzwa.