Riwaya: Mke wa Rais

MKE WA RAIS



Alipoangalia kwa pembeni Akawaona watu wawili, watu ambao walikuwa wakimtizama Mudy katika namna ambayo kanali Jamila Aliitambua. Muonekano wa watu wale ulimtia mashaka, akajikuta akipatwa na hamu, hamu Ya kuujua Mchezo Mzima.. Sasa Akawa akiwinda ndege Wawili kwa wakati mmoja.. Ndege ambao Hawakuwa katika kutambua kuwa nyuma na pembeni Ya walipo kulikuwa na mwanadada mrembo akiwatizama.. Kuonekana mikono Yao kuwa ndani Ya Suruali Zao na wakati mwingine kuongea kwa Ishara, Ilikuwa ni mbinu ambayo kwa Jamila hakuhitaji Kuwasoma Zaidi. Na hata alipo jiuliza hawa ni watu gani? Bado hakupata jibu kwa kuwa hakuwahi kuwaona katika ofisi Zao. Akaamua kutulia kuutazama Mchezo.. Mkono wake haukubanduka sehemu penye bastola Yake....

******
wakati wao wakiendelea kumuangalia Mudy katika namna ambayo waliifahamu wao.. Mudy alikwisha tambua muda mrefu kuwa kuna Watu wawili ambao walikuwa wakimfuatilia kwa Nyuma.. Hakuwa na papara katika kuwaangalia muda Wote alikuwa Akitabasamu kuonyesha kuwa hakuwa na Wasiwasi. Watu wawili watatu waliokuwa wakiongea naye Kuhusu siasa Walimpa Uhueni.. Uhueni ambao Ndio nafasi Pekee Aliyokuwa Akiihitaji.. Hakujua kuwa katika Watu waliokuwa wakimfuatilia palikuwa na mtu wa tatu.. Mtu ambaye kama angemuona nadhani kila kitu chake kingebadilika.. Ni hapo alipoinama kuzuga kama anafunga Kobazi lake Mguuni.. Macho Yake akaangaza huku na Huku kutizama Iwapo kulikuwa na Watu wengine.. Naam Alichokiwaza na Kukihisi kilikuwa hivyo.. Jicho lake likamuona mwanadada ambaye alimtoroka Usiku wa jana baada ya Kumpa mapigo kadhaa... Yes... Hakuwa mwingine Bali Kanali Jamila Hassan, Jasusi Kutoka kitendo cha kijasusi ndani ya Idara ya Usalama Wa Taifa... Mudy hakulitegemea Hilo wala kuliwazia hilo... Hapo akahisi kengele Ya Hatari Ikilia Katika Kichwa chake.. Kutoka Aliposimama akapiga Hatua na Kuingia katika mkusanyiko Zaidi Wa watu, Mkusanyiko ambao ulikuwa ni wa abiria Wengi waliokuwa Wakisubiri kivuko.. Kuingia kwake pale, macho Yake Yakacheza kila Upande... Hapo akawaona Watu wale wawili Wakihangaika kumtoa katika Upeo wa Macho Yao.. Lakini Kilichomshangaza Zaidi ni Kule kupotea kwa ghafla Kwa Kanali Jamila... Kupotea kwake Kulimaanisha Kulikuwa na Uwezekano wa Kuondolewa katika Uso Wa dunia. Hakutaka Iwe mapemba kiasi Hicho.. Na hakupenda Iwe Kirahisi Kiivyo.. Akaziangalia bastola Zake mahali Zilipo, Alipoziona Akatabasamu.. Kutoka Pale akasogea Zaidi Mpaka karibu na Mlango Wa kutokea kwa abiria waingiao Kwenye Kivuko, Hapo Akatulia kuangalia Huku na Huko.. Hakuwa Akimuona Kanali Jamila na Hakuwa Akiwaona Watu Wawili Waliokuwa Wakimfuatilia.. Kivuko Kikafika na Abiria Kuanza kushuka... Hapo ndipo Mudy Alipopataka.. Mkono Wake Mwepesi Ukapenya na Kulifungua Lango la Abiria Waliokuwa Wakisubiri Kivuko.. Muda Ule ule purukushani Kubwa Ikatokea Miongoni Mwa abiria na Walinzi Wa kivuko Kile.. Ni purukushani Hiyo Iliyomuwezesha Mudy Kujichanganya na Abiria Watokao ndani Ya kivuko Kile kisha naye akaongoza kama anatoka lakini katika Uwepesi ule ule akarudi katika Kivuko kwa kukata tena Tiketi... Akaingia huku akitizama tena katika Utizamaji Ule Ule, lakini hakuambulia Kumuona yeyote kati Ya watu wale. Hapo akajua kumekucha.. Hakujisumbua tena kuvuka na kivuko kile.. Akatoka Katika jengo la kusubiria kivuko.. Akaongoza Mpaka Ndani Ya Soko la Samaki Pale Fery.. Akamuendea Mvuvi mmoja Ambaye Alikuwa ndio Kwanza Ameupaki Mtumbwi Wake, akaongea naye Mawili matatu.. Sekunde Tatu baadae Walikuwa ndani ya Mtumwi Ule Wakielekea Katika Mji Wa Kigamboni.... Kufuatwa na Watu wale kulimuacha Mudy Katika Tafakuli Zito.. Ilikuwa Akifikiria Kipi ambacho anatakiwa kukifanya.. Kikubwa ambacho ilikuwa ni lazima Akifanye ni Kumtafuta Yule Mwanamke, Mwanamke Aliyeuawa kwa Kupigwa Risasi kisha Kuja Kuibuka katika Upeo wa Macho Yake.... Kilikuwa kitu ambacho Hakuwahi kupambana nacho wala kukutana nacho, lakini Alijipa moyo lazima akutana na mwanamke Yule kwa Vovyote.

Kutoka Soko la Feri mpaka Eneo maarufu kigamboni lijulikanalo kama mikinda, ni Muda Wa dakika Zisizopungua tano kwa Mtumbwi.. Aliposhuka pale Akalipa Ujira na Kuongoza Kuitafuta barabara Ya lami.. Akachepuka upande Wa pili wa barabara, Akaongoza Kinjia Kidogo Ambacho Kilikuwa Kikitokea Moja kwa Moja Maeneo Ya Makao Makuu Ya Jeshi la Wanamaji (NAVY) kutoka hapo Akaongoza mpaka Maeneo Ya kwa Dany (Kwa watu wanaoishi kigamboni wanapafahamu) nia Yake Ikiwa ni Kwenda kupata Chochote Cha kutoa Tumboni.. Lakini Wakati Akipanga hilo Akakumbuka Kuongea na Mtu Mmoja.. Huyu Alikuwa Ni Mwanajeshi Mwenye Cheo Cha Koplo.. Huyu Aliitwa Rajab Hija Rajab... Alikuwa ni Mtu ambaye alikuwa akimsaidia Mengi.. Akaandika namba kadhaa Kisha Kuipeleka Simu Katikati Sikio Lake... Lakini Wakati Simu Ikilikaribia Siko Lake Akajikuta Akipigwa Kikumbo Kisha Mlio Wa Risasi Ukafuatia... Mudy Alikuwa Chini Pembeni Yake Alikuwa Alikuwepo Kanali Jamila, Huku Risasi tatu Zikiwakosa Kwa Hatua Chache tu....
 
MKE WA RAIS



Wakati Akiipeleka simu katika Sikio ili aongee na Koplo RaJab Hija, Akashangaa akipigwa kikumbo na kuanguka chini huku kukifuatiwa na mlio wa Risasi... Taharuki ikazuka katika kujiondoa pale.. Wote walikuwa wakibilingita Chini huku wakijaribu kujibu risasi Zile. Mji wa kigamboni ukageuka kama Uwanja wa vita.. Hakukuwa na mtu aliyekuwa amebaki eneo lile.. Mudy Alikuwa amekamata bastola moja akifyatua huku na Upande mwingine alikuwepo kanali Jamila Hassan Akishambulia kwa Upande wake... Kila kitu kilikuwa shaghalabaghala.. Watu waliacha ofisi Wazi na Wao Wenyewe kukimbia kuyanusuru Maisha Yao. Bado risasi zilikuwa Zikilindima katika namna Ya ajabu.. Muda mfupi Sehemu Yote Ilikuwa kimya Huku miili ya watu watatu Ilikuwa imetambarajika Chini katikati Ya Dimbwi la Damu, Huku Mudy na Kanali Jamila Wakipotea katika Mazingira Ya kutatanisha. Sehemu yote kwa wakati Huu ilikuwa imejaa watu kila mmoja akiongea lake na hata Kikundi maalumu Cha Askari polisi na Wale Wa jeshi la Wanamaji walikwishafika Huku Wakiwa na Silaha Nzito Mikononi Mwao. Lakini hapakuwa na Watu wengine zaidi ya Miili ya Watu wale.

*******

Kepteni George Simon alisimamisha gari Yake katika packing Ya magari katika Eneo la Mlimani City. Akashuka na Kumuendea mlinzi aliyekuwa Akiangalia usalama, Akaongea naye maneno mawili matatu, kisha Akaongoza moja kwa moja katika eneo lenye mkusanyiko mkubwa ndani ya Jengo lile. Alitembea huku kila wakati akitumia Hila kutazama alipotoka kama angefanikiwa kuona mtu yoyote wa kumtilia mashaka, lakini haikuwa hivyo.. Kila alipopita palikuwa salama salimini... Akaendelea na Safari Yake huku Akiangalia Hiki na kile mpaka pale alipoikuta Sehemu ambayo alikuwa anaitafuta. Aliingia kama wateja Wengine kisha akasimama kwenye foleni Kusubiri huduma... Baada ya kuhudumiwa kwa wawili watatu ikafikia zamu Yake.. Akasogea huku akiunda tabasamu, lilikuwa tabasamu bandia.. Alikuwa mbele Ya mhudumu wa mtandao wa mawasiliano... Aliingiza mkono wake mfukoni na kutoa kikaratasi kidogo ambacho ndani Yake Kilikuwa kimeandikwa namba Ya Simu... Akampa Yule msichana Huku akiendelea kutabasamu.. Msichana Yule akakifungua kile kikalatasi na kukutana na Ile namba.. Msichana Yule akayarudisha Macho Yake Usoni kwa kijana aliyempa kikataratasi alichoshika, akataka Kuongea kitu Lakini sauti Haikuwa inatoka.. Baada Ya kuona Yule msichana anababaika Kepteni George akatoa kitambulisho Chake na Kumpa msichana Yule.... Kisha kwa sauti yenye msisitizo na Isiyo na masihara Kepteni George akamwambia Yule Mwanamke... '''Nahitaji Kujua namba Hiyo Imewasiliana na nani tokea wiki mbili Zilizopita''' baada ya kuongea Hayo akasogea pembeni ilikuwapisha watu Wengine... Muda mfupi baada ya kusogea, wakaingia Wasichana wawili wazuri Kupindukia, walikuwa wakiongea huku wakicheka na kugongesheana Mikono Yao... Wakati macho Yake Yakisanifu katika maumbo Ya warembo hao walioingia pale kwa mbwembwe, akashangaa kutokumuona Mhudumu aliyemhudumia Muda mfupi uliyopita na Wakati Ule ule Akashangaa kumuona Mhudumu akiwa amebadilishwa na Safari Hii alikuwa wakiume. Hakuwa Mjinga katika kuamini kile ambacho hisia Zake Humwambia.. Kengele za Hatari Zikagonga katika kichwa Chake... Alipoyapeleka Macho Yake kwa mhudumu mpya Wa kiume na kukutana na yake, Wote wakajuana, wakajuana kuwa wote walikuwa ni watu wa fani moja.. Wote walikuwa majasusi Kupindukia... Ulikuwa mshangao katika macho Ya kepteni George Mshangao ambao Uliishia katika Moyo Wake pasipo kutoka nje na Kuenea Usoni.. Wakati Huo huo Mkono Wake Ulikuwa katika sehemu Husika... Wakati Akifikiria kuondoka pale, akamuona Mhudumu Yule wa kike Akirudi kisha Akashuhudia Wa kiume Akiondoka Huku macho yake Yakimuangalia kepteni George.. Kepteni George alikuwa akikiona kitendo kile lakini Macho Yake Yalikuwa Yamezama kwenye Maswali kibao juu Ya kampuni Ile Ya Simu.. Mhudumu yule Wa kike hakuwa kwenye Uchangamfu Ule wa mwanzo, Hata lile tabasamu lake Lilikuwa limeyeyuka Usoni kwake.. Kepteni George akalitambua Hilo. Akainuka na Kuelekea pale tena. Alipofika hakuongea bali alipewa kikaratasi Kidogo ambacho katika kukipokea kwake kulimsisimua Sana.. Kilikuwa kikalatasi kilichotolewa kwa siri kubwa huku macho Ya mhudumu Yule Yakizungumza..

Baada Ya kukipokea kikaratasi kile akatoweka katika eneo la ofusi ile.. Hakutaka kukikunjua Kikalatasi Kabla Hajaondoka katika Maeneo Yale. Watu aliyokutana nao pale kuanzia Yule mhudumu wa kike, wakiume na Wale wadada kulimpa mashaka Sana.. Kutazamana Na Jasusi Yule Aliyejifanya mhudumu kulimpa picha kuwa kampuni ile haikuwa ya Simu tu, bali kulikuwa ni Siri nzito Nyuma Yake... Muda mfupi alikuwa Nje Ya Jengo lile Maarufu pale Mlimani City.. Akaangalia Huku na Huko kisha akaenda Sehemu ambapo palikuwa pakiuzwa Simu lengo lake likiwa si kununua simu Bali Kuangalia Je kuna mtu ambaye alikuwa Akimfuatilia... Alipokaribia Sehemu Ile Akamuona Yule mhudumu wa kike Akitoka katika Jengo Lile Huku akionekana kutembea kwa Wasiwasi Mkubwa.. Kepteni George akatulia.....
 
MKE WA RAIS


Wakati Akiangaza macho Yake Huku na Kule hasa katika lango la kutokea, Akamuona Yule mhudumu akitoka huku akionekana ni mwenye wasiwasi mkubwa.. Kepteni George akabaki kumuangalia kwa umakini huku wakati mwingine macho Yake yakiangaza huku na huko katika namna fulani.. Punde tu baada ya kutoka kwa mhudumu Yule, akawaona wale wasichana wawili ambao nao walikuwa wametoka huku Wakicheka na kuelekea upande tofauti na ule ambao Alikuwa ameelekea mhudumu aliyetoka ndani.. Hapo akaendelea kuwa makini kuusoma Mchezo ambao bado haukuweza kumuweka katika Mwanga bali katika Giza... Kilichozidi kumchanganya zaidi ni Upi uhusiano ule wa mtandao wa Simu na Kifo cha Mke Wa Rais? Kuliwaza hilo kulimfanya awe makini huku macho Yake yakitembea eneo lote. Hakutaka kukurupuka kumfuatilia Yule mhudumu kwa kuwa alikuwa akijua kuna sehemu kulikuwa na macho ya mtu au watu wakimtizama, ingawa hakujua walipo. Mhudumu yule aliyetoka ndani aliongoza mpaka kwenye packing Ya magari, akatoa kikalatasi ambacho kilipokelewa na Mlinzi wa packing baada ya hapo akaingia katika Gari na kuliondoa taratibu kuelekea Eneo la Chakanyikeni.. Muda wote Kepteni George Alikuwa ametulia kabisa kama hakuwa na Muda na mhudumu Yule.. Mara likatokea tukio ambalo alilikusudia, wasichana wawili waliokuwa wakicheka kwa mbwembwe waliingia katika gari kisha kwa mwendo wa kawaida wakaanza kuondoka kuifuatilia gari Ile ya Yule mhudumu kwa nyuma.. Hapo akautambua Mchezo ambao Ulimuacha katika msisimko Wa Mwili Wake.. Akapiga Hatua Ya kwanza kuelekea kwenye packing, Hatua Ya Pili Akaiona Gari Nyingine Ikiondoka katika packing.. Lakini hii haikufata usawa Ulielekea magari Yale.. Gari hii safari Hii Ilikuwa Ikionekana kuelekea Maeneo Ya Mwenge.. Ni muda Huo aliyoutumia Kepteni George Kuifuata Tax iliyokuwa jirani ya pale na kujipakia kisha kumpa Dereva Maelezo Ya nini akifanye. Yalikuwa maelezo ya Kuifuatilia Gari ya Mhudumu Yule kwa kificho Huku wakiacha nafasi kwa magari Matatu kutoka ilipo gari Ya Wasichana wale wawili na magari matano kutoka pale Ilipo gari Ya Mhudumu Yule. Lengo likiwa ni kutokuwashtua wale wanawake kujua kuwa wanafuatiliwa.

Ilikuwa ni kitendo cha kiusalama ambacho alikifanya kepteni George, kitendo cha kutoitumia Gari Yake kilikuwa kitendo sahihi hasa kutokana na Usalama Wake. Tax ikaendelea kuendeshwa kwa umakini mkubwa huku dereva Yule Akihakikisha kuwa gari Za Mbele Hazimpotei katika Macho Yao. Wakati Mambo Ya mfukuzano yakiendelea ndipo alipokumbuka kile kikaratasi, Kikaratasi ambacho alipewa na Mhudumu Yule.. Akapatwa na Hamu kubwa Ya Kukifungua.. Hakujua kwanini Yule msichana Alimpa kikalatasi kile, Lakini Alipokikunjua na Kukiangalia Akakutana na namba, Namba Ambayo Haikuonekana kuwa Ya Gari Wala Ya Simu.. Hii Ilikuwa Namba Ya Nyumba. Naam.. Ilikuwa namba Ya Nyumba.. Damu Ikasisimka katika Mwili wa Kepteni George.. Sasa alikuwa akiuona Mwanzo Wa Mchezo Ukianza.. Mwanzo ambao Ulikuwa wa Hatari kubwa. Hakuijua ni Hatari Gani lakini kuiona gari Ya wanawake wale wakimfuatilia Yule msichana Wakajua Kuna Kitu. Akajiweka tayari na Mapambano, mapambano ambayo Hakujua Uwezo wa maadui Zake.. Mkono wake Ulikuwa ilipo bastola Yake... Lakini Wakati Akilifikiria Hilo Akakiona kitu Kingine, kitu ambacho Kikaendelea kumpa picha kuwa Msichana wa mbele alikuwa katika hatari. Gari ambayo Alikuwa aliiona Ikiondoka Mlimani kuelekea mwenge kipindi akiwa pale, Sasa Alikuwa Akiiona Mbele Yake karibu kabisa na Ilipo gari Ya yule Mhudumu... Kepteni George akaiona Hatari Ya kutokumkuta Hai Yule msichana Iwapo Atamuacha Afike kabla Yake... Kwa kuwa Aliijua namba Ya Nyumba na Jina la mtaa anaoishi Yule Msichana. Kepteni George Akaona amwambie Dereva Wa Ile Tax aegeshe pembeni kisha Yeye akashuka na Kulipa harafu Akapiga Hatua Kukiendea Kijiwe Cha Madereva Bodaboda, Akamchukua Dereva Mmoja kisha Safari Ya kuelekea Nyumbani Kwa Mhudumu Yule Ikaanza.

Alitaka wao wamkute ndani badala Ya yeye kuwakuta wao.. Na ndio ilikuwa hivyo. Kutokatana na pikipiki kupenya Huku na Huko matokea Akajikuta Akiufikia Mtaa Husika.. Hapo akaomba kushushwa Kisha Akalipa Kabla hajaanza Kupiga Hatua Kuitafuta namba Ile. Alionekana kuwa mtu wa kawaida huku Mluzi Ukisikika katika Mdomo wake. Hatua Kumi mbele Akaiona Nyumba ambayo Alikuwa Akiitafuta.. Nyumba ambayo Alipewa namba na Mhudumu Yule. Akaisogelea kwa umakini wa Hali ya juu.. Akalifikia geti na Kujaribu Kulifungua, lakini lilikuwa gumu.. Ukimya katika nyumba Ile kukampa picha Kuwa hapakuwa na Watu Wengine.. Hapo Akaona Njia pekee ni Kuchupa na Kuingia ndani.. Ndicho Alichokifanya.. Muda Mfupi Alikuwa ndani Ya Uzio wa Nyumba Ile... Akaangalia Huku na Huko kama Kulikuwa na Mtu, alipouona Ukimya umeendelea mpaka ndani akaamua Kuendea mlango Wa kuingilia Ndani.. Safari Hii Bastola Yake Ilikuwa Mkononi.. Akaufikia Mlango na Kutoa Funguo Zake malaya.. Muda Mfupi Alikuwa ndani Akitazamana na thamani kubwa sana.. Akaufunga Mlango kisha Akatafuta sehemu Nzuri akatulia kuwasubiri wenyeji Wake
PATAMU HAPO
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 19

Akatoa funguo Zake malaya na sekunde ya pili, alikuwa akitizamana na Sebule kubwa yenye thamani nyingi sana. Akaufunga mlango kwa ndani kisha akaitafuta sehemu nzuri yenye nafasi ya kuweza kumpa fursa ya kufanya shambulizi pale itakapobidi. Hakuwa na uhakika juu ya mtego ule lakini kile alichokiona barabarani Kilimpa imani kubwa kuwa Msichana Yule mrembo alikuwa katika hatari kubwa... Hatari ambayo Imeletwa na yeye kutokana na kufika katika Ofisi Ile ya kampuni Ya Simu. Kumuona mtu ambaye macho yake yalimshuku na kumjua kuwa ni jasusi kukaanza kumpa picha Juu ya Kampuni Ile. Akiwa katika wazo hilo mara akakiona kitasa Cha mlango kikitingishwa na muda mfupi Akawaona Watu wawili Wakiingia tofauti na wale aliyowadhania. Hawa walikuwa Wanaume, wanaume wenye miili mikakamavu.. Wote walikuwa katika mavazi sare.. Mavazi ambayo yalimfanya Kepteni George Kujiweka sawa. Kuingia Kwa watu tofauti katika Nyumba ile kisha kufanya kama yeye kwa kuufunga mlango. Wao wakajigawa mmoja akienda Chumbani kwa mwanamke Yule Mwingine Akielekea Sehemu ambapo palionekana kama Jikoni. Hapo kepteni George akajiandaa kufanya kitu, kitu ambacho kingeweza kumpa urahisi wa kutoka salama akiwa pamoja na mwanamke Yule. Ni pale wakati akijiandaa kwahilo ndipo alipouona Mlango Ukifunguliwa Kisha Mwanamke Aliyemtarajia Akaingia huku akionekana ni mwenye wasiwasi mkubwa.. Ilimchukua Muda mfupi sana pale sebuleni kabla ya kuingia chumbani, chumba ambacho kulikuwa na mkora mmoja. Kepteni George Aliijua Hatari ambayo Ingetokea kama Angemuacha Mwanamke Yule kuingia katika Chumba kile. Lakini kutokana na pale alipo kuwa sehemu Hatarishi sana kama Angeamua Kumshtua mwanamke yule, akaamua Kutulia tuli kuangalia kile ambacho kingetokea. Kuondoka kwa mwanamke Yule Kuingia Chumbani kulimpa nafasi George kutoka pale na kumfuata kinyume nyume... Akamuacha Yeye atangulie kuingia Kisha akabana kwa pembeni, lengo likiwa ni kumsaidia iwapo atakuwa Hatarini. Wakati ametulia kitizama jinsi Ya kufanya, akaisikia Sauti Ya mwanamume Ikimuamrisha mwanamke Yule atulie kama alivyo. Hakusubiri sana, bali alikinyonga kitasa na kuingia huku mdomo wa bastola Ukiwa umetangulia mbele.. Kama Alivyotarajia ndicho kilichotokea.. Kama aliamini mwanamke Yule mhudumu alikuwa mzembe, basi alikuwa Amekosea Sana.. Akiwa anatizamana na mdomo wa bastola iliyoshikwa sawasawia na Mwanaume Asiyemjua, likafanywa kosa la Mwanaume Yule kutizama mlangoni, baada ya mlango kufunguliwa... Hapo akaachia teke kali, teke ambalo lilimpata mwanaume Yule na kumrudisha Kinyumenyume.. Kurudi kwake nyuma kulimfanya akutane na George akiwa anaingia ndani..

Hakumpa nafasi ya Kujiandaa Pigo moja la Shingo likamuangusha Chini na kumpotezea fahamu.
George akaingia bastola mkononi.. Binti akataka kuongea kitu lakini George Akampa Ishara kuwa kuna mtu mwingine pale ndani.. Wakauvuta Mwili wa mwanaume Yule na Kuuficha Ili iwe ngumu kwa waingiaji kumuona kisha Wao Wakaendelea Kutulia kusubiri ambaye amebakia mle ndani.. Muda Mfupi wakasikia Nyayo Za mtu zikija usawa wa Chumba walichomo wao.. Muda Mfupi kitasa kikanyongwa Akazama Mtu mzimamzima bila Kuangalia huku wala kule, akapokewa na Ngumi Nzito Ya Shingo.. Akapesuka lakini Hakuanguka... Akasimama Akiwa Tayari kukabiliana na Kepteni George Sambamba na Mwanamke Yule.. Hakumjua George, Hakujua Yeye ni nani katika Medani Ya mapigano.. Laiti angemjua basi Asingesimama Mbele Yake... Alipewa nafasi Za kutupa Ngumi Mbili Tatu ambazo Zote Zilipita Hewani... Ngumi Ya Tano na Sita Akajikuta Mkono Ukidakwa Kisha Ukapigwa Pigo Moja Takatifu Mkono Ukageuka mbele nyuma.. Akapiga Yowe kubwa sana La Uchungu... Hapakuwa na Mtu Wa kumuonea Huruma.. Akapewa Upcurt moja Ambayo Ilimlegeza na Kumuangusha Chini... Muda Mfupi Chumba kilikuwa kimetulia Huku mizoga Miwili Ikiwa sakafuni... Mara Hii Walikuwa wakitazamana kati Ya George na Yule mwanadada ambaye bado Jina Lake Lilikuwa halijajulikani.

''hutakiwi Kuishi hapa, Chukua Vile vitu muhimu tuondoke hapa.. Mengi Unayotaka kujua Utayajua Mbele kwa mbele.. Aliongea kepteni George Huku akiendelea Kuwapekuwa Wale watu ambao bado alihitaji Kuondoka nao... Lakini Hakujua vipi Angeondoka Na watu wale Eneo Lile... Wakiwa Bado Wameduwaa Mlango Ukafunguliwa kwa nguvu Kisha Risasi Mfululizo Kumiminwa ndani Ya Chumba kile... Kila Mmoja Akachupa Upande Wake na Kuingukia Pembeni.. Risasi Zikapita na Kutua Zilipotakiwa... Wale wanaume wawili walikuwa wamepigwa Risasi Kiustadi Sana.. Wote Wallishakuwa Maiti... Kepteni George Akang'ata kwa Hasira.. Watu ambao Alitegemea kupata Angalau Mwanga katika Upelelezi wake wa Kifo Cha Mke Wa Rais, Walikuwa wameuawa katika Kuificha Siri.. Siri ambayo Angeijua tu.. Hapakuwa na Muda Wa Kupoteza tena Maeneo Yale.. Akamsaidia binti Yule Kukusanya Kile ambacho Alikiona ni Cha maana Na Muda Mfupi Walikuwa kwenye bajaji Wakielekea Tabata.

Wakati Wao wapo Kwenye Bajaji Hawakujua nyuma Yao kulikuwa na Wanaume watano wenye Silaha nzito Wakiwafuatilia, Laiti wangejua????
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 20

Muda mfupi walikuwa ndani ya bajaji Wakiondoka pale huku wakiacha maiti Wakiwa wametambarajika. Hawakujua kuwa Nyuma kulikuwa na Watu wa tano, Watu ambao walikuwa na Silaha nzito wakiwafuatilia Wao.. Bajaji ilikuwa ikitembea katika mwendo wa kawaida, huku ndani Yake akiwepo Kepteni George na Msichana yule. Safari Yake ilikuwa ni kuelekea moja kwa moja tabata lakini alipoufikiria Unyeti wa makao Yao, Akaamua kughairi na Safari hii Wakaamua kurudi Kuelekea Mwananyamala. Ni wakati dereva wa bajaj akigeuza bajaj ndipo walipoiona Gari Ikija kwa kasi kwa dhumuni la Kuwagonga.. Hapo ndipo wepesi wa abiria wale Ulipowaacha watu wachache midomo Wazi.. Wote walikuwa Wamechupa kutoka ndani Ya bajaji na Kuangukia pembeni kabisa kicha kuchupa tena katika namna ambayo hakuna Aliyedhania kama watu wale walikuwa wametoka ndani Ya bajaji Ile.. Kutua kwao chini Kikafuatia kishindo kikibwa, Kishindo ambacho kilifuatiwa na Mlio wa matairi Yakipata tabu katika Lami... Hawakuondoka, Wala hawakwenda mbali, bali walirudi Wakiwa Sio Wale waliotoka kwenye bajaji... Wakajichanganya na Watu Waliokuwa Wakiishangaa ajali ile. Dereva Wa bajaj alikuwa amekufa pale pale kwa kubanwa kichwa.. Damu Zilikuwa Zikimwagika mfano wa Maji... Wakaiangalia gari Hilo lakini Halikuonekana kujulikana katika macho Ya George, Lakini Kwenye macho Ya mwanamke Yule ile gari Ilikuwa Moja kati Ya Magari Ya kampuni Yao.. Akamgusa George Begani na Kumnong'oneza kitu.. Muda mfupi walikuwa njiani Wameshikana mikono wakielekea Upande Wa Shekilango.. Nia Yao Ilikuwa ni kutizama yoyote ambaye wangemhisi Kuwa ni Mmoja kati Yao Ili wamshughulikie. Lakini walitembea mpaka maeneo ta Legho Lakini hawakufanikiwa kuona wala kumtilia mashaka Mtu Yoyote. Wakaendelea na kutembea walipofika mbele kidogo Walichukua pikipiki na kuondoka kuelekea kinondoni Huku George Akiwa na matumaini Ya kupata Chochote cha maana katika Upelelezi Wao Juu Ya Kifo cha mke Wa Rais.

*******

Makaburi Ya kinondoni Yalikuwa yamefurika watu wa Aina mbali mbali, Kuanzia Viongozi Wa kidini, Viongozi wa Serikali, vyama pamoja na Wananchi, huku wote hao wakionekana ni Wenye Huzuni Sana... Katika Safu Ya Mbele Walikuwa wamesimama Marais wa nchi Jirani pamoja na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri Ya Tanganyika. Muda Wote kitambaa kilikuwa Machoni Akifuta Machozi Yaliyokuwa Yakiporomoka Kutoka katika Macho Yake. Ni Ukweli Usiofichika Kuwa mheshimiwa Rais Alimpenda Sana Mkewe.. Alikuwa Akifanya kila kitu kwa Ajili ya kutokuhitaji Mkewe ahangaike.. Lakini hakujua kwanini Mkewe ameuawa? Kwa nini mkewe alibadilika? Ni nani Aliyeingia mpaka ndani Ya Ikulu na kumuua Mkewe? Kama mtu anaweza kuingia Ikulu na Kuuawa Atashindwaje Kuniua na Mimi? Ni maswali Hayo Yaliomuumiza na kumliza sana.. Kila Alipokuwa Akiwatizama Watoto Wake Walivyokuwa Wakilia, Rais Alikuwa Akilia Sana.. Hata Marais Wenzake Walipokuwa Wakimbembeleza bado hawakufanikiwa Hilo. Ni pale Wakati Yupo makaburi Alipomkumbuka Mtu Mmoja, Mtu ambaye angeweza kumnsaidia Kutoka katika Giza Totoro... Alimkumbuka Sana Mpelelezi Mashuhudi Mohamed Abdallah.. Mtu ambaye Alikuwa Akiujua uwe Wake na Kumtambua Vilivyo.

Wakati Akimuwazia Mudy Hakujua kuwa Mudy Tayari Amejiunga katika kukijua Chanzo Cha Mauaji Ya Mkeo.. Akasibiri Muda Upite uende na Wamalize Mazishi Ili Akutane na Mudy...

Msururu Wa Magari Ulikuwa Ukiingia katika Viunga Vya Makaburi Ya Kinondoni.. Yalikuwa ni magari Yaliokwenye msururu Wa kuusindikiza Mwili Wa Mke Wa Rais.. Walinzi na Makachero Mbalimbali Walikuwa Wamejaa na kumwagika katika Maeneo Yote Ya Makaburi.... Ukiondoa pale makaburini lakini Sehemu Zote Ambazo Ziliizunguka Sehemu Ya makaburi zilikuwa Chini Ya Uangalizi Wa Watu Wa Usalama Wa Taifa...

Wakati Usalama Wakiifanya kazi Yao, pembeni Kabisa Ya mstari Aliokaa Mheshimiwa Rais, Vijana Wake watatu walikuwa wamesimama Wakiangalia kila kitu ambacho kilikuwa kikiendela maeneo Yale. Wakiwa wanaendelea kutizama Huku na kule mara Wote Wakaonyesha Mshangao baada ya kumuona Mtu Mmoja Ikijipenyeza na Kusimama Mbele Yao.. Alikuwa mwanamume wa makamo ambaye Alikuwa Amevaa Suti Nyeusi, lakini Kilichowashangaza ni kuondoka ghafla kwa mwanaume Yule.. Kitendo Cha kutokea kisha Kurudi Nyuma Hakikuonwa na Vijana Wale Watatu tu bali Kwa mbali Alikuwepo Mtu Mwingine ambaye hakuwa pale kwa sababu ya Mazishi, Huyu Alikuwa pale kwa kuwaangalia Watu Kama Wale. Huyu Hakuwa Mwingine Bali Alikuwa Mudy.. Alikuwa Ameshamuona kitambo mwanaume Yule.. Hata pale Alipokuja na Kuondoka, Mudy Alikuwa Nyuma Yake katika Namna ambayo Haikuwa Rahisi Kujulikana... Aliendelea kumfuatilia mwanaume Yule kwa Usiri Mkubwa bila Yeye kujishtukia mpaka pale alipomuona Akiingia kwenye ghari Moja Ya Kifahari na Gari Kuondoshwa kwa Haraka Kufuata barabara ya Masaki....

Mudy Hakutaka Kuifuata gari Yake bali Alisimamisha pikipiki, muda mfupi walikuwa katika barabara ile umbali Mfupi kutoka Ilipo Ile gari... Hakupenda kuwashtua mapema bali alikuwa Amepanga kuwafuatilia kimya kimya kujua wapi watakapoishia ili iwe
 
MKE WA RAIS



Mudy alikuwa Nyuma ya pikipiki akiifuatilia gari ya mtu yule aliyeondoka katika makaburi ya Kinondoni kwa wasiwasi mkubwa. Alikuwa amempa nafasi kubwa kwa kumuongoza mbele kwa tofauti ya Magari matatu ili kumfanya asije kushtuka kuwa anafukuzia.. Safari na mfukuzano wao uliishia tamati katika fukwe za bahari ya Hindi maeneo yale Ya masaki. Mudy hakutaka kusimama katika bar Ile bali alichokifanya ni kunyoosha mpaka katika bar ambayo ilikuwa katika eneo lile, akashuka na kuanza kurudi taratibu hasa baada ya kumlipa Dereva Yule. Macho Yake Yalikuwa yakiangaza kila Upande, Alikuwa anaujua mchezo wa watu wale.. Lakini kwa kuwa Alikuwa ameamua kufuatilia tukio la kuuawa kwa mke Wa rais hakujali sana katika lolote ambalo lingetokea. Alikuwa na kila kitu katika mifuko Yake... Akaendelea kulisogelea eneo lile kama Mtu wa Kawaida.. Akaingia katika Hoteli moja ambayo ilikuwa na Bar ndani Yake. Akavuta kiti na kukaa, mara Akamuona Mhudumu akadika haraka na kuuliza kipi ambacho angehitaji Mudy... Huku macho Yake Yakiangalia kwa chati kila mtu katika bar ile, Mudy Akaomba Aletewe Mzinga Wa konyagi... Kuagiza kwake mzinga kukawa kama kumemzubaisha mwanadada Yule... Hata pale Mudy aliporudia tena yule mhudumu alionyesha Kusita.. Lakini kile ambacho hakuna Ambaye amekitarajia kutokea, kikatokea.. Dakika moja mhudumu alikuwa ameduwaa na Ndani Ya Sekunde Ya dakika Ya pili, Mudy Akashangaa kumuona Mhudumu Yule akipaa angani na Kwenda Kuanguka Umbali Mrefu kutoka pale alipokaa Mudy.. Damu Nyingi Ikimvuja katika kifua Chake

Mudy Akaduwaa kwa sekunde na Sekunde Iliyofuata Alikuwa Akichupa na kudondokea upande wa pili wa ukuta wa Bar ile.. Akachomoa bastola Yake tayari Kukabiliana na chochote.. Sehemu Yote Ilikuwa tafrani Huku Wa hudumu wakiangua vilio kupita kiasi... Macho Ya Mudy hayakuwatazama watu waliokuwa wakilia na Kupiga kelele, bali Macho Yake makini Yalikuwa Yakikitazama Chumba ambacho kilikuwa katika Ghorofa Ya nne.. Dirisha Ya Chumba kile lilikuwa limefunguliwa kwa Upenyo Mdogo sana.. Upenyo Ule ungekuwa si Lolote kwa mtu Wa kawaida.. Lakini Kwa Mudy Ulikuwa ni Zaidi Ya Kile ambacho kingedikiriwa na Wengine.. Akajiondoa taratibu na Kuifuata lifti Ya hoteli ile na Muda Mfupi alikuwa katika Korido katika Ghorofa Ya Nne kukifuata kile Chumba Huku mkono wake Ukiwa juu Ya bastola Yake. Akatembea kwa Haraka.. Akakifikia kile Chumba, Akatulia kwa kama Sekunde kuangalia Usalama kwanza kama kutakuwa na Yoyote,,, lakini ukimya Ulikuwa imetawala na Hapakuwa na Mtu Yoyote.. Mudy Akauendea mlango na kujaribu kukinyonga kitasa, akashangaa kuuona Mlango ukifunguka. Macho Yake Yakaangalia kwa Chati na Muda mfupi alikuwa Chumbani huku bastola Mkononi.. Mbele Ya macho Yake Alikuwa Akitizamana na Tukio la Kutisha.. Mtu aliyemfuatilia Kutokea kwenye makaburi Ya kinondoni alikuwa Ameuawa kinyama mle chumbani. Mwili wake Ulikuwa Uchi wa Mnyama Juu Ya kitanda Huku Kisu kikubwa kikiwa katika kifua Chake.. Hali ilikuwa ikitisha sana.. Kwa Mara Ya kwanza Mudy Akahusudu uwezo wa mtu Aliyefanya Mauaji Yale... Akauangalia Mwili wa Marehemu Huku macho Yake Yakizunguka katika Chumba kile.. Hapo Akavutiwa na Kitu Ambacho Alikuiona Pembeni Ya Maiti Yule.. Zilikuwa Picha Za Hayati Mke Wa Rais Akiwa Amepiga na Mwanaume Yule Aliyeuawa Pamoja na Mhudumu ambaye Aliuawa Muda Mfupi uliyopita, Wakati mtu wa Tatu katika Picha Ile alikuwa ni Yule msichana Aliyeuawa kwa Risasi kule Hotelini Sinza lakini akaja kumuona Akiwa Hai... Akainama ili Kuichukua Picha Ile, lakini akasita baada ya Kusikia mtu Akimpigia makofi Kutoka Nyuma Yake... Akageuka Huku tabasamu Usoni... Akajikuta Akitizamana na mdomo Wa bastola kutoka kwa Mtu ambaye Alimjua na Kumtambua... Hakuwa Mwingine Bali Alikuwa Mkurugenzi Mkuu Wa Usalama Wa Taifa Mr Kassim Adnan Kwangay.. Mudy Akahisi Damu Zake Zikimsisimka Kupita kiasi.. Maswali Lukuki Yalikuwa Yakipishanana katika Kichwa Chake.

Akaamua kuyapuuza maswali Na kuitiliza Akili Yake ili kuangalia ni Jinsi gani Anaweza kujiokoa mikononi kwa mtu yule ambaye aliamini ametekwa.. Kukutana uso kwa uso na Mkurugenzi Yule kilikuwa ni Kitu ambacho hakikutegemea kabisaa... Akakiona kiza kinene na Maswali Lukiki katika Mauaji Ya Mke Wa Rais.. Akiwa bado katika tabasamu lile mara Akashangaa kuwaona Watu Wengine Wakiingia pale ndani.. Hawa walikuwa watu Wengine ambao Walimfanya Mudy Auone ugumu katika Kujinasua... Mbele Ya macho Yake alikuwa akiangalia na Waziri wa Ulinzi na Mwenzake Wa Mambo Ya Ndani.. Wote walikuwa wakimtizama mudy Katika Aina Ya hasira na Chuki.. Hapo Mudy Akaiona Hatari Ambayo Ilikuwa Mbele Yake.. Ni Wakati Huo Akiangaliana na Wazito wale ,kitasa kikanyongwa, Wote Wakakosea Kugeuza Sura Zao Kuangalia Nyuma.. Hawakuujua wepesi wa Mudy.. Sekunde Moja ilitosha kufanya Kitu ambacho Kilikuwa hatari katika Maisha Yake... Ni sekunde moja ambayo Ilimkuta Mudy Ikiliparamia dirisha La Kioo na Kuangukia katika Maua Ya Hoteli Ile Kisha akatokomea mitaani Huku Akiwa Amepata mwanga katika uchunguzi Wake Dhidi Ya Mauaji....
 
MKE WA RAIS



Pembeni Ya Maiti Yule akaiona Picha, picha ambayo ilimuonyeshe mke wa rais Akiwa pamoja na yule marehemu pamoja na msichana Aliyeuawa muda mfupi uliyopita. Akavutiwa na kutaka kuichukua.. Lakini mkono wake kabla Haujaifikia Ile Picha akashtuka baada Ya kusikia Mtu akipiga makofi tena Akitokea Nyuma Yake... Mudy Akageuka Huku akitabasamu, Akitabasamu katika tabasamu ambalo halikuwa na Amani.. Alipogeuka Tu Akakutana na Mdomo wa Bastola Ikimtizama katika namna ya kutokuwepo kwa Masihara. Akashtuka katika mshtuko wa Kijasusi, mshtuko ambao ulisababishwa na kumuona Yule ambaye ameikamata bastola kumlenga Yeye. Akailazimisha Akili Yake iamini kile ambacho alikuwa akikiona lakini bado akili yake Ikamgomea.. Haikutaka kuamini Yule ambaye alikuwa ameikamata bastola na kumlenga yeye kuwa ni Mtu wa Kufanya hivyo... Lakini kuiangalia sura na kutokuwepo kwa tabasamu... Kulimpa majibu Mudy Kuwa Ameingia katika mikono mibaya.. Mikono Ya jasusi Aliyeiva kupindukia... Hakuwa Mwingine bali alikuwa Adnan Kassim Kwangaya Mkurugenzi Mkuu wa Usalama Wa Taifa... Wakati Akilishangaa lile, akawaona Watu wawili waliovalia Suti wakiingia katika Chumba kile... Macho Yake yalipowatazama Mudy Akajikuta akizidi kupata mkanganyiko katika Ubongo wake.. Akaitamani Iwe ndoto na kile anachokiona kiwe cha uongo, lakini Haikuwa Hivyo.. Alikuwa Akitizamana Na Mawaziri WawiLi Wenye Dhamani Kubwa katika Nchi Hii... Waziri Wa Ulinzi na Waziri Wa Mambo Ya ndani... Yanakuwaje Mambo Haya? Lilikuwa swali ambalo liliibuka katika Kichwa Cha Mudy.. Hapo hapo akashuhudia Kitasa kikinyongwa.. Waliokuwepo ndani Ya Chumba Wakatizama Mlangoni.. Lilikuwa kosa kwao na nafasi kwa Mudy... Muda Mfupi Alikuwa Akiliparamia Dirisha la Kioo na Kuangukia Chini kabisa.. Kutua kwake chini kulikuwa ni kwa muda mchache kisha Sekunde Nyingine ilikuwa akiruka na kuelekea upande ambao Hakuonekana Kwa Urahisi...

Akaingia mitaa miwili mitatu, Kisha akalichukua gari na Kuelekea Maeneo Ya mbagala Sehemu ambayo alikuwa na Uhakika wa kufanyakazi Yake bila kugunduliwa na Watu ambao kwasasa alikuwa ameshagundua ni Watu gani... Aliendesha gari huku akisonya kila wakati.. Tukio la kuwashuhudia Watu Wenye dhamana Ya usalama wa Nchi kuwa pamoja Huku mmoja akisadikiwa kupotea na kuuawa kwa familia yake, Kilikuwa kitu tofauti Sana.. Kwa mara ya Kwanza Akaanza Kuhisi kuwa Kabla Ya kuuawa; Mke Wa Rais Alikuwa ni Mmoja kati Ya Waratibu Wa Mpango wa Kutaka Kumpindua Rais lakini, kama suala ni kumpindua, Kwanini Walimuua mke wa Rais na Walinzi Wake? Je walitaka kuficha kitu gani? Kuna Uhusiano gani Wa mauaji Ya mke Wa Rais na Ya Walinzi wake? Ina maana Muuaji Alikuwa analengo la kuwaua wote? Maswali Hayo yote hayakuwa na Majibu lakini akichanganya na Kile Alichokiona Kule hotelini.. Hapo akajua kumbe ndio maana Mke Wa Rais Aliuawa Akiwa ndani Ya Ikulu.

Pale pale akaona sio vizuri kwenda mbagala wakati walinzi waliouwa anawajua na anajua sehemu ambazo Walikuwa Wakiishi? Akageuza Gari.... Alikuwa ameamua kuingia Rasmi katika Mapambano.

*******

alisimamisha Gari hatua mita Mia moja na Hamsini kutoka ilipo nyumba Ya mlinzi Wa mke wa Rais... Baada Ya kushuka akafunga milango Ya gari Yake, akaongoza moja kwa Moja ilipo nyumba ya Marehemu ambayo Ilikuwa amezungukwa na Watu Wengi sana, Huku Wengi wao wakilia kwa kuomboleza, Wengine wakipiga Soga za hapa na pale... Aliingia ndani ambako walikuwepo Mama pamoja na ndugu Wa Marehemu... Akatoa pole Kisha kutoka tena nje... Wakati anaukaribia mlango wa kutokea Nje akagongana na Mtu ambaye Alikuwa Amevaa baibui kwa kujifunika Usoni.. Kugongana kwao hakukuwa kwa bahati mbaya bali kulikuwa kwa makusidi na Kulikuwa na Ujumbe ambao alipewa Mudy Kwa Kuwekewa kwenye Mfuko wa Shati lake Kwa Namna Ambayo Hakukuwa na Mtu Mwingine Aliyegundua Zaidi Yao Wenyewe.. Mudy Hakugeuka kumuangalia mwanamke Yule, Bali aliendelea na Safari Yake kurudi kwenye Mchanganyiko Wa watu huku kila Wakati Macho Yake yakitembezwa kijasusi Kuangalia eneo Zima... Kila alipokuwa Akitizama Alikuwa akikutana na Sura Za Makachero kibao.. Ingawa wengi walikuwa wamevaa kiraia Lakini bado Hawakumfanya Mudy Ashindwe Kuwajua...

Akajisogeza katikati Ya vijana Waliokuwa wakiongea kuhusiana na kifo cha mwanamke Huyu ambaye alikuwa mlinzi mahiri wa mke wa Rais.. Kuingia katikati Ya Vijana Wale kukampa Upenyo Wa kuichomoa Kalatasi Iliyopewa na Mwanamke Yule na Kuisoma.. Akakutana na Maneno Yaliousisimua Mwili Wake... Alikutana na Ujumbe Uliondikwa Hivi...

USIJE UKAITUMIA GARI ULIYOKUJA NAYO...

yalikuwa maneno machache sana lakini Yenye Maana kubwa sana.. Kufikia kuambiwa Asitumie gari Yake basi ni Ujumbe ambao Amefikishiwa kuwa Amejulikana kuwa Yupo pale.. Na Msichana Aliyegongana naye wakati akitoka Hakuwa Mwingine Bali ni Mwanausalama....

Akairudisha Ile kalatasi Kisha Akaondoka pale Kuelekea Nje Ya Eneo ambalo lilikuwa na Msiba lengo likiwa ni kujua kama Anafuatiliwa ama lah! Hakuwa Mbali na Ukweli na Hakuwa Amekose
 
MKE WA RAIS

Alikuwa akitizamana na sura ya mwanaume, sura ambayo haikuwa ngeni katika macho yake. Mbele yake Alisimama Mudy Akiwa kwenye mavazi Ya Mazoezi.. Mikononi mwake alikuwa amekamatia Sinia ambalo lilikuwa na Vikombe viwili vya maziwa... Mwanamke Yule akaganda kama sanamu.. Hakuwa akiamini kile alichokuwa akikiona mbele Yake. Licha ya kuishika bastola yake katika mikono yake lakini alikuwa ameshindwa kuitumia.. Muda wote Mudy alikuwa akitabasamu.. Tabasamu ambalo halikuweza kumlewesha mwanamke Yule na kumfanya amuamini Mudy.. Tabasamu ambalo lilikuwa tofauti katika macho Ya mwanamke Yule.. Mudy Hakumjali mwanamke yule.. Akaufungua Zaidi mlango na kwenda kulitua sinia lile katika meza Ile.. Muda wote alikuwa akitembea katika umakini wa hali ya Juu... Aliujua uwezo wa mwanamke Yule.. Ingawa hakuwahi kupambana naye lakini alishuhudia pale alipokuwa akipambana na kepteni George. Alipolitua Sinia lile akageuka Kutaka kumwambia mwanamke Yule asogee pale mezani.. Lakini Akashtuka baada Ya kukutana na midomo miwili ya Bastola Ikimtizama katika kichwa chake. Ingawa alikuwa akijiamini katika mapambano lakini Hakutarajia Kuiona bastola tofauti na Ile ambayo Aliiona pale mwanzo. Mudy Akaendelea kutabasamu kama hakukuwa na kitu cha hatari mbele yake.. Tabasamu ambalo lilivuka na Kuwa kicheko.. Kicheko chake kikaifanya Sura Yake Iwe katika mikunjo... Lakini kwa mwanamke Yule kicheko kile kilimfanya akipeleke kidole Chake katika kiwambo cha kuruhusu kutoka kwa Risasi... Hakuujua Uwezo wa Mudy na Hakumjua Mudy ni nani... Hakuipata nafasi Ya kuifyatua risasi yake... Sekunde mbili alikuwa Chini Ya Sakafu baada ya kupigwa Pigo moja la karate ambalo lilimmaliza nguvu na Kumfanya abaki pale chini Akitweta....

Mudy Hakutaka kumuendea pale na Vile vile hakutaka kumuua kwa kuwa alijua binti Yule alikuwa akijua mambo Mengi sana katika kisanga kile cha kuuawa kwa mke wa Rais.. Akamuendea pale alipoangukia kwa Sura Ya Upole.. Akamuinua na kumkalisha.. Akaanza kumfuta damu Iliyokuwa ikivuja ikitokea Puani...Kumfuta damu Mwanamke Yule kulimfaya Mudy Akumbuke Tukio ambalo Hatokaa Alisahau. Tukio ambalo litaendelea kubaki katika kumbukumbu Zake... Hasa pale aliporudi nyumbani na kuukuta Mwili wa mkewe na mwanawe kipenzi Wakiwa wamechinjwa. Ni Kisa hicho kilichomfanya awahurumie wanawake.. Licha Ya kuwahurumia huko lakini Bado alikuwa katili kwa kila mwanamke ambaye atakuwa kinyume na Sheria.. Akaifuta Ile damu Ya mwanadada Yule na baada ya Muda walikuwa wamekaa katika Meza Moja wakinywa maziwa Huku Waiongea Hili na Lile kama Watu ambao walikuwa wakifahamiana tokea Zamani.

*******
muda wa dakika kumi mbele wakaonekana wanaume wawili wakitoka katika hoteli ile.. Walikuwa wanaume watupu ambao walikuwa katika mavazi ya kanzu huku vichwa vyao vikiwa vimefunikwa kwa baraghashia.. Wakati Watu wake wakiondoka wakapishana na wanaume wengine watano ambao walikuwa Wamevaa mavazi meusi. Kupishana kwa Wanaume wale kukawafanya wanaume waliovalia Kanzu na baraghashia kutabasamu... Watu wale Watano Wakaingia katika Hoteli ile.. Kila mmoja alikuwa ameupeleka mkono wake Mfukoni.. Hawakuuliza mapokezi bali wakaongoza moja kwa Moja mpaka ghorofa Ya pili ambapo kulikuwa ndipo kwenye kitu walichokuwa wakikihitaji. Safari Ya Wanaume wale Ikaishia kwenye mlango Wa Chumba ambacho alikuwemo Mpelelezi mashuhuri Mohamed Pamoja na Mateka wake.. Kuufikia Mlango kukafuatiwa na Kitendo kingine cha Kuburudisha Machoni katika Kuutazama.. Mlango Ulipigwa teke kisha kila Mmoja Akizama ndani Huku akiruka samasoti na Kuangukiwa upande Mwingine.. Ukimya Wa Ajabu ukatawala Mle ndani.... Hata pale wanaume wale kila mmoja alipoingia hawakukuta kitu chochote Cha maana Zaidi Ya damu ambayo Ilionekana kusambaa katika Chumba kile. Wote Wakachoka Huku wakitizamana... Walikuwa wameachwa katika Mazingira Ambayo Kila mmoja akajua kuwa walikuwa wameingia katika Vita na Mtu mmbaya na mwenye mbinu kali Kushinda wao... Mmoja wa Vijana Wale akatoa simu na kuongea maneno mawili matatu Kisha Akakata..
*******
wanaume wale ambao walionekana katika mavazi Ya kanzu hawakuwa wote wanaume bali mmoja alikuwa mwanamke na Mwingine alikuwa mwanaume. Hawakuwa wengine bali alikuwa mohamedi na Yule mwanamke wakiondoka katika staili ambayo Ilikuwa vigumu Kushtukiwa. Na hata walipopishana na Wanaume wale watano walikuwa wamewatambua..

Safari Yao ikaishia maeneo sinza Mori, Wakatafuta Guest moja nzuri Wakalipia kwa kuandikisha MaJina ya Bandia, muda mfupi baadae walikuwa katika chumba kizuri Wakiwa wao wenyewe wawili... Mohamedi akamsaidia mwanamke Yule kulivua lile vazi kisha wakakaa kitandani Wakitizamana Huku kila mmoja Akisoma mawazo Ya Mwenzie... Walitizama kwa muda kisha Mudy akasimama na Kusogea pale ambapo Alikuwa amekaa Yule msichana, lakini hakufanikiwa kumfikia kwani Alishangaa mwanamke Yule Akijirusha na kumsukuma, Hapo hapo Akashangaa kumuona mwanamke Yule akivuja Damu katika Paji La Uso huku ametambalanyika Chini..
HALI ILITISHA SANA...
Hongera mkuu hadithi nzuri
 
MKE WA RAIS



Mudy alikuwa Nyuma ya pikipiki akiifuatilia gari ya mtu yule aliyeondoka katika makaburi ya Kinondoni kwa wasiwasi mkubwa. Alikuwa amempa nafasi kubwa kwa kumuongoza mbele kwa tofauti ya Magari matatu ili kumfanya asije kushtuka kuwa anafukuzia.. Safari na mfukuzano wao uliishia tamati katika fukwe za bahari ya Hindi maeneo yale Ya masaki. Mudy hakutaka kusimama katika bar Ile bali alichokifanya ni kunyoosha mpaka katika bar ambayo ilikuwa katika eneo lile, akashuka na kuanza kurudi taratibu hasa baada ya kumlipa Dereva Yule. Macho Yake Yalikuwa yakiangaza kila Upande, Alikuwa anaujua mchezo wa watu wale.. Lakini kwa kuwa Alikuwa ameamua kufuatilia tukio la kuuawa kwa mke Wa rais hakujali sana katika lolote ambalo lingetokea. Alikuwa na kila kitu katika mifuko Yake... Akaendelea kulisogelea eneo lile kama Mtu wa Kawaida.. Akaingia katika Hoteli moja ambayo ilikuwa na Bar ndani Yake. Akavuta kiti na kukaa, mara Akamuona Mhudumu akadika haraka na kuuliza kipi ambacho angehitaji Mudy... Huku macho Yake Yakiangalia kwa chati kila mtu katika bar ile, Mudy Akaomba Aletewe Mzinga Wa konyagi... Kuagiza kwake mzinga kukawa kama kumemzubaisha mwanadada Yule... Hata pale Mudy aliporudia tena yule mhudumu alionyesha Kusita.. Lakini kile ambacho hakuna Ambaye amekitarajia kutokea, kikatokea.. Dakika moja mhudumu alikuwa ameduwaa na Ndani Ya Sekunde Ya dakika Ya pili, Mudy Akashangaa kumuona Mhudumu Yule akipaa angani na Kwenda Kuanguka Umbali Mrefu kutoka pale alipokaa Mudy.. Damu Nyingi Ikimvuja katika kifua Chake

Mudy Akaduwaa kwa sekunde na Sekunde Iliyofuata Alikuwa Akichupa na kudondokea upande wa pili wa ukuta wa Bar ile.. Akachomoa bastola Yake tayari Kukabiliana na chochote.. Sehemu Yote Ilikuwa tafrani Huku Wa hudumu wakiangua vilio kupita kiasi... Macho Ya Mudy hayakuwatazama watu waliokuwa wakilia na Kupiga kelele, bali Macho Yake makini Yalikuwa Yakikitazama Chumba ambacho kilikuwa katika Ghorofa Ya nne.. Dirisha Ya Chumba kile lilikuwa limefunguliwa kwa Upenyo Mdogo sana.. Upenyo Ule ungekuwa si Lolote kwa mtu Wa kawaida.. Lakini Kwa Mudy Ulikuwa ni Zaidi Ya Kile ambacho kingedikiriwa na Wengine.. Akajiondoa taratibu na Kuifuata lifti Ya hoteli ile na Muda Mfupi alikuwa katika Korido katika Ghorofa Ya Nne kukifuata kile Chumba Huku mkono wake Ukiwa juu Ya bastola Yake. Akatembea kwa Haraka.. Akakifikia kile Chumba, Akatulia kwa kama Sekunde kuangalia Usalama kwanza kama kutakuwa na Yoyote,,, lakini ukimya Ulikuwa imetawala na Hapakuwa na Mtu Yoyote.. Mudy Akauendea mlango na kujaribu kukinyonga kitasa, akashangaa kuuona Mlango ukifunguka. Macho Yake Yakaangalia kwa Chati na Muda mfupi alikuwa Chumbani huku bastola Mkononi.. Mbele Ya macho Yake Alikuwa Akitizamana na Tukio la Kutisha.. Mtu aliyemfuatilia Kutokea kwenye makaburi Ya kinondoni alikuwa Ameuawa kinyama mle chumbani. Mwili wake Ulikuwa Uchi wa Mnyama Juu Ya kitanda Huku Kisu kikubwa kikiwa katika kifua Chake.. Hali ilikuwa ikitisha sana.. Kwa Mara Ya kwanza Mudy Akahusudu uwezo wa mtu Aliyefanya Mauaji Yale... Akauangalia Mwili wa Marehemu Huku macho Yake Yakizunguka katika Chumba kile.. Hapo Akavutiwa na Kitu Ambacho Alikuiona Pembeni Ya Maiti Yule.. Zilikuwa Picha Za Hayati Mke Wa Rais Akiwa Amepiga na Mwanaume Yule Aliyeuawa Pamoja na Mhudumu ambaye Aliuawa Muda Mfupi uliyopita, Wakati mtu wa Tatu katika Picha Ile alikuwa ni Yule msichana Aliyeuawa kwa Risasi kule Hotelini Sinza lakini akaja kumuona Akiwa Hai... Akainama ili Kuichukua Picha Ile, lakini akasita baada ya Kusikia mtu Akimpigia makofi Kutoka Nyuma Yake... Akageuka Huku tabasamu Usoni... Akajikuta Akitizamana na mdomo Wa bastola kutoka kwa Mtu ambaye Alimjua na Kumtambua... Hakuwa Mwingine Bali Alikuwa Mkurugenzi Mkuu Wa Usalama Wa Taifa Mr Kassim Adnan Kwangay.. Mudy Akahisi Damu Zake Zikimsisimka Kupita kiasi.. Maswali Lukuki Yalikuwa Yakipishanana katika Kichwa Chake.

Akaamua kuyapuuza maswali Na kuitiliza Akili Yake ili kuangalia ni Jinsi gani Anaweza kujiokoa mikononi kwa mtu yule ambaye aliamini ametekwa.. Kukutana uso kwa uso na Mkurugenzi Yule kilikuwa ni Kitu ambacho hakikutegemea kabisaa... Akakiona kiza kinene na Maswali Lukiki katika Mauaji Ya Mke Wa Rais.. Akiwa bado katika tabasamu lile mara Akashangaa kuwaona Watu Wengine Wakiingia pale ndani.. Hawa walikuwa watu Wengine ambao Walimfanya Mudy Auone ugumu katika Kujinasua... Mbele Ya macho Yake alikuwa akiangalia na Waziri wa Ulinzi na Mwenzake Wa Mambo Ya Ndani.. Wote walikuwa wakimtizama mudy Katika Aina Ya hasira na Chuki.. Hapo Mudy Akaiona Hatari Ambayo Ilikuwa Mbele Yake.. Ni Wakati Huo Akiangaliana na Wazito wale ,kitasa kikanyongwa, Wote Wakakosea Kugeuza Sura Zao Kuangalia Nyuma.. Hawakuujua wepesi wa Mudy.. Sekunde Moja ilitosha kufanya Kitu ambacho Kilikuwa hatari katika Maisha Yake... Ni sekunde moja ambayo Ilimkuta Mudy Ikiliparamia dirisha La Kioo na Kuangukia katika Maua Ya Hoteli Ile Kisha akatokomea mitaani Huku Akiwa Amepata mwanga katika uchunguzi Wake Dhidi Ya Mauaji....
Mudy kiboko
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom