Riwaya: Mke wa Rais

Riwaya: Mke wa Rais

MKE WA RAIS

SEHEMU YA 28

Katika kuwapekuwa wakora wale, wakaikuta picha ya kanali Jamila Ikiwa moja kati ya vitu walivyovikuta katika mifuko Ya watu wale. Mudy na George wakatizamana kwa muda.. Hapo hapo wakapeana mikono kuonyesha kuwa wameshakuwa wa moja. Cha kwanza kilichotakiwa kutoka pale ni Mudy kuelekea Nyumbani kwa Jamila.. Huku Kepteni George akienda kwenye ile kampuni ya Simu.. Licha ya kuonyesha kuungana lakini Mudy bado hakutaka kumwambia George kuhusu kuitwa kwake na Rais. George akatangulia kuondoka Huku akimuacha Mudy pale. Baada ya mudy kubaki peke Yake Alichokifanya ni kukiendea Chumba Cha marehemu. Katika chumba hicho hakujua kilichokuwemo lakini Kutokana na kuambiwa kuwa aje aangalie... Akajikuta akipatwa na Hamu ya kuchunguza na kugusa hapa na pale. Akaiendea sehemu ambapo palikuwa na kabati kubwa sehemu ambayo aliambiwa na yule msichana kuwa kuna kitu na atapata mwanga katika kile alichokuwa akikitafuta pale. Kulifikia kabati lile kikafuatia kitendo cha kulisogeza pembeni. Kulisogeza kabati hilo, akapokewa na mlango mbele ya Macho Yake. Hapo akainua mkono na kupapasa juu ya kabati, akakiona kile ambacho alikuwa akikitafuta. Ulikuwa ufunguo wa kukifungulia kimlango kile ambacho kilikuwa kimetengezwa ukutani.

Akauingiza ufunguo, mlango ukakubali.. Kukubali kwa mlango kukafuatiwa ni Mudy kuzama ndani. Hapo akalakiwa na Meza kubwa ambayo Juu yake palikuwa na makaratasi mengi. Akaisogelea ile meza huku moyo ukimdunda.. Alipoifikia Akajipweteka Juu yake na kuanza kupekua hiki na Kile. Punde katika upekuzi Wake akakutana na Bahasha kubwa Ya kaki.. Ilikuwa imetuna kuonyesha kuwa kulikuwa na Vitu ndani Yake. Kabla hajaifungua akaigeuza Nyuma kuitizama.. Hapo akakutaNa na maandishi Yaliyosomeka kama TOP SECRET maandishi ambayo Yaliandikwa Kwa kalamu Yenye Wino mwekundu. Mudy Akifungua.. Ndani akakutana na karatasi kibao ambazo Zimechapwa.. Akaifungua Karatasi Ya kwanza akakutana na Neno MKAKATI WA KUMPINDUA RAIS.. damu Zikamsisimka Mudy.. Hakutegemea Msichana yule kutunza Siri nyeti kama ile. Akatulia akili na kuanza kuisoma. Ulikuwa mpango mahususi Uliowahusisha watu wengi sana.. Mkakati ambao Ulionekana kusimamiwa na Watu watatu ambao wote walikuwa wakijulikana kwa Herufi tu. Mkakati huo pia ulikuwa ukiwashirikisha watu Wengine hasa wanausalama. Na kila mwisho wa Neno kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kikiandikwa ambacho Mudy Hakukitambua kwa wakati Ule.

Karatasi ya pili ilikuwa na neno kubwa lisomekalo KIAPO. hapo kwa Mara ya Kwanza akaliona Jina la Mke wa Rais na Jina la Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa taifa. Pia chini kulifuatiwa na yale Majina ambayo yalikuwa yameandikwa kwa Herufi tu. Na Mwisho kabisa lilikuwa likiandikwa Neno ambalo bado lilikuwa Vigumu Mudy Kulitambua. Mudy akaona kuendelea kusoma akiwa pale ni kuupoteza Muda. Akazikusanya Zile karatasi na kuzichomeka katika Shati lake kisha akapekuwa hiki na kile na alipoona ameridhika akatoka katika Chumba kile.. Lakini Wakati anataka kuufungua mlango wa chumba ili atokee Sebuleni, akahisi Uwepo wa watu katika Sebule. Mkono wake Ukashuka na kuichomoa Bastola Yake Aina Special Colt48.. Akaikamata mkononi kisha kwa macho Yake yaliozoea giza akakiona kivuli cha mtu kikiwa mbele yake. Hapo akaongeza Umakini na kuendelea kuangalia iwapo kulikuwa na Mtu mwingine.. Yeah! Akagundua Uwepo wa mtu mwingine ambaye Alikuwa kwa nje na mtu kwenye Simu. Mudy akaingia pale sebuleni mfano wa kivuli.. Alikuwa hajaonekana kwa Watu Wale. Wakati hajajua kipi cha kufanya akasikia mngurumo wa Gari Ukisimama Nje Ya Nyumba. Mudy akatabasamu.. Alihitaji kuwajua waliokuja na Waliokuwepo. Punde tu mlango ukafunguliwa na Kuingia watu kama Watano Hivi.. Ingawa kulikuwa na Giza lakini hapakuwa na Ugumu Mudy kuwagundua. Kwa Mara Ya pili alimuona Kanali Jamila akiwa na Watu wale.. Ile imani kuwa kanali Jamila Alikuwa msaliti ikajengeka katika kichwa Cha Mudy.

Akasogea taratibu huku umakini ukiongezeka.. Punde akasikia kitu cha baridi kikitua katika kisogo Chake kisha sauti nzito Ikasikika Nyuma Yake. ''' Usijaribu kutingishika.. Ukifanya Hivyo nitausambaratisha Ubongo Wako.. Mudy akatii na Kutulia... Punde akamuona mtu mmoja kati Ya watu wale waliongia na Kanali Jamila Akielekea ilipo swichi Ya kuuwasha Umeme.. Lakini Hakupiga hata hatua moja mlio wa Risasi Ukasikika.. Mudy akashangaa kumuona mtu yule aliyekuwa nyuma yake Akianguka Chini.. Mudy Hakuchelewa alichupa na kuangukia karibu na Swichi.. Kuanguka pale kukafuatiwa ni Risasi Mfululizo Kuelekezwa kwake.. Mudy Akachupa na Kuangukia Nyuma Ya sofa ambalo lilikuwa pale Sebuleni.. Punde akasikia gari Ikiondolewa kwa Kasi Huku milio ya Risasi Ikirindima.. Mudy akaendelea kutulia... Punde Ukimya Wa ajabu Ukatokea... Sehemu Yote ilikuwa kimya Lakini Punde tu akasikia Ving'ora Va Magari Ya polisi.. Mudy akainuka na Kuondoka kwa kupitia Dirashani kabla ya Magari Ya polisi Kufika na Akaianza Safari Kuelekea Nyumbani kwa Kanali Jamila huku kichwani Akijiuliza ni nani amemuokoa Pale?

KESHO
Kiongozi nimeikubali sanaaaa dah naona kesho mbali
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 33

Jenipher alikuwa akisubiri Ruhusa kutoka kwa Mudy ili aondoke Usiku ule kuelekea Arusha. Mkononi alikuwa na kikaratasi ambacho kilikuwa kimeandikwa Namba Ya Nyumba. Lakini Mudy Bado alikuwa Akimshangaa Jenipher... Wakati bado wanatizamana.. MARA MLANGO UKAGONGWA! Bado wote wakatizamana tena.. Hapakuwa na desturi ya kugongwa usiku katika Nyumba ile... Macho Yenye maswali ya Mudy Yakamuangalia Jenipher... Jicho la Sijui la Jenipher likampa Mudy Fursa Ya kuuendea mlango.. Alikuwa katika kiwango Cha Hali Ya juu cha kutamani kuua. Kuuawa kwa George hakukumfanya Mudy asiwe makini na kila alichokuwa akikifanya. Alipiga hatua Katika mwendo wa Tahadhari.. Bastola Ilikuwa mkononi.. Hakuwa peke Yake katika kuufuata Mlango.. Nyuma Yake alikuwepo mwanadada Jenifer naye akiwa na bastola Yake mkononi.. Mkono wa Mudy Ukashika funguo na kuufungua mlango ule.. Aliufungua akiwa ndani.. Akasubiri mtu wa kuingia lakini hawakumuona.. Mudy hakutaka kumtizama Jenipher. Lakini alipohitaji kumuangalia Hakumuona... Hakumuona hata pale Nyuma ambapo alisimama.. Akaipa akili yake kufikiri.. Kufikiri ugongajwi Ule. Mgongaji ambaye amepotea katika namna ya kizungumkuti... Mgongaji ambaye aliugonga mlango mara moja.. Ilikuwa ni kama Ishara Ya namna fulani.. Ishara ambayo hawakuijua na Wala kuitambua ilitoka kwa nani na Kwenda kwa nani.. Hakutaka kujisumbua kumuangalia jenipher alipoelekea.. Bali Mudy Alikuwa Akienda nje kuangalia nani mgongaji.. Huku mdomo wa bastola Ukiwa Umetangulizwa Mbele, Mudy akakishika kitasa na kuuvuta mlango.. Muda mfupi alikuwa Nje..

Alikuwa nje Ambapo alikutana na Mshangao.. Mshangao ambao ulimfanya Amgeukie Mtu aliyemkuta pale Nje. Chini ya Sakafu kulikuwa na Miili ya Watu Wawili wakiwa wameuawa.. Hawakuwa wameuawa kwa risasi bali kila mmoja Alikuwa Amenyongwa Shingo.. Harafu Jenifer alikuwa amesimama mbele Ya miili ile akimuangalia Mudy... Yeah! Ni kweli waliangaliana kwa sekunde.. Mudy akaukubali Uwezo wa Jenipher...

Wakasaidiana kuwaondoa wale maiti pale na kwenda kuwatupa Baharini. Wakarudi ndani wakiwa katika maswali mazito.. Licha ya kuwa katika maswali Hayo, lakini Jenipher bado alikuwa akihitaji Ruhusa Ya kwenda Arusha.. Kwenda kuangalia kile ambacho Hayati Kepteni George Aliwahi kukiona Huko. Kwa mara nyingine wakaangaliana... Na wakati uliofuata walikuwa ndani Ya gari wakiliacha Jiji la Dar es Salaam tayari wakielekea katika Uwanja wa mapambano.. Ilikuwa ni safari Ngumu na ndefu sana.. Lakini kutokana na wote kuwa katika Hamu ya kukijua kilichosababisha kifo Cha mke wa Rais, hawakuuona Ugumu huo..

******

Saa mbili kamili asubuhi baridi Ya jiji la Arusha iliwaraki Mudy na Jenipher ambao ndio kwanza walikuwa wanafika asubuhi ile. Baada ya Mazungumzo Machache Mudy Alimuacha Jenipher Akiendelea na Safari huku wakiahidiana wakutane usiku katika Hoteli ambayo atakuwa amefikia. Ingawa walikwenda kwa pamoja lakini hawakupenda kuishi Hotel Moja kutokana na Usalama wao na kutokujua kwao uwezo wa Watu ambao waliwafuata. Mudy Yeye alikuwa amefikia katika Hotel Mt Kilimanjaro.. Wakati Jenipher alikwenda kufikia katika Hotel Ya Usa River..

Mchana ule kila mmoja aliutumia kwa kujipumzisha ili kuiweka miili yao Sawa tayari kwa Kazi iliyowapeleka Arusha.

Alianza kufika Mudy Katika Hotel Ile Ya Usa River na kuelekea upande wa ukumbi wa chakula.. Akaagiza chakula ambacho alipenda sana kukila.. Muda mfupi alikuwa ameshaanza kula huku macho Yake yakiangaza huku na Huko katika namna ambaye ingekuwa vigumu sana kugundulika na Mtu. Nia yake Ilikuwa nikuona kama kuna mtu ambaye anamfuatilia. Lakini kila mmoja alionekana akiwa na hamsini Zake. Aliendelea kula taratibu Huku akiangalia huku na Huko, mara akamuona Msichana Mrembo akiingia katika Ukumbi ule Wa Hoteli. Alionekana kuwa mwanamke mrembo kupindukia. Mudy alimuangalia mara mbili mara tatu kama Alivyokuwa Akiangalia watu wengine, kisha akampuuzia na kuhamisha Macho Yake kuangalia Sehemu Nyingine. Hapo Macho Yake Yakamuona Jenifer akiwa amekaa mwisho kabisa wa ukumbi ule Wa Chakula akiangalia Sehemu kwa chati.. Mudy aliligundua hilo.. Akafuata Uelekeo wa Macho Yake.. Uelekeo Wa macho ya Jenifer... Akamuona mtu wa makomo akiwa amekaa peke Yake.. Alikuwa ni mwanaume ambaye alionekana Yupo busy na kila wakati alikuwa akitupia Macho mlangoni na wakati mwingine kumwangalia Mudy Katika namna Ya kijasusi..

Mudy akatabasamu, tabasamu ambalo halikuonekana kwa Mtu yoyote zaidi Yake Mwenyewe.. Bado alikuwa akiyatupa Macho Yake kwa Watu wawili.. Yule mwanaume na Yule Mwanamke Mrembo.. Walikuwa Ni Watu walionyesha kuwa wanajuana na Wamekuja pale kwa mpango Maalumu.. Akaichomoa Simu Yake ya mkononi kisha kwa njia ambayo Ilikuwa ngumu Kuonekana kwa Wengine akamtumia Jenipher Sms.. Ilikuwa sms Ya kumwambia awe makini.. Jenipher Akajibu kwa kutabasamu.. Tabasamu ambalo hakulionyesha kwa Kumuangalia Mudy, bali kumuonyesha mwanaume aliyekuwa mbele Yake... Mwanamke Mrembo aliyeingia punde akasogea alipokaa Mud
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 034

Muda Mfupi Baadae Jenifer alikuwa akiinuka na kuelekea msalani. Kuondoka kwa Jenifer kukafuatiwa na Yule mwanamke Mrembo kusogea pale alipokaa Mudy, Bila hata kuuliza akavuta kiti na kukaa... Mudy akashangaa, lakini haukuwa mshangao mkubwa.. Ulikuwa mshangao Wa sekunde mbili kisha ukayeyuka. Hakutaka muongelesha mwanamke Yule.. Kwa kuwa kuna kitu alichokihisi kutoka kwake. Punde macho Yake yakawaona Wanaume wawili waliojazia wakiinuka pale na kuelekea kule msalani alipoelekea Jenipher. Mudy hakuonyesha kushtuliwa na kile alichokiona.. Hakutaka kufanya Hivyo kwa kuwa alijua nini kilichomleta Mwanaumke yule. Ndio kwanza akaendelea kutabasamu Huku akiendelea na Chakula chake. Macho Yake bado yalikuwa yakimwangalia mwanamke Yule... Bado alikuwa akiangalia kwa namna ya Hila.. Punde akamuona Jenifer akitokea msalani.. Safari Hii hakuwa Jenifer Yule.. Mikono Yake Ilionekana kutoka kufanya shughauli Nzito.. Macho Yao yakakutana.. Mudy Akampa Ujumbe kwa Macho... Kutoka kwa Jenifer kulileta mshtuko kwa Yule Dada na Punde alikuwa ameinuka na sekunde mbili baadae alikuwa akielekea Msalani.. Mudy AkamuangaliaJenifer kwa Chati... Kisha akainuka na kuelekea kule kule msalani.. Akampita Jenipher kama Hamfahamu akaongoza bafuni... Mkono wake haukuwa na sababu ya kushika bastola.. Akaongoza mpaka vilipo vyoo vya kiume... Kuingia kwake pale akakutana na mwanamke Yule akiwa anatoka. Wakaangalia kwa sekunde.. Wakasomana wao walikuwa nani kupitia Macho Yao.. Mudy bado tabasamu lake Lilikuwa mdomoni.

Tabasamu ambalo lilionyesha kumdhihaki mwanadada Yule.. Akamtizama tena kisha kwa sauti Ya upole akamuomba Waongee.. Binti akaona ndio muda wa kufanya Walichotumwa.. Mkono wake ulikuwa ukishuka alipo hifadhi bastola Yake.. Lakini hakuujua Wepesi Wa Mudy.. Hakujua kuwa mbele Yake alikuwa amesimama mpelelezi bora wa Afrika... Sekunde alikuwa akiichomoa bastola yake, lakini Sekunde Ya pili alijikuta akiisalimia Ardhi kwa pigo moja la
karate Ambalo lilimuingia sawa sawia. Wakati Mudy akitarajia binti yule angesalimu amri.. Akashangazwa na Binti alipoinuka katika Staili ya Tai kwong do.. Staili ambayo hupendwa kutumiwa na wapiganaji Wengi wa kichina hasa Hayati Bluce Lee. Ilikuwa stali aliyoambatana na Mateke mfululizo.. Mudy akamkinga kwa Ufundi lakini binti lipokuja kubadili mtindo na kutumia Mtindo wa Martial Combart.. Mudy Alijikuta kwa Mara Ya kwanza akipokea Mapigo matatu Mfululizo Ambayo Yalimtupa Chini kama Furushi.

Yeah! Kazi ilikuwa nzito tofauti na alivyotegemea. Akainuka kwa kuchupa na kumuendea binti kwa mapigo Mchanganyiko... Yalikuwa mapigo ambayo aliyapiga kwa Minajili Ya kuuwa.. Hakulifikia lengo lake.. Kwani Binti alikuwa Amechupa na kuangukia upande wa pili wa Hoteli Ile... Mudy maye akafanya hivyo.. Akaruka na kutua nje.. Alipotua hakumuona Mtu zaidi Ya kuliona gari likipotelea katika Vichochoro vya Jiji la Arusha. Mudy akajua kazi Ilikuwa imeanza.. Walikuwa wamekwisha gundulika Kwamba wapo katika jiji la Arusha. Hakutaka kurudi ndani Alichokifanya ni kumtumia Jenipher ujumbe Mfupi kuwa wakutane kwenye bar fulani ambayo Ilikuwa Jirani na Pale.

*******

walikuwa watu watatu katika sebule kubwa yenye thamani nyingi sana Za ndani. Walikuwa katika kikao kizito juu ya nini kifanyike katika kumnyamazisha Mohamedi.. Wote walikuwa katika kiwango cha juu Cha Hasira na Tangu walivyokuwa wakimuwekea Mudy Mitego ya kumnasa alikuwa akiikwepa na Kuwakimbia kirahisi sana.. Kiti kikubwa mbele Alikuwa amekaa Waziri Wa Ulinzi Wa Nchi Mr Daniel Mtoto... Kushoto kwake alikuwa amekaa Waziri Wa Mambo Ya Ndani mheshimiwa Salim Salim na kulia kwake Kulikuwa na Waziri Wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Bi Cecilia Bruno Peter.. Wote kwa pamoja Walikuwa kimya wakijaribu kuongea Hili na lile.. Punde mlango Wa Ukumbi waliokuwemo Ulifunguliwa na Wote wakasimama kwa Heshima. Yule yule mwanaume mkakamavu na Mwenye cheo kikubwa katika Nchii alikuwa akiingia akiwa Ametangulizana na Watu wengine watatu. Kuingia kwao kukafuatiwa na Ukimya Wa Muda Mfupi.. Ukimya Ambao Ulivunjwa na Mlio Wa Simu Iliyokuwa ikiita pale Ndani... Wote Wakaangaliana kwa Sekunde kadhaa kisha Mwanaume Yule akauvuta mkono wa Simu na Kuipeleka Sikioni... Muda mfupi alikuwa akipokea Habari kutoka sehemu fulani katika nchi hii.. Baada Ya Simu kukatwa.. Akawageukia Wanamkutano Wenzake na kuanza kumtizama mmoja baada Ya Mwingine. Alikuwa akiwaangalia katika Namna Ambayo wenzake Wote waliitambua kuwa mambo bado Sio Mazuri Kwa Upande Wao... Kutazamana kwao kukafuatiwa na kauli kutoka kwa Mtu Yule Mzito.

'''Mohamedi yupo arusha.. Na amepambana na watu wetu lakini walishindwa kumdhibiti na kuishia kumkimbia.. Lakini licha Ya Mohamedi nasikia Kuna Mwanamke Mwingine amejitokeza na kuwauawa Watu wetu Wawili ambao walimshuku na kuanza kumfuatilia... Mtoa habari Wetu anasema Anahisi Mwanamke Huyo Yupo pamoja na Mohamedi, Ingawa hilo hana uhakika nalo. Kutokana na Hilo naomba kuahirisha kikao hiki na Tutume Vijana Zaidi kuelekea Arusha Kwa Mapambano..
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 35

Ilipoishia

kutokana na hilo naahirisha kikao ili tuwaandae vijana waende arusha kwa sababu ya kupambana..

Sasa Endelea

Kujulikana Mapema kuwa walikuwa Arusha kilimshangaza Sana Mudy... Akajiona ni mjinga kupindukia. Hawezi kuwa Salama Wakati watu unaowawinda wanajua kila unachokifanya. Muda mfupi alikuwa akiuacha mtaa ule na kutokea mtaa wa pili.. Kisha akaingia mtaa wa Tatu kabla Hajaingia katika bar Ambayo waliikusudia kuwepo pale. Aliingia ndani na kutafuta sehemu Ya pembeni ambayo hapakuwa na Watu, Mudy akakaa na kuagiza kinywaji.. Punde mhudumu akafika akiwa na kinywaji akamuwekea Mudy kisha Yeye akaondoka. Macho Ya Mudy Yaliyozoea Giza na Macho Yenye Uwezo mkubwa wa kuwatambua watu wa aina tofauti. Yalikuwa Yakiangaza huku na Huko kutizama kama kulikuwa na Chochote ndani Ya bar Ile.. Lakini Hayakugundua Chochote. Akaendelea kunywa bia Yake kwa Utulivu Huku wakati mwingine akiacha hili na kufanya lile.. Mpaka muda huo hakuwa amemuona Jenipher wala kujibiwa ujumbe ambao alimtumia, lakini kwa kuwa alimtambua Jenifer hakuwa na Wasiwasi... Akaendelea kunywa Huku Macho yake Yakizunguka Sehemu Zote. Punde akamuona Jenifer akiingia akiwa katika Vazi la Usiku.. Vazi ambalo liliwafanya Baadhi ya wanaume katika Bar Ile kugeuza Shingo Zao kumwangalia Binti Yule.. Mudy alimtazama tu kisha kuhamisha Macho yake na kuangalia Sehemu fulani.. Kuangalia pale Macho yake Yakanasa Sura Ya mtu mmoja.. Alikuwa mtu ambaye alimfahamu. Alikuwa Mwanamke Ambaye aliwahi kumuokoa kipindi alipokwenda kwenye jumba ambalo aliuawa Mke Wa Rais. Mtu ambaye alishuhudia akipigwa Risasi Mbele Ya Macho Yake... Lakini ikatokea mwanamke Yule kuwa mzima kitu ambacho bado kilikuwa kinasumbua kichwa Cha Mohamedi.. Bado Macho Yake yalikuwa Yakimuangalia yule mwanamama.. Mwanamama Ambaye alikuwa ametulia huku kila wakati akiangalia Saa Yake kuonyesha kuwa palikuwa na Mtu ambaye alikuwa Akimsubiri..

Upande Wa Jenifer, Bado alikuwa akiendelea na kila kitu ambacho alikusudia kukifanya.. Kila wakati alikuwa akimuangalia Mohamedi, lakini Mohamedi alionekana Hakuwepo pale.. Macho Yake Yalikuwa Yakiangalia Upande fulani... Upande ambao ulimpa jenifer hamu ya kukiona kile ambacho kilikuwa kikiangaliwa na Mohamedi. Hakufanikiwa kukiona alichokusudia.. Alijikuta Yupo Chini ya Ardhi, risaasi ikimpita sentimita Chache.. Wakati huo huo Mohamedi Alikuwa akichupa hapa na kutua pale Huku bastola Yake ikikohoa mfululizo.. Ulikuwa mchezo wa kitaalamu; Mchezo ambao Ulikuwa ukipigwa kwa Utaalamu Wa Hali Ya Juu.. Punde Taa Zikazimwa.. Sehemu Yote ikawa giza... Kipindi yote hayo yanafanywa Jenifer alikuwa ameshahama pale alipokuwa ameangukia, na Sasa alikuwa katika Upande Ule ambao alikuwa amekaa Yule mwanamke... Hata Mudy alikuwa hapo.. Alikuwa Hapo akiwa na Dhumuni la kumteka Mwanamke Yule... Wote walikuwa wakimuwania Mwanamke Yule...

Hawakuujua utamu na utaalamu wa mwanamke Yule... Hawakuuona wepesi Wake Wakati alipomsukuma Jenifer na kuanguka Chini, kisha Yeye kuondoka katika Aina ambayo Ilikuwa akileta Mvuto katika Macho Ya Watu wachache ambao walikuwa wakimtizama... Punde wakakifikia kiti.. Kiti ambacho kilikaliwa na Mwanamama Yule huku mwenyewe akionekana kutoweka Eneo lile pasipokuonekana.. Mudy na Jenifer Wakaangaliana Kwa Mara Nyingine kisha wakainuka na Muda Mfupi walikuwa Nje Ya bar ile wakitembea Mtaani kama Bibi na bwana wakionekana kabisa kupotea kwa Ile Furaha Yao..

*******
saa saba na Nusu usiku Mudy alikuwa akirudi hotelini kwake huku akiwa katika Mawazo mazito Sana.. Hiki alichokutana nacho Arusha si kile ambacho alikitegemea Hapo Mwanzo.. Kujulikana kwa Uwepo wake katiKa Jiji la Arusha kulimfanya Mohamedi Kuiona kazi Iliyombele Yao kuwa ngumu sana.. Kushambuliwa na kufuatiliwa katika matukio Ya aina moja kulimpa picha kuwa kulikuwa na Mtu au Watu ambao walikuwa wakiifuatilia Mienendo Yao tokea Walipokuwa Dar Es Salaam.

Haiwezekana kuingia Jana na leo maaduI wajue kuwa Mudy na Jenifer wapo Arusha, kisha kuwashambulia katika matukio mawili. Ilikuwa ni Picha tosha kuwa wanajulikana. Alizapanda Ngazi kwa haraka huku akiendelea kuwa makini kwa kila hatua... Wakati Akiukaribia Mlango Wa Chumba Chake, nyuma yake akahisi Michakato na vishindo Vya Miguu Ya Binadamu.. Akageuka akitegemea kumuona Mtu lakini alikuta patupu.. Mkono Wake ukaitembelea Bastola Yake pale alipoihifadhi... Alipohakikisha bado imetulia akaendelea hatua kuufuata mlango Wa Chumba Chake.. Akaufikia na Kuingiza Ufunguo Katika Sehemu Yake, punde Mlango Ukatii.. Mudy Akaingia Ndani. Kuingia ndani akapokelewa na kitu kisichokuwa Cha kawaida.. Juu ya kitanda cha Chumba Chake alikuta kichwa Cha mtu... Mtu Huyu alikuwa Ameuawa kwa kukatwa kichwa.. Mudy Akaduwaa huku Mkono Wake Ukiwa umeifikia Bastola Iliyonayo.. Akapiga hatua katika kuelekea pale Kitandani kilipo kichwa kile... Lakini kabla hajafanya Lolote:. Simu Yake Ikaingia Sms... Akaichomoa Simu na kutaka Kuusoma ujumbe, lakini kabla hajafanya hilo, akasikia Kitu Cha Baridi kikimgusaa..
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 36

Ilipoishia

Wakati akipiga hatua kwenda pale kitandani palipo na kile kichwa kitupu.. Simu Yake ikaingia Ujumbe Mfupi... Mudy akachomoa simu kutaka kuusoma ujumbe ule, lakini hakulifanya Hilo.. Akahisi kitu cha baridi kikimgusaa

SASA ENDELEA

ulikuwa mdomo wa bastola ukiwa kisogoni kwake... Mdomo ambao ulisindikizwa na Sauti nzito Nyuma yake.. ''Usijaribu Kujitingisha'' .. Mudy Akatii bila kuonyesha Ubishi... Kutii kwake hakukumaanisha kuwa alikuwa akiogopa.. Hakumaanisha kuwa hakuwa na uwezo wa kulianzisha.. Lakini alitulia kuipa akili Yake muda wa kufikiria na kuamua kitu sahihi.. Bado alikuwa na bastola Yake mkononi na Bado alikuwa na Uhuru Wa kufanya kitu Chochote.. Lakini hakuwa na Haraka, alikuwa akisubiri kuona mwisho wa mtu aliyemuweka Chini... Lakini huko hakufika.. Punde mlango ukasukumwa kwa nguvu.. Yule mtu aliyemteka Mudy Alifanya Kosa kugeuka.. Akakutana na Teke la Shingo kutoka kwa Jenifer... Akapepesuka lakini hakuanguka.. Ni wakati huo akakutana na mateke aina ya Round kick mfululizo.. Hakuweza kuhimili hilo.. Akaanguka Juu Ya kitanda akiwa amelegea kama Mlenda.. Mudy Akamuwahi kwa kumtuliza na Pigo Moja la Nyuma Ya kisogo.. Muda Mfupi hakuwa Yule tena.. Alikuwa amekwisha zimia. Ni hapo walipotaka kumbeba kuondoka naye, ndipo lilipotokea tukio ambalo hawakulitarajia.. Taa Zikazimwa Hotel nzima.. Kisha milio ya risasi kusikika kwa mfululizo kama wa Dakika Tano.. Mudy na Jenifer Walikuwa wamesharuka pembeni pale Risasi Zilipomuingia Yule Jambazi na kuufumua Mwili wote. Punde ukimya ukarudi katika eneo la Hotel..

Mudy na Jenifer bado walikuwa wametulia.. Bado hawakuamini kama hapakuwepo na watu pale ndani Ya Hotel. Lakini Ukimya alipozidi Mudy na Jenipher Wakajiinua.. Muda mfupi baadae Walikuwa wakiiacha Hotel ile huku wakionekana ni wazee wa umri mkubwa kutokana na Walivyojibadilisha. Mudy Alikuwa amevaa kanzu Fupi na Baraghashia kichwani, huku akibandika mindevu mingi Ya bandia.. Jenifer alikuwa katika Juba lililofunika mpaka Uso wake. Mavazi hayo yaliwasaidia sana, hata pale walipopishana na Askari Hawakuweza kujulikana. Walionekana ni watu wazima waliochelewa kutoka sehemu fulani na sasa walikuwa wakirudi Nyumbani. Wakaikatisha mitaa ya Jiji la Arusha bila wasiwasi Wowote.. Na hata walipotokea sehemu ambayo alikuwa akiishi Jenifer Hawakutaka kusimama.. Walikuwa hawaamini makazi Yao tena. Kitendo cha wao kujulikana mapema kuwa wapo Arusha kilikuwa kitu hatari sana kwao.. Sasa iliwabidi wawe makini.. Lakini umakini huo nilazima Waende Sehemu ambayo marehemu George aliwaandikia Sehemu. Walikuwa wakipambana kwa sababu ya kifo cha George lakini Pia walikuwa wakikitafuta Chanzo cha kuuawa kwa Mke Wa Rais.. Kwahiyo haikuwa Picha Nzuri kujulikana mapema kuwa wapo pale...

*******

wazee wawili wa kike na kiume walionekana wakiwa wamesimama mapokezi katika Hoteli moja kando kando ya Mji Wa Arusha. Ukiwaangalia kwa mara Ya kwanza ungedhani ni Wenye Miaka Sabini ama sitini.. Mwanaume aliyevaa koti kubwa Chini Akiwa na makata mbuga Alionekana ni mwenye kuonyesha kuchoka Sana.. Mwanamke Alikuwa katika gauni refu aina Ya Dela, Huku Chini Ya miguu Yake kukiwa na malapa. Walikuwa wakihitaji Chumba kimoja katika Hoteli ile.. Hawa hawakuwa Wengine Walikuwa ni Kanali Jamila na Luteni Sevenlee.. Walikuwa wapo Arusha kwa kazi Maalumu. Kazi Ambayo ilikuwa lazima Ifanyike ndani Ya Siku tatu.. Baada Ya kuingia katika Chumba Chao, Cha kwanza kufanya ni kuwasiliana na MwanamKe Aitwaye Revina Michael ambaye alikiwa spy wa siri kutoka shirika la Kijasusi la Rwanda. Huyu alikuwa komando ambaye alipitia mashirika mengi Ya kijasusi. Alikuwa ni Mwanamke mpole kwa kumtizama lakini unapokutana naye akiwa amebadilika Alikuwa mtu Mbaya Kupindukia... Mawasiliano Yakafanyika na wakapewa ramani Ya kile ambacho kinaendelea... Punde walikuwa wameshabadili mavazi Yao.. Wakaondoka katika Hoteli ile kwa kupitia njia ya panya.. Wakatokea mtaani na kuongoza kuelekea sehemu ambayo waliambiwa kuwa Mudy Alionekana Hapo akiwa na mwanamke Ambaye haikujulikana mara Moja alikuwa nani kwake.

*****

mudy na jenifer walikuwa umbali wa hatua kumi kutoka ilipo hoteli fulani.. Nao walikuwa wakielekea katika hoteli hiyo ili kupata chumba cha kujihifadhi.. Kukaribia kwao katika hoteli ile, wakaliona tukio Jingine.. Tukio la Watu kutoka ndani Ya Hoteli kwa kupitia Dirishani.. Akamvuta Jenifer pembeni.. Mudy alikuwa amehisi kitu fulani kutoka kwa watu Wale... Hakukuwa na Mtu sahihi asiye na Dhambi Anayeweza kupitia Dirishani Wakati ameshalipa pesa Yake.

Akahisi kuwa lazima walikuwa watu kama wao.. Lakini Hakulitilia maanani Hilo Suala. Kutoka pale pembeni walipojibanza Mudy akawaona Watu anaowajua.. Watu ambao walimsaliti na kumuua George.. Watu ambao walikuwa ni Wamoja kati Ya Watu ambao walikuwa kwenye Kikosi Cha Uchunguzi Juu Ya Kifo Cha Mke Wa Rais.. Alikuwa Na Uwezo wa kuwaua, lakini Hakutaka Kufanya Hivyo.. Alihitaji kumjua nani ambaye alikuwa amepanga kufanya mapinduzi.. Kisha hawa watafuata
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 33

Jenipher alikuwa akisubiri Ruhusa kutoka kwa Mudy ili aondoke Usiku ule kuelekea Arusha. Mkononi alikuwa na kikaratasi ambacho kilikuwa kimeandikwa Namba Ya Nyumba. Lakini Mudy Bado alikuwa Akimshangaa Jenipher... Wakati bado wanatizamana.. MARA MLANGO UKAGONGWA! Bado wote wakatizamana tena.. Hapakuwa na desturi ya kugongwa usiku katika Nyumba ile... Macho Yenye maswali ya Mudy Yakamuangalia Jenipher... Jicho la Sijui la Jenipher likampa Mudy Fursa Ya kuuendea mlango.. Alikuwa katika kiwango Cha Hali Ya juu cha kutamani kuua. Kuuawa kwa George hakukumfanya Mudy asiwe makini na kila alichokuwa akikifanya. Alipiga hatua Katika mwendo wa Tahadhari.. Bastola Ilikuwa mkononi.. Hakuwa peke Yake katika kuufuata Mlango.. Nyuma Yake alikuwepo mwanadada Jenifer naye akiwa na bastola Yake mkononi.. Mkono wa Mudy Ukashika funguo na kuufungua mlango ule.. Aliufungua akiwa ndani.. Akasubiri mtu wa kuingia lakini hawakumuona.. Mudy hakutaka kumtizama Jenipher. Lakini alipohitaji kumuangalia Hakumuona... Hakumuona hata pale Nyuma ambapo alisimama.. Akaipa akili yake kufikiri.. Kufikiri ugongajwi Ule. Mgongaji ambaye amepotea katika namna ya kizungumkuti... Mgongaji ambaye aliugonga mlango mara moja.. Ilikuwa ni kama Ishara Ya namna fulani.. Ishara ambayo hawakuijua na Wala kuitambua ilitoka kwa nani na Kwenda kwa nani.. Hakutaka kujisumbua kumuangalia jenipher alipoelekea.. Bali Mudy Alikuwa Akienda nje kuangalia nani mgongaji.. Huku mdomo wa bastola Ukiwa Umetangulizwa Mbele, Mudy akakishika kitasa na kuuvuta mlango.. Muda mfupi alikuwa Nje..

Alikuwa nje Ambapo alikutana na Mshangao.. Mshangao ambao ulimfanya Amgeukie Mtu aliyemkuta pale Nje. Chini ya Sakafu kulikuwa na Miili ya Watu Wawili wakiwa wameuawa.. Hawakuwa wameuawa kwa risasi bali kila mmoja Alikuwa Amenyongwa Shingo.. Harafu Jenifer alikuwa amesimama mbele Ya miili ile akimuangalia Mudy... Yeah! Ni kweli waliangaliana kwa sekunde.. Mudy akaukubali Uwezo wa Jenipher...

Wakasaidiana kuwaondoa wale maiti pale na kwenda kuwatupa Baharini. Wakarudi ndani wakiwa katika maswali mazito.. Licha ya kuwa katika maswali Hayo, lakini Jenipher bado alikuwa akihitaji Ruhusa Ya kwenda Arusha.. Kwenda kuangalia kile ambacho Hayati Kepteni George Aliwahi kukiona Huko. Kwa mara nyingine wakaangaliana... Na wakati uliofuata walikuwa ndani Ya gari wakiliacha Jiji la Dar es Salaam tayari wakielekea katika Uwanja wa mapambano.. Ilikuwa ni safari Ngumu na ndefu sana.. Lakini kutokana na wote kuwa katika Hamu ya kukijua kilichosababisha kifo Cha mke wa Rais, hawakuuona Ugumu huo..

******

Saa mbili kamili asubuhi baridi Ya jiji la Arusha iliwaraki Mudy na Jenipher ambao ndio kwanza walikuwa wanafika asubuhi ile. Baada ya Mazungumzo Machache Mudy Alimuacha Jenipher Akiendelea na Safari huku wakiahidiana wakutane usiku katika Hoteli ambayo atakuwa amefikia. Ingawa walikwenda kwa pamoja lakini hawakupenda kuishi Hotel Moja kutokana na Usalama wao na kutokujua kwao uwezo wa Watu ambao waliwafuata. Mudy Yeye alikuwa amefikia katika Hotel Mt Kilimanjaro.. Wakati Jenipher alikwenda kufikia katika Hotel Ya Usa River..

Mchana ule kila mmoja aliutumia kwa kujipumzisha ili kuiweka miili yao Sawa tayari kwa Kazi iliyowapeleka Arusha.

Alianza kufika Mudy Katika Hotel Ile Ya Usa River na kuelekea upande wa ukumbi wa chakula.. Akaagiza chakula ambacho alipenda sana kukila.. Muda mfupi alikuwa ameshaanza kula huku macho Yake yakiangaza huku na Huko katika namna ambaye ingekuwa vigumu sana kugundulika na Mtu. Nia yake Ilikuwa nikuona kama kuna mtu ambaye anamfuatilia. Lakini kila mmoja alionekana akiwa na hamsini Zake. Aliendelea kula taratibu Huku akiangalia huku na Huko, mara akamuona Msichana Mrembo akiingia katika Ukumbi ule Wa Hoteli. Alionekana kuwa mwanamke mrembo kupindukia. Mudy alimuangalia mara mbili mara tatu kama Alivyokuwa Akiangalia watu wengine, kisha akampuuzia na kuhamisha Macho Yake kuangalia Sehemu Nyingine. Hapo Macho Yake Yakamuona Jenifer akiwa amekaa mwisho kabisa wa ukumbi ule Wa Chakula akiangalia Sehemu kwa chati.. Mudy aliligundua hilo.. Akafuata Uelekeo wa Macho Yake.. Uelekeo Wa macho ya Jenifer... Akamuona mtu wa makomo akiwa amekaa peke Yake.. Alikuwa ni mwanaume ambaye alionekana Yupo busy na kila wakati alikuwa akitupia Macho mlangoni na wakati mwingine kumwangalia Mudy Katika namna Ya kijasusi..

Mudy akatabasamu, tabasamu ambalo halikuonekana kwa Mtu yoyote zaidi Yake Mwenyewe.. Bado alikuwa akiyatupa Macho Yake kwa Watu wawili.. Yule mwanaume na Yule Mwanamke Mrembo.. Walikuwa Ni Watu walionyesha kuwa wanajuana na Wamekuja pale kwa mpango Maalumu.. Akaichomoa Simu Yake ya mkononi kisha kwa njia ambayo Ilikuwa ngumu Kuonekana kwa Wengine akamtumia Jenipher Sms.. Ilikuwa sms Ya kumwambia awe makini.. Jenipher Akajibu kwa kutabasamu.. Tabasamu ambalo hakulionyesha kwa Kumuangalia Mudy, bali kumuonyesha mwanaume aliyekuwa mbele Yake... Mwanamke Mrembo aliyeingia punde akasogea alipokaa Mud
Cc jogoo mtata
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 36

Ilipoishia

Wakati akipiga hatua kwenda pale kitandani palipo na kile kichwa kitupu.. Simu Yake ikaingia Ujumbe Mfupi... Mudy akachomoa simu kutaka kuusoma ujumbe ule, lakini hakulifanya Hilo.. Akahisi kitu cha baridi kikimgusaa

SASA ENDELEA

ulikuwa mdomo wa bastola ukiwa kisogoni kwake... Mdomo ambao ulisindikizwa na Sauti nzito Nyuma yake.. ''Usijaribu Kujitingisha'' .. Mudy Akatii bila kuonyesha Ubishi... Kutii kwake hakukumaanisha kuwa alikuwa akiogopa.. Hakumaanisha kuwa hakuwa na uwezo wa kulianzisha.. Lakini alitulia kuipa akili Yake muda wa kufikiria na kuamua kitu sahihi.. Bado alikuwa na bastola Yake mkononi na Bado alikuwa na Uhuru Wa kufanya kitu Chochote.. Lakini hakuwa na Haraka, alikuwa akisubiri kuona mwisho wa mtu aliyemuweka Chini... Lakini huko hakufika.. Punde mlango ukasukumwa kwa nguvu.. Yule mtu aliyemteka Mudy Alifanya Kosa kugeuka.. Akakutana na Teke la Shingo kutoka kwa Jenifer... Akapepesuka lakini hakuanguka.. Ni wakati huo akakutana na mateke aina ya Round kick mfululizo.. Hakuweza kuhimili hilo.. Akaanguka Juu Ya kitanda akiwa amelegea kama Mlenda.. Mudy Akamuwahi kwa kumtuliza na Pigo Moja la Nyuma Ya kisogo.. Muda Mfupi hakuwa Yule tena.. Alikuwa amekwisha zimia. Ni hapo walipotaka kumbeba kuondoka naye, ndipo lilipotokea tukio ambalo hawakulitarajia.. Taa Zikazimwa Hotel nzima.. Kisha milio ya risasi kusikika kwa mfululizo kama wa Dakika Tano.. Mudy na Jenifer Walikuwa wamesharuka pembeni pale Risasi Zilipomuingia Yule Jambazi na kuufumua Mwili wote. Punde ukimya ukarudi katika eneo la Hotel..

Mudy na Jenifer bado walikuwa wametulia.. Bado hawakuamini kama hapakuwepo na watu pale ndani Ya Hotel. Lakini Ukimya alipozidi Mudy na Jenipher Wakajiinua.. Muda mfupi baadae Walikuwa wakiiacha Hotel ile huku wakionekana ni wazee wa umri mkubwa kutokana na Walivyojibadilisha. Mudy Alikuwa amevaa kanzu Fupi na Baraghashia kichwani, huku akibandika mindevu mingi Ya bandia.. Jenifer alikuwa katika Juba lililofunika mpaka Uso wake. Mavazi hayo yaliwasaidia sana, hata pale walipopishana na Askari Hawakuweza kujulikana. Walionekana ni watu wazima waliochelewa kutoka sehemu fulani na sasa walikuwa wakirudi Nyumbani. Wakaikatisha mitaa ya Jiji la Arusha bila wasiwasi Wowote.. Na hata walipotokea sehemu ambayo alikuwa akiishi Jenifer Hawakutaka kusimama.. Walikuwa hawaamini makazi Yao tena. Kitendo cha wao kujulikana mapema kuwa wapo Arusha kilikuwa kitu hatari sana kwao.. Sasa iliwabidi wawe makini.. Lakini umakini huo nilazima Waende Sehemu ambayo marehemu George aliwaandikia Sehemu. Walikuwa wakipambana kwa sababu ya kifo cha George lakini Pia walikuwa wakikitafuta Chanzo cha kuuawa kwa Mke Wa Rais.. Kwahiyo haikuwa Picha Nzuri kujulikana mapema kuwa wapo pale...

*******

wazee wawili wa kike na kiume walionekana wakiwa wamesimama mapokezi katika Hoteli moja kando kando ya Mji Wa Arusha. Ukiwaangalia kwa mara Ya kwanza ungedhani ni Wenye Miaka Sabini ama sitini.. Mwanaume aliyevaa koti kubwa Chini Akiwa na makata mbuga Alionekana ni mwenye kuonyesha kuchoka Sana.. Mwanamke Alikuwa katika gauni refu aina Ya Dela, Huku Chini Ya miguu Yake kukiwa na malapa. Walikuwa wakihitaji Chumba kimoja katika Hoteli ile.. Hawa hawakuwa Wengine Walikuwa ni Kanali Jamila na Luteni Sevenlee.. Walikuwa wapo Arusha kwa kazi Maalumu. Kazi Ambayo ilikuwa lazima Ifanyike ndani Ya Siku tatu.. Baada Ya kuingia katika Chumba Chao, Cha kwanza kufanya ni kuwasiliana na MwanamKe Aitwaye Revina Michael ambaye alikiwa spy wa siri kutoka shirika la Kijasusi la Rwanda. Huyu alikuwa komando ambaye alipitia mashirika mengi Ya kijasusi. Alikuwa ni Mwanamke mpole kwa kumtizama lakini unapokutana naye akiwa amebadilika Alikuwa mtu Mbaya Kupindukia... Mawasiliano Yakafanyika na wakapewa ramani Ya kile ambacho kinaendelea... Punde walikuwa wameshabadili mavazi Yao.. Wakaondoka katika Hoteli ile kwa kupitia njia ya panya.. Wakatokea mtaani na kuongoza kuelekea sehemu ambayo waliambiwa kuwa Mudy Alionekana Hapo akiwa na mwanamke Ambaye haikujulikana mara Moja alikuwa nani kwake.

*****

mudy na jenifer walikuwa umbali wa hatua kumi kutoka ilipo hoteli fulani.. Nao walikuwa wakielekea katika hoteli hiyo ili kupata chumba cha kujihifadhi.. Kukaribia kwao katika hoteli ile, wakaliona tukio Jingine.. Tukio la Watu kutoka ndani Ya Hoteli kwa kupitia Dirishani.. Akamvuta Jenifer pembeni.. Mudy alikuwa amehisi kitu fulani kutoka kwa watu Wale... Hakukuwa na Mtu sahihi asiye na Dhambi Anayeweza kupitia Dirishani Wakati ameshalipa pesa Yake.

Akahisi kuwa lazima walikuwa watu kama wao.. Lakini Hakulitilia maanani Hilo Suala. Kutoka pale pembeni walipojibanza Mudy akawaona Watu anaowajua.. Watu ambao walimsaliti na kumuua George.. Watu ambao walikuwa ni Wamoja kati Ya Watu ambao walikuwa kwenye Kikosi Cha Uchunguzi Juu Ya Kifo Cha Mke Wa Rais.. Alikuwa Na Uwezo wa kuwaua, lakini Hakutaka Kufanya Hivyo.. Alihitaji kumjua nani ambaye alikuwa amepanga kufanya mapinduzi.. Kisha hawa watafuata
Ubarikiwe ibra
 
Back
Top Bottom