Riwaya: Mke wa Rais

Nilimpoteza mtu muhimu sana katika maisha yangu. Picha mnayoiona hapo ni yakipenzi changu Neema. Mwanamke ambaye alikuwa ndio furaha yangu. Lakini Mungu aliamua kunipokonya kwa kuwa alimpenda kuliko mimi. Ndio nimeinuka naendelea kukusanya nguvu ili kuifikisha tamati. Nipo kwenye kipindi kigumu sana lakini nisameheni sana kwa muda wote huo.
Pole sana ibra Mungu akutie nguvu
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 002

Mwanaume akageuka kumtazama mwanamke akashangaa kukutana na mdomo wa bastola, bastola ambayo ilikuwa mikononi kwa mwanamke Yule. Macho Yalikuwa mekundu kwa Hasira.. Bastola Ikakohoa mara Mbili Risasi mbele Zikapenya Katika Paji la Uso la Mwanaume Yule. Ubongo Ukaruka na Kusambaa Chumba Kizima. Mwanaume Akaanguka chini na Kutulia.. Alikuwa Tayari ni Maiti.

Mlio wa bastola Uliosikika kutoka ndani uliwashtua walinzi wake na kila mmoja akaupeleka mkono wake kiunoni wakaibuka na Silaha.. Hawakuta kuingia kwa Kupitia getini... Wote walichupa hewani na kudondokea ndani.. Wakauendea mlango wa ndani kwa Kasi Ya Ajabu.. Kazi ambayo haikuwahi kutokea.. Sekunde kumi baadae walikuwa ndani ya Jumba lile. Wakapigwa na butwaa baada ya kukuta kiza totoro.. Wakatazamana na Kupiga hatua kuelekea ndani Zaidi... Walipofika karibu na Mlango wa Kutokea Upande wa Pili wa Jengo lile.. Wote wakahisi kukanyaga kitu kama Maji.. Lakini Uzito wa kitu kile kikawafanya walinzi Wainame na Kugusa yale maji.. Kila mmoja Kengele Ya Hatari Ikalia kichwani mwake.. Wakajua mke wa Mheshimiwa Alikuwa Hatarini.. Hawakusubiri.. Mmoja Akarudi nyuma na Kuruka Flyng kick Na Kuingia na mlango mpaka ndani... Kufika ndani Walichupa tena kila Mmoja Akaangukia pembeni Huku Bastola Mkononi.. Chumba Kilikuwa giza na Hawakusikia Hata mkoromo wa Binadamu... Mmoja Alipoangukia Akachupa tena Mpaka Iliposwtch ya Kuwashia taa na Kuifyatua..

Chumba Kizima Kiliwaka taa.. Kitu cha kwanza kuonekana machoni kwa walinzi wale ilikuwa maiti, maiti ambayo ilikuwa imelala katikati ya dimbwi kubwa la damu. Ubongo ulikuwa umesambaa mule ndani... Wakahamisha macho Yao na Kuyapeleka Kitandani wakapigwa na Butwaa Baada Ya kumuona Mke Wa Rais akiwa na Bastola Ya Kirusi Mkononi Huku akionekana MachoZi Kumtoka na Kumlowanisha. Hawakutaka kusubiri... Wakamuinua pale na Kumkokota Mpaka nje.. Walipofika Nje Cha kwanza kukifanya Waliichukua Ile Bastola Mikononi mwake kisha wakamuingiza ndani Ya Gari na kuliondoa maeneo Yale kabla polisi Hawajafika Eneo lile.

Gari Ikatembea kwa Mwendo Wa kasi sana kuelekea Nyumbani kwa Mheshimiwa maeneo Ya Kinondoni... Gari ikafika na Moja kwa Moja Kuingia ndani.. Maafisa Usalama Waliokuwepo waliiona Hali Ile ya kuonyesha kuchanganyikiwa kwa Mke Wa Rais lakini kwa kuwa Alikuwa na Walinzi Wake maalum Walimuacha bila Ya Kumuuliza.

Baada ya kuingia pale na Kushuka kwenye gari Kisha kuingia Ndani, aliongoza moja kwa moja bafuni huku akionekana ni Mwenye huzuni na Majuto Usoni. Aliingia bafuni na kuyavua mavazi Yake... Akafungulia maji na kuyaacha yaendelee kushuka katika mwili wake. Tukio zima la kupigwa Picha Lilimuumiza sana.. Hakujua ni Watu gani waliofanya vile na Walifanya kwa Lengo lipi... Akaiona Heshima yake kama Mke wa Rais Ikianza Kushuka.. Akawaza kile ambacho alikuwa akikifanya kikimfikia Rais au Wananchi Wakiona Atakuwa katika Wakati Gani? Aliuona Mwisho Wake mbaya, alijiona Mjinga Kushawishika kufanya ujinga.. Je ni Wakina nani lakini? Na Walifanya kwa Lengo lipi na ni Upi mwisho wangu katika Kadhia hii? Hakuwa na Majibu kwa Muda ule.. Hakuwa na jibu la kumfanya Ajisikie Vizuri.. Akakata Tamaa na Kukaa Juu Ya Sinki La Kuogea.. Macho Yake yakitazama Paa la Jumba lile la Kifahari... Mawazo Juu ya Mumewe Yakawa yanapita Usoni Mwake... Akajilazimisha Kutabasamu Lakini Haikuwa Hivyo.. Hakukuwa na Tabasamu Wala Hakukuwa na Kicheko.... Yalikuwa machozi, machozi Na Majuto.. Akainuka pale na Kuchukua Vali lake Maaulum... Akajiangalia kisha Kwa Sauti Ya Kujiamini Akanena... NITAMUUA YOYOTE NITAKAE MUHISI.. kisha akatoka Mle Bafuni na Kuingia Chumbani Kwake... Alipoingiza Mguu wake Ndani akapokelewa na Mlio Kuonyesha Kulikuwa Sms Kwenye Simu Yake.... Moyo Ukampiga Paaa!! Kisha Mikono kumtetemeka. Hakujua kwanini lakini alijikuta Akiiogopa mpaka simu yake. Akapiga hatua kisha Akaichukua Simu na Kuusoma Ujumbe Ule... Alichokiona Kwenye Simu kilimfanya Aanguke Chini Kama Mzigo.....

UNADHANI AMEONA KITU GANI?
Story nzur
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 054

AKASIKIA YOWE LIKITOKEA NYUMA YAKE. Mudy akageuka bastola ikiwa mkononi.. Macho yake yakatua kwenye mwili wa mtu uliyolala chini ukivuja damu. Mudy hakujiuliza mara mbili wala tatu, akaondoka katika purukushani zile. Aliondoka huku akijua vijana wake walikuwa Nyuma yake. Kitendo cha kuuona mwili wa mtu ukiwa na matundu ya Risasi lilikuwa ni jibu kuwa Yupo mtu, mtu ambaye alikuwa akisafisha masalia. Hakutaka kubaki katika giza.. Alihitaji kumuona Huyo kijana.. Alitaka kufahamu alitoka wapi? Lakini hakumuona, hakumuona kwa kuwa feri haikuwa salama tena. Watu walikuwa wakikimbia hovyo.. Mudy akajiunga kwenye mbio zile, mbio ambazo hakuujua mwisho wake utakuwa upi. Hakujali hilo, bali alihitaji kuliacha eneo lile. Huku mkono wake ukiwa umekamata bastola iliyofichwa na vazi lake, akatoweka katika macho ya watu.. Sasa alikuwa akielekea kule walipo Jenifer na Didas. Alihitaji kushiriki katika kumlinda Rais. Mawazo yake yalikuwa mbali sana huku akili Yake ikichemka katika kufikiria jinsi Ya kumuokoa Rais.

Wa kwanza kufika msibani alikuwa Jenifer.. Miwani myeusi machoni, mavazi meusi Ya heshima na kuonyesha msiba, alikuwa amewahi na kubana upande wa kushoto wa kuingilia.. Upande ambao ulikuwa na uwezo wa kuona kila kiumbe ambacho kinaingia Eneo lile. Macho yake hayakutulia Sehemu Moja.. Alikuwa akitizama kila upabde kwa hila.. Wakati akitizama akawaona watu wawili wakiingia.. Wa mbele aliweza kumtambua lakini wa nyuma hakuwahi kumuona popote. Mbele alitangulia REVINA MICHAEL na nyuma alikuwa akifuatia mwanadada mwingine.. Mwanadada ambaye hakuonyesha Uhatari wa Aina Yoyote.. Bado alikuwa akiwatizama.. Hata Macho Yake yalipokutana na Yale ya Revina akaliona tabasamu. Tabasamu Ambalo halikuwa Rasmi. Lilikuwa tabasam tofauti sana, tabasamu lililobeba maswali lukuki kichwani kwa Jenifer. Hakujua kwa nini alihisi kitu katika kutokana na tabasamu la revina.. Lakini aliona kuna Ujumbe ambao ulifikishwa kwake pasipokuambiwa. Akatulia.. Alitulia kwa muda wa Dakika kama Tano, punde akawaona wanaume wengine wawili wakiingia. Hawa walionekana kuwa ni wageni. Wageni katika jiji la Dar es salaam, na wageni katika nchi Ya Tanzania. Kila mmoja alikuwa katika suti matata, suti ambazo ziliwatoa na kuwafanya wapendeze sana.. Kengele Za hatari zikagonga kichwani mwake. Mwendo wa wanaume wale ulikuwa mwndo ambao aliufahamu.. Aliufahamu kwa kuuona Sehemu. Lakini hakujua aliuona wapi na katika Shughuli gani, alichokumbuka ni kwamba kuna mahali aliwahi kuuona huu mwendo wa watu hawa. Licha ya kutokukumbuka huu mwendo wa watu hawa bado alikuwa akiwatilia mashaka huku akiwatizama wanapoelekea.

Sehemu yote iliwekwa chini ya vijana kutoka Idara Ya Usalama wa Taifa. Kila mgeni aliyeingia alipewa utaratibu wa kukaa na kusubiri ratiba kamili ya Mazishi ya Captain George.

Wakati yote hayo yakiendelea, katika Jumba fulani karibu na sehemu yenye msiba alionekana mwanadada Akiingia. Aliingia kama mgeni wa kawaida.. Aliingia kama mteja, na hata alipoulizia Chumba hakusita kuambiwa kuwa vipo na vilikuwa vikimsubiri. Haukupita Muda mrefu kukamilisha ulipaji na kukabidhiwa Funguo ambazo zingemuwezesha kuingia chumbani kwake. Alipoondoka tu kuzikwea Ngazi Nyuma Yake akafika mtu mwingine.. Huyu alikuwa mwanaume wa makamo.. Alikuwa mwenye uwalaza na mwenye kuonekana na mvi kichwani. Macho yake yalionekana kuwaka yakitizama kila kona ya Jengo lile. Naye akakiulizia Chumba, alipotajiwa akataka kujua kama ni Jirani na mwanamke aliyeingia Muda mfupi Uliyopita.. Akajibiwa kama alivyotarajia kuwa ni karibu na chumba cha mwanadada aliyeingia hivi punde. Akatabasamu, akabeba mzigo wake na kuelekea juu. Alipanda ngazi huku akiwa makini kwa kila kitu, alitegemea chochote kutokea pale..Kuondoka kwa mwanaume Yule kukaleta ukimya... Ukimya ambao ulivunjwa na kuingia kwa mwanaume Mwingine.. Huyu alikuwa ni mwanaume ambaye alioneka kama mcheza Sinema. Suti yake aliovaa ilimpendeza Sana na kutengeneza maswali kwa Watoto wa kike.. Alipoingia tu hakwenda mapokezi kama waliomtangulia, yeye aliongoza moja kwa Moja kuelekea Juu.

Bastola ilikuwa ikichungulia kuwaonyesha watu kuwa huyu alikuwa mtu Hatari. Mtu ambayr hakuwa na Muda wa kucheka.. Akazipanda ngazi kwa Haraka bila kuhisiwa.. Alipomaliza ngazi akapokewa na Ukimya wa Ajabu.. Ukimya ambao ulimfanya mwanaume Yule kuongeza Umakini, Umakini Uliosababisha Achomoe Badstola Yake.. Akaongeza Hatua mbili mbele, akapokewa na Mwili wa Mwanaume Ukielea Katikati Ya dimbwi la DAMU HUKU KISU KIKUBWA KIKIONEKANA KIMEZAMISHWA TUMBONI. utumbo ulikuwa umetoka nje.. Mwanaume Yule hakujishuhulisha na Ule mwili.. Bado alihitaji kumpata Aliyemkusudia, Kumpata akiwa Hai au Mfu.. Hakuwa Mwanaume Mwingine, hakuwa mpiganaji Mwingine.. Huyu Alikuwa Mohamedi... Naam Huyu alikuwa Mudy akiutafuta ushahidi Kwa udi na Uvumba.. Bado Ukimya Ulitawala na Bado Damu ilinukia.. LANINI MOHAMED HAKUOGOPA..
Dah hii hadithi balaa
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 29

Kilikuwa kitu ambacho hakikuaminika machoni kwa mpelelezi Yule. Kila alipokuwa akitafuta mwenye majina yenye herufi tu hakuweza kugundua lolote lile. Mudy akaondoka katika Nyumba ile Kwa kupitia njia ile ile alioingilia. Kichwani alikuwa ameshapata mwanga kuwa chanzo cha mauaji Ya mke wa Rais ni kutaka kwao kumpindua Rais.. Lakini licha ya kuhisi Hivyo, lakini bado kitendo cha mke wa Rais kuuawa kulikuwa na Sababu ambazo bado hakutaka kuziamini kwa wakati Ule. Maswali mengi kwa nini mke wa Rais alienda Kule mbezi yalikuwa ni Mashaka. Mashaka ambayo yalileta Hisia. Hakutaka kuzidharau Hisia Zake akaamua kutafuta na kujua kiini cha tatizo lililopo.. Pia kuwajua wale Watu watatu ambao majina yao yapo kwa herufi tu. Ingawa katika akili Yake alijua kuwa Waziri Wa Mambo Ya ndani na Waziri Wa ulinzi Walikuwemo katika kile ambacho alikuwa akikitafuta. Akaiendea Tax moja kati Ya nyingi Zilizojipanga Pale. Akaingia na kumuamuru Dereva Ampeleke kibaha. Kupelekwa kwake kibaha kulikuwa tofauti na Mawazo Yake ya Kwanza kwamba aende kupekuwa nyumbani kwa kanali Jamila.

Aliamua kwenda kibaha kwa sababu ya kuhitaji utulivu pia akihitaji kupekua mafaili mengi sana ambayo aliyachukua kutoka nyumbani kwa mwanamke Yule aliyeuawa. Tax ilitembea katika mwendo wa kawaida huku Muda Mwingi Mudy Akiutumia kutupia macho Yake nje kuangalia Iwapo kuna watu wanaomfuatilia. Lakini hakukuwa na kitu Cha Aina Hiyo.

*********

Gari Ya Captain George Ilisimama mtaa wa Tatu kutoka Sehemu ambayo Alikuwa akielekea. Akashuka na Kuingia katika barabara Ambayo kwa Usiku ule haikuwa na Watu Wengi kutokana na kuwa Usiku Mwingi sana. Alitembea kwa Umakini katika Eneo lile la Mlimani mpaka alipoivuka barabara na kuingia Eneo la mlimani City.. Hapo akahisi kuwa hakuwa peke yake katika safari Yake hiyo.. Hakumuona mtu lakini katika hisia Zake ambazo hutakiwa kuheshimiwa alikuwa amehisi kuwa kulikuwa na mtu sehemu fulani akimuangalia ama Kumfuatilia. Akaendelea kutembea huku Akiangaza Jicho lake katika namna ambayo ingeweza kuona Chochote hata kama pangekuwa na Giza la Aina gani. Licha ya kutizama kote lakini Hakumuona mtu. Akaendelea kutembea Huku Kengele Ya Hadhari akimkumbusha. Muda Wote mkono wake ulikuwa ndani ya Mifuko Ya Suruali Yake alipohifadhi bastola Tayari kwa kumlipua Yoyote ambaye angetokea. Akatokea Upande Wa chini ambapo palikuwa giza Lengo likiwa ni kuwazuga endapo kulikuwa na Watu wakimfuatilia. Baada ya kuingia upande Wa Chini akaanza kurudi kinyumenyume mpaka alipolifikia lango la Kuingilia Ndani akachomoa Funguo zake Malaya na Kuamza kufungua.. Lakini kabla hajafanikiwa Mlinzi Wa Eneo Lile akafika akiwa na Kirungu na kumtaka Kepteni George Atulie. Hakujua alikuwa anaongea na Mtu gani.. Akiwa amemsogelea kwa ukaribu Sana.. George akafyatuka teke kali ambalo lilimpata Yule mlinzi kwenye Korodani. Akapiga Yowe kubwa kwa maumivu.. Lakini hapo hapo akakutana na pigo jingine la Karate Mlinzi Akaanguka Chini kama Mzoga. George akamburuza na Kumuweka Kando. Akaliendea lango tena lakini kabla hajalifungua Akahisi Vishindo vikitokea Nyuma Yake. Akatulia tuli. Mara akamuona mlinzi Na wakati huo huo akasikia mlinzi Yule Akimuita Mwenzake. Hakumpa nafasi.. Alimnyatia na Kumtia Pigo moja la Shingo akazimia.. Akamchukua na kuweka pamoja na mlinzi Wa mwanzo.

Akaliendea geti na Kulifungua.. Muda Mfupi alikuwa ndani Sehemo iliyoonekana kuwa kama Ukumbi Wa mikutano. Akatembea Haraka Haraka mpaka pale alipouona Mlango Wa Chumba kilichoandikwa MAWASILIANO. Akausogelea kisha Akachoa funguo na kuanza kuufungua.. Kabla Hajafika popote Taa za Ukumbi Ule Zikawaka... Hapo hapo akasikia Sauti za makofi kutoka kwa watu ambao Walionekana kuwa Zaidi Ya Mmoja wakimpongeza kwa Kuingia Mle ndani.. Mkono wake Mwepesi Ulikuwa Tayari Umeshafika mahali alipoihifadhi bastola Yake.. Lakini vile vile Hakujua Wepesi wa Watu ambao walikuwa ndani Ya Ukumbi ule.. Akajikuta akikutana na Teke kali... Ingawa alijaribu kulikinga lakini kiasi fulani Lilimuingia. George Akasimama Vizuri kisha akawatazama watu waliomo.. Hapo ndipo alipobaki mdomo Wazi... Mbele Yake Kulikuwa na Watu Saba.. Wote walikuwa watu ambao aliwajua. Macho Yake Yalikuwa Yakiwaangalia Kanali Jamila, Luteni Sevenlee... Mkurugenzi Wa Usalama Wa Taifa Mr Adnani Kassim Kwangaya pamoja Viongozi Waandamizi katika Serikali Ile.. George akaduwaa Zaidi.. Alikuwa ameduwaa kwa kuwa Hakuwa na Ujanja tena.. Alipowaza kuhusu Mudy Kwenda Nyumbani kwa Kanali Jamila Akauona Mwisho Wake. Hakuona Atatokaje na Kuwa hai katika Mikono ile. Kwa Mara Ya kwanza marafiki Zake ambao walitoka Wote Masomoni katika Chuo Cha makomandoo kule Urusi Walikuwa Ameshamsaliti.

Wakati Akifikiria Hilo akawaona Watu wale Wakimsogelea Kwa Karibu Zaidi na Mbaya Zaidi Kila mmoja Alikuwa na Bastola Tayari kuifyatua na kuusambaratisha Mwili Wa Kepteni George. Hapo George Akakaa tayari Kwa Mapambano.. Hakuwa Tayari kufa kikondoo. Hatua Tano kabla HawaJAfikia TAA ZIKAZIMWAAA

SEHEMU YOTE IKABAKI GIZA

MKE WA RAIS

SEHEMU YA 35

Ilipoishia

kutokana na hilo naahirisha kikao ili tuwaandae vijana waende arusha kwa sababu ya kupambana..

Sasa Endelea

Kujulikana Mapema kuwa walikuwa Arusha kilimshangaza Sana Mudy... Akajiona ni mjinga kupindukia. Hawezi kuwa Salama Wakati watu unaowawinda wanajua kila unachokifanya. Muda mfupi alikuwa akiuacha mtaa ule na kutokea mtaa wa pili.. Kisha akaingia mtaa wa Tatu kabla Hajaingia katika bar Ambayo waliikusudia kuwepo pale. Aliingia ndani na kutafuta sehemu Ya pembeni ambayo hapakuwa na Watu, Mudy akakaa na kuagiza kinywaji.. Punde mhudumu akafika akiwa na kinywaji akamuwekea Mudy kisha Yeye akaondoka. Macho Ya Mudy Yaliyozoea Giza na Macho Yenye Uwezo mkubwa wa kuwatambua watu wa aina tofauti. Yalikuwa Yakiangaza huku na Huko kutizama kama kulikuwa na Chochote ndani Ya bar Ile.. Lakini Hayakugundua Chochote. Akaendelea kunywa bia Yake kwa Utulivu Huku wakati mwingine akiacha hili na kufanya lile.. Mpaka muda huo hakuwa amemuona Jenipher wala kujibiwa ujumbe ambao alimtumia, lakini kwa kuwa alimtambua Jenifer hakuwa na Wasiwasi... Akaendelea kunywa Huku Macho yake Yakizunguka Sehemu Zote. Punde akamuona Jenifer akiingia akiwa katika Vazi la Usiku.. Vazi ambalo liliwafanya Baadhi ya wanaume katika Bar Ile kugeuza Shingo Zao kumwangalia Binti Yule.. Mudy alimtazama tu kisha kuhamisha Macho yake na kuangalia Sehemu fulani.. Kuangalia pale Macho yake Yakanasa Sura Ya mtu mmoja.. Alikuwa mtu ambaye alimfahamu. Alikuwa Mwanamke Ambaye aliwahi kumuokoa kipindi alipokwenda kwenye jumba ambalo aliuawa Mke Wa Rais. Mtu ambaye alishuhudia akipigwa Risasi Mbele Ya Macho Yake... Lakini ikatokea mwanamke Yule kuwa mzima kitu ambacho bado kilikuwa kinasumbua kichwa Cha Mohamedi.. Bado Macho Yake yalikuwa Yakimuangalia yule mwanamama.. Mwanamama Ambaye alikuwa ametulia huku kila wakati akiangalia Saa Yake kuonyesha kuwa palikuwa na Mtu ambaye alikuwa Akimsubiri..

Upande Wa Jenifer, Bado alikuwa akiendelea na kila kitu ambacho alikusudia kukifanya.. Kila wakati alikuwa akimuangalia Mohamedi, lakini Mohamedi alionekana Hakuwepo pale.. Macho Yake Yalikuwa Yakiangalia Upande fulani... Upande ambao ulimpa jenifer hamu ya kukiona kile ambacho kilikuwa kikiangaliwa na Mohamedi. Hakufanikiwa kukiona alichokusudia.. Alijikuta Yupo Chini ya Ardhi, risaasi ikimpita sentimita Chache.. Wakati huo huo Mohamedi Alikuwa akichupa hapa na kutua pale Huku bastola Yake ikikohoa mfululizo.. Ulikuwa mchezo wa kitaalamu; Mchezo ambao Ulikuwa ukipigwa kwa Utaalamu Wa Hali Ya Juu.. Punde Taa Zikazimwa.. Sehemu Yote ikawa giza... Kipindi yote hayo yanafanywa Jenifer alikuwa ameshahama pale alipokuwa ameangukia, na Sasa alikuwa katika Upande Ule ambao alikuwa amekaa Yule mwanamke... Hata Mudy alikuwa hapo.. Alikuwa Hapo akiwa na Dhumuni la kumteka Mwanamke Yule... Wote walikuwa wakimuwania Mwanamke Yule...

Hawakuujua utamu na utaalamu wa mwanamke Yule... Hawakuuona wepesi Wake Wakati alipomsukuma Jenifer na kuanguka Chini, kisha Yeye kuondoka katika Aina ambayo Ilikuwa akileta Mvuto katika Macho Ya Watu wachache ambao walikuwa wakimtizama... Punde wakakifikia kiti.. Kiti ambacho kilikaliwa na Mwanamama Yule huku mwenyewe akionekana kutoweka Eneo lile pasipokuonekana.. Mudy na Jenifer Wakaangaliana Kwa Mara Nyingine kisha wakainuka na Muda Mfupi walikuwa Nje Ya bar ile wakitembea Mtaani kama Bibi na bwana wakionekana kabisa kupotea kwa Ile Furaha Yao..

*******
saa saba na Nusu usiku Mudy alikuwa akirudi hotelini kwake huku akiwa katika Mawazo mazito Sana.. Hiki alichokutana nacho Arusha si kile ambacho alikitegemea Hapo Mwanzo.. Kujulikana kwa Uwepo wake katiKa Jiji la Arusha kulimfanya Mohamedi Kuiona kazi Iliyombele Yao kuwa ngumu sana.. Kushambuliwa na kufuatiliwa katika matukio Ya aina moja kulimpa picha kuwa kulikuwa na Mtu au Watu ambao walikuwa wakiifuatilia Mienendo Yao tokea Walipokuwa Dar Es Salaam.

Haiwezekana kuingia Jana na leo maaduI wajue kuwa Mudy na Jenifer wapo Arusha, kisha kuwashambulia katika matukio mawili. Ilikuwa ni Picha tosha kuwa wanajulikana. Alizapanda Ngazi kwa haraka huku akiendelea kuwa makini kwa kila hatua... Wakati Akiukaribia Mlango Wa Chumba Chake, nyuma yake akahisi Michakato na vishindo Vya Miguu Ya Binadamu.. Akageuka akitegemea kumuona Mtu lakini alikuta patupu.. Mkono Wake ukaitembelea Bastola Yake pale alipoihifadhi... Alipohakikisha bado imetulia akaendelea hatua kuufuata mlango Wa Chumba Chake.. Akaufikia na Kuingiza Ufunguo Katika Sehemu Yake, punde Mlango Ukatii.. Mudy Akaingia Ndani. Kuingia ndani akapokelewa na kitu kisichokuwa Cha kawaida.. Juu ya kitanda cha Chumba Chake alikuta kichwa Cha mtu... Mtu Huyu alikuwa Ameuawa kwa kukatwa kichwa.. Mudy Akaduwaa huku Mkono Wake Ukiwa umeifikia Bastola Iliyonayo.. Akapiga hatua katika kuelekea pale Kitandani kilipo kichwa kile... Lakini kabla hajafanya Lolote:. Simu Yake Ikaingia Sms... Akaichomoa Simu na kutaka Kuusoma ujumbe, lakini kabla hajafanya hilo, akasikia Kitu Cha Baridi kikimgusaa..
 
MKE WA RAIS

MWANDISHI IBRAHIM MASIMBA
*****
Kazi ambayo alitaka kuifanya tayari ilishafanywa na Sohwa. Hata pale alipomuona Sohwa akimburuza yule jasusi hakutaka kushangaa wala kusubiri. Akajitoa pale akiwa na bastola yake mkononi. Hawakuongea kitu zaidi ya kutizamana. Muda mfupi walikuwa wakiondoka eneo lile wakiwa sambamba na mtu yule ambaye alikuwa akiburuzwa na Sohwa. Hapo ndipo Jenipher akipotambua kuwa mtu huyu hakuwa maiti, mtu huyu hakuwa mfu bali alikuwa Amepotezwa fahamu kwa makusudi ilikusaidia kazi ambayo ilikuwa mbele yao. Alitakiwa kuwa chanzo cha kuwapata na kuwarudisha wahaini wote. Kwa kuwa ulikuwa usiku na hawakujua nani yupo ama alikuwepo eneo lile, walichoamua ni kutokutumia usafiri. Waliamua kutembea kwa miguu huku mateka wao akiwa begani kwa sohwa. Jenipher alikuwa nyuma akiwa amekamatia bastola mbili na Sohwa alikuwa mbele akiwa na mwili wa mtu yule begani. Kila mmoja alikuwa akimlinda mwenzake, kila mmoja alikuwa hapo akielekea katika kuhakikisha wanafika salama na mateka wao. SOHWA hakuwa katika wasiwasi, sohwa hakuwa katika kuamini kwamba mateka huyo angeweza kurudiwa na fahamu kwa muda ule kutokana na sindano aliomchoma. Wakazidi kutembea usiku huo bila kukutana na kizuizi chochote, lakini umbali kidogo wa hatua kama tano wakaanza kukutana na miili kadhaa ya binadamu ikiwa imelaliana. Miili ambayo haikuonekana kuwa na majeraha ama matundu ya risasi, miili ambayo haikuonyesha suluba. Bali ilikuwa miili ilioonyesha kuvunjwa shingo iwe kwa karate, judo ama martial combart. Hilo likamfanya sohwa amgeukie Jenipher na kumtizama kwa jicho la maswali, jicho lenye kutaka majibu kuhusu yule aliefanya mauaji yale ya kupendeza machoni mwake. Majibu kuhusu uuaji ambao kwa mara ya mwisho Sohwa aliuona akiwa katika Jiji la Monaco nchi ufaransa walipokwenda kwenye mission moja ya kumchukua Mtu mmoja ambaye alikuwa akitafutwa na idara zote za usalama katika nchi ya urusi kutokana na kuvujisha taarifa ambazo hazikuipendeza Urusi. Jennifer naye akamuangalia kwa jibu la sijui. Sio kwamba alikuwa anaujua, la hasha hakuwa anajua, hakuwa anamjua mtu huyo alieua kwa kuvunja shingo..

"Hii ni Kama Staili ya Willy Gamba ama Joram Kiango." Akanong'ona Jenipher kwa sauti ambayo ilitoka pasipo na uhakika.

"Willy Gamba ama Joram Kiango? Hapana Huyu ni mwanaharamu Mwingine. Huyu ni mwanaharamu mwingine kutoka Afrika.. lakini bado siamini kama bado yupo katika medani hii." Akajibu Sohwa kwa kirefu. Aliujua ufundi wa mtu huyu, aliutambua uuaji huu, uuaji ambao haukuwa mgeni katika kumbukumbu zake.

"Mwanaharamu? " akauliza Jenipher.

"Yeah! Mwanaharamu kutoka Afrika kusini." Akajibu Sohwa akianza kupiga hatua akiondoka eneo lile huku tabasamu likiupamba uso wake, tabasamu likichukua nafasi katika sura yake nzuri. Lilikuwa tabasamu la kukipenda kile, tabasamu la kujua kwamba mwanaharamu mwingine ameongezeka katika hili. Akazidi kutembea akicheka na kutabasamu kisha kwa sauti tamu na ya kujiamini akasema.

"Kazi imekwisha."

********
Mwanga wa Jua la asubuhi ndio kitu kilimshtua Mohamedi, kutoka kwenye usingizi wa kifo. Alikuwa bado amefumba macho wakati alipohisi kitu kama mwanga ukimmulika usoni. Akaanza kufumbua macho taratibu akiangaza huku na huko. Hapo akashangazwa na mazingira, mazingira ambayo kwanza yalikuwa mageni kwake. Alishangaa kujiona amelala juu ya kitanda tena akiwa amefunikwa shuka Jeupe. Akafumbua macho zaidi huku akiendelea kushangaa.. bado hakurudiwa na kumbukumbu kwamba ilikuwaje. Bado hakurudiwa na kumbukumbu ya kukumbuka wapi alikuwepo kabla ya kufika pale. Hilo likamfanya aitulize akili yake na kuanza kukumbuka kila kitu. Alitulia kwa muda akijaribu kuupa nafasi ubongo wake lakini hilo halikutendeka, alitaka kujiondoa kwanza pale. Alitaka kujua wapi alipo. Kitendo cha kujikuta yupo sehemu ngeni machoni mwake, kilimshangaza na kumpa wasiwasi. Wakati akiliwaza hilo, akaisikia michakato ya Viatu, michakato ambayo ilikuwa inakuja pale pale mlangoni mwa chumba alichokuwepo. Akajifunua shuka tayari kwa kuinuka kumkabiri mwenyeji wake. Lakini wakati akiianza kufunua shuka ndipo alipouona mlango ukifungukiwa kisha akamuona mtu akiingia, mtu ambaye alivalia koti kubwa huku akiwa ameachia mindevu. Licha ya mabadiliko hayo lakini Mudy hakuchelewa kumtambua, hakuchelewa kumjua mtu huyu, licha ya kumjua na kumuona hapa lakini alishakutana naye katika matukio kadha wa kadha.

"Bastard!? Akaita Mudy kwa mshangao.

"MOA!" Akaita yule mwanaharamu. Kisha akaendelea. "Pole sana kwa tukio la jana. Sindano waliokuchoma ilikuwa hatari sana kama usingepata tiba ya Haraka. Nashukuru huyu dada hapa amewahi kukufanyia huduma ya haraka kuitoa sumu mwilini. Anaitwa Neema Habibu (pumzika katika Amani Mama. Bado machozi Yangu Yanatoka Na hayajaacha tokea uliponiacha. I still loving u). Huyu ni Daktari pia ni mtu kama sisi katika fani hii." Aliongea mwanaharamu huku akinyoosha kidole sehemu ambayo alisimama Neema. Mudy akaigeuza shingo yake kutizama kule alipo. Akakutana na mwanamke mrembo kupindukia. Tabasamu halikubanduka mdomoni.

"Karibu MOA! Jisikie upo nyumbani. Tupo hapa kwa ajili ya africa na safari hii tumekuja hapa kwa ajili ya TANZANIA. Yalikuwa maneno matamu kutoka kwenye kinywa cha mwanamke Mrembo. MOA akatulia na kuendelea kumtizama huku akikumbuka kile ambacho kilimkuta kule mpaka kumfikisha pale. ALIHITAJI NA ALITAKA SANA KUJUA. LAKINI ANGEJUAJE?

TUSUBIRI TUONE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom