Riwaya: Mke wa Rais

Kumbe bado inaendelea dah! Niliikatia tamaa siku nyingi. Asante Ibra, nimejiunga tena.
 
MKE WA RAIS
MTUNZI IBRAHIM MASIMBA

Zilibaki sekunde thelathini katika muda ambao alipewa na Sohwa. Hakutakiwa kuzidisga hata sekunde. Hakutakiwa kuongeza hata Nukta. Haikuwa hivyo kwa Jenipher, haikuwa hivyo kwa kuwa alizidisha sekunde tatu katika muda ambao alipewa. Alikiuka miiko ya kiusalama, alikiuka miko ya kijasusi, miko ya kutokudharau chochote kile, miiko ya kutozidisha kitu katika kitu kingine ulichopewa. Ndipo hapo alipotaka kukifanya kile ambacho alitakiwa kufanya. Yes akafanikiwa kufanya.. lakini wakati anataka kufanya kile ambacho alitakiwa kufanya kabla, taa zikawashwa wakati huu risasi zikivurumishwa kuelekea pale alipokuwa amesimama. Alihisi kutendeka kitendo kile, hivyo pale taa Zilipowashwa Jenipher alikuwa amesharuka na kuangukia pembeni kabisa mwa chumba kile. Risasi bado hazikukoma, risasi bado hazikuacha kurushwa. Lakini kitu ambacho kilikuwa kikimsumbua ni kule kutokuwaona ama kuwasikia watu wanaovurumisha Risasi. Akaipa akili yake uhuru wa kutulia, akaupa ubongo muda wa kufanyakazi. Macho yakawa na kazi ya kuangalia kisha mikono yake ilikuwa na kazi mbili tofauti. Mmoja ulikuwa umeshikilia bastola, huku mkono mwingine ukiwa umeshikilia CD ndogo ambayo aliichukua pale kwenye mitambo. Bado Risasi hazikusimama, licha ya kutokusimama lakini pia bado hakuwa akiwaona wala kuwasikia watu ambao mwanzo alijua ni walinzi wa jengo lile. Hilo likamfanya aongeze umakini, kwanini hakuna watu? Kwa nini siwasikia? Mbona risasi haziji upande wangu? Yalikuwa maswali ambayo hayakupata majibu. Muda mfupi akatingisha kichwa baada ya kugundua kitu. Alijua hapakuwa na walinzi na risasi ambazo zilikuwa zikivurumishwa, zilikuwa zikitokea kwenye mitambo maalum ambayo ilisetiwa. Kulitambua hilo likampa fursa ya kusimama na kuanza kuipiga tena hatua, hatua ambazo hazikutofautiana na kule macho yalipotazama. Akaiweka akili katika utayari wa kufanyakazi. Akakivuka kizingiti huku risasi zikiendelea kuvurumishwa. Wakati anaukaribia mlango ili awezekutoweka katika eneo lile, akakiona kitasa kikitingishwa, kabla hajakaa sawa akamuona mtu akiingia. Wakati akimshangaa mtu huyo, mara akamuona mwingine akiingia. Walikuwa watu wawili, watu ambao walionekana ni watu kweli. Walikuwa wazungu , lakini walikuwa na miili mikubwa kama ya wabeba vitu vizito. Alikuwa na uwezo wa kuwaua kwa risasi, lakini hakutaka kufanya hivyo. Siku zote aliheshimu kile ambacho alikiwaza. Wakati akiendelea kupanga kipi cha kufanya, akamuona mtu wa tatu akiingia. Huyu wa tatu ndie aliemvutia, huyu wa tatu ndie ambaye alifurahi kuja kwake. Hakuwa mwingine, bali alikuwa Sohwa, tena akiingia kwa mwendo wa mapozi. Bastola mbeli zilikuwa mikononi mwake. Hilo likamvutia Jenipher akatambua chochote kinaweza kutokea, chochote kinaweza kumfanya aondoke akiwa salama. Akakipeleka kidole kwenye kitufe cha kufyatulia risasi, aliamua kutenda kitu katika muda ule ule. Hakutaka kuchelewa, hakutaka kuchelewa kwa kuwa alitakiwa kuwa nje ya pale ili kupeleka kile alichokichukua, katika mikono ya Mudy.

Mkono ukaanza kunyooka taratibu, mkono ukainuka na kuinuka tena na tena, ukafika kwenye usawa sahihi, usawa wa kufanya alichokusudia kufanya. Bastola ikakohoa mara moja, kikohozi ambacho kilipokelewa na mtu ambaye alipaa angani kisha kwenda kuanguka hatua kama tano kutoka pale ambapo alisimama. Kilikuwa kitendo kilichofanywa katika kasi ambayo haikutegemewa. Akawaona watu wale wawili wakiruka na kuanguka kila mtu akitua sehemu. Ukimya wa ajabu ukatokea pale ndani. Kila mmoja alikuwa kimya akitizama kile kilichotokea pale.. Hata Jenipher bado alikuwa akitafuta nafasi nyingine ya kummaliza yule mtu mwingine ambaye alikuwa pembeni kidogo ya pale alipoangukia Sohwa. Lakini kila alipokuwa akijaribu kuitafuta nafasi ya kufanya hivyo bado hakuipata. Bado mtu yule hakuwa akionekana pale alipoangukia. Hilo likampa wasiwasi , wasiwasi kwa kuwa hakuwa mwenyeji wa jengo lile. Lakini wakati akiendelea kusikilizia kile ambacho alihisi kitatokea, ndipo alipopatwa na mshangao, mshangao wa kumuona Sohwa akisimama tena akiburuza mwili wa binadamu. Alishaifanya kazi ambayo Jenipher alitaka kuifanya.
 
Nilimpoteza mtu muhimu sana katika maisha yangu. Picha mnayoiona hapo ni yakipenzi changu Neema. Mwanamke ambaye alikuwa ndio furaha yangu. Lakini Mungu aliamua kunipokonya kwa kuwa alimpenda kuliko mimi. Ndio nimeinuka naendelea kukusanya nguvu ili kuifikisha tamati. Nipo kwenye kipindi kigumu sana lakini nisameheni sana kwa muda wote huo.
Pole sana,Mungu akutie nguvu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom