ibra87
R I P
- Jul 22, 2015
- 5,614
- 5,338
- Thread starter
- #841
MKE WA RAIS
Mwandishi: Ibrahim Masimba
*****
Kilikuwa kitu kigumu kukiamini kwa wakati ule. Hakuamini kama mwisho wa Sohwa ulikuwa wa aina ile. Chozi likashuka huku mikono yake ikijikunja na kutengeneza kitu mfano wa ngumi. Macho yake yaliolowa machozi bado hayakuganduka kwenye kioo cha simu. Bado yalikuwa yakiitizama picha ya kutisha, picha ya mtu shujaa. Picha ya mpiganaji aliejitolea kuisaidia Tanzania licha ya kuwa katika Idara nyeti ya Ujasusi katika shirika kubwa kama KGB. Akaitamani ingekuwa ndoto, alitamani ingekuwa ni kitu kisichokuwa cha kweli. Hilo halikubadilika, bali alikuwa akiitizama kichwa cha Sohwa, kichwa kisicho na kiwiliwili. Mudy akainuka na kuuendea mkoba wake, hapakuwa na sababu ya kujificha tena ikiwa watu wanaomsaidia wanauliwa kinyama. Ni nani amemuua Sohwa? Ni vipi wamegundua kuwa yupo pamoja nao? Kwa nini wameamua kumtumia yeye picha za kifo cha Sohwa? Yalikuwa maswali lukuki yenye majibu machache. Jibu ambalo lilimfanya ajione ni mpumbavu kupoteza muda. Tayari alikuwa amejulikana, tayari alikuwa anasakwa. Kama Sohwa ameauwa kisha yeye kutumiwa picha hii ilimaanisha kwamba anajulikana na baada ya hapo kinachofuata ni mtafutano. Hilo hakuliogopa. Akaufungua mkoba wake na kutoa bastola zake mbili pamoja na vitu vingine vingi. Baada kutoa vitu vile aliupima mwili wake kama ulikuwa na nguvu za kupambana. Aliporidhishwa na hicho alichokifanya, akavaaa mavazi yake kwa haraka muda mfupi alikuwa akitoka akielekea sehemu ambayo alikuwa akiishi Sohwa. Kila alipokuwa akitembea bado picha alizotumiwa zilikuwa zikijirudia. Picha hizo zilimpa majibu kuwa watu wanaopambana nao walikuwa wanyama kupindukia.
******
Alipokelewa na ukimya wa kutisha katika nyumba ile. Hapakuwa na sauti ya kitu chochote. Ingawa ilikuwa ni asubuhi lakini hilo halikumtisha Mudy. Alitaka kumuona rafiki yake kipenzi. Alitaka kumuona mpiganaji mwenzie hata kama atakuwa mfu. Funguo zake za kufungulia aina zote za milango zikaifanya kazi yao, zikaifanyakazi ya kufungua mlango baada ya mlango. Ukimya wa jengo lile ukailazimu mikono yake kuifuata bastola ilipo na kuikamatia. Hapo akasogea kwenye sebule pana, sebule ambayo aliikuta ikiwa katika hali ambayo ilisadifu kile ambacho kilitokea hapo. Matone ya damu na mburuziko wenye damu ulionekana mbele ya Mohamed. Kengele za umakini zikazidi kugonga kichwani. Sebule yote ilikuwa ikinuka harufu ya damu. Vitu vilipasuliwa na vingine kutupwa ovyo. Mudy akatumbua mapambano ambayo yalikuwepo kabla ya kifo cha sohwa. Akaipita sebule akiufuata mburuziko ule. Bastola mkononi, bastola ikiwa tayari kwa chochote, mwili ulikuwa huru katika kupambana. Macho yaliangalia sehemu zote huku masikio yakiwa huru kunasa hata kama ni mende wanatembea. Akaufuata ule mburuziko akiamini angeweza kuukuta mwili wa Sohwa. Mburuziko ukaishia nje ya chumba ambacho mlango ulikuwa wazi. Macho yakapokelewa na mwili wa mtu uliolala katika dimbwi la damu. Akasogea huku kidole kikishula rasmi mpaka kwenye kitufe cha kufyatulia Risasi. Akasogea tena na tena. Alipofika karibu, akagundua kuwa alikuwa mbele ya mwili wa Sohwa ambao ulikuwa hauna kiwiliwili. Akahisi chozi likimtoka, chozi la kiume. Wakati anataka kuinama kuuchunguza mwili wa Sohwa, akausikia mlango wa nyumba ile ukifunguliwa, kisha zikafuatia sauti za kunong'ona. Mudy akatulia na kutega sikio. Licha ya kutega sikio lakini hakuweza kunasa kitu chochote kuhusu kinachozungumzwa na watu hao. Akiwa bado hajajua afanye nini, akasikia vishindo vikisogea kule alipo. Ukauruka mwili wa Sohwa kisha kuingia ndani ya chumba kile. Punde akawaona watu wawili wakiingia kila mmoja akiwa na SUB MACHINE GUN mikononi. Bado aliwaangalia wakati wanakuja, bado aliwasubiri wamfikie karibu. Ingawa alikuwa na uwezo wa kuwatwanga risasi lakini hakutaka kufanya hivyo, hakutaka kuharibu risasi zake. Watu wale wakatifika pale wakiwa wanaongea.
Mudy bado hakutaka kufanyakitu kwa haraka. Alihitaji kutuliza kichwa ili awezekuwamaliza kwa urahisi. Damu ya sohwa aliibeba mikononi mwake, aliapa kulipa kisasi kwa yeyote aliyehusika na kifo cha kinyama cha binti huyu shupavu. Watu wale bado waliendelea kuongea huku wakiwa wamejisahau. Mudy akautumia muda huo kujitokeza mbele yao, kilikuwa kitu ambacho kilifanyika ndani ya sekunde, muda huu walikuwa
Wamesimama wakiwa wawili, ndani ya sekunde walikuwa wamesimama wakiwa watatu, tena mtu wa tatu alikuwa mwanamume mweusi ambaye macho yake yalisadifu kile ambacho wao walikijua. Hayakuwa macho ya utani na hayakuwa macho ya mzaha. Sura yake iliongea kifo na macho yake yaliongea kukosekana kwa huruma. Haikujulikana ulikuwa muda gani lakini wote walijikuta wapo chini wakigalagala.hawakuchelewa kuinuka kwa sarakasi, lakini haikusaidia kitu, mateke mfululizo yalitosha kuwarusha tena chino. Hakusubiri wasimame, mikono yake miwili ikafanyakazi ya kunyonga shingo za wakora wale. Hakuwa na huruma tena. Alipohakikisha amewamaliza akawepekua, baada yakupata kile ambacho alikihitaji aliugeukia mwili wa Sohwa uliokuwa umelala katikati ya dimbwi la damu, akachuchumaa na kuweka kidole katikati ya dimbwi lile la damu, lakini wakati akifanya hayo mlango ukasukumwa kisha akawaona watu wakiingia katika aina ambayo ilimpendeza Moyoni na hata machoni.
KUMEKUCHA