MKE WA RAIS
Mwandishi: Ibrahim Masimba
Phone: 0743990480
WhatsAp: 0675191162
******
Hatua ya tatu akapokewa na mwili wa binadamu, mwili ambao ulionekana kulala kihasara kuonyesha kuwa haukuwa na uhai. Kengere ya hatari ikazidi kulia kichwani. Akaikamata vizuri bastola yake, akatembea zaidi kuusogelea mwili ule. Aliusogelea akihitaji kuujua ulikuwa wa nani. Kila kitu kilikuwa huru mwilini mwake. Alihitaji kurudi katika uhalisia wa kimapambano. Hapo akakumbuka alipokuwa kwenye msitu wa Katanga katika nchi ya congo. Alikumbuka Mission ile ya kuwakomboa watafiti. Akaukumbuka ugumu wa kimapambano na kimbinu aliokutana nao huko. Kulifikiria hilo kulimfanya azidi kusogea huku akijiamini zaidi. Alitembea kama paka na hata kugeuka aligeuka mfano wa bundi. Akairuhusu miguu kutembea huku macho yakishuhudia. Alitembea mdomo wa bastola ukiwa mbele tayari kwa mauaji. Akaufikia mwili na kuinama kwa makini kuugusa. Ulikuwa wa moto, ulikuwa moto kuonyesha uhai wake haukuondolewa muda mrefu. Aliamini alichokiona muda mfupi ndio chanzo, alitambua mtu alieondoka muda mfupi ndie aliefanya mauaji yale. Hakutaka kukisumbua kichwa chake kuhoji. Hakutaka kuuchelewa kuupekua mwili ule. Lakini hata alipopekua hakuambulia chochote. Akajua alieondoka pale alifanya kazi zote kuonyesha hata yeye ni Jasusi alieiva. Atakuwa nani? Hatimaye akaruhusu nafsi yake kujiuliza mwenyewe. Ni Mudy? Hapana! Angekuwa Mudy asingembeba mtu. Sasa ni nani? Bado swali lake halikuwa na majibu. Akamgeuza mtu yule akakutana na sura ambayo hakuwahi kuiona. Akaamua kuachana naye sasa alikuwa Akielekea kule ambapo walielekea Sohwa pamoja na majasusi wa CIA na KGB. Alikuwa akielekea sehemu hatari sana, alikuwa akielekea kwenye mdomo wa kifo. Akafuata ramani ambayo alipewa na Sohwa. Ramani ya kumfikisha sehemu ambayo ilikuwa ni lazima afike. Hilo likafanyika katika utimamu, hilo likafanyika katika utulivu wa mwili na kiakili. Akanesa kama kinyonga akihama hapa na kuangukia pale. Hatua kumi mbele akamuona mtu amesimama gizani. Akaona ni wakati wa kuitumia mikono yake. Akairudisha bastola mahala pake kisha kusogea adui yule kwa kuzunguka kwa upande mwingine. Akatembea kisha akafanikiwa kutokea kwa nyuma yake. Pigo moja la kareti lilitosha kumnyamazisha. Akamvuta taratibu na kumlaza chini kwa utulivu. Akaupeleka mkono mfukoni kwa maiti yule, lakini kabla hajafanya lolote akashangazwa na kishindo na sauti ya mtu Vikitokea nyuma yake. Akageuka huku muda huo huo mkono ukizama na kuibuka na bastola. Sauti ndogo mfano wa chafya ukatamalaki katika ngoma za masikio yake, muda ule ule akamuona mtu yule akipaa angani kisha kuanguka chini. Akatulia. Akaondoka hapo akisogea ndani zaidi
Kila wakati alikuwa akiitizama saa yake ya mkononi. Alitakiwa kufika sehemu aliyoambiwa na sohwa ndani ya dakika tano. Hakutakiwa kuchelewa wala kuongeza hata sekunde katika Muda ule. Saa yake ilimwambia bado dakika tano tu kwahiyo ni lazima aingie. Ilikuwa ni lazima aingie, ilikuwa ni lazima afike kwa kuwa ilikuwa ni muhimu katika kupambana na watu hatari kama KGB,MOSSAD na CIA. Ilikuwa ni kazi ya kuuza roho zao, ilikuwa kazi ya kuhatarisha maisha yao. Lakini waliibeba kazi hiyo kwa ajili ya Watanzania, na Kwa ajili ya bara la africa. Waliapa kutokupumzika mpaka pale watakapoondoka na watu wao. Akasonga mbele mpaka kuufikia mlango ambao ulikuwa ukiingilia huko anakotakiwa aende. Akabonyeza namba alizopewa na Sohwa mara akaliona lango likifunguka. Akaingia ndani huku bastola mkononi.
Alipoingia tu akapokelewa na ukimya wa ajabu kisha akalishuhudia lango likijifunga tena. Akasimama katikati ya varanda huku giza likimpa tabu kujua wapi anatakiwa kuelekea. Akachomoa kikaratasi akakiangalia akatingisha kichwa. Alipeleka macho yake kwenye saa yake, akakuta zimebaki dakika mbili tu kufika sehemu ambayo ilikuwa lazima afike. Akachepuka haraka na kuufuata mlango wa chumba cha pili, chumba ambacho alitakiwa kuingia ndani yake. CHumba ambacho ilikuwa lazima afike katika muda husika. Akaufikia mlango kisha kuchomoa kitu kama sindano na kuichomeka kwenye tundu la funguo, mlango ukaachia na kumpa uhuru wa kuingia. Muda wote mdomo wa bastola ulikuwa umetangulia mbele tayari kwa kumwaga ubongo wa mtu. Mbele ya chumba kile akawa anatizamana na mitambo mingi sana. Akafuata alichoambiwa kuwa katikati ya ile mitambo kuna kitu ambacho anatakiwa akichukue na kuondoka nacho.
*****
Wakati Jenipher akikaribia kuuchukua mzigo alioambiwa kuuchukua, huku upande mwingine Sohwa alikuwa kwenye chumba fulani sambamba na Jasusi mwenzake wakifanya mapenzi. Ilikuwa ni picha nzuri kuitizama pale Sohwa alipokuwa akiumenya mhogo na kuutumbukiza kinywani. Ilikuwa tamu pale alipokuwa akiuruhusu ulimi wake utue juu ya kichwa cha nyoka na kupalaza pale. Hakuyafanya hayo kwa mapenzi yake, hakufanya hivyo sababu alipenda kufanya hivyo, bali alifanya hayo akiuvuta muda ili Jenipher achukue kile ambacho alitaka. Kilikuwa kitendo kilichopagawisha hata wale wengine ambao walikuwa wakiisikia sauti na hata kuchungulia. Kila mmoja alituliza macho yake kuangalia jinsi Sohwa alivyokuwa akijihukumu juu ya mnazi. Alikipekecha kiuno huku akibadili mikao ya kila aina. Akafanikiwa kuwapumbaza wote, aliweza kuwafanya wote wamtizame yeye. Alifanya hivyo kwa muda maalum na kwa dakika maalum. Alijua tayari Jenipher atakuwa ameshafanikisha kile ambacho alihitaji akichukue. Kitu ambacho kilikuwa muhimu sana katika kuwapata na kuwarudisha wahaini katika ardhi ya Tanzania bila kumwaga damu za watu wengi. Pia aliogopa kushtukiwa kama yupo sambamba na watu hao.
Jenipher akaufikia ule mtambo na kuanza kuutizama kwa makini. Alikuwa ni jasusi wa hali ya juu kwahiyo asingeweza kuamini kila neno kirahisi. Akaitizama saa yake tena, akakuta zimebaki sekunde thelathini kufika mwisho wa muda sahihi. Akaupeleka mkono na kukishika kile ambacho alitakiwa kuchukua. Lakini kabla hajajua nini afanye Taa zikawashwaaa......