Riwaya: Mke wa Rais

MKE WA RAIS

SEHEMU YA 068

Mwili wa kijana aliyetoka ndani ulikuwa umelala kifudifudi huku damu ikichuruzika. Wakapita kama hawakuwa na shughuli na ule mwili. Vichwa vyao vilishang'amua kuwa ule ulikuwa ujumbe mahsusi kwao, ujumbe ambao ulitumwa kwa njia ya damu. Njia ambayo hupenda kutumiwa na majasusi wengi katika ulimwengu huu. Kila mmoja akatambua kipi kipo mbele yao. Kuuawa kwa kijana yule hakukuwashangaza sana kwa kuwa walijua kile ni Chambo, chambo kilichotumwa kisha kufutiliwa mbali katika Ulimwengu huu. Wakaendelea kutembea huku wakijua na kutambua kuwa kuna watu wapo sehemu wakiwaangalia na kuwachunguza kwa kila hatua. Mohamed na Jenifer wakajiweka sawa kiakili na kimwili. Mbele kidogo ya barabara ya mwenge umbali mfupi kutoka yalipotokea mauaji ya kijana yule, wakamuona mwanamke akiivuka barabara, hakuwa katika kawaida, bali alikuwa akipiga kelele huku akikimbia 'MTEGO' ndiyo neno pekee liligonga vichwa vyao. Haikuwa rahisi kutokea kwao barabarani kisha kukutana na tukio lile. Macho yao hayakumjali mwanadada yule aliyekuwa akipiga mayowe, bali yalivutiwa na wanaume watatu waliokuwa wamesimama kando ya barabara wakionekana kutokujali na kutokuwa pamoja.

Kila mmoja alionekana kufanya mambo yake. Wawili wakiongea na simu, mmoja alionekana kuvuta sigara. Hilo halikuwafanya wapelelezi mahiri kama wale washindwe kung'amua kitu. Ni hilo lililowafanya washuhudie kile ambacho hawakukitarajia. Sekunde Moja Kurudisha macho kwa mwanadada yule, wakashuhudia akipaa hewani na kuanguka miguuni mwao kama furushi la Mahindi, kifuani akivuja damu. Lilikuwa tukio la kuburudisha machoni mwa wapita njia, waliona kama Mchezo wa kuigiza, waliuona ni kama mchezo wa Sinema. Mwanadada Yule alishakuwa maiti, lakini kilichoburudisha Zaidi ni Pale Mohamedi na Jenifer walivyotoweka katika mazingira tatanishi. Mazingira ambayo si wale watu watatu walioupande wa pili wa barabara, wala wengine watatu waliosimama gizani. Ulikuwa mchezo mtamu uliyochezwa na watu watamu katika medani ya mapambano. Watu ambao waliyeyuka mbele ya macho kumi na mbili ya watu sita. Watu ambao walikuwa wenzao katika fani moja. Ni wakati watatu wakishangaa na wengine wakitafuta likaibuka Jingine.

Watatu kati ya watu sita walianguka chini katika sekunde moja na wakati mmoja. Kitendo kilichowaduwaza wengine watatu waliobaki. Wakahamanika kila mmoja akichomoa bastola yake. Walikuwa katika wakati ambao hawakuwaza kukutana nao. Wakasambaa kila mmoja na upande wake.

Wakati wakitawanyika hawakujua kuwa kulikuwa na mtu wa tatu ambaye aliongezeka. Hawakujua kuwa palikuwa na mpiganaji mwingine. Mmoja akakutana na Ummu, Mwingine Akagongana na Jenifer kisha watatu akaangukia mikononi kwa Mohamedi. Haikuchukua dakika mbili wote watatu walikuwa chini wakivuja Damu, huku wawili wakiwa maiti na mmoja akipumua kwa tabu sana. Hawakuupoteza Muda wakaondoka eneo lile pamoja na kijana aliyekuwa akipumua kwa tabu na kutokomea naye mafichoni kwao tayari kwa Mahojiano.

****
Ilikuwa saa tano za asubuhi mohamed aliposimamisha gari mbele ya Jumba moja la Siri linalomilikiwa na Idara Ya Usalama Wa Taifa. Akaruhusu kukaguliwa kisha akaingia ndani akiongozwa tayari kwenda kuonana na Mke Wa Rais kwa Mahojiano Zaidi. Alitembea Huku akiwa hana wasiwasi, alitembea huku akiwa makini na kila kitu. Bado hakuwa anamuamini mke wa Rais, na Bado alikuwa akiihisi hatari kila alipokuwa akitembea kuelekea ndani Zaidi. Bastola Zake mbili zilikuwa zimetulia katika mifuko yake ya Siri, Mifuko ambayo ilikuwa ni ngumu Sana kugundulika hata kwa mashine za ukaguzi. Akapokewa na Mke Wa Rais kwa Tabasamu pana na Hongera Nyingi sana. Alipongezwa na Kusifiwa Sana, licha Ya kusifiwa kote lakini bado Mohamed aliitilia mashaka Sauti ya Mke Wa Rais. Sauti ambayo licha ya ukawaida wake katika msikio ya Watu wengine, lakini kwenye masikio ya Mohamed kulikuwa na Kitu kingine kabisa. Sauti iliyobeba kebehi ma Dharau. Sauti yenye viulizo Vingi sana. Mudy akaipokea Pongezi Huku Macho yake akiyalazimisha yatizamane na macho ya Mke Wa Rais.

Hilo halikufanikiwa mke Wa Rais aliyakwepesha macho yake kila pale alipohisi anatizamwa na Mohamed. Hilo likaleta mtafaruku kwenye kichwa cha Mohamed. Kwa mbali akaisikia kengele ya Tahadhari ikigonga kichwani mwake. Akahisi kuwepo kwa Siri kubwa. Siri kutoka kwa Mke Huyu wa Rais. Kebehi, dharau na kukwepesha macho kwake, kuliamsha Hisia Mbaya katika Kichwa cha Mohamed. Alihisi kuwepo kwa kitu kikubwa kinachofichwa na Mke Wa Rais. Akaamua kukaa kimya ili kuangalia kipi ambacho kingetokea. Pia kutokumuona Rais pale Kulimpa mashaka makubwa. Haikuwa kawaida kwa Rais abaki ndani wakati anamtambua Mohamed na anautambua msaada Wake. ''Yuko Wapi Mheshimiwa Rais? Lilikuwa swali kutoka kwa Mohamedi. Swali ambalo lilionyesha kumshtua sana Mke Wa Rais, ingawa baadae alijikausha lakini alishachelewa kwani Mohamed Alishaugundua zamani Sana. ''namtaka mheshimiwa Rais''. Ilikuwa Kauli Iliyobeba Mamlaka Yote. Kabla Mama Hajajibu, Mohamed Akainuka na kuanza Kuelekea CHUMBA CHA RAIS.

KESHO
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 69

Hakusubiri Jibu la mke wa Rais. Muda ule ule alikuwa ameshasimama akielekea chumba alichowekwa Rais. Alikuwa akivuta hatua moja baada ya nyingine. Masikio yake yalikuwa wazi kunusa kila sauti. Akazifikia ngazi na kuanza kuzipanda kwa tahadhali. Bado hakumuamini Mke Wa Rais, bado hakuuamini uwepo wa mwanamke Yule. Kile kilichotokea mwanzo bado kilibaki kama kumbukumbu muhimu na funzo la kutokumuamini mtu. Aliipanda vizuri ngazi ya Kwanza, akaja kwenye ngazi Ya pili, wakati mguu wake wa kulia unataka kuikanyaga ngazi ya tatu. Masikio yake yakasikia kitu. Kitu ambacho hutokea na huendana na hisia. Alihisi kidole cha mtu kikibonyeza kitufe cha kuruhusu Risasi. Hakutaka kugeuka wala kuuliza. Mkono wake mwepesi ulishazama pale palipo na Bastola na wakati huo huo akiruhusu risasi ikitoka kwenye bastola huku akiwa bado anatizama kule anapokwenda. Mlio wa Maumivu kutoka kwa mtu wa Nyuma yake haukumgeuza kichwa chake kutizama. Alishajua aliyenyuma hakuwa mke wa Rais, ingawa walifanana na Mke huyo. Alipofanya kile alichokifanya. Akairudisha bastola mahala pake. Akaendelea kupiga hatua huku akiwa makini tofauti na mwanzo.

Akazimaliza ngazi na kutokea kwenye Korido ya Jengo lile. Mbele yake akapokewa na maiti wawili. Maiti ambao walimshtua kupita kiasi. Mkono wake ukashuka tena pale alipomuhifadhi mwanawe. Akapiga hatua kuifuata miili iliyolala Chini. Ulikuwa miili ya walinzi Binafsi wa Rais. Kuwaona walinzi katika aina ile, kulimaanisha kuwa Usalama wa Rais ulikuwa mashakani. Alipowafikia Maiti wale akainama kutaka kuchunguza kitu. Lakini hakufikia popote pale. Muda mfupi akahisi kitu kizito kikitua kisogoni kwake. Akaanguka chini kama furushi. Macho yakaanza kuingia Giza, lilianza kwa mbali kuingia machoni. Akajaribu kupambana kwa nguvu zote na giza lile, lakini hakuweza kuhimili hilo. Muda mfupi akafumba macho na kunyamaza kama Mfu. Hakuwa na uwezo hata wa kuinua mikono.

******

Alikuja kirudiwa na fahamu baada ya masaa manne, akijikuta amefungwa katika Chumba kidogi na Chembamba sana. Chumba kilichokuwa na joto kali kupindukia. Licha ya Joto chumba kile kilitapakaa Damu kila mahali. Chumba chote kilinuka Harufu ya Kifo tu. Mohamedi ayafumbua macho yake na kuanza kutizama vizuri. Kila alipokuwa akitizama hakupata kuona sehemu ambayo ingemuwezesha kutoka nje. Kila alipotizama hapakuonekana kuwepo kwa mlango ama Dirisha. Akajiinua pale Chini huku joto likiuchemsha mwili wake. Ingawa chumba kilikuwa hivyo lakini hakujali sana. Hakujali kwa kuwa alishawahi kupitia mafunzo kama Hayo alipokuwa Kule Chini Urusi. Mafunzo ambayo humsaidia sana anapotokea kufungwa sehemu kama Hizo. Aliendelea kukitizama kile chumba huku maumivu ya nyuma ya kisogo yakiendelea kumsumbua kutokana na Kitu alichopigwa nacho. Akaipa Uhuru wa kufikiri zaidi akili yake. Akaupa uhuru Ubongo wake kupata jibu katika nini cha kufanya kuweza kumuondoa pale. Hakutaka kuwafikiria Jeni na Ummu kwanza. Hakutaka kuamini kuokolewa na Watu hao, alitaka kujiokoa yeye kwanza kabla Ya kuokolewa. Alitaka kupambana yeye kwanza kabla ya Jenifer au Ummu Kufika.

Akiwa katika kuwaza hilo akahisi kama Ukuta ukifunguka na kuacha Uwazi Mkubwa wenye uwezo wa kupita Mtu. Haikupita Muda wakaingia watu wawili. Hawa Walikuwa wazungu. Wazungu ambao walionekana kama Wa Israel. Mohamedi hakusubiri kuambiwa kuwa wale ni Majasusi Wa Mossad. Aliwatambua mapema walipokuwa wakiingia. Akawa kwenye giza totoro sana. Wapi na wapi MOSSAD NA KGB kuungana kwenye MISSION kama hii? Kuonekana kwa Majasusi Wa MOSSAD na Wale wa KGB lilikuwa swali zito sana katika kichwa Cha Mohamed. Alijua Mataifa ya Ulaya yalikuwa nyuma ya mapinduzi Ambayo yalipangwa kufanyika. Mataifa ya Ulaya yalikuwa yakipambana kwa Siri kumuondoa Rais madarakani kwa Faidi Zao. Hapo bado akaiona kazi nzito Iliyombele yao. Kazi ya Kuiambia Dunia kuhusu kinachofanywa na Nchi Za Jumuiya ya Ulaya kuhusu kutengeneza Migogoro na Mapinduzi Katika Nchi Za Kiafrika.

Akawasubiri waendelee kumsogelea, alijiandaa kwa mapigano, mapigano ambayo Hakuijua hatma yake katika kichumba kile kidogo. Akawa anahesabu hatua za Majasusi wale. Alihesabu Huku macho akiwa amefumba. Akaiona Hatia Ya kwanza, Akaiona Hatua Ya Pili, Akaiona Hatua Ya Tatu. Hatua ya Nne kupigwa na watu wale Ilimkuta Mohamed akiwa Hewani kwa Mapigo ambayo hayakutarajiwa. Alipokuja kutua chini, majasusi Wote wawili walikuwa Chini wakivuja damu. Yakuwa mapigo makali Sana, Yalikuwa Mapigo Ambayo Yaliweza kuvunja Shingo Za Watu wale. Baada ya kuhakikisha wote wameshalainika, aliwasachi mifukoni mwao Akachua bastola Mbili, Magazine za Risasi Tatu na visu Viwili. Vyote akaviweka kwenye Mifuko Yake. Akatoka ndani ya Kichumba kile kwa kupitia uwazi ule Ule, alipokanyaga mguu wake nje tu, akapokewa na Mkono Wenye nguvu. Lilikuwa pigo ambalo hakulitaraji akajikuta Akianguka Chini kama Gunia. Kabla hajajua afanye maamuzi Gani akamuona Mtu yule Hewani akimfuata pale pale alipoangukia. Hakumjua Mohamed ni nani na Hakujua kwanini Yuko pale. LAITI ANGEJUA?
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 001

Mwili wa mwanaume ulionekana ukiwa sakafuni huku damu Nzito Ikiwa imetapakaa kila sehemu ya Chumba kile. Mwili ambao ulionekana kutokuwa na Uhai, mwili ambao utumbo wote ulikuwa nje Huku katika Paji la Uso kukiwa na Matundu mawili ya Risasi ambayo yalikifumua kichwa na kutapakaza ubongo katika Chumba kile.

UNADHANI KWANINI?

SONGA NAYO.


Ilikuwa Yapata Majira Ya Saa tano Za Usiku, Gari yenye namba Za Ikulu Ilionekana ikisimama katika Jumba fulani kubwa liliopo kando kando ya Bahari Ya Hindi maeneo Ya Mbezi Beach. Wakashuka watu wawili ambao wote walikuwa wanawake. Baada ya kushuka Watu wale walionekana kuangalia kitu nje ya Maeneo Yale na waliporidhishwa na Kile ambacho Walikuwa Wakikitazama. Mmoja Akauendea mlango wa Gari Walilokuja nalo Wakaufungua.. Kisha Akaonekana Mwanamke Mwingine akishuka.. Mwanamke Huyu Alikuwa amevaa mavazi meusi ambayo Yalikuwa yamemficha mpaka Uso wake. Alikuwa mwanamke wa makamo lakini ambaye Anaonekana ni mkakamavu.. Akatembea kwa Mwendo wa taratibu Huku wadada wale walionekana ni Walinzi Wake wakimfuatia kwa Nyuma Huku kila Mmoja Mkono Wake akiwa Ameupeleka Sehemu ambayo alikuwa amehifadhi bastola yake.

Mlango ukafunguliwa kisha mwanamama Yule akaingia ndani huku walinzi wake wakiishia nje. Baada ya Mama Yule Kuingia Ndani Akalakiwa na mwanaume wa Makamo.. Alikuwa mwanaume Mrefu na Mweusi.. Sura yake na kutazama kwake kulimuonyesha Kuwa Alikuwa ni Mtu Fulani Katika kitengo ambacho kilikuwa ni kikubwa Sana Katika Nchi Hii. Baada ya kumlaki mwanamama Yule kwa Kumkumbatia na Kumbusu walishikana Mikono kama Watu wanaopendana wakaingia ndani katika chumba ambacho kilionekana kuwa ni Chumba maalum wakajifungia Humo.

Wakati Wao wakijifungia mle ndani Huku walinzi Wa Yule mama Wakiendelea kuangalia Huku na Huko.. Umbali wa Hatua kama Mia mbili kutoka katika Jumba Lile walionekana Watu Watatu wakiwa wamejibanza Kwenye giza kama wanaosubiri kitu.. Watu wale ambao kama ungebahatika kuwaona kwa Mara ya kwanza ungedhani ni Waandishi wa Habari Kutokana na Camera Walizokuwa nazo. Walikuwa wako pale wakitokea kitendo cha Kijasusi Cha Usalama wa Taifa Ambao walipewa Amri Ya Kufuatilia Mienendo Ya Mke Wa Rais Hasa baada ya kuonekana ni Mtu wa Kutokutulia Ikulu tokea rais alikwenda Ziarani Nje Ya Nchi. Walikuwa Vijana Watatu, wanawake wawili na Mwanaume Mmoja.. Walikuwa vijana Ambao walikuwa wameaminiwa kama wapelelezi na Majususi Walioiva katika kazi Yao, hivyo waliamini kuwa ndani Ya Muda Mfupi watakuwa wameshakamilisha kazi Waliokabidhiwa na Rais.

Wakazichomoa bastola Zao na Kuanza kuambaa kuelekea lilipo jengo lile.. Lilikuwa Jengo ambalo walilipeleleza tokea asubuhi, na lilikuwa ni Jengo ambalo walitegesha camera Zao kuchukua Matukio Yote yanayoendelea Pale Ndani.. Walitembea katika hatua Za Paka, hatua ambazo Hata uwe na Masiko gani Kamwe Usingweza kusikia... Walipofika Nyuma ya Jumba Lile Kila Mmoja Alirudisha bastola Yake Mfukoni kishwa kwa Spidi Ya Chui wakachupa kwa Pamoja na Kuingia ndani Ya Jumba lile bila Kutoa Hata Kishindo. Walipotua tu wakaongoza mpaka Mlango Wa Kuingilia Ndani Huku kila Mmoja Bastola Yake Ikiwa Mkononi. Wakafungua na funguo Zao Malaya walizokuwa nazo muda mfupi Wote Walikuwa ndani Ya Jumba Lile.

Baada Ya kuingia cha kwanza kusikia ni Kelele Za Mapenzi kutoka ndani ya Chumba kimoja Mle Ndani. Wakatazamana na kupeana Ishara........

Ndani Ya Chumba kile maalumu mapenz Yalikuwa yamepamba moto huku kilio na Miguno ya Raha Ikisikika Kutoka kwa Wote Wawili.. Walikuwa wakifurahi na Kufurahisha nafsi Zao... Mwanamke alikuwa Juu ya Mwanaume akiendelea kuwajibika.. Alikuwa akiwajibika katika ufundi ambao Ukimuangalia wakati akiwa na mavazi Yake Usingezani kama Anao... Ni Wakati Huo wakiwa Kwenye Kilele Cha Mahaba Jambo la Ajabu Likawatokea.. Mwanga Wa Flash ya Camera Iliwagutusha.. Wote wakakurupuka.. Lakini bado mwanga wa flash Ulikuwa Ukiendelea Kuwamulika kuchukua Picha Zao... Kwanza Wote wakazubaa kwa Sekunde wasijue la kufanya... Walipokuja kugutuka Walikuwa wameshachelewa kwani Watu waliolifanya tukio lile hawakuwa pale tena kwa Muda Huo... Mwanaume Akageuza Shingo kumtazama Mwanamke.. Akashtuka na Mapigo Kumuenda Kasi.. Alijikuta Akitazamana na Mdomo wa Bastola iliyoshikwa sawia na Mke Wa Rais... Mara bastola Ikakohoa mara tatu.. Risasi zikapenya kichwani kwa Mwanaume Yule, Akaanguka Chini Mithili ya Fulushi la Mahindi.. Ubongo ulitapakaaaa....

HAKIKA HALI ILITISHA.
 
Asanteeeee
 
Muendelezo
 
Nzuri
 
Nimeianza jana mpaka kufikia sasa nineimaliza yote.!!

Kazi nzuri kijana, inavutia, inashawishi kuisoma, inaondoa stress..!! Halafu nikupongeze kitu kimoja, Huboi....Hunanyodo... Unatupia story kila siku, kila baada ya masaa kadhaa, Yaani hauzingui. Ni tofauti na baadhi ya waandishi wa Story wengine Uchwara ambao hawaandiki story bila kuwabembeleza..!!

Hongera kwa hilo, kazi yangu ni kusoma na kugonga like!!

BACK TANGANYIKA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…