MKE WA RAIS
SEHEMU YA 071
Alitaka kumjua alikuwa nani? Alitaka kumjua kwa nini alikuwa ameweka sura ya bandia yenye kufanana na mke wa rais ambaye tayari alishaakufa. Lilikuwa ni jibu pekee, lilikuwa jibu lililobaki katika kumpa Mohamedi majibu ya mkasa huu. Akapiga hatua huku bastola mkononi, akainama na kukishika kichwa cha mwanamke yule ambaye alilala katikati ya dimbwi la Damu. Kile alichokitegemea ndicho alichokikuta. Alikuwa amevikwa kitu kama sura. Sura yenye kufanana na mke wa Rais. Mohamed akatizama kwa umakini wa hali ya juu. Hakutaka kuwa na papara. Alitaka kuujua ukweli wenyewe. Punde alikuwa akitoka na mwili wa mwanamama Yule Ukiwa begani. Alitembea huku masikio, macho na miguu vikiwa sambamba katika kufanya kile ambacho kingetokea. Bastola mkono wa kulia na marehemu bega la kushoto. Akakivuka kizingiti cha kwanza bila wasiwasi. Akakiendea kizingiti cha pili kwa tahadhali kubwa. Masikio yake yakahisi mchakato wa viatu kutoka ndani. Akautua mwili wa mwanamke yule na kuuweka pembeni. Aliziamini hisia zake kuliko kitu kingine. Punde mlango ukasukumwa kisha mbele yake akamuona mwanamke Mrembo. Huyu alikuwa mpya katika macho yake. Mpya katika mapambano na mpya katika hisia zake. Licha ya Upya Huo lakini kuna kitu kama alikihisi na kukikumbuka Juu ya Binti Huyu. Naam alimtambua, alikuwa Ni Neema Ben Mtobwa. Msichana Shupavu kutoka kikosi maalum. Msichana ambaye mara ya Mwisho alimuacha kule Cuba akiwa katika mafunzo ya Juu ya kikomando.
Leo alikuwa machoni mwake na leo alikuwa hatua chake kutoka alipo yeye. Tena alikuwa akitembea bila wasiwasi. Alikuwa akitembea kuonyesha kuwa hakuwa akiogopa kitu. Kwa nini haonyeshi kuogopa? Kwa nini Yuko hapa mbele Yangu na anahusika vipi katika mission Hii? Yalikuwa maswali yaliyopita kichwani kwa Mohamedi kwa sekunde moja. Hakutaka kuendelea kusimama, akajitokeza Na kukutana uso kwa macho na Neema Mtobwa. Wakatizamana katika namna ya kipekee, mtazamo wa kila mmoja akimuacha mwenzake asome kile kilichopo ndani yake. Ndicho kilichofanyika na ndicho kilichotendeka. Hapakuwa masihara machoni kwa mwanadada Neema Mtobwa. Hakuuona urafiki uliokuwepo wakati walipokutana Cuba. Macho ya Neema yalisadifu vita, tamaa na kubwa zaidi ni Damu. Mohamedi akahisi ni wakati husika wa kufanyakile ambacho anataka kukifanya. Wakati anajiandaa kutenda kitu mlango ukasukumwa kisha Vijana wanne kuingia wa aina ambayo ilimburudisha Mohamedi katika macho na mwili wake. Licha ya kuburudika kule lakini hakubakia pale, hakuendelea kusimama pale, alikuwa ameshajitupa na kuangukia pembeni huku Risasi zikipita na kuuchimba Ukuta. Akaangukia Sehemu huku akiamini kuwa hata mwanadada Yule inawezekana ameshapigwa Risasi. Lakini alipoona ukimya umetawala akajua wote walioingia pamoja na Neema Mtobwa walikuwa ni wa moja. Hapo ndipo alipoamini kuwa mapinduzi yalikuwa yamepangwa kwa muda mrefu sana. Kuwepo kwa majasusi wa CIA NA MOSSAD kuliimaanisha Mipango ya mapinduzi ilipangwa huko nje. Aliamini mipango hii inabaraka za serikali ya Marekani ndio maana hawakuonyesha kushtuka kwa tukio la Mke wa Rais kuuawa ndani ya IKULU. Hapo akauona Ugumu wa hii kazi. Kama watu wote waliopo mafunzoni Nchi mbalimbali wamekubali kuasi na kutengeneza mapinduzi, Basi Shughuli itakuwa ngumu kupindukia,
aliujua uwezo wa kimkakati na kimapigano kwa vijana waliopelekwa nje. Aliuona ugumu wa kupambana na watu wa aina hiyo, lakini alipomkumbuka Ummu Sammy Na Jenipher Dominic alitabasamu. Lilikuwa tabasamu la karaha. Bado hakutaka kuinuka na bado hakutaka kufanya lolote. Aliendelea kutulia akipanga hili na kupangua lile.
******
wakati Mohamed Akiendelea kutulia pale chini, huku upande wa pili Neema na Vijana wake walikuwa wameshaondoka Sehemu ile. Hawakuwa wao tu bali waliondoka na mwili wa mwanamke ambaye alikuwa na sura ya bandia Yenye kufanana na Mke Wa Rais. Ulikuwa ni mpango maalum ulioandaliwa na Makamo wa Rais Wa nchi kuhakikisha kila kitu kinafichwa ili kupoteza ushahidi wa kuhusika kwake Katika mkakati Ovu. Hata kile ambacho kilikuwa kikitokea kipindi kile hakikuwa kinatokea Kwa bahati mbaya. Kuletwa kwa Neema Mtobwa katika Mission hii ni kujaribu kuficha kile ambacho kilikuwa kinakwenda kugundulika. Na hilo wakafanikiwa baada ya kumdhidi Mohamedi. Licha ya kufanikiwa katika hilo lakini hawakujua kuwa eneo lile hakuwa Mohamedi peke Yake bali kulikuwepo na Ummu Pamoja na Jenifer ambao waliushuhudia mchezo wote ukitendendeka na hata pale Neema na Watu wake walipoamua kuondoka walionekana na walifuatiliwa kwa nyuma.
*****
Ukimya Ulizidi kutawala Eneo lote. Mohamed hakuona Sababu ya kuendelea kukaa. Aliamua kutambaa Chini kwa Chini, akafanikiwa kutokea upande wa pili. Alipofika hapo alisimama na Kuchungulia kwa Chati, lakini akashangazwa na Ukimya. Ukimya ambao ulitafsiri Vitu vingine. Kufikia hapo Akaukumbuka Mwili wa mwanamke Yule, Mwili ambao ungetegua kitendawili juu Ya mkasa wa Kuuawa Kwa MKE WA RAIS...