Riwaya: Mke wa Rais

 
Mudy daah
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 066

Wote walikuwa wamepoa na wote walikuwa wakitokwa na mapovu mdomoni. Mohamed na Ummu Wa katizamana. Hawakuwahi kupambana na watu wenye Roho mbaya kama hawa. Kitendo kilichofanywa na wasichana wale kilionyesha ni jinsi gani walikuwa Majasusi wa kutisha. Ilikuwa ni kawaida kwa majasusi Kutoka kundi la Mafia la kule Nchini Italy kutumia njia ya kujiua kuliko kukubali kutoa Siri papote pale. Hii mbinu ikazagaa katika mashirika mbali mbali ya kijasusi. Nao wakaona ndio njia pekee ya kuficha siri hata kama ukiwa kwenye mateso makali kiasi gani. Licha ya kutambua hilo lakini hawakuwaza kukutana na watu tena watoto wa kike wenye kufanya hivyo. Waliporidhika na kila kitu walichokichunguza, ikiwemo kuwapekua wakatoka ndani ya kile chumba na Kuanza kukiendea chumba kingine.

*****
wakati Mohamed na Ummu wakiendelea upande wa jumba lile. Jenifer alikuwa ndio kwanza anaingia katika Chumba kimoja kipana Sana. Alitembea kwa makini huku kila kitu kikiwa tayari. Bastola mkononi na Bunduki kubwa Mgongoni vilimpa nguvu ya kutembea katika chumba kile bila kuogopa. Mfujoni alikuwa na funguo za Chumba walichofungiwa watoto wa Rais. Akaendelea kutembea mdomo wa Bastola ukimtangulia. Kidole kilitulia sawia kwenye Triggle. Alikuwa tayari kufyatua Ama kuua. Alikuwa tayari kuachia risasi pale ilipobidi. Akakivuka Chumba kile kwa Usalama. Akaingia katika chumba cha pili. Kuufungua mlango na kuchungulia kwa ndani akapokewa na Ukimya wa Ajabu. Ukimya wa kila kitu. Hapakuwa na taa wala feni. Hapakuwa na mchakato wa kitu chochote bali ukimya wa Ajabu. Jenifer akatulia kwa Muda Akiuruhusu Ubongo wake kufanyakazi. Akiiruhusu akili Yake kufanya usahihi katika chumba kile. Ukimya ulimuogopesha, ukimya Ulimtisha. Akasita kuingia na kusimama nje. Lakini Ghafka akaisikia Sauti ya mwanamume ikimkaribisha kutokea ndani ya kile Chumba. ''karibu binti Mzuri'' hilo la kukaribishwa likausisimua mwili wake,l likaisisimua damu yake. Akajiuliza aitikie ama aache kuutikia. Akabaki katikati akiwaza hilo. Hakuwahi kuwa Muoga katika kufa. Daima damu ndio kitu alichopenda kucheza nacho. Sasa kwa nini leo naogopa? Lilikuwa Swali lililopita kichwani mwake. Akajiona ni Mjinga kukiogopa kifo, akajiona mpumbavu kuogopa kupambana. Punde akauruhusu Mguu wake utangulie katika kile Chumba.

Kuingia kwake kukafuatia na mlango kujifunga kwa nyuma. Moyo wake ukapiga mapigo kadhaa. Wakati akiangalia huku na huko kumuangalia aliyemkaribisha. Akashangaa kumuona mwanaume wa Kizungu akitokea kwa Mbele yake. Uingiaji wa mwanamume Yule Ulikuwa Uingiaji wa Ajabu sana. Jenifer hakumuona wakati anaufungua mlango na hakumuona wakati alipompita na Kusimama mbele yake. Alishtukia mtu mfano wa kivuri akisimama mbele Yake. Akisimama mfano wa mzimu. Macho yake yalikuwa yakiwaka kama yawakavyo macho ya paka Usiku. Hakuwa na Tabasamu hakuonyesha kicheko. Sura Yake ilionekana ni Sura iliyozoea kuua. Sura Iliyozoea Kuondoa Roho Za Watu. Hapa ndipO Jenifer alipokikumbuka kitabu alichowahi kusoma Udogoni kwake. Kitabu kilichoandikwa na HAYATI BEN MTOBWA kiitwacho MALAIKA WA SHETANI ingawa huyu mtu hakufanana na yule wa kwenye kitabu lakini kwa kuiangalia Sura Ya Mtu Huyu alikiona kile ambacho kinaendana ama kufanana na Jitu lililoelezewa kwenye kitabu kile. Hapo alihitajika kuwa Jasiri kama Alivyokuwa NURU. Hakujisumbua wala kuhangaika nalo, akabaki kuzuga kama hakuwa amemuona. Lakini akishtukia akipigwa pigo moja la Haja. Pigo ambalo lilimfanya apepesuke hadi kuufikia ukuta. Wakati anataka kujiandaa kukabilana na Mtu Yule, ajashtulia na ngumi pamoja na Mateke Mfululizo kuelekea kwake. Akajaribu kukinga kwa ufundi wake lakini Safari hii akajikuta akienda Chini baada ya mapigo matatu kumuingia Sawa sawia
. Hakuchelewa pale chini hasa pale alipomuona yule mwanaume akiruka Juu kumfuata pale alipo. Alichokifanya Jenifer ni Kuchupa kutoka pale chini na kusogea pembeni, yule mtu akatua patupu lakini wakati huo huo akajigeuza kutoka pale chini na kupeleka mateke kadhaa Kwa Jenifer.

Safari Hii Jenifer Aliyaona, aliyaona kwa ukaribu na kuyakwepa kwa Ufundi Mkubwa na wakati huo huo akiruka martials Combart Moja ambayo iliingia sawa sawia kwa mtu yule na Kupepesuka. Wakati akijitahidi kukaa sawa Jenifer aliruka Angani na kumshindilia na Ngumi tatu za Hewani. Ngumi ambazo zilimfanya yule Jasusi Wa kizungu kuzamisha mikono mfukoni na Kuibuka na Bastola. Lakini Hakuweza kushindana na Mkono mwepesi wa Jenifer, Mkono ambao ulitumia nukta moja kuzama mfukoni kuchomoa bastola, Kisha nukta ya pili Kuiruhusu bastola kufanyakazi Yake. Risasi Zikapenya Kichwani kwa Mzungu Yule na kumrusha hewani. Alipokuja Kutua chini alikwisha kuwa maiti. Jenifer akampekuwa hapa na pale Katika mifuko yake. Akakutana na Kitambulisho. Kitambulisho kinachoonyesha Mzungu Yule Anaitwa Dimitri Poloshkovic na Alikuwa Jasusi Wa Shirika la Kijasusi la Urusi KGB. AKATASAMU KISHA KUONDOKA NDANI YA CHUMBA KILE.
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 067

AKATABASAMU NA KUTOKA NDANI YA CHUMBA KILE. Akaongoza ndani kabisa ya Chumba kingine. Bastola mkononi huku mwili ukiwa kwenye utayari wa kupambana. Akaupita uchochoro fulani na kutokea upande wa pili. Hapo akauona mlango wa chumba alichokuwa akikihitaji. Chumba walichofungiwa watoto wa Rais. Akaongeza umakini huku hatua zake zikiendana na utazamaji wa macho yake. Kila mguu mmoja ulivyokuwa ukisogea ndipo jicho lake lilipozidi kuangalia. Jicho lilikuwa likitupwa kwa Hila kutizama katika aina ya utizamaji kwa wale wahitimu na wakufunzi Wazuri katika medani ya mapambano. Mdomo wa bastola ulitizama mbele, macho yakatazama mbele. Akili yake ikapelekwa ndani ya Chumba kile. Hatua tano kabla ya kuufikia Mlango akaichomoa funguo, funguo ambayo alipewa na Mohamed. Akautizama ufunguo Huku tabasamu hafifu likiifunuka Sura Yake yenye kila ishara Ya Uovu. Sura Iliyobeba mtu mpambanaji. Kuutoa ufungua kukafuatiwa na Hatua mbili tatu mbele. Hatua ya Nne akausikia mchakato katika masikio Yake. Mchakato ambao ulipenya na kugundulika katika ngoma za Masikio ya Jenifer. Aliutambua uwezo wake na Aliziheshimu Hisia Zake. Hakuudharau mchakato aliousikia masikioni mwake.

Hata pale alipousikia mtikisiko wa kitu mfano wa bomu likitokea umbali mdomo kutoka pale alipo. Aliweza kuruka kabla na kuangukia pembeni. Hakuinuka kwa Muda ule, aliendelea kujificha pale chini macho Yake yakitembea katika Ukungu. Ukungu uliyomuwezesha kuwaona watu sita wakiwa wamemuweka Rais wa Nchi katikati. Akaupa mwili wake nguvu ya kusimama. Akaupa mkono wake Nguvu ya Kuifikia bastola iliyokuwa imeanguka pembeni. Akaivuta na kuisogeza karibu Yake. Akakiruhusu kidole kuelekea kwenye kitufe cha kuruhusu Risasi. Sekunde mbili bastola ilikuwa akitema cheche, bastola ilikuwa ikimwaga mwani. Risasi Zake zikatua pale alipozitaka Ziende. Watu wawili kati ya Sita walikuwa wameanguka Chini. Wanne waliobaki kila mmoja alikuwa amechupa pembeni Huku wakimuacha Rais akibabaika peke yake. Punde wakatokea watu wawili, watu ambao aliwatambua kwa Haraka Zaidi. WAlikuwa Mohamed na Ummu, walitokea kusikojulikana na kumkumba Rais kisha kuanguka naye pembeni. Wakamuondoa Ile sehemu na Kumuingiza ndani kabisa ya Jengo lile. Walipoona Sehemu walipomuacha ilikuwa ni Salama. Wakarudi katika uwanja wa mapambano. Uwanja ambao ungekuwa mwisho ya Wapanga mapinduzi wote. Mwisho wa Waroho wa Madaraka na Mwisho wawafuja Mali. Waliamua kuteketeza kila walichokiona mbele ya Upeo wa Macho Yao. Yalikuwa mapambano makali, mapambano yaliyosababisha kukamatwa kwa Makamu Wa Rais, mtu ambaye alikuwa akiratibu mpango wote Wa Mapinduzi kwa kuwatumia Viongozi Wa Chama na Wa Serikali. Wakisaidiwa na Makomandoo pamoja na Askari Wa kikosi maalum Walifanikiwa kuiondoa familia ya Mheshimiwa Rais Kuipeleka mafichoni. Licha ya hilo kufanyika lakini bado Mohamedi, Ummu na Jenifer Walitaka kujua. Walihitaji kujua nani ambaye alipigwa Risasi ndani ya Ikulu na Nani ambaye aliuawa wakati mtu aliyesemekana kuuawa Alikuwa hai? Yalikuwa maswali yenye uwezo wa kujibiwa na Mke wa Rais pekee. Yeye ndiye aliyekuwa anajua kila kila kitu.

Lakini haikuwa rahisi kufanya naye mazungumzo kwa kipindi kile. Kipindi ambacho bado alikuwa katika matatizo Ya kiafya. Kipindi ambacho alihitajika kuwa Chini ya Uangalizi wa Madaktari ..

Lakini Bado Mohamed Alihitaji kujua, bado alitaka kufahamu kwa kuwa kitendo kilichofanyika ndani Ya Ikulu Ya Nchi. Kuliitangazia Dunia kuwa Sehemu hiyo haikuwa salama tena kwa kufanywa makazi Ya Kiongozi wa Nchi. Kama watu wanaweza kuingia Ikulu na kutengeneza mchezo Mchafu watashindwaje kuingia na kumuua Rais? Yalikuwa maswali mazito yaliyokuwa yakipishana kwenye vichwa vya Wapelelezi wale Watatu. Hawakutaka kumuacha mtu yoyote iliyehusika kutengeneza hili tukio.

*****
Zilipita Siku tatu tokea litokee lile tukio la kuokolewa kwa Rais. Mohamedi akiwa amekaa sehemu na Jenifer wakipata chakula cha Usiku, wakamuona kijana mmoja mtanashati akiingia pale Hotelini. Kijana yule hakuwa mgeni machoni kwake kwani alishawahi kumuona sehemu, lakini bado hakuwa akijua ni Sehemu gani.. Baada ya yule kijana kuingia wakamuona Akiangaza Huku na Huko kanakwamba alikuwa akitafuta kitu ama mtu. Macho yake yalipokutana na Macho ya Mohamed akatabasamu kisha Akapotea eneo lile. Punde Mohamedi alikuwa amesimama na Jenifer alikuwa ameshafika mlangoni akitoka nje Huku Mkono wake ukishuka kiunoni ilipohifadhi bastola yake. Akaupita mlango na kutoka nje kabisa, Nyuma yake Alifuatiwa na Mohamed mikono yake Ikiwa mifukoni. Hatua kumi mbele wakakutana na Kitu Ambacho walikitarajia. Yule kijana aliyetoka pale ndani Alikuwa Amelala Chini ya Ardhi huku damu ikichuruzika na Kusambaaa. Wote hawakusimama wakapita kanakwamba hawakuwa wao.. Vichwani Vyao walishajua Ule ni Ujumbe. Ujumbe Uliyoletwa kwa Kuwakumbusha kuwa Mambo Badoo tena BADO SANA..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…