RIWAYA; Mapambano

RIWAYA; Mapambano

It has been a while,ndugu zangu hamjambo nimewakumbuka sana, majukumu mengi ila nitajitahidi kila nipatapo nafasi...MAPAMBANO YANAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE (EP 14)

"Chagua! ndiyo ni wewe pekee unayejua kwa ufasaha kipi unataka.Ukishindwa kuchagua utachaguliwa na hapo,utalazimika kukipenda ulichochaguliwa hayo ndiyo maisha,kila wakati unafanya machaguo ambayo yataleta tofauti katika maisha yako.Hivyo chagua mema badala ya mabaya ,utajiri badala ya umasikini afya njema badala ya magonjwa ndiyo kila unapofanya machaguo sahihi unapiga hatua chanya katika maisha yako".

Sasa tuendelee,Ni mwaka na miezi sita sasa tangu Brian arudi kijijini,na katika msimu wa pili tu tayari alishaanza kuyaona mafanikio hivyo alifungua kampuni yake ya kuuza mazao mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Alikuwa mwenye furaha sana hakuwaza mapenzi tena katika moyo wake kwa wakati huu,alijibidiisha kuongeza idadi ya mauzo ya bidhaa zake za mazao na kuongeza idadi ya hekari za mashamba katika mikoa mbalimbali,sasa alikuwa amewekeza katika mikoa minne ,Morogoro,Rukwa,Mbeya na Simiyu.

Wengi tumezoea kufikiria vitu vidogo sana,na tunaridhika tunapopata mafanikio kidogo sana.Bahati mbaya wanaofikiria mambo makubwa huonekana vichaa wakibezwa na jamii,kama huamini waambie wanaokuzunguka kuwa unataka kumiliki benki yako utasikia hata Bakhresa ,na Dewji hawana itakuwa wewe!

Hivi ndivyo ndoto nyingi huharibika kwa kukatishwa tamaa na wanaotuzunguka,Kijana Brian hakukatishwa tamaa alikuwa na malengo ya kuliteka soko la ndani na nchi za jirani katika sekta ya mazao.

Nchi za kiafrika husifika kuwa za 'wakulima' ilhali wakiagiza asilimia kubwa ya mazao kutoka nje Africa inatumia hadi dola za kimarekani bilioni 50 kuagiza mazao nje ya bara la africa.Nani ashawaza kuanzisha kampuni ambayo italilisha bara la Africa na kuuza nje ya bara hili?

Tayari alikuwa ameanza kuonesha nia kwa uwekezaji aliopanga kufanya,na wengi walishangazwa na mafanikio ya kijana yule aliyekuwa amejikita katika kilimo.

LONDON ,UNITED KINGDOM
Katika jiji hili lililosheheni watu kutoka mataifa mbalimbali,mzee aliendelea kupata starehe.Wadada walioumbwa wakaumbika,kila mmoja akionyesha ujuvi wake katika masuala ya kimahaba.Mzee alikuwa na kila starehe mara simu yake ikaita,.......

Turejee nyuma kidogo,Wengi wa wanachama wa Eagles waliofikia idadi ya 13 hadi sasa walikuwa wanafanya kazi wakijua wako chini ya mzee huyu aliyetorokea ulaya.Ni E1 pekee aliyejua kuwa mzee yule ni sehemu ndogo tu ya mtandao mpana wenye matawi kila pembe ya ulimwengu.

MAKABURI YA KINONDONI
Padri alikuwa akihutubia katika msiba huu ,kijana E3 alikuwa akiwekwa kwenye nyumba yake ya milele,kifo acheni kiitwe kifo hata E1 alikuwa akiltokwa na machozi ya huzuni alitamani amkamate kijana aliyemuua ndugu yake comrade E3 alitamani angekufa yeye,lakini ulikuwa wakati wa kumpumzisha kwa amani ndugu yao.Wanakwaya waliimba na hatimaye maziko yalihitimishwa na neno la shukrani na hatimaye umati wa watu waliokusanyika ukaanza kutawanyika.

Katika ulimwengu wa kisiasa tukio la kuuawa kwa kijana huyu lilitikisa vyombo vya habari,wanasiasa wengi walijitokeza kila mmoja akiiomba serikali isaidie kupatikana kwa muuaji wa kijana yule.Kwa ulimwengu huu unaoonekana marehemu alikuwa mwanaharakati wa masuala ya demokrasia na usawa na mwanafunzi wa kitivo cha sheria chuo kikuu cha Dar Es salaam.

Katika ulimwengu usioonekana alijulikana kwa code name E3,akiwa mtu hatari sana mwenye utitiri wa matukio magumu kabisa yaliyotekelezwa kwa weledi wa hali ya juu.

E1 alirudi kwenye jumba lao walilokuwa wakilitumia,ukimya ulikuwa umetanda ,wakati kama huu hata ujasiri hawakuwa nao tena Eaglet alikuwa akitetemeka kwa hofu akifikiria yatakayompata.Kwa upande wa Eagles walikuwa wakifikiria matukio ambayo E3 aliwaokoa,Simanzi ilitawala.

LONDON ,UK
Simu ya mzee iliita ,Amanda akaileta na kumkabidhi aliipokea na kusikiliza sauti nzito kutoka upande wa pili,
Ni sauti ya nani na anamwambia nini? Fuatilia sehemu ijayo
 
Back
Top Bottom