Mpo wadau ,Kama mmemaliza sehemu ya Tisa tuidrop sehemu ya kumi.
Mungu akipenda kesho nitakutilia hata kiji elfu 10Mlioniahidi jamani ,mnikumbuke kijana wenu na wanaojiskia kutoa chochote namba yangu ni 0785386036.Sehemu ya Tisa soon
mkuu, naomba mwendelezo basiSEHEMU YA KUMI NA MOJA
Sarah alikuwa katika lindi la mawazo,alikuwa njiapanda akishindwa kuamua aende ulaya kuonana na Sir McAllison ama abaki nchini kuendelea na kesi ya Nick.Kimaslahi safari ya ulaya ilikuwa kila kitu,Hata katika taaluma yake ya sheria ilikuwa na maana kubwa maana kufanya kazi na kampuni hii kubwa lilikuwa ni tamanio la kila muhitimu wa sheria.Aliendelea kuwaza na kuwazua,mara hii akiyakumbuka maneno ya secretary wa Sir McAllison,ukishindwa kufika nchini wiki ijayo hutapata nafasi nyingine ya kuonana na mzee huyu.Alimhurumia rafiki yake Nick,kesi yake ilikuwa ikimtegemea ,aliwaza kuwaachia ofisi yake waishughulikie lakini hakuona sababu ya kufanya hivyo.Akaamua kuchagua
Ndiyo-Kuchagua ni sifa kubwa aliyopewa mwanadamu,kila wakati mwanadamu hulazimika ama kulaazimishwa kufanya uchaguzi,achilia mbali chaguzi z kisiasa,za mavazi kabatini,chaguzi za kula chakula kipi,chaguzi za nani wa kuongea naye na nini cha kuongea naye,chaguzi za mahali pa kuishi n.k.Chaguzi hizi zimeanza kutoka enzi zamababu wakati fulani Adam alitakiwa kuchagua kati ya matunda mengine na tunda la mti wa katikati,Alichagua la mti wa katikati.Hivyo upatapo fursa hii ni vyema kuchagua kitakachokufaa ili uchaguzi wako uwe na maffanikio,haijalishi unapitia lipi CHAGUA.Ulivyo leo ni kwa sababu ya machaguo uliyochagua maishani.
Sarah alichagua kubaki nchini,ili apate muda mzuri wa kumsaidia Nick,kijana asiye na hatia ambaye alikuwa anateseka gerezani.Aliamua kuyaacha mengine yapite,ili mradi Nick atoke gerezani.Hiyo ndiyo furaha aliyokuwa akiingojea,alijiandaa kuelekea mahakamani kusikiliza kesi hii ya kijana Nick.
GEREZANI
Kijana Nick alipanda katika gari tayari kwa kuelekea,mahakamani ,hatima ya maisha yake aliiacha mikononi mwa Mungu.Maisha tunajifunza vipya kila siku,hapa gerezani kijana Nick alikuwa amejifunza kula kwa muda uliopangwa na gereza,na kula pasi nakubagua chakula,alijifunza pia kuwa sio wote waliopo mahali hapa walikuwa ni wakosaji.Kutokana na simulizi mbalimbali alizozipata hapa,wengine kwa kusingiziwa kesi mbalimbali na wengine kucheleweshewa kesi zao pasipo sababu za msingi.Aliyazoea maisha haya na kuyaona kama nafasi nyingine ya kujifunza,kwa leo alimuomba Mungu ombi moja tu Haki itendeke.
Watu wengi walihudhuria mahakamani hapo,ukiacha mawakili,na mahakimu,ndugu mbalimbali waliohudhuria mahali hapa,waandishi wa habari walijazana kila mmoja akijitahidi kuipata habari hii kwa undani.mahakama ilifurika.
********************************************************************************************************************************
E1 alikuwa katika chumba chake akiwa na kundi la vijana wapatao sita.Vijana wengine 10 walikuwa wamelizunguka jengo hili la kifahari walilokuwa wamelikodi.Walikuwa wakifatilia kwa umakini nyendo za mzee yule,walikuwa wameweka watu wao kila mahali kuhakikisha mzee yule anatii amri zao.Kwao kuipata Package ilimaanisha maana kubwa kwao,package ambayo wamekuwa wakiitafuta kwa muda mrefu sasa.Hawakutaka kuiachia fursa hii muhimu.E1 aliwaita wenzake na kuwagawia majukumu,E2 na E5 hakikisheni mnawareplace ,vijana wanaomfatilia mzee ili kusitokee kosa lolote,E3 hakikisha mawasiliano hayaingiliwi na ripoti ifike kwangu.Mimi nitafanya nini aliuliza E4 ,Be standby tuna kazi ya kuhakikisha tunaipata hiyo package kabla ya kesho alfajiri.
Kazi ya kuzipanga silaha ilimalizika,na kila Eagle kama walivyojiita kwenda katika majukumu waliyokubaliana,watu hawa wote walikuwa wasomi wa shahada ya juu,katika vyuo vikuu mbalimbali.Waliungana na walikuwa kama ndugu wakizifanya kazi walizokubaliana bila kusita,Walikuwa kama ndugu.Waliwashawishi na wengine kujiunga nao, wanafunzi hawa waliitwa Eaglets waliotakiwa kupitia mafunzo ya kimbinu kwa muda wa wiki 12,sawasawa na kipindi ambacho ndege Eagle huhitaji ili kuota manyoya.Eaglets walikuwa wakishirikiana na Eagles wakubwa nao wakipewa namba kulingana na seniority.Kikundi hiki kilikuwa hatari zaidi kwakuwa kilihusisha wataalamu wa kila nyanja.Kwanzia kompyuta,mawasiliano,udaktari,uinjinia,na fani zingine mbalimbali.Waliogopeka kwani hawakuwahi kushindwa katika mission yoyote waliyoipanga.
E1,we have an emergency,i repeat we have an emergency.Ilisikika sauti ya kiongozi wa Eaglet,aliyekabidhiwa jukumu la kufatilia nyendo za mzee yule.Alikuwa ameona kitendo kisicho cha kawaida,naam mzee yule alitwaliwa katika gari nyeusi na kuendesha kwa kasi kuelekea kusikojulikana.E1 aliita kikosi chake kikutane kwa dharura,ili kujadili tukio hili la ghafla.Katika uwanja wa intelijensia ni kosa kukurupuka,na madhara yake huwa makubwa.Eagles walijiamini na kuwaachia Eaglets jukumu la kufatilia nyendo za mzee yule lakini waligundua muda huu kuwa walikurupuka,katika kulifanya hili.Hawakuwa wamefanya uchunguzi wa kutosha kuwajua maadui wa mzee huyu,maana katika vita ni vyema kumjua adui yako,kuwajua maadui zake na marafiki zake ndipo utapanga mashambulizi yako.Uzuri wa kumjua adui wa adui yako ni kukusaidia kufanya urafiki naye,na hivyo kupambana naye bila kutumia nguvu nyingi.Mzee alikuwa ametekwa na kikundi kingine ambacho hawakukijua.Sasa ikaja zamu ya E1 kukifungua kikao hiki,"Eagles and Eaglets,hamjawahi kuniangusha,tumeshindwa kumdhibiti mzee huyu lakini tuna nafasi kubwa ya kuandaa shambulizi kuhakikisha tunaupata mzigo wetu"."Sasa priority ni kumtafuta mzee yule,mipango mingine yote inasitishwa kwa sasa,"Get him alive" aliamuru E1 huku akikifunga kikao hiki.Mara moja magari yakatawanyika,hili likielekea kigamboni,hili likielekea bagamoyo,Lililombeba E1 likielekea kawe na mengine yakizunguka kutafuta uelekeo wa magari yale.
Hatimaye ukaja wakati uliosubiriwa na kila mtu hapa mahakamani,muda wa kuzijua mbichi na mbivu za kesi hii.Jaji alianza kutoa historia fupi ya kesi hii akielezea jinsi maamuzi yalivyofikiwa na hatimaye kutaja kilichosubiriwa na wengi hukumuya kesi hii."Baada ya kujiridhisha na ushahidi kutoka pande zote mbili mahakama imemkuta Nickson,akiwa bila hatia ya mauaji.Hata hivyo amekutwa na hatia ya kutotoa taarifa polisi ambayo ingeweza kusaidia upelelezi.Alitulia kidogo,hivyo kwa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya ishirini,ninamhukumu mshtakiwa adhabu ya miaka saba gerezani".Alimaliza Jaji yule
Kila mtu alisema lake ,wazazi wa Ben hawakuona kama haki ilitendeka,Hali kadhalika ndugu na jamaa wa Nick waliona kaonewa lakini Jaji yule alimalizakesi ile na kutoa nafasi ya rufaa kama upande wowote hautaridhishwa na hukumu ile.
Kijana alilia,sio kwa sababu aliliogopa gereza,hapana alishakaa zaidi ya miezi sita sasa,sio kwa sababu ya biashara yake ya ushonaji ambayo hakujua inaendelea vipi ila kwa sababu ya wazazi wa Ben alitamani Mungu awaonyeshe kilichotokea na kwamba hakuhusika hata kidogo.Ilikuwa huzuni kubwa kwake.
Uelekeo wa magari mengine ulibadilishwa naam,waligundua uwepo wa idadi kubwa ya walinzi katika jumba hili,Kwa sasa lengo halikuwa kupigana bali ni kumuokoa mzee yule ili awape Package ambayo ilikuwa kipaumbele chao.Waliamua kuingia kivingine kabisa ,kwanza kwa kutumia simu maalum waliyokuwa nayo walijitambulisha kama askari maalum wa kikosi cha zimamoto waliokuja kuangalia miundmbinu ya kisima cha kuzima moto.kilichokuwa katika jengo lile.Msafara huu uliongozwa na E2 na kwa weledi mkubwa wakiwa na sare zao wakawahadaa walinzi na kuingia katika jengo lile.
Je watafanikiwa kumuokoa mzee yule,je ni nani aliye nyuma ya mpango ule wa kumteka ? Tukutane sehemu ijayo heri ya krismasi na mwaka mpya ,TUKUMBUKANE
Samahani wakuu sina PC hivyo natumia napopata nafasi nashusha uzi na tunaendelea,leo tukijaaliwa tutapandisha sehemu inayofuata