RIWAYA; Mapambano


nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Messages
265
Likes
232
Points
60
nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2016
265 232 60
DEDICATED TO IBRA87 RIP, Inspired by true story.

UTANGULIZI
Katika maisha mapambano hayaepukiki,Wakati wa kutunga mimba mbegu moja ya kiume hupambana na zingine milioni 45 kurutubisha yai moja,hata wakati wa kuzaliwa kiumbe hiki hupambana na mazingira mapya ya makazi yaliyo tofauti natumboni alimoishi kwa miezi tisa.Achilia mbali mapambano ya madaraka,ya vikundi vya magaidi na serikali,ya ndugu ya fikra na namna nyingine yoyote......Hii inathibitisha kwamba uwapo duniani huna budi kupambana kwa hiari au kwa lazima maana ndiyo njia pekee ya kuishi ,Lakini ni upi mtazamo wetu katika mapambano haya karibu ufuatane namimi.........

BAGAMOYO-PWANI
Hali ya hewa mahali hapa ilikuwa ya utulivu kabisa,jua lilikuwa likiendelea kukusanya makali yake,Ilikuwa ni asubuhi nyingine,Pilika zilikuwepo za hapa na pale za kujitafutia riziki ni kijana huyu pekee aliyekuwa kalala muda huu,si kwa sababu ya uvivu au kukosa kazi HAPANA

Alikuwa na mawazo,

Mawazo yaliyompelekea kutoka Nyumbani kwake maeneo ya Kinyerezi hadi hapa mjini Bagamoyo usiku wa manane.Kijana huyu aliyepitia mitihani mbalimbali maishani hakutegemea kwamba mawazo ya aina hii yangemzuia kwenda kazini kwake,Sasa aliiangalia tena saa yake ya mkononi ,09:45 Ilionyesha ,ndipo akagundua alikuwa amekaa mahali hapo zaidi ya saa 10 bila ya usingizi,ALIKESHA,akashangaa,akajaribu kujilaza kitandani apate japo usingizi kidogo ila akagutuliwa na sauti ya mhudumu aliyekuwa anataka kufanya usafi,akaanza kujiuliza maswali,au pengine kujilaumu kwa kilichotokea lakini akatamani iwe ni ndoto ,Aliwaza akawazua lakini hakupata majibu akaishika simu yake ya mkononi ndipo akagundua kuwa simu 25,meseji 10,na Email 9 zilizohitaji majibu kutoka kwa wateja wake,Alihitaji huruma kijana huyu ambaye wiki iliyopita alishinda tuzo ya kijana anayefanya vizuri katika sekta ya mitindo na ubunifu wa mavazi

OFISINI-TABATA SEGEREA
Hapo ndipo ilipokuwa ofisi ya kijana huyu,kijana wa miaka ishirini na tatu,mrefu wa wastani ,maji ya kunde kwa mwonekano ,hapa alikuwa ni mmiliki na mstendaji mkuu wa duka hili maarufu la ushonaji wa nguo.Alishona nguo za kiume na kike na hata watoto ,lilikuwa duka maarufu na wateja wengi waliamini na kuzipenda kazi zake.Leo wafanyakazi wake walikuwa tayari ofisini kama ilivyo kawaida lakini kijana huyu hakuwepo,walijaribu kumpigia lakini simu yake haikuwa ikipokelewa,Walianza kushauriana, Labda atakuwa kasafiri fundi mmoja akauliza,
"Hapana" akajibu Irene ,msaidizi wa kijana huyu anayepanga ratiba zake za siku na kusaidia mawazo ya kuiendesha biashara hii,Jana tulikuwa naye na alikuwa salama kabisa itakuwqa kapatwa na nini waliendelea kujiuliza.Mjumbe mmwingine katika kikao hicho kisicho rasmi akauliza,Irene jaribu kuwapigia marafiki zake,MMMMH,aliguna Irene rafiki yake ninayemfahamu ni mmoja tu na anafanyakazi benki kuu.Alipiga simu haikupokelewa,
Wafanyakazi wote 12 wa duka hili walibaki nje ya duka lao la ushonaji wasijue la kufanya wakapata wazo la kutoa taarifa polisi,Lakini wakati huu wakapokea simu kutoka kwa kijana huyu ambaye kwa ofisi zingine anaitwa BOSS jina ambalo kijana huyu alikataa kuitwa na badala yake kumuita kwa jina lake,NICKSON, naam,au kwa ufupi Nick ,alipopokea tofauti na siku zingine alimuita Irene na kutoa maelekezo.
"IRENE,utakaimu madaraka hapo ofisini hakikisha unafanya shughuli zote hadi hapo nitakapokwambia,kazi ziendelee kama kawaida na kama una tatizo lolote utanifahamisha"
Lakini Nick ukowapi,hakujibiwa swali lile na badala yake alishuhudia simu ikikatwa akabaki na mshangao.
**************************************************************************************
Kijana aliamka na lindi la mawazo aliyafikiria maisha yake ,lakini zaidi aliyafikiria maisha yake bila uhai na shida watakaozipata wafanyakazi wake akiondoka ,akalia,naam Mwanaume akilia kuna jambo kijana huyu jasiri leo alilia japo sauti wala kilio hakikusikika lakini macho yake yalitoa machozi.Alitamani dakika zirudi nyuma afute kumbukumbu zilizopita muda uliopita wa maisha yake ,kumbukumbu za tukio la kusikitisha aliloshuhudia kijana yule alihuzunika sana,Alikuwa kama mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na maambukizi ya ukimwi bila kushauriwa na daktari japo ni siku tu iliyopita ila kwake ilikuwa na matukio ya kutisha alitamani aende polisi akaeleze kilichotokea lakini akakumbuka onyo aliloachiwa kwenye usukani wa gari yake akatulia ,Hata kitabu cha The Alchemist alichoanza kusoma juzi hakikuwa na maana tena,Alitia huruma.
Akainuka kutoka katika kitanda cha hoteli hii maarufu hapa mjini Bagamoyo kumpisha mfanya usafi aliyemuangalia kwa jicho la huruma ,alivalia kaptula ya jeans na fulana nyeupe,akaanza kuzipanda ngazi kuelekea juu ya hoteli ile.Huku juu kabisa kulikuwa na mandhari ya kuvutia lakini kijana huyu hakuhangaika kuitazama badala yake alitafuta kiti pembezoni kabisa akaketi akayakubuka maneno ya William shakespear, "THE HELL IS EMPTY,ALL DEVILS ARE HERE" kwake yeye aliiona dunia kama sio mahali salama tena kwake Alimuomba Mungu amsaidie,akaita mhudumu mwingine na kumuagiza supu ya samaki,akainywa taratibu,lakini hamu ya chakula hakuwa nayo na hakumaliza dakika chache akaanza kushuka ngazi kurejea kwenye chumba chake,Akiwa kwenye nganzi akapishana na mmoja wa vijana alioonana nao usiku naam vijana walioweka ujumbe kwenye usukani wa gari lake,japo alikuwa kajibadilisha lakini kijana huyu alimtambua ,mapigo yake sasa yalizidi kwenda mbio kijasho chembamba kikazidi kuchuruzika aliingiwa na woga ,woga wa kumuona mbaya wake tena uso kwa uso, kijana huyu alisikitika.
OFISINI-TABATA
Leo kazi zilikuwa nyingi sana ,Irene ndiye alikuwa Incharge akipokea malipo yote ya wateja na kuzungumza nao huku mafundi wakiendelea na kazi zao,alizungumza na wateja wengi sana na mmoja wapo alikuwa Ben,rafiki mkubwa wa Nick mmiliki wa duka lile la ushonaji kijana anayefanya kazi Benki kuu hapa nchini,kijana ambaye hivi karibuni almetangaza kuwa anamtaka Irene awe mchumba wake lakini akakataa,pengine kwa sababu mbili kuu
kwanza hakuwa na hisia naye na pili alikuwa tayari ana mpenzi wake.mpenzi aliyenaye kwa mwaka sasa toka amalize chuo na Irene kupata kazi hapa dukani kwa Nick amekuwa akimtegemea kwa kila kitu.Irene alikuwa njiapanda alitamani azifuate pesa za Ben lakini upande mwingine wa akili yake ulimwambia atulie na mpenzi wake.Leo Ben alikuwa hapa dukani kwa shughuli mbili ya kwanza ni kutoa oda ya suti za wafanyakazi wenzake na pili,pengine ya muhimu zaidi ni kuonana na Irene.

Aliingia kama ilivyo ada ,akamsalimia Irene na kumueleza
"Irene sitaki kupoteza muda wako,unaona nimekuja kutoa oda tunahitaji suti za kiume 6 kwa ajili ya sherehe ndogo ya idara yetu na hivyowiki mbili ziwe tayari" alimaliza Ben,Irene akatabasamu akiandika andika kwenye kitabu chake,Ben akaongezea naomba kama utakuwa free nikupitie jioni Irene kama kawaida yake alitolea nje ofa hii.wakaagana, Ben akauliza simuoni Nick ametoka? Irene akajibu nilifikiri unajua alipo maana nimekupigia simu hujapokea,hapana akajibu kwa mkato na kuondoka.
Kijana Nick alikuwa katika lindi la mawazo,alitafakari kwa kina sababu za kupokea ujumbe ule hakuzipata hivyo akaamua kupiga simu,akapiga asikie upande ule wa pili lakini haikupokelewa....Akazidi kuwa na wasiwasi ni miaka 23 tokea kijana huyu mzaliwa wa mwanza azaliwe na miaka hii yote hajawahi kuingia katika hofu kama hii hofu iliyosababishwa na vitisho alivyoachiwa jana yake kwenye usukani wa gari yake ujumbe huu haukumtaja nani aliyeutuma lakini ulielekeza vitisho kwa Nick kwani alitajwa,akakumbuka kuipiga simu ya rafiki yake Ben ambae alimuona kama msaada mkubwa wakati wa shida ni Ben huyuhuyu anayemshauri kwenye mambo yake ya muhimu ,baada ya kupokea akamueleza ndugu yangu naomba uje hapa Bagamoyo mara moja sababu sitaweza kuondoka peke yangu ,kuna nini aliuliza Ben lakini kijana huyu alisisitiza, mmmh sawa Ben alijibu.kijana akakata simu yake.

SIKU MBILI KABLA HYATT-KIVUKONI
Kikao cha wamiliki wa Hyatt cha kutangaza kampuni iliyoshinda tenda yakushona nguo za wafanyakazi wake kwa miaka mitano kilikuwa kikiendelea wajumbe wote walikubaliana na mwenyekiti kuidhinisha kampuni ya kijana huyu Nick ikishinda zabuni na kuyaacha,makampuni mengine ya ndani na nje ya nchi.Ilikuwa ni taarifa njema kwa duka lake la ushonaji kwani huu ungekuwa mradi mkubwa wa 5 kwa mwaka huu pekee na mitatu ikiwa kushonea wafanyakazi wa ndege sare zao.Mafanikio haya yalilifanya duka lake kupata umaarufu na kukubalika pengine kuliko maduka mengine ya ushonaji.
Upande wa pili pembezoni kidogo ya barabara iendayo kibada gari aina ya Ford ranger lilikuwa limebeba wazee wawili wote wakiwa na asili ya asia walikutana mahali hapa kwakuwa hawakutaka kufahamika na hivyo kuchagua eneo hilo.walianza kujadili kwanini Hyatt imezikacha kampuni tanzu zao ambazo kwa miaka mitano iliyopita zimewapatia ukwasi mkubwa,lakini hili halikuwauma zaidi kilichowauma ni kwamba sasa wangekosa biashara halali ya kutakatishia pesa zao.Unafikiri nini kifanyike?Aliuliza mzee wa kwanza na yule wa pili akamjibu nina vijana naomba uniachie kazi hii wataimaliza.Hakikisha "they don't leave any tail behind" mzee wa kwanza akasema akikunja sura yule wapili akamjibu nice and clean.wakaagana.

******************************************************************************************************
Kijana yule aliendesha gari lake kuelekea Kivukoni kwa ajili ya kusaini hati ya makubaliano au ungeweza kuiita mkataba wa kushona nguo za hoteli hii kwa kipindi cha miaka mitano ijayo,Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwake kushuhudia dili nono kutoka hoteli hii ya kimataifa,Alifika na kukaribishwa na msaidizi wameneja na moja kwa moja wakaelekea kwenye kusaini,alipewa nakala yake kisha akampa mwanasheria wake aliyeambatana naye kwa ajili ya kuipitia baada ya kujiridhisha ,mwanasheria yule alimshauri kuwataka Hyatt kurekebisha baadhi ya vipengele kisha zoezi likafungwa.wino ukamwagwa ,picha zikapigwa.
Baada ya kutoka hapa kijana alirejea ofisini mwake ambako habari zilikuwa zishafika kila mtu alimpongeza lakini yeye aliwaambia kwamba wa kupongezwa ni nyinyi na wateja wetu ambao kila wakati wanatuamini na kutupa nafasi hii ya kufanya kilicho bora.kazi zikaendelea kama kawaida na muda wakufunga kijana huyu akafunga ofisi na kuondoka,kwenye gari lake alikuwa peke yake akisikiliza nyimbo za asili ya afrika hasa mitindo ya zouk,hii ndio ilikuwa furaha yake.Akaelekea nyumbani kwake kinyerezi alipoiacha barabara inayoelekea majumba sita akakata kulia mbele kidogo akaiona gari nyeupe ikiwa nyuma yake huwa hapendi kufuatwa akaongeza mwendo ,gari ile haikuongeza mwendo badala yake ikasimama pembeni mwa barabara kijana yule hakujali alifika nyumbani kwake geti lilikuwa wazi akashangaa,akakumbuka alilifunga vizuri asubuhi,akashuka garini na kwenda kulifunga geti majabu,
Gari ile iliyokuwa imepaki sasa iliingia getini kwake kwa kasi akaogopa,kijana huyu akashika simu yake lakini kabla hajafanya chochote akasikia sauti yenye mamlaka ikimwamrisha kuweka mikono yake juu akatii,akapigwa na kitako cha bunduki vijana wale wakaondoka kwa spidi kubwa"
Nini kiitaendelea ,tafadhali fuatilia sehemu ya piliu
 
wambura wa Itnd

wambura wa Itnd

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2017
Messages
344
Likes
1,525
Points
180
wambura wa Itnd

wambura wa Itnd

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2017
344 1,525 180
Amani mkuu,seatbelt moja kwa moja.
 
nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Messages
265
Likes
232
Points
60
nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2016
265 232 60
stay tuned part 2 soon
 
nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Messages
265
Likes
232
Points
60
nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2016
265 232 60
SEHEMU YA PILI

Dunia ni pana,wakati mwingine anatumia milioni kwa siku , mwingine anahangaika kupata japo mlo mmoja kwa siku,kwa kijana huyu ulimwengu wake ulitiwa kiza au tuseme alikuwa katika hali ya kutokujitambua, Alikuwa kama mfu.kuna wakati mtu hatambui kinachoendelea duniani,kijana huyu hakujua hata pengine jina lake kwa wakati huu,hakuwa katika fahamu zake.Vijana waliendelea kuendesha gari kwa kasi sasa wakiiacha boko kuelekea bagamoyo mbele kidogo mwendo wa saa moja gari lilikata kushoto na kufuata njia ya vumbi na baada ya muda mfupi ikasimama mbele ya nyumba moja,nyumba hii ilikuwa kama imetelekezwa kwa muda lakini ikiwa na huduma zote za kijamii.walisimama na kumshusha kijana yule aliyekuwa hajarejewa na fahamu zake ,wakamuingiza katika chumba kimojawapo na kumkalisha kwenye kiti.

Eagles,kama walivyojiita, kikundi cha shughuli maalum walikuwa na vijana wengi wenye weledi wa hali ya juu,wengi wao wakiwa wastaafu wa idara mbalimbali za kijasusi, walikuwa wamehitimisha kazi waliyopewa,na mzee yule aliyewapa kiasi kikubwa cha pesa kwa kazi hii tu ambayo walikuwa wanaianza, hivyo kiongozi wao waliyemuita E1,aliinua simu yake na kumtaarifu mzee yule kwamba kazi ya awali ilikuwa imekamilika na kusubiri maelekezo yake,"amezinduka "? akauliza mzee yule ,bado, jibu likatolewa na E1,make him talk ,we dont have much time left alimaliza mzee yule asiye na maneno mengi.

Kijana huyu alizinduka toka usingizini,usingizi ambao hakuelewa jinsi alivyoupata,akajaribu kuinuka kitini ndipo akagundua kuwa amefungwa kamba mikononi na miguuni,alihisi maumivu makali,shingoni,mpaka sasa hakujua ni kwa sababu ipi yuko maeneo haya na ni kwa namna gani angeweza kujinasua,habari yako "E1 alimsalimia kwa dharau kubwa na kuongezea ,"nahitaji ushirikiano wako na sitakuwa na muda mwingi wa kukaa nawe"
'nimewakosea nini naomba mniachie tafadhali" Alilalama kijana yule
E1 alicheka na kumpiga kofi zito shavuni kofi ambalo lilimpelekea kukaa katika hali yakizunguzungu ,

Eagles wakapokea simu muda si mrefu kutoka kwa bosi wao,wakabadilisha kila kitu yaani kitaalamu 'changing plan'

**************************************************************************************************************************************
Kijana huyu hakujua ni mda gani alifika hapa nyumbani kwake, kumbukumbu zake zilikuwa kuwa na watu asiowajua ,aliangalia huku na kule lakini ukimya ulitawala alikaribia kuamini kuwa ile ilikuwa ndoto ya kutisha kabla ya kuusoma ujumbe ujumbe kutoka kwa watu hawa hatari waliomteka muda si mrefu,maneno ya ujumbe huu yalimfadhaisha akawakumbuka wafanyakazi wake akakumbuka nyumbani kwao,Mwanza akatamani hali hii ya mpito ipite haraka.Kwenye usukani wa gari yake ,ulikuwepo ujumbe,ujumbe huu wa maneno machache ujumbe uliotoa onyo kwake,ujumbe uliomtisha kijana huyu,ujumbe uliomlazimisha kuondoka usiku huu kuelekea Bagamoyo,watu waliouandaa hakujua lengo lao haswa ila alitambua kuwa hawakuwa na nia nzuri na yeye na kwamba maisha yake yalikuwa hatarini.

OFISINI TABATA-
Leo shughuli ziliendelea kama kawaida ila ,bila kijana yule waliemzoea kijana ambaye kila mtumishi wa duka hilo la ushonaji alijihisi amanin kufanya naye kazi,kijana ambaye aliyajua maisha ya wafanyakazi wake na palipohitajika kuwa mshauri mzuri wa maswala yao,kila mtu kwa imani yake alimuombea kijana yule ambaye sasa walihisi hayuko sawa kiakili walimfahamu na walijua atakuwa kwenye matatizo makubwa.Maana ilikuwa kawaida ya kijana huyu kuwapigia simu asubuhi na mapema kuwajulia halinna kuwataarifu juu ya kazi za siku hiyo na alitumia muda huu kuyajua maisha ya wanaomzunguka na kuwatakia asubuhi njema,leo siku ya pili bila simu yake ilikuwa kama mwaka kwao.

Wateja mbalimbali waliendelea kumiminika,Irene msaidizi wa kijana huyu alikuwa kwenye lindi la mawazo ,mawazo ambayo sio ya mchumba wake aliye na tabia za ugomvi,au ya Ben kijana ambaye muda huu amekuja juu akilitaka penzi lake kwa hali na mali,bali mawazo ya kijana yule ambaye hakuchosha kukaa naye.kijana ambaye kufanya naye kazi kutakufanya kugundua hata vipaji vilivyo ndani ya mtu.Kijana mstaarabu asiye na makuu,kijana aliyemshauri hata akavumilia maisha ya kuwa na mchumba wake huyu ambaye ugomvi usioisha ilikuwa tabia yake,mchumba wa Irene ambaye japo hakuwa akifanya kazi yoyote ya kumuingizia kipato alikuwa akimuendesha Irene kama gari bovu,Irene alitamani angekuwepo kijana huyu asahau japo kwa muda shida za nyumbani kwake,Pamoja na ukaribu wa kikazi walionao na kijana yule Irene hakuwahi kumuona akiwa na mwanamke yoyote,ukiacha wateja wake ambao kwake wote walikuwa sawa wakihudumiwa sawasawa na falsafa ya 'mteja ni mfalme' kwa vitendo.Katika mazungumzo yao Irene alipogusia swala hilo kijana yule aliliepuka swali hili mara nyingi huku akitoa utani wa hapa na pale.

Katika maisha kuna wakati unalazimika kufanya maamuzi,maamuzi haya ukiyachukua unakuwa kama mtu aliyejitupa katikla mkondo wa majin mengi,ambayo yatakupeleka mahali ambapo hukuwahi kufikiria unaweza kufika kijana alikuwa akisoma maandiko haya ya hekima kutoka kwa mwandishi maarufu Paul Coelho,katika hadithi ya Alchemist akielezea hadithi ya kijana aliyeacha seminari na kuamua kuwa mchungaji ili apate kuufurahia moyo wake,na kusafiri nchi ya mbali kuitafuta hazina iliysitirika katika mapiramidi ya misri.Kijana sasa alikuwa na machaguo mawili,la kwanza kujiona kama mhanga wa tukio la jana yake na chaguo la pili ni kujiona kama kijana mwenye mafanikio aliyeshinda zabuni ya HYATT katika siku za karibuni kijana alichagua chaguo la pili na tabasamu likarejea.Alilichagua chaguo hilo kwa sababu hakuogopa tena kupoteza maisha yake kwa kuwa hata angetoweka leo hii tayari alikuwa amegundua kusudi lake la kuwepo duniani na kuyaangaza maisha ya wachache waliomzunguka.

Sasa aliaga hotelini na kurudi ofisini kwake lakini kabla alipita nyumbani kwake kubadilisha mavazi,alioga nakuchagua suti nzuri,suti iliyomkumbusha alipotoka alipoivaa suti hii alijihisi mtu wa thamani,thamani iliyokuja baada ya kuhangaika,alizikubuka siku zilizopita akamkumbuka mpenzi wake Pendo,akashika simu akampigia,simu ilikatwa ,Laiti angejua atakayokutana nayo asingepiga simu ile,ila kijana huyu alipiga simu nyingine na nyingine mwisho sauti nzito toka upande wapili ikamuuliza
"wewe nani,mbona unamsumbua mke wangu" alishikwa na butwaa
kwa muda huu wa mwaka na miezi sita ambapo alipambana kuhahakikisha duka lake la ushonaji linakua alisahau,kuwa moyo wa mwanamke ni siri anayoijua mwenyewe ambayo kuifurahia lazima ujitahidi kuwa naye na kutenga muda,naam muda ambao kijana huyu alikuwa akihangaishwa na changamoto za kazi zake,muda huu binti huyu Pendo aliamua kuolewa,Kitendo hiki kwa kijana huyu kilitafsiriwa kwamba ni ukatili usio na mithili yake,

"Kama aliamua kuolewa si angeniambia" akawaza kijana huyu
sasa alipiga simu ya pili kwa kaka yake na Pendo kujiridhisha kama aliyoyasikia ni kweli,kaka huyu alimwambia aliyokuwa anajua yaani Pendo yuko kigamboni kwa shangazi,anafanya kazi.Akashangaa,hakujua amuamini yupi,akaamua kuiga tena namba ya pendo safari hii akaisikia sauti nzuri ya mrembo huyu,mrembo mwenye haiba ya kiafrika,rangi yake nyeusi nyororo ambayo kwa kipindi hiki haikuwepo kwa watu wengi,mrefu ,mwenye kiuno kilichowekwa mahala pake na kutunukiwa zawadi ya nyama zinazostahili zilizosababisha mtikisiko alipokuwa akitembea,sauti iliyomkumbusha Mara ya kwanza alipompata mrembo huyo,wakati kijana huyu akiwa kidato cha tano,akakumbuka sauti yake aliposema NAKUONA KAMA KAKA YANGU,akakumbuka ushawishi alioutumia kuibadili kauli hii kuwa NITAKUFIKIRIA,kauli ambayo kwa watanzania wengi humaanisha kukubaliwa kwani warembo wa haiba hii hawana uthubutu wa kusema NDIYO,sijui kinachofikiriwa huwa ni nini lakini kijana huyu alijua sheria hii,akakumbuka furaha aliyokuwa nayo alipolimega tunda kwa mara ya kwanza huku wakipeana ahadi,akakumbuka jinsi alivyojitoakwa binti huyu ,akakubuka yote waliyoyafanya katika enzi za uhai wa penzi laoambalo lilikuwa likiyumba kama dakika za mwisho kabla ya kuzama kwa kivuko cha MV.Nyerere,kijana huyu akagutuliwa kutoka kwenye lindi la mawazo na sauti,sauti ya kiume kando ya binti,iliyomwambia
"mwambie"
Sauti hii iliashiria mambo mawili,kwanza alikuwa kawekwa loudspeaker na muhimu zaidi walikuwa wote yaani pendo na mme wake ,Pendo akasema tushaachana mimi na wewe ,sasahivi nimeolewa,kijana akajaribu kujiuliza ni lini waliachana asipate majibu badala yake akagundua kuwa alikuwa AMEACHWA,katika mahusiano mwanamke anaweza kuanzisha mapenzi bila kumwambia mpenzi wake wa sasa na mwanaume hali kadhalika ,sababu za kufanya hivyo zinatofautiana lakini kati yao hakuna ajuaye madhara anayoyasababisha kwa upande mwingine,kijana alijiuliza ni kipindi kipi haswa aliachwa hakuwa na majibu,ila alijua kwa hakika kwmba pengine ilichangiwa na umaskini wake,akakumbuka jinsi alivyotoa kidogo alichokuwa nacho akakumbuka,hata alivyopewa pesa na wazazi wake kwa ajili ya matumizi ya chuo atoe kiasi kwa ajili ya binti akakumbuka ahadi aliyomuahidi binti,wakati ule ikionekana sio tu ngumu bali haitekelezeki,kijana aliwahi kumwambia Pendo kuwa atanunua Ford Ranger siku moja ambebe,hadi kwao mwanza,akawasalimie,akakumbuka kicheko cha dharau kutoka kwa binti huyu aliyemwambia kodi ya chumba chako inaisha mwezi wa nane huna kazi iweje uwaze kununua gari tena Ford,binti huyu alijua mambo mengi ikiwemo bei ya gari hili lakini hakujua kuthamini ndoto za mtu na pengine hakujua kwamba haina ubaya wowote kutamani mafanikio maishani,kwakuwa hii niyonjia pekee ya kufikia mafankio, leo hii Ford alikuwanayo lakini binti anadai kaolewa,alisikitika,kilichomuuma zaidi ni wazazi wake Pendo kutokuwa na taarifa na ndoa bubu hii,akayakumbuka maneno ya mtunzi mmoja aliyewahi kusema "The expectationof dream coming true is what makes life exciting" kwake yeye alikuwa katimiza Angalau moja kati ya ndoto zake lakini alipata Ford akamkosa Pendo akasononeka,Lakini akayakumbuka maisha ya kondoo akakumbuka jinsi gani kondoo asiye na ufahamu anavyomzoea mchungaji mpya,akapata faraja,akajisemea kama mnyama asiye na ufahamu anazoea maisha mapya mimi ntashindwa vipi, akaondoka kuelekea kazini kwake,ilikuwa siku ya simanzi kwake lakini aliamua kuwa mtu mwenye furaha kwa sababu haijalishi uko kwenye hali gani,kinachokutofautisha ni mtazamo wako juu ya swala hilo,wakati anelekea ofisini akaiona gari ile gari iliyosababisha simanzi kwake kwa muda wa siku moja uliopita,safari hii akaamua kufanya kitu.

Ni kitu gani kijana kafanya,tafadhali fuatilia sehemu inayofuata.
 
nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Messages
265
Likes
232
Points
60
nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2016
265 232 60
Jumamosi njema ndugu zangu,mzigo huo
 
Mtepetallah

Mtepetallah

Senior Member
Joined
Jun 30, 2016
Messages
170
Likes
105
Points
60
Mtepetallah

Mtepetallah

Senior Member
Joined Jun 30, 2016
170 105 60
Nipo kiti cha mbele kabisa nasubiri uhondoo
 
Bigjahman

Bigjahman

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2011
Messages
704
Likes
143
Points
60
Bigjahman

Bigjahman

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2011
704 143 60
Mkuu ongeza ongeza
 
nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Messages
265
Likes
232
Points
60
nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2016
265 232 60
SEHEMU YA TATU
Kupitia vioo vya pembeni kijana aliiona gari aina ya Nissan ikimfuata kwa kasi kubwa,Gari hii nyeupe ilizidi kuikaribia gari ya kijana Nick ambaye alianza kuingiwa na hofu,sio kwa sababu ya gari kumfuata LA! Kwa sababu ni gari hilihili lililotumika kumteka kijana huyu,Alivuta breki kwa nguvu na kubadilisha uelekeo kwa haraka tukio ambalo halikutegemewa na Dereva wa ile gari nyeupe,mbele kidogo gari nyeupe ikapatwa na msongamano mkubwa na kushindwa kuifuata gari ya Nick,kijana huyu alizidi kuingiwa na wasiwasi mkubwa.

Simu ya E1 Ilianza kuita mfululizo ,alipoiangalia kuona jina la mpigaji aliingiwa na mashaka,Mzee anapiga, alisema kwa sauti ndogo,sauti iliyosababisha kuingiwa na mshtuko mkubwa miongoni wa vijana hawa ambao walikuwa ndani ya gari hilo.Sio kawaida ya mzee huyu kuwapigia simu vijana wake wanapokuwa kazini ,kwa sababu za kiusalama ila leo aliwapigia simu,na hilo liliwashangaza.Japo walikuwa wamefungulia AC lakini jasho liliwatoka vijana hawa.
"E1 mna taarifa zozote za kunipa",aliuliza mzee yule,"Tuna tatizo kidogo mkuu", alijibu E1,
"kijana kabadili uelekeo ghafla,tumempoteza"akaongezea E1 ,You know what I want,don't fail me again akamaliza mzee yule.

Kijana sasa alipunguza mwendo na kupinda kushoto na kuelekea nyumba moja iliyokuwa umbali wa mita kama 350 kutoka barabarani maeneo ya Baracuda,alipiga honi mara mbili kisha akatulia na kusubiri mlango ufunguliwe,aliendelea kusubiri kwa dakika zingine 20,Lakini geti halikufunguliwa, akaamua kushuka achungulie ndani ya uzio wa nyumba ile,ndipo akagundua mlango ulikuwa wazi umerudishiwa tu, kijana huyu akaamua kuitii hamu yake ya kuingia kwenye nyumba ile,sauti ya mziki hafifu ilisikika kijana huyu akagonga tena mlangoni wakati huu alisikia sauti ya kilio hafifu toka ndani ya nyumba hii,IRENE,IRENE Aliita kwa nguvu lakini mlango haukufunguliwa akachukua simu yake ya mkononi na kuipigia simu ya IRENE lakini haikupokelewa ,akajaribu kupigia mafundi ofisini kwake tabata,akapewa taarifa kuwa Irene aliondoka muda mrefu uliopita alielekea nyumbani kwake,Kijana akapatwa na wasiwasi .Akaamua kuzunguka nyuma ya nyumba ile huku alimkuta Irene akilia mfululizo,alikuwa kakaa asijue nini cha kufanya,hata ofisini alipaona pachungu.Kijana alimuonea huruma.

Kuna wakati mtu hutamani kuwa peke yake ,ili apate mda wa kukaa sawa kiakili,muda huu ni muhimu kuleta msawaziko wa kifikra haswa linapotokea jambo zito,kijana huyu japo alikuwa na mawazo mengi aliamua Kumbeba Irene na kumtegemeza kwenye sofa kisha akafungua jokofu na kumpa maji ya baridi,Japo kijana alikuwa na matatizo makubwa lakini hakupenda kumuona mtu hasa mwanamke akilia,kijana hakusema neno lolote badala yake alimuaga Irene na kuondoka kurudi kazini.Aliamua kulitelekeza gari lake pale kwa Irene na kuchukua usafiri wa pikipiki hadi nyumbani kwake akaingia ndani.
kijana huyu alikuwa ana wakati mgumu alihitaji faraja asiipate,alitaka mtu wa kumsikiliza akimsimulia kilichotokea asimpate.Akaamua kufungua TV yake aangalie japo taarifa ya habari.Alishangazwa na kichwa cha habar i" KIJANA NICK ANATAFUTWA NA POLISI KWA KOSA LA KUSHIRIKI MAUAJI YA RAFIKI YAKE BEN".Milango ya kuzuia machozi ilionekana kufunguka dhahiri kwani kijana huyu alilia mfululizo,asijue la kufanya ni kama mkosi ulikuwa ukimwandama.

Eagles sasa walijipongeza kukamilisha hatua ya tatu ya mwisho katika oparesheni hii ya kumchafua kijana huyu,sasa walikuwa wakijipongeza kwa vinywaji vikali,Huyu akinywa Vodka na huyu akinywa Valeur,ilikuwa furaha kwao kwani walishapanga mpaka hoteli watakayofikia watakapoenda fukwe za Bahamas kupumzika.Mzee aliwapigia simu kuwapongeza, vijana mmefanya kazi nzuri " Lazima huyu mpuuzi afie jela,na tutahakikisha tunamfilisi mali zake zote" lakini vipi yule mwanamke Irene mmemshughulikia kweli,aliuliza kijana mwingine ,"yule tunashirikiana naye" alijibu E1.

Taarifa za mauaji ya Ben zilisambaa kwa kasi kubwa,lakini upande wa pili kuhusishwa kwa rafiki yake Nick katika mauaji haya kuliisababisha habari hii kuwa mbele ya magazeti karibia yote asubuhi hii,Kijana Nick aliendelea kulia na kumuomba Mungu ampe nguvu za kulikabili wimbi hili lililokuwa linaelekea kumpoteza,na kutishia maisha yake kwa ujumla,Leo alikuwa mnyonge kupita kiasi,akijiuliza ni kwa namna gani watu hawa wameyavuruga maisha yake,alitia huruma.

Gari lililobeba mwili wa Ben sasa liliwasili Hospitali ya Hindu Mandal kwa ajili ya kuhifadhiwa ,katika msafara huu pia lilikuwepo gari la kamanda wa polisi wa mkoa ule likiusindikiza msafara,watu wenye nyuso za majonzi walifika hospitalini kuonyeshwa kuguswa na msiba ule.

Irene sasa aliamka kwenye sofa alilokuwa kajilaza,alioga akabadilisha nguo na kuvaa gauni refu la rangi ya zambarau,alionekana mrembo kweli ,alienda kuonana na uongozi wa HYATT kujadili mustakabali wa ofa yao baada ya mkurugenzi wao kupatwa na tuhuma ile nzito ya mauaji.Irene alifika mahali pale na kukuta wazee wale wakiwa katika mkahawa uliopo juu kabisa ya ghorofa ile,aliwasalimia kisha akawaambia juu ya lengo la ujio wake mahali pale,wazee hawakuona umuhimu wa kufanya vile lakini Irene akawaambia wafanye vile ili kuondoa wasiwasi wa watu wanaomtilia shaka.

Kila siku ina utofauti wake,siku ya leo kijana alikuwa anapelekwa rumande akisubiri kusomewa shtaka lake,Alizidi kumwomba Mungu amuepushie na lile balaa lililoko mbele yake,alitamani japo angepewa dakika mbili azitumie kuongea na Irene lakini hakupata wasaa ule.Hakuwahi kufikiria kuingia maeneo haya ya gereza,alipita kwa nje akielekea airport au kwenye mashamba yake chanika ,hakuwahi kufikiria kulala humo japo siku moja.

OFISINI-SEGEREA
Kikao kidogo kilichochukua muda wa nusu saa cha mipango ya kazi muda ambao Boss wao hatakuwepo kazini kilimalizika na kuamua Irene aendelee kukaimu madaraka ya uongozi wa duka hilo na waliomba kijana huyo aweze kuachiwa kwani walihisi hana hatia.kijana huyo alijua uongozi haswa,japo hakuwahi kuwa kiongozi katika shule alizopitia lakini akiwa jeshi la kujenga taifa alifundishwa maana na umuhimu wa uongozi,Nick alifundishwa kwamba hakuna askari mbaya ila kuna kiongozi mbaya.Aliitumia kanuni hii katika maisha yake akiwajibika hata kwa makosa ya wafanyakazi wake kwa kuwa alijua lawama haziwezi kusaidia kitu.Kila mtu aliutamani uwepo wake na kumuombea aweze kuachiwa huru.

Basi la magereza lilielekea mahakamani kisutu kulipokuwa na msururu wa magari na waandishi wa habari wakitaka kujua kinachoendellea kwenye kesi hii iliyoshika hisia za watu wengi mmojawapo kati ya watu wengi waliohudhuria alikuwa ni Sarah mwanasheria Nguli aliyekuwa kiongozi wa mawakili kwenye taasisi yake iliyoitwa Sarah Attorney,alikuwa zaidi ya rafiki kwa kijana huyu hivyo alikuja kutoa utaalamu wake kumsaidia kijana huyu.Mahakama ilifurika isivyo kawaida,muda wa kuanza kesi ukaanza,Mwendesha mashtaka wa serikali alisoma mashtaka yaliyoelekezwa kwa kijana huyu ambaye alikuwa akilia muda wote huu,na kijana huyo kukana mashtaka hayo.katika maombi ya dhamana ,mahakama ilikataa kutoa dhamana kulingana na kosa la mtuhumiwa kuwa la mauaji,Hakimu akaahirisha kesi hadi wiki iliyofuata.

Hali ya kijana Nick ilizidi kuimarika,alifarijiwa na mzee mmoja aliyemkuta gerezani mzee huyu wa makamo ya baba yake mzazi alimsimulia jinsi alivyopewa kesi ya mauaji baada ya kulala na mke wa kigogo mmoja,kijana alifarijika haswa na busara za mzee huyu alisahau machungu yake alianza maish mapya akiwa gerezani,Akimuomba Mungu amsaidie.
Leo hii Afande mmoja alikuja na kumuita NICK,kuna mgeni wako anahitaji kuonana nawe?
Nani huyo anamtembelea Nick, tafadhali toa utabiri wako.Tukutane sehemu ijayo
 
macson3

macson3

Senior Member
Joined
Nov 10, 2017
Messages
184
Likes
159
Points
60
macson3

macson3

Senior Member
Joined Nov 10, 2017
184 159 60
Nahisi ni Sarah. Good job mkuu.
 
nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Messages
265
Likes
232
Points
60
nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2016
265 232 60
SEHEMU YA NNE
"NICKSON" Aliita afande na kumtaarifu juu ya ujio wa wakili wake,Sarah.Nick hakuweza kuificha furaha aliyokuwa nayo ,katika sehemu ya mazungumzo ,Afande aliwapa dakika 30 tu za kuzungumza.
"Pole sana Nick,kwa unayopitia" Alianza ,Sarah akimgutua Nick aliyekuwa akifuta machozi machoni pake.Kijana huyu alimshukuru Sarah kwa kufika na kumuwakilisha katika tuhuma nzito za mauaji zilizokuwa zikimkabili.Sarah huku akimfariji kijana alimwambia kuwa alikuwa pale kama ambavyo mtu mwingine anavyojali mtu anayemthamini.
"vipi Sarah, tutashinda kweli mtihani huu", aliuliza kijana Nick huku akionyesha dhahiri,hofu aliyokuwa nayo.Sarah alimfariji kuwa atafanya kila kinachowezekana,Mwanamke huyu Nguli wa sheria,alimtoa wasiwasi Nick.Dakika hizi zilizoonekana kwenda haraka hatimaye zilielekea ukingoni,

"Vipi Pendo ,amekuja kukuona aliuliza Sarah,Lakini wakati huu hakuweza kupata jibu kutoka kwa kijana huyu,Jibu la kijana huyu pengine lilicheleweshwa ama na Sauti ya afande aliyemtaka kurudi kwenye chumba chake au,Kwa uhakika zaidi Majonzi aliyokuwa nayo juu ya Pendo.Waliagana huku kila mmoja akitoa machozi na dada huyu kurejea nyumbani mwake.

Binadamu au pengine viumbe hai,vimenyimwa fursa ya kuona matukio yatakayokuja mbeleni,hii sababu imepelekea kuibuka kwa makundi ya watu wakijiita watabiri na kujigamba kutafsiri nyakati zijazo.Kwa kufanya hivi wanapata watu ambao huuliza kuhusu hatima yao,kuhusu kazi,mahusiano,na ndoa zao na mengineyo mengi.Kwa kijana huyu alikuwa akiikumbuka miaka takribani mitano iliyopita alipofanya uamuzi mzito,ambao pengine aliujutia kwa kipindi hiki,Uamuzi huu pengine ungemuweka kuwa mtu tofauti kwa kipindi hiki.Kijana alitamani pengine angerejea miaka mitano iliyopita na kuibadili historia yake kitu ambacho kisingewezekana,alihuzunika.

Nyumbani kwa Sarah katika moja ya nyumba za kisasa zilizoko masaki,mwanadada huyu alifungua jokofu lake na kuchukua Champagne aina ya Dom Perignon kutoka kampuni ya MOET iliyotengenezwa Champagne,kaskazini mwa nchi ya ufaransa.Ili kinywaji kuitwa champagne, ni lazima kitokee katika eneo hili la champagne na pia lazima kipitie hatua inayoitwa "methode champenoise",Kinywaji kingine cha aina hii kisichotokea jimbo hili la ufaransa huitwa sparkling wine.Kinywaji hiki hufukiwa pia ardhini kwa njia za kiasili kuruhusu hatua ya fermentation iendelee na hii huongeza utamu wake,hiki cha Sarah kilikuwa cha miaka 7 iliyopita.kwake kilikuwa ni kinywaji pendwa hasa anapomkumbuka kijana Nick,asiwezekumsahau.

Sarah alikumbuka alivyokutana na kijana huyu miaka mitano iliyopita katika moja ya kambi za jeshi la kujenga Taifa iliyoko Dodoma,ambapo wahitimu wa kidato cha sita kutoka shule mbalimbali nchini walihudhuria,katika mafunzo ya mujibu wa sheria.Wakiwa jeshini,mwanadada huyu mrembo alikumbuka ukaribu waliokuwa nao na kijana huyu aliyemfanya aone jeshini kama nyumbani kwao,japo wengi hufikiria jeshi kama sehemu ya mateso.Hii ni sehemu ambapo askari hufundishwa ushirikiano,upendo,na ukakamavu.Huku wakiwa na kaulimbiu yao isemayo "one for all,and all for one" yaani mmoja kwa ajili ya wote na wote kwa ajili ya mmoja.Katika utekelezaji wa kaulimbiu hii tofauti na shuleni ambapo mtoro hupewa adhabu,jeshini mtu akitoroka kipindi kombania yake hulazimika kupokea adhabu kwa ajili yake,hii hujenga kuthaminiana na kupendana,ili walipo wenzako nawewe uwepo.Sarah na kijana huyu wote walibahatika kupangwa kombania moja ,iliyopewa jina la FIRE , Au kwa kifupi Fcoy,na walishirikiana katika kila jambo.
Kwa kijana huyu alimchukulia Sarah kama,rafiki yake wa karibu lakini hisia za mapenzi ya binti huyu kwa kijana Nick,hazikuwahi kujificha,pamoja na jitihada alizozifanya binti huyu hapa jeshini za kuwa pamoja na kijana huyu kimapenzi lakini kwa kijana huyu mawazo akili,pengine hata baadhi ya ufahamu wake ulikuwa kwa Pendo,sio kwa Sababu ni mzuri sana,LA!

Kwa sababu ya mapenzi,aicheni yaitwe mapenzi
Mapenzi yaliyomfanya ,Adam kulila tunda lile la mti wa katikati,Naam yale yaliyomfanya shujaa Samson kukubali kunyolewa nywele zake,Pengine yale ya Yusufu aliyekubali kumuoa Maria ilhali akijua ana mimba isiyo yake.Kijana huyu alikuwa kwenye ulimwengu wa mapenzi.
Wengine huyafikiria mapenzi kama ugonjwa,au upofu au,kwa namna yeyote wanavyoyaita,lakini ukitaka kujua tafsiri yake halisi Pengine,chukua muda wako kutazama kuku anavyoatamia mayai yake kwa siku 21,na kulinda kila kifaranga chake ,kwa kuvikumbatia,pengine jinsi anavyofukua chakula na kuwaruhusu vifaranga wadonoe kabla yake,Naam haya ndiyo Mapenzi.Mapenzi haya anapokuwa nayo mtu humuwazia mema ampendaye akitamani japo kila wakati wakae pamoja.

Kwa upande wa Sarah,japo kutakwa kimapenzi na wengi kati ya "kuruta" wenzake na maafande wao,na idadi isiyomithilika ya wanaume waliobahatika kumtia katika upeo wa macho yake yalikuwa,kwa kijana Nick.Aliulizwa na marafiki zake waliokuwa wakimhoji sababu ya kumng'ang'ania kijana huyu aliyetokea shule za kata,kijana huyu wa hadhi ya kimaskini.Lakini Sara hakuwa na majibu,Ndiyo,when you love you,just love,There is no reason needed for loving.Kwake kila dakika aliyopoteza na kijana huyu aliifurahia na kutamani japo angeweza kuyasimamisha majira ili kijana awe karibu naye.

Jeshini ndiko mahali pekee ambapo hakuna utengano wa kidini,kipato wala kikabila.Japo wanafunzi walitoka familia mbalimbali lakini walivyofika mahali hapa waligawiwa sare za kufanana,kula chakula kinachofanana na kufanya shughuli zinazofanana.Hali hii ilikuwa ikimfariji kijana Nick ambaye kila wakati alitamani kuwa afisa wa Jeshi.Japo alikuwa akitokea familia ya kawaida kabiisa,hakuwahi kuihisi tofauti hii.Siku zilienda hatimaye matokeo ya mitihani ya kidato cha sita yakatoka wote walifaulu,zikaja siku za kufanya applicaion ya vyuo mbalimbali.

Kwa kijana huyu na wanafunzi walio wengi leo hii,walikuwa maeneo ya Jaamatini,wengine Nyerere square kila mmoja akijitahidi kuomba chuo alichokitaka.Hawa wakiomba MUHAS kilichokuwa ndoto ya kila msomi wa PCB,hawa IFM na UDSM,Ilimradi kila mtu akiomba chuo chake.Kijana huyu,aliomba chuo cha Udom,Udsm,na mwisho chuo cha Kampala university.kwa binti huyu na baadhi ya vijana wengine walikuwa wanajiandaa kwa safari za kuelekea jijini Dar es Salaam,kwa ajili ya kuomba kusoma nje ya nchi,huyu Marekani,Mwingine India na China.walirudi kikosini shughuli zikaendelea wakati wa chakula cha jioni,kabla ya kufoleni kwa ajili ya roll call ya jioni binti huyu aliuvaa ujasiri na kumwambia kijana,"kesho naondoka kuelekea nyumbani,ninaenda kuomba chuo nchini Marekani kusomea Sheria,nitarudi wiki ijayo hapa kikosini,nikirudi salama kuna kitu ningependa kukwambia"

Upande wa kikosini maisha yaliendelea,sasa kijana huyu alikuwemo katika kikundi maalum cha kupiga kwata ya mwisho wa kufunga mafunzo yao,upande wa binti alifanikiwa kufika jijini DAR salama na kuomba maombi yake,wazazi wake walimtafutia chuo cha Yale university,kwa ajili ya shahada ya kwanza ya sheria.Baada ya wiki moja alirejea kikosini,na kuendelea na mafunzo na kuwa katika kikundi kisicho na kazi maalum maarufu kama KO Yaani kazi za ovyo ovyo,utawakuta muda huu wakifagia,baadaye watatakiwa kurukaruka wakiimba,ilimradi siku ziende.

Hatimaye siku za mafunzo ziliisha,gwaride la kufunga mafunzo hayo lililohudhuriwa na mmoj wa maafisa wakuu kabisa katika ajaeshi mwenye cheo cha Luteni jenerali,na akiwa mnadhimu mkuu wa Jeshi yaani Chief of staff ambaye alikuwa mgeni rasmi.Sherehe zilifana,bunduki kadhaa zilivunjwa,wageni mbalimbali walifurika wakiwemo wazazi wa Sara,upande wa kijana ,wazazi wake na familia yake haikuweza kuhudhuria sherehe hizo.Askari hawa waliopandishwa na kuwa cheo cha Servicemen and women walikula kiapo cha utiifu na kuaswa kuzishika sheria za nchi.Ilikuwa furaha kubwa kwa watu wote.

Sasa ilikuja siku ya kutengana kwa familia hii iliyokuwa pamoja kwa kipindi cha miezi mitatu,huyu akielekea kwao Tunduma,huyu kigamboni,yule Nyaishozi,huyu Utegi,hawa ikungi,wale Mbarali magari ya kwenda kila ukanda yalikuwepo kikosini vijana walitumia simu zao za mkononi kubadilishana namba za simu,ilikuwa ni huzuni kwa Nick,lakini huzuni zaidi kwa Sarah,alikuwa akitamani japo aungane na vijana waliokuwa wakielekea mwanza na siyo Dar alipotakiwa kwenda kwa mujibu wa taarifa za awali zilizoelezea makazi yake,Alimsogelea kijana Nick wakakumbatina kwa dakika chache huku akilia,kwa upande mwingine nyimbo mbalimbali maarufu kama "chenja" zilitawala hawa wakiimba Aidama,hawa Dunia duara na nyingine nyingi ,Nick akafungua ukimya kwa kumwambia Sarah,"nitakukumbuka sana ila kwa kuwa nina namba zako tutazidi kuwasiliana",Ndiyo Nick lakini naomba nikwambie kitu ambacho nimetamani kukwambia siku zote,"nakupenda Nick'naomba tuwe wapenzi na baadaye ikiwezekana tufunge ndoa,alilalama mrembo huyo.Nick akatoa jibu lililomhuzunisha mrembo huyu"

Jibu gani kalitoa Nick,tukutane sehemu ya tano
 
nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Messages
265
Likes
232
Points
60
nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2016
265 232 60
Ndugu wasomaji,nazidi kufarijika kwa usomaji wenu.Napenda pia kuwapa mawasiliano kwa ajili ya ushauri na mchango wa kimawazo na atakayejaliwa pia kiasi cha fedha kwa ajili ya kunisupport.Ikumbukwe kuwa hadithi hii itaendelea kutolewa hapa na sio mahala pengine popote,na kwamba mchango ni wa hiari kwa anayeguswa kuthamini kazi yangu.pia mnaweza kunipa maoni yenu juu ya hadithi hii kupitia namba hii Airtel 0785386036 Kwa watakaotuma pesa Pia namba hiyo itumike.
 
nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Messages
265
Likes
232
Points
60
nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2016
265 232 60
SEHEMU YA SITA
Sio kawaida ya wanawake wa kitanzania kusema wazi bila kificho,hata wanapoonyesha dhahiri kupenda kuwa na mwanaume fulani.Ndio utamaduni wetu,Naam katika utamaduni huu mwanamke anayemtamkia mwanaume waziwazi kuhusu habari za kimapenzi huchukuliwa kama au kahaba ama asiyefundishwa vizuri.Lakini binti Sarah aliuvaa ujasiri mkubwa na kumtamkia wazi kijana Nick pengine hii ilitokana na kukulia katika familia ya kitajiri na shule za kimataifa alizosoma kuanzia shule za awali mpaka kidato cha sita ambazo pamoja na mambo mengine zilichangia kumpa sifa ya kujiamini.Lakini kijana Nick alimjibu kwa kifupi

"Samahani Sarah,Nina Pendo wangu nampenda"

Japo binti huyu alijikaza na kuficha huzuni aliyokuwa nayo kijana Nick aliweza kuigundua huzuni hii aliyokuwa nayo,lakini hakutaka kumfarijibinti yule badala yake akafanya wanachokiita vijana wa sasa "kumpa makavu" wengi kati yamarafiki zake walimlaumu kwa uamuzi huu wa kikatili,Hivi unaanzaje kumkatalia mrembo kama yule ,hata mimi nisingeweza, lakini kijana aliamini kwenye mahusiano yake.Waliagana,safari zikaanza kila mmoja kwenda makwao kuashiria mwanzo wa maisha mapya.

Hatimaye muda wa kujiunga na vyuo ukaanza,kijana akachaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Kampala huku binti Sarah akimalizia taratibu za kuondoka nchini,kuanza maisha yake ya chuo nchini marekani.Sarah alimuomba kijana amsindikize uwanja wa ndege kijana huyu hakupenda kumuona binti huyu akiteseka,hivyo alihudhuria safari hii ambayo iliishia kumliza binti huyu alikuwa kama kafiwa akimuomba kijana abadilishe mawazo yake lakini kijana alishikilia msimamo wake.siku zikapita,miezi miaka hatimaye binti alirejea nchini akiwa mhitimu wa shahada ya sheria LLB.

Sarah aliendelea kunywa Champagne yake akipitia baadhi ya vifungu vya sheria kuona jinsi ya uwezekano wa kumsaidia kijana Nick.Kwa binti huyu Sheria aliipenda kutoka moyoni,alipenda kuwasaidia wanyonge wanaoteseka bila msaada wa kisheria akiweka mbele maslahi ya wateja wake,na wakati mwingine akijitolea bila malipo.Alikuwa akihisi uchovu sasa akaizima Laptop yake na akaamua kujipumzisha kitandani.

Akiwa kitandani aliota ndoto ya kusisimua,katika ndoto hii aliota akiwa kamshika kijana akijitahidi kumvuta kwa nguvu zote kutoka shimoni alimokuwemo mwanamke ambaye hakumtambua mara moja.Alijitahidi kuvuta huku jasho jingi likimtoka, akashtuka ghafla kutoka usingizini akihema kwa nguvu.Ilikuwa ndoto ya kusikitisha ,Alitamani ajue maana ya ndoto hii aliyoota muda mfupi uliopita.Aliangalia saa yake ilikuwa saa tisa za usiku hivyo akaamua kujipumzisha tena.

GEREZANI-UKONGA
Kila mara kijana huyu alipomfikiria Pendo alijilaumu kuwahi kuchukua maamuzi ya kuwa naye,alijilaumu sana na kutamani yote anayopitia kwa kipindi hiki yapite kama ndoto,lakinihayakuonekana japo kuwa na dalili za kuisha.Kuna wakati mtu hutamani kurejea nyuma na kuibadili historia yake,lakini hili haliwezekani.Hivyo kinachowezekana ni kuchukua maamuzi sahihi sasa kwa ajili ya manufaa ya siku zijazo.

Alimkumbuka Sarah,akatamani uje wakati ule,wakati wa binti huyu mrembo kulitaka penzi lake ambalo leo angekuwa tayari hata kumuoa bila maswali yoyote.Aliyakumbuka maisha ya furaha aliyoyapitia kule jeshini,akiwa na binti huyu SARAH,ama kweli hakuna aijuaye kesho alijisemea kijana huyu.

Pamoja na kwamba Pendo kwa sasa alikuwa akiishi na mwanaume mwingine,kijana huyu aliikumbuka sana tabia yake ya kubeza mipango yake.Kila alipomwambia kuhusu mipango ya baadaye ,Pendo aliichukulia kama baadhi ya vipengele kwenye filamu ya kusisimua na mafanikio yote aliyoyapata kijana yalikuwa ni kujitahidi kumthibitishia Pendo kwamba aliyoyaahidi yatakuwa.Lakini leo hii akiwa na kila kitu alichokiona kuwa ndoto kwake ,alikosa furaha,furaha ya kumhisi Pendo karibu yake.

Kuna wakati mtu hutakiwa kuyaruhusu yaliyopita yapite na kuitumia fursa hii kujipanga kwa mambo yajayo,hii itakupa ukomavu wa akili na utulivu ndani ya nafsi.katika maisha mtu mmoja akiondoka ,ni kwa sababu kuna mtu mwingine anatakiwa kuwasili hivyo badala ya kuwa na anayeondoka ni heri kujituliza na kujiandaa kwa ajaye.Kijana alimuomba Mungu amuepushie tuhuma hizi nzito za mauaji.

Usingizi haukuja tena kwa Sarah alikuwa akijigeuza kitandani,katika akili yake ailikuwa akiwaza mfadhaiko alioupata kijana alipomuuliza kuhusu Pendo.
"sijui Pendo atakuwa kapatwa na nini" alijisemea Sarah.
Aliangalia tena saa yake tayari kulikuwa kumepambazuka,hivyo akaanza kujiandaa na ratiba za siku mpya.Alioga,na kuvaa suti nyeusi ,alikuwa katika mwonekano safi kama watu wengi wa taaluma hii ya wanasheria.Alipanda gari lake nakuelekea ofisini kwake.Leo kama kawaida ya ofisi hii walikuwa na kazi nyingi sana.Alijadiliana na baadhi ya mawakili wake kuhusu kesi ya kijana huyu.Mwafaka ulifikiwa,kumtembelea tena gerezani wapate kujua namna ya kumsaidia.

KIGAMBONI

Leo hii katika nyumba moja ufukweni mwa bahari maeneo ya kigamboni ilikuwa ikifanyika sherehe ya kusherehekea ushindi.Vijana wa Eagles na binti Irene walijumuika na bosi wao katika sherehe hii,ilikuwa ni katika harakati za kupongezana na kuhakikisha kuwa hakuna kinachoharibika katika hatua za mwisho.

"Nimeipitia upya sheria ya uanzishwaji wa kampuni inayosimamia duka lenu ,inaonyesha kuwa endapo nafasi ya mkurugenzi itakuwa wazi kwa kipindi cha miezi zaidi ya 6,mtu aliyeikaimu nafasi hii atapewa mamlaka kamili ya kuwa mkurugenzi" alisema mzee yule akijiamini.

"Hivyo kuanzia wakati huu jihesabbu kama mkurugenzi kamili na una kila baraka yangu" Alimalizia mzee yule akimkazia macho Irene.mzee alimwambia kuhusu mipango ya kuitumia kampuni ile na duka lake la ushonaji kama biashara kivuli huku wakijikita zaidi katika kuimarisha mtandao wao wa madawa ya kulevya na utakatishaji wa fedha uliokuwa umeyumba sana.Vijana wa Eagle walipewa bahasha za khaki zilizobeba ndani yake kiasi kikubwa cha pesa,walijivunia kufanya kazi chini ya mzee huyu.


***************************************************************************************************************
Sasa Sara alipitia nyumbani kubadilisha mavazi na kupata japo kinywaji kabla ya kwenda ukonga kuonana na kijana yule.Alivalia gauni refu jekundu huku akizibana nywele zake ndefu nyeusi kwa nyuma,ama kweli alionekana mrembo sana.Alifika gerezani na kuonana na afande wa zamu aliyemueleza juu ya haja yake ya kuonana na mteja wake.Afande aliwaruhusu na kuwaacha mahali pa faragha kwa ajili ya mazungumzo ambayo yangeanza muda mfupi kutoka sasa.

"Sarah asante kwa unavyojitoa kwa ajili yangu,nashindwa hata jinsi ya kukushukuru" alisema kijana yule akiufungua ukurasa wa mazungumzo kati yao.
"Hapana ,usiseme hivyo tumekuwa pamoja katika magumu mengi hata katika hili tutapita"alijibu Sarah kwa upole
'Si unaukumbuka ule wimbo kule jeshini"?,aliuliza Sarah
"Upi" Alijibu kijana yule
"Aidama niimbie kama unaukumbuka"Alisema Sarah akitabasamu.

Aidama yoyoyo,aidama X2
Aidama yana mwisho jamani,Aidama
Aidama tuvumilie jamani,Aidama
Waliimba kwa furaha iliyowakumbusha mazoezi waliyopitia jeshini huku wakiimba kuwa yana mwisho wake,wimbo huu uliwafariji sana hasa walipokumbuka nyumbani kwao.Tabasamu la dhahiri lilichanua usoni mwao.

'Kuhusu ujio wangu hapa ninataka kufahamu zaidi juu ya kuhusika kwako kwenye mauaji ya Ben,tafadhali usinifiche kitu ili nijue jinsi ya kukusaidia"alisema Sarah ,Kijana alivuta pumzi ndefu na kuanza kumhadithia jinsi kifo cha Ben kilivyotokea.

Je kijana atashinda kesi hii nzito? ni nini kilichomuua Ben haswa? Tafadhali fuatilia sehemu ijayo
 
nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Messages
265
Likes
232
Points
60
nyandaad

nyandaad

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2016
265 232 60
Wakuu hakuna aliyesoma post yangu hapo juu,mnikumbuke kijana wenu japo 1000 kwa wasomaji wangu wakati natype napata pepsi baridi:):):) ....Tukumbukane jamani
 
Bengazuu

Bengazuu

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2013
Messages
974
Likes
1,133
Points
180
Bengazuu

Bengazuu

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2013
974 1,133 180
Shusha mzigo mkuu muamala soon
Wakuu hakuna aliyesoma post yangu hapo juu,mnikumbuke kijana wenu japo 1000 kwa wasomaji wangu wakati natype napata pepsi baridi:):):) ....Tukumbukane jamani
 
K

kisukari

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2010
Messages
4,076
Likes
1,510
Points
280
K

kisukari

JF-Expert Member
Joined Jul 16, 2010
4,076 1,510 280
Wakuu hakuna aliyesoma post yangu hapo juu,mnikumbuke kijana wenu japo 1000 kwa wasomaji wangu wakati natype napata pepsi baridi:):):) ....Tukumbukane jamani
Aisee nimekuonea huruma. Ila hiyo avatar badilisha wewe mtoto wa juzi unajizeesha. Mimi nitakusaidia nikija bongo baada ya wiki 2. I promise
 

Forum statistics

Threads 1,237,176
Members 475,465
Posts 29,280,321