RIWAYA; Mapambano

RIWAYA; Mapambano

SEHEMU YA KUMI NA MBILI
Kundi la Eagles sasa walizipandisha ngazi za jengo hili,kwa umakini mkubwa sasa walibadili mavazi yao wakiyavua yale ya askari wa zimamoto na kuvaa sare za walinzi walioonekana kulilinda jengo hili.Walizidi kusogea huku wakiziweka tayari silaha zao kuweza kuifanikisha operesheni hii muhimu.Vijana hawa walio imara mithili ya majabali ya Bismarck ya jijini mwanza waliukaribia mlango mkubwa uliokuwa mbele yao.E3 Take the rear entrance i'll lead the main force,alikoroma E2,ilikuwa kama kikosi cha special activities division katika operesheni GERANIMO, hapa waligawanyika E2 akajaribu kuufungua mlango,umefungwa.Ikabidi itumike C4 explosive.Patupu...

Wakaingia katika vyumba vilivyokuwemo katika jengo lile lakini hakuwemo mtu,wakapanda juu katika ghorofa la pili,wakati huu E2 na E3 wakaungana tena kuzidi kumtafuta mzee huyu tena akiwa hai,walivyoanza kupandisha ngazi za ghorofa la pili walianza kunyeshewa na mvua za risasi,kama walikuwa wamejiandaa walijiweka tayari kila mmoja akichupa na kujificha katika milango na samani zilizokuwemo katika jengo lile ni Eaglet mmoja aliyekuwa akivuja damu nyingi katika kiganja chake,wengine walijipanga wakitumia bullet proof za safeguard armour,E2 alisogea akijivuta kwa tumbo wataalam wanaita ku'claw' alijivuta na kukaribia upande ule zilipotokea risasi ama kweli kuna watu wana mioyo ya jiwe alituppia guruneti dogo la kurushwa kwa mkono paah mchezo ukawa umeisha,Eagles wakainuka na kuangalia uwepo wa mzee yule,walifungua vyumba vya karibu lakini hawakuona dalili za uwepo wake katika vita hakuna kurudi nyuma,walibakiza ghorofa moja kulimaliza jengo hili kabla hawajaskia sauti za ving'ora zikiashiria polisi waliokuwa wakija kwa fujo maeneo yale.

We have a situation,aliongea E1 aliyekuwa kwenye skrini kubwa akifuatliia tukio lile,aliwaagiza kutumia maarifa yao kujiokoa katika jengo lile .Walitumia kamba kushuka upande wa pili na tayari wakaungana na vijana waliokuwa wanashangilia mpira wa ndondo,kwa mwonekano sasa usingeweza hata kuwatilia shaka kama sio kuwashuku.

OYSTERBAY
Gari ilizidi kukaribia maeneo yale,iliingia kwa kasi katika geti la nyumba alilokuwemo irene,Mzee yule alishuka na kupandisha ngazi kwa pupa akiita Irene,Irene.....Hakuskia sauti kutokana na Irene kuwa amefungwa vitambaa akiwa uchi wa mnyama,alimuona irene akiwa pale chini,Wote walitia huruma alimfungua na kumkokota na kumuweka kitandani,next stop ilikuwa kwenye jokofu kubwa alilofungua na kumpa maji aliyochanganya na glucose Irene aliyabugia kwa haraka kama ambavyo utaziokota pesa zilizodondoka ghafla mbele yako.

Yalikuwa mapenzi mubashara kati ya hawa wawili mmoja akimuigizia mwenzake na mwingine pengine hajui alitendalo lakini kwa wakati huu tuwaite wapendanao,wakati huu ndipo utajua ukweli wa mtu.Japo watu wanaoyapinga mapenzi ya wapendanao huchukia lakini wengine wanakuwa na sababu za mashiko,wapendanao wanapaswa kuwapuuza lakini wasiyapuuze yale yanayotajwa,Kwaa upande wa Irene wote waliomtaja Briaan walionekana maadui kwake kila aliemsifia mzee huyu alionekana wa maana kwake.

Ndani ya muda huu mfupi walikuwa wamekumbatiana,huyu akilia na huyu pia asiwepo wa kumtuliza mwenzake,mzee akamwambia Irene ,jiandae tunaondoka,kuna watu wabaya wanatutafuta.Tukutane Ukonga baada ya saa moja ili tuweze kutoroka linakufata gari baada ya mimi kuondoka,Wakakumbatiana tena.

Usilolijua ni kama usiku wa giza wakati mazungumzo haya yakionekana ya siri E1,alikuwa akiyafatilia kwa umakini mkubwa huku akiwa kwenye gari lake aina ya Ford alilolichagua kwa safari hizi za jioni kuelekea eneo la tukio.Aliongeza mwendokasi wa gari lakemshale sasa ulisoma 130 akapunguza nakuiacha njia ya kuelekeamikocheni akapita ubalozi wa marekani kuitafuta Oysterbay,akafika mahali palipotarajiwa.Akafungua mlango wa gari lake akatembea taratibu kuelekea getini,alikuwa kavalia maridadi chelsea boot aina ya ORO ,jeans ya balmain na shati la kijani mpauko.Alipendeza na kuvutia.Akatoa funguo za maalumu kwaajili ya kufungua vitasa akafanikiwa kulifungua geti akaingia ndani na kubisha hodi mara tatu.Mlango ulifunguliwa na akatoka Irene akiwa na mkoba wake,alivalia suruali ya jeans nakikoti cha leather kwa haraka alionekana kama mtu anayejiandaa na safari.E1hakuongea neno lolote alimsaidia kubeba begi lingine dogo na kulipakia kwenye gari lake ,safari ikaanza.

Wakati huu alimtumia ujumbe E2 arudi kumsubiri kijana aliyetumwa kumfuata Irene,walikuwa wamejipanga kila idara,E1 alikuwa kashatimiza nusu ya lengo lao na sasa walikuwa wanajitahidi kumtumia kijana atakayetumwa kuwafikisha kwa mzee.

OFISINI TABATA
Hali ya kifedha sasa ilikuwa mbaya,kila mfanyakazi wa duka hili la ushonaji alikuwa akimlaumu Irene ambaye aliachiwa uongozi kwa muda,Alishindwa kabisa kumudu kuliendesha baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu wakautumia muda huu kufanya yaliyowapendeza,ndiyo tunatofautiana kiwango cha tamaa nainapofikia hatua fulani tamaa iliyo ndani ya mtu hujidhihirisha.Hali ilikuwa mbaya,wema walimkumbuka bosi wao.Walizikumbuka siku za shida walizopitia walikumbuka uongozi imara wa kijana Nickson aliyelifikisha duka hilo mahala lilipo.Ama kweli kukosekana kwa mtu mmoja kunaweza kuwa pengo.

KIJIJINI
Kijana Brian sasa aliyabadili maisha ya babu yake na kijiji chao kilianza kupata mwanga wa mafanikio.Alimsahau Irene na kuutumia muda mwingi kufanya shughuli zake kwa bidii.Watu husema ukitaka kufanikiwa fanya kazi kwa bidii lakini huwa hatujiulizi nifanyeje kuipata hiyo bidii ya kufanya kazi? Hapo ndipo utaijua nguvu ya upendo naam upendo,Upendo unaweza kuleta mafanikio? NDIYO-kuipenda kazi unayoifanya kutakufanya kuwa na bidii katika kazi na ubunifu utakaokuza kazi unayoifanya na hatimaye UTAFANIKIWA.Hiyo ndiyo siri ya mafanikio bilaa kuipenda kazi yake mwanasheria hawezi kukesha akipitia vifungu vya sheria,mfanya biashara hawezi kukesha akiwaza namna ya kutatua changamoto mpya,mwanamuziki hawezi kukesha akitunga na kuandika nyimbo mpya,mhasibu hawezi kukesha akifunga mahesabu Naam bila upendo haiwezekani.Swali lingine je wanaofanya kazi wote wanazipenda? jibu ni HAPANA,naadhani tutakubaliana kuwa wapo watu wanaolalamika kuhusu kazi zao kuhusu bidii inaonekana wanayo.jibu ni moja kwenye maisha FANYA UKIPENDACHO ukishindwa basi PENDA UNACHOKIFANYA nadhani ushajua wako kundi gani.

Kijana alizidi kukubalika kijijini pale,uzuri wakijijini hata wasomi wachache hivyo huwaheshimu na kuwapa thamani wanayostahili.Ushawahi kujiuliza ingekuwaje kama wasomi wote kila mmoja japo kidogo angefanya kitu kwa ajili ya jamii yake maendeleo yangekuwa dhahiri,hii ndiyo tofauti ya wasomi wa africa na Ulaya,wa ulaya wanasaidia ulaya na Waafrica pia wanasaidia ulaya ,Ndiyo nani ana uthubutu wa kurudi kwao na kuibadilisha jamii yake,au kutumia machache aliyojifunza kwa ajili ya jamii yake,utakuta mtu kamaliza Law school,halafu mtaa anapotoka mtu kakosa msaada wa kisheria anasota rumande na yupo hachukui hatua do we need him? Una CPA ndiyo je umewahi kuwasaidia wananchi wangapi kufill tax returns hapa ndipo utagundua shida sio elimu tuliyoipata shida ni tamaa ya pesa inayotuandama.

Kukaa kijijini kwa muda sasa kulimfanya Brian kuwa shujaa kwa sababu sasa alitambua nafasi yake,aliipa jamii kilichostahili aliiweza kuishawishi jamii yake juu ya umuhimu wa elimu.Wanakijiji walihamasika kila mmoja akimuona kama mwokozi aliyeletwa kwa ajili yao.

UKONGA
Gari la E1 sasa lilikata kona kuiacha barabara ya Pugu road na kupaki pembeni kidogo ya kanisa,walikuwa wakisubiri ujio wa mzee na E2 walilipaki gari vizuri huku macho yote yakiwa barabarani ,Je nini kitatokea next episode
 
SEHEMU YA KUMI NA TATU

Maisha yana changamoto nyingi,hivyo kila wakati binadamu huwa katika mapambano tatizo ni kwamba sio wote wanajua wapo kwenye mapambano na hata wanaojua hawajui muda upi wa kupambana.Wahenga wanasema mwenye hekima anajua muda upi wa kupambana au kukaa kimya.

Walikaa zaidi ya saa moja bila dalili zozote za gari kujitokeza ,wasiwasi ulianza kumuingia mrembo huyu.Alihisi uoga uliouondoa ukimya aliokuwa nao kwanzia mwanzo wa safari,alijikaza kisabuni na kumueleza E1 ,Alisema tumsubiri hapa sasa amechelewa?E1 alijibu kwa kichwa kushangazwa na kuchelewa kwa kiumbe huyu.Aliyemkosesha usingizi kwa siku kadhaa zilizopita.Kuna wakati unakisubiria kitu kwa hamu hadi inakuwa sababu yako ya kuishi,ndiyo tunaishi kwa sababu tuna sababu ya kufanya hivyo.Aliendelea kusubiri na mwisho E1 akatoa maelekezo ,nakuomba ushuke kwenye gari alisema E1 akiondoa lock ya mlango wa gari.Alimuelekeza kusimama nje kidogoya gari kisha akalipaki gari pembeni.

Hapa nusu saa nyingine ilikatika mwisho ikaonekana gari moja ikija taratibu na kupakiwa mahali aliposimama binti Irene,walishuka vijana wawili na kumsogelea ,Akawauliza yuko wapi Mzee,wakacheka kana kwamba wanamdhihaki kisha wakasema ameshaondoka muda mrefu,binti aliogopa,vijana sasa walitoa bastola zao kumnyooshea binti yule na kumuamuru aingie kwenye gari walilokuja nalo.

Kuna nafasi ya udhaifu kwa kila mtu,kwa E1 udhaifu wake ni kumuona mtu mnyonge tena asiye na silaha akinyooshewa bastola kana kwamba wanamteka gaidi maarufu,kwa ustadi mkubwa aliwanyunyizia mvua ya risasi bila kumgusa Irene.Akamsogelea na kumuambia waingie kwenye gari. E1 aliiweka miili ya vijana wale kwenye gari lao na kuliendesha hadi pembeni kidogo akatelekeza gari lile na kulimwagia mafuta ya petroli,kisha akapanda gari na kuendesha.

Aliendesha na kuifuata barabara iendayo kivukoni,aliwahi pantoni iliyokuwa ikivuka na kwenda upande wa kigamboni akiwa na mrembo Irene.Kuna wakati unatazama nyuma na kujuta kwanini ulichukua maamuzi kama hayo,wakati huu unakuwa ni majuto makubwa,Bahati mbaya ni kwamba unakuwa huwezi kurudi nyuma na kubadili kilichotokea.Irene alikuwa akijuta kumtelekeza Brian,alimkumbuka sana,aliukumbuka usaliti aliomfanyia,alikumbuka mpaka idadi ya siku alizolala na mzee yule, 23 ndiyo,baada ya kutumika kwa siku hizi amemtelekeza,tena akimtumia watu wa kumuua.

LONDON ,UK
Wakati Irene akilia na kujilaumu,mzee huyu alikuwa katika jumba kubwa alilokodi siku moja iliyopita,baada ya kufikisha document ile salama mikononi mwa mtu hatari kabisa,alipewa kiasi kikubwa cha pesa na kilichobaki kwake ilikuwa ni kufurahia maisha.Alikuwa na wanawake wanne kila mmoja akijibidiisha kumridhisha.Wote wamezivua nguo na kubaki kam walivyozaliwa,katika kitanda hiki cha king size bed.Ilikuwa tu miguno ya mzee huyu akifurahia maisha,kwa raha alizozipata alikuwa anaelekea kupagawa.Ama kweli pesa ni sabuni ya roho.Alishasahau hata habari za Tanzania,alikuwa akiwaza ahamie nchi gani nyingine kuendeleza starehe,Amandaaaaa.....
Aliita akaingia mrembo mwingine,akiwa na bikini huku kifuani hana chochote cha kuzuia chuchu zenye ustahimilivu wa kusimama,aliingia akiwa na tablet ndogo akauliza kama amepata location ya kula bata? BAHAMAS boss,alijibu Amanda huku akiutia ulimi wake masikioni kwa mzee yule.

KIGAMBONI, TANZANIA
Mbele ya jumba kubwa gari iliyowabeba Irene na E1 iliingia taratibu katika jumba hili la kisasa,baada ya kushuka kijana aliyekuwa mmoja wa Eaglets alimkaribia boss wake kupata maelekezo,akashangazwa na uwepo wa bini Irene,This is Irene,alimkatiza E1,Kisha akamwambia tell everyone to meet me in my study, alimaliza E1 akauchukua mkono wa Irene na kupandisha ngazi taratibu,walipanda mpaka ghorofa ya pili,kisha akamwonyesha Irene,chumba atakachopumzika.Irene alikuwa akilia tu.E1 akafungua mlango na kumwambia Irene,be free kama kuna kitu unahitaji piga simu hiyo mezani kitaletwa.Akatoka na kumpa nafasi Irene.

Katika chumba hiki cha chini kabisa ambacho Eagles hukiita Study,walikaa vijana wote alikosekana E2 na Eaglet mmoja ,E1 alipofika wote walisimama na kuinua mikono yao kutengeneza mfano wa mabawa,E1 Alijibu kwa kufanya vile,akaketi kisha wote wakaketi,kisha mara mlango wa geti ukafunguliwa akaingia Eaglet akiwa amebeba mkufu uliobeba kidani kilichoandikwa E2 ,Alilia na kupiga magoti, akakitupa chini na kusema,I betrayed the brotherhood ,I could not protect the Eagle,Machozi yalikuwa yakimtiririka na kuufunika uso wake.

Eagles,today we lost a brother,aliongea E1,Katika kipindi hiki hatupaswi kukurupuka,visasi vitalipwa kwa utaratibu mzuri.Na kuhusu Eaglet asante kwa kutuletea medani ya ndugu yetu afadhali,hatujawapoteza wote kwanzia sasa E3 unakaimu nafasi ya E2, Eagles,waliinua mikono tena na kukaa.Hivyo kwa sasa mwili uko wapi,Umehifadhiwa mochwari japo umeharibika vibaya sana,alijibu Eaglet yule,akiwa bado kapiga magoti,Tunatawanyika kila mtu aendelee kukusanya taarifa zitakazotusaidia.kikao kimefungwa alimaliza E1.

CHUMBANI
Irene alimaliza chupa tatu za Robertson wine zilizokuwa kwenye jokofu la mle chumbani,alikuwa mtupu,akiwa kalewa akilia pasipo kituo.E1 alimhurumia baada ya kumtazama akiwa Study,alipanda kule ghorofani na kufungua mlango,Irene alikuwa kaanguka akiwa kalewa chakari,E1 akatumia nguvu alizokuwa nao akamnyanyua Irene na kumpeleka kwenye Jacuzzi lililokuwa mle ndani,akafungulia na bomba la maji ya mvua kumuelekea,maji yale angalau yalimpa nguvu.Alianza kutapika,E1 akampa maji kidogo hakuweza hata kunyanyua glasi E1 akambeba tena baada ya kumkausha maji,na kumrudisha kitandani,kuna wakati unampinga shetani na kufanikiwa,E1 alifanikiwa muda huu bila kuwa na tamaa ya mapenzi japo aliona kila kiungo cha mrembo huyo.Alimuweka kitandani na kumfunika shuka kisha akamuacha apumzike,alirudi kule bafuni na kusafisha pale chini alipotapika,mrembo huyu.Alimaliza na kuubamiza mlango akaelekea chumbani kwake kupumzika.

E1 aliamka mapema na kufanya mazoezi,baada ya kumaliza akaoga na kuelekea jikoni hapa aliandaa uji mwepesi na kuiweka chupa katika meza iliyokuwa mle chumbani,Drink me aliiandika na kuiweka mezani.kisha akarudi chumbani kwake kuendelea na kazi zake.Irene aliamka akiwa mchovu hakuwa akikumbuka vizuri kilichotokea lakini alikumbuka kuwa alikunywa sana jana yake,hakukumbuka pia kama alilala na alishangaa kujikuta kafunikwa vizuri shuka.kwanza alijishika "kuhakiki usalama" alipotibitisha kuwa yuko sawa aliamka na kukuta kawekewa uji aliuweka kwenye kikombe na kuanza kunywa,akajifunga taulo lililokuwa pale kitandani alijisikia ahueni.Sasa E1 akapanda tena na muda huu alibisha hodi akiwa na sinia la matunda.

Habari mrembo,aliulza E1 akitabasamu
Salama alijibu Irene akiangalia chini,alikuwa akiona aibu,alianza kumpenda kaka huyu aliyeyaokoa maisha yake mara mbili sasa.

Je nini kitaendelea tukutane sehemu ya 14
 
Back
Top Bottom