SEHEMU YA TISA
Simu ya Sarah ilikuwa ikiita kwa sauti aliinua mkoba wake uliokuwa juu ya meza kuitoa simu yake,akaangalia kioo ili kuliona jina la mpigaji......
MSHANGAO-Sarah alibaki ameduwaa asijue la kufanya.
Ulikuwa ni mshangao uliochanganyika na furaha aliyokuwa nayo.Kuna jambo ambalo hutokea mtu asiamini limetokea vipi,kwa Sarah namba hii yenye code number +44 Ilikuwa na maana kubwa kwake.Alikuwa ni Sir Walters McAllison mmiliki wa kampuni maarufu ya bidhaa za kielektroniki kutoka Uingereza.Sarah alitamani na kuthubutu mara nyingi,kuwa mwanasheria wa kampuni hii lakini mara zote hakuweza kukubaliwa.Sio kwa sababu walikuwa na mashaka naye au taaluma yake ila kwa sababu ya ugumu wa mzee huyu wa cheocha Sir.Mzee Walters,alikuwa mgumu sana kuonana nae kama sio kupata namba zake za simu.
Mshangao huu ulimduwaza mpaka simu ikakata,Alikuwa akifikiria alivyotumia pesa zote alizolipwa katika kesi yake ya kwanza ili apate tiketi za ndege kujaribu kuonana na mzee Walters.Hakufanikiwa na akaamua kuomba walau namba yake ya simu,pia aligonga mwamba,alijaribu tena na tena hakufanikiwa.Hakukata tamaa aliamua kupanda ndege nyingine hadi nchini ufaransa katika jiji la Monaco kujaribu kupata mawasiliano ya mzee huyu,siku hii alimpata msaidizi wake aliyemkatisha tamaa.Alimwambia Simu ya mzee Walters ina namba tatu,moja ya mke wake,ya pili ya bintiye na yatatu ya waziri mkuu wa Uingereza.Hata yeye mlinzi mkuu wa mzee huyu hakuwa na namba zake za simu.Watu wote waliojaribu kumpigia mzee Walters ilikuwa lazima wapitie simu yake ya ofisini na kama kuna dharura yoyote ndipo huelekezwa kwa mzee Walters.
Mlinzi huyu alimuonea huruma Sarah akampa namba za binti yake ikawa bahati yake Sarah.Binti huyu wa Mzee Walters ndiye akaja kumpa namba za baba yake.Lakini akaambiwa habari zilizomkatisha tamaa zaidi.Mzee Walters hapigiwi simu akikuhitaji atakupigia.Hivyo leo ulikuwa mwaka wa nne na miezi tisa,na siku ishirini na saba baada ya tarehe ile jina la Sir Walters kwenye kioo chake alikaribia kuzimia kwa furaha kubwa aliyokuwa nayo.
Akaamua kuipokea,"Hello,Sarah",Sauti nzito ya mzee huyu ilimshtua .I am offering you an opportunity to be my legal representative in one of my cases,My personal secretary will call you for further information".Alimaliza na kukata simu yake bila ya Sarah kujibu,neno pekee alilolitamka ni "YES SIR".
STENDI YA MABASI -UBUNGO
Kijana Brian alilivuta begi lake dogo na kulipandisha katika Basi lililokuwa linaelekea mjini Bariadi,mkoani Simiyu.Huko angepanda lingine tayari kwa kwenda kijijini Ikungu yalipo makazi ya babu na bibi yake.Hakutaka kwenda nyumbani kwao jijini Mwanza ila aliamua kwenda kwa babu yake akiamini itakuwa ni sehemu salama ya kutuliza akili yake kwa kipindi hiki.
Maisha hutufunza mambo mengii,lakini mafunzo haya hutuachia maumivu makubwa.Ili kuyatumia mafunzo haya kufanikiwa tunatakiwa kubadilika,lakini mabadiliko huwa tunayapinga kwani yatabadilisha kila kitu tulichokizoea.Brian aliamua kuanza maisha upya ili ayasahau yaliyojitokeza huko nyuma.Safari iliendelea wakiivuka mikoa ya morogoro na Dodoma,Singida na Tabora,Shinyanga na Mwanza na hatimaye kama kila safari inavyofikia mwisho walifika mjini Bariadi.Alilazimika kulala pale na kusubiri hadi kesho yake ili kupata gari la kwenda kijijini kwa Babu yake.Alifika nyumbani kwa babu yake majira ya asubuhi na kupokelewa kwa shangwe na furaha.Mzee huyu alikuwa na busara nyingi,japo hakufanikiwa kwenda shule lakini alijua mambo mengi na alikuwa maarufu katika kijiji kile.
Baada ya salamu ,zikaanza mbio za hapa na pale kufukuza kitoweo rasmi cha mgeni wa kiafrika,Kuku.Sehemu nyingi za nchi yetu hasahasa maeneo ya vijijini mgeni hukaribishwa kwa kuchinjiwa kuku.Kijana alipewa majukumu hayo akiwasaidia Babu na bibi yake kumkamata.Japo lilikuwa saa la pili tu kwanzia afike mahali hapa aliiona furaha na amani ikiichukua nafasi ya huzuni aliyokuwa nayo.Hadithi za hapa na pale za mzee huyu machachari zilimsahaulisha hata maswahibu aliyokutana nayo.Jikoni nako bibi aliendelea na upishi,harufu nzuri iliwafikia wanaume wawili waliokuwa waki'yajenga'.Kwa kijana Brian ilikuwa ni zaidi ya siku kwake alitamani hata siku zote angekuwa na babu yake.
Watu huamini,au wamelazimishwa kuamini kuwa hela ndiyo kila kitu,hakunatena nafasi ya upendo,kuthaminiana imani,uaminifu.Hata makazini mtu akitumia matumizi inavyopaswa ataitwa anajipendekeza huku anayeiba akijiita anapiga 'dili' bila kujua kuwa bosi wake akifilisika atakosa kazi.Baadhi ya watu wachache wanatambua kuwa hela ipo kwa ajili ya kutimiza mahitaji yao lakini sio kila kitu.Babu yake aliyekuwa na miaka 75 sasa,alikuwa akionekana kama kijana wa miaka 40.Alikuwa mtu mwenye furaha wakati wake,nyumba yake iliyotengenezwa kwa miti imara,kitanda cha wastani ,zizi lenye ng'ombe wengi kiasi,akiishi na mjukuu wake mmoja tu hapa kijijini.Alikuwa na amani na kila mtu akiwa pia kiongozi wa kijiji hiki kwa miaka 15 sasa akipita mara zote bila kupingwa,alikuwa mtu wa watu.
Ukafika wakati wa jioni,kijana alimsaidia babu yake kuwasha moto kwa kutumia kinyesi cha ng'ombe,na baada ya chakula walipiga stori wakiota moto huu.Mzee huyu alimuuliza kijana swali fikirishi,"unajiona wapi katika miaka ijayo"?.Swali hili lililenga kupima ufahamu wa kijana wake.Kijana Brian,hakujua ajibu nini,Japo alikuwa muhitimu wa shahada ya masomo ya Biashara lakini hakujua atakuwa nani miaka ijayo,kwanini?.Kwa sababu hakuwa na uhakika ataajiriwa kama nani kwake yeye aliwaza ije siku apate ajira na hivyo alimjibu mzee yule sijui Babu,Sijui hata nifanye nini.
Babu alijiweka vizuri kwenye kiti na kumtazama kijana Brian,kisha akamwambia."Wakoloni walivyokuja ,walitukuta tukiwa na mfumo wetu wa maisha,waliingiza elimu yao na kuitumia kujinufaisha".Wakati huo watu walilima mazao ya chakula yaliyotosheleza mahitaji yao,walikuwa na elimu iliyosaidia kutatua matatizo yao,Mfano kijana wa kiume alifundishwa ujenzi wa nyumba ya kuishi.Au uhunzi wa kutengeneza,silaha na zana za kutumia katika shughuli mbalimbali.Hivyo,elimu kama haijatumika kusaidia matatizo ya jamii haina maana yoyote.Maneno ya mzee huyu wa miaka 75 yalimuingia barabara kijana Brian.Alizidi kumpenda mzee yule hata akathubutu kumfananisha na gwiji la sayansi Albert Einstein aliyewahi kusema "Kama huwezi kumueleza mtoto wa miaka sita akakuelewa basi hujui hicho unachokieleza".Japo mzee huyu hakusoma lakini aliweza kuiona hekima yake.Aliyahifadhi maneno ya mzee yule.
COLLOSEUM HOTEL
Leo Irene alikuwa na mzee wake,aliyempa "all of her" usiku wa jana,mahali hapa alikuwa akipata chakula cha mchana.Alikuwa amechangamka kwa mara ya kwanza maishani mwake akifanikiwa kunywa glass nzima ya Smirnoff X1.Alikuwa kavalia kaptula fupi na blouse iliyoonyesha sehemu kubwa ya kifua chake.Alionekana kupendeza sana.Wanawake wamejaaliwa upendo,lakini baadh yao hawajui hata mtu wa kupenda,kuna hulka ya watu kuona kilicho mbali kama chenye thamani zaidi kuliko ulichonacho ndiyo iliyomsumbua Irene,akiona Brian hakuwa na maaana yoyote kwake.Kwake yeye muda huu mzee huyu alikuwa ameiteka na kuiweka kusikojulikana akili ya binti huyu mrembo.
Baada ya chakula waliingia katika gari la mzee yule tayari kwa kurejea nyumbani kwa mzee yule maeneo ya Oysterbay.Gari hii ya Volkswagen Amarok,liliwafikisha katika geti kubwa nje ya jengo la ghorofa mbili yalipokuwa makazi ya mzee huyu.Kijana wa kazi alifika na kufungua geti lile,kuipisha gari hii kuingia.Mzee yule alilipaki gari likiungana na mengine matatu na kufikisha idadi ya magari manne yaliyokuwa ndani ya jumba hili kubwa.Walishuka kwenye gari wakiwa wamekumbatiana,japo ungewaangalia walivyotofautiana umri ungefikiri mzee huyu alikuwa na binti yake akimkaribisha kutoka masomoni,lakini alikuwa ni mpenzi wake.Labda tuite mmoja kati ya wapenzi wengi wa mzee huyu.
Walipandisha juu na kuelekea moja kwa moja chumbani kwao,Walivuana nguo kwa kasi ,huku wakitoa miguno ya kimahaba,Sasa mzee huyu alinyanyua mguu wa binti huyu na kuushikilia kwa mguu mmoja.kihisabati tungesema mguu huu ungekuwa umetengeneza angle ya 90 "to the horizontal' mzee huyu aliuvuta mmoja wa miguu yake usiovalishwa viatu kuisherehekea sherehe hii ya dharura.Lakini kabla ya kufanya chochote" mikono juu" ilisikika sauti nzito ya mamlaka ikiamrisha mzee yule.
"E1 nimekukosea nini" alisema mzee yule akitetemeka
"paaaaaaaaaah" Risasi moja kutoka bunduki hii ya kivita hii aina ya Daniel defense AR 15 Semi automatic ilikita katika paja la mzee yule.
Damu zilichuruzika na kukichafua chumba kile,binti Irene sasa alikuwa ameshafanya mojawapo ya sifa za viumbe haiyaani excretion,akitoa mkojo,macho yake yalitoa machozi alikuwa akilia sana.
Nini kimesababisha E1 Kuasi,je nini kitatokea? Nani unampenda katika hadithi hii usiache kucomment.