Riwaya: Kombora kiotani-1

KOMBORA KIOTANI-23

BONIFACE BIRAGE

Rais Kilua akiwa kwenye ofisi yake anaingia mtu.Alienda moja kwa moja hadi alipoketi kwa heshma zote.Kilua aliinua macho nakumsikiliza kwa makini bwana huyu.

“Madam kuhusu kufanyiwa ushushushu kwa bwana Serambovu kwa mawasiliano yake.”alisema wakala huyo kwa umakini.Kilua alimwangalia huku akipitisha ulimi kwenye papi za midomo yake kwa haiba ya kike.Urembo wake ulikuwa umesimama dede na kila aliyemuona alihisi wivu kwa mwanaume aliyemuoa nakuona kama ananyimwa wasaa wa kufurahi na bibi huyu mwenye wajihi kama hurulaini.

“Mmegundua nini?”aliuliza Kilua.

“Jukumu hili nilipewa na bosi wangu bwana Masha.Na katika kupitiapitia nilIpata simu nyingi tu alizokuwa anapata bwana Serambovu kila mara nilijitahidi kuwa makini.Nanilichukulia kila mawasiliano kuwa ni makini sana nakuyapatiliza.Ila kuna simu moja ilinitatiza sana.Hii ilitoka hivi karibuni.Hii ilikuwa na mazungumzo yanayohusu kukamatwa kwa mwanausalama wa KISS.Simu hii iliuliza kwamba kama kuna oda yoyote kutoka ikulu kuhusu kufanyiwa ushushushu kwa meli ya mizigo iliyopo bandarini.Nilijaribu kufuatilia mazungumzo na hasa meli hiyo kwanini ifuatiliwe na kama kweli ilikuwa inafuatiliwa kwanini mfanyakazi wa ikulu atoe siri kwa wanaofuatiliwa?Nilichojua kupitia njia zangu meli hiyo inahusika kukamatwa kwa wanausalama waliokuwa katika operesheni zao.Idara ya usalama hadi sasa haijafanikiwa kuwaokoa watu wake.Hivi ni kwamba meli hiyo kama ina jeuri ya kuwaweka vizuizini watu wa usalama halafu hapohapo isifuatiliwe na bado kuna mtu kutoka ikulu anaongea nao inaonesha kuna mazito kuhusu uhusiano wa meli hii na Serambovu.”

Kilua alitumbua macho.Palepale alichukua simu nakumpigia Bwana Toti,”Halo bwana Toti?”

“Ndiyo mheshimiwa.”

“Kuna agent wako anaitwa Shuni?”

“Ndiyo na ndiye aliyekamatwa kwenye meli ile tulioishuku kuhusu madawa ya kulevya na hadi sasa bado hatujam-recover”

“Dame it!Nimeisha jua aliyemkamata ni nani?Njoo ofisini kwangu.”alisema rais Kilua kwa kujiamini bila kupepesa macho.

Alikata simu nakumuangalia kijana aliyepembeni yake,”Ulifanya kazi nzuri sana unastahili pongezi sana kijana wangu.’’

Kijana alishukuru kwa pongezi hizo.Zilikuwa pongezi za kuridhisha kutoka kwa mkuu wa nchi.Kilua alitilia shaka sana kuhusu Serambovu kuwa na mawasiliano na meli iliyohusika kuwaweka vizuizini watu wa idara ya usalama.Hilo lilikuwa kosa kubwa sana kuhusika kwake.Kilua alionganisha matukio kadhaa pamoja na lile la kupigiwa simu kwa yule mtu anayetaka file namba 13:14.Pia alikumbuka alizungumza naye na akaambiwa kuna wakala wa usalama amekamatwa na huyo wakala anaitwa Shuni!Aliongea na wakala huyo nakumthibitishia kwamba yupo mikononi mwao akiwa kwenye operesheni zao akatekwa na adui.Adui mwenyewe naye anahushwa na utekaji wa familia yake.Ina maana ni kweli Serambovu alijua watu hawa walimteka mwanaye?Anakumbuka siku fulani akiongea na Serambovu alimtajia kuhusu kutekwa kwa familia yake.Ni kweli Serambovu anajua.Ila alijuaje?Kilua hakuwa amemwambia na kwasababu hiyo aliweka ushushushu wa kuchunguzwa kwa Serambovu hadi sasa anapogundua wanaounganishwa na utekaji wa familia yake.Waliokuwa kwenye meli na yule anayempigia simu za vitisho kuhusu kuteka familia yake wanaushirikiano au kwa lugha nyepesi ni timu moja!Kama waliweza kuongea na chifu wake wa ushauri bila shaka walijua vyema nyendo zake.Hata walipomwambia wanajua hata akitema mate wanajua basi mvujishaji wa habari ni Serambovu!Kilua aliuma meno kwa hasira sana.Tena huyu mshenzi aliongea na watu hao wakiwa kitandani kwake!Kampa kila kitu na penzi lake lakini bado kafikia hatua ya kumsaliti?

Baada ya muda mfupi Toti na Masha waliwasili ikulu nakueleza walichogundua kuhusu faili nambari 13:14.Walimueleza yote waliyoyapata kutoka kwa bwana Pasha.Kilua aliwasikiliza kwa umakini nakuanza kupata picha kuwa ikulu iliingiliwa na sasa imengiliwa zaidi!

***

“Gentlemen kama mlivyoniambia basi na mimi nimegundua moja ya staff wangu alikuwa ana mazungumzo ya siri na kaptein wa meli hiyo na kwa mujibu wa ripoti niliyopata nikuwa kapteni wa meli anaitwa Mr Zungu.”

“Mheshimiwa pia kulingana na uchunguzi wa awali Shuni alikuwa akimpeleleza mtu anaitwa bwana Tufe huyu alikuwa na data zot kuhusu meli hiyo.”alisema bwana Toti.

“Kama huyo Tufe anahusika na meli basi anajua vyema alipo binti yangu na mume wangu!Namtaka huyo mtu atiwe nguvuni haraka sana.Alipo Shuni na familia yangu ipo.”

Kilua alikwisha waeleza watu hawa jinsi familia yake ilivyotekwa na watu na hadi Shuni kutekwa na ikatokea sadfa kwamba wote wamekutana sehemu moja!Hilo lilitosha kuwapa muelekeo kwamba adui alianza kuonekana ni nani.Kilua hakupenda kumuuza Serambovu kwa haraka kwa namna ile alitaka kumshtukiza.

“Na huyu stafu wako anatakiwa akamatwe.”alishauri Masha ambaye alionekana hampendi Serambovu hata kidogo.”
“Huyu tumuweke kwenye uangalizi wa hali ya juu.Tutamtumia kama chambo kuwapata hao wengine.Nikimshtukiza sasahivi itakuwa hasara kwetu.Huyu nitamshughulikia mwenyewe!”alisema Kilua hali iliyofanya Masha kuwaza mara mbilimbili kama ni kweli Serambovu na Kilua walikuwa na uhusiano wa mapenzi au la!Maana pozi la Kilua lilikuwa kama kuna uaminifu mkubwa kati yake na Serambovu hivyo kuwa na imani kwamba kwa uaminifu huo Serambovu atakiri kuhusika na wabaya wake.Hilo halikutosha kumpa lile jibu la swali gumu!

“Inatakiwa tuwe makini.Tukiweza kudhibiti watu hawa tutajua nani alilipua serikali nzima!”

“Kesho ni siku ya mazishi kwa mashujaa wetu waliofia kwenye ile ajali natumai iende vizuri.Kuna ujio wa wageni wengi kutoka nchi za nje.Naomba muweke vijana wenu ulinzi uwe wakutosha.”

Kilua aliinuka kuashiria kikao kimeisha.Kisha alienda moja kwa moja kwenye chumba cha mikutano.Humu kulikuwa na kamati ya ulinzi iliyokuwa inamsubiri kwa hamu kwa siku ile aseme nao.Waliketi walipomuona.Rais wao kafika.Kilua mwanzoni alikuwa amepitisha utaratibu wake wa ulinzi ambao ungetumika kwa siku ile.Kilichomleta pale ni kuhakikisha tu kwamba utaratibu alioupitisha upo sawa.Tofauti na mategemeo akakuta utaratibu umebadilishwa.

“Nani aliyebadili utaratibu huu?”

“Ni Serambovu pamoja na jenerali Lupogo.”alisema moja ya wajumbe wa kamati ya ulinzi.Jambo hilo lilimkera Kilua nakuona kama anaingiliwa kwenye maamuzi yake.Huo ulikuwa utaratibu ambao kuna maeneo uliacha mwanya na kama kuna mtu angetumia mwanya huo bila shaka angeingilia mzingo wa usalama jambo ambalo Kilua hakuwa tayari kulishuhudia hata kwa dawa.Mchoro mpya uliopitishwa na Serambovu na jenerali Lupogo haukumshibisha Kilua.Na aliupinga toka mwanzo lakini hawa wamepindua uamuzi wake nakumfanya aonekane kituko.Hicho kilimpeleka mbali ikiwa kweli Serambovu ndo anayemwendesha au kuna laziada linalotokea.Kilua alihisi mambo siyo sawa na hisia zake zikazidi kuwa za mashaka hasa jamaa alivyozidi kukumbwa na sakata la kuhisiwa vibaya.Yote haya yalimuweka Kilua katika wakati mgumu dhidi ya watendaji wake wawili muhimu sana.Jenerali Lupogo!

“Kwanini walibadili utaratibu?”

“Walipitia itifaki upya na kujiridhisha kwamba mchoro huu wa kiusalama ungekuwa mzuri zaidi kuliko ule tulioupitisha mwanzo na Serambovu alisema atazungumza na wewe kuhusu jambo hili.”alitaarifiwa.Kilua hakutaka kuonesha mashaka yake dhidi ya jambo hilo nakuona kweli kuna watu hawajajua sauti yake ni nini?

Kilua aliondoka katika kikao kile bila kumsemesha mtu.Alirudi hadi eneo jingine la ikulu.Kisha aliongea na walinzi wake kwamba anataka kudhuru eneo ambalo shughuli ya msiba wa kitaifa utafanyika.Hapo marehemu watapewa heshma zao za mwisho.Kulizuka mabishano kwamba asiende pale maana bado hawajafanya uhakiki wa barabara kwa rais kupita.Lakini alifanikiwa kuwashawishi walinzi wake.Ndani ya muda mfupi tofauti na utaratibu msafara wa rais uliandaliwa kwa yeye kwenda eneo lile.Kilua aliondoka na walinzi kadhaa.Magari yalianza mwendo huku Kilua akiwa amekasirika moyoni kwa jinsi Serambovu alivyomtenda!

Alijua akifika eneo hilo atamkuta jenerali Lupogo.Ving’ora vya msafara vilizidi kusambaa hivyo kuyafanya magari mengine kupisha njia.Kilua alikuwa anafikiria mambo sana ikiwemo hisia kali alizopata dhidi ya bintiye kwamba kuna mtu alitishia kumtenda unyama na toka wakati ule hadi sasa bado roho ya yake imekosa imani kama kweli mwanaye ana usalama huko alipo au kuna sintofahamu zinaendelea kati yao!

Baada ya dakika chache alikuwa amefika eneo lile.Kulizuka mshtuko mkubwa sana baada ya watu kugundua ujio wake rais Kilua ambao hakuna aliyemtegemea.Wengi walijua wangemuona siku ijayo atakuja akiwa na msafara wake kuwaongoza wananchi na wageni katika kutoa heshma za mwisho kwa mashujaa wa taifa walioaga dunia.Tofauti na vile Kilua ametokea eneo la tukio kwa kushtukiza sana!

Jenerali Lupogo alishtuliwa na ujio huo sana.Ilibidi awe wa kwanza kwenda kumlaki mkuu wake wa kazi.Kilua alijikuwa mpole.Aliwapa moyo wote waliokuwa wanafanyakazi kuandaa uwanja ule kwa shughuli ile maalum.Baada ya hapo aliomba kuongea na jenerali wake.

“Mheshimiwa nakushukuru sana kwa ujio wako hapa.Na…”jenerali alikatishwa na Kilua.

“Jenerali nafikiri tuna sahau mipaka yetu ya kazi?”Kilua alianza kwa jazba.Hilo halikutegemewa

“Kwanini mheshimiwa?”

“Inakuwaje mnabadili protokali niliyopitisha nakuweka mchoro wenu?”Kilua akawa mkali.

“Mheshimiwa unajua…n…”

“Jeneral nadhani hujui ni nani mwenye mamlaka?Sasa nasema hivi nakusimamisha kazi na kwaanzia hadi pale nitakapoamua vinginevyo.Agents mkamateni.”

“Ngoja hawa hawana mamlaka yakunikamata?”jenerali Lupogo alijitetea huku akibabaika.Lilikuwa jambo baya sana kwa mkuu wa nchi kukusimamisha kazi halafu anakuweka kizuizini!

ITAENDELEA WIKI IJAYO
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 68
KOMBORA KIOTANI-24

BONIFACE BIRAGE

Kilua akasogea hatua chache nakumshika jenerali,”Am the commander in chief therefore am overiding your duties from now on you are under arrest!”Kilua alisema kwa ujasiri huku walinzi wake wakiwa makini na silaha zao maana anayekamatwa ni mkuu wa majeshi!Lilikuwa tukio la ghafla hakuna aliyetegemea litokee.Eneo lile lilichemka na hali kuwa tete.Rais anamweka chini ya ulinzi mkuu wa majeshi!

“What are my charges?”jenerali Lupogo alikuwa mkali kidogo!

“Am detaining you till further notice general so don’t question my orders!Or do you want me to charge you for treason?You defied my orders general and that gives me enough doubt if you are capable of handling your duties?”Kilua alikuwa mkali.

Walinzi wakamshika jenerali.

“Nipe silaha yako.”alisema Kilua.Jenerali alisimama wima akijua fika lolote atakalo sema au kutenda halafu lionekane ni kero mbele ya uso wa rais Kilua bila shaka angekuwa mashakani!Alisimama kwa nidhamu ya kijeshi kisha alitoa silaha yake akamkabidhi Kilua.

“Jeneral kuwa makini na mimi!”alipiga mkwara Kilua.Kisha aliichukua silaha.

“Nitauacha mchoro uliopitisha kwa sasa.Lakini chochote kikienda kombo tutaongea vizuri.”alisema Kilua kisha akaondoka lile.Jenerali Lupogo aliondoka na walinzi wa Kilua.Kuna walioona tukio lile wakastaajabu huku minong’ono ikianza kupita huku na kule kufuatia uamuzi huo.Kesho kulikuwa na ujio wa ugeni mkubwa sana kiasi haikutakiwa itokee makosa yoyote ya kiusalama.Kumsimamisha kazi jenerali sio jambo la kawaida kabisa hasa ukizingatia kuna shughuli kubwa ya kitaifa inaenda kujiri siku inayofuata.Uamuzi wa Kilua ulimtisha hata jenerali mwenyewe kuona kwamba mwanamke huyu hana utani na kama walidhani wangempelekesha wanavyotaka basi wamenoa pakubwa sana!Kilua alikuwa anawashtukiza kwa hatua hiyo siyo na utani.

Kilua akampigia simu bwana Toti na Masha aliwapa maelekezo mazito.Mchezo ulikuwa umebadilika!

***

Kikosi maalum cha usalama kiliwasili nyumbani kwa kapten Pangabutu.Ujio huu ulikuwa wa ghafla kiasi wale waliokuwa wanaweka ulinzi wa kizuizi wakashtushwa maana hakuna ujio kama huo uliokuwa unategemewa hata taarifa haikutolewa.Walipotaka kuhoji walipewa vibali maalum kutoka ikulu kwamba wana amri ya kuingia eneo lile.Walifanikiwa kuingia hadi ndani nakuanza kufanya upekuzi wanyumba hiyo.Tofauti na vile walivyodhani kwamba bwana Pangabutu ni marehemu na wangekuta kuna hali ya msiba akiwemo mkewe.Kulikuwa hakuna dalili ya msiba wala ya watu kujikusanya.Walimkuta Pangabutu akiwa sebuleni kwake na mkewe!

“Pangabutu?”aliita Pablo!

Pangabutu alisimama kwa mshtuko.Ujio ule ulimpa ishara kichwani!

“Kuna nini?”

“Tunakuhitaji.”

“Basi naenda na mke wangu.”alisema kapten Pangabutu akitetemeka!Walimchukua pamoja na mkewe.Uwepo wa magari ya usalama eneo lile uliianza kutengeneza picha nzito ya kushuku eneo lile.Waliwachukua pamoja na walinzi waliokuwa pale wakawekwa chini ya ulinzi kwa pamoja!

“Tunaenda wapi?”aliuliza kwa wasiwasi moyo ukimwenda mbio.Akili ilizunguka huku na kule.Kulingana na mazingira ya kazi yake na jinsi alivyoishi kwa miaka yote hii alijua fika hajajiwa kwa amani.Kuna shari imejificha!Shari inayomtafuta kwa udi na ambani!

“Tuna oda maalum kutoka kwa rais Kilua.”alisema Pablo akiwa kama kiongozi wa operesheni ile pamoja na msemaji wa kila hatua.

Msafara huo uliendelea kwenda kwa kasi.Njia nzima Pablo alikuwa anataka kitendawili hiki kitatuliwe iliaweze kumpata mchumba wake.Alijua mzunguko wote huu mwisho wa siku Shuni yumo mikononi mwa watu hawa.Wote wameunganishwa na matukio ya ajabu ajabu.Familia ya mkuu kutekwa imeshaingia kwenye dimbwi zito la hofu na mashaka makubwa.

Kazi ilikuwa kazi kweli na imeshawafikisha kwenye mzingo mgumu sana.Wakiwa njiani ghafla mlio wa risasi ulisikika kasha ikafuatia risasi kadhaa kupasua kioo upande alimo keti dereva!Pablo gusa gia Fulani kwenye kiti kwa haraka nakukifanya kilale nay eye akalala chali.Akampa ishara Pangabutu ambaye naye alilala upande huohuo.Lakini alichelewa risasi ilipenya kwenye nakumfyetua mguu mmoja.Kisha zikafuatilia nyingine ambazo zilipiga kwenye mkono!Jamaa walikuwa wanamimina!

Mke wa Pangabutu alizimia!Risasi zikaendelea kumiminwa.Kwa haraka Pablo alichomoa bastola yake na kuanza kutafuta shabaha!Milio ikaanza kujibishana!

Taa!Taaa!Taaa!Milio yaa risasi ilishtua eneo lile huku raia wakikimbia.Mapigano yakawa rasmi baina ya watu wasiojulikana na Pablo na kundi lake.Kwa ujuzi wa hali ya juu kikosi cha Pablo kilianza kujibu!Barabara ilichafuka!Wakati Pablo anatafuta namna ya kulisimamisha gari risasi ilipigwa kwenye matairi kulifanya gari kupoteza mwelekeo!Alikamata breki na kusababisha matairi yalipoteza pumzi na kuacha vyuma visugue lami huku mlio mkali ukisikika!Gari lilienda kando nakujipigiza kwenye mti!Pablo alijigonga kichwa kwa mbele hali iliyofanya apate jeraha la haraka nakuanza kuvuja damu!

Pablo alipatwa na maumivu makali lakini alijikaza.Wakati anaanza kujiandaa kujibu mashambulizi alishtukia wale waliowashambulia wakielekea upande wao kwa kasi ya ajabu.Walisimamisha gari nakuwafuata!

Pablo alijikazaa nakuvuta nguvu zote alizokuwa nazo mithili ya Samson alivyobomoa hekalu!Alielekeza silaha yake upande huo nakuanza kuwa fyetulia wavamizi hao!Kwa haraka alifanikiwa kuwalenga wane!Wawili kati yao aliwaondoa uhai palepale!Ghafla kwa kutarajia Pablo alipigwa risasi ya bega nakumfanya ahangaike kwa pupa!Mwili ukatepetevuka!Damu ikaanza kuvuja bega upande wa kushoto!Walipofika karibu walimlenga kwa risasi Pangabutu tumboni!Gari lilikuwa libondeka kwa mbele kwa kule kujipigiza kwenye mti!

Hatari ilikuwa imewadia!Kisha walimshambulia na mke wa Pangabutu kwa risasi za kutosha.

“Wamekufa wote!”alisema moja ya watu wale!Wakageuka nakuchukua maiti za wenzao kisha wakarudi kwenye gari lao.Ile wanataka kuliwasha,Pablo alizinduka nakulenga shabaha usawa wa tanki la mafuta na kufyetua risasi kadhaa!Haikuchukua muda mlipuko mzito ukajiri!BUUM!

Waliomo kwenye gari walikuwa wanateketea!Pablo akajikokota nakuchukua simu yake akapiga kwa bosi!

“Pablo uko wapi?”

“Tupo Kisusi Road…tumevamiwa na watu wasiojuliikana.Naomba msaada wa matibabu!”alizungumza kwa taabu sana!Toti kule alipoalianza kuita timu ya matibabu pamoja na sekta nyingine kuzitaarifu kwamba vijana wao wamevamiwa!Ndani ya muda mfupi gari la matibabu pamoja na vikosi vya usalama vilikuwa njiani kuelekea eneo hilo.

Ving’ora vilisambaa barabarani.Dharula ilikuwa imejiri kwa wakati ule.Ilichukua muda mfupi sana kwa timu ya usalama pamoja na polisi kufika pale.Pablo alitolewa kwenye gari pamoja wenzake.Ni Pablo pamoja na Pangabutu na mkewe Pangabutu waliojeruhiwa kwa risasi.Hao wengine walikoswakoswa!

Pablo alikuwa amepigwa risasi kwenye bega!Pangabutu yeye alikuwa amejeruhiwa kwenye tumbo mguuni na mkono upande mmoja!Mkewe alikwisha fariki kwa kupigwa risasi shingoni!Madaktari walifanya kazi kwa haraka ilikuweza kuokoa maisha ya watu hawa!Ilitakiwa wajipange kwa haraka lasivyo mambo yangekuwa mabaya zaidi ya vile yalivyokuwa.Kwa waliojua mfumo mzima wa operesheni ile walikuwa na mashaka makubwa!Muda mchache tu baada ya Pangabutu kutolewa kizuizini walikuwa wamevamiwa na watu wasiojulikana!Iliwapa ishara kwamba uwepo wake mikononi mwa watu wengine ni ishara tosha kuwa jamaa huyo ni tishio kubwa kwao na kwa usalama wao hivyo ni bora kumvamia nakumfutilia mbali sana!

Kwanini Pangabutu awindwe kiasi kile?Kuna kipi anachojua?Kuna siri gani kiasi anakuwa mikononi mwa mauti.Uhai wake umekuwa kama yai mkononi kwa mtu mwenye njaa!Muda wowote anaweza futwa au alelewe hadi awe kifaranga lakini bado tu ataliwa kama kuku!Mwendo ukawa na utata!Idara ilikuwa imesimama nakutatizwa.Imekuwaje ikajulikana kwa haraka kwamba Pangabutu kafunguliwa?Pia ilikuwaje ikaamuliwa usalama waende kumchukua?Uamuzi wa kujakumchukua kwa uwazi kwa namna ile kumeleta uvamizi.Na hata wangemchukua kwa namna ya siri bado siri ingevuja.Idara ya KISS ilikuwa ya siri sana na kila hatua yake ilipochukuliwa ilikuwa ya kuaminika lakini inapotokea kwamba usiri huu hauna imani kwamba utasimama basi shaka ipo.Toti alitamani idara hii ifumuliwe upya kabisa!Maana inaongozwa kwa kila hatua inayochukuliwa na kutikisa utendaji wao!

Jambo lakuvamiwa sio dogo!Hadi sasa uhai wa bwana Pangabutu unapumulia gesi!Mkewe kaondolewa na yeye ameshambuliwa kwa minajili ya kumfutilia mbali kabisa!

Jambo limezua jambo! Muda utaongea!

***

Serambovu akiwa amekasirika alisimama akimhoji Kilua kwanini amemsimamisha kazi jenerali Lupogo katika kipindi hicho kigumu sana.

“Uamuzi wako utatugharimu!Yaani mimi sikuelewi inakuaje unakuwa na maamuzi ya kukurupuka!Siungengoja hadi kesho ndo utoe hiyo oda?”Serambovu alilalama!

“Najua ninachokifanya.”

“Hata kama lakini kwanini ufikie uamuzi huo?Kama hukupendezwa na sisi kuondoa mchoro wako wa usalama ungetuambia tu!Lakini kumsimamisha kazi kwa wakati huu?”

Kilua alimwangalia nakupandwa na hasira sana!Pozi lile alilijua Serambovu na yeye hakuchelewa akamwangalia pia,”Siuseme au na mimi unataka kunisimamisha uniweke ndani?”

“Kama usingekuwa baba wa mwanangu leo hii ningekufanya kitu…”

Serambovu alitumbua macho kwa mshtuko!Ulikuwa ujumbe mzito kuliko ujumbe wote aliwahi kuupokea!Huu ujumbe ulimsaga ini na moyo!Yeye kuitwa baba wa nani?...

ITAENDELEA WIKI IJAYO
UNAMPA KILUA ASILIMIA NGAPI?
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 66
KOMBORA KIOTANI-25
BONIFACE BIRAGE
“Unasemaje?”aliuliza Serambovu akitetemeka!
“Kama ulivyosikia.”Kilua alijibu kike.Kwa Serambovu Kilua alikuwa hazungumzi kama rais bali alizungumza kama mtu na hawara yake walioshea mambo mengi ya siri.Kuambiwa kuhusu mtoto kuliifanya akili ya bwana huyu kuanza kuchuja kila tukio.
“Ina maana unasema mimi ni baba wa mwanao?”
Kilua hakumjibu kitu akamuacha vilevile kuonesha amekasirika.Alifanya vile ili kama kweli huyu bwana anahusika na utekaji wa familia yake basi afikirie mara mbilimbili kwamba huyo Shani anaweza kuwa wa kwake!Ulikuwa mtego mzuri alioucheza kwenye karata zake.Kalamba dume!Na anageutumia ipasavyo kudhibiti viwembe hawa!
“Hivi upo sawa au unanitania?”
“Serambovu get out of my office!Kilichompata jenerali kinaweza kukupata na wewe.Next time msijaribu kutengua maamuzi yangu lasivyo nitawageuza vibaya!”
Serambovu alitoka akiwa mwingi wa maswali.
Kilua alichukua glasi ya maji akanywa huku akivuta pumzi ndefu nakuzishusha!Tayari alikuwa ameingia kwenye hali ngumu zaidi.Akiwa pale akapokea simu.
“Ndiyo bwana Toti…Yes…What?”alishtuka Kilua akipokea taarifa kuhusu kuvamiwa kwa Pangabutu.
Alipopata taarifa ile aliomba kuletewa jenerali Lupogo haraka sana.Jenerali Lupogo aliletwa ofisini kwake.
Jenerali Lupogo aliletwa akiwa chini ya ulinzi mkali sana,”Jeneral kesho utakuwepo kwenye msiba.Kila kitu nimeshakipanga lakini uwepo wako utakuwepo kwa heshma ya jeshi.Utakuwa chini ya uangalizi wangu any mistake order ni shoot to kill!”alitamka Kilua.Sauti yake ilikuwa ya amri Fulani.Aliwatisha sana walinzi wake kiasi walihisi bifu lao na jenerali halikuwa na utani.
“Mheshimiwa tafadhali naomba usiniweke kwenye utata nina familia.”jenerali aliomba.
“Jenerali mimi sikuwa na tatizo na wewe.Nilichukia ulivyochukua uamuzi wa kupindua maagizo yangu pamoja na Serambovu.Unatakiwa ujue ni nani anakupa mamlaka.Serambovu alinipa jina lako nikijua kwamba wewe unania njema kwangu kumbe unamsikiliza Serambovu kuliko mimi!Kesho utakuwepo kwenye shughuli lakini utulie.Any movement nakupoteza!”
“Nakuelewa mheshimiwa naomba uelewe fika ninaomba samahani sana kwa hatua nilizochukua na wala sikudhani kama ningekukwaza!”
“Just know this general.You are taking orders from me!”
“Sawa mheshimiwa.”alijitetea jenerali.
“Kesho ukishatokea kwenye hafla hiyo nitakusimamisha tena.”
“Sawa mheshimiwa.”aliitikia jenerali kwa adabu.Kisha aliondolewa tena chini ya ulinzi na kuwekwa moja ya vyumba pale ikulu.Kisa kile kilivuja kwa wanajeshi kadhaa ambao wapo waliounga mkono kwa hatua alizochukua Kilua kumwadabisha jenerali wao kupindua agizo la rais nakufuata alichodhani ni sawa.Pia wao waliompinga.Kila mmoja alikuwa na wazo lake.Lakini waliopata habari ile walihakikisha haivuji kwenye vyombo vya habari!Ingekuwa tishio kubwa kwa wageni wajao.
***
Serambovu alikuwa ameondoka ikulu nakuelekea katika mgahawa Fulani maarufu hapo mjini.Huko alikuwa kwenye kikao na bwana mmoja hivi kibosile.Mwenye kitambi na wingi wa majigambo ya kifedha.Alikuwa ameshiba sana mali.Hakuwa na sura njaa.Alikuwa ni bwana Tufe nakofia yake ya kisasa mtindo wa kofia za pama!
“Kijana nyumba kuu inaenda tunavyotaka?”
“Hapana mzee.Kuna mushkeli kidogo ila najua nitaukabili.Mama atatulia tu.”
“Kwani vipi huko?”
“Ni mambo madogo.Nilitaka kukwambia nataka kesho mshtue kidogo kwenye hafla ya msiba.”
Mr Tufe alitumbua macho kwa mshangao,”Eti unataka nini?”
“Nataka kesho mshtue kwenye hiyo hafla.”
Mr Tufe alicheka kicheko cha dharau ambacho kilimshusha kilo za heshma bwana Serambovu.Alionekana kama mjinga fulani asiyejua lolote.Akili yake ilionekana kwenda kwa haraka sana kwenye ulimwengu huu wa ujuaji.Mipango yao ilikuwa inapangwa kiakili na siyo kukurupuka kama vile alivyodhani.
“Kijana wazo lako mbona lina haraka sana tofauti na sisi tunavyopanga?”
“Mzee naona kuna haja kuu ya kufanya hivyo.Bila kumshtua rais ataonekana jasiri na sisi lengo letu ni kuitikisa nchi!”alieleza Serambovu huku akichukua glasi ya kinywaji chake nakupiga funda moja kwa hadhi ya kizungu,makali ya kinywaji kile yalimiminika kwenye mfumo wake wa ladha na kumchechua mdomo!Hoteli ilikuwa ya kitulivu iliyo sheheni watu wazito wenye majina yao.
“Hapana lazima uwe na subra hatuwezi kukurupuka ghafla halafu itokee kwamba eneo lile livamiwe.Kumbuka kamati yetu itakuwepo hapo sasa kwanini tuweke rehani usalama wetu?”
Serambovu alifikiri kidogo,”Bwana mimi namjua huyu mwanamke zaidi ya nyinyi mnanvyomjua.Kuna mambo anayoyafanya lazima tumshtukize.”
Tufe alimwangalia kijana huyu nakuona uchu wa machafuko ukiwa umeweka makao kwenye akili yake na ukitamani kulipuka muda wowote ule angekuwa hatari ya vile alivyotegemewa.Lakini alijua fika bila kuwa na nguvu zaa kumdhibiti anaweza kuwa tatizo huko mbeleni!
“Kijana tunashukuru kwa mchango wako.Nadhani huelewi kwamba tuna taka kitu gani na kwa minajili gani.Hiyo haraka yako ni mwiba tosha unaotutishia sisi.Hivi unadhani unavyoamua kutekeleza hatua kama hizo ndo unajenga?”alisema huku akimwangalia kwa pozi la kuonya kati ya baba na kijana wake.
“Haujengi!”alisema kwa busara kisha akaendelea,”Unabomoa.Nidhamu ya kundi letu ndo iliyofanya tufanye mambo haya bila kuwa na mushkeli.Hatufanyi kwa kukurupuka bali tunafanya kwa akili kubwa sana.”
“Lakini…”alitaka kusema jambo bwana Serambovu ila alikatishwa na mzee Tufe.
“Siyo cha lakini.Becareful kwa hatua zako la sivyo utapoteza.”
“Mimi nilitaka kesho rais apigwe risasi ila siyo ya kumuua.”alisema Serambovu kwa umakini.Mzee Tufe alimwangalia.
“Nani awe mrithi wake kama akifa?”
“Hawezi kufa nataka tu ashambuliwe kwa wakati huyo tutaweza kumuonesha kwamba hatari bado ipo.”
“Kijana kuwa makini…tutakuachia uicheze karata hii lakini tunataka Kilua afe.Nataka nione huo mpango wako kama utawezekana.”alisema bwana Tufe kisha akaamka kwenye kiti alisimama nakulinyoosha kidogo koti lake nadhifu akaanza kuondoka.Kusimama kwake kulifanya vijana kadhaa waliovalia kinidhamu kusimama kisha wakaongozana naye.Huo ulikuwa ulinzi wake mkuu.Serambovu alijua wazo lake limepata baraka nusu na huo ndo mtindo wao wa kutenda mambo huwezi kukubaliwa kwa asilimia mia moja.Alichukua rununu yake nakubofya namba fulani.
“Ndiyo bosi.”upande wa pili ukawa umepokea.
“Ule mpango utafanyika kesho ila nataka ashambuliwe kwelikweli.”alisema Serambovu akijiamini.
“Sawasawa mkuu.”
Serambovu aliamka pale nakurudi ikulu akijua mpango umekamilika.Ilikuwa lazima aoneshe makucha yake kwa wakati ule.Alitaka amuweke rais Kilua kitandani.Hakutaka kabisa mwanamke huyo awe na kiburi dhidi yake.
Alirudi ikulu.
IKULU
Alipofika viunga vya ikulu alikuta kuna ujumbe wake kuwa rais Kilua alimuhitaji kwa haraka sana waonane.Serambovu alienda hadi ofisini kwake.Alimkuta Kilua akimaliza kikao na kamati ya msiba iliyokuwa inasimamiwa na bwana Mambosasa.
“Nashukuru kwa kazi mliyofanya naomba tushikamane hivyo hadi kesho kwenye shughuli kamili natumai tutamaliza salama.Asanteni.”alisema Kilua kikao kikiwa kimeisha.Watu hao waliinuka.Wakapeana mikono ya kheri kisha wakaanza kuondoka Kilua alimpa ishara bwana Mambosasa asubiri kidogo kitu ambacho Mambosasa alitii amri hiyo.
“Ndiyo mheshimiwa.”
“Baada ya shughuli ya kesho nitakuhitaji ikulu kwa kazi maalum so be ready.”alisema Kilua.
“Nitakuwepo mheshimiwa.”alisema Mambosasa akiachia tabasamu la ushindi.Akaondoka.
Mlango ulifunguliwa akaingia Serambovu na uso wa tabasamu alienda nakumbusu Kilua.Kilua alimkumbatia Serambovu kisha akambusu kwa nguvu kama sekunde kumi akamuachia nakumwangalia usoni aliushika mkono wake nakuupeleka tumboni.Kulikuwa na ukimya fulani umepita.
“You know I love you so much.”alisema Kilua kwa utulivu wa hali ya juu.Serambovu alihisi hatia.
Kilua akaendelea,”Nina mimba!Na hii si mara ya kwanza.”
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 59
KOMBORA KIOTANI-26
BONIFACE BIRAGE
Serambovu alihisi mdomo kumkauka!Lilikuwa jambo zito sana!Hofu aliyokuwa ameibeba sasa imewadia dhahiri machoni mwake nakupenya kwenye masikio yake!Halikuwa jambo lakufanyia mzaha!Kilichotokea ni kweli kwamba Kilua ni mjamzito.Hilo hawezi kulikataa na hivi amekuwa na ukaribu sana kiasi cha kuvuka mipaka kana kwamba mwanamke huyo wa mtu ni wa kwake.Mchezo huo ungewafikisha hapa bila kupepesa macho wala nini.Rais Kilua alikuwa ana mimba ya mfanyakazi wake!Rais Kilua alikuwa mke halali wa bwana Dedani Tabiri ambaye ametekwa.Mwenendo mzima wa rais Kilua na siri zake na huyu afriti Serambovu zilikuwa na matokeo.
Kwake Kilua mwendo wake na Serambovu ulikuwa na nguvu ni kama alikuwa mutribu wa nyimbo tamu za mahaba ambazo asingezikwepa hata iweje na sasa imejiri fika kwamba kuna hatari kubwa sana imetokea ya kupachikwa mimba na bwana huyu!Ilikuwa kama dhihaka!
Ilibidi ajitathmini mara mbilimbili maana uzembe wowote ungepelekea matatizo kuwa makubwa zaidi.
“Una mimba?”aliuliza tena akiwa na hofu kuu.Mwili wake ukatetemeka.
“Ulitegemea nini?Lazima jambo hili lingejiri tu iwe isiwe.Imetokea kwamba nimeshika mimba.Tumekuwa kwenye mapenzi mazito sana kwa muda mrefu na bila shaka lingetokea.Hatukuwahi kutumia kinga hata siku moja!Unadhani jambo hili lingenipeleka wapi?’’
“Ni kweli tumekuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu.Lakini mimi sikutegemea kama ingetokea ungepata mimaba.Kwani siyo ya…”alitaka kusema kitu lakini bi Kilua akamzuia kwa kumuwekea kidole mdomoni kumnyamazisha.
“No!Hii mimba siyo ya Dedani.Ni yako.”alisisitiza bi Kilua akiwa na uhakika wa anachokisema.
“Kwanini ukaruhusu?”aliuliza Kilua.
“No nakupenda wewe.Kwa penzi unalonipa nilikuwa tayari kwa lolote.Wewe unajua toka mwanzo jinsi wazazi walivyozuia mapenzi yetu hadi kunileta mikononi mwa Dedani.Alijitahidi sana kunipenda nakunionesha kila hali kwamba ni yeye ndo anayenifaa!Lakini nisingezuia mapenzi yangu kwako.Ulikuwa moyoni mwangu nakuhisi penzi lako linatembea kwenye damu yangu.Tafadhali naomba unienzi mimi nalihitaji penzi lako.Huyu mtoto ni wako angekuwepo Dedani ningemshikisha huyu mtoto lakini katekwa but I will do anything to bring him back to me kulinda heshma ya cheo cha urais.Dedani atakuwa ubavuni mwangu kama mume ana sifa zote.So please usijaribu kusema lolote kuhusu mimba hii.”alisema vile Kilua,kisha akabofya kidude fulani.Wakaingia maaskari.
Kilua aliwapa ishara wasonge.Walikuja hadi alipo Serambovu wakamkamata.
“Kilua unamaanisha nini?”aliuliza Serambovu kufuatia hatua hiyo ya kukamatwa na Kilua.Aiiogopa sana kwa jambo hilo la kuogofya.
“From now on hutaruhusiwa kuonana na mtu yeyote.Hata kuwasiliana na yeyote yule.Nahitaji uwakabidhi watu hao simu zako.Nakuhakikishia hakuna ataakayedukua simu yako wala hakuna atakayegusa mafaili yako.Mambo yako utayakuta kama yalivyo.Kukuacha wewe siri zangu zitajulikana kama nilivyo kwambia kuhusu zao la siri yetu.”
“Kilua please usithubutu kufanya hivyo!’’
“Utakuwa sehemu salamu lakini ya siri no one will know where you are.I promise no harm will come to you.”alisema Kilua akionesha anasikitika kwa uamuzi huo na kwamba hakupenda kumuweka Serambovu kizuizini lakini inabidi tu afanye hivyo.Serambovu alijaribu kuwasukuma watu wale amfikiei Kilua lakini walinzi wakamuwahi nakumshika kwa nguvu.Kilua alionesha masikitiko yake.Yeye Serambovu alijua Kilua anamuweka chini ya ulinzi ilikuficha siri yake ya kumpa mimba..Ina maana hadi sasa haaminiki kwamba anaweza kuficha siri ya ujauzito huo?Mbona kaficha mengi ikiwemo uhusiano wake na Kilua.Serambovu alidata maana Kilua alikuwa amebadilika sana tofauti na vile anavyodhani kitu ambacho hakukitegemea kabisa kwamba kingejiri hata siku moja?Alikuwa na wakati mgumu sana kupinga kauli hiyo maana angeipinga vipi?Huyu ni rais na alichosema ni mwisho!Ikiwa kaamua kumuweka kimya!
Alianza kumshikisha adabu jenerali sasa ni Serambovu mwenyewe.Serambovu aliondolewa kutoka uwepo wa Kilua.Alinyang’anywa simu na kila kitu akachukuliwa nakupitishwa njia za siri pale ikulu.Alipelekwa hadi kwenye maegesho ya magari huko aliweza kufunikwa usoni asijue anaenda wapi kisha alifunikwa mdoni pia asiweze kusema kitu chochote.Kichwani aliwaza sana kama Kilua ni mjamzito na yeye ni baba wa huo ujauzito hata kiwi kumdhuru Kilua.Tayari kesha wapa vijana wake ishara ya kumshambulia Kilua hapo kesho.Na bado hajawapa amri ya kusitisha mpango huo.Bila shaka watatekeleza kazi yao kwa weledi nakuweza kudhuru rais Kilua.Wakimdhuru wamemdhuru na mtoto aliyepo tumboni mwake!Hiyo ni hatari kubwa sana kwake kama baba mtarajiwa.Kama kweli mwanamke huyu amebeba ujauzito wake basi ni kweli ana mapenzi ya dhati kwake nay eye badala ya kuyarudisha amekuwa akimzunguka.Kilua alikuwa mwanamke wa ndoto zake.
Mabadiliko hayo ya ghafla yalimfanya ajiulize kama kagundua yeye ana mipangao ya siri na watu wan je?Kama kagundua basi mambo yake yanaenda kubuma vibaya nay eye atakuwa uwanja wa kupigia ngumi kwa uzembe sana.Lakini aliamini Kilua hawezi kuwa amejua kuhusu ajenda zake za siri kwamba anamzunguka na tayari kasha panga mkakati wa kumfanyia shambulizi ambalo linaweza kumuaa au lisimuue.Hapo alijikuta akikuna kichwa!
Serambovu alijikuta akikasirika sana kwa jinsi mambo yalivyobadilika.Kuwekwa mbali na Kilua kulimfanya ajihisi hana nguvu na hatia ambayo hakuwa tayari kuikubali japo ilizidi kumpenya kwenye mishipa ya moyo!Kilua aliyeonekana dhaifu alianza kuonekana anachukua hatua kali sana.Kujua kwamba ana mimba Serambovu angewapigia vijana wake awasimamishe wasijaribu kufanya shambulizi lolote kwa rais Kilua.Lakini sasa Kilua kamtia mafichoni kabla hata hajapata muda wa kujitete.Hivyo una baki ukweli kwamba Kilua bila Serambovu hatakuwa salama!Isitoshe kizuizi anachoweka hata toka maapema kama anavyodhani bali atafungiwa kwa muda mrefu sana!Muda huo wote atakuwa mafichoni kwa ukimya way eye kupotea kwa jamii!Ataweza vipi kumuonya Kilua?
Aliuma meno kwa hasira kuona amefeli vibaya sana!Akakumbuka kauli kwamba hii siyo mara ya kwanza kwa Kilua kubeba mimba?Ina maana alishabeba na akazaaa?Ina maana wana mtoto na rais Kilua?Huyo mtoto atakuwa ni Shani?Alijiuliza sana!Kama ni kweli basi yeye aiyefanikisha familia ya rais Kilua kutekwa akijua anamkomoa Dedani alikuwa anaiteketeza damu yake mwenyewe!Serambovu aliona mambo ni mazito sana.
Sasa alijiapiza moyoni kwamba kama kweli yeye ni baba kwa watoto wa Kilua basi Dedani hakuwa na haja ya kuwepo kama baba wa familia hiyo.Kwa namna nyingine alitakiwa kumuondoa asiwepo tena ili yeye aichukue familia hiyo.Alijua akitumia udhaifu wa kupendwa na Kilua anaweza kumshawishi waoane.Sasa atakuwa na nafasi nzuri kwenye shughuli za kitaifa na kukamilisha mipango yake.Au anaweza tumia mwanya huu wa Kilua kuwa rais nay eye aweze kujiingiza kwenye siasa ili msimu ujao aweze kuirithi nchi kutoka kwake.Angejiimarisha kupitia Kilua.Anayetakiwa kushambuliwa akaona ni Dedani na si Kilua.Mawazo yake yalimfanya aone mbali zuio lilikuwa hili la Kilua kumtia nguvuni!
***
Shughuli za kutoa heshma kwa marehemu waliokufa kwenye mlipuko ule zilikuwa zikiendelea siku hii mpya.Vyombo vya habari vya mataifa mbalimbali vilikuwa vikitangaza tukio hilo ambalo liliingia kwenye historia ya nchi hiyo.Historia ambayo ingedumu vizazi kwa vizazi ikieleza namna wana serikali ya Kisusi ilivyofutiliwa mbali kwa ajali mbaya.Lilikuwa tukio baya ni kama kombora lilipigwa kwenye kiota.Huzuni iliyokuwa imeikumba taifa haikuwa na maelezo kwa kweli.Watu walikuwa katika majonzi mazito sana!Halikuwa jambo dogo.Kulikuwa na ugeni mkubwa sana kutoka mataifa jirani ndani na nje ya bara kuja kuwapa pole taifa la Kiota kwa kujiriwa na msiba huo ulivunja mioyo ya watu.Mioyo kugugunwa kwa huzuni iliyoleta kuvuja kwa mawimbi ya machozi.
Rais wa Savanna Lands pamoja na vuguvugu la mzozo wa kidiplomasia kujiri kati yake na taifa la Kiota lakini alifanikiwa kuja katika msiba huo.Ujio wake ulitafsirika kama moja ya hatua za kupunguza makali ya mzozo wao wa kidiplomasia.Ila walihakikisha anaketi mbali na rais Kilua ambaye alipowasili kuwalaki wageni mbalimbali hakuweza kumpa mkono rais wa Savanna Lands.Ugomo huo wa Kilua uliwashtua wanadiplomasia wake kiasi kila mmoja akawa anafanya juhudi sana marais kutokabiliana mbele za umma.Lakini Kilua alijitahidi kutulia kwenye kiti chake huku akijaribu kuwaweka wageni wake karibu kwa kuwatuliza waridihike na uwepo wao katika Kiota.Tayari Kilua alishapitia protakali za kiulinzi nakuongeza ulinzi ikiwemo kufunga mitambo maalum ya kudungua makombora yatakayorushwa eneo lile.Vyombo vyote vya ulinzi vilikuwa makini kuhakikisha shughuli zote zinakwenda sawa.
Kilua alihutubia mkutano vizuri akiwataka watu wawe wapole nakuwaa wajasiri hasa katika kipindi hicho kigumu taifa linapita.Aliwapa moyo wananchi wake huku akiwasifu viongozi waliotangulia mbele za haki ushujaa wao wakulitumikia taifa hilo hadi mauti yalipowakuta.Aliahidi kuhakikisha taifa linasonga mbele.Hakutaka kusema waziwazi kama serikali inashuku kuwa ajali ile ilikuwa imepangwa na kuna watu wanahusika.Japo kila dalili na maneno ya chinichini yalipita kwa wananchi wakihisi ni kweli kuna mkono wa mtu katika vifo vile na serikali ipo katika wakati mgumu kudhibiti mikono hiyo ili kurudisha imani kwa wananchi wake.Shughuli za msiba zilifanyika kwa utu hadi zilipokamilika na kila mtu kuridhika kabisa kwamba shughuli zimekwenda sawa.
Kilimeta kadhaa kutoka uwanjani palimokuwa na shughuli za msiba,kulikuwa na kikundi cha watu fulani wakiwa kwenye gari lao.Watu hao walishuka kwenye gari lao nakutoa mtambo fulani wakufyetulia kombora.Waliuweka sawa nakuanza kuuseti wakijua fika watafyatua kombora kutoka pale hadi uwanjani.Walipima viwango vya digrii wakizingatia vipimo vyote vya mzingo wanaotaka kuulipua.Lengo lilikuwa kufyetua kombora hadi uwanjani waombolezaji walipo.Leo hawakupanga tu kummaliza Kilua bali wangevamia na wageni waliokuja kutoa pole.Yaani wangekamilisha msiba juu ya msiba!
‘’Burkan 2h ballistic missile ndo tutalitumia kulipua kombora hili.”alisema moja watu wale akiendelea kurekebisha vipimo vya ulipuaji.
“Mwamba sasa situtamaliza uwanja mzima?”
“Lina madhara makubwa kama litaanguka eneo hilo.”alijibu Mwamba akiwa amekamilisha shughuli ya kupima.Kisha wakajiandaa kufyetua.Walihesabu kwa utaratibu wao kisha wakafyetua kombora lile ambalo ndani ya muda mfupi litakuwa limetua uwanjani nakusambaratisha kila kiumbe katika kiwanja kile.Kombora la Burkani 2h ballistic missile lilikuwa hewani huku kwa nyuma likitoa moshi flani ulioashiria kupaa kwake kwa kasi ya ajabu ukielekea mlimo kuwa uwanja waliopo kina rais Kilua.Ungekuwa mlipuko wa aina yake ambaye ungeandika historia katika taifa hilo.
ITAENDELEA WIKI IJAYO
 
KOMBORA KIOTANI-27
BONIFACE BIRAGE
Rada ya kijeshi iliyokuwa macho masaa yote wakati shughuli za msiba zikiendelea kutoa heshma za mwisho kwa viongozi waliofariki katika ajali mbaya ya ndege kuangukia jukwaani alimo kuwa ameketi hayati rais Kisusi na serikali yake.Rada ya jeshi ilipata signal nakuona kuna kombora linakuja kwa kasi ya ajabu.Aliyekuwa ameketi kwenye mtambo wa kuongozea rada aliona jambo hilo nakuanza kutoa taarifa.Mlio wa kuashiria kunaswa kwa mawimbi ya kombora ulisikika!
“Missile detection!”alianza bwana huyo huku akitoa ripoti kwa wenzake ambao walianza kushughulika kwa haraka ili kuweza kudhibiti hali hiyo kwa haraka sana.Viti walivyokalia vikawa moto!
Waliokuwa na shughuli ya kulinda pale uwanjani walikuwa katika wakati mgumu kudhibiti kombora hilo kwa namna yoyote ile.
“Find the bearings and get me a theat vector.We will take the missile out and the threat!.”huyo alikuwa kanali Pasua alipohabarishwa kuna kombora limerushwa na linakuja katika ardhi ya Kiota.Hapo alikuwa akitoa maelezo wapate vipimo haraka sana nakulitungua kombora hilo kabla halijafika ardhini kisha watungue na mahasidi wanaotaka kutungua Kiota.Vijana kwa kasi ya ajabu walipata vipimo na kasi ya kombora hilo.
“Threat vector localized bearings 098”
“Activate Patriot Missile System to neutralize the threat…take it out at my order!”alikuwa akitoa maelezo Kanali Pasua ambaye alikuwa mita chache kutoka uwanjani.Alikuwa makini kabisa akiangalia kioo kikubwa cha mitambo yao iliyokuwa inaonesha hali ya usalama.Macho yalikuwa makavu yaliyoshiba weledi wa kazi na ukomavu!
“Target acquired!”alihabarisha kijana aliyekuwa kwenye mtambo wa kudungua hatari ya kombora.
“Fire!”
Mwanajeshi aliyekuwa katika operesheni hiyo alibofya kifyetua kombora la kujihami ambalo lingekabiliana na kombora lililokuwa likirushwa kuja eneo lile.Mungu mkubwa alifanikiwa kudhibiti hali hiyo kabla hata halijafika uwanjani.Kombora la kujihami likatoka kwenye mtambo wake kwa kasi ya haraka nakuingia hewani tayari kukabiliana na kombora lililokuwa linakuja eneo hilo.Ilikuwa ni sekunde chache nakulifyetua lile kombora likiwa juu kwa juu!BOOM!Alitabasamu!
Mlipuko ulisikika!Eneo la mji mkuu wa Kiota watu walishtuka sana kusikika kwa mlipuko ule.Kwa bahati nzuri mabaki ya makombora yaliangukia kwenye msitu uliokuwa una mto hivyo kuepusha madhara kwa makazi ya watu.Lakini taharuki kwa waliokuwa karibu ilikuwa kubwa sana huku waliosikia mlipuko huo kukosa amani!
“Eagle one what is the status?”
“Incoming Threat neutralized!”
“Have you found their location?”
“Confirmed sir location on my eyes.”
“Take them out.”
Yalikuwa ni mazungumzo kutoka usalama wa jeshi uliokuwa ukilinda shughuli ile.Tayari walikuwa wamepata shabaha ya eneo kombora lilipotoka.Na sasa walikuwa mbioni kuliondoa kabisa.
“I want three birds on air now got the location.Send the missile on my order.Give the birds coordinates.”kanali Pasua alizungumza akiwa makini wakati ule helikopta zilizokuwa zikishika doria angani zilikuwa zimepewa amri kuelekea mahali kombora lilipotoka.Helkopta takribani tatu zilikuwa hewani kufuatilia eneo lile kwa kasi ya ajabu.Wakati huohuo eneo la usalama lilikuwa tayari kutuma kombora eneo la adui kuwafuta kabisa kwenye uso wa dunia.
“Target north-east fifty kilometres.Birds you are adviced clear the way for the missile.”
“One…two..three fire!”alisema Kanali Pasua ambapo muda uleule kombora likaachiwa kwa kasi ya hatari kuelekea sehemu ya adui ilikuwa sekunde mbili tu kombora la kumdhibiti adui likawafikia nakuwalipua pamoja na gari lao.Walimalizwa ndani ya muda mfupi sana.Jeshi la Kiota lilikuwa makini sana katika kudhibiti tukio hilo.
Helikopta zilipohakikisha kombora limefanya kazi yake zilishika kasi kuelekea kwenye mlipuko.
“Vikosi vya ardhini alert move.”
Nchi ilikuwa makini katika kiwango cha usalama.Kwa kuwa walikuwa namba tatu uwepo wa utayari hivyo walikuwa makini sana.
“Nendeni msitu wa Shaka mto shaba muangalie mabaki nataka kujua ni kombora gani walitumia.”kanali Pasua alikuwa akiongoza mapambano.
“Kitengo cha intelijensia kazini nahitaji majibu hawa waliorusha kombora Kiota ni kina nani?Mipaka yote umakini uongezwe.”
Hali ilikuwa imetishia na hawakujua kama kuna jaribio lingine lingetokea muda gani kwa wakati ule!.
“Kuna utata shughuli ya msiba inatakiwa iendelee kama ilivyokuwa bila kuleta taharuki yoyote.”alisema kanali Pasua.Habari zilitakiwa zimfikie Kilua haraka sana la sivyo mambo yangekuwa hatarini.Wanajeshi walizidisha ukaguzi wa hali ya juu.Ndani ya muda mfupi kikosi cha ardhini kilifika eneo mabaki ya kombora yalipoangukia nakuanza kukagua aina ya kombora.Wengine walifika eneo kombora limetoka nakukuta gari likiwa linaunguwa.
Mwili wa dereva ulikuwa umeharibiwa vipandevipande!Miili kadhaa ilikuwa imeanguka chini isijitambue.Lakini ipo miwili iliyokuwa na uhai bado.Hii waliweza kuichukua nakuwakimbiza hospitalini wangetoa ripoti kuwa wao ni kina nani.Kibati chenye namba za usajili wa gari kilirushwa wakati kombora lilipotua pale.Kibati kile kilikuwa hatua kadhaa kutoka na moja ya wanajeshi alifanikiwa kukiona akakichukua nakuwapa timu ya intelijensia ambao kwa ukaguzi wao gari lilikuwa mali ya ubalozi wa Savanna Lands.Hali ilitia shaka hasa baada ya kujua kuwa balozi wa Savanna Lands alikuwa ametoweka pale.Watu wawili waliokuwa hai walikimbizwa hospitalini.Katika zile purukushani walitambua kati ya wawili wale alikuwepo balozi wa Savanna Lands katika hali mahututi.
Swali kuu alikuwa anafanya nini eneo lile?Hilo lilitosha kabisa kuleta uhatari wa hali ya juu!.Wanajeshi walikamata eneo lile nakuanza kukagua kwa weledi wa hali ya juu.Kazi llikuwa moja tu kuhakikisha hatari iliyochipuka inadhibitiwa vya kutosha.
“Nataka rais Kilua apewe taarifa.Balozi wa Savanna Lands aliyetoweka nchini tumemkuta sehemu adui alipokuwa.”alikuwa ni kanali Pasua akiongea na vijana wake kupitia redio call zao.Kiota ilikuwa imefanyiwa jaribio la shambulizi kwa mara nyingine tena lakini jeshi lake makini lilifanikiwa kudhibiti tukio hilo.
***
Vikosi vya usalama vilizidi kuwa makini kuhakikisha Kiota ipo salama.Muda ule ulikuwa wakutoa heshma za mwisho.Kilua alikwishatoa heshma zake kama mkuu wa nchi.Itifaki ilizingatiwa wakawa wanapita wengine kutoa heshma zao.
Kilua akiwa ameketi kwenye kiti chake aligutushwa kwa habari.
“Mheshimiwa Kiota inashambuliwa.”aliambiwa na chifu wake wa ulinzi.
“How?”
“Kuna ripoti kombora lilirushwa kuja hapa lakini jeshi letu limelitungua likiwa hewani.”
“My God?”
“Mheshimiwa naomba utulivu wako ilitusiwashtue wageni tuna subiri amri yako kama shughuli iendelee au tusitishe?”aliuliza chifu wa ulinzi.Kilua hakumjibu haraka akamgeukia jenerali Lupogo.
“General Kiota is underattack!”alisema Kilua akimwambia jenerali wake ambaye hadi muda huo kamuweka chini ya udhibiti mkali kiasi hawezi fanya lolote.
Jenerali Lupogo alishtuka sana.Nafsi ilimuuma maana mchoro wa ulinzi walioupitisha yeye na Serambovu ulikuwa umedhibitiwa na adui wamepenya.Hali ilikuwa tete kwa wakati ule.Sasa alishindwa namna ya kujisaidia maana lawama zote zitatua kwake.
“Makombora ya kuzuia kombora angamizi yaliyokuwepo kwenye mchoro wangu mliyaondoa kwenye mchoro wenu kama nisingeamuru asubuhi kuyaweka sasa hivi tungekuwa tunazungumza mengine!Jenerali fix this situation la sivyo sitawaelewa wewe na Serambovu!Nataka hatua za haraka zichukuliwe!”
“Madam unamaanisha nini kwa hatua?”
“General I am activating your duties right now!”alisema Kilua akiwa amekwazika sana kusikia Kiota inashambuliwa akiwa madarakani.
Jenerali,”Ok ila naomba tusitishe shughuli hii?”alisema jenerali akitetemeka.
“Tangu mwanzo nilihisi mnataka kuniaibisha leo kwenye umati huu wote.Sasa narudia tena shughuli inaendelea zimebaki dakika chache maana baada ya hapa miili itapelekwa kuzikwa kwa rais Kisusi na timu nzima ya serikali yake watazikwa kwa pamoja.Wengine watasafirishwa maeneo yao.”
“Mheshimiwa nashindwa kuhakikisha kama usalama utakuwepo hadi tuzike naona kuna hatari bado.”alisisitiza jenerali Lupogo.
“General give the order I need our commandors to be in the field right now!”alisema Kilua.Jenerali alitii heshima ile ambapo muda uleule alichukua simu yake maalum kwa shughuli za kiusalama.Kisha alipiga namba Fulani.
“This is general Lupogo am activating special force commandors code name 23899kiota alpha team delta tango full attack!”alipotamka maneno yake vikosi vilivyopewa amri ile walitoka kambini nakuingia kwenye magari yao.Umbali wa pale na eneo la msiba ingewachukua dakika kumi tu.Ndani ya muda mfupi vikosi vya komandoo wakiwa na mavazi maalum ya kijeshi walikuwa kwenye magari yao ya kasi wakija eneo lile huku wengine wakitumwa eneo lakuzikia makaburi ya dhahabu ambapo huzikwa viongozi wa Kitaifa.Vifaru vya kijeshi vilikuwa tayari endapo hatari ingetokea basi inngedhibitiwa kwa weledi wa hali ya juu!Vikosi vilizidi ongezeka ambapo ulinzi sasa ulikuwa imara.
“General no movement in and out our land seal everything!”alisema Kilua akifunga mipaka yote ya nchi!
UNAMPA KANALI PASUA ASILIMA NGAPI ZA UTENDAJI
RAIS KILUA UNAONAJE UTENDAJI WAKE LEO?
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 60
KOMBORA KIOTANI-28

BONIFACE BIRAGE

Tayari mipaka ya Kiota ilikuwa imefungwa kwa muda hadi marehemu watakapozikwa.Wakati shughuli zikiendelea rais wa Marekani aliyekuwa amekuja pale alipewa taarifa kwa kinachoendelea.Usalama wa marekani uliomba kumuondoa rais wao haraka sana eneo lile.

Ilibidi Kilua aongee naye chemba rais marekani bwana Silver,”Kwa heshma zote rais Kilua itabidi usalama wangu uniondoe hapa.”

“Mheshimiwa najua unataka kuondoka lakini nakuhakikishia timu yangu ya usalama ipo kazini hakuna atakayethubutu kuleta shida eneo hili.Naomba marehemu wetu wapewe heshma zao.”

“Ila hata kama nitabaki basi naomba wanausalama wangu waungane na wa kwako.”aliomba rais Marekani ambaye mwenyewe hakuwa na lengo la kutaka kuondoka eneo ingawa hali ya hatari ilikuwa imeripotiwa muda ule.

“Nashkuru kwa msaada wako ila naliamini jeshi langu.”

“Najua lakini marekani ina usalama wake.”alihakikisha rais huyo ambaye alikuwa na nia njema na tayari walikuwa na kaurafiki na rais Kilua.

“Nitashukuru kama mkilipa jeshi langu uhuru wake.”

“Sina maana kwamba tunalidharau ila ni msaada wa kirafiki nchi zetu ni marafiki wakubwa na wakati wa kuonesha urafiki huo ni sasa!”alishauri rais Silver

“Ni kwa heshma yako tu.”alisema Kilua akimpa mkono rais huyo!Rais Silver aliongea na vyombo vyake vya usalama ambao waliungana na wenzao wa Kiota nakuendeleza ulinzi wa hali ya juu!Kilua alijitahidi kutuliza akili yake hadi shughuli itakapoisha.Heshma za mwisho zilikamilika na msafara ulielekea kwenye makaburi yaliyoandaliwa.Wanajeshi walikuwa wametapakaa kila kona kuhakikisha ulinzi unakuwa imara.Viongozi wa kigeni waliokuwa pale walipewa taarifa kilichokuwa kinaendelea na hatua zilizochukuliwa.Ulinzi uliimarishwa na wakaondolewa hofu dhidi ya shambulio lolote.Wengi walimuonea Kilua huruma kwa jinsi alivyokuwa anapitia hali ngumu wapo waliolalamika wakiona ni uzembe ila wote waliweka usiri wa hali ya juu ili umma usipatwe na woga dhidi ya tishio lililokuwa likiendelea.Makomandoo wa kikosi maalum walikuwa wameungana na wanajeshi wenzao hali ikawa shwari ndani ya muda mfupi walichosubiri ni huyo kidudu mtu atakaye thubutu kuinua kidole dhidi ya taifa hilo.

Helikopta zilikuwa hewani kushika doria huku ndege za kivita zikipitia anga lote la Kiota kuhakikisha usalama.Ndege zisizotumia rubani zilikuwa zikipita angani kupitia usalama.Ndege maalum pia za kudhibiti makombora ambazo hazitumii rubani nazo zilikuwa tayari kudhibiti jambo lolote ambalo lingeashiria udhibiti wa kiusalamaa.Anga la Kiota lilikuwa na utayari.Ndege zote zilizokuwa zikiingia zilizuiwa na hakuna iliyotoka!

Kilua alikuwa anatamani alipize kisasi kwa dharau za shambulio lile.Yaani watu wamepenya na silaha nzito wanataka kumuaibisha kwenye shughuli muhimu hii kwake aliona ni dhihaka!Na hata huyo balozi wa Savanna Lands aliyekutwa eneo la tukio aliapa kumuangamiza kwa nguvu zote!

Watu walifanya mazishi ya wafu wale kwa amani.Taratibu zote zilikamilika baada ya masaa kadhaa ambapo shughuli zilipoisha waombolezaji waliondoka eneo lile.Viongozi wakigeni waliomba kuondoka pale haraka sana wapo walioruhusiwa na wengi waliondoka pale akiwemo rais wa marekani.Isipokuwa rais wa Savanna Lands alizuiliwa kuondoka.Ilibidi viongozi kadhaa waingilie kati mzozo huo na kikao kikaitwa ikulu cha dharula wakiwemo takribani marais sita pamoja na wamarekani.

“Mheshimiwa huwezi kumzuia aondoke.”alisema moja ya marais aliyekuwepo kikaoni pale.

“Mimi nashangaa huyu mwanamke tangu apewe kiti amekuwa akiniandama mimi na taifa langu.Kesha tungua hadi ndege ya jeshi letu na mwanagalia tu!”alikuwa akizungumza kwa ukali rais wa Savanna Lands.

“Jamani tutumie busara kwa nini rais Kilua hataki rais wa Savanna Lands aondoke hapa.”

“Anataka kusema mimi nahusika na hili jaribio la leo!”rais wa Savanna Lands alikuwa muongeaji hodari wa kulalamika.

”Kumzuia huyu bwana kutasababisha mgogoro mkubwa wa kidiplomasia kati ya taifa lako na lake.Pengine muingize vita kabisa!”

“Mimi sihusiki kwa lolote!’alijitetea.

Kilua alipiga meza kwa hasira wanaume wote wakamuangalia pale,”Waheshimiwa msidhani nachukua hatua hii kwa kumuonea!Huyu bwana taifa lake lilianza kuleta majeshi yake mipakani mwetu haitoshi akarusha ndege ya kivita sikuwa na budi nikaidhibiti!Balozi wake alitoweka hapa akanitishia sana kwamba nahusika lakini cha kushangaza leo mlipuko ulipotokea tunamkuta balozi wake.Silaha hizi zimetoka Savanna Lands na ripoti hizi hapa zinasema kabisa gari lilikuwa la ubalozi na leo hii kamera za mipakani zimethibitisha kwamba gari hili lilipita huko jana!Halafu linakutwa eneo la shambulizi mnataka nifikirie nini?”

Hali ilikuwa tete,”Madam Kilua hadi sasa majeshi yangu yanajua kwamba umenizuia ikulu kwako huu ni utekaji nakutahadharisha tutaingia vitani!”
“Mheshimiwa kwanza achia watu wa ubalozi wangu waliopo kwako!”alitamka Kilua kwa ujasiri!Thubutu aliyoifanya ilionesha hatari sana.Kikawaida mizozo huwepo lakini hatua ya Kilua ilishtua wote nakuona kwamba mwanamke huyu alikuwa msumeno na kama hawatajifunza kushirikiana naye kwa nidhamu la sivyo anaweza akafanya tukio la kuogofya!Alionekana kama dikteta kumshikilia rais wa taifa lingine ni ishara ya vita.Ilibidi wawahini viongozi wote kuhusu ugomvi wao.

“Nimewasikia mimi nawahakikishia Savanna Lands haihusiki kwa lolote na shambulio la leo na kama inahusika basi nitaachia madaraka!Naomba nitoe hilo kama ahadi.”

“Kabla ya yote watu wangu waliopo ubalozini kwako ambao umewaweka chini ya ulinzi nataka waachiwe huru.Asiguswe hata kidole.”Rais Kilua hakuwa na ubembelezo wowote kwa wakati kama ule.

“Nitawaachia ila kwa sharti moja.”alitamka rais wa Savanna Lands.

“Huna mamlaka ya kuniwekea masharti kama ulikuwa unamchezea rais Kisusi mimi hutathubutu!”

“Punguzeni jazba wote tunataka tufikie muafaka ila wataalamu kutoka nje watachunguza ikibainika serikali ya Savanna Lands ina mkono katika shambulio hili basi itawajibishwa!”moja ya viongozi wa nje alisihi kuhusiana na jambo hilo.Alieleweka ikabidi wakubaliane dhidi ya mabishano yale.Kilua aliogopwa sana.

“Pia tunaomba habari hii isitoke itachochea fujo kati ya watu wenu.Ibaki kuwa top secret.”alishauri rais mwingine maana katika kuzuiwa kule ni wachache sana walijua hatua aliyochukua Kilua.

“Lakini nasema tena ni ukweli rais wa Savanna Lands anataka kingilia nchi yangu mimi nilisema toka mwanzo na hata mkichunguza mtagundua hilo.”alisema Kilua akiwa ameanza kupoa .Mazungumzo yalidumu takribani masaa manne ndipo suluhu ikapatikana usiku na hali ikawa imepoa na hata rais wa Savanna Lands alikiri baada ya pale hakupenda swala lile lifikie umma.Ilikuwa aibu kubwa sana ikiwa ingegundulika kwamba alikuwa amezuiwa na mwanamke huyo!Wao walimuona kama dhaifu tofauti na mategemeo Kilua alikuwa anajua wapi pagusa.Ndege za jeshi lake zilipogusa anga lake alishambuliwa kwa haraka sana.Hiyo ilimpa tafsiri kwamba mwisho wa siku Kilua alikuwa mbabe na alijua anapiga wapi anakumaliza.Kikawaida ni kama juhudi zake za kumuingilia Kilua badala ya kumdhoofisha walijikuta wakizidi kumuimarisha zaidi maana hatua alizochukua pengine zilionekana za kibabe zaidi ila ziliondoa tabasamu la kinafiki kwa maadui zake ambao sasa walikuwa wakilowa woga kwa ubabe wake.

Kilua hakuonekana tena yai bali mbabe anayesubiri kuchokonolewa kisha akufumuwe nakukuvua nguo mbele ya kadamnasi na kwa hatua ile si ajabu mataifa hayo yakizidisha uhasama.Na badala ya Kilua kutafuta amani ikawa ni zamu ya rais wa Savanna Lands kujiondoa katika shutuma hizo za Kilua.Hata kama alihusika kwa shambulio lile bila shaka alikuwa amevuliwa nguo mbele ya viongozi wenzake.Na kisasi cha Kilua kilikuwa cha akili sana.

“Mshemiwa watu wako wanaweza thubutu kutikisa anga langu kwa sauti za makombora lakini mimi nimekuanika mbele ya viongozi wengine na ninakuhakikishia taswira ta taifa lako hadi uje ulioshe itakubidi ujishushe hasa.Mimi nimepewa hiki kiti nakitumia ipasavyo kulinda taifa langu.”

“Nalijua hilo na ndo maana nataka mniamini kwamba sikuwa nania yoyote kuhujumu utawala wako.Najuwa tuna mizozo baina yetu lakini hiyo siyo lengo la kukutikisa bali ni ushindani wa kibiashara.”

“Hapana!Wewe ulijileta direct iweje silaha hizi ziingie kwangu kupitia kwako halafu leo wanafanya jaribio.Kinachonishangaza iweje urushe kombora mahali unajua kabisa nawewe upo?”Kilua alihoji hilo.

“Ndo maana nasema siuhusiki kwa jambo hili mheshimiwa.”alikuwa mpole rais wa Savanna Lands.

“Huku jiuliza kuna mataifa mangapi viongozi wao walikuwepo hapa?Huku nitishia mimi bali mlitishia na viongozi wengine.”Kilua aliendelea kumshambulia rais wa Savanna Lands na jinsi mazungumzo yalivyo ilionesha Kilua alikuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwamba shambulio hilo lilikuwa na baraka kwa taifa hilo.

“Tafadhali naomba uondoe kauli ya kunishutumu moja kwa moja.Mimi sijui kama balozi wangu alikuwa na mkono wa jambo hili.Hawa wanafanya mambo kutuchonganisha tu!”

“Mheshimiwa unakumbuka ulivyonitishia kwenye simu!”

Chumba kikawa kama kinachemka tena baada ya majibizano magumu baina ya watu hawa wawili!Mambo yalikuwa yana badilika.

“Ok jamani tuwe na nidhamu tafadhali sisi ni viongozi wa mataifa na wote tunategemewa naomba tufuate utaratibu kama tulivyokubaliana.Kwanza raia wa Kiota waliopo kizuizini huko Savanna Lands tunaomba waachiwe huru.Halafu wachunguzi kutoka nje watafanya uchunguzi dhidi ya shambulio hili na atakayekutwa na utata basi atawajibishwa.Mabishano haya yanaonesha fika kwamba nyote hamuelewani na kwa namna hii itatulazimu tulete majeshi ya umoja wa mataifa yalinde amani ikiwa hamuwezi kutuliza hasira zenu.”alishauri rais marekani.

“Mimi sina haja ya kwenda vita na huyu.Ninachotaka ni ukweli ujulikane muhusika wa shambulio hili ni nani.Nianze vita kwa lipi.Namfuata adui wanajeshi wako wanafuata amri tu.Mimi na mfuata anayehujumu taifa langu tu!”
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 67
KOMBORA KIOTANI-29

BONIFACE BIRAGE

Kikao kilifikia muafaka na rais Kilua alikubali kumuachia rais wa Savanna Lands aondoke.Ilionekana ndege yenye chapa ya jina AIR SAVANA LANDS ikikatiza angani kuondoka.Kwa rais wa Savanna Lands alipakwa fedheha kufuatia shutuma alizotoa Kilua.Haikuwa hatua ya kirahisi kama vile ilivyotokea na ilitakiwa aharakishe kusimamia uhusiano wa kidiplomasia na taifa la Kiota la sivyo angezidi kuonekana kituko mbele ya kadamnasi na jamii kwa ujumla.Mambo ilikuwa nzito sana na bila kuzima moto huu kwa busara alikuwa katika mashaka!Hasira ya mwanamke yule ilizidi kumshushua kila alipowaza na kweli siku ile ilikuwa ngumu katika historia ya maisha yake kuzuiwa na rais mwenzake!Akiwa angani alitizama kioo alihisi hasira na woga ukamwingia hadi akajikuta kichozi kikimtoka kwa jinsi alivyofedheheshwa.Alikuwa tayari kulipa kisasi lakini ingekuwaje mbele ya mwanamke huyo mbabe ambaye kesha uwekea utawala wake vitisho na kama hata imarisha uhusiano wa taifa lake na Kiota bila shaka kutakuwa na vikwazo vingi kwake kiuchumi!

Alitamanii kisasi kwa hali ya juu lakini alishindwa maana kwaanzia wakati ule lolote lingetokea dhidi ya Kilua mlaumiwa wa kwanza angekuwa yeye.Ilibidi ageuke awe mlinzi badala ya mshambuliaji.Tayari alipiga simu kwake nakusitisha hatua zote za kuidhibiti Kiota kwanza hadi hapo mambo yatakapokuwa sawa.Ndege yake ilitua salama katika ardhi ya taifa lake.Alipokelewa na usalama wake kisha alienda hadi ikulu kwake.

***

Shuni alikuwa amemshika mtoto wa Kilua ambaye bado ukimya wa maonevu ulikuwa umemtafuna ini na moyo.Alikuwa ameharibika kisaikolojia hasemi la bee wala tee.Ni uharibifu wa hali ya juu ukimtafuna ini na moyo!Shuni aliweza kuoneshwa kwa mara ya kwanza bwana Dedani mume halali wa rais Kilua akiwa amefungwa kamba nzito mikononi na miguuni!Alijikuta kwa siku ya kwanza akimkodolea macho bwana kana kwamba ameona kitu fulani au aliona zaidi kwenye bilula za macho yake.Aliona kitu zaidi ya upeo na taswira iliyomfifisha hali ya sintofahamu!Moyoni alihisi amefeli katika kumuokoa mwana wa rais Kilua lakini kama mumewe ypo na mwanaye bado wana pumua basi alikuwa na uhakika wa kuisaidia familia hii kwa udi na ambani.

“Walimfanyaje mwanangu?”aliuliza Dedani akiona mwana wake akiwa kwenye wingu la huruma lisilo na msalia mtume wa faraja.Kapotezwa kabisa na hajijui wala kujielewa.Picha ya zee Kavu na fimbo yake nyama ilikita katika kuta za usichana wake nakumfedhehesha alihisi kupasuka kwa mashaka ya wasiwasi nakutokujiamini!Shani alikuwa si Shani iliyong’aa na nuru yenye kumliwaza kila mtu.Sasa alikuwa mwana huzuni mbeba kilio cha shake akijuaye moyo wenye kiza kinene!

“Walimbaka!”alisema Shunie kwa huzuni kedekede zenye mchakato uliotindwa hofu!

“Kwanini kwa mwanangu?”alijiuliza Dedani akiwa haamini kabisa kuhusu tukio hilo lenye dhihaka kwake.

“Bwana najua wote tuna huzuni kwa unyama aliofanyiwa Shani.”alianza Shunie akijaribu kutuliza.

“Huu si unyama!Hata wanyama wana hafadhali!Simba hawezi kubaka kinda!Binadamu huyu ndiyo mkatili,Unawezaje kumnajisi mwanangu ninaapa nitairudisha familia yangu ikiwa salama!They hurt my baby girl I will kill them!”aliapa Dedani akizidi kudata na tukio lile ambalo lilifedhehesha sana moyoni!

Shunie akiwa pale kaketi akitizama akijaribu kumfariji bwana huyu akili ilifanya kazi mara mbili kati ya kutoroka pale nakuikoa familia ya rais Kilua.

“Tutashinda jambo hili.Nakuhakikishia bwana lazima tuondoke hapa hawawezi kutuzidi kete watu hawa.”

Dedani alidata kwa namna fulani akili ikifa ganzi.Mlango ulifunguliwa akaja akachukuliwa kisha akatolewa nje yeye pamoja na Shunie.Hakutaka kuwa mbali na mtoto wake ilibidi wamlazimishe kwa nguvu zote hadi alipotoka.Waliletwa kwenye chumba kingine.

“Bwana Dedani nina jambo nataka ulifanye.”alianza mzee Kavu akiwa kashika sigareti kubwa iliyonona nakukaa vyema kwenye mdomo wake.Moshi mzito ulionekana kufuka kwa mbwembwe za ukwasi.

“Kazi gani mnataka nifanye?”aliuliza japo alikuwa na hasira sana na alitamani kumvaa bwana huyu nakumfutilia mbali lakini hakuwa na uwezo ule kwa wakati ule.

“Nadhani ulipata ujumbe kwamba mkeo na mahusiano ya siri ya kimapenzi bwana Serambovu.Uhusiano huo ni mkubwa sana hata imefikia mahali Kilua yupo tayari kuishi na huyu mtu kama mumewe na wewe ndo tatizo.’alisema bwana Kavu akimwangalia shabaha yake.

“Kwa sasa wapo wote ikulu na siajabu mkeo anazidi kuliwa na huyu bwana ingawa anajua wewe umetekwa hata ile heshma kwako haipo.”

Dedani alimeza jambo hilo.Mzee Kavu aligeuza kioo cha tarakilishi yake ya mpakato.Kulikuwa na video ikionesha hafla za Kilua akiwa kama rais huku pembeni Serambovu akitanda bila hiyana!

Dedani alikerwa na jambo hilo.Halafu mlango ulifunguliwa katika chumba kile akaingizwa binti fulani.

Dedani alimwangalia msichana yule pasi nakumjua hivyo hakumpatiliza sana.

“Huyu msichana alikuwa mfanyakazi wa ikulu.Msichana hebu tueleze.”

“Ni kweli nilikuwa mfanyakazi wa ikulu hivi karibuni niliingia chumbani kwa rais asubuhi kumuandaa.Ajabu walinzi waliniruhusu niingie kwamba rais bado amelala.Niliingia nakusikiia kelele za mahaba.They were deep making love and seems they didin’t notice me.Nilidhani ni mumewe inawa ikulu tulishangazwa kwanini familia ya rais hadi muda ule haijaja ikulu.Kuja kushuhudia nilimkuta rais Kilua kwa macho yangu akifanya mapenzi na Serambovu!Habari hii kuna mwandishi alitaka kuichapa lakini akazuiwa.Mimi nilimkuta Kilua akizini na Serambovu.Niliona haya halafu nikasikitika kwanini rais anakosa heshma nakutembea na mfanayakazi wake ikiwa wewe upo?Kwani rais wetu ni kicheche?”alihoji binti yule akimakinika.

“Dedani act like a man!”

Dedani hakujibu kitu.Alitulia kimya huku machozi yakimtoka kwenye chemchem ya moyo wake kwa kasi!Aliujua huu udhaifu wa Kilua kutoka kwa bwana Serambovu ameishi nao ukimsugua ini na moyo hadi akawa na vidonda vya tumbo.

“Bwana Dedani mkeo nimsaliti wa ndoa!”

“Nifanyeje?Hili ni swali unatakiwa kulijibu bwana Dedani.Jibu ni rahisi mimi ninatoa wazo zuri tu.Tutakuachia na useme kwamba mkeo anakusaliti ndo maana hujaonekana tangu yeye kuwa rais wa nchi.Then sisi tutakuandaa kisiasa uwe mpinzani wa mkeo.Kwa masharti ya jambo moja hapo mbeleni kuna kitu tunataka uje utusaidie kukipata.”

“Jambo gani?”
“Nyaraka namba 13:14.Nahisi mkeo anakaribia kutambua jambo hilo.Lakini sisi tunaandaa baada yake nani ataurudisha tena?Tunataka uwe mpinzani wa mkeo.Japo tulitegemea awe dhaifu lakini katushangaza baada ya kugeuza mwenendo tunahitaji njia mbadala na wewe ndo njia hiyo.Kwa hatia ya kukusaliti anaweza akakupa kiti ilituweze kumdhibiti!”

“Mnataka kunitumia mimi kwa faida yenu?”alihoji bwana Dedan akiwa bado amepandwa na hasira.Alitaka kabisa kulipa kisasi dhidi ya usaliti wa mkewe kwa usaliti wake uliovuka mipaka.

“Ndiyo tunataka kumchafua mkeo tena sana.Huu ni wakati wako wakutusaidia sisi kulipa kisasi.Ukiwaanika mbele ya umma lazima Serambovu aondoke kwa Kilua kulinda heshma ya Kilua!Vilevile wewe utakuwa na nguvu ya kumdhibiti mkeo!Utadai unataka muwe na suluhu!”

Dedani alifikiri kiasi lakini hakusema kitu.Ilibidi wamrudishe kwenye chumba kingine cha kizuizi.Shuni alibaki kwa mzee Kavu.

“Tuna hitaji na wewe jambo moja toka kwako!”

Shunie alishtuka akimwangalia Mzee Kavu na chongo lake ambalo Shunie ndo aliyemtoboa jicho hilo.

“Kitu gani?”
“Mrubuni ulale naye leo.Ukifanikiwa tutawaachia!”

“What?”

“Ulipewa mafunzo kumrubuni mwanaume yeyote yule utashindwaje kumlaghai huyu?”

Shunie alitumbua macho kwa mshangao wa aina yake.Atawezaje kufanya jambo hilo na mume wa mtu kweli huyu bwana hana nia njema na Shunie bali uonevu wa kijinsia.Shunie alihisi mwili wote kufa ganzi.

“Siwezi kufanya hilo jambo!”Shunie aliweka mgomo.

“Wewe mpe jambo lakumsahau mkewe.That fool anampenda sana mkewe.Anahitaji kujua ladha nyingine.Ukipita kwake anaweza asihisi sasa ila hapo mbeleni kikatokea kitu.”

“Mna malengo gani?”aliuliza Shunie.

“Just do it siunataka kuwaokoa?Wewe wafanyie jambo hilo nakuhakikishia inawezekana kabisa mkatoka huku mkiwa salama pia itaokoa kuondoa hatari ya Shani kuendelea kudhalilishwa.”alitamka mzee Kavu kisha akaamuru Shunie na Dedan waweke chumba kimoja.Hilo lilifanyika.

“Bosi unadhani jambo hilo litafanyika?”aliuliza yule binti.

“Vinywaji watakavyokula na vyakula vitasaidia kuwashawishi wao wafanye jambo hilo then tuta rekodi tukio hilo.”

***

Dedani alipapasa godoro nakujikuta akiwa ameshika mwili wa mtu wenye ulaini wa hurulaini.Alijihisi mtawala wa dunia na ardhi yote.Hakuhisi huzni bali ujaisiri wa hali ya juu.Mguso huo wenye mpapaso ulirudishiwa kwa mbwembwe za aina yake kisha yeye mwenyewe alijikuta akiinuka kwa mtikiso uliopeleka moyo na mzunguko wa damu kuwa kwa kasi ya ajabu.Alijikuta akimshambulia mwanamke aliyekuwa kitandani mwake.Ujio wa mwili wake kwa msichana huyo ulipatwa na joto na kila fahamu ya hisia ya mwili wa mwanamke yule aliutambua uwepo wake nakumpokea kwa katazo lililokinzana na uhitaji wa miiili yao!Kulikuwa na joto katika kitanda kile.Pengine nikutokana na akili zao kupoteza kumbukumbu mbaya za mateso waliokuwa wanapitia zaidi walikuwa wao wawili na akili zilikuwa haziwazi matatizo bali kiwango cha kilele chenye faraja raha!
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 62
Back
Top Bottom