Riwaya: Kombora kiotani-1

Riwaya: Kombora kiotani-1

KOMBORA KIOTANI-30

BONIFACE BIRAGE

Wawili walikuwa wanafanya mapenzi.Mtu mume na kike.Walikuwaa wamezama kabisa katika dimbwi walilolijua wao wenyewe nakutopatiliza ulimwengu uliwazunguka.Walijua wapo mahali hata kuona walipo lakini hawakugundua lolote kwa muda ule wa wingi wa hawaa na chachu ya penzi lenye uzito wa kijuaji!.Dunia iliwaweka kwenye kiota cha mapenzi yao wawili wenye miili.Mtu nke alikitia joto kitanda kile na kuzama kwenye bahari yao isiyo na maelezo.Unyevu wa jasho ulitota kwenye mgongo wa mwanaume yule aliyekuwa akijitahidi kuzama nakutoka kwenye kisima cha mwanamke yule.Vidole vya msichana vilikuwa vikishika mgongo wenye utelezo wa jasho huku kucha zikichomachoma kwenye nyama za mgongo.Yalikuwa mahaba mazito ya ghafla bila kutarajia kwa hawa viumbe waliozama kwenye bahari yao ya muda mfupi.

Safari ya mahaba ilikuwa kwenye kilele kila muda ulivyoenda nakuwafanya wote wazinduke katika mvuke ule uliowatotesha kwa kuwapika na mfukuto wa hawaa.Dakika zilipokinzana na haja ya mwili viumbe hawa walijikuta wakiachiana nakuhema kwa pupa pumzi zikishindana kuingia nakutoka.Usingizi mzitoo ulimchukua mwanaume yule nakumfanya apotee kwenye kiota cha pumziko.Msichana alimwangalia mwanaume yule alivyofumba macho nakupotelea kwenye usingizi wa pono.Alimtizama kwa wingi wa maswali hata asimmalize.Alifikiria mbali sana kiasi usingesema wawili hao walikuwa pamoja muda ule.Tayari akili ya binti ilianza kurejea kwa umbali nakujua tukio hili litaanzisha mambo mengine.Hatimaye Shunie katimiza lengo alilotumwa na mzee Kavu kumhini Dedani afanikiwe kuwa nawe kwa muda.Pengine tukio hilo lingezaa jambo ambalo lingempa sababu Dedani kuwa na mawazo kinzani kati ya kuwa naye au la!

Aliupapasa uso wa mwanaume huyo aliyekuwa ubavuni mwake nakuuangalia.Halafu akajichukia sana kutumika kwa namna ile nakuhofia hatma yake na nafasi kama mwanamke katika jamii ipoje?Ni sawa kuendelea kutumika kwa namna ile.Leo kalala na mume wa rais Kilua!Hilo tiyari na tatizo kubwa sana kwa upande wake akijiuliza kama ataeleweka mbele ya rais siku akijua kitu hicho!Haijalishi alikuwa katika hali gani hadi jambo hilo likajiri lakini limejitokeza.Akili yake ilikufa ganzi nakumhofisha sana kama ataendelea katika hali au la!Dedani yu ubavuni mwake muda ule.Tayari kesha fanya alichotakiwa sasa angesubiri tu bwana huyu aamke ajue kaama tukio hilo lilikuwa na maana au ni jaribio hewa.Kinachohitajika nikuhakikisha Dedani anakuwa mikononi mwake!Lakini kwanini apewe jambo zito kama hilo alitekeleze?Kwaninii yeye na asipewe mtu mwingine?

Aliogopa wakati mwingine kwa jambo hilo.Lakini alipiga moyo konde kwamba nitukio la mara moja na pengine halitajirudia tena na yeye atakuwa imara.Ila picha ya uwepo ubavuni mwake ilizidi kumshawishi asonge zaidi pengine kwa dakika hizo chache aweze kulifaidi joto la mwanaume huyo!Alijisogeza nakukilaza kichwa chake katika kifua cha Dedani.Chakula walichokula kilifanikiwa kumlevya Dedani kuondoa ufahamu wake kwa kiasi fulani hivyo kutoa mwanya kwa wawili hao kufanya lolote ambalo ufahamu ungelidhibiti!Shunie alihisi kuridhika na kitu fulani kuchepuka katika moyo wake huku masikio yake yakihisi mapigo ya moyo ya Dedani aliyelala kwa amani!Shunie alihisi tofauti katika kulaza kichwa chake juu ya kifua cha Dedani .Ilikuwa tofauti hata akiwa na Mzee Tufe na Pablo.Kumbukumbu zake zilikoma na akili kutulia kisha amani fulani ilipita kwenye fahamu zake.Usingizi wa amani ulimjia na yeye kulala kwa amani.Kwa muda mfupi alijihisi yumo kwenye kiota cha paradiso na akili kuliwazika kabisa na yeye kujisahau.Alisahaau hata matatizo yote ya kuwekwa kizuizini na watu wale wenye roho za kutu…

***

Pumzi yenye joto nakaubaridi kidogo ilikuwa ikipuliza kifuani mwake bwana Dedani.Alizinduka kwa taratibu huku akili ikijaribu kujua mahali alipo lakini uzito wa kichwa ulimfanya azubae na punde alipojua kuna mtu mke pembezoni mwako nakuipata harufu maridhawa ya mwanamke huyu alihisi kama ni Kilua wake kwenye bustani ya maua.Alijikuta akimkumbatia kwa nguvu nakumgeuza tayari kumkabili lakini pua zake zilimwambia utuli wa mwanamke huyu laini kama hurulaini hakuwa wa Kilua.Huyu alikuwa mtu tofauti na mazoea yake.Japo ni kwa muda sasa hajaonana na Kilua wake lakini bado anakumbuka mazoea yake pindi wakiwa pumziko nyumbani basi angekuwa bustani akipalilia maua yao.Hizo ni siku njema za uhai wa penzi lao.Hazipo tena zimefika kifo!Akagundua si Kilua bali ni mtu tofauti kabisa na huyu aliyepo hapo.Alinukia kama malaika kwa utuli ulio na tarabizuna halisi ya mwili pengine ni kule kuzoea kutumia tarabizuna fulani ambazo bado ziliacha utuli wake kwenye mwili.Dedani alichachawa ule utuli.Kwa dakika alimwangalia mwanamke yule nakugundua ni Shunie!Akili yake ikazinduka muda ule nakujua kilichotokea kati yao hakikuhitaji ufafanuzi wa manunuzi ya kumbukumbu japo hakuna kumbukumbu ya lolote lililojiri usiku uliopita lakini hali ilimwambia hakuna usalam na kwa mara ya kwanza alifanikiwa kumsaliti mkewe!Dedani alimtoa mwananke yule kwa utaratibu pasi nakumuamsha akamlaza vizuri kisha yeye akaamka nakutoka kitandani huku ameshika kichwa kwa hofu na majuto!

Dakika tatu mbele Dedani akiwa amejishika kichwa asijue kinachoendelea alimuona Shunie akiamka nakumkazia macho!Wote walishindwa kukabiliana machoni.Aibu fulani ilikuwa imewameza kwa ghafla!Hakuna aliyejua ni wapi waliacha mavazi.Lakini kichwani kwa pamoja likawajia jina la Shani.

“Shani” walitamka kwa mkupuo halafu wakajishika vinywa kwa aibu fulani.Ni kweli walikuwwa wamepigwa na butwaa.Dedani aliona maliwato aliyafuata kwa haraka.

***

Mzee Kavu akiwa kwenye chumba chake cha uongozaji alikuwa akiangalia kupitia tarakilishi yake yenye kamera zilizofungwa kile chumba alimokuwa Shunie na Dedani.Alikuwa amerekodi kila tukio.

“Game over.”alisema mzee Kavu akiangalia kishujaa tukio zima kwa mbwembwe.Nimefanikiwa kumlaghai Dedani mikononi mwa Shunie akijua kwaanzia pale Dedani na Shunie hawatakuwa kawaida tena.Wataangaliana tofauti na hatia kuwala kila watakapowaza tukio lile hapo alijua fika hata mambo mengine kwenye fikra zao yatakosa uungwaji mkono sanasana litakalo chukua nafasi maalum ni hili lla wao kulala pamoja!

“It was the best romantic scene ever!Watu wawili wasiojuana wanalala pamoja kwa mahaba mazito huku wwasijue kama wanapendana au la!Wote wana watu wao wanaowapenda.Hii inaitwa kuwachanganya kiakili.Na kila uchao watatamani kulizungumzia jambo hili bila ujasiri hawataweza na kila uchao watakuwa na maswali ilikuwaje?Anachohisi mwenzake na yeye ndo anachohisi?Kutakuwa na taharuki kubwa sana kwao mtu hizi mbili!”alisema Mzee Kavu akiangalia matukio yale kwenye tarakilishi.

“Ni mpango wa ajabu sana.”

“Hawatakuwa na amani kati yao hadi watalkapokuwa tayari kulizungumzia swala hili.”

“Naona wameshajiandaa chakufanya walete hapa.”alisema bwana Kavu.Baaada ya muda mfupi Dedani na Shunie walikuwa mbele ya Pilato zee Kavu lenyewe!

“How was your night?”aliuliza zee Kavuu kwa tabasamu la kejeli.Shunie na Dedani walichukizwa kwa kauli ile.Aibu ilizidi kuwatafuna ini na moyo!

“Tambueni ninao ushahidi wa tukio lote mlilofanya ninachohitaji nikubofya kitufe tu halafu na sambaza video hizo wapenzi wenu waone kila kitu!Najua hamtapendezwa kabisa na hatua hiyo.Unachotakiwa kufanya bwana Dedani ni kwenda kwenye mahojiano na kituo cha habari ambacho tumekiandaa.Huko utatakiwa kumsema rais ambaye ni mkeo kwamba humuamini katika ndoa yenu na unataka kumrudia kwasababu unampenda.Lengo ni kuonesha rais haaminiki katika ndoa yake na wewe upo tayari kuonesha umma udhaifuu wa mkeo.Tutamchafua kabisa nakuharibu taswira yake katika jamii.Natumai utatupa ushirikiano mzuri.”

Lilkuwa ombi zito sana kulifanya japo ni kweli kwa shutuma hizo lakini vipi amuaibishe mkewe kiasi kile hasa akiwa na wadhfa wa urais wan chi?

“Kama nikikataa?”alihoji Dedani akitetemeka sana.

“Nani alikwambia una kauli kwa hili!”alisema zee Kavu kasha akaendelea,”Mkeo alijiletea aibu hii sio ya kwako wewe tekeleza kile unachoambiwa!”

“Lakini…”

“Unajua mwanao yupo mikononi mwangu au umesahau?”aliuliza bwana Kavu akiwa na umakini.Sura yake haikubeba mzaha wowote zaid ya umakini wa kuhukumu!Dedani alitumbua macho kama vile mjusi amebanwa na mlango!

“Nipe mwanangu halafu nitafanya unachokitaka.!”

“Mwanao hawezi kutoka hapa hadi nitakaporidhika na ninachotaka ufanze.”alisema zee Kavu. Maandalizi ya mahujiano yalikuwa yameandaliwa.Lingekuwa bomu kubwa sana kwa rais Kilua kwa serikali yake.

“Kuna gari lipo hapo nje utaenda nalo nategemea ndani ya muda mffupi kutikisa anga za habari kwa skendo ya aina yake.”alisema Kavu.Dedani alichukuliwa pamoja na Shunie wakavalishwa mavazi nadhifu na pamoja wakapakizwa kwenye gari tayari kuelekea kituo cha habari kwa mahojiano maalum ambayo yalikuwa yametangazwa kuhusu mtu muhimu nchini kuhojiwa ila matangazo hayakusema ni nani.Promosheni iliyofanywa ingemshawishi yeyote kutizama kipindi kile ingawa hakujulikana muhusika ni nani?

Dedani alikuwa amekunywa kido go kupandisha stimu tayari kwa vamizi kubwa kwenye habari akimshutumu mkewe kuwa msaliti na ushahidi anao!

Alifika katika viunga vya kituo cha televisheni ya Pamekucha katika kipindi maarufu cha NYUMA YA PAZIA.Killikuwa kipindi maalum chenye wafuasi watiifu hasa vikijikita kwenye stori nzitonzito za watu wazito kitaifa na kimataifa.Kipindi kilikuwa kikongwe na maalum kujenga au kubomoa sura za Fulani.Leo wafuasi wa kipindi hicho akiwamo rais Kilua pia walikuwa mbioni kukitizama kupata hatma ya vitendawili vyao.

Dedani alikaribishwa kwenyee studio za Pambazuko kwa shwangwe tayari kupanda studio kwaajili ya mahojiano maalum.Utaratibu ulikamilika nay eye kuketi huku kamera zikianza kuchukua picha!
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 66
hii stori siielewi sehemu ya kwanza ipo fresh sehemu ya pili hamna imeruka mpaka sehemu ya 14 ,,mkuu FANANI MTENZI msaada wako hapo
 
Back
Top Bottom