Riwaya: Kombora kiotani-1

FANANI MTENZI

Senior Member
Jul 4, 2017
106
95
KOMBORA KIOTANI-1

Uwanja ulipambwa kwa tabasamu za wana nchiMagwaride kadhaa yameshapita kutoa heshma zao kwa mkuu wan chi aliyekuwa jukwaa kuu.Mavazi yaliyovaliwa hapa asilimia kubwa yalikuwa yakizalendo hasa kwa rangi zilizopo kwenye bendera ya taifa.Uzalendo ulitukuka baina ya taifa hili linalokumbuka siku ya uhuru wa taifa lao kutoka kwa wakoloni waliowatawala.Kiuhalisi taifa limeshapiga hatua kutoka kwa mkoloni.Kuimarika kiafya,elimu,ulinzi na mengine mengi.Lilikuwa taifa imara na linaendelea kuimarika japo kwa mapungufu kadhaa wa kadhaa.

Jeshi la taifa la KIOTA kwa sasa katika sherehe za uhuru lilikuwa linafanya mazoezi kuonesha wana nchi wake uimara na ukakamavu wa jeshi.Pia walikuwa wakimuhakikishia mkuu wan chi ulinzi uliotukuka.Vyama mbalimbali vya siasa vilikuwepo katika sherehe hii pamoja na viongozi wa kitaifa.Vilevile kulikuwa na mialiko ya mataifa ya kadhaa japo wengi wao walituma udhuru na kuleta wawakilishi wao katika uwanja wa taifa.Ulinzi ulikuwa umeimarishwa katika jiji kuu la nchi ambapo taifa lilikuwa linashuhudia maadhimisho haya.

Rais Kisusi akiwa ameketi meza kuu,pembeni yake alikuwepo mkuu wa majeshi upande mmoja na upande mwingine alifuata naibu rais wake na viongozi wengine.Waliteta na mkuu wa majeshi.

“Kinachofuata ni nini jeneral maana leo sijisikii vizuri sijui kwanini?”aliuliza rais Kisusi.

“Ni mwite daktari?”aliuliza jenerali Tindikali.

“Hapana aliniambia sina tatizo.”alijibu rais Kisusi.

“Itakuwa msongo wa mawazo mkuu.Usijali nchi ipo salama.”

“Na wasiwasi na uchaguzi ujao.Lakini sio kwa hilo ni kwamba roho inanienda mbio sana.”

“Kivipi mkuu?”

Walikuwa maswaiba wakuu tangu shuleni tofauti ni majukumu ya kazi lakini wote ni wazalendo wazawa wa taifa la Kiota walioamua kuitumikia nchi yao.

“Au ni vile majirani zako hawajaja?”

“Hapana Tindikali.”

“Au tuhairishe shughuli?’”

“No!Leo ni dhifa muhimu sana sidhani kama kuna haja ya mimi kuondoka ghafla.Ngoja niimalize then tutaondoka.Unajua file namba 13.14 linanitatiza sana kiasi nakosa Amani.”alisema rais Kisusi ambapo alipitisha kitambaa kufuta kijasho kilichokuwa kina msumbua.

“Lina ufumbuzi hakuna kidudu mtu atakayesumbua.”Alijibu jenerali Tindikali.Waligutushwa na mshereheshaji aliyekuwa akielezea makundi mbalimbali ya ulinzi yaliyokuwa yanafanya mazoezi.

“Halafu Mkuu kinachofuata ni Maonesho ya ndege mpya za kijeshi tulizo tengeneza.”

Rais alipitisha ulimi kwenye papi za midomo yake nakuachia tabasamu hafifu.Akaangalia juu kusubiri maonesho ya ndege.

“Ndege inaendeshwa na Kapteni Pilipili ya kwanza kabisa kufanya onesho lake.Inatoka makao ya Msanda.Mh RAIS unasikia sauti ikizizima uwanja mzima.Haya ni mafanikio chini ya utawala wako.Ni ndege yetu wenyewe MI fighter Jet ian uwezo wa kwenda kilomita mia tatu kwa saa.Ina beba makombora kwa kumshambulia adui.Kwa heshma mh rais Kaptein…”MC alikuwa anahutubia.

Kaptein Pilipili akiwa angani kuelekea uwanja wa taifa kuonesha ndege mbele ya rais wao.Alianza kuhisi mikono mkimtetemeka.Makao yakuongozea ndege yalikuwa yakiwasiliana naye kumpa maelekezo ya kipi cha kufanya.Lakini ghafla alipoingia kwenye anga la uwanja aliekeza ndege moja kwa moja kwenye meza kuu walimoketi Rais na watu wake.Halafu akabonyeza kitufe cha kuachia kombora lakini hakubonyeza la kuruhusu kombora kutoka bali mlango wa kombora ulibaki wazi.Na kwa kasi atakayoenda nayo mpaka kufika kwenye jukwaa halitakuwa limeanguka kutoka kwenye eneo lakuhifadhi bali kama ndege ikiwaka moto au kulipuka bila shaka kombora lingelipuka.Kasi yake ilikuwa ya sekunde.

“Mh Rais kaptein Pilipili ndo….”hata kabla hajamaliza tayari ndege ilipigiza kwa kasi kwenye jukwaa.Kishindo kizito kilikuwa kimejiri.Lakini wakati wa butwaa lile likiendelea kuna mlipuko mwingine ulitokea pale uwanjani!Mlipuko mzito.Moto ulipanda juu na moshi mzito kufuka.Kilio kilikuwa kimesikika kikubwa sana tena cha kuogofya kiasi watu walishtuka ambao hawakupatwa na mlipuko ule.Vikosi vya kijeshi vilivyokuwa pale uwanjani nakubahatika kukoswa na mlipuko ule vili taharuki kwa harka maana mshtuko uliotokea ni waaina yake.Vyombo vya habari kadhaa vilipoteza mawasiliano hasa kamera zilizokuwa karibu jukwaaani.Lakini kwa kamera zilizo mbali kidogo hazikupatwa na kadhaia hiyo.Mambo yote yalionekana mubashara kwenye vyombo vya habari.Taharuki iliyokuwepo katika taifa haikuwa na maeleoz!Nchi ya Kiota ilikuwa taabani.Na kwa haraka tu ilikuwa vigumu kujua ni wangapi walikuwa wamekumbwa na kadhia hii!Ilichukua muda kwa vyombo vya habari kuanza kutangaza kinachotokea uwanjani.Waliopo studio waliona kama ni sinema wana tazama lakini ukweli ni kwamba balaa kubwa lilikuwa limetokea.

Wakati simu zikipigwa maeneo mbalimbali huku vyombo vya ulinzi vikijitahidi kujua ni ktiu ganoi kimetokea hadi ndege ilyokuwa ikirushwa kwa maonesho ikapoteza mwelekeo nakuanguka jukwaa alimokuwamo Rais Kisusi.Jukwaa ambalo serikali nzima ilikuwemo!Ilikuwa maapema mno kubashiri tukio hili ambalo bichi sana!Nchi ya Kiota ilikuwa imesimama hakuna kilichosonga.Waliokuwa karibu na maeneo yale nje ya uwanja walianza kutimua ovyoo.Waliopo ndani walianza kutoka nje msongamano ambao ulisababisha purukushani hadi watu kubanwa chini nawengine kupoteza fahamu.

Taharuki!Taharuki kuu!

Taifa limetetemeshwa!Kiota imeanguka chini kwa kishindo!

****

Makao makuu ya jeshi!TRIANGLE

Meza kuu yahali ya hatari ilikaliwa na viongozi wa kijeshi waliokuwa wamebaki kambini.Kulikuwa taharuki.Hakuna kilichotulia kila mmoja aliongea lake.Simu ikipigwa huku na kule.

“Nimesema tuna tuna tangaza hali ya hatari nakuipeleka kwa kiwango cha DEFCON 3.”alisema kanali Rama.

“Hapana huna mamlaka yakupandisha hiyo amri.DEFCON 3 nikubwa sana wewe huoni ni mwenzetu ndokaangusha ndege.”alijibiwa na Major Kanda.

“Major huu siwakati wa mzaa Kiota imepigwa hatucheki na mtu vilevile nataka kujua ikulu nani anachukua napia nijue nani anajua hali ya rais na serikali nzima.Tukisubiri mambo yaendee kijinga tutapoteza nchi!Tuamue hapa hapa kufungulia vikosi vya kijeshi kuingia mtaani.Hivi.”

“wewe ni nani katika nchi uamuru upuuzi huuo!”

“Huna mamlaka hana mamlaka!”

“Pumbavu hujui lolote nimekufundisha kazi mimi.”

Kila mtu alikuwa na wasiwasi na hasira.Hakuna aliyejua ni uamuzi gani wakuchukua kwa wakati huo.Ilihitajika busara na amani ya hali ya juu.Nchi ilikuwa imetikiswa kwa pigo kubwa kuliko yote pona ya watu ilikuwa na wakati mgumu usio na maelezo yakuridhisha.Hali ilikuwa tete.Hakuna aliyemuamini mwingine.Mfumo mzima wa utawala uliingia dosari ya ajabu.Utamwamini nani?Aliyetekeleza mauaji ni nani?Kwa dhamira gani?Na mpango upi?Ni ajali?Lilikuwa swali lililoshibisha meza nzima ya eneo lile.

“Jamani hebu tutulie natuwe na uvumilivu wa hali ya juu.Nchi nzima inahitaji amani.”alisema moja ya wazee wa jeshi aliye na umri mkubwa.Ni mstaafu lakini mtu mwenye busara alishashinda medani kadhaa kwa juhudi zake jeshini pamoja na ushirikiano mbalimbali alioutoa jeshini.Vyeo Alisha vipata.Pamoja na mambo mengine,alikuwa mzalendo kwa taifa lake huru.Alilipenda.Alilijali nakulithamini kama kwa uzalendo uliotukuka.Mwili wake wenye ngozi iliyozeeka,sharubu zenye uzito halafu nyeupe pamoja na pua yenye mchongo ilimpa sura ya busara.Utuuzima dawa.

“Ni sawa nchi imepigwa pigo kuu.Hii ni ajali mbaya…”kabla hajamaliza alivamiwa kwa kauli zenye utata.

“Sio ajali!”

“Wewe mzee unazeeka vibaya utaitaje tukio hili ajali?Unaona kuna ushawishiwi wa ajali hapo?”

“Huu ni uvamizi tumepigwa na adui zetu.Haiwezekani rubani wa jeshi ambaye ni mwanajeshi aangushe ndege mahali alipo mkuu wa majeshi na amiri jeshi mkuu ambaye ni rais?Hii ni dharau kubwa sana na haivumiliki kamwe!Lile eneo lilikuwa na umma mkubwa.Kulikuwa na mazoezi ya kutosha yaliyofanyika kabla ya leo.Rubani alijua fika anachopaswa kusema sasa iweje adondoshe ndege hapo?”

Mzee Gwamaka alivuta pumzi ndefu na kuzishusha kwa muda akiangalia hali ya hewa kwa ujumla.Alifikiria kidogo kitu gani cha kufanya.Alizitafuta busara zake zilizojificha ndani ya mvi zake.Akapitisha ulimi kwenye baraza la mdomo wake kasha akasema,”Najua tukio lililotokea ni zito.Tena ni kubwa sana.Sio tukio la kawaida.Ni la hatari.Tumepata pigo!Kulalamika sio suluhu.Muhimu tumuombe Mungu atupe ujasiri.Hili sio jambo la mzaa kabisa.Ni jambo lenye huzuni isiyo na mipaka.Kupigwa tumepigwa kweli.Ila sio kwamba ni lazima tuanguke chini kwa pigo hili.”

Wakamsikiliza,wengine walishayaacha makoti yao purazai.

“Ni kweli serikali nzima imetikiswa hatujui nani kapona nani kafa?Bado ni maapema mno.Pamoja na umaapema wote huu hatuna budi kujipanga nakuwa tayari kukabiliana na lolote litakalo tokea.Tuchunguze kwanza,tujue ni nini halafu hali ya dharura itangazwe.Kila sekta iliyopo pale jukwaani ilikuwa na wawakilishi wake.Wengi wao wakiwa ni viongozi wa sekta hizo.Bila kuficha kuna sekta nyingi zenye pengo hivi tunavyozungumza.Zinahitaji wasimamizi wapya ili nchi iendelee.Inaweza kuwa siyo ajali bali ni kundi la kivamizi kwa lengo lakuiadabisha serikali yetu tukufu.Ndiposa natoa tamko kwamba tufuate protokali.Uchunguzi ufanyike wa haraka sana ila tuwe na bodi maalum yakufanya uchunguzi huu pamoja na shghuli za uokoaji.
 
KOMBORA KIOTANI-14

BONIFACE BIRAGE

Kisha akatoa kijitabu Fulani akafungua kurasa akamwambia asome maneno yale punde simu itakapopokelewa.Kisha sekretari akapiga simu kuelekea makao ya kijeshi Kibatari.Mtandao ukawa umeunganishwa.

“Halo!”alianza rais Kilua.
“Yes CIC!”sauti upande wa pili ikaitikia kwa ukakamavu.
“This is C-I-C 1 1 order to shoot enemy trespassing in our airspace scan the air take them down immediately!”alitamka kwa kujiamini Kilua.

“Roger that cic 1 1!”sauti iliitikia upande wa pili.

Kilua akashusha simu ile,”Madam unajua ulichofanya?”aliuliza Sada.

Kilua alimwangalia bila kumwambia chochote huku mikono ikivuja jasho.Mambo yameivaa!

“You have just issued an order to kill someone.”alisema Sada kwa huzuni,Kilua akashtuka.Lakini ndo shughuli ilipompeleka…

Kilua akavuta pumzi ndefu nakuzishusha.Alihitajika muda ule kuwa sehemu maalum maana ametoa amri kushambuliwa kwa ndege ya Kibatari iliyopo kwenye eneo lake.Jambo hilo lilitakiwa kufanywa kwa umakini wa hali ya juu.Tayari keshatoa mari na matokeo yake lazima ataulizwa ilikuwaje akakubali kutoa amri.Je,vyombo vyake vya intelijensia vinajua jambo kiasi cha kushauri nini kifanyike?Hilo lilikuwa kama mtego Fulani uliotakiwa majibu ya hali ya juu.Uzembe wowote lazima utamgharimu kwa maamuzi yake.

“Najua nilichofanya.”alisema Kilua baada ya ukimya wa sekunde chache.Alipitisha mkono kwenye paji la uso kama anajifuta jasho jepesi lililokuwa likifuka kutoka kwenye ngozi yake.Ilikuwa ni kuchemka haswaa.Mambo yamezua mambo na mkuu kawekwa kiti moto.

Wakiwa pale ndani mlango wa kile chumba ulifunguliwa akaingia Serambovu akiwa na umakini kidogo kwenye uso wake.

“Mheshimiwa unahitajika kwenye mkutano.”alisema Serambovu kwa heshma.Kilua alimwangalia tu bila kusema kitu huyu ndo mtu aliyepo karibu kwa wakati ule.Alifikiria sana.Palepale machozi yakaanza kumtoka mfululizo.Serambovu alimsogelea nakumshika mikono akijaribu kumtuliza.Kuna wakati Kilua alitaka kusema ukweli kwamba familia yake imetekwa lakini alikumbuka kwamba Serambovu ni hawara wake wa siri hivyo kumwambia jambo lile lingekuwa mtaji kwa Serambovu kwamba bwana wa Kilua katekwa nayeye angeutumia muda ule vizuri kumshawishi Kilua awe mbali naye.Hilo siyo la msingi kwa wakati ule kumwambia bwana huyu.Alifiha tu.Lakini akawaza kuhusu wanawe wengine wawili.Hao walipaswa kulindwa kwa gharama zozote ilikuwaepusha na hatari hiyo.

“Usijali kila kitu kitakuwa sawa.”alisema Serambovu akimpigampiga mgongo kwa kumpa bembelezi.Serambovu alikuwa ameteka viuno vya mwanamke huyo.

Kilua akajikaza nakuacha kuangua kilio.Kisha alijifuta machozi.Sada alitoa kwenye mkoba wake vifaa vya urembo nakumtengeneza rais vizuri kisha wakaondoka na kwenda kwenye kikao.Ndani ya muda mfupi walikuwa kwenye ukumbi wa vikao.Kilua lipoingia walisimama wote hadi alipowaruhusu kukaa.

“Ajenda kuu leo tunaomba tuangalie swala lililopelekea ajali ile iliyoua viongozi wote wa serikali.”alisema Kilua akisoma muongozo uliopo mezani mwake.

Mbele yake walikuwepo kamati ya ulinzi.Kuna msururu wa kamati nyingi unaotakiwa kuonana naye.Kazi ile ilikuwa na mambo mengi sana kiasi ilimchanganya Kilua katika kufanya maamuzi sahihi.Michango mbalimbali ilitolewa pale mezani kila mmoja akieleza kwa upande wake.

“Tunasubiri ripoti toka kwa vyombo vyetu vya usalama.Lakini kwa mtazamo wa kwanza kuna tetesi kwamba jambo hili halikuwa ajali tu.Rubani Kaptein Kipilipili alikuwa sawa kabisa siku ile na hata alikuwa amefanya mazoezi ya kutosha kwaajili ya zoezi lile.Lakini cha ajabu nikule kutokea ajali ikiwa anajuafika pale kulikuwa na umma mkubwa.”

“Inawezekana kuna hitilafu za kiufundi.”

“Isingekuwa rahisi kuangusha ndege eneo lile.”

“Kwani tunachoangalia hapa ni kitu gani kuhusiana na tukio hili?Was it normal accident?”mwingine akauliza.
“Hapana.”alitamka kiongozi wa DCU wote wakamtizama kwa mkupuo.

“Unajua tukio zima lilikuwa la ghafla natumejaribu kuangalia tangu jana sekta zote kwa ule uchunguzi wa mwanzo ndege isingeanguka kirahisi.Pili kuanguka kwa ndege…ukiangalia ndege yenyewe haikutakiwa kutoa mlipuko mkubwa kiasi kile.Kumaanisha kulikuwa na milipuko zaidi ya mmoja!Kwa ukaguzi ndege ile ilivyoundwa hata kama ingetokea ianguke inauwezo wakujidhibiti isitoe mlipuko mkubwa kiasi kile!Pili ilipoanguka inaonekana fika muongoza ndege aliyekuwepo control tower alikuwa akimpa maelekezo vizuri sana rubani isingekuwa rahisi asijue kama ndege ina hitilafu.Upembuzi zaidi unaonesha rubani hakutoa taarifa kwamba alikuwa na tatizo katika udhibiti wa ndege ile.Ina maana aliipeleka moja kwa moja akijua anachoenda kukifanya!”director alikuwa anatoa ripoti aliyopokea kutoka kwa timu yake iliyofanya uchunguzi hii ilijumuisha DCU 1 na DCU 2

Watu wakaduwaa!Ilikuwa habari nzito sana kutolewa.Lakini kwa kuwa chombo hicho kilijulikana kwa kuwa na weledi wa hali ya juu wasingeweza kukwepa ripoti yao iliyoenda zaidi ya vile kila mmoja alivyotazamia.

“Una maanisha nini director Masha?”aliuliza rais kwa mshtuko.

“It was a suicide mission perfomed by Captain Pilipili!”alisema kwa sauti yenye ukavu kidogo huku macho yake yakithibitisha ukakamavu Fulani wa kijasiri!

“Una maanisha mwanajeshi wetu mwenyewe aliamua kuangusha ndege maksudi jukwaa walimoketi viongozi wa serikali?”

Director aliwaangalia kwa jicho Fulani kila mmoja abebe ugunduzi huo mpya!Hilo lilikuwa na maana nzito sana kwani nikupeleka lawama jeshini.Viongozi wa kijeshi waliokuwa pale wote walionesha mshtuko wa hali ya juu.

“Kama ni mwanajeshi ina maana yalikuwa mapinduzi?”aliuliza mwingine bila kuonesha dhumuni la kauli yake.Aliijibu kwa njia ya swali!

“Ndiyo yalikuwa tukisema ni mwanajeshi wetu alishiriki kuua serikali nzima itafasiriwa kama mapinduzi ya kijeshi na hilo halitaiweka nchi yetu pazuri ni hatari kubwa sana!Wageni tunaotegemea kuja watakuwa katika sintofahamu kama Kiota ni paradise tena.”alishauri mwingine.

“Sasa…”alikwama Kilua akikosa cha kusema.

“Nina uhakika haikuwa ajali hiki kitu kilipangwa!Tayari tumekuta kuna ushahidi wa bomu kulipuka eneo lile muda uleule ambao ndege ilianguka.Pia makombora ya ndege yalilipuka pamoja.Vitu vitatu.Mlipuko mdogo wa ndege,pili mlipuko wa makombora yaliyokuwepo kwenye ndege na tatu mlipuko wa bomu la kutegwa hapa sina shaka.Ni ukweli bomu lilitegwa kabla ya shughuli kuanza.Ina maana muda wote wakiwa kwenye shughuli bomu lilikuwa chini yao!”

“Nashauri taarifa hii istolewe kwa umma bado kuna shida kubwa.Rais anatakiwa atoe hotuba muda simrefu watu wanangoja kumsikia kiongozi wao!Lazima aende na majibu kwa wananchi wake.Majibu ya matumaini nasio jibu la jeshi kuhusika katika kumuondoa rais Kisusi na serikali yake madarakani!”alishauri mwingine.

Kilua alionekana kuogopa kwa upande Fulani.Yeye mwenyewe kuna vitisho vinamuandama.

“Kama ni mwanajeshi alifanya tukio hili basi hatuna budi kuchukua hatua za haraka kulinda nchi na utawala wa rais Kilua.Uchunguzi ndani ya jeshi ufanyike wa haraka na wote walioshiriki wawekwe vizuizini kwa uhaini!”alisema Serambovu.

“Utawala wa rais Kilua lazima utunzwe kwa gharama zote.Japo ni mwanajeshi mmoja hatuwezi sema ni jeshi zima.”moja ya maafisa wa jeshi alitamka hilo.Jambo hilo likapingwa vikali.

“No!Hata kama ni mmoja lazima kuwe na mnyororo wa watu waliopanga jambo hilo.Hatua lazima zichukuliwe kwa haraka sana.”mjumbe mwingine aliingilia kati.

“Ok.Natoa oda.Nataka uchunguzi ufanyike kwa siri sana na mtu yeyote asitumie jambo hili kumwingiza mtu kwenye conspiracy hii bila kuwa na uhakika.Najua inapotokea hali kama hii kuna wanaotokea kuingiza wasio na hatia ndani ya muda mfupi nchi yetu itakuwa na wageni wengi.Lazima tuwe imara wakulinda amani yetu.Sitapenda kuona tukiigeuza nchi jangwa.”alisema Kilua ambapo wenzake walitii amri.

“Kikao nakiharisha nahitaji kuongea na taifa kwanza.”alisema Kilua ambapo aliinuka muda ule.Wote wakasimama nakumpa heshma zake kisha akaondoka kwa haraka.Mwili wake ulitetemeka.

Kila alipomuwaza mwanaye na mumewe alikosa amani.

Waandishi wa habari walikuwa tayari wakingoja tamko la rais wao.Kamera zilikuwa zimfungwa mahsusi kwa hotuba hiyo ya kwanza kabisa Kilua kuitoa.Nchi na dunia ilikuwa tayari kumsikiliza rais Kilua.Aliomba akae kwenye meza.Aliketi pale kisha akaendelea kutoa hotuba yake.

“Tukio hili laweza kuwa limetafuna misingi ya jukwaa walimoketi viongozi wetu nakutujaza huzuni.Lakini haliweza kutikisa uimara wa imani yetu katika kusimamisha taifa letu hata kama tumeguswa pabaya.Tumesimama.Tutasimama kuliinua taifa letu.Kiota iliyokumbwa na huzuni itasimama.Hata waliotutangulia hawapendezwi na sisi kujikunyata kwa huzuni tukiliacha taifa letu lianguke.Wangependa tuwaenzi kwa kulisimamia imara!Nchi ni wewe.Tusikubali kushika tama.Kama rais wenu nawahidi kuilinda nchi yetu kwa gharama zote kuhakikisha usalama wa taifa letu unakuwa wa kwanza.Hakuna mwanadamu aliyepanga mimi kuwa rais wenu bali matendo Mungu anayopanga leo ni mtumishi wenu katika kiti cha urais.Nitalitumikia taifa langu kwa kipindi chote nitakachokuwa madarakani nakuhakikisha nchi inazidi kusonga mbele.Temepanga na kuaandaa maandalizi ya msiba wa taifa ambao utakuwa wa pamoja…”

Aliendelea kutoa hotuba yake.Watu walimsikiliza lakini kukawa na tatizo!Rais wa Savanna lands alikuwa mbioni kujibu mashambulizi baada ya ndege yakle ya kivita kutunguliwa na majeshi ya Kiota!
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 120
KOMBORA KIOTANI-15

BONIFACE BIRAGE

Ilibidi aharakishe mazungumzo yale maana kulikuwa na tatizo kubwa linaenda kutokea.

Watumishi waikulu walimfuata rais mmoja wao alimwambia anahitajika haraka chumba cha hali ya dharula.Rais ilibidi afupishe maelezo nakumuachia msemaji wa ikulu aendelee na mazungumzo.Kilua alitoka kwa haraka nakuongozana na walinzi wake kuelekea chumba cha dharula.Kule alikutana na timu ya wajumbe wakiwa tayari kwenye meza ya kikao.Walisimama walipomuona rais wao.

Kilua aliketi chini nakuwapa ishara wa keti.

“Kuna nini?”aliuliza.

“Tumepokea taarifa kwamba jeshi letu limetungua ndege ya kijeshi ya Savanna Lands muda mchache uliopita.Na taarifa zaidi zinasema serikali ya Savanna Lands imetuma vikosi vyake vya kiusalama kwenye ubalozi wetu uliopo kwao.Kuenda kwa vikosi hivyo siyo ishara nzuri!”
“Ilikuwaje ndege ikatunguliwa?Who gave the order?”walijuliza pale mezani.Kilua aliwatizama alichokiamua kimetoa matokeo na kweli hakuwaambia kama angefikia uamuzi huo.

“Mimi nilitoa amri hiyo!”ilisikika sauti ya rais Kilua,kitu ambacho kiliwashtua wengi.Hawakujua kama alikuwa na jeuri hiyo.Kiongozi aliyeonekana dhaifu kapewa madaraka wakaujua angefeli lakini cha kushangaza siku ya kwanza tu ofisini hata masaa 24 hayajaisha tangu aapishwe katoa amri kutungua ndege ya taifa lingine!Hilo halikuwa jambo la kawaida kabisa!Ni tishio kwamba rais anaelekea kuanzisha vita na taifa jirani!

“Mheshimiwa?Ilikuwaje ukatoa amri hiyo?”

“Ilinibidi nifanye hivyo walikuwa wanachezea anga letu.Nimeshapokea vitisho kutoka kwao so I had to act incase they pla with us!”alijitetea Kilua.Kila mtu alijishika kichwa kwa wakati ule.Ilikuwa taarifa mbaya sana kuipokea hasa kwa siku kama ile.Tayari walikuwa na mambo mengi mbeleni yakushughulikia tena lina jiri hili katika wakati mgumu kama ule.NI wazi kwamba utawala wa Kilua ulikuwa katika wakati mgumu baada yay eye kutoa amri kushambuliwa kwa ndege ya kivita iliyokuwa ikipita kwenye anga lake.

“Mheshimiwa tukio ulilofanya ni hatari sana!Umeua mwanajeshi wa Savanna Lands they will seek revenge!Tunategemea wageni hapa kwenye msiba huu wa taifa itakuwaje wakijua kwamba leo umetoa oda kutungua ndege ya jirani yetu?”moja ya wajumbe alihoji.

Kilua alikosa jibu akikumbuka alifanya vile kwa shinikizo la mwanaye na mumewe wapewe chakula alijihisi kuwa kiongozi dhaifu anayefuata hisia binafsi bila kuweka utaifa mbele.Ni kweli ndege ya Savanna Lands ilipita kwenye anga lao na bila shaka walitakiwa kujibu japo yeye aliwahi kutoa maamuzi.Kusema alipotoa taarifa ile lilikuwa jambo zito sana!

“Tupo katika hali ngumu ya kidiplomasia na nchi ya Savanna Lands bila shaka tujiandae kwa lolote.”

***

Kulikuwa na kikao cha siri sehemu Fulani kando ya mji mkuu wa taifa la Kiota.Kikao kilifanyika pembezoni mwa bahari.Mawimbi yalipiga nakuja na harufu ya chumvi ya bahari.Tetemo la upepo uliokinzana kwa pambio za mawimbi ulitengeneza mandhari tulivu iliyoshiba.Kulikuwa na vibosile wane wakiwa kwenye viti vyao.Wameshiba maisha yao.Njaa haikuwa taabu kwao labda tu mwenendo wa mambo.Suti zenye uzito wa ukwasi zilikaa vyema kwenye miili yenye vitambi vya utajiri kwa nakshi za rangi mbalimbali.

“Tayari ameshaingizwa kiongozi mpya.Lazima tufanye hatua inayostahili.”mmoja wa mabosi wale alizungumza kwa sauti yenye ukavu.

“Ndiyo tunatakiwa kuharakisha kuweka mizizi yetu kabla wengine hawajaanza kushika serikali vizuri.Pia lazima kila sekta tuweke watu wetu angalau tuwe na asilimia ya uhakika wa kulindwa.”mwingine alijibu akiwa ameshika glasi ya kinywaji akapiga funda mbili.

“Mnaonaje tukitoa mchango wa viti katika msiba huu kama njia yakuanza kupenyeza mizizi yetu?”mwingine aliongeza hoja kwenye kikao hiki.

Walitikisa vichwa kuonesha kufurahishwa na hoja hiyo.Walikuwa na ajenda zao.Haya ndo mambo yaliyokuwepo katika taifa hili kwa wakati huo wenye shaka kuu.Kila mmoja alijipanga kivyake hasa kwa kujua utawala mpya umeapishwa kwa hivyo lazima wajichimbie mizizi yao.

“Lakini ajenda yetu ile ya Kibatari ibaki kama ilivyo.Wakubwa wameshasema wataanza ile ajenda na watahakikisha hakuna wakuingilia chochote.Tayari vitendea kazi vina karibia kuingizwa nchini muda simrefu lakini kwa taarifa nilizopata jana kikaoni ikulu rais hakuwa ameongeza viwango vya usalama hivyo shaka haipo.Bahari ipo shwari na hata bandarini hakuna taabu.Mzigo utaingia kwa haraka sana.”alisema bwana Tufe.Wote walimgeukia.Walikatizwa kidogo na binti aliyekuja na sinia la vinywaji alivitenga pale mezani kwa ustaadi mzuri.Alivalia nguo nadhifu suruale nyeusi na shati la pinki pamoja na kizibao cha rangi nyeusi.Uso wake ulijaa ushaufu,alijikwatua kwa tarabizuna zenye utuli wa kushawishi kiasi mabosi wote waliokuwepo pale walijikuta wakiivuta utuli wake.Kila mmoja aliwaza lake.Halafu binti aliwapa tabasamu la kiasili la ukaribishwaji.Kisha aliondoka na ndani ya dakika moja alirudi na sinia lingine la nyama choma.Aliweka vitu hivyo mezani kwa heshma zote.

“Karibuni.”aliwapa tabasamu.Vibosile wetu walitamanika na ukaribisho huo.Huku uchu wa mate ukiwachachua midomoni mwao.

Wakati binti akiinuka kuondoka alipigwa kikofi cha kalio akaruka kidogo,”Aah!”alitoa mlio wenye mbwembwe.Bwana Tufe alimkonyonyeza huku msichana akitabasamu.Halafu alimpa ishara waonane baadae.Ishara ilieleweka.

Wakiwa pale walikamata minofu ya nyama nakuanza kushughulikia kwa utamu wake.Walioguguna mifupa walipata wasaa kushughulika kama jamvi kwenye shughuli.Mlo uliwaweza wakishushia na vinywaji vyao vizito.Walimalizia kwa mazungumzo ya kawaida.Ni kwamba watu hawa watalala katika hoteli hii kwa siku ile.Baada ya milo na mazungumzo ya hapa na pale bwana Tufe aliinuka kuelekea kilipo chumba chake wenzake walicheka walijua anachokifuata ni Yule msichana.Alisugua kitambi chake nakuondoka kwa haraka hadi kilipo chumba alichokodi.Alifika nakukifungua maana tayari kulikuwa na mtu ndani.Bwana huyu alimuona Yule msichana akiwa kajifunga khanga akjilaza juu kitanda kikiwa kimetandazwa asumini.Msichana alitabasamu alipomuona mzee wake.Akiwa kapatwa na pombe kidogo kuchwani alichapuka baada ya kufunga mlango akamshukia binti Yule pale kitandani.Kwa mbwembwe alianza kumpapasa.Msichana alikutana na harufu ya nyama pamoja na pombe japo hakuipenda harufu ya pombe ilibidi tu acheze ngoma hiyo isiyo yake.

Mzee aliparamia huku binti akimvua koti.Alimpindua mzee kwa haraka kwa ustaadi wa hali yajuu.Mzee akawa chini na msichana akawa juu yake.Msichana alianza alifanikiwa kuondoa koti lile.Akaikamata tai nakuifungua kisha akafungua vifungo vya shati ya mzee.Mzee alikuwa na uchu uliochungulia kwenye kichwa ukiumuka kwa joto la hawaa.Msichana alijua fika jambo moja tu lingemsaidia kwa wakati ule ni kumpa huyu mzee anachotaka!Wakati anaiendea suruale yake alishtushwa na mlio wa simu uliokuwa kwenye mfuko wa suruale yam zee Yule.Msichana alimsaidia mzee kuitoa ile simu nakumpa.Mzee aliipokea kwa kuangalia pembeni.Alipokea maelezo Fulani kisha uso ukabadilika!

“Habibi kuna nini?”msichana aliuliza kwa kujali.

“Siunajua tena mambo yamebadilika mzigo wetu unaoingia utakwama.”mzee alisema akiwa ameshika kiuono cha msichana Yule.

“Kwani vipi.”msichana aliuliza.Mzee alichukua simu yake tena aakaandika ujumbe Fulani kisha akautuma kwa watu kadhaa. Wakati alibaki kimya iliasipoteze pointi.

“Naskia rais alitoa oda ndege ya Savanna Lands kutunguliwa.”

Msichana akashika mdomo kwa mshangao,”Mtumee!”

“Bila shaka viwango vya usalama vitapandishwa na kila kona kutakuwa na ulinzi mkali.Hii itatuletea shida kwa mzigo wetu kupita bandarini.”alisema mzee akiendelea kupapasa kiuno kibichi cha msichana Yule.

“Pole habibi wangu sasa itakuwaje?”

“Ndo nimewaambia wenzangu wajue kabla hatujachukua hatua nyingine.”

Msichana alishika kifua cha mzee akapapasa kisha akamata chuchu nakuziminya ukapita mshtuko wa shoti ya umeme.Mzee alifumba macho nakujibana.Tayari binti alikuwa anamtawala.

“Kwani ni mzigo gani huo habibi?”aliuliza kwa deko za kike.Mzee alikuwa amefumba macho akisikilizia utamu wake.Binti aliziminya tena chuchu za mzee kama ana finya hivi hadi mzee wawatu akajikuta akikaza makalio!

“Kuna mambo mazito nitakwambia utakapokuja.”

Msichana aliendelea na zoezi lake akizidisha utundu na njonjo za hapa na pale ilimradi bwana Tufe ajihisi yupo peponi.Alipoona msichana anazidi kumfanyia shere alimkamata kiuono nakumuinua juu kidogo.Alimpa ishara amfungue zipu ambapo binti alitii nakutekeleza agizo la bwana Tufe.Ndani ya sekunde chache walikuwa dunia yao.

***

Shuni alikuwa alikuwa anakatiza njia kutoka mtaa wao.Kwisha muacha bwana Tufe kule kwenye ngome yao.Shuni alienda moja kwa moja hadfi kwenye moja ya majengo yao ya kazi.Alifika kwenye jingo nakuingia ndani.Alikutana na bosi wake aliyekuwa amejimwaga kwenye kiti. Shuni alipomuona bosi alipewa ishara ya kuketi.

“Agent unaendelea?”

“Tupo pazuri lakini kwa sasa naona wamechanganyikiwa baada ya rais kutoa amri kutungua ndege ya Savanna Lands.”alitoa taarifa Shuni.

“Kwanini inavyoonekana mzigo wao ni shehena kubwa.”

Bwana Toti alikunja ndita kwa umakini,”Shuni good job kama ameweza kudokezea kwako basi anaelekea kukuamini.”

“Bosi nimefanya kila namna naelekea kupata ukweli.Huyu Tufe ni msiri sana.Nahisi itakuwa ni shehena la madawa ya kulevya.”

Toti alizidi kupagawa,”Tukikamata ishu hii lazima turudishe heshma kwenye idara yetu ya usalama wa taifa KISS.Nakuhakikishia jambo hilo.
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 107
KOMBORA KIOTANI-16

BONIFACE BIRAGE

“Ndiyo hilo litampa mheshimiwa Kilua uwajibikaji wetu na lazima atutambue.”alisema bwana Toti.

‘Kwa maelezo ya Tufe ni kwamba shehena inaingia leo usiku ingawa wana mashaka na ujio wa usalama.Hivyo tutafanya ushushushu kujua kuna nini kwenye shehena hilo usiku wa leo.”alishauri Shuni,shushushu hatari sana katika ardhi ya Kiota.Ukimuona ni binti mlaini asiye na makuu mpenda mpole.Lakini alikuwa ni mtambo unaoweza kusavaivu popote pale.

“Ok tutaandaa kikosi cha uhakika muende kwenye eneo husika nashauri muwe makini.”

“Bosi naomba Pablo asiwepo kwenye hiki kikosi!”aliomba Shuni kwa bosi wake.

“Kwanini?”
“Amekuwa akipinga sana mimi kushiriki kwenye operesheni hii?”

“Nilisema msiwe na personal issues kwenye kazi.Unakumbuka mafunzo yako yanasemaje?”

“Ndiyo bosi.”aliitikia Shuni.

“Mkiwa hapa hakuna cha mambo ya binafsi.Hapa ni kazi tu.”alisisitiza bosi Toti.Shuni alimuelewa bosi wake.Shuni aliinuka kwenye kiti nakwenda chumba cha silaha.Alitoa kifaa chake cha mawasiliano akaandika namba kadhaa kisha akafanya mawasiliano nakuita wakala kadhaa ambao wangeshiriki pamoja katika operesheni kabambee anayokwenda kuifanya.Aliwapa muhtasari kuhusiana na shughuli hiyo.Wote walikuwa na weledi wakutosha katika kufanya operesheni hiyo.

***

Ikulu

“Napandisha kiwango cha usalama hadi defcon 3 majeshi yetu yote yapewe taarifa hiyo.Savanna Lands wakiwa tayari tutakabiliana nao muda wowote meanwhile nataka majina ya viongozi wote wa jeshi nataka kuteua jenerali.”alisema Kilua akiwaambia viongozi wa jeshi waliokuwa kwenye kikao.Ilikuwa ni tamko lake.Alikuwa na kibarua kizito sana kukabiliana na vyombo vya habari pamoja na simu kutoka matifa mengine wakihoji hatua yake yakutungua ndege ya Savanna Lands.Tayari taifa la Savanna Lands lilianza kutoa malalamiko kuhusiana na hatua ya Kiota kutungua ndege yao.

Presha ilipanda kila kona na yote ilihitajika majibu ya rais Kilua aliyekuwa na wakati mgumu sana kuelezea.Muda mwingi alikuwa akishughulikia mambo mengine huku wasaidizi wakijitahidi kujibu maswali ibuka dhidi ya serikali hiyo.Utata ni kwamba jana taifa hilo limepatwa na msiba mzito wakufiwa kwa viongozi wa serikali baada ya ndege ya kijeshi kuangukia kwenye jukwaa walimoketi viongozi wa serikali leo jeshi hilohilo linatungua ndege ya jeshi la nchi jirani.Swali lilikuwa kubwa je,ni Savanna Lands waliosababisha ajali ya jana?Kamati ilikubaliana kutokuleta habari kuhusiana na serikali kushuku ajali iliyotokea kuwa ni mkono wa mtu!Sasa tayari maswali yameanza kuzuka.

Kilua alikuwa kwenye kipindi kigumu sana!Ni siku nyingine lakini tayari ugumu unazidi.Alitamani kuachia madaraka!Lakini alijikaza.Nafasi pekee yakuokoa familia yake ni kubaki madarakani.Majina yaliletwa mbele yake aliyapitia pamoja na wasifu wa watu hao akitaka kumteua mkuu wa majeshi haraka iwezekanavyo maana hali ilikuwa tete kwa wakati ule.Alihitaji mkuu wa majeshi tena wakuaminika.Ndani ya muda mfupi anaenda upekua jeshi pande zote apate majibu ya kwanini mwanajeshi aliangusha ndege nakuua serikali nzima!Kuna usaliti katika taifa.

Kilua alielekea kwenye ofisi yake walinzi wakimsindikiza.Aliingia nakuachwa mwenyewe huku akipitia orodha ile.Lakini ndani ya muda mfupi aliingia Serambovu nakuichungulia orodha kisha akatabasamu.

“Kanali Lupogo anafaa kwa kazi hii.”alisema Serambovu.

“Amefikia viwango vyote vya kuwa jenerali?”

“Wewe ni amiri jeshi unampa yeyote tafadhali mteue.”wakati huo Serambovu alishampigia simu kanali Lupogo aje ikulu kwaajili yakupokea madaraka.Na tayari alikuwa amefika hapo.

“Nataka nimteue haraka sana sitaki tuchelewe Kiota inahitaji kusimama.”alisisitiza Kilua hasa akijielewa hana kauli kwa bwana huyu.

“Kanali anakusubiri kupewa madaraka.”alisema Serambovu.Kilua alimwangalia nakushukuru maana Serambovu anajua kupeleka mambo haraka hivyo anatua mzigo.Aliinuka nakuongozana naye hadi eneo maalum la kumuapishia kanali Lupogo.Kwa jinsi mambo yalivyofanyika hali ilikuwa tete.Ndani dakika kama thelathini ikulu ilitulia kushuhudia kanali Lupogo akiapishwa kuwa mkuu wa majeshi ya Kiota.Zoezi lilisimamiwa na rais Kilua mwenyewe.

“Nimeamua kumwapisha kanali lupogo kuwa jenerali wa majeshi yetu pia hafla hii itafuatia kwa mimi kumteua Bi Sada kuwa katibu mkuu wa serikali.Hivyo tushirikiane katika zoezi hili.Kiota ina hitaji uongozi na mambo lazima yaende.Najua bunge lingetakiwa kupitia wateule hawa kabla ya kuwapa mamlaka lakini huo muda ni mchache natunahitaji watendaji.”

Chumba kilikuwa kimya wakati rais Kilua akizungumza.Zoezi lilianza mara moja.Kiota ilikuwa imepata mkuu mpya wa majeshi pamoja na katibu mkuu mpya.Cheo cha ukatibu mkuu ilikuwa kidogo Sada akatae maana alijua angeandamwa na faili namba 13:14

***

Mlio wa boti ulikoma punde walipofika usawa waliotaka wa bahari.Walivalia mavazi yakupigia mbizi pamoja na vifaa vya kupumulia.Giza lilikuwa la kiasi litandazwa na mwanga hafifu wa mbalamwezi angani.Uwepo wa nyota ni kiasi tu.Bahari ilikuwa shwari kwa usiku ule wenye utulivu.Injini ya boti ilikimya na kuacha sauti ya maji ambayo kutokana na utulivu wa bahari ilikuwa kiasi ya kuliwaza.Shuni na kikosi chake wakiwa na mavazi yao maalum kwaajili ya uchunguzi walivalia vifaa vyote nakurukia kwenye maji!Chubwi!Waliingia huku mavazi yao yakitota kukutana na maji ya bahari.Walianza kupiga mbizi.

Walikuwa na uhodari wa kuogelea kwa mwendo mrefu bila kukata tamaa na hivi walikuwa na vifaa vya kupumulia kazi ilikuwa rahisi kwa upande wao.Waliendelea kuogelea kwa umbali Fulani.Masikioni walikuwa na vifaa vya mawasiliano maalum.Pamoja na vifaa vya kufuatilia vya satellite vilivyoonesha usawa waliopo kwenye uso wa dunia.Baada ya muda mfupi walikuwa usawa husika ambapo kulikuwa na meli inaelekea bandarini.Waliogelea kwa kasi kidogo hadi walipoifikia meli yenyewe.Walifanikiwa kupanda kwenye meli hiyo bila kujulikana na yeyote kwa usiri wa hali ya juu na ustadi mkubwa.

Walitegemea kukutana na upinzani mkali ambao ungehatarisha usalama wao.Walifanikiwa kuvua vifaa vyao vya usafiri kwenye hasa vipumulio wakaviweka mahali ambapo mmoja wao alibaki anavichunga.Ilikuwa operesheni ngumu hasaa ukizingatia hawajui ni meli aina gani inakuja.Walikuta ni meli kubwa sana iliyobeba shehena kubwa ya makontena!Shuli alikuwa na kamera maalum iliyokuwa imehifadhiwa kwenye vifaa maalum kukwepa kuloana.Alianza kuchukua picha za mnato pamoja na maeneo kadhaa ya ile meli.Waliingia hadi ndani nakuchukua picha nyingi za mnato.Waliona watenda kazi wa meli wakiwa bize na shughuli nyingine wakijiandaa kutia nanga.Mpango wa Shuni ulikuwa kuchukua ushahidi wa kutosha kabla meli haijatia nanga.Zilikuwa zimebaki umbali mchache meli ifike bandarini walichokifanya wao kina Shuni walishukia mbali na bandari kisha wakaiwahi meli nakuizamia kabla haijafika bandarini.Walishukuru hawajaonekana hadi kuingia sasa ilibaki kazi moja tu kuchukua ushahidi wa kutosha.

Moja ya kontena walikuta lina kauwazi kidogo.Shuni alijizamisha humo nakuchukua picha za kutosha mlikuwa na vifaa vingi vikubwa vikiwemo mabomba makubwamakubwa!Shuni alikuwa mwepesi katika kuchukua picha zile kwa haraka!Wakiwa pale walisikia vishindo nyuma yao!

“Nyie kina nani?”sauti kavu iliuliza!Shuni aliuma meno kwa hasira alipogeuka walikutana na mtu mwenye miraba mine akiwa anawaangalia!Palepale bila ajizi walianza kumshambulia maana ikitokea huyu mtu akapiga kelele watakuwa wamekwisha.Wakati haya yanaendelea Toti alikuwa akisikia hatua zote kupitia vifaa vya kupitishia sauti!Mapigano mazito yalifanya kazi kwa takribani dakika tatu hadi wakafanikiwa kumzidi bwana Yule nakumuangusha chini walimpiga akazimia!

Shuni alitegemea kupata shehena kubwa la madawa ya kulevya lakini tofauti alikutana tu na vyuma vikiwa vimepakiwa!Kwa kuvitambua aliona vifaa kama drill line,drawa-works,stand pipe,crown block.Kwa akili ya haraka alijua fika hivi ni vifaa mahsusi kwaajili ya kuchimbia mafuta!Baada yakuona hakuna umuhimu aliwapa ishara wenzake waondoke eneo lile.Zile picha alichukua memory kadi kutoka kwenye kamera akaiweka kwenye simu yake kisha akazinyonya picha zote halafu akazituma kwenye barua pepe yake.Tayari ameshatoa kopi za kutosha.Walianza kutoka kwa uangalifu warudi majini.Walipofika eneo walipomuacha mwenzao aliyekuwa analinda vifaa vyao vya kupumulia majini walimkuta kaanguka chini akiwa katoa macho huku kwenye kifua kukiwa damu!Kitu chenye ncha kali kilikuwa kimepenya kisawasawa!Wote wakataharuki!Walikuwa wamegundulika!Wakati Shuni anataka kuegeuka watafute njia nyingine alishtukia kitu chenye ugumu wa chuma kikimpiga kwenye kisogo akahisi kupoteza fahamuAlijikuta akilewa kwa ustadi mkuu aliitupa simu yake baharini!Akaanguka chini nakuwa kimya!

Waliomtwanga waliwapiga na wenzake!Wote walikuwa kimya!

Hatua nzito zikasikika akatoea mtu mzima mmoja mzungu!Alikuwa kavalia miwani ya macho!

“Ni kina nani?”aliuliza akiwa amekunja uso.Hakupendezwa na ujio wa watu hao kwenye meli yao!

“Bado hatujajua wameingiaje lakini kwa mavazi walikuwa wanaogelea.Hawa sio watu wakawaida hadi wavamie meli yetu usawa huu!Walikuwa na nyambizi nini?”aliuliza mmoja ya walinzi.

“Nadhani tutawaua wote halafu tumbakize mmoja tu.Huyu mwanamke ndo atajibu kila kitu wamewezaje kuingia humu ndani.Ila nataka tuongee na informer wetu wa ikulu aweke mambo sawa.”alisema Yule mzungu.

“Bosi hii imeshakuwa mbaya kwa sisi kuvamiwa na wazawa kwenye meli yetu.Ni nani kafanya uzembe huu hadi watu hawa wajue kwamba meli yetu inakuja usiku huu?”aliuliza moja ya walinzi.

“Ndo maana nasema hadi niwe na majibu na informer wetu wa ikulu.Lazima tujue anayevujisha hizi habari.Au labda hawa wawe maharamia ndo mnishawishi!”mzungu alijibu vile.

Palepale mzungu aliondoka akiwaacha walinzi wanaowachukua mateka wao nakwenda nao hadi ndani nakuwafunga kwenye chumba!

Mzungu aliingia kwenye chumba cha kuongoza meli.Alichukua simu ya mkononi nakubofya namba Fulani.Kulikuwa na maelekezo mazito anaenda kuyatoa!Ni nani anayepigiwa simu ikulu!
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 96
KOMBORA KIOTANI-18

BONIFACE BIRAGE

Director Masha alipigwa na butwa pamoja na bumbuwazi lenye kukereketa ini na moyo.Kichwa kile kilizidi kumtisha hasa baada ya kuwa na hakikisho kwamba mume wa rais Kilua yupo mateka.Sasa linapokuja swala lakumuandika rais kuwa anamchepuko lilizidi kumtishia na kudhaifisha ustaarabu wa rais Kilua.Ni kweli rais huyo anapitia kipindi kigumu na wakati sio wa kuja na habari kama hizi zenye kumkashifu nakuitia doa heshma yake.Alipitia habari ile inayomshtumu Kilua kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine amabaye siyo mume wake.Pia habari hiyo inahoji uwepo wa mume wa rais Kilua maana haonekani ilihali rais anahusishwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu mwingine ambaye ni stafu wake!

Hilo lingeilazimu stafu nzima ya ikulu iwe matatani hasa kwa kipindi kama kile chenye wingi wa mashaka na huzuni.Iwe kweli au uongo habari ile ilihitajika kudhibitiwa sana.

“Inachapishwa leo hii habari?”
“Ndiyo leo inahitajika iwe sokoni.Magazeti yamechelewa kisa hii habari niliokuwa nakutafuta sana tangu jana ukawa bize.Nilitaka uijue kwanza kabla habari haijaenda hewani gharama za magazeti yote ni kwa kila nakala ni milioni 40!”alisema mhariri wa habari ile bwana Sudi.

“Una maanisha nilazima habari idhibitiwe kwa pesa?”
“Ndiyo la sivyo hatuna bahati.Your President will get it from me.”
Masha alitaka kuchomoa bastola yake lakini akakumbuka sheria hairuhusu hawa ni waandishi wa habari wana uhuru wao.Muda ule haitakiwi kabisa kuingiza ubabe japo habari yenyewe imekuja wakati mbaya.Alivuta pumzi ndefu na kuzishusha.Hili lilikuwa jambo zito na lazima lidhibitiwe kwa nguvu zote anazojua.

“Nipe kopi ya hilo gazeti naenda ikulu mara moja naomba usisambaze gazeti hili hadi hapo nitakapokujulisha.”alisema Masha akiwa anasisitiza ujumbe wake.Sudi alionesha kumwelewa.Sudi alikuwa na tabia kama hiyo yakutoa vitisho katika kutishia habari nyeti zisitoke au matakwa yake yatimizwe lasivyo atausambaza.

Ilibidi Masha arudi ikulu muda ule japo alikuwa na miadi yakumtafuta mkuu wa idara ya usalama lakini wazo hilo likafa kibudu kwa muda hadi pale habari mbaya kumhusisha rais zikapodhibitiwa nakufukiwa katika kaburi la sahau.Alikamata usukani wa gari nakwenda mbio kuwahi ikulu.Dakika zilipokatika alikuwa keshafika ikulu asubuhi ile mida ya saa kumi na mbili.Aliomba nafasi ya kuonana na rais.Kwa kuwa alikuwa na kibali maalum hakuchelewa kupata wasaa wakumuona rais wake.

“Kuna nini tena Mr Masha?”aliuliza Kilua maana alijua kama huyu mtu karudi basi bila shaka kutakuwa na jambo gumu.Wameongea muda mchache uliopita.

Masha aliweka lile gazeti juu ya meza paap!Kilua alilipokea nakulitizama moyo ukapiga mkambi.Ilikuwa habari mbaya kwake.Ilikuwaje ikavuja jambo hilo.

Rais Kilua aliwaza nakuhisi kichwa kuwa kizito kwa msongo wa mawazo.Habarii ile ni kweli.Yawezekana kweli ikawa imevuja lakini kutoka kwa nani?Aliyujua kwamba alicheza karata hizo kwa usiri lakini sio kwa namna ambayo kuna kiumbe angekuwa na thubutu ya kujaribu kuandika habari hiyo kwenye kurasa za gazeti tena kuitoa ukurasa wa mbele.Nchi ilikuwa kwenye wakati mgumu na sio kupokea kitu kama kile.Pale ingemlazimu kusema familia yake ilipo bila shaka mumewe angetafutwa kuthibitisha habari ile au kuikana.Lilikuwa tukio lisilo na urafiki wowote kwa upande wake!

Pia maadui zake wakisiasa wangeweza kutumia habari ile kumuadabisha yeye sasa na huko mbeleni kadri siku zitakavyokuwa.Nilazima jambo hili lidhitiwe kwa hali zote.

“Wanataka milioni arobaini la sivyo habari hiyo itaingia sokoni muda si mrefu.”alisema Masha.

“Unaamini habari hizi?”aliuliza Kilua.

“Hapana.Ninachojua wewe ni rais wangu na mishale ni mingi inaelekezwa kwako.Jukumu langu nikukulinda.Unaweza muita mhariri Yule ukampiga marufuku kuitoa habari.Lakini tupo katika wakati mgumu hatua yoyote ina matokeo.”alisema bwana Masha akionesha kumpa ushirikiano rais Kilua.

“Ngoja ni mwite chifu wangu wa ushauri.”alisema Kilua kisha alichukua simu yake na kumpigia simu Serambovu ambaye alikuja muda uleule.Aliingia ndani ya ofisi kisha akapewa lile gazeti na Kilua.Aliliangalia kisha akainua macho kumwangalia Masha.

“Huyu mhariri kesha toa hii habari?”
“Anatishia kuitoa tayari imechapishwa lakini bado nakala hazijasambazwa na kama zikisambazwa ni mauzo ya milioni arobaini.Anataka hizo fedha alipwe yaani tulipie gharama za nakala zote tuzichukue sisi ili umma usizione.”

Serambovu alihamaki kisha akasema,”Hadi muda huu bado huyu fala anapumua?”

Masha alitegemea jibu kama hili kutoka kwa rais lakini badala yake akaona kama mwenye kauli ni Serambovu.

“Unamaanisha afutiliwe mbali?”
“Ndiyo huu sio muda wakupokea habari kama hii!Ni muda wakumfutilia mbali kabisa.”
Kilua aliinua kikombe cha kahawa alikunywa tena kuchangamsha ubongo.Lakini alihisi kama kuumwaumwa.

“Sihitaji mauti lakini nahitaji huyo mtu anyamaze na habari hii isitoke mbele ya umma.”alisema Kilua akihisi kutapika alikimbilia bafuni kwa haraka kwenda kutapika.Ofisi yake ilikuwa na bafu alienda huko nakutapika asubuhi ile.Alihisi kama kuumwaumwa asubuhi ile.Mwili wake haukuwa wa kawaida.Alinawa nakupiga mswaki kisha akarudi ofisini kwake.Aliwakuta Masha na Serambovu wakimsubiri.

“Upo sawa?”aliuliza Masha.Kilua alitikisa kichwa kuonesha yupo imara lakini sio kivile.

“Nataka habari hii isitoke kama ni pesa apewe lakini nakala zote ziteketezwe!”alisema Kilua.

Serambovu aliomba apewe nafasi yakushughulika na jambo hilo.Alipewa maelezo na Masha kisha akaanza hatua za kuidhibiti habari ile isitoke.

***

Masha aliondoka moja kwa moja hadi makao ya usalama wa taifa.Alifika nakukaribishwa asubuhi ile ambayo nimbichi.Alikuta kuna kama taharuki akiomba kuonana na mkuu wa idara ile.

Kwa kuwa alikuwa na kibali maalum kutoka kwa rais alipita mara moja hadi ofisini kwake.Alimkuta mkuu Yule akiwa mwingi wa mawazo na wasiwasi.

“Vipi bwana mbona kama haupo sawa?”

“Kuna tatizo kubwa limetokea.”

“Tatizo gani?”
“Tulikuwa kwenye oparesheni ya undercover bahati mbaya mashushushu wetu wamekamatwa.Tunashindwa kuvamia nakuwatoa maana tutaharibu operesheni nzima.”alisema bwana Toti akiwa ameshika kichwa.Siku ile alikuwa na wakati mgumu sana.Operesheni ya jana imeshaondoa uhai wa watumishi kadhaa wa idara hiyo na leo hali imekuwa tete.

“Nikawaida kwa kazi zetu lakini naimani vijana wako wana mafunzo ya kutosha na watasalimika inshallah!”

Toti alitikisa kichwa kuonesha kukubali jambo lile.Palepale Masha alitoa kibali chenye muhuri wa rais kuonesha kwamba amepewa nguvu ya kuvuka mipaka yote kukamilisha uchunguzi wake.

‘Nikusaidieje bwana Masha.”
“Nataka kujua kuhusu mikataba iliyoingiwa hapa nchini.”

Toti alikaza ndita kidogo kuwa makini kwa swala la Masha,”Kuna mikataba mingi sana taifa letu iliyoingia pengine uwe specific na swali lako ni mkataba upi?”
“Kuna mkataba mmoja ambao umekuwa wa siri sana na umetesa serikali iliyopita nahii iliyopo.Huu mkataba uana dira umekuwa gumzo kila anayeutaka anaishia kati ya kuwa chizi au kufa.Ninaamini taasisi hii ina ufahamu wa mkataba huo.”

Toti alitetemeka kwa wasiwasi sana.Alishangaa kugusishwa kwa jambo kama hilo kwamba huo ni mkataba gani?Kichwa chake alikihamisha kutoka kwenye zimwi la kutekwa kwa vijana wake akajileta kwa Masha amsikilize.

“Kuna mikataba ndiyo iliingiwa kwa nguvu na kuwanyamazisha watu Fulani.Sasa sijajua unataka kujua ipi naweza kupitia kaukaguzi kidogo halafu nitakuletea mikataba hiyo yenye kutishia maisha.”

Masha alitoa shajaa yake akaandika namba 13:14 kisha akampa bwana Toti,”Naomba uangalie hii namba halafu ukipata faili lenye utambulisho huu nitahitaji kujua nila nani?”alisisitiza bwana Masha.Toti alimwangalia kisha akafungua tarakilishi yake nakufungua faili Fulani alianza kupitia wakati huo Masha alikuwa akibofya simu yake akisoma kitu.Ilimchukua bwana Toti dakika tano kupata faili hilo lenye jina nywila (CODE NAME 13:14)Alimuonesha bwana Masha faili hilo.Kilichomshtua zaidi waliamua kuliangalia pamoja kisha waligeukiana kwa pamoja.

“Tutalikagua hapa kwa muda kisha tumpelekee rais taarifa ya nyaraka hizi.Pia nitampa kijana ninayemuamini anifanyie upekuzi kuona kitu gani kinashabihiana.”ilikuwa kazi iliyohitaji mambo mengi sana na majibu kadhaa.

***

Shuni alizinduka nakujikuta akiwa kafungwa kwa kamba nzito juu ya meza.Pembeni alisimama Yule mzungu.Macho yakiwa makali na ukavu wa ukatili ulijichora kwenye wajihi wake.Alipojaribu kuinua shingo yake alihisi imefungwa kwa kitu kama mkanda iliyomshikilia kwa nguvu kwenye meza ile.Ungesema kapigiliwa misumari!

Watesi wake walichukua kitambaa wakamfunika usoni kisha likaletwa jagi lililojaa maji wakalimimina kwenye uso wake.Maji mengine yaliingia kwenye pua na mengine yalinyeshea paji la uso!Aina ya fedheha aliyopatwa nayo bi Shuni ingebaki daima rohoni mwake.Yalikuwa mateso makubwa sana alijikuta akifurukuta nakuachia kelele nyingi zilizotoka kwenye moyo wake!

Walifanya vile kumfedhehesha mwanamke Yule!Kisha wakaacha nakufunua kile kitambaa.Shuni alizitafuta pumzi kwa hali na mali
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 104
Back
Top Bottom