Riwaya: Barua Kutoka Jela

Riwaya: Barua Kutoka Jela

Afadhali igp kwa kuliona hilo,kazi nzuri Insp. Jamila,pamoja sana mkuu Casuist
 
Last edited by a moderator:
Kiukweli sina imani kabisa na huyu IGP....huu wema huu sijui..shukrani mkuu Casuist kwa kuniita
 
Last edited by a moderator:
Nyamaza kulia wewe, mwanaume analia ndani, nje mkax!
 
Aisee, hadithi imetulia hii, huyo Eshe Muhidini ndie ninaemfahamu au mwingine?

teh teh! huyo Eshe unaemjua mume wake aliangukiwa na jumba bovu?? Inawezakuwa hii ni true story (joke)
 
Yule jirani alietoa maelezo juu ya kifo cha Hamida aliuawa, wasije tu wakamuua na huyu inspekta Jamila
 
RIWAYA: BARUA KUTOKA JELA
MTUNZI: IBRAHIM GAMA


SEHEMU YA NANE


"Nikiwa huku jela kama mahabusu nimeiweka nadhiri ya kwamba, ikiwa nitashinda kesi hii na kuachiwa huru, basi nitauandika mkasa huu uwe filamu. Ili wale wote waliodhani kuwa mimi ni jambazi na Jamii yote ya Tanzani kwa ujumla wapate somo kutokana na filamu hiyo. Lakini pia kuielimisha Jamii yetu ijue kwamba serikali ipo na inawajali raia zake.
Na pia watambue wapo maaskari wanaojali haki za raia na kuthamini ubinaadamu, ambao hawafanyi kazi kwa nguvu ya rushwa, kama wewe Inspekta Jamila!"

Alipofika hapa Mwaduga sasa akawa analia kwa sauti akiwa hawezi kuongea kwa vile donge la uchungu lilivyomkaa rohoni.

Inspekta Jamila na Eshe walimnyamazisha Mwaduga na Eshe akampa mkono wa pole mumewe huku akimpa moyo.
"Hakuna lenye mwanzo lisilokuwa na mwisho, lakini pia likiwapo la kuchukiza lipo na la kupendeza. Hivyo usilie sana, kwani tambua ya kwamba, Mbwa hafi maji akiuona ufukwe!"

Inspekta Jamila akafungua mkoba wake na kutoa picha nne alizokuwa nazo, akaziweka mbele ya macho ya Mwaduga Dingo na kumwambia!

"Je kuna yeyote katika picha hizi unayemfahamu?"

Zilikuwa ni zile picha ambazo mbili kati ya tatu alizozichukua nyumbani kwa Marehemu Hamida, na mbili ni zile picha alizopewa na Dokta Zahala.

Zile picha mbili alizochukua kwa marehemu Hamida, moja alishaifahamu ni ya Dr. Masawe. Zile nyingine bado hajazitambua.

Mwaduga akaziangalia picha zile, kwa umakini mkubwa kisha akasema.

"Hapa nimeitambua picha moja tu"
Mwaduga alisema maneno hayo huku akionyesha picha aliyoitambua.

Ilikuwa ni ile picha aliyoipata kwa marehemu Hamida iliyomuonyesha marehemu Hamida akinyweshwa kinywaji na kijana mmoja aliyeonekana mtanashati.

Mwaduga akasema "huyu jamaa anaitwa Bitozi ni muuzaji magari maarufu kule Kijitonyama. Hata gari nililokuwa ninaendesha, aliyekuwa tajiri yangu Bwana Shaame aliinunua kwenye Show Room yake."

Inspekta Jamila aliandika neno Bitozi nyuma ya ile picha iliyotambuliwa.

Baada ya mahojiano ya hapa na pale kuhusu ofisi ya bwana Bitoz ilipo, Inspekta Jamila alipata taarifa za kutosha, na wakaagana na Mwaduga. Yeye na Eshe wakaondoka, wakimuacha yule askari Magereza na Mwaduga akiwa na matumaini tele.

*****

Siku ya Jumatatu Inspekta Jamila alikuwa amekaa ofisini kwake akifuatilia ripoti ya picha zile alizozipeleka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, ili kuzifanyia kazi.

Picha zile za watu wawili moja kati ya picha zile ilitambuliwa!
Na ile picha nyingine haikuwepo kumbukubu yoyote ya sura ile katika ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai.
Hivyo majibu ya picha zile yalikuwa kama ifuatavyo.

Picha ya mwanaume aliyevaa fulana nyeupe anatambulika kwa jina la Geradi Mwaipopo, kabila Mnyakyusa, aliwahi kuwa askari wa Jeshi la Polisi aliyekuwa na cheo cha Staf Sajent ambaye alifukuzwa kazi katika Jeshi la Polisi, baada ya kugundulika kufanya vitendo vya uhalifu katika kivuli cha Jeshi la Polisi.

Alipobainika aliachishwa kazi mara moja. Kiasi miaka miwili iliyopita! Wakati huo alikuwa anaishi Magomeni Mwembechai, Mtaa wa Mengo, Nyumba Namba 8. Hupendelea kutembelea Mikoa ya Mbeya, Songea, Tanga, Arusha,Pwani na Dar es Salaam. Kwa sasa haijulikani anaishi wapi wala anafanya nini. Ni mrefu wa futi 6 na inchi 3, rangi ya mwili wake ni nyeusi ya asili. ilimalizia ripoti ile. Na nyuma ya picha ile liliandikwa jina kamili la mwenye picha na kufuatiwa na maandishi "WANTED".

Inspekta Jamila alitingisha kichwa kwa taarifa ile, kwani aliona askari anafukuzwa kazi hali ya kuwa ana ujuzi wa kutumia silaha, lakini pia mbinu mbali mbali za kijeshi halafu hajulikani anaishi wapi na anafanya nini, hii ni hatari kubwa kwa taifa letu.

Inspekta Jamila baada ya kuipitia ripoti ile kwa kina, akaiendea gari yake aina ya Toyota RAV 4 maarufu kwa jina la "Kitchen Party" yenye milango mitatu, akafungua mlango wa gari na kuingia ndani ya gari. Kisha akatoa simu na kumpigia Dokta Zahala akitaka kujua kama yuko kazini muda ule.

Alipopata jibu la ndiyo akamwambia.
"Nipo njiani nakuja Muhimbili ofisini kwako"

Inspekta Jamila akakata simu.
Baada ya dakika kumi Inspekta Jamila alifunga breki katika Hospitali ya Muhimbili nje ya jengo la ofisi ya Dokta Zahala.

Akatia lock milango ya gari yake, akahakikisha vioo vimefunga vyote, na kuelekea ofisini kwa Dokta Zahala.

"Dokta nashukuru kwa msaada wote ulionipa tangu unipe kazi hii! Ila sasa siifanyi kwa siri tena kwani sasa nimekabidhiwa faili rasmi kwa ajili ya kufuatilia kesi hii."

Alisema Inspekta Jamila akimshukuru shoga yake wakiwa wawili katika ofisi ile na kuendelea.

"Hivyo basi sikuja hapa kwa ajili ya kukushukuru peke yake laa! Ila bado ninahitaji msaada wako mwingine."

Inspekta Jamila alisema huku akimwangalia shoga yake ambaye alikuwa kimya muda wote akiwa anamtazama.

"Wee! Hongera shoga kwa kupewa rasmi kazi hiyo, sasa msaada upi huo unaouhitaji kutoka kwangu?"
Aliuliza Dokta Zahala.

"Nataka unifahamishe kwa Dokta Masawe ofisini kwake na hata nyumbani kwake ikibidi."

Alijibu Inspekta Jamila.
"Ahaa sawa shoga, Dokta Masawe ni Daktari Bingwa, hapa huwa kazini siku za Jumanne na Alhamisi. Siku kama ya leo anapatikana katika Hospitali yake iliyopo maeneo ya Sinza Madukani. Karibu na Guest ya Namnani. Nyumbani kwake ni Kinondoni Mtaa wa Kasaba nyumba ya mwisho kwenye kona, kabla hujafika baa maarufu sana inayoitwa Patchoto."

Inspekta Jamila aliposikia jina la Sinza, Karibu na Namnani moyo wake ukamlipuka na akaazimia kwenda muda ule ule kwa Dokta Masawe.

Akamshukuru shoga yake na akaagana naye,kisha akatoka nje ya ofisi ile akaielekea gari yake tayari kwa safari ya Sinza kwa Dokta Masawe.

Akiwa hatua kama tatu hivi, kutoka eneo alipoegesha gari yake, Inspekta Jamila aliona kitu kisicho cha kawaida katika gari yake!

Kwani alipoondoka pale katika eneo la maegesho ya magari, vioo vya gari yake vyote vilikuwa vimefungwa kama kawaida yake, ila wakati huu pale aliposimama, aliweza kuona kioo cha upande mmoja kipo nusu mlingoti!

Yaani kimefunguliwa nusu. Moyo wake ukaenda mbio akihisi kuwa ameshaibiwa na vibaka!

Akiwa mwenye hasira aliiendea gari yake, nakuanza kuikagua kwa nje kabla hajapanda. Lakini gari yake yote kule nje ilikuwa salama usalimini!
Akatazama Lock za milango, akaziona kama alivyozifunga ndivyo zilivyo kaa!
Alipofungua mlango ili aingie ndani ya gari, alipatwa na mshangao asioutegemea!

Bahasha ya khaki ilikuwa imewekwa ndani ya gari yake, katika kiti cha dereva.

Inspector Jamila aligeuka kushoto na kulia, ili kuangalia kama kuna mtu anaeshughulika nae, akaona kila mtu aliekuwa katika eneo lile, alikuwa yupo katika hamsini zake!

Akaingia ndani ya gari yake huku akiwa na tahadhari zote katika kichwa chake.

Aliichukua ile bahasha na kuiweka katika kiti cha pembeni na kuwasha gari, huku akikipandisha kile kioo na kutumia vioo vya pembeni vya gari yake, akawa anatazama kama kuna mtu yeyote anaeshughulika nae, kwa mara nyingine kukawa kupo shwari!

Aliiondosha gari kwa mwendo wa pole, akielekea Sinza kupitia Barabara ya Morogoro.

Alipofika Magomeni Mapipa, akaegesha gari yake katika kituo cha basi, kisha akaiangalia kwa mara nyingine ile bahasha, akaichukua na kuifungua.

Ndani ya bahasha ile kulikuwa na karatasi iliyoandikwa maneno yafuatayo; HABARI INSPEKTA JAMILA. NAKUSHAURI KWAMBA, WACHA KUJIINGIZA KATIKA MATATIZO YASIYOKUWA YA LAZIMA! KWANI HUU NI MTEGO WA PANYA. BORA KWAKO KUACHANA NA KESI HII. NA KAMA UTAKAIDI UTAKIONA CHA MTEMA KUNI!

Alimaliza kuusoma waraka ule Inspekta Jamila, huku akipigwa na mshangao wa mwaka!

Kilichompa mshangao ni kwamba, huyo mtu au watu alieandika walaka huu ni nani, amejuaje kama yeye ndiyo anaefatilia kesi ile kwa sasa, kwani alipokabidhiwa kesi ile, alikuwa yeye na "IGP" tu, watatu wao ni mwenyezi mungu! Lakini pia mtu alieandika waraka ule, amejuaje kama yeye atakuwa pale kwa Dokta Zahala muda ule?!

Isitoshe waraka ule haukuandikwa kwa mkono, bali umechapishwa kwa kutumia kompyuta, kisha ukaprintiwa!

Kazi ile rasmi alipewa Jumamosi, na leo ni Jumatatu, iweje ndani ya siku mbili tu iwe imeshavuja kwamba yeye ndiye! Ukizingatia kwamba hata shoga yake Dokta Zahala, ndiyo amempa taarifa ile muda mfupi uliopita!

Alipofikia hapo ubongo wake ukawa unazidiwa kwa maswali yasiyokuwa na majibu. Pia akikubali kimoyomoyo kama kweli ule ni MTEGO WA PANYA. Mara akaona vipele vya baridi vikizizima katika mwili wake.

Akapeleka mkono mgongoni mwake usawa wa kiuno na kuigusa bastola yake ndogo ya kipolisi na faraja ikamrejea upya!
Alisonya msonyo mkubwa kiasi gari yake ingekuwa imefunguliwa vioo basi hata watu wa nje wangesikia.
Akaiweka ile karatasi ndani ya bahasha na kuitumbukiza katika mkoba wake.
Akaiweka gari barabarani na safari ya Sinza kwa Dokta Masawe ikaendelea.

Alipofika Sinza maeneo ya madukani akachepukia barabara inayoelekea katika Guest ya Namnani, na mbele kidogo akakiona kibao kinachoitambulisha Hospitali ya Dokta Masawe, kilichoandikwa "DOCTOR MASAWE DISPENSARY", huku kikionyesha mshale kuelekeza ilipo Hospitali hiyo.

Inspekta Jamila akazidi kusisimkwa na damu isivyo kawaida.
Katika kona ya pili mbele ya barabara ile akaona maandishi mekundu na meupe pamoja na picha ya nyoka yanayosomeka "Doctor Masawe Dispensary."

Inspekta Jamila akatambua kwamba amefika eneo alilolikusudia.
Katika eneo la maegesho ya magari la hospitali ile kulikuwa na magari kadhaa yaliyokuwa yameegeshwa katika sehemu hiyo.

Naye akawa katika harakati za kutafuta eneo la kuegesha gari lake ndipo moyo wake ulipompiga ghafla!

Gari nyekundu aina ya Toyota Caldina ilikuwa imeegeshwa mbele ya hospitali ile.
Akagundua kwamba Dokta Masawe amemkuta. Akatafuta sehemu nzuri ya kuegesha gari lake na kuiegesha gari na kushuka, akajichoma ndani ya hospitali ile.



***JAMILA amefika katika hospitali ya MASSAWE……kuna nini kitajiri hapo???
***NI NANI WALIOMUWEKEA UJUMBE KATIKA GARI YAKE….



Jagarld Jullie Z Sangomwile Khantwe Mr Rocky Gunda66 Himidini VAN HEIST BPM ABUBAKAR SHEKAU NYIRO mamsapkhan born again pagan princetx Ennie mcubic jonnie_vincy slim5
 
Sasa upelelezi umenoga look dk zahala nae namuhofia kutoa siri
 
Kazi nzuri Casuist nakufuatilia kwa uangalifu mithili ya Inspekta Jamila
^^
 
Last edited by a moderator:
Mh!
Mtego wa panya,mtegaji Sio IGP kweli?
 
Jamila ama kweli kazi umeipata,igp kageuka al shabab mara hii,ahsante sana mkuu Casuist
 
Last edited by a moderator:
teh teh! huyo Eshe unaemjua mume wake aliangukiwa na jumba bovu?? Inawezakuwa hii ni true story (joke)

Huyu ninaemjua mimi ni mtangazaji wa radio moja hapa nchini
 
IGP keshaanza vimbwanga, pole inspector jamila but kazana buti usirudi nyuma
 
Back
Top Bottom