Inspekta Jamila alimuuliza Masudi kwa shauku. Na Masoudi akajibu.
"Kwa kweli yule mmoja aliepanda mbele namkumbuka kwa sura. Jamaa ana kithethe anapoongea, kwani hata neno tunazo Elfu tatu, yeye alitamka TUNADHO ELFU TATU! Wale wengine wawili sikuwakariri sura zao sawasawa kwani gari ilikwisha ondoka! Ama nguo alizovaa yule jamaa aliepanda mbele, alivaa suruali ya jinzi na fulana moja nzuri sana iliyokuwa imeandikwa MKIMBIZI ikiwa na picha ya mwana dada mmoja akiwa kama anakimbia! Ile jinzi ilikuwa na Rangi nyeusi na fulana ya rangi nyeupe."
Inspekta Jamila akamuhoji Masudi mambo mengi kiasi akaridhika kwa hatua aliyopiga. Na kiasi alianza kupata Mwanga kuwa, Mwaduga hakuwa anajua chochote katika mkasa unaomkabili, lakini ataihakikishiaje serikali ili ielewe kile anachosema?! Na kama Mwaduga si muhusika, je nani ataesimama akiwa ndiye muhusika halisi?
Inspekta Jamila. Akaagana na Masudi huku wakipeana mkono wa kwa heri yeye na mkewe, ambae sasa alikuwa ni mtulivu na mwenye nidhamu ya hali ya juu!
Wapelelezi wawili walikuwa wamekaa kwa pamoja wakijadili hali ya upelelezi wao walioufanya katika kesi inayomkabili Dereva Taxi Mwaduga Dingo, kwani kesi ya mauaji inayomkabili, sasa jalada lake, upelelezi umeshakamilika, na mwendesha mashtaka wa serikali anatarajia kulipeleka jalada mahakama kuu kwa ajili ya kesi kuanza kusikilizwa. Baada ya kutajwa mara kadhaa katika Mahakama ya hakimu mfawidhi ya Kisutu, Mahakama ambayo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji kwa mujibu wa sheria za nchi.
Afande Kubuta ambae ndie mpelelezi, aliekabidhiwa kupeleleza kesi zinazomkabili Mwaduga Dingo, akiwa na mpelelezi mwenzake Afande Magane, walikuwa wanalipitia lile faili kwa kituo, ili liwasilishwe Mahakama kuu kwa kusikilizwa.
Afande Kubuta alianzisha mazungumzo. "Yule kijana kwa jinsi nilivyo muhoji na kumpa kibano lazima angesema kila kitu yule, lakini yule kijana kama ni sugu basi yule ni mwalimu wao! Kwani katika mkono wangu, haijawahi kutokea mualifu nimuweke katika kiti moto kisha asinieleze ukweli, ndiyo kwanza yule kijana amefanikiwa! Ameharibu CV yangu yule!"
Afande Magane akasema: "Inawezekana yule ameshawishiwa na wale jamaa akaingia katika mkumbo kwa tamaa ila wale jamaa hawajui wala nini!"
Afande Kubuta nae akasema. "Tulipokwenda kumpekua, nyumbani kwake hatukukuta vitu vya maana sana, ila kulikuwa kuna Tv moja aina ya Sony nchi 14 mpya kabisa, na nilipohitaji stakabadhi iliyonunulia Tv ile, nikahisi kuwa yule kijana anahusika kwa namna moja au nyingine. Kwa sababu stakabadhi ile tarehe yake ilikuwa inaonyesha kuwa, Tv ile imenunuliwa siku moja baada ya mauwaji ya Hamida kutokea! Na kwa kuwa Silaha ya Marehemu Hamida amekutwa nayo yeye, kisha Tv yake imenunuliwa siku moja baada ya kifo kile, hii wala haihitaji Digirii kutambua kwamba baada ya kijana yule kushiriki katika tukio lile la mauwaji, mafao yake ndiyo amenunulia Tv"
Hivyo Wakiwa katikati ya Mjadala ule simu ya Mkononi ya Afande Kubuta iliita na alipoiona namba ya simu iliyokuwa inaita, moyo wa Afande Kubuta uliruka sarakasi na kuipokea simu ile.
"Ndiyo Afande, sawa mkuu, nimekusoma Afande!" Kisha ilikatwa simu ile.
Afande Magane akamuuliza.
"Vipi ni mkuu wa kituo huyo aliepiga simu hiyo?!"
Afande Kubuta akamjibu "Hapana huyo ni IGP bwana, na sijawahi kupigiwa simu hata mara moja na IGP"
Afande Kubuta akamueleza yote aliyoongea bosi wao.
Afande Magane akashangaa sana kusikia habari hiyo, na akasema.
"Bila shaka kuna mtu amekwenda kwa IGP anayehusiana na mtuhumiwa, na kuongea na IGP! Sasa kama hivyo ndivyo basi kesi hii rafiki yangu, inabidi uwe makini sana. Kwani wewe ndiye mpelelezi wa kesi hii mwenye Jalada lake! Sisi wengine tunapewa amri tu, Fatana na afande fulani kwa upekuzi na majadiliano tunafanya hivyo! Duh hii hali sasa ishakuwa pevu, je? unayo ripoti iliyokamilika ya upelelezi wa kesi hii sasa? Kwani ndiyo inatakiwa ili ionekane bila shaka afande kama angetaka kujua angeuliza umefikia wapi kwenye upelelezi wa kesi hii. Ila hapa naona kuna kitu cha ziada kutoka kwa Bosi kwani Photo Albam na Note Books vya marehemu yeye vya nini? Okay sasa mimi naona twende Mikocheni kwanza kutekeleza amri ya Bosi kisha uvipeleke kama alivyoagiza, kisha tusikilize atakwambiaje kwani tunaweza kuumiza vichwa kumbe mambo yenyewe ni shwari tu!"
*******
Afande Kubuta na Afande Magane walibisha hodi nyumbani kwa marehemu Hamida, walipofunguliwa mlango wakajitambulisha ikiwa ni pamoja na kutoa vitambulisho vyao vya kazi.
Wakakaribishwa ndani, walipofika ndani wakaeleza walichokiendea pale. "Kama tulilvyokwisha jitambulisha, tupo hapa kikazi hivyo tunahitaji Photo Albam zote za marehemu Hamida pamoja na vitabu vyake vya kumbukumbu."
Yule dada aliyewapokea akaanza kuvitafuta vitabu vyake vya kumbukumbu marehemu Hamida chumbani kwake kwani "photo albam" zilikuwa mezani chumbani mle.
Yule dada akawakabidhi "photo albam" nne afande Kubuta akazichukua na kuziweka kwenye mfuko wake wa ngozi alioushika mkononi, akifarijika angalau anachokitaka Bosi wake kutoka kwenye nyumba ile, kimoja amekwisha kipata. Iliwachukua kama nusu saa kuja kukiona kitabu cha kumbukumbu cha marehemu Hamida. Yule dada aliyejitambulisha kama mdogo wa Hamida, anayejulikana kwa jina la Neema, akawaambia askari wale.
"Jana alikuja afande mwenzenu wa kike aliyejitambulisha kwa jina la afande Jamila, amechukua picha tatu kutoka katika albamu hizo, na ameahidi kuzirudisha mara baada ya kukamilisha upelelezi wenu!"
"Whaat?!"
Afande Kubuta na mwenzake afande Magane walijikuta wakisema kwa pamoja huku wakiwa hawaamini masikio yao kwa kile walichokisikia kutoka kwa Neema!
"Umesemaje?!" Afande Kubuta akamuuliza Neema.
"Mbona mmeshituka sana, ina maana hamna taarifa za picha hizo kufika ofisini kwenu? Mimi nimejua mmekuja kuchukua nyingine ili mkamilishe huo upelelezi wenu!" Neema badala ya kurudia kauli yake, akatoa maneno yalioonyesha kumshangaza, kwa namna kesi ile inavyoshughulikiwa!
Hatimaye akairudia tena kauli yake, sasa akiwa makini zaidi ya mwanzo.
"Juna alikuja afande mwenzenu wa kike, aliyejitambulisha kwa jina la afande Jamila. Amechukua picha tatu kutoka katika albam hizo, na ameahidi kuzirudisha mara baada ya kukamilisha upelelezi wenu."
Neema alirudia kauli ile huku akiwatazama machoni maafande wale wawili waliopigwa butwaa ya mwaka!
"Yaani mnataka kuniambia, kwamba afande Jamila hamumtambui?" Aliuliza Neema huku akivuta tafakari na kuwa makini zaidi.
"Jibu swali mwanamke", afande Kubuta akasema huku akiwa amechanganyikiwa kwa kauli ya neema.
"Jibu maswali mwanamke." Afande Magane akadakia na huku akiendelea kusema. "Hii ni kesi ya mauaji hivyo usije kuleta mzaha umesikia?"
Neema aliitikia kwa kutikisa kichwa. Kisha akajibu, "Alipokuja hapa jana alijitambulisha yeye ni askari polisi na akatoa kitambulisho chake kama nyinyi mlivyofanya. Ila hakusema ametokea kituo gani cha polisi! Akataka "photo albam" kama nyinyi mlivyotaka, nami nikampa na baada ya kuzipekua, akachomoa picha tatu akatia kwenye mfuko wake kama nyinyi mlivyochukua hizo albam na kutia katika mfuko wenu. Ila yeye hakutaka kitabu cha kumbukumbu, baada ya kupata picha zile akaaga na kuondoka."
Afande Kubuta akamuuliza "je alikuonyesha picha alizochukua?"
"Hapana" Neema akajibu.
"Ila unazitambua picha zilizokosekana katika albam hizo?"
Afande Magane akamuuliza Neema huku akimkazia macho.
"Hapana kwani mimi nimekuja hapa ulipotokea msiba, kabla ya hapo nilikuwa siishi hapa, hivyo picha za marehemu dada zote alizopiga ukiondoa za harusi yake ambazo nimeziona nyingine zote sizijui." Akamaliza Neema huku akifuta machozi yaliyoanza kumtoka, labda baada ya kukumbuka picha zilizomuonyesha dada yake akiwa katika maisha yake ya ndoa!
"Hapana hakuacha, ila alichukua namba yangu ya simu na kusema angenipigia pindi ambapo angelihitaji msaada kutoka kwangu."
Ama kwa hakika askari wale walichanganyikiwa sana kwani kila kitu walichokitarajia kuwasaidia kumtambua huyo afande Jamila waliambulia jibu la hapana! Ama kweli walikuwa wamepigwa bao la kisigino. Mwisho wa yote wakaacha namba zao za simu na kumwambia Neema.
"kama atakuja tena huyo afande Jamila muulize anatokea kituo gani, na unipigie simu mara moja. kwani mimi ndiye mpelelezi katika kesi hii. Hivyo mtu yeyote atakayejihusisha na kesi hii, lazima mimi nimtambue."
Afande Jamila ni jembe la ukweli lakini nanusa harufu ya IGP kuhusika fulani hivi....!! Mnakumbuka kifo cha jirani ya Hamida? Nyie mnafikiri ile ilikuwa ni ajali ya kawaida ile..?? Jamila should watch out
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.