- Thread starter
- #41
RIWAYA: BARUA KUTOKA JELA
MTUNZI: IBRAHIM GAMA
SEHEMU YA TANO
Ama kwa hakika askari wale walichanganyikiwa sana kwani kila kitu walichokitarajia kuwasaidia kumtambua huyo afande Jamila waliambulia jibu la hapana! Ama kweli walikuwa wamepigwa bao la kisigino. Mwisho wa yote wakaacha namba zao za simu na kumwambia Neema.
"kama atakuja tena huyo afande Jamila muulize anatokea kituo gani, na unipigie simu mara moja. kwani mimi ndiye mpelelezi katika kesi hii. Hivyo mtu yeyote atakayejihusisha na kesi hii, lazima mimi nimtambue."
Mwisho wakaaga na kuondoka.
*******
Afande Kubuta alibisha hodi Ofisini kwa Bosi wake na kutoa heshima za kijeshi kama inavyotakiwa na kuketi kitini baada ya IGP kumuashiria kufanya hivyo.
IGP akanyoosha mkono kuchukua vitu alivyoagiza kutoka kwa afande Kubuta na kitu cha kwanza kuanza kuangalia zilikuwa ni zile albam nne zilizokuwa mbele yake.
Aliangalia moja baada ya nyingine huku akiangalia hadi zile picha zilizokuwa zimewekwa nyuma ya picha, mwisho akazimaliza zote albam nne bila kuona kitu alichokikusudia!
Akainua uso na kumtazama usoni kijana wake afande Kubuta. Na kwa mara ya kwanza akanyanyua mdomo wake kusema.
"Kuna picha humu ambazo zimetolewa! Kwani zipo sehemu zilizokuwa tupu kuonyesha kwamba kulikuwa na picha! Kwani si kama picha zilizomo humu hazitoshi kuijaza albam kwani kuna picha nyingi hadi nyingine zimewekwa picha tatu katika sehemu moja! Je picha hizo umezitoa wewe? Na kwa sababu gani wakati nilikwambia ulete kama utakavyozichukua?"
Akauliza IGP huku akiwa amechukia na amefula kwa hasira!
"Hapana Mkuu, kama ulivyoagiza ndivyo nilivyotekeleza. Ila picha zilizopungua, nimeambiwa kwamba amekwenda afande Jamila amezichukua na kuahidi angezirudisha baada ya upelelezi kukamilika!"
Sasa ikawa zamu ya IGP kufadhaika, aliinuka kwenye kiti chake na kusimama huku akiwa ametoa macho pima! Kitu ambacho hata afande Kubuta naye alishangaa. Kwani alidhani labda huyo afande Jamila, alitumwa na Bosi huyo kama yeye alivyotumwa kwenda kuchukua zile albam. Sasa kama naye anashangaa je kuna nini kinachoendelea. Na je hizo picha ni za nini? Hatimaye IGP akauliza.
"Huyo afande Jamila nani kampa kesi hii?!" Sasa IGP alionekana kama ana hofu katika sura yake lakini pia jazba ilimtawala vile vile.
Afande Kubuta akaisoma hali ya Bosi wake akawa makini sana.
"Sielewi mkuu, lakini pia katika kituo chetu cha Magomeni hatuna jina la afande Jamila, achilia mbali kuwa mpelelezi. Pia nilidhani labda amri hii imetoka juu, katika kuweka askari mwingine bila mimi kujua! Ili naye afatilie mwenendo mzima wa kesi hii. Sasa kama mkuu hujui lolote kuhusu afande Jamila, nini kinaendelea katika kesi hii?"
Afande Kubuta aliuliza huku akiwa amechanganyikiwa kwa mawazo. Pia baada ya maelezo yake "IGP" akagundua mchezo wote atakuwa anaufahamu huyo afande Jamila, lakini yeye kwa nini asifahamishwe alipohitaji kujua mpelelezi anayeendesha kesi ya marehemu Hamida?!
Ila yeye alipewa jina la afande Kubuta, nambari ya faili na nambari ya simu ya afande Kubuta. Sasa huyo afande Jamila anafanya kazi kwa kutumwa na nani na kwa faida ipi hatimaye "IGP" aliwaza na kuinua mkono wa simu kisha kubonyeza nambari kadhaa na simu ikawa inaita upande wa pili.
*******
Madereva Taxi katika Kituo cha Taxi Magomeni Usalama, walikuwa katika harakati za kazi yao. Wapo waliokuwa wakifuta magari, wengine kuyaosha kabisa. Pia wapo waliokaa juu ya Boneti na wapo waliokaa juu ya Buti. Wapo waliokuwa ndani ya magari yao wakisinzia ili mradi kila mtu alikuwa na harakati zake.
"Karibu dada, hii hapa pamba nyepesi full kiyoyozi na bei sina, ngoma full tank siyo mafuta ya kidebe."
Dereva wa taxi alijinasibu kwa kuipamba gari yake, na kumshawishi Yule abiria ili apande kwenye gari yake. Huku akifungua mlango wa nyuma wa gari yake, ili abiria aweze kuingia, kisha watapatania ndani bei ya sehemu atakayompeleka.
Yule abiria aliekaribishwa bila kujishauri wala kusita, akazama ndani ya gari ile.
Dereva badala ya kuingia ili waanze safari, akaanza kupiga honi mfululizo! Mara kijana mmoja mfupi mweupe alikuja mbio alitokea upande wa kushoto wa gari lile ambalo walikuwa wamekaa vijana wengine kadhaa wakicheza draft.
"Mpeleke huyo Dada sijaongea naye kitu chochote mtaelewana."
Aliongea yule kijana aliyemkaribisha yule abiria.
Alipopanda yule dereva na kuwasha gari, yule abiria akatambua kwamba, yule kijana wa mwanzo alikuwa ni shanta, huyu sasa ndiye Dereva.
"Samahani Dada tunaelekea wapi?" Yule Dereva Taxi aliuliza huku akiondosha gari.
"Nipeleke Kimara Suka, itakuwa shilingi ngapi?"
"Ahaa Kimara Suka kubwa dada yangu, unakwenda pale pale kituoni, au kule shule, au kule Golan au kwa yule Mwandishi maarufu wa riwaya Hussein Tuwa?"
"Nakwenda Kimara Suka Hotel utanichaji shilingi ngapi?"
"Alaa kama pale ni shilingi elfu nane tu Dada yangu!" Alijibu yule dereva wa Taxi huku akigeuza Gari na kuanza safari.
"Wewe una bei sana kwani nilikuwa nikimchukua yule kijana Mwaduga, alikuwa akinipeleka kwa shilingi Elfu sita tu! Sijui leo kapakia, kwani sijamuona yeye wala gari yake!"
Yule abiria alimwambia Yule dereva wake kwa upole.
"Usinikumbushe sister Bwana. Mshikaji wetu jumba bovu limemdondokea! Jamaa ana bahati mbaya sana Yule."
Dereva alimwambia abiria wake kwa masikitiko huku akionyesha huzuni usoni mwake!
"Umesema jamaa kaangukiwa na jumba bovu siatakuwa ameumia sana?!"
"Sio hivyo unavyofikiria, jamaa yetu kapatwa na matatizo. Kapewa msala wa mauaji hivi hivi, majambazi na wauaji wanaachwa wanatembea mitaani tu!"
Alijibu Yule taxi dereva, katika lugha yao ya kijiweni, ambayo ilimpa wakati mgumu, abiria wake kumuelewa kwa urahisi, maana ya baadhi ya maneno!
"Aaaaaa Bwana usiniambie!"
Yule abiria aliuliza swali kwa mfadhaiko, na fadhaa kubwa.
"Kweli sister wangu, jamaa ana miezi miwili na kitu, sasa yupo katika maisha mabovu mahabusu. Yaani kama alikupakia basi ni siku nyingi kidogo. Sasa bei zimebadilika mafuta yamepanda bei sana."
Alijibu yule dereva Taxi nakutoa ufafanuzi huku akibadilisha gia, sasa wakiwa maeneo ya Aljentina Manzese.
"Kwani kilimpata nini jamani kaka wa watu duh kama namuona vile!?"
Yule abiria aliuliza kwa masikitiko, na kuonyesha sura ya huruma na kuendelea kueleza.
"Mimi nilikuwa Chuoni nimekuja pale kituoni kwenu kama miezi mitatu iliyopita, na Mwaduga ndiye alikuwa ananizungusha katika mizunguko yangu!"
"Yaani sister we acha tu, kwani kesi ya mshikaji imekaa vibaya sana!"
Dereva Taxi akaongeza msisitizo wa jambo lile.
"Umesema kesi ya Mwaduga imekaa vibaya sana, kwa sababu gani, wakati umesema ni jumba bovu tu limemwangukia, yaani yeye hakufanya jambo lile?"
"Dada, yule mshikaji keshapotea yule kwani amepewa soo nne. Mauaji, kukutwa na silaha, kula njama ya kutenda kosa na wizi wa kutumia silaha. Haya yote anaweza kuchomoa, lakini kosa lakukutwa na silaha, jamaa si washamuachia msala?! Huwezi kuamini sister lakini nakuambia yule Demu alieuliwa ni mali ya wakubwa, kwani Bosi wa polisi wa cheo cha juu kabisa, ndiyo alikuwa anaburuza ule mzigo"
"Ha ha haa, sasa kaka unafika mbali sana, yaani wewe unajua pia kuwa huyo marehemu, anaeshitakiwa Mwaduga kuwa alimuua, kuwa ni kimada wa mkubwa wa jeshi la polisi!?"
Yule abiria alionyesha kutaharuki kupita kiasi, lakini pia alijiona ni mwenye bahati kubwa kuichagua gari ile, kwani dereva wake ni mtu mropokaji! Kwani anatoa taarifa nyeti kwa gharama nafuu sana!
"Siyo mzaha sister wangu, mimi nina mshikaji wangu anapaki Town yeye ndiyo ilikuwa kazi yake! Ameisha mpakia sana yule Demu kumpelekea Bosi wa polisi, karibu mara tatu! Na yule Bosi alikuwa anamlipa pesa nzuri sana! Yaani jamaa anaweza kumchukua yule Demu Mikocheni nyumbani kwake, na kumpeleka labda bwalo la polisi ostabey akalipwa shilingi elfu ishirini! Au siku nyingine humpeleka Bagamoyo na kumuacha kwenye hoteli za kitalii siku za mwisho wa wiki, akalipwa laki moja! Sasa aliposikia mshikaji wetu Mwaduga yuko ndani tena kwa kesi ya mauaji ya yule Demu, mshikaji aliniambia haya ninayokwambia, na akasema Bel white mshikaji wangu jamaa yenu keshapotea, kwani ile ni mali ya wazee Yaani tumsahau! Sasa wewe sister unadhani hiyo ni kesi ya kitoto hiyo?"
Yule abiria alisogea katikati ya kiti cha dereva na abiria, huku akiwa na simu yake mkononi muda wote tangu amepanda gari ile, akasema kwa shauku kubwa.
"Duh ebwana we! Hiyo kweli ni kasheshe, Yaani ndiyo ilivyokuwa hivyo? Na mbona kule mwanzo ulisema wauaji na majambazi wanaachiwa tu wanatembea na jamaa yenu anaozea jela, kwa nini msiisaidie polisi kuwakamata na jamaa yenu akaachiwa?"
Yule abiria akazidi kuchimba. Na hadi walipofika Kimara Suka hotel akawa ameshapata hadi jina la yule Dereva Taxi wa mjini na namba yake ya simu, pamoja na namba yake Dereva Taxi huyu aliempeleka Kimara aliemtambua kwa jina la Bel white.
******
Ilikuwa siku ya Ijumaa Dokta Zahala akiwa nyumbani kwake maeneo ya Keko bora, alikuwa anaonekana kuwa ni mtu wa mawazo mengi, kisha kama aliyekumbuka jambo akatoa simu yake kwenye "Hand Begi" na kubonyeza tarakimu kadhaa na simu ya upande wa pili ikatoa maelezo badala ya kuita!
"IMU UNAYOPIGA IMEZIMWA AU IPO NJE YA ENEO, TAFADHALI JARIBU TENA BAADAE."
Dokta Zahala akakata na kubonyeza namba zingine na simu ya upande wa pili ikaanza kuita.
"Shoga vipi mbona kimya au ndiyo nimekupa kazi kubwa kiasi hata simu yako ya kawaida umeizima?"
Aliongea Dokta Zahala mara tu simu ya upande wa pili ilipopokelewa, na kuongeza kuwa.
"Duh pole sana, sasa leo nipo mapumziko, kama unayo nafasi njoo nyumbani nitakuwepo. Kwani nina neno lililonifanya nikupigie simu!"
Aliongeza Dokta Zahala na kisha akakata simu.
Dakika Arubaini baadae kengele ya geti la mlango iliita, na mfanyakazi wa Dokta Zahala akakimbilia kwenda kufungua mlango. Dokta Zahala akamkaribisha shoga yake, na wakakumbatiana kama kawaida yao wanapokutana!
Dokta Zahala na Inspekta Jamila walikuwa marafiki tokea chuoni pale Mlimani, walipomaliza masomo, Jamila akaenda kujiunga na Jeshi la Polisi na kutokana na Elimu yake haikumchukua muda mrefu kupata nafasi aliyonayo, baada ya kuongezeka utendaji kazi wake katika Jeshi la Polisi.
Na Dokta Zahala alikuwa anachukua masomo ya udakitari, Baada ya mama yake mdogo aliekuwa nesi katika hospitali ya Kcmc Moshi, kumshawishi asomee mambo ya utabibu akimwambia unalipa sana, na kweli leo hii yupo katika nyumba yake mwenyewe pale Keko Bora!
"Leo soda yako ya lemon unayoipenda sina kwenye jokofu langu, je ukatafutiwe huko nje madukani au utakunywa hizi zilizopo?"
Dokta Zahala alimwambia shoga yake huku akiangua kicheko.
"Akili yangu ilivyovurugwa, sina chaguo lolote lililo bora, wewe nipe kinywaji chochote mimi nitakunywa, ilimradi kisiwe na kilevi!"
Alijibu Inspekta Jamila na akamalizia kwa kicheko. Baada ya wote kupata vinywaji cha juice, hatimae Dokta Zahala akavunja ukimya.
"Haya shoga yangu ukamwona yule Dada siku ile na mwanae sijui umefikia wapi, kwani alinitia huruma sana yule Dada."
Inspekta Jamila akamuhadithia shoga yake kila kitu bila ya kumficha chochote huku akimwambia kuwa, ameamua kumueleza yote kwa ukamilifu! kwani kazi na maisha yake yapo hatiani toka yeye kujihusisha na kesi ile bila maelekezo kutoka kwa wakubwa zake, na ikija kubainika kwamba anajua hadi uhusiano uliokuwepo wa "IGP" na Marehemu Hamida, basi atakuwa katika mashaka mazito!
"Lakini pia nataka wewe shoga yangu uwe unalifahamu kwa undani jambo hili, ili ikitokea lolote kuhusu maisha yangu uwe na pakuanzia!"
Alisema kwa masikitiko Inspekta Jamila.
"Duh pole na hongera shoga!" Alisema Dokta Zahala.
"Sasa mimi nilikutafuta ili nijue kama ulimsaidia yule Dada, lakini pia kuna kitu kipya nataka kukueleza!"
Alisema Dokta Zahala na kuinua glasi ya Juice nakupiga funda moja, huku akimuangalia shoga yake alivyokaa kwa umakini mkubwa.
Jagarld Jullie Z Sangomwile Khantwe Mr Rocky Gunda66 Himidini VAN HEIST BPM ABUBAKAR SHEKAU NYIRO mamsapkhan born again pagan princetx