SEHEMU YA MWISHO
Umeyajuaje yote haya
nilimuuliza hatimaye.
Kuna bwana nilimuagiza akuletee barua, ndo huyo alinieleza
kila kitu juu ya Michigani, akanisemelea juu ya geti namba
saba pia. Niliwahi pia kuletwa huku, na huu mlango wa
dharula ni kwa ajili ya walinzi japo huwa hautumiki mara
kwa mara mpaka hatari kubwa ikiwepo
.. alisema kwa
ufupi na hapo wakaanza kusukumwa watu kuingia katika
uwazi mkubwa.
Asilimia kubwa walikuwa ni wale waliokuwa nje tayari
wamekombolewa, mzee Matata alikuwa amelegea, Mama lao
alikuwa amefungwa kamba mikono yote. Nikajisikia hasira
kali sana.
Vikashushwa vitanzi upesi na hapo baadhi ya askari feki
wakaanza kuwasukuma raia katika vitanzi.
Na hapa ndipo ikafuata VITA YA MWISHO CHINI YA ARDHI
MICHIGANI
Ni aidha kufa ama kupona lakini siri lazima
ifichuke.
**JIFUNZE kuwa hakuna marefu yasiyokuwa na ncha!!!
Usikate tamaa!!
Risasi zilimiminika kuwaendea wale mahayawani takribani
watano wa kiafrika ambao walitaka kuwaweka katika kitanzi
waafrika wenzao.
Kambi yetu ilikuwa imara haswa!!
Kuangushwa kwa watu wale wabaya kukazua tafrani mpya,
mateka wao wakaanza kukimbia huku na kule. Wao wakabaki
katika sintofahamu. Wakiwa katika taharuki kali zaidi.
Walijaribu kuwazuia huku wakikishambulia kwa risasi kile
kibanda cha dharula ambacho tulijihifadhi ndani yake. Lakini
hawakuwa na shabaha murua.
Adui katika kambi hii
adui katika kambi hii, bomu la mkono
linatupwa katika maficho yenu ndani ya dakika moja. Kwa
usalama wenu na wenzenu jisalimisheni, la sivyo ninyi
pamoja na wenzenu wote mtapoteza uhai. Angalizo ni
kwamba hakuna njia yoyote ya kutoka Michigan ukiwa hai,
njia zote zimefungwa. Ilikuwa ni sauti kubwa ikielezea kwa
ufasaha juu ya usalama wetu na wenzetu. Sauti hii ilirudia
mara ya pili na wakati ikirudia haya mara Michigani ilianza
kupanda juu tena. Kambi yetu iliingiwa na kiwewe baada ya
tangazo lile ambalo mtangazaji wake hakuonekana na wala
kinasa sauti na kipaza sauti vyote havikuonekana.
Majambazi yakiwa na silaha mkononi yalishindwa kufyatua.
Hatimaye Michigani iliyokuwa imezama chini ikarejea usawa
wa kile kibanda chetu cha dharula!!!
Na wakati huu yule mtangazaji alikuwa akihesabu namba
kadhaa kwa ajili yetu kujisalimisha.
Tulikuwa tumepatikana!!
Heka heka za kule chini za mateka ziliendelea huku wakikosa
mahali sahihi pa kukimbilia, kwani kila mahali palikuwa
pamefungwa!!
Kambi yetu ilikuwa na bunduki mkononi bado kwa lolote
litakalotokea mbele yao. Mimi, Masawe na Anitha tukiwa
tumepigwa butwaa tu.
Na mara kikatokea kisa cha kushangaza. Ukaanza kuvuma
upepo mdogo kiasi na mara majambazi wakaanza kuhamanika,
wakionekana kuvutana na kitu kisichoonekana, na hata
walipozidiwa nguvu wakaziachia bunduki zikivutwa kwa kasi
na kutokomea na upepo ule.
Shit! Magnetic wind
.. alilalamika Anitha akionekana
kujua nini kinatokea pale.
Sasa wakatokea watu wanne!!
Cheupe dawa na yule mwafrika mwenzake wakiwa katika
jopo. Walikuwa wanacheka kwa dharau na namna fulani ya
kuridhika sana.
Cheupe alikuwa amebeba faili mkononi.
Unaanza vipi kutoka Michigan ukiwa hai
we ----- wewe
ulibahatika kutoka umejileta tena eeh.. aliongea huku
akinitazama, nikakwepesha macho nisimtazame.
Salim!! Hakuna kupoteza muda tena
. Alikaripia yule
mzungu. Na hapo akatokea bwana mmoja mwenye ndevu
ndefu haswa.
Akapiga miluzi wakatokea wengine wawili. Wakawakwida
mashati raia wawili wakiwa uchi na dhaifu, wakawaingiza
katika kitanzi kisha wakabonyeza mahali, ardhi yao
ikafunguka.
Wakawanyonga wale watu wasiokuwa na hatia.
Ilisikitisha kuwatazama. Nilifumba macho kwa uchungu na
uoga ukanitawala nikiyafikiria maisha mafupi katika kitanzi
kile.
Bonge waiti amesema kuwa wao wameua watano sijui sita,
sisi tunaanza na sitini na sita kama mfano tu
na wale
vichwa ngumu kama Sam na baba yake huyu Matata ni adhabu
takatifu kabla ya kifo.. cheupe dawa alimweleza mwenzake
kimadaha na majigambo.
Sam
Sam
. Anitha aliniita huku akitazama mbele
asijulikane kama anasema nami.
Wanamuua baba Sam
.. Anitha alinieleza kana kwamba
nilikuwa sijasikia lolote. Niliuma meno yangu kwa uchungu
nisijue nafanya nini.
Wakati huo raia wengine sita walikuwa katika kitanzi.
Na hawa wakauwawa katika namna ileile.
Mbona watoto hawauwawi ama!! Nilijiuliza baada ya kuona
kuwa ni watu wazima pekee waliokuwa wananyongwa.
Awamu ya tatu ya kunyonga haikwenda kama ilivyopangwa
badala yake ikaingia doa.
Cheupe dawa aliyekuwa mwenye tabasamu muda wote, akiwa
na tabasamu lake vilevile ghafla alirushwa nyuma kimyakimya
akitua katika umati mkubwa wa mateka, na doa jekundu
likaonekana katikati ya kifua chake kimyakimya.
Yule muafrika kibaraka wa yule mzungu akafanya kosa
kugeuka upesi kutazama nini kinamtokea mwenzake.
Akauachia mgongo wake wazi, ghafla akarushwa mbali
akifunuka kifua chake na kutokwa na yowe kubwa kabisa.
Akaungana na mzungu katika safari ya milele.
Kimya kikatanda asijulikane ni nani anayeshambulia,
majambazi hawakusogea mbele kwa sababu hawakujua ni nani
aliyefanya shambulio hilo, na wenyeji wa humo wakapigwa na
bumbuwazi.
Mluzi ukasikika katika namna ya kuvutia masikioni,
majambazi kwa pamoja wakasema.
Kigulu
nikalikumbuka jina hilo kuwa ni la mzee Sendeu.
Yule fundi makufuli.
Hakuna bunduki, vamia
. Hakuna bunduki magnetic wind
imepita
. Anitha aliyasema hayo huku akiongoza mbio
kumkabili yule bwana aliyekuwa anawanyonga mateka. Lakini
kabla hajamfikia alijikuta katika mikono yenye nguvu sana.
Alikuwa ni mzee Matata!!!
Baba
.. Anitha akamuita lakini hakujibiwa na badala yake
mzee Matata akamrukia yule mnyongaji na kumkaba koo yake
huku akipiga mayowe hadi pale alipotulia tuli.
Alikuwa ameua!!
Niliendelea kuwa shuhuda na miguu yangu mibovu, majambazi
wakipambana ana kwa ana na maadui.
Mzee Matata akazifungua kamba zilizomfunga afisa wa jeshi
la serikali. Akiwa kama mbogo na yeye akafanya mashambulizi
makubwa tena ya upesi upesi. Makabiliano ya ana kwa ana
maana upepo uliokuwa umewashwa haukuruhusu bunduki
wala chuma yoyote kuwa pale, ilisafisha kila kitu pale.
Afisa aliambatana na mama lao. Kipigo alichokuwa anatoa
mama huyu sikuwahi kukidhania lakini kilinifanya
nitabasamu, nilitabasamu kwa sababu niliwahi kuwa pembeni
ya shujaa huyo.
Michigani mini office Geti namba saba, yupo huko
. Yupo
na faili.. sauti ikaniambia kwa shida sana, nikageuka na
kukutana tena na ule mzimu wa maajabu.
Ezekiel!!!
Alikuwa anatabasamu tena.
Nikaanza kupiga kelele nikitafuta wa kumwelewesha juu ya
hili!!
Afisa akanisikiliza, akawatambua baadhi ya vijana wake wa
kazi ambao walikuwa na nguvu bado. Wakaunda jeshi la
dharula, msako wa geti namba saba ukafuata
..
Niliungana na msako huu nikiwa nachechemea, hatimaye
tukalifikia geti hilo la vioo.
Amri ikatoka na kundi lote la ukombozi na mateka wetu
kutoka kwa wapinzani wakazingira geti namba saba.
Kisha ufumbuzi wa kufungua pale ukafanyika, kwa sababu
palifungwa kwa utaalamu, basi ni nguvu pekee ingeweza
kufungua, kila kitu kizito kisichokuwa chuma kilitumika
kuponda vile vioo. Hadi vilipovunjika vipande vipande.
Bosiiiiiiii
alipiga kelele mzee Matata. Huku akiiziba
midomo yake. Watu hawakugeuka kumtazama bali walimkazia
macho kiumbe aliyekuwa ananinginia katika mkono wa koti
la kuvalia suti, ulimi ukiwa umemtoka nje.
Mzee Matata anamuitaje bosi wake sasa? Nilijiuliza!!
Sam
ni huyu
. Ni huyu Kenton!!! Anitha naye alipiga
kelele.
Sikumsikiliza tena baada ya kuliona faili mezani!!
Nikatimua mbio kwa kusuasua hadi nikaifikia meza na
kulikwapua faili lile. Faili lenye siri nzito.
Afisa alitoa wazo kuwa tutafute namna ya kutoka nje ya
Michigan lakini Ezekiel, yule mwanadamu wa ajabu
alininongoneza kuwa anahitaji kusedma neno kabla hajaaga
dunia kwani hali aliyonayo anaijua mwenyewe tu na si vyema
akifa huku ameacha utata. Kubwa zaidi aliongezea kuwa
kufikia hatua ya bosi yule kuuwawa basi hakuna hofu tena
katika chimbo hilo la Michigan.
Upesi nikaisambaza ile taarifa, na nilikuwa nasikilizwa sana.
Mimi, Mama lao pamoja na Anitha tulisikilizwa zaidi. Na
tuliheshimiwa kama mashujaa hata kabla hatujaimaliza vita
hiyo.
Umati ukamzunguka Ezekiel ukimya ukairuhusu sauti yake
kupenya. Askari watiifu wakiwa makini kutulinda.
ALVIN
.
Niliishi na kufanya kazi michigani kabla haijawaka moto na
kuteketea na nikiwa kama mfanyakazi mtiifu sana
nililazimika kuyafumbia macho mabaya ili niendane na sera za
mkuu wangu wa kazi, ambaye kwa wakati ule nilimtambua
kama cheupe (akamwonyeshea mkono yule mzungu mwenye
upara niliyemzoea kama cheupe dawa)
lakini baada ya
kugundua mambo kadha wa kadha ndani ya jumba la Michigani
hasahasa suala la kukamata watoto wasiokuwa na hatia.
Nikajisikia nipo hatiani na kuamua kupingana kabisa na
mfumo huo, nilijaribu kuwahamasisha wenzangu lakini baadhi
walinisaliti na mwisho kunichomea utambi. Bahati nzuri kuna
mkuu mmoja alinishtua kuwa nilikuwa hatarini. Ndo
nikatimua mbio mapema kabla ya dhahama. Siku nne baada ya
mimi kutoka Michigani, ilichomwa moto na kupotea kabisa
huku watanzania wasiokuwa na makosa wakitupwa jela na
serikali ikiendelea kumkumbatia mmiliki wa Michigani kisa tu
anaongeza pato la taifa kwa sana.
Niliishi kama digidigi ndani ya mji niliozaliwa. Baada ya
Michigani kuchomwa ndipo kwa usiri ikaanzishwa Michigani
nyingine miezi kadhaa baadaye, niliamini kuwa nimesahaulika
tayari hivyo nikaendelea na harakati zangu za kusanua
mpango kabambe wa mmiliki wa Michigani. Bwana aliyekuwa
muuzaji katika duka la Michigani alikuwa ni jamaa yangu wa
karibu na niliwahi kufanyanaye kazi Michigani ya zamani
huyu anaitwa Kindo, ni yeye aliyekuwa akinieleza kila
kilichokuwa kinaendelea katika duka dogo la Michigani.
Alifanikiwa kunipatia picha kadha wa kadha ambazo aliamini
kuwa zinaweza kunisaidia, mimi pia nilikuwa na picha zangu
zinazoionyesha Michigani. Masawe alikuwa muuzaji
mwenzake na Kindo japo yeye hakuwa akifuatilia mambo
yetu, kama ilivyo kwamba Ngombe wa masikini hazai wakati
tunakaribia kufanikiwa kuingia katika himaya ya chini kwa
chini ya Michigani ndipo mkuu akashtukia na nikaanza
kusakwa huku kindo akitiwa uchizi. Nilifanikiwa kuchukua
nyaraka kadhaa muhimu pia funguo chakavu. Funguo ambao
niligundua kuwa unaingia karibia kila kitasa. Na ni huu
funguo ambao ulifungua jumba hili.
Maisha ya udigidigi yalivyonishinda nikaamua kuelekea Dar es
salaam nikiwa na nyaraka zangu.
Ili nisiishi kama digidigi nikaamua kuishi kama Alvin mwingine
kabisa, nikalikuta neno Anti likitumika kuwaita mashoga
jijini Dar es salaam, na huku nikijua mashoga wanachukiwa
sana na mimi nikahitaji kuchukiwa na jamii ili nifanye mambo
yangu kimya kimya!!
Na hapo nikajitambulisha rasmi kama Anti Ezekiel, wao
wakidhani jina la anti kwangu linasimama kama shoga, kumbe
ninamaanisha Mpinga Ezekiel (ANTI-EZEKIEL kwa
kiingereza)
Akanyamaza kidogo akivuta pumzi!!
Akaelezea namna tulivyokutana mara ya kwanza na ya pili
kisha akaendelea
Sikuwa na mtu mwingine wa kumuamini basi ule funguo
nikamkabidhi yeye, nilitaka kumkabidhi Sam funguo huo
usiku mmoja baada ya kutumiwa ujumbe wa kurejea Michigan
lakini nikamkuta katika faragha na mkewe, nikasikia kuwa
atasafiri siku inayofuata, nikaamua kwenda kuonana naye
Ubungo, na nikafanikiwa japo nilikuwa chini ya uangalizi
mkali, nilitumia mbinu ya yeye kuupata tu funguo na kwa
kuwa ni mwandishi wa hadithi za kipelelezi nikajua lazima
atapeleleza tu na sasa yu hapa. amefanikisha alizungumza
haya huku akitokwa na machozi ndani ya tabasamu.
Machozi ya furaha
Na ni kwa nini unachanganya majina, mara Alvin mara Anti
Ezekiel
afisa alimuuliza swali ambalo alikuwa amelijibu
tayari
.
Mimi naitwa Alvin, Anti Ezekiel, hili sio jina bali neno Anti
ni la lugha ya kigeni na linamaanisha Mpinga ama kuwa
kinyume, yaani mpinga Ezekiel ama mkataa Ezekiel, hivyo
mimi namkataa na kumpinga Ezekiel na maisha aliyotaka
kuyaleta Tanzania hasahasa Iringa. Alijibu swali hilo
nikastaajabu. Yaani siku zote namtafuta Anti Ezekiel kumbe
hata mimi mwenyewe ni Anti Ezekiel!!
Jojina naye akacheka kidogo!! Na yeye alikuwa akimchukia
Anti Ezekiel kumbe alikuwa akijichukia?
Na hapo nikatambua kuwa lile jina E.F.Kenton, ile E
inasimama badala ya Ezekiel!!
Kufikia hapo sasa nikaamua kulitoa lila faili, mbele ya umati
haya yote yalifanyika maana yalikuwa mambo muhimu kwa
ajili ya watanzania.
E.F.Kenton kumbe ndo bosi wa haya yote!! Mzee Matata
alitahamaki, masikio yakageukia kwake wakati akimuelezea
Ezekiel Kenton kama mmiliki wa gazeti ambalo alikuwa
anafanyia kazi huko!!
Aliezea zaidi hatua ya yeye kufukuzwa kazi na kufungiwa
kazi baada ya kuandika makala kuwa Sam ameonekana mjini!!
Kumbe nilikuwa namtumikia shetani!!! alimalizia mzee
Matata kwa masikitiko.
Nami sikungoja tutoke nje ya ngome ile, nikaamua kulifunua
lile faili na kuumakinisha umma ukatulia na kunisikiliza
nikielezea
MKAKATI WA KUDUMU KUIFANYA TANZANIA NCHI TEGEMEZI.
Hicho kilikuwa kichwa cha habari kikubwa zaidi.
Ndani ukaelezewa ule mkakati kwa urefu!
Nchi zilizoendelea ama nchi za dunia ya kwanza zilikuwa
katika mkakati wa kuua nguvu kazi ya taifa kwa
kuwapunguza vijana na kiasi cha kuzaana.
Mkakati huu ulikuwa na dhima ya kuzifanya nchi masikini
kuwa masikini zaidi ili kuwezesha uhuru linapokuja suala la
uwekezaji. Kama wakishindwa kujizalishia mali zao wenyewe
basi kwa namna yoyote watakuwa tayari kuruhusu nchi za
kigeni kuwekeza kwa kadri ziwezavyo jambo ambalo
litaongeza pato kwa nchi zilizoendelea. Na kuongeza tatizo
la umasikini katika mataifa masikini, Tanzania ikiwa
mojawapo.
Mkakati nambari wani waliouanzisha ulikuwa ni kuongeza
idadi ya ndoa za jinsia moja hasahasa wanaume kwa
wanaume.
Mkakati ambao waliamini utazaa matunda sana, maana kwa
wanaume kuoana basi vijana watapungua na si kupungua tu,
ndoa zaj insia moja hazizai mtoto hivyo, idadi ya watu
ingepungua pia. Kupitia mkakati huu ilimaanisha kuwa
mwanaume aliyeolewa ndo mwisho wa utendaji kazi wake!!
Mkakati huu ukaenda mbali zaidi na kuhamasisha maandamano
ya kuomba haki kwa wanaume wanaotetea ndoa za jinsia
moja. Maandamano haya yasingewezekana ikiwa idadi ya
wanaounga mkono ndoa hizi ikiwa ndogo!!
Mkakati huo ukaanzia kwa watoto, yaani wanakamatwa
wakiwa wadogo kisha wanafunzwa vitendo vya kishoga na
wakishakomaa wanaachiwa huru wakachafue hali ya hewa
mtaani. Hii ingewasaidia kuwa na idadi kubwa sana ya
wanaounga mokono upuuzi huo.
Na iwapo yangetokea maandamano basi nchi zenye sauti
duniani ambazo tayari zimeyaruhusu mambo haya zingeingilia
kati na kufanya ziara za kuhoji juu ya maandamano hayo
yanayohatarisha amani.
Kwa sababu nchi hizo zina sauti kubwa sana na pia zikiwa
zimewekeza mamilioni katika ardhi ya Tanzania basi mkuu wa
nchi hatakuwa na sauti na badala yake atasikiliza ni kitu
gani wao wanataka!!
Na hapo ndoa za jinsia moja zitaanzishwa rasmi na
kuruhusiwa!!
Huu unakuwa mwisho wa mkakati huu thabiti!! Katika namna
ya mafanikio makubwa!!
Mwanzo wa mkakati huu ukawa kuanzisha kambi ya kwanza
ambayo itaanzishwa kama hoteli kubwa ya kifahari lakini
lengo kuu likiwa kuwa kambi ya kuanzia mkakati.
Na hapo ikaanzishwa MICHIGANI ya juu ambayo ilitoa ajira
kwa wananchi wengi hasahasa wakazi wa Iringa!!
Hoteli ilivyokamilika, likaanza tatizo la watoto kupotea
kimyakimya!! Ili lengo lisijulikane wakawa wanawachukua
watoto wa kike na wa kiume!!
Vilio vikasikika na kupotea bila msaada wowote ule kutoka
serikalini.
Akina mama wakasahau juu ya watoto wao!! Hawakujua
kama wanapelekwa Michigani kuandaliwa kuwa mashoga!
Wazee wa kimila na wakongwe wa mji wakalitilia mkazo
tatizo la watoto kupotea mara kwa mara tena kwa wingi na
wasionekane tena.
Mzee mmoja akatilia mashaka Michigani, mwanzoni
akapingwa lakini mwishowe akakubaliwa, malalamiko
yakapelekwa kituo cha polisi, polisi wakaenda kufanya
upelelezi bila mafanikio.
Kikafuata kipengele cha mkakati wa kuitokomeza Michigani.
Nakala ile ikaelezea vikao kadhaa vilivyokaa na hatimaye
kuamua Michigani iteketezwe!
Kambi ya juu ikateketezwa makusudi, wale wazee walioleta
malalamiko wakashukiwa kuhusika katika uteketezaji.
Sheria ikachukua mkondo wake!
Wengi wao wakafia jela! akiwemo baba yake Anitha.
Kambi ya chini kwa chini ikaanzishwa kwa siri baada ya ile ya
Michigan juu kuonekana ipo wazi sana na muda wowote
itafichuka.
Baada ya vipengele vingi ambavyo vilihitaji umakini sana
kuvielewa hatimaye nikakifikia kipengele cha muhimu
ambacho tuliwahi kukitafsiri kama UKIMJUA UNAPOTEZWA.
Yeyote atakayepingana na sera za Ezekiel lazima aidha
auwawe ama kuteswa hadi afe
.(For any Anti- Ezekiel side
.
..) ilijieleza hivyo! Nilijikuta najiuliza kama niliewahi
kukubaliana na sera yake!
La! Sijawahi hata siku moja kukubaliana na sera ile kwa hiyo
nikajitambua rasmi kama Anti Ezekiel. Kumbe wakati wote
huo nahangaisha akili yangu kumtafuta Anti ezekiel nilikuwa
najitafuta mimi mwenyewe, kumbe hata mama lao ni Anti
Ezekiel pia na Anitha vilevile ni Anti Ezekiel. LABDA HAYA
WEWE!!
Ilistaajabisha.
Kumtafuta mtu asiyekuwepo na baadaye kugundua kuwa
unajitafuta mwenyewe!!
WATOTO wadogo walielezea walichokuwa wanafundishwa
ndani ya jengo lile kubwa!! Walikuwa wanafundishwa uchafu
tupu lakini ilikuwa bahati kubwa sana walikuwa hawajabobea
katika mambo hayo. Ilisikitisha sana kumsikiliza mtoto
mmoja kwa jinsi alivyoweza kujieleza vyema jinsi
alivyokamatwa kwa kulaghaiwa kisha kuingizwa katika ngome
ile. Akaelezea namna walivyoanza kufundishwa kuishi kama
wanawake!!..... aliongea sana na waliomsikia walitokwa
machozi.
Akiwa bado anaendelea kuongea nilimwona mwanamke
akimkimbilia na kumkumbatia. Na hapo nikabaini kuwa
alikuwa ni Jojina!! Akamtoa yule mtoto pale alipokuwa
amesimama na kusogea naye kando.
Justin
. Niliita, yule mtoto akanitazama.
Naam! Alifanania vyema kabisa na Jojina!!
Alikuwa ni mtoto wake wa pekee ambaye alitekwa miezi
kadhaa nyuma na kuhisiwa kuwa alipotea katika mambo ya
kishirikina.
Tayari askari watiifu walikuwa wameongezeka kwa wingi na
eneo lote lilikuwa katika ulinzi wa hali ya juu.
Mwisho tukatoweka bila kipingamizi chochote, Michigani
ilikuwa wazi hapakuwa na wa kutuzuia, tukawatoa majeruhi
wetu wote, simu zikapigwa na kupata msaada wa haraka
kutoka serikalini.
Afisa aliamuru watuhumiwa wote waingizwe katika
karandika na baada ya hapo mashahidi tulioonekana kuwa
tuna ulazima wa kuhudhuria katika mlolongo wa kesi hiyo
tuliambatana nao pia!
KIHITIMISHO!
MAKABURI ya Morogoro mjini yalinipokea kwa simanzi kubwa
sana, mama lao na Anitha walinisindikiza. Anitha akiwa
amembeba Eva ambaye alikabidhiwa kwangu kutoka katika
hifadhi ya serikali muda wote ambao nilikuwa natafutwa
Nilipiga hatua za kinyonge sana hadi nikalifikia kaburi la
kwanza.
Hili lilikuwa la mama yangu! Nikazungumza naye kwa kina.
Mama mwenye upendo na msimamo, mama uliyekuwa radhi
kunipigania mwanao, mama ambaye umeniamini hadi nukta ya
mwisho, mama ambaye umeteswa mpaka kifo chako huku
neno lako la mwisho likiwa nakupenda Sam.. ulazwe pema
peponi mama. machozi yalikuwa yakinichuruzika,
nikamgeukia Anitha naye alikuwa analia kwa uchungu, Jojina
alikuwa anaonekana dhahiri kuwa anajikaza tu lakini
alikuwa kwenye uchungu mkubwa sana!!
Nikahama kutoka pale na kujumuika na familia ya mama Eva,
tukasogea hadi katika kaburi alilopumzika mke wangu
mpenzi. Niliyebahatika kumwona akiwa hai lakini hoi sana
akitolewa katika chimbo la Michigani, jitihada zikazidiwa na
uwezo wa Mungu. Akaamua kumtwaa.
Wewe mwanamke ambaye ulinibadilisha mitazamo yangu,
ukautwaa utoto na ujana wangu na kunifanya mtu mzima.
Hukufaidi sana matunda ya harakati hizi lakini amini kuwa
bila wewe huenda hata nisingefanikisha zoezi hili gumu,
asante sana kwa mtoto uliyeniachia, najua atalia sana lakini
hatuwezi kubadili ukweli huo kuwa haupo nasi tena.
Ulazwe pema peponi mama Eva!!
Nikatoweka pale, sasa Jojina na anitha wakiwa wamenishilia
mikono yangu, tukarejea garini alipokuwa amelala Eva,
nikaingia na kumpakata. Jojina akashika usukani, safari ya
kuelekea Dar es salaam.
Huko tukakutana na taarifa katika vyombo vya habarai!!
Watumishi wa marehemu Ezekiel ambao wote waliutumikia
mkakati wa kudumu walihukumiwa vifungo vya maisha jela.
Hili lilikuwa jema sana kwa kila mpenda amani na mzalendo
katika nchi yake.
Bwana Masawe aliachiwa huru baada ya kukosa hatia!!
Hilo lilinifurahisha pia.
Na mwisho majina kadhaa likiwemo jina langu yalitajwa kwa
ajili ya kwenda ikulu kuonana na mheshimiwa raisi.
Baada ya siku kadhaa!!
Anitha akarejea chuoni huku akipewa heshima kubwa ya
kuwa mwanaharakati, heshima hiyo pia ilituzwa kwa Jojina,
na mimi pia! Si tu kwa nishani alizotuvika raisi la!!
Nilimsamehe mzee Matata na mkewe kwa imani waliyopoteza
kwangu, Enock na mkewe pia waliupata msamaha wangu pasi
na kinyongo!!
Kwa jiji la Dar es salaam, mama lao akiwa amerejea Tanga,
Anitha akabaki kuwa mtu wangu wa karibu zaidi.
Mazoea yakazaa tabia, tukawasiliana kwa ukaribu zaidi hadi
Eva akalitambua hilo. Akampenda Anitha naye Anitha
akampenda haswa.
Mzee Matata na mkewe ni kama walitarajia kuwa itakuwa
hivyo. Walisema kiutani wamkidai kuwa tunaendana sana
.
Naam kweli ikawa!! Na wao wakabariki.
ANITHA AKAGEUKA KUWA MAMA EVA!!!
JIFUNZE: DUNIA ina mapito mengi, ukijikwaa na kuanguka
amini kuwa haujaanguka moja kwa moja, zipo njia zaidi ya
milioni moja za kusimama tena. Usijaribu njia moja tu na
kusema nimeshindwa kusimama nami nitakuwa wa kulala
milele. Jaribu njia zote.
Amini hazitafika njia kumi bila ya wewe kusimama tena!!
Mungu anaziona jitihada zetu kwa jicho la huruma, jaribu
kufanya ukishindwa yeye yupo kusaidia!! Yapinge yale
yasiyopendeza kwa taifa na usoni mwake pia
Naupinga USHOGA na tabia zote za zinazofanania hivyo.
Mimi ni ANTI - EZEKIEL
. WEWE JE?
MWISHO!