Riwaya: Ant Ezekiel

mzaramo

JF-Expert Member
Sep 4, 2006
6,371
5,174
SIMULIZI: ANTI EZEKIEL
MTUNZI: George Iron Mosenya

SEHEMU YA KWANZA
Marashi yaliyopuliziwa na mtu ambaye nilikuwa sijauona
uso wake wala kujua yu umbali kiasi gani kutoka katika kiti
nilichokuwa nimekaa kwa ajili ya kunyolewa nywele zangu
yalinivutia kiuhakika, nikaamua kumshirikisha yule kinyozi
aliyekuwa ametingwa katika kuninyoa nywele zangu katika
mtindo niliokuwa nimeuchagua.
“Kausha….” Alinambia na sikuelewa ni kitu gani
anamaanisha. Nikahisi hakuwa akizungumza na mimi.
Marashi yale yakaendelea kutawala na sasa yalisadikika
kuwa karibu kabisa na pua zangu. Hapo nikajikuta
nanyanyua kichwa changu, kwa lengo la kutazama ufundi
ambao kinyozi aliufanya katika kichwa changu.
Badala ya kutazama kichwa changu nikajikuta natazamana
na tabasamu murua la kike. Kichwa chake cha mviringo
kilikuwa kimefunikwa na koti lisilokluwa maalumu kwa ajili
ya kupambana na baridi bali mojawapo ya kivazi
kinachoenda na wakati.
Nilipoendelea kubung’aa mara yule mmiliki wa sura ile
ambaye nilikuwa natazamana naye katika kioo alinikonyeza.
Hapo nikakumbwa na aibu na kisha nikajifanya kutazama
pembeni.
“Ana aibu mwenyewe looh!!” ilimtoka sauti fulani yenye
mchanganyiko wa besi na nyororo. Nikalazimisha tabasamu
lakini sikukitazama kioo.
Hakujishughulisha na mimki tena badala yake aliendelea
kuzungumza na mmiliki wa ile saluni ambaye pia alikuwa
kinyozi mkuu na wakati huo alikuwa katika kuzishughulikia
nywele zangu. Baada ya hapo akatoweka huku nyuma
akiacha harufu kali ya marashi isiyokera pua za mnusaji.
“Bwege katoka kwa wanaume” yule kinyozi akasema ili
nisikie,
“Nd’o wasichana wa siku hizi hao…” niliunga mkono hoja
pasipo kutilia maanani.
“Wasichana!!! Bora angekuwa msichana basi….yaani mi
ananikera sana ujue. Kidume kizima kabisa.” Akatokwa na
kauli iliyorindima katika mawimbi ya hasira na kupokelewa
na ngoma ya siko langu katika hali ya mshangao na
sintofahamu. Nikaamua kuuliza.
“Mwanaume? Mwanaume kivipi sasa ama umbo lake.”
Niliuliza na bado sikutilia maanani mazungumzo yale kama
yangeweza kunifikisha popote. Niliamini ni mazungumzo tu
ya hapo saluni na yanaishia hapo hapo.
“Shoga huyu!!! Halafu yupo wazi hata aibu haoni, kuna
washkaji wangu washalala naye, mimi siwezi hata kwa
bunduki yaani.” Aliongea kwa kunong’ona. Nikamsikia
vyema.
Sasa niliishughulisha akili yangu kuelewa kile alichokuwa
ananieleza.
Kumbe yule dada aliyenikonyeza na kunisia kuwa
nimependeza si dada ni mwanaume anayeupenda udada?
Niliduwaa hakika. Na hapo nikamuuliza maswali mengi sana
yule kinyozi, naye akafurahia kuyajibu.
Haikuwa mara yangu ya kwanza kusikia kuhusu jina hilo la
‘shoga’ la!! Lakini huyu macho yake ni kama yalitangaza kitu
fulani cha ziada, alikuwa kama shoga anayejilazimisha japo
yule kinyozi alidai kuwa yeye mwenyewe anajitangaza
waziwazi kuwa ni shoga.
Nilipozidi kuuliza maswali mengi, kinyozi akarusha kijembe.
“Vipi kaka na wewe unataka kukamatilia?” sikumjibu badala
yake tukajikuta tunacheka, na hapo alikuwa anamalizia
kunifuta kichwa baada ya kuninyoa.
“Vipi na ndevu niondoe..” aliniuliza nikakataa. Nikafanya
malipo na kisha nikajiondokea huku nikijilazimisha yale
mawazo kuhusu yule kijana anayeupenda usichana yanitoke.
Nilipofika nyumbani sikuwa na mawazo hayo tena na
sikutaka hata kumfikiria maana kwa kashfa alizotoa yule
kinyozi basi zilitosha kumaanisha kuwa kijana yule alikuwa
mdhambi tena asiyestahili hata kupewa salamu.
Inakuwaje mwanaume anajigeuza kuwa mwanamke??
Nililala nikiwa na swali hilo kichwani!!!
Asubuhi hapakuwa na lile swali tena na jibu lake pia
halkikufanania kuwepo.
Siku ikaanza nikiwa nimeyasahau ya jana.
*****
SAFARI YA KUKUTANA ANA KWA ANA NA MUHUSIKA.
UCHAGUZI mdogo wa serikali za mitaa kata ya
Makangarawe wilayani Temeke uliambatana na mechi ya
kukata na shoka katika mchezo wa soka.
Timu mbili pinzani zilikuwa zinaumana na mshindi
angejiondokea na kitita cha shilingi laki tano.
Mchezo ule ulivuta mashabiki wengi sana kutokana na
upinzani wa wazi wazi baina ya timu hizo. Nikiwa mmoja
katika ya wapenzi wa mpira wa miguu niliungana na
mashabiki wengine uwanjani.
Hali ya usalama ilikuwa nzuri kuanzia kipindi cha kwanza
hadi ilipokuja kuchafuka kipindi cha pili majira ya saa kumi
na mbili ambapo mwamuzi wa mchezo huo alipokataa goli
la waziwazi. Walianza wachezaji kumzonga mwamuzi mara
mashabiki nao wakaingilia kati, hapo ikazuka vita kubwa ya
mashabiki wa kila upande.
Kikosi cha kutuliza ghasia hakikuwa mbalki, mabomu
yalipopigwa ndipo kikazuka kizaazaa cha aina yake, kila
mmoja akikimbia kuelekea upande wake. Kipigo kilitolewa
haswaa na ungekuwa mwenye mikosi kama ungejikuta
katika mikono ile ya maaskari.
Nilichanja mbuga huku machozi yakinitoka kwa wingi baada
ya kuuvuta ule moshi wa bomu. Niliruka matuta hapa na
pale.
“Kakaaa…” nilisikia sauti ya kike ikiita, sauti iliyotia
simanzi, sijui ilikuwaje lakini licha ya hatari ile ya kuishia
kulala rumande na kipigo kupokea niligeuka kutazama
kulikoni.
Macho yangu yakakutana na macho yaliyonitia mashaka
siku moja nikiwa mahali fulani ambapo sikupakumbuka,
nilitaka kuendelea kukimbia lakini nafsi ikasita. Nikiwa
bado sijapata maamuzi mara kijana mmoja aliyekuwa katika
harakati za kukimbia alipita kwa kasi na kumkanyaga mtu
yule, akatokwa na kilio cha maumivu.
Nikataka kuzuia huruma yangu, lakini nikakumbuka kuwa
nimeajiriwa katika kampuni ya kutetea haki za wanadamu
na mimi mwenyewe ni mwandishi, mara kwa mara naandika
makala zinazosisitiza usawa na pia utu.
Kwa maana hiyo kama ningekimbia basi ninachokiandika
mara kwa mara kisingekuwa na maana. Nisingekuwa na utu.
Haraka nikakimbia mahali alipokuwa, nikamnyanyua,
hakuwa mzito sana nikagundua naweza kumuhimili.
Nikambeba begani! Nikajikokota hadi aliponielekeza kuwa
nyumbani kwake ni jirani tu….nikafuata uelekeo aliokuwa
amenielekeza.
Tukaufikia mlango, nikamshusha. Akajikongoja na
kuufungua mlango baada ya kujipekua na kutoka na
ufunguo.
Niliaga na kutaka kuondoka, akanisihi kuwa niingie ndani
hadi vurugu zipungue. Naam alikuwa amewaza jambo la
maana sana, nikakubaliana naye. Nikaingia ndani.
Nilipoingia ndani nikakuta picha yake, nikatazamana na ile
picha nikakumbuka sasa wapi tulionana.
Ni huyu kijana tulionana saluni, nikaambiwa kuwa ni shoga!!
Damu ikachemka nilipofikiria kuwa nipo katika chumba cha
shoga.
Nilifananisha sebule ile na sebule yangu, hakika alikuwa
ameniacha kwa kila kitu. Hali hii ya kuniacha kwa kila kitu
ikanivuta kuendelea kukaa pale.
“Unaitwa nani kakangu.” Aliniongelesha kwa sauti ilele ya
mchanganyiko.
“Sam!!” nilimjibu kwa kifupi.
“Mimi naitwa Ezekiel…asante sana kwa kuniokoa, sijui kama
ningelala nyumbani kwangu leo.” Alinijibu huku akiachia
tabasamu. Sikusema neno nami nikatabasamu huku
nikikwepa kumtazama machoni.
“Nyumbani kwako pazuri sana!!” nilimsifia.
“Ah kawaida tu, lakini asante si unajua tena mwanamk…..si
unajua tena kujipenda jambo la muhimu.” Akajibu kwa
kigugumizi.
“Unaishi peke yako?” nilimuuliza pasipo na wasiwasi
wowote kumtilia.
“Yah ni nyumbani kwangu naishi peke yangu……khaa!
Nimejichubua jamani kucha zangu.” Alijibu kisha
akalalamika akizitazama kucha zake zilizopakwa rangi.
Tofauti na siku niliyomuona pale saluni, siku hii alikuwa
amedhoofu sana. Alikuwa amekonda na uso wake ulikuwa
umebonyea. Hali hii ilinishangaza, lakini nikalazimika
kuuliza baada ya yeye kuanza kukohoa kwa fujo.
“Unaumwa…”
“Bora ningekuwa naumwa….mimi naumwa sana.” Alinijibu
kwa uchungu. Sasa sauti yake haikuwa mchanganyiko sana,
bali ilisikika kama ya kiume waziwazi. Sauti ilikuwa
inakoroma.
“Nini tena maana siku ile tunaonana saluni haukuwa hivi, au
kioo kilikuwa kinanidanganya.”
“Saluni? Saluni gani?” aliniuliza huku akistaajabu.
Nikamkumbusha siku ile ambayo ilikuwa miezi miwili
iliyopita. Hapo chozi likamtoka sikujua kama ni kwa furaha
ama uchungu.
“Lazima nife lakini basi tu….basi tu nasema. Ipo siku yao na
wenyewe” Alilalamika peke yake na sikujua kama alikuwa
ananishirikisha ama la.
“Mbona unasema hivyo bro.” nilihoji. Akanyanyua kichwa
akanitazama. Hakusema neno akakohoa tena kikohozi
kikavu ambacho kwa kukisikia tu nilitambua kuwa kilikuwa
kinamuumiza koo.
“Wewe ni nani?” aliniuliza…..kabla sijajibu akazungumza
tena. “Umesema unaitwa Sam lakini bado sijajua wewe ni
nani hadi umeamua kurudi nyuma na kuniokota mimi wakati
mama yangu mzazi alishindwa kuniokota.” Alitamka haya
huku akiniazia macho.
Kauli yake ikanitetemesha kidogo, ni kama alikuwa
ananikaripia. Sikushtuka sana nikaendelea kumtazama,
kwani nilishazoea harakati hizi.
“Mimi ni Sam, mwanaharakati na pia ni mwajiriwa kwenye
kampuni fulani hivi……” nilimjibu.
“Hivyo tu!” aliuliza na sikujua ana maana gani.
“Unamaanisha nini.”
“Ndo hivyo tu kuhusu wewe maana sura yako si ngeni sana
kwakweli, licha ya kukuona siku ile saluni bado kuna mahali
nadhani tumewahi kuonana ama nimekuona.”
“Labda gazetini, huwa naandika vihadithi hadithi.” Nilijibu
bila kutarajia kuwa anaweza kuwa ananifahamu.
Akasimama na kujipigia makofi, lakini kikohozi kikaondoka
na cheko lake akakaza sura na kuugulia maumivu lakini
bado aliweza kuzungumza.
“Nimesoma hadithi zako kadhaa, wewe si nd’o umeandika
ile ya NISAMEHE KABURI…..na nyingine ile ya dada fulani
hivi chuoni hana miguu wala mikono na anataka kuwa
rubani….yaani napenda hadithi zako hasahasa za kipelelezi,
hivi wewe ni mpelelezi eeh….” Alizungumza kwa sauti yake
ya kubana pua, bila shaka alikuwa ameizoea. Alionyesha
kunifahamu vyema.
Baada ya koo kukaa sawa aliendelea kuorodhesha makala
na hadithi zako ambazo amewahi kuzisoma, na hatimaye
tukaagana huku nikiwa sina shauku kubwa sana ya
kuendelea kumsikilia Ezekiel, kwani hakuonyesha kama
anajitambua vyema. Na mbaya zaidi niliamua kuondoka kwa
kuhofia kujitekenezea skendo nikionekana natoka katika
nyumba ya yule shoga.
Mke wangu na wivu wake!! Nilimjua mimi mwenyewe.
Nikamuaga Ezekiel na kuondoka, huku nikijiapia kuwa
hakuna ninalohitaji kujua zaidi kutoka kwa mwanaume
qaliyejigeuza mwanamke.
UTATA MKUU
Siku iliyofuata nilikuwa na safari ya kuelekea mkoani, hivyo
asubuhi na mapema niliwahi kwenda Ubungo. Kiubaridi
kilikuwa kinapuliza na nilikuwa nimejiegesha mahali
nikipuliza hewani moshi wa sigara kupasha mwili wangu
joto.
Nilijitenga eneo la mbali kabisa na abiria wengine ili
nisiweze kuwabughuzi. Mawazo yangu yalikuwa yote juu ya
safari yangu kuelekea Singida, niliwaza kuhusu watu wa
Singida jinsi walivyo wakarimu na hapo nikajengea picha
mara yangu ya mwisho mjini Singida.
Nikiwa bado pale nilipojiegesha mara nilisikia naguswa
begani.
Nilipogeuka nyuma nilikutana na maajabu.
Ana kwa ana na yule shoga!!
Hakuwa anatabasamu ba alionekana kama anayefanya
mambo kwa shinikizo. Alinikazia macho kama anayetaka
nielewe kitu fulani, nilijitahidi kung’amua jambo nikasafiri
na macho yake hadi katika mguu wake, akatabasamu na
kisha kutoweka pale katika mguu wake wa kuume akaacha
kifurushi kidogo tu cha nguo. Nikataka kumfuata
anapoelekea lakini akanionya kwa vitendo. Mwendo wake
ulinishangaza sana, alitembea mithili ya ngongoti, alikuwa
amenyooka na ni kama hakutaka kupinda, masikioni alikuwa
ana vifaa vya kusikilizia, sijui alichokuwa anasikiliza lakini
bila shaka walikuwepo watu ambao alikuwa anawasikiliza.
Ezekiel akatoweka na sikumuona tena.
Nikarejea hadi pale nilipokuwa nimesimama mwanzo,
nikaanza kukitafuta kile kifurushi alichokiacha pale lakini
sikukiona, nilihaha sana na kujiuliza nini kimemsibu yule
kijana. Na ni kitu gani alikuwa ameniachia katika fundo lile
la nguo??
Lazima kilikuwa kitu cha msingi maana alionyesha kusihi
sana.
Swali gumu jingine likawa, yule bwana amejuaje kama
nitakuwa stendi asubuhi ile hadi aniletee ujumbe ule.
Nikiwa bado katika mtihani mgumu, mara basi nililotakiwa
kusafiri nalo likapiga honi kuashiria kuwa dakika yoyote ile
linaondoka.
Ule utata ambao huwa naujenga kwa wahusika katika
simulizi sasa ukajijenga katika nafsi yangu na sikujua
nautatua vipi?
Katiba basi tayari begi langu lilikuwa kule, sikukipata
kifundo nilichoachiwa na mtu niliyeamini kuwa ni Anti
Ezekiel.
Na ubaya mwingine sikujua hata kitu kilichokuwa kinamsibu
Ezekiel.
Nikayakumbuka maneno yake usiku uliopita “nitakufa …
lakini….IPO SIKU YAO NA WENYEWE”
Hakumalizia, na sikujua alitaka kusema nini.
Kwanini afe na hao wenyewe ni kina nani??
 
SEHEMU YA PILI

Nikarejea hadi pale nilipokuwa nimesimama mwanzo,nikaanza kukitafuta kile kifurushi alichokiacha pale lakini sikukiona,nilihaha sana na kujiuliza nini kimemsibu yule kijana.Na ni kitu gani alikuwa ameniachia katika fundo lile la nguo??
Lazima kilikuwa kitu cha msingi maana alionyesha kusihi
sana.

Swali gumu jingine likawa,yule bwana amejuaje kama nitakuwa stendi asubuhi ile hadi aniletee ujumbe ule.
Nikiwa bado katika mtihani mgumu,mara basi nililotakiwa
kusafiri nalo likapiga honi kuashiria kuwa dakika yoyote ile
linaondoka.
Ule utata ambao huwa naujenga kwa wahusika katika
simulizi sasa ukajijenga katika nafsi yangu na sikujua
nautatua vipi?
Katiba basi tayari begi langu lilikuwa kule, sikukipata
kifundo nilichoachiwa na mtu niliyeamini kuwa ni Anti
Ezekiel.
Na ubaya mwingine sikujua hata kitu kilichokuwa kinamsibu
Ezekiel.
Nikayakumbuka maneno yake usiku uliopita “nitakufa …
lakini….IPO SIKU YAO NA WENYEWE”
Hakumalizia, na sikujua alitaka kusema nini.
Kwanini afe na hao wenyewe ni kina nani??
Nafsi yangu haikubariki wazo lolote kati ya hayo matatu
yaliyokuwa yakinihangaisha kwa wakati ule. Ni kama
nilikuwa mbumbumbu wa sekunde kadhaa. Ufahamu
ulinirejea baada ya kumuona mtoto mdogo akiwa na
mfanowe kile kifundo mikononi mwake akirandaranda
maeneo ya pale stendi, nilimwendea mbio mara akageuka
na aliponiona akaanza kutimua mbio, sijui ni kipi alikiona
kwangu hadi akaanza kutimua mbio kiasi kile, nilitamani
sana atambue kuwa sikuwa na ubaya wowote bali nilihitaji
kile kifundo, lakini angeanza vipi kunielewa iwapo watoto
wadogo wasiokuwa na makazi maalumu maisha yao ni kama
kivuli tu hawaishi kukimbia siku zote, na ningejuaje huenda
alinifananisha na mgambo wa jiji ambaye husafisha
mazingira hadi watoto wasiokuwa na makazi.
Niliendelea kutimua mbio hadi akafikia lile geti la kutokea
nje ambalo magari huytumikia kupita pale, kwa sababu
yeye alikuwa mbele alifanikiwa kupenya lakini mimi nikiwa
mtu mzima nilizuiliwa, hakuna mtu aliyeruhusiwa kupita
pale pasipo na sababu za msingi, nilijitahidi kumweleza yule
bwana kuwa nina haja sana na mtoto yule lakini
hakuonekana kukaribia kunielewa, akaniomba nimpe tiketi
yangu ambayo itaonyesha kuwa nilikuwa ni abiria kweli
lakini hata ile tiketi sikuwa nayo kwani niliiacha katika begi
langu lililokuwa ndani ya gari. Kitendo cha kurejea ndani ya
basi kufuata tiketi kingekuwa cha kizembe tena
kisichostahimilika na kile kifundo nisichokijua kingepotea
hivihivi mbele ya macho yangu na kila kukicha ningeendelea
kuteseka pasi na kujua ni ujumbe gani ulikuwa katika
kifundo.
“Naomba nipite yule mtoto ameniibia!!!!” nilidanganya ili
yule jamaa aweze kunielewa lakini aliendelea kuweka
ngumu. Hasira zikanipanda na kuamua kufanya maamuzi,
nikamsukuma kando kwa nguvu, akajikwaa na kupiga
mweleka huko. Hapo sasa nikapenya kwa kasi, nyuma
nikasikia filimbi ikipigwa, sikujali nilichohitaji ni kile
kifundo, kwani kwa kukipata kile basi ningeweza kuituliza
nafsi yangu.
Niliangaza huku na kule pasi na mafanikio ya kumwona yule
mtoto, nilijaribu kuwaulizia watu juu ya mtoto yule lakini
hakuna aliyejishughulisha nami, nd’o kwanza kulikuwa
kunakucha na kila mtu alikuwa akijipanga kuikabili siku ile.
Sikukata tamaa, niliendelea kuangaza huku na kule,
nilijitahidi sana kukumbuka kuwa mtoto yule hakuwa na
nywele kichwani na alikuwa na kaptula iliyopasuka pajani,
sikuwa nikiijua sura yake.
Nikajificha mahali na kuendelea kufuatilia nyendop za watu
mbalimbali, baada ya dakika zipatazo kumi nikafanikiwa
kumuona mtoto yule, mkononi hakuwa na kile kifundo lakini
alikuwa ni yeye.
Nikamnyemelea na kufanikiwa kumkamata, nilimuuliza
maswali kadhaa, akakiri kukiokota kifundo kile na alikitupa
mahali, niliongozana naye hadi mahali alipodhani
amekitupa.

Tukafanikiwa kukipata, nikampataia pesa ambayo angeweza
kunywa chai na kula chakula cha mchana siku hiyo,
nikakishindilia mfukoni, na hapo nikachukua pikipiki na
hima nikamuamuru dereva alifukuzie gari ambalo lilikuwa
na begi langu na tayari lilitoka stendi.
Wakati tunakubaliana bei na dereva mara niliguswa bega, ni
kama alivyonigusa Ezekiel. Nikageuka upesi nikidhani ni
Ezekiel tena, lakini sasa sikukutana na sura ya mtu bali
ngumi kali katika shavu langu.
“We mpumbavu umejifanya mjuaji kunikimbia sivyo.”
Alikoroma kipande cha mtu ambaye nilimsukuma kule
getini ili niweze kukimbilia kile kifundo alichokuwanacho
yule mtoto.
Wakati nataka kujitetea nikamuona yule jamaa akijiandaa
kunirushia ngumi nyingine, nikajihami na kuruka kando.
Mwendesha pikipiki akaona isiwe tabu, akawasha pikipiki
yake na kutoweka mbali.
Akaniachia kizaazaa kinikumbe peke yangu.
Amakweli mchuma janga hula na wa kwao!!
Kipande cha mtu kikiwa na hasira, kikanikaba mkono wangu
kwa uimara wa hali ya juu. Akaanza kunivuta kuelekea
anapotaka yeye. Nikatambua kuwa nikifanya uzembe tu
hata lile begi katika gari litapotea, huyu kipande cha mtu
lazima angenifikisha katika chombo cha dola na hapo ndipo
mlolongo ungeanza, mbaya zaidi hata kitambulisho changu
cha kazi sikuwa nacho tena. Vyote vilikuwa katika begi
langu.
Akili yangu ikanituma kufanya tukio la mwisho ambalo
litaniweka huru, yule kipande akiwa ameridhika jinsi
alivyonikwida nami nilijilainisha na kisha ghafla
nikamfyatua mtama, mguu wake wa kushoto ukakutana na
ule wa kuume, akaniachia kisha akayumba na kuanguka
chini tena.
Nikatimua na kufanikiwa kuvuka upande wa pili wa
barabara, nikakuta pikipiki nyingine, nikakwea na kutoa
maelekezo kama yale niliyotoa awali kwa yule aliyenikimbia
baada ya kupata msala.

Tukatoweka!!

Baada ya dakika thelathini nilikuwa nahema juu juu nikiwa
ndani ya basi siti ileile, yaliyotokea yote yalikuwa kama
ndoto. Sikuamini kama nimefanikisha mambo yote kwa
wakati na sasa nilikuwa katika safari yangu kana kwamba
hakuna kilichotokea.
Bahati nzuri nilikuwa siti ya dirishani hivyo upepo ulipunga
vyema na kunirejeshea amani pamoja na usawa katika akili
yangu ambayo kidogo ilikuwa imeanza kuvurugika.
Hapo sasa nilijipekua mahali ambapo nilihifadhi kile
kifundo, nilipanga nikifungue mwisho wa safari lakini
kihoro kikanisukuma kukifungua kabla hata safari ya
kuikaribia Morogoro haijakaribia.
Nilifungua kwa makini na tahadhari ya hali ya juu huku
nikijitahidi nisiiingie katika taharuki kwa kitu ambacho
nilikuwa sijakiona bado.
Kifundo kikawa wazi hatimaye na ndanmi yake kulikuwa na
funguo moja ambayo ilikuwa na kutu sana. Haikuonekana
kama ilifungua mahali fulani katika siku za karibuni na wala
haikuonyesha kama hata siku za usoni itakuwa na manufaa
kwa kufungua mahali. Ama la hapo pa kufunguliwa na
penyewe pana kutu na pamechakaa kwa kiasi kikubwa.
Funguo ya nini hii? Nilijiuliza huku nikifadhaika na kujiona
kuwa nilihangaika na kukaribia kuiokosa safari yangu kwa
sababu ya kitu kisichokuwa na mantiki.
Nikakifunga kile kifundo na kisha nikakiweka katika mfuko
wa suruali yangu!!
Na hapo nikamkumbuka Ezekiel, hali niliyomshuhudia akiwa
nayo maeneo ya Ubungo na hali niliyomshuhudia usiku
mmoja kabla baada ya vurugu kumkumba nami
nikamwokoa.

Alikuwa katika muonekano wa tofauti sana hasahasa
asubuhi hiyo, alikuwa muoga nma alitembea kikakamavu na
ni kama alikuwa akiongozwa na watu!! Kisha akatoweka.
Akatoweka na asionekane tena!! Ufunguo ule mmoja ni wa
nini? Na kwanini alinipa mimi?

Maswali haya yalinisumbua sana.
Simu yangu iliita na mlio wake ukayakatisha mawazo yangu
yasiyokuwa na dalili ya kufika kikomo.
Ni namba kutoka ofisini kwetu, nikaipokea na kupewa
taarifa kuwa semina iliyotakiwa kufanyika mjini Singida
imesogezwa mbele kwa siku mbili kutokana na sababu
ambazo nitaelezwa baada ya kufika Singida. Aliyenipigia
simu akanieleza kuwa nitapewa posho ya kutosha kuniweka
mjini pale hadi siku ya semina.
Simu hii ikanipa mwongozo mwingine, kama Singida hakuna
semina kwa siku hiyo basi ningeweza kurejea jijini Dar na
kama kuna lolote kuhusiana na Ezekiel na ule ufunguo basi
nitaling’amua.
Katika maisha yangu hakuna kitu nilikuwa sipendi kama
kubaki na majibu nusunusu!!!
Nilishuka Chalinze na kuchukua usafiri wa kurejea jijini Dar.
Bahati nzuri nikapata basi linaloenda Kariakoo moja kwa
moja. Nikakwea, na baadaye tulikuwa tunapita Ubungo,
nikatabasamu na kukumbuka balaa nililozusha asubuhi ile.

****

Niliujua ukorofi wa mama Eva ambaye ni mke wangu japo si
wa ndoa. Hivyo nilimjulisha kuwa narejea jijini Dar baada ya
dharula hiyo.
Nilifika nyumbani na kulitua begi langu kisha nikiwa na ule
ufunguo uliochakaa nilienda nyumbani kwa Ezekiel ili kama
kuna lolote niweze kutambua na nijue maana ya ufunguo
ule uliochakaa tena wenye kutu. Nilishukuru kuwa muda ule
nafika nyumbani mama Eva alikuwa ametoka kwenda sokoni
maana sikuliona kapu ambalo huwa anabebea mazagazaga
mbalimbali.
Upesi nikatoweka, safari hii sikumpa taarifa kuwa nimefika
na kuondoka kwani nilitarajia kurejea upesi.
Katika safari yangu kwa Ezekiel nilitarajia kukuta lolote lile
ambalo lingeweza kunipa mwanga iwapo kuna tukio
limemsibu Ezekiel, lakini hapakuwa na lolote la kushangaza
kila mmoja alikuwa katika harakati zake.
Chumba cha Ezekiel kilikuwa kimefungwa, nilijaribu
kugonga hodi japo kwa ushahidi tu lakini hapakuwa na
majibu.
Ili kuingia ndani ya nyumba ile nilihitaji kuwa na funguo!!
Kutaja neno ufunguo nikakumbuka kitu!
Ni hapo nikaukumbuka ule ufunguo wenye kutu.
Nikajipekua na kuibuka na kile kifundo nikakifungua upesi
na kuibuka na funguo wenye kutu. Japo sikuwa naamini
sana kama yaweza kuwa kweli nililazimika kujiaminisha.
Nikatazama kushoto na kulia hakuna hata mtu mmoja
aliyejishughulisha na mimi, nikajikoholesha kama yupo
ambaye atasema nami bado hakujitokeza mtu yeyote.
Naam!! Ufunguo ukakifungua kitasa, nikaingia ndani.
Sasa mbona una kutu huu funguo?? Nilijiuliza huku roho ya
kipekuzi ikiniandama, na ni hii roho ilinituma mara kwa
mara kufanya upekuzi mara kwa mara. Hata katika ofisi
niliyoajiriwa walinitambua kwa tabia hii isiyokera bali
kuwashangaza.
Mara nikakizoea kile chumba, nikaangaza huku na kule
sikuona mabadiliko yoyote yale, nikajiuliza kama niliota
kuonana na Ezekiel ama tulionana kweli.
Kama hatukuonana ule funguo ningeutoa wapi? Macho
yangu yakavutika na karatasi iliyokuwa mezani, ilikuwa
imeandikwa kwa wino mweusi mwandiko wa
kuyumbayumba, bila shaka mwandishi aliandika huku akiwa
na haraka sana.

“CHUMBANI USIACHE…PEKUA HATARI OKOA” maandishi
yalisomeka vile, mapigo yangu ya moyo yakaenda
mbiombio, nikaukumbuka mdomo wa Ezekiel kule Ubungo
ulikuwa unachezacheza ukisema maneno haya kwa kurudia
na sikuweza kutambua lolote lile.
Roho ya kidadisi ikazidi kunitawala, nikajiingiza kwa
tahadhari kubwa katika chumba cha Ezekiel. Nilipoufikia
mlango na wenyewe ulikuwa na tatizo lilelile, haukufunguka
hadi ule ufunguo wenye kutu ulipoutekenya!
“Vitasa vinafanana ama…..” nilijiuliza huku nikiufungua
vyema mlango.
Chumba kilikuwa kikubwa lakini hakikusheheni vitu vingi
sana, kabati la nguo na meza ya kujirembea ya wanawake.
Meza ile ya kisasa ilikuwa na mtoto wa meza, na juu
ulikuwa na vipodozi tele, haraka nikauendea mtoto wa
meza, nikauvuta na hapo nikakutana na makaratasi mengi
yakiwa yameandikwa mambo ambayo sikuyaelewa,
nikayatwaa yote na kuyajaza katika mfuko mmoja mweusi,
nikapapasa huku na kule sikukutana na kitu kingine
ambacho niliona kina maana kwangu.
Katika hayo makaratasi kuna yaliyokuwa yameandikwa na
mengine hayakuandikwa chochote.
Nikabeba, wakati nataka kutoka nje nikakumbuka karatasi
ile ilinisihi kupekua zaidi tena ilisema nisiache.
Nikaishughulisha akili yangu, nikapekua zaidi na zaidi,
mwisho kabisa nikatoa mashuka kitandani.
Hapa ndipo nilipokutana na jambo la kushangaza na
kushtua kuliko yote ambayo hadi kipindi hicho cha utu
uzima wangu macho yangu yaliwahi kushuhudia.
Sura haikuwa ngeni na ilifanana kabisa na ile niliyoonana
nayo asubuhi ya siku hiyohiyo maeneo ya Ubungo!!
Sura ya Ezekiel!!
Alikuwa ametulia tuli kitandani, bora angekuwa anasema
neno lolote ama anatabasamu.
Haukuhitaji utaalamu wa kidaktari kutambua kuwa
mwanadamu yule alikwishapoteza uhai siku nyingi sana, na
alikuwa ameanza kuharibika. Ezekiel hakuwa mweupe tena,
ngozi yake ilikuwa nyeusi, alikuwa uchi mnyama.
Kifurushi cha makaratasi kikanitoka mkononi, lakini
nilikumbuka kuuzuia mkojo uliotaka kunitoka. Miguu
ilikuwa inatetemeka na jasho jembamba lilinitoka.
Ezekiel aliyenipa funguo, Ezekiel sasa ameozea kitandani!!!
Tofauti ya masaa matatu tu!!

Hapana!!

Nikaanza kurudi kinyumenyume na hapo nikajikwaa kwenye
kile kifurushi na nikakumbuka kukiokota, ujasiri ukakaa
kando, nikashindwa hata kumfunika Ezekiel pale kitandani.
Mara mlango wa Ezekiel ukagongwa!!!
Sikujibu chochote kile!! Mara sauti ya kike ikaita jina lake.
Hofu ikazidi kutanda, yule ni nani anayemtafuta Ezekiel, na
je anamtafuta Ezekiel aliye hai ama huyu anayeozea
kitandani!!
Maswali yakawa lukuki huku nikiwa sina majibu, na sauti
kutoka nje ikazidi kuita.
 
Ngoja nijiwekee alama, huenda mpaka ikiendelea ntakuwa nimeshasahau nilipoishia👌👌👌👌
 
SEHEMU YA TATU
Sura haikuwa ngeni na ilifanana kabisa na ile niliyoonana
nayo asubuhi ya siku hiyohiyo maeneo ya Ubungo!!
Sura ya Ezekiel!!
Alikuwa ametulia tuli kitandani, bora angekuwa anasema
neno lolote ama anatabasamu.
Haukuhitaji utaalamu wa kidaktari kutambua kuwa
mwanadamu yule alikwishapoteza uhai siku nyingi sana, na
alikuwa ameanza kuharibika. Ezekiel hakuwa mweupe tena,
ngozi yake ilikuwa nyeusi, alikuwa uchi mnyama.
Kifurushi cha makaratasi kikanitoka mkononi, lakini
nilikumbuka kuuzuia mkojo uliotaka kunitoka. Miguu
ilikuwa inatetemeka na jasho jembamba lilinitoka.
Ezekiel aliyenipa funguo, Ezekiel sasa ameozea kitandani!!!
Tofauti ya masaa matatu tu!!
Hapana!!
Nikaanza kurudi kinyumenyume na hapo nikajikwaa kwenye
kile kifurushi na nikakumbuka kukiokota, ujasiri ukakaa
kando, nikashindwa hata kumfunika Ezekiel pale kitandani.
Mara mlango wa Ezekiel ukagongwa!!!
Sikujibu chochote kile!! Mara sauti ya kike ikaita jina lake.
Hofu ikazidi kutanda, yule ni nani anayemtafuta Ezekiel, na
je anamtafuta Ezekiel aliye hai ama huyu anayeozea
kitandani!!
Maswali yakawa lukuki huku nikiwa sina majibu, na sauti
kutoka nje ikazidi kuita.
Upesi nikatoka kule chumbani na kujichanganya sebuleni
nikiwa na kifuko changu mkononi nikijiandaa kukabiliana na
huyo ambaye alikuwa anabisha hodi.
Mapigo ya moyo yalikuwa juu sana na sikuweza kujizuia
kuitangaza hofu yangu waziwazi.
Nilipofika sebuleni na Yule mgongaji alikuwa anaingia.
Haikuwa mara ya kwanza kuonana na yule mwaamke, lakini
haikumaanisha kuwa nilikuwa naye karibu sana. Mara kwa
mara tulikutana asubuhi katika kituo cha mabasi kila mmoja
akienda anapojua mwenyewe.
“Mambo….mambo kaka” alinisalimia huku akionekana
kuusoma uso wangu katika namna ya wasiwasi.
Labda alidhani najihusisha kimapenzi na yule mwanaume
anayesadikika kuwa ni shoga.
Yule dada lazima alihisia kuwa nina uhusiano na Anti
Ezekiel. Nilijilazimisha kutabasamu ili kumwopndoa
wasuiwasi na hapo akanishambulia kwa swali moja zito
ambalo sikujiandaa kulijibu. Wakati nadhani ataniuliza
Ezekiel kama yupo ama la, aliniuliza kama Ezekiel bado
amelala.
Hapo nikajaribu kuzungumza lakini nikashindwa kusema
neno lolote. Ina maana Ezekiel alikuwa amelala na kuna
baadhi ya watu walikuwa wanafahamu ama. Sasa akama
alikuwa amelala na yule aliyenipa funguo kule Ubungo ni
nani?
“Aaah…hayupo Ezekiel hayupo…kwani nani alikwambia
alikuwa amelala.” Nilimweleza bila kujipanga. Na hapo
nikausoma wasiwasi wake moja kwa moja usoni.
“Acha utani basi kaka….” Alilaumu huku akionyesha fadhaa
waziwazi.
“Hayupo dadangu…” nilisisitiza.
Yule dada akaamini kuwa nilijaribu kufanya naye utani
wakati hakuwa na utani hata kidogo, na hapo nikatambua
kuwa alikuwa na ufahamu mkubwa na uzoefupia katika
nyumba ile. Akanipita na kuelekea chumbani kwa Ezekiel
huku akiita jina la Ezekiel kwa mikogo.
Akili ikaniambia kuwa kama ni mtego tayari ulikuwa
umefyatuka na ni lazima ningejikuta nimenasika.
Upesi nikapepea na mfuko wangu mfukoni.
Nilipotoka nje nikaamua kutimua mbio kabisa, nikiwa na
kile kifurushi kuelekea nyumbani, nilijikwaa mara kwa mara
lakini sikusimama baada ya dakika tano tayari nilikuwa
katika mlango, na nilitanabai kuwa mke wangu naye
alikuwa amefika muda si mrefu kutokea sokoni.
“Na wewe…nini kimekusibu.” Aliniuliza huku akinishangaa,
alikuwa ameshika kiuno. Macho yake aliyakazia miguuni
mwangu na nilipojitazama nikagundua kuwa sikuwa na
viatu mguuni bali nilikuwa nimevaa soksi pekee.
“Viatu vipo wapi?” alinitupia swali jingine. Bado sikuweza
kujibu na niklibaki kubung’aa kama zezeta tu. Mama Eva
akanikaribia na kunitikisa na hapo kidogo nikatanmbua
kuwa kuna kitu nilitakiwa kufanya, nikaingia ndani huku
nikitweta, nikautua ule mfuko kitandani. Mama Eva
akanifuata huku akisisitiza kuwa kuna jambo natakiwa
kumweleza, sikumjibu kitu chochote kile.
“Niwekee maji ya kuoga,…ama acha nitaweka mwenyewe
maji ya kuoga…hivi yanatoka bombani ama…” nilizungumza
bila kituo nikijitahidi kujizuia bila mafanikio.
“Umekuwaje baba Eva…” alihoji sasa alimaanisha zaidi.
Sikumjibu na badala yake nikachukua ndoo, nikaenda
bombani na kuchota maji, nikamwahidi kuwa nikitoka kuoga
nitamsimlia kilichojiri huko nilipotoka, akanikubalia kwa
shingo upande.
Wakati naoga nilizidi kuilazimisha akili yangu ikae sawa.
Nilimuwaza yule mwanamke niliyeonana naye wakati
natoka katika chumba cha Ezekiel. Swali kubwa lilikuwa ni
iwapo yule dada anatambua nyumbani kwangu ni wapi, na
swali jingine lilikuwa juu ya maongezi yake. Alidai kuwa
Ezekiel alikuwa amelala chumbani wakati mimi nimemuona
tena akiwa anaelekea kuoza.
Haikuwa mara yangu ya kwanza kuona maiti!! Sikuwa na
shaka kwa nilichokiona.
Nilijimwagia maji nisipate walau hisia kama ni ya baridi
ama ya moto, manukato yaliyotoka katika ile sabuni
hayakuniingia katika hisia hata kidogo. Nilikuwa niponipo
tu, nilijua kuwa ninaogopa lakinbi sikujua nafanya nini ili
kujitoa katika hali hii.
Mara katika mawazo yangu ikaniajia sauti ya yule
mwanamke, ni kama alikuwa anapiga kelele, anapiga kelele
akinitaja, nikajigongagonga kichwa mara sqauti zile
zikakatika, lakini tena zikarejea kama mauzauza sasa
nilimsikia akiongea na watu, sauti ileile. Baada ya yeye
kuzungumza nikasikia sauti ya kiume, baada ya sauti ya
kiume nikasikia sauti ya kike. Sauti hii sasa ilikuwa ya mke
wangu,mama Eva.
Bafu letu la nje halikuwa refu sana, nikanyanyua miguu juu
nikisimamia kucha ili niweze kuona kama hizo sauti ni kweli
ama ni mawazo yangu tu!! Wakati huohuo nikajiapiza kuwa
kama nikimaliza kuoga, nitammweleza mke wangu kila
kilichotokea naye atanishauri nini cha kufanya, lakini
nitaenda na wazo langu kuwa sitakiwi kuwa kimya!! Na
kubwa zaiodi sitakiwi kuwa mtaa huo.
Nilitambua kuwa itakuwa ngumu kwa m,ke wangu
kunielewa kutokana na wivu wake, lakini ilikuwa lazima
anielewe ili niwe huru na mwenye amani.
Kichwa kilifanikiwa kutoka nje na hapo nikamuona mke
wangu, na wanaume wawili na mwanamke mmoja ambaye
sikuhangaika kumtambua kuwa alikuwa ni yule ambaye
tulikutana katika nyumba ya Ezekiel na kisha nikatoroka
nikimwacha akakabiliane na kimbembe chumbani.
Kimbembe cha maiti ya Ezekiel.
Mapigo ya moyo yakaongeza kasi yake na hapo nikasikia
joto kwa mbali miguuni. Nilikuwa najikojolea.
Maaskari!! Niliwaza kitu kile, nikataka kujipa moyo kuwa
sasa ningeweza kutoka na kuzungumza nao lakini
nilipowatazama kwa makini walikuwa na nywele ndefu.
Si kwamba hakuna askari mwenye nywele ndefu lakini
mmoja alikuwa ni mzungu.
Wametoka wapi upesi kiasi kile.
Hatari!! Kengele zikapiga katika kichwa changu.
Kuendelea kushangaa isingeweza kusaidia, upesi
nikakwapua kaptula yangu na kuivaa, nikaachana na taulo,
nikapanda juu na kupitia katika dirisha nikaangukia kwa
nyuma, sikuishia hapo nikazunguka upesi upande wa pili
wa nyumba nikiwa vilevile na bukta yangu, nikawaona wale
watui wakiendelea kuhojiana na mke wangu na yule
mwaamke akiwahakikishia kitu ambacho sikiweza kukisikia.
Mikono ya mama Eva ilielekezea kule bafuni, nikajua
anawaambia kuwa nitatoka muda wowote. Nao
wakaendelea kusubiria, hadi yule mzungu alipomwambia
mwenzake akatazame, yule mtu mweusi akajipapaasa
kiunoni na hapo nikaona bastola.
Wanataka kuniua???
Kuna nini? Nilijiuliza huku nikitetemeka. Sikuwahi kuingia
katika mlolongo mzito kama huu hapo kabla, nilizoea
kupambana kwa maneno lakini sasa kuna mtu ananitafuta
akiwa na bunduki, nina hatari gani mimi?
Yule mtu mweusi alirejea akiwa ametaharuki, aliangaza
huku na kule kama anayetafuta kitu.
Mzungu akampokea kwa mfadhaiko, na baada ya chochote
walichoweza kuongea nilimwona mzungu akijipekua,
akatoka na kitu mfanowe pingu, akamfunga mama Eva na
kumuunganisha na yule dada.
Nilichanganyikiwa, nikataka kujitokeza na kupambana, nafsi
ikakubali lakini mwili ukasita, yule mzungu akaingia ndani
mwangu na kutoka baada ya muda, hakuwa amebeba
chochote. Nikamshuhudia kitoa maneno makali nisiyoweza
kuyasikia, kisha wakaongozana wote na kutoka eneo lile.
Nikabaki kuwasindikiza kwa macho.
Punde baada ya wao kutoweka nilitaka kurejea nyumbani
lakini nikahisi kuwa patakuwa na mtego wameweka, na
kuninasa mimi ingemaanisha kuwa kama ni taarifa kufia
hapo basi ni mimi chanzo.
Nilidumu katika fumbo hilo hadi alipopita Selemani, mtoto
mtukutu aliyejulikana mtaa mzima, nilimwita huku
nikijifanya kuwa niliamua tu kuwa katika vazi lile la kaptula.
Selemani alinishangaa lakini mkubwa mkubwa tu
hakuniuliza.
“Sele, nenda pale ndani kwangu, angaza pale katika kochi
kuna mfuko mweusi una makaratasi niletee, nenda sasa
hivi.” Nilimsisitiza naye akatoweka huku akiruka huku na
kule na kuimba nyimbo za wasanii anaowajua yeye.
Alipoondoka nilimsindikiza kwa macho hadi alipoingia pale
ndani, nil;iangaza kwa makini kama kuna mtu atamvamia
lakini hakutokea.
Hatimaye akatoka na mfuko mkononi, hakika nilikuwa
nimecheza pata potea. Maana kama wale watu walihitaji
mfuko ule basi ulikuwa umepatikana kirahisi. Mapigo ya
moyo yalienda mbio wakati nangojea kukabidhiwa mfuko
ule.
Hakuna lolote lililotokea Selemani akanifikishia mfuko ule
wenye makaratasi kama ulivyokuwa. Nikastaajabu kuwa
kivipi watu wale hawakuuona mfuko ule pale sebuleni hadi
waamue kumchukua mke wangu??
Ama hawatafuti mfuko?? Nilijiuliza tena.
Nikamuita Selemani tena, safari hii nikamuagiza suruali
yangu na shati.
“Nikuletee na karatasi lile?”
“Karatasi gani tena.” nilihoji.
“Utamfuata mkeo.” Alinambia huku akicheka, yeye
alichekeshwa nay ale maandishi lakini mimi yalinistaajabis
ha.
“Leta tuone..” nilimwambia naye akatoweka mimi nikabaki
na ule mfuko wenye makaratasi ambayo sasa niliamini
kuwa hayakuwa na maana tena.
Safari hii niliamini kuwa hapakuwa na uangalizi wowote wa
nyumba yangu, sikuwa katika uoga. Nikamsindikiza kwa
macho huku nikiamini atarudi salama.
Lakini haikuwa hivyo, wakati Selemani anaingia chumbani
mwangu, niliwaona anaume wawili. Sio wale wa awali lakini,
wakamvamia na kumvuta nje, wakamuuliza kitu nikaona
ananyoosha mkono kuelekea upande niliokuwa.
Na mara wale watu wakaanza kutimua mbio kufuata
uelekeo huo huku wakiwasiliana kwa simu zao.
Swikungoja kuambiwa, nikaanza kutimua mbio na kaptula
yangu mfuko mkononi, miiba ilinichoma lakini sikukumbuka
kupunguza mwendo. Hali ya hatari ilikuwa nyuma yangu.
Nilikaza mwendo zaidi na hatimaye nikaanza kusikia
vishindo vikijongea nyuma yangu kwa kasi kubwa!!
Nimekwisha!!! Nilijisemea!!
 
SEHEMU YA NNE
Lakini haikuwa hivyo, wakati Selemani anaingia chumbani
mwangu, niliwaona anaume wawili. Sio wale wa awali lakini,
wakamvamia na kumvuta nje, wakamuuliza kitu nikaona
ananyoosha mkono kuelekea upande niliokuwa.
Na mara wale watu wakaanza kutimua mbio kufuata
uelekeo huo huku wakiwasiliana kwa simu zao.
Swikungoja kuambiwa, nikaanza kutimua mbio na kaptula
yangu mfuko mkononi, miiba ilinichoma lakini sikukumbuka
kupunguza mwendo. Hali ya hatari ilikuwa nyuma yangu.
Nilikaza mwendo zaidi na hatimaye nikaanza kusikia
vishindo vikijongea nyuma yangu kwa kasi kubwa!!
Nimekwisha!!! Nilijisemea!!
KILICHONISAIDIA ni uenyeji wangu katika mitaa ile,
niliongeza kasi na kisha nikapinda mkono wa kushoto
ghafla na baada ya hatua mbili nikayumba kulia na hapo
nikakutana na kichochoro kingine na kwa mbali ulikuwa ni
uwanja wa mpira. Uwanja ambao zilizuka vurugu siku
kadhaa nyuma na kunikutanisha na Ezekiel na sasa nipo
katika balaa.
Kulikuwa na wachezaji uwanjani wakiwa katika mazoezi,
nikaona hiyo ni nafasi ya kipee ya kupata wasaidizi.
Nikaanza kupiga mayowe kwa jitihada zote huku nikipepea
mikono juu.
Kumbuka nilikuwa kifua wazi!! Wanasoka wale wakabaki
kunishangaa mimi huku wengine wakisogea nyuma na
pembeni kwa tahadhari ya lolote baya ambalo nilikuwa
nakabiliwa nalo.
Walinipokea huku wakisubiri kuona ni kitu gani kinanifanya
nirukwe akili vile.
“Majambaziii majambaziiii…..” nililalamika huku pumzi
zikikata na hofu ikitanda zaidi.
Kusikia neno majambazi, tahadhari kubwa zaidi
ikachukuliwa kila mmoja akawa katika mkao wa kujiokoa
mwenyewe. Macho yakatazama pande kuu nne za dunia
lakini hakuna kilichotokea. Umakini ukaongezeka hadi wa
kutazama pande zote kumi na sita, thelathini na mbili na
hadi sitini na nne. Hapakuwa na kitu chochote cha hatari
kilichojongea pale uwanjani.
“Huyu chizi huyu labda…” mchezaji mmoja akatoa hoja hiyo.
Wenzake wakamkanya na hapo wakamtambulisha kuwa
mimi ni mwandishi wa habari katika gazeti fulani. Licha ya
yeye kuduwaa, mimi niliduwaa maradufu. Kumbe najulikana
sana.
Yule aliyetoa shutuma za kuwa mimi nina wazimu
akagwaya!! Akaungana na wenzake kuendelea kungoja hayo
majambazi.
Bado hayakutokea!!
Wakaanza kupungua mtu mmoja baada ya mwingine,
nikahisi vichwani mwao wamekubaliana na wazo la yule
mwenzao kuwa huenda nimepandwa na wazimu.
Hatimaye nikabaki peke yangu, kifua wazi!! Kifurushiu
mkononi. Kila mmoja akaendelea na shughuli zake, hakuna
ambaye alikuwa tayari kuniamini. Nikiwa kifua wazi
nikalazimika kuendelea kukimbia maana niliamini kuwa
wale watu wabaya walikuwa wakinifuatilia.
Nilitembea kwa tahadhari huku nikiamini kuwa watu
kadhaa waliokuwa wananifahamu walikuwa wakinishangaa.
Nilipenya nyumba kadhaa hatimaye nikafika nyumbani kwa
Enock, rafiki yangu ambaye kabla ya kuhamia kwake ni
mimi nilimkaribisha jijini na akaishi nami chumba kimoja
kabla sijaamua kuishi na mama Eva.
Nilimkuta mnkewe yeye alikuwa ametoka kidogo. Mke wake
ambaye ni shemeji yangu alishtuka kuniona katika ile hali,
nikiwa katika pensi na mkononi kifurushi kikiwa na
makaratasi ambayo ni mimi pekee niliamini yalikuwa yana
umuhimu.
Shemeji alinikaribisha ndani huku macho yake yakikwepa
mara kwa mara kunitazama.
“Shem…hebu mwambie Enock akatishe zoezi la kuoga aje
kunisikiliza” shemeji akaruka upesi na kuelekea bafuni,
hakurejea tena badala yake Enock akiwa amevaa taulo
alitokea sebuleni.
“Kaka nini tena hiki….kimetokea nini…mama Eva ama??
Yaani mmefikia huku.” Alizungumza upesiupesi asinipe
nafasi ya kusema lolote, nikaamua kumkatisha, “Noki eeeh!!
Hebu nisikilize bwana…..” nilifoka kisha nikamsimulia kwa
ufupi kuwa haja yangu ya kwanza ilikuwa nguo. Hilo
hapakuwa na utata, miili yetu iliendana hivyo ningeweza
kuvaa nguo zake. Akanitimizia hilo mara moja nikavalia
palepale sebuleni. Na baada ya pale nikamwomba anipatie
kiasi fulani cha pesa, uzuri ulikuwa mwisho wa mwezi na
alitambua ni fadhila kiasi gani nimewahi kumtendea.
Nikamtajia kiasi akaniahidi kunipa kiasi chote kama
nilivyoomba.
“Mengineyo nitakupigia simu uje mahali tukae tuzungumze,
hapa si mahali sahihi hata kidogo. Kuna watu wabaya wasije
wakazua lolote la kuzulika.
Enock hakunielewa kabisa lakini hakuwa na la kufanya,
nilikuwa nimefedheheka na akili yangu ilikuwa haijakaa
mkao wa kusimulia juu ya Ezekiel kisha mazingaombwe ya
kumuona akiwa Ubungo hai na kisha akiwa maiti
anayeharibika kitandani baada ya nusu saa, mkasa wa mke
wangu kuchukuliwa kisha kuachwa ujumbe, mkasa wa
Selemani yule mtoto kukwapuliwa na watu wabaya kisha
kuanza kunifukuza mimi. Ningeweza vipi kusimulia tukio
lote kwa ufasaha wakati shemeji yangu alikuwa ameniona
nikiwa kama tahira tayari aliponikaribisha ndani.
Hakika sikuweza!!
“Enock….shemeji yako yupo matatani hadi sasa sijui alipo,
tukionana hiyo jioni ama muda wowote ule uje unishauri.
Sijui kama yupo mwingine wa kunishauri zaidi yako”
nilimnong’oneza Enock kisha nikajivika vyema kofia
aliyonipatia, kifurushi changu nikakiweka katika mpangilio
mzuri, badala ya ule mfuko mweusi sasa niliyapanga
makaratasi yale katika bahasha kubwa ya kaki.
Dereva wa pikipiki akapigiwa simu, akafika hadi mlangoni.
Nikapanda pikipiki na kuagana na Enock mwenye mashaka.
“Nipeleke Ubungo maji.” Nilimpa maelekezo.
“Shilingi ngapi?” nilimuhoji.
“Jamaa amesema atalipia kila kitu cha msingi nikupeleke
popote utakapoenda.” Alinijibu. Kisha akavaa ngao ya
kichwani na kutokomea.
Wakati huo ilikuwa tayari saa saba mchana!!!
Upepo uliovuma wakati pikipiki ikizidi kushika kasi, kidogo
ulinipa ahueni ya kufikiri. Nilijiona mtu kati ya watu. Lakini
mtu asiyekuwa mkamilifu!!
Mke wangu alikuwa matatani. Na hawa jamaa hawakusema
naenda kumchukua wapi. Baadaye kidogo nikatabasamu
baada ya kugundua kuwa kile ninachokiandika kila siku sasa
kilikuwa kinanitokea. Maisha ya kwenye simulizi!!
Tulipofika Ubungo maji nilishuka na kumshukuru yule
bwana.
Baada ya kuondoka nikachukua daladala iliyonipeleka
maeneo ya kimara. Nilifanya vile ili kukwepa kupatikana
kirahisi iwapo tu mambo yatakuwa makubwa zaidi ya pale.
Nilichukua chumba maeneo ambayo yalikuwa yamejificha
sana. Nikajiandikisha jina la uongo na hatimaye nikawa
chumbani huru.
Nilihisi uchovu lakini sikutaka kulala, nikafungua bahasha
yangu. Kitu cha kwanza kukitoa ilikuwa ni picha ndogo ya
mtoto wa kiafrika alikuwa anatabasamu. Haikuandikwa
chochote kwa mbele lakini nyuma yake iliandikwa
‘MICHIGAN’.
Jina likanichanganya sana, hii Michigan ya bara la Amerika
ama Michigani ni jina la yule mtoto katika picha. Na inahusu
nini sasa picha hiyo!!
Nikabakli na swali kuu la kwanza, nikaiweka kando ile picha
nikakutana na makaratasi mengine, moja lilikuwa na
maandishi yaliyoandikwa na mtu ambaye anajifunza
kuandika ama ni maksudi aliamua kuhadaa kwa namna ile.
“THE DON 20 MKAKATI WA KUDUMU” Halikuandikwa neno
jingine zaidi.
Makaratasi yalikuwa mengi sana na pia picha mbalimbali,
nyingine nikamuona Ezekiel, alikuwa amekumbatiana na
mwanaume wa kizungu, kwa namna walivyokuwa Ezekiel
alionekana kama hapendi kushikwa vile lakini ilimlazimu tu.
Katika picha ya mzungu paliwekwa alama ya ‘x’….hapakuwa
na maelezo kwa nyuma.
Katika kila karatasi nilijaribu kubashiri majibu yangu lakini
hata moja halikuonekana kuendana na ukweli wowote
bambao ungeweza kunivusha hatua moja mbele.
Ina maana Ezekiel alikuwa analazimishwa kuwa alivyokuwa?
Nani alikuwa anamlazimisha?
Michigan? Ni kitu gani hiki?
Picha ya yule mtoto na yule mzungu aliyewekewa alama ‘x’
zinahusika vipi?
Haya yalikuwa baadhi ya maswali yaliyolundikana katika
kichwa changu!!
Kabla sijamaliza makaratasi mengine, nilihisi njaa kali, hapa
ni baada ya kusimama. Nilipoangalia saa ilikuwa saa kumi
na mbili na nusu jioni. Nikakumbuka sikuwa nimekula kwa
siku nzima.
Ahadi ya kukutana na Enock nayo ikawa imekufa, kwa
sababu simu yangu ya mkononi niliiacha ndani wakati
naenda kuoga na sikurudi tena kuichukua.
Nikajikongoja hadi nje na kufanikiwa kupata chakula. Nikala
kwa kadri ya mahitaji yangu na kisha nikalipia na kurejea
chumbani ambapo nilioga na kujaribu kujinyoosha kidogo.
Usingizi ulipoanza kuninyemelea nikajiahidi kuwa nitalala
kidogo na kisha kuamka, nipitie tena makaratasi yaliyosalia
ili siku inayofuata niende polisi kisha nifike kazini pia
kutafuta watu waelewa ambao wangeshirikiana nami katika
mkasa huu wa ajabu ambao hadi wakati huo ulikuwa
umenitia matatani.
Haikuwa kama nilivyojiahidi, nilikuja kushtuka majira ya saa
saa kumi na mbili asubuhi. Kitu cha kwanza kusikia zilikuwa
ni kelele zilikzokuwa zinapigwa na mwanamke, nilizisikiliza
kwa makini nitambue kama kuna hatari yoyote eneo lile
lakini nikang’amua kelele zile hazikuwa na wasiwasi
wowote na wala hazikuelezea uchungu wowote na badala
yake zilikuwa zinaelezea raha fulani na huyo aliyezipiga
hakujua kama alikuwa anapiga kelele na kusumbua wengine
ambao walikuwa wamelala tena peke yao.
Nikaghafirika na kuwashangaa wawili hao waliokuwa
wakifanya mapenzi kwa raha zao na kutupigia kelel
wengine.
Nikachukua rimoti na kuwasha luninga bila dhumuni lolote
ilimradi tu kukwepa kuzisikia kelele za mwanamke yule
ambaye kwa lugha moja ningeweza kusema hajastaarabika.
Nilisimama na kujinyoosha viungo kisha nikauendea mlango
wa bafuni, nikaingia kwa ajili ya kujistiri na haja ndogo.
Niliacha mlango wazi, sikuwa na shaka kwa sababu nilikuwa
mwenyewe.
Nikiwa maliwatoni, nilisikia vitu ambavyo akili yangu
ilinituma kuwa ni muhimu nivisikilize, upesi nikarejea
chumbani na kukuta mtangazaji akizungumza juu ya habari
fulani ya kuvutia.
“……mwandishi huyo ambaye alitimua mbio baada ya tukio
anasadikiwa kufanya mauaji hayo kwa makusudi.
Mwanamke aliyemshuhudia kwa jicho lake akitokea
chumbani mwa marehemu anadai mwandishi alitimua mbio
baada ya tukio hilo. Uthibitisho zaidi wa suruali yake
ambayo ilisheheni simu ya mkononi ambayo imethibitika ni
mali yake, pochi iliyokuwa na pesa taslimu laki tatu, katika
suruali palikutwa pia na sumu kali ya kuulia wanyama.
Jitihada za kumpata yeye na mkewe waliyekuwa wanaishi
naye ziligonga mwamba. Hata hivyo mtoto wao mdo
aliyejitambulisha kwa jina la Eva amehifadhiwa na jeshi la
polisi Tanzania. Huku upelelezi wa kuhakikisha Samson
Josephat na mkewe wanaingizwa nguvuni kwa kosa hilo la
mauaji.” Alipomaliza kusoma habari hiyo, ilionyeshwa picha
kwa ukaribu kabisa, ilikuwa ni suruali yangu, na pochi
ilikuwa yangu lakini sumu na zile pesa hazikuwa mali
yangu!!!
Na mbaya zaidi waandishi na maaskari wakaaminishwa
kuwa nguo zile zimekutwa katika chumba cha Ezekiel.
“Mungu wangu..kwani yule dada hakuniona kuwa nilikuwa
nimevaa suruali yangu na shati zuri kabisa!!” nilijiuliza kwa
sauti kama kwamba kuna yeyote wa kushirikiana nami
katika mjadala huu.
Wakati nawaza juu ya mchezo huu wa ajabu na mchafu
kuwahi kunikumba nikaikumbuka kauli ya mwisho ya
mtangazaji…”Mtoto wao mdogo aitwaye Eva…..”
Mapigo ya moyo yakapiga maradufu!!
Eva alinizoea mimi na mama yake tu!! Hakuna mtu
mwingine ambaye angeweza kuishi na Eva.
Mtoto wangu jamani!! Nilijikuta katika manung’uniko na
majuto wakati sijui najutia jambo gani!!
Mambo yalikuwa yameharibika.
Wakati nahangaisha kichwa changu kufikiria ni jambo gani
sahihi natakiwa kufanya, habari ile ikaendelea, wananchi
kadhaa walikuwa wakihojiwa juu ya tukio lile, macho yangu
yakamwona yule mchezaji aliyeniita mwehu. Alizungumza
kwa hisia kubwa sana akinishutumu kuwa alihisi tu kuna
jambo baya nimefanya lakini wenzake wakampinga!!
Nilitaka kumpiga ngumi lakini nikakumbuka kuwa kile ni
kioo, yeye hayupo pale.
Kwa siku ile sikuiona sura yangu ikirushwa kwenye luninga
lakini ningejuaje labda vituo vingine walirusha picha
yangu!! Hii ni hatari sana.
Mke wangu yupo wapi?? Hii ni hila ya watu wabaya kwa
sababu nimewakimbia basi wamemuunganisha na mke
wangu katika tukio mili kuunda ukweli, maana kwa
kumwacha yule angenitetea mpaka tone lake la mwisho la
damu.
Lakini hakuwepo tena!!
Safari ya kwenda kituo cha polisi kutoa taarifa ikaishia pale
na sasa nikawaza mengine, lakini hata yenyewe
hayakujiweka katika mkondo mahususi!!!
Nikapagawa!!!
 
SEHEMU YA TANO
Kwa siku ile sikuiona sura yangu ikirushwa kwenye luninga
lakini ningejuaje labda vituo vingine walirusha picha
yangu!! Hii ni hatari sana.
Mke wangu yupo wapi?? Hii ni hila ya watu wabaya kwa
sababu nimewakimbia basi wamemuunganisha na mke
wangu katika tukio mili kuunda ukweli, maana kwa
kumwacha yule angenitetea mpaka tone lake la mwisho la
damu.
Lakini hakuwepo tena!!
Safari ya kwenda kituo cha polisi kutoa taarifa ikaishia pale
na sasa nikawaza mengine, lakini hata yenyewe
hayakujiweka katika mkondo mahususi!!!
Nikapagawa!!!
Nikiwa na utambuzi fika kuwa mambo yamenikalia vibaya
mimi na familia yangu nikaamini kuwa huu ulikuwa wakati
muafaka wa kuishughulisha akili yangu mara elfu moja zaidi
nilivyojishughulisha kuandika simulizi ya KWAKO
MPENDWA, simulizi ambayo ilinipa tunzo katika kampuni
yangu.
Nilitambua kuwa thamani yangu haikuwepo tena na mtu
pekee wa kuweza kuirejesha ni mimi pekee. Upesi bila
kuoga nikavaa suruali yangu na kisha nikatoweka kutoka
katika nyumba ile ya kulala wageni. Wakati natoka
nilipishana na muhudumu wa kike ambaye alinipatia
chumba siku iliyopita.
“Shkamoo….habari za asubuhi kaka…” alijing’atang’ata
wakati wa kunipa salamu, kivipi binti ambaye tunalandana
katika suala la umri anisalimie ‘shkamoo’ tena alionekana
kubabaika waziwazi.
Sikumjibu chochote, badala yake nilitoka nje na kisha
kutokomea mbali zaidi na nyumba ile.
Usafiri wangu kwa mara nyingine ukawa pikipiki. Nikapenya
mitaa kadhaa na hatimaye nikafika Kibamba.
Nikiwa na kofia kichwani, nikafanikiwa kununua na miwani.
Nikajipachika usoni. Sasa niliamini kuwa hakuna ambaye
angeweza kunona. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuyaficha
macho yangu nyuma ya miwani.
Nilitazama huku na kule hadi nikayafikia magazeti. Gazeti la
kwanza kutazama lilikuwa ni Mwangaza. Gazeti ambalo
nilikuwa nafanya kazi hapo.
SAMSON AMESINGIZIWA: ASEMA MATATA.
Nilijikuta natabasamu kidogo, Alfred Matata; huyu ndiye
alikuwa mmiliki wa kampuni inayochapisha gazeti lile na
kwa namna ya pili alikuwa bosi wangu. Aliniamini sana
kupindukia na mara kwa mara alinishirikisha juu ya mambo
yake ya siri.
Walau mwajiri wangu ameutambua upande wa ukweli, huyu
ndiye ambaye angeweza kunisaidia mimi kujua naanzia
wapi. Nikalipia lile gazeti nikapatiwa nakala yangu na kisha
nikapuuzia vichwa vingine vya habari vilivyosisitiza kuwa
mimi ni muarifu na ninasakwa kwa udi na uvumba.
“MATATA MATATANI KWA KUMTETEA MUUAJI” Kichwa
hiki cha habari pia kilinivutia lakini nilipuuza baada ya
kugundua kuwa lile ni gazeti la udaku.
“Pumbavu kabisa…” nilijisemea huku nikitowewka eneo lile
na kuambaa upande mwingine wa barabara, nikafikia kwa
mama lishe ambaye alikuwa akichochea moto kwa ajili ya
kuanza rasmi kuisaka riziki yake, nikachukua nafasi katika
dawati lililokuwa pale.
“Chai bado sana…” nilizungumza huku nikilifunua gazeti.
“Kidogo tu baba yangu, lakini kitafunwa tayari, maandazi
yapo na mihogo hii hapa nageuza.” Alinijibu kwa staha.
Nikaendelea kusoma kurasa za gazeti lile.
Nikaipitia taarifa kuhusu Matata kukanusha juu ya madai
kuwa nimeua na kisha kukimbia. Kadri nilivyozidi kusoma
moyo wangu ulisuuzika na lile barafu gumu la uchungu na
wasiwasi lililokuwa limeniganda nikahisi likiyeyuka. Moyo
wangu ukafanya majuto kidogo kwa kitendo changu cha
kuwahi kujihusisha kimapenzi na binti wa mzee huyu, lakini
cha kushukuru ni kwamba hakuwahi kugundua. Na hata
baada ya kuanza kuishi kinyumba na Mama Eva,
nikamtupilia mbali binti yule ambaye alidai ataendelea
kunipenda kila siku.
Potelea mbali, sikuwahi kumpa mimba na wala sikuwahi
kumfelisha katika masomo yake!!
Nikaimaliza makala ile huku nikipata mwanga juu ya wapi
naenda kuanzia.
Kwa sababu mama Eva alikuwa amekamatwa kiujanjaujanja
basi mzee Matata angeweza kuwa mtu sahihi wa kuanza
kuzungumza naye na hata kumkabidhi makaratasi yale ili
tusaidiane katika ufumbuzi.
Nikaanza kuifikiria safari ya kurejea jijini Dar es salaam kwa
tahadhari kubwa ili niweze kuonana na mzee mwenye
hekima,. Mzee Matata. Tena nilitakiwa kufanya maamuzi
haraka sana kabla mambo hayajawa mazito na zile tetesi za
kipuuzi kuwa mzee Matata matatani kwa kutetea muuaji
hazijawa kweli.
Nilitambua kuwa kwa mujibu wa muda ingeweza kuwa saa
mbili za asubuhi, hata mama muuza naye nilipomuuliza
alinijibu kwa uhakika kana kwamba ana saa mkononi,
akasema ni saa mbili.
Wakati huo nilikuwa namalizia pande la muhogo!! Nikagida
chai na kufanya malipo kisha nikaambaa kuelekea kona
nisizozifahamu, maeneo ambayo hayakuwa karibu sana na
barabara.
Huko nikakutana na kibao kilichoonyesha nyumba ya kulala
wageni!!
Eneo muafaka kabisa kwangu kwa wakati ule.
Nikaingia pale na kukutana na muhudumu.
“Vyumba havijafanyiwa usafi kaka hadi saa nne ndo wateja
wa mwishomwisho wanatoka.” Balinijibu kichovu huku
akijifuta tongotongo machoni.
Nilijipigia hesabu za kichwa na mara nikakumbuka kuwa
wasiwasi wangu wa kurejea mjini, ulikuwa wa bure.
Mwanzo nilihisi kuwa mzee Matata atakuwa kazini, lakini
nikakumbuka kuwa asubuhi hiyo ilikuwa jumapili. Lazima
angekuwa nyumbani kwake. Nikaondoka na kisha
nikachukua pikipiki tena, bahasha yangu ikiwa kitu cha
muhimu kupita chochote katika mwili wangu!! Nikapepea
hadi maeneo ya Shekilango!!
Nikafanya malipo na kuchepuka kwa hatua kubwa kubwa
nikavuka barabara na kuingia vichochoro kadhaa, hatimaye
nikatazamana na nyumba ya mzee Matata. Makala yake
kuhusu mimi ikaendelea kunijengea uaminifu kwake,
nikagonga hodi nikapokelewa na mlinzi ambaye alikuwa
akinifahamu, sikutaka kuzungumza naye sana, nikaingia
hadi ndani, nikaufikia mlango mkuu wa kuingilia.
Aliyenipokea alikuwa mke wa mzee Matata, akanikaribisha
kwa ukarimu wote kama ilivyo kawaida yake, baada ya
salamu akaniuliza kama nitakunywa chochote, nikataka
kukubali lakini nikahisia nitapoteza muda wakati mihogo ya
mama lishe bado ilikuwa tumboni.
Nikashukuru na hapo nikamuulizia mzee Matata.
“Ameenda kanisani.” Akanijibu kwa sauti tulivu huku
akihangaika kupunguza sauti katika runinga iliyojiongeza
sauti kimakosa.
Jibu la mwanamke huyu likanistaajabisha lakini nikajificha
nisijulikane kama nimestaajabika, mzee Matata na kanisa
wapi na wapi? Kila siku ofisini alikuwa akitukashfu sana
watu tunaojifanya kuhudhuria kanisa wakati kanisa ni
biashara. Mzee Matata hakuwahi kusifia lolote juu ya
nyumba za ibada ambazo mkewe alikuwa muhudhuriaji
mzuri sana na hata watoto walifuata nyendo za mama yao.
Kasoro yeye tu!!
Iweje leo ameenda kuhudhuria ibada. Tena asubnuhi yote
ile.
Nikaguna lakini sikuuliza kingine nje ya uwezo wa yule
mama, badala yake nikaulizia atarudi saa ngapi.
“Ibada huwa inamalizika saa sita, nadhani unaweza
kukadiria.” Alinijibu, sasa alikuwa ananitazama machoni.
Nikapiga mahesabu yangu upesiupesi nikakutana na jibu la
uongo!!
Ibada ipi ya kumalizika saa sita wakati kwa maelezo ya
awali mzee Matata alitoka asubuhi sana.
Kwanini ananidanganya? Nilijiuliza huku nikijisikia vibaya
kudanganywa na mama yule mtu mzima.
“Haya mimi nipo jikoni mara moja…rimoti hiyo unaweza
kubadili chaneli” alitoa kauli hiyo huku akisimama na
kujifunga kanga yake vyema kisha akatoweka.
Hakuelekea jikoni!!! Uongo mwingine. Mzee Matata kama
nilivyokwisha elezea alikuwa mzee wangu wa karibu kuna
kipindi mkewe akiwa masomoni niliishi nyumbani kwake,
kwa siku kadhaa nilizijua kona nyingi sana. Na hata mtoto
wake nilimpata kipindi hicho.
Nililifahamu jiko lilipokuwa, lakini mwanamke huyu
hakwenda jikoni!!
Kwanini?
Wakati najiuliza na kuumiza kichwa juu ya hayo mara mtu
alivamia sebuleni ghafla huku akiweka tahadhari juu ya
uwepo wake katika sebule ile.
Nikashtuka kidogo, nikamtazama na kuwahi kutaka
kumsalimia, lakini kabla sijasema lolote akaniziba mdomo.
Mikono yake ya uvuguvugu iliyokuwa inanukia marashi
haikunikera.
“Sam….wanasema umeua, umeua jana Sam. Sikia kama ni
kweli umeua Sam, hapa si mahali sahihi hata kidogo pa
wewe kukaa hata kwa sekunde moja. Baba na mama
wametishwa sijui na nani? Wameambiwa wanatambua
wewe ulipo Sam, kama mama amekwambia baba ameenda
kazini ni uongo mtupu, amepeleka vyeti vyako vyote vya
shule polisi amepeleka picha na kila kitu kuhusu wewe,
alama yako ya dole gumba, jaribu kunielewa sam.
Amepeleka kila kitu!!! Kila kitu sam….Sam pliiiz Sam unajua
kuwa nakupenda, na kwa namna yoyote aidha umeua ama
hujaua, sam nakutambua kama mwanaume mkarimu kupita
wengi katika maisha yangu, sikukosea kukupenda sam, na
nilikuahidi kuwa nitakupenda milele, Sam ukiendelea kuwa
hapa watakufunga Sam. Sitaki kujua kwa nini uliua lakini
sitaki kusikia ukihukumiwa kunyongwa. Mlizni getini
aliambiwa ukionekana hapa asikuruhusu kutoka tena. Na
makala aliyoiandika upesi upesi alitaka kukujenfea imani
naye. Baba anatamani upatikane ili kampuni yake iendelee
vizuri Sam….” Alishindwa kuendelea kuzungumza yule binti
akaanza kutokwa na machozi. Bado alikuwa ameniziba
mdomo. Alikuwa anatetemeka na uso wakle ulimaanisha
kila alichokuwa anasema.
“Anitha…sikia Anitha ukilia si ndo utanipoteza mimi ama…
nyamaza nambie nafanya nini, Anitha sijaua hii ni njama tu.
Njama ya kuniteteketezaq family yangu kutokana na siri
nzito Anitha. Siri ambayo…..yaani aaah…Anitha nisaidie
nitoke.” Nilimwambia kwa kunong’ona huku kiganja changu
kikiwa kimejikita katika kubadili Chaneli hovyohovyo bila
sababu za msingi, nilikaa mfumo wa nusu tako kitini nusu
nyingine isieleweke kama ipo hewani ama imefanya mgomo
wa kukaa.
Ni kama nilitaka kusimama.
“Sam….Sam…mama mama huyooo atajua….” Aliweka
tahadhari na kisha akatimua mbio kuelekea vyumbani.
Na hapo akafika mama mwenye nyumba, nilirudisha miwani
usoni asiweze kuisoma hofu yangu!!
“Anakuja baada ya kama nusu saa hivi, kumbe wametoka
tayari. Pole kwa kumsubiri shemeji yangu jamani.”
Alinikarimu, lakini sasa sauti yake ilikuwa katika namna ya
maigizo na uso wake ukitangaza hasira.
Nikayaamini maneno ya Anitha, msichana ambaye aliwahi
kuwa mpenzi wangu lakini kutokana na heshima kubwa
niliyokuwanayo kwa mzee wake nikaamua kuyatupia
mapenzi kando.
Sasa alikuwa amenionyesha maana ya upendo!! Anitha
hakuwa ameamini hata kidogo juu ya tetesi za mauaji
niliyofanya, na hata kama ni kweli alikuwa amesisitiza kuwa
hatajali.
Mwanamke wa kipekee!!
Mama aliendelea kupiga porojo zake nami nikaweka
tabasamu bandia, alisema anarejea baada ya nusu saa na
Anitha alinieleza kuwa mlinzi alizuiwa asiniruhusu nitoke
baada ya kuingia.
Hawa jamaa ni akina nani hawa? Inawezekana wakawa ni
polisi kweli wameamini kirahisi hivyo kuwa nimeua?
Nilijiuliza na dakika kumi na tano zilikuwa zimekatika!!
Mama alikuwa akiongea maneno mengi tofauti na kawaida
yake!! Nikajua hii ni njama nyingine ya kunihadaa, njama ya
kunipotezea wakati ili mumewe afike na polisi ama na
yeyote yule waweze kunikamata.
Na kama ni njama walikuwa wamefanikiwa haswa! Ningeaga
vipi pale na kuweza kutoroka na kisha kujipanga upya.
Ghafla wazo likajikita katika ubongo.
“Hivi mama zile picha za sherehe ya kutimiza miaka hamsini
zipo ujue siku ile mama Eva alinighasighasi hata
sikuzitazama vyema…”
“Wacha weee!! Haukuziona kumbe ngoja nikuletee maana
zipo katika albamu…nzuri hizo.” Alisifia huku akiondoka,
nikaisoma akili yake kuwa yule mama alikuwa
amejidanganya kuwa kwa kuangalia albamu ile nitakuwa
nimemsaidia katika zoezi la kuuvuta muda maana kama ni
maongezi hakika alikuwa ameishiwa.
Wakati huo zilisalia takribani dakika tisa itimie ile nusu saa
aliyoisema mama huyu kuwa mzee Matata atarejea.
Alipotoka na mimi nikaishika vyema bahasha yangu na
kusimama, kumbe Anitha alikuwa akinitazama kupitia
alipokuwa amejificha.
“Anitha, kama wakinikamata usiachie hii bahasha iende
kizembe. Humu kuna kila kitu!!” nilimwambia kwa sauti ya
kukwaruza kwaruza. Na nikamwona macho yake yakilengwa
na machozi. Sikugeuka tena.
Nikaondoka na kulifikia geti, geti lilikuwa limefungwa kwa
kufuli lakini halikuwa limebanwa, nilipojongea nd’o kwanza
mlinzi akalibana lile kufuli kisha akaendelea kuvuta sigara
huku akipuliza moshi hewani.
Ametimiza wajibu!! Nilijisemea huku akili ikigoma kabisa
kujua ni kipi nafanya kwa wakati huo. Nilijua kuwa Anitha
ananitazama kwa huzuni kubwa, nilijua mama amekaribia
kufika tena sebuleni akiwa na albamu, na kubwa zaidi
nilitambua kuwa mzee Matata si rafiki tena bali adui
mkubwa na muda wowote ule anawasili hapo kwa ajili ya
kunikamata aidha akiwa na polisi ama akiwa amehadaika na
njama za wale watu wabaya waliochanganyikana na
wazungu!!!!
Miguu ilikuwa inatetemeka na bahasha ikaanza kulowa
jasho, jasho jepesi kutoka katika kwapa lililokuwa limeibana
vyema.
Nimekamatika!!
 
SEHEMU YA SITA
Nikaondoka na kulifikia geti, geti lilikuwa limefungwa kwa
kufuli lakini halikuwa limebanwa, nilipojongea nd’o kwanza
mlinzi akalibana lile kufuli kisha akaendelea kuvuta sigara
huku akipuliza moshi hewani.
Ametimiza wajibu!! Nilijisemea huku akili ikigoma kabisa
kujua ni kipi nafanya kwa wakati huo. Nilijua kuwa Anitha
ananitazama kwa huzuni kubwa, nilijua mama amekaribia
kufika tena sebuleni akiwa na albamu, na kubwa zaidi
nilitambua kuwa mzee Matata si rafiki tena bali adui
mkubwa na muda wowote ule anawasili hapo kwa ajili ya
kunikamata aidha akiwa na polisi ama akiwa amehadaika na
njama za wale watu wabaya waliochanganyikana na
wazungu!!!!
Miguu ilikuwa inatetemeka na bahasha ikaanza kulowa
jasho, jasho jepesi kutoka katika kwapa lililokuwa limeibana
vyema.
Nimekamatika!!
**Rafiki hugeuka adui, usimwamini mtu kwa asilimia mia.
Jiamini wewe kwa sababu kamwe huwezi kujidanganya na
hata ukijidanganya utatambua kuwa unaponda maji kwenye
kinu!!!! Yaani ni kazi bure……
Lakini moyo wa mwenzako ni kiza kinene!! Huwezi kujua…….
JIFUNZE
ENDELEA
AKILI ilikuwa imesimama na si haba nilielekea kuwa
mwendawazimu huku nilichokumbuka pekee ni midomo
yangu kutetemeka huku nikimtaja Eva na mama yake.
Mizimu niliyoiomba haikuniletea muujiza wowote.
Mlinzi Yule aliendelea kucheka kifedhuli huku akijitahidi
kadri ya uwezo wake kuvuta sigara na kupuliza moshi
hewani katika namna ya majigambo.
Nikiwa katika hali ileile niliisikia sautio nyembamba ya kike
ikisema name katika namna ya kusihi, nilipata nguvu ya
kugeuka huku nikiilazimisha akili yangu isijiruhusu
kukutana na mama mwenye nyumba.
Kha!! Hapakuwa na mtu yeyote, hii nayo ikanistaajabisha.
Lakini sauti iliendelea kusihi. Nikajipa ujasiri huku nikijitoa
hofu kuwa mimi si mwizi wala sijaua. Na kwa misingi hiyo
sitakiwi kuwa muoga.
Kwa mtazamo huo na masikio yangu yakafunguka. Nikasikia
sauti ikisema name kiingereza.
Maneno yakaniingia na nguvu ziukanijaa tena, ilikuwa ni
sauti ya Anitha ikinisihi jambo, macho yangu yakang’ara na
kung’amua kuwa Yule mlinzi alikuwa amezeeka na hakuwa
na ubavu wa kunizuia kwa lolote lile. Na hapo nikagundua
kwa nini nilikuwa na hofu kubwa mwanzoni.
Kauli ya Anitha ikanisukuma. Nikatoka mbio na kumvamia
Yule mzee, nikamjaza kilo kadhaa za ngumi usoni. Tukio
ambalo hakulitegemea, akapepesuka huku sigara ikimtoka
mdomoni. Akatoa miguno ya maumivu, na hapo nikapata
upenyo.
Kauli ya Anitha ikarudi tena kwa nguvu katika kumbukumbu
zangu. Kauli aliyoniambia kwa lugha ya kiingereza.
“Hilo kufuri ni bovu….”
Nikalivuta likaachia, nikatoka mbio huku bahasha yangu
ikiwa mkononi. Wakati napepea nikaiona gari aina ya
difenda ikitimua vumbi kuja katika nyumba yam zee
Matata.,
Walikuwa wamenikamata hawa wajinga!!
Nilijisemea huku nikijilazimisha kurejea katika hali ya
kawaida.
Nikaingia mitaa miwili ama mitatu na kutokea Sinza
kijiweni. Nikajichanganya na umati wa watu wengi, kwa
tahadhari kubwa kabisa nikachukua tena pikipiki na
kuondoka hadi Mbezi ya Kimara. Huko nikachukua chumba
kama kawaida katika nyumba ambayo ni ngumu kufikika
katika mazingira ya kawaida.
Nilipojifungia ndani nilifikiria jambo moja tu!!
Nilikuwa napambana na nguvu kubwa!! Nilitakiwa kuwa
makini.
Anti Ezekiel!!!!
Jina hilo likanijia kwa kasi katika namna ya kustukiza, kijana
ambaye nilionana naye mara tatu katika maisha yangu huku
ile ya nne ikiwa utata. Utata mtupu!!
Huyu Ezekiel anayesadikika kuwa ni shoga ni nani hasa hadi
asababishe yote haya?
Na nkwanini haya yote yatokee baada ya mimi kufahamiana
naye kwa uchache sana?
Nilijiuliza bila majibu!! Nikabaki kufahamu kuwa jambo
pekee nililokuwa nalifahamu kiuhakika kabisa ni kuwa Yule
bwana aliitwa Ezekiel. Sikujua jina la baba wala mama yake.
Nikaifungua bahasha yangu tena na kuanza kupekua huku
na kule, nilikuwa sijamaliza kupitia zile karatasi ambazo
nilizichukua nyumbani kwa Ezekiel. Nikaamua kuzipitia
zilizokuwa zimesalia.
Nikapekua huku na kule, nikakutana na karatasi moja
ambayo iliandikwa jina tena, si karatasi hii pekee iliyokuwa
imeandikwa jina lakini hili lilikuwa na utofauti katika akili
yangu.
Kindo!!!
Kindo halikuwa jina geni katika akili yangu, ika karatasi ile
chini ya jina iliwekwa tarehe, tarehe ya mbali sana.
Takribani miezi tisa iliyopita.
Cha kushangaza sikutaka lile jina linipite kama mengine
kuna mahali nimewahi kulisikia, ama nimewahi kumuita mtu
jina lile.
Nikaigeuza ile karatasi kwa nyuma na hapo nikakutana na
neno lililonipa uhai wa kuendelea kutafuta jibu la wapi
nimeskia jina lile.
Sinza.
Mwandiko ule mbovu uliandika vile. Hivyo nikawa na kazi ya
kuunganisha mwezi jina na mahaliu.
Kwanini kindo, Sinza na mwezi huo.
Ghafla nikasimama wima na kukibinya kichwa change, kuna
kitu kilijileta katika mstari.
Jina la Kindo nililisikia wakati natafuta pikipiki ya kunibeba
na kunifikisha Mbezi. Nilisikia kama si yeye akijitambulisha
kwa jina basi alikuwa ameitwa na mwenzake.
Mtu sahihi wa kunisaidia katika safari ya kuutatua utata
huo alikuwa ni Kindo!!
Lazima kuna kitu alijua juu ya Ezekiel, huenda ni ndugu ama
jamaa au vyovyote vile lakini lazima tu!!
Lazima angefahamu lolote kuhusiana na Ezekiel.
Nikataka kutoka chumbani muda uleule nikamtafute Kindo
lakini nikahofia kujiingiza matatani mapema sana, Sinza na
Shekilango hayakuwa maeneo yanayoachana kwa mbali
sana.
Shekilango nilikuwa nimezusha balaa tayari nyumbani kwa
Mzee Matata, hapakuwa mahali sahihi hata kidogo
kuonekana hata kwa bahati mbaya.
Muda huo nikataka kujipumzisha lakini nikamkumbuka
Enock. Niliahidi kuzungumza naye kwa njia ya simu siku
iliyopita lakini nikashindwa kutimiza ahadi. Nilifikiria
ugumu ambao atakuwa anapitia katika kichwa chake
kutokana na ukimya wangu na pia akilinganisha na
vuguvugu hizo zilizosambaa mtaani tayari.
Nikautambua umuhimu wa simu, nikakifunga chumba
change, bahasha nikiiweka chini ya godoro na kuondoka
kuingia mitaani, nikapata simu ya bei rahisi, nikanunua na
kadi mpya nikaiwekea pesa. Nikaondoka na kurejea
chumbani.
Nikaiandika namba ya simu vyema kutoka katika
kumbukumbu ya kichwa change na kisha nikapiga.
Simu ilinitia matuamini ilivyoanza kuita na baadaye
kupokelewa.
Alikuwa mke wa Enock. Nilitaka kujitambulisha lakini mara
Enock akawa ameichukua simu.
“Noki eeh!!” nilimwita. Na hapo akaitambua sauti yangu!!
Simu ikakatwa nisijue nini tatizo lakini baada ya dakika
zisizozidi kumi na tano alinipigia.
“Kaka, nini tena hicho umefanya lakini eeh nini kaka, halafu
hata hujaniambia. Mimi na wewe tumeanza kufichana
mambo yetu tangu lini Sam eeh Sam…” alilaumu Enock.
“Sikiliza Enock…hivi umeyaamini hayo uliyoyasikia.”
Nilimuuliza kwa sauti iliyotulia kabisa.
“Sijaamini hata moja Sam lakini kama ulijua una msala kwa
nini usiniambie. Sikia polisi wamekuja kunisumbua hapa
yaani wamepekua kila kona ya nyumba hii kaka. Hivi mbona
hata hukuwahi kuniambia kuwa una bunduki Sam eeh Sam
ilikuwa nia yako kuniingiza matatani ama?” sasa alisikika
kupandwa na hasira.
Nikastaajabu, ina maana hawa watu wameunda uongo kiasi
hicho hadi wamebambika kesi kuwa mimi namiliki bunduki?
Nilikaa kimya Enock akaendelea kulalamika, “Sasa mimi hiyo
kesho naenda kutoa maelezo gani kituoni eeh naenda
kusema nini mimi. Urafiki gani huu sasa?” alizidi kufika
mbali na nikaisikia ile kauli yake ya mwisho iliyokuwa katika
mtindo wa kujutia urafiki wetu.
Yaani Enock niliyempokea Dar es salaam maisha yangu
magumu lakini nikamtunza, nikamtafutia kazi na mwisho
akaweza kujitegemea na kuoa, leo hii anasikitika kuwa
rafiki yangu.
Nilitaka kumweleza mengi kuhusiana na ule mfuko wenye
makaratasi lakini sikuona umuhimu wowote ule kwa sababu
tayari alikuwa mguu ndani mguu nje. Nusu aliniamini na
nusu hakuniamini.
Hakunifaa hata kidogo katika harakati.
Nikakata simu na kuizima kabisa, hasira ilinichemka
kichwani!!!
Nilijua kuwa anaweza kunitumia ujumbe wowote ule na pia
nilijua kuwa namba yangu ile ipo matatani tayari.
Sikuiweka tena katika simu!! Nikatoka nje na kwenda
kununua kadi nyingine. Zote nilikuwa nazisajiri kwa majina
feki.
Ile namba ya awali nikaitupilia mbali kabisa baada ya
kuivunjavunja, sikutaka kumfikiria Enock tena, nikazitazama
nguo zilizokuwa katika mwili wangu, zilikuwa mali yake.
Nikachukia kujitazama.
Nikatamani kununua nguo nyingine lakini nikatambua kuwa
katika kipindi hicho nilikuwa naihitaji pesa kuliko wakati
mwingine.
Nikarejea chumbani!!
Nikajitupa kitandani usingizi nao ukasusa kunipitia,
nikagalagala huku na kule pasi na mafanikio!! Saa kumi na
moja ikanikuta nikiwa bado sijaupata usingizi. Nikaishika
simu yangu yenye kadi mpya nisijue ni kitu gani inanisaidia.
Nikabofya namba nyingine nilizozikariri huenda nitapata
msaada wa kimawazo. Sikujua kama nitabonyeza namba zile
kwa usahihi, lakini nilifanikiwa kubofya.
Simu ikaita kwa muda mchache sana na kisha ikapokelewa.
Alikuwa yeye!!! Sauti yake haikuwahi kupotea masikioni
mwangu kamwe!!
“Nani mwenzangu mbona huongei?” alikaripia
nilivyoendelea kuwa kimya.
“Anitha…..Sam hapa….upo mahali sahihi tuzungumze
kidogo.” Nilinong’ona. Kimya kikatanda, na mara Anitha
akazungumza name, alikuwa amejifungia chumbani mwake.
Sikutaka kujua nini kilitokea baada ya mimi kufanikiwa
kutoroka lakini nilitaka msaada wake kimawazo kama bado
angekuwa radhi kunisaidia. Anitha aliniambia kauli moja
nzito ambayo ilinifanya niamini kuwa sasa nimepata wa
kunishika mkono.
“Sam, kwa lolote lile nipo na wewe, najua wewe si muuaji,
najua kuna kitu nyuma ya pazia japo sijakijua kitu hicho,
nipo tayari kushirikiana na wewe ilimradi tu mimi na wewe
tukivumbue kitu hicho.” Kisha akashusha pumzi na
kunisikiliza.
“Anitha wewe ni msichana wa kipekee, nisizungumze sana
lakini naomba nikuamini wewe. ….aaahm ni lini unaweza
kutoka nyumbani.’
“Siku yoyote ile, si unajua nipo chuo siku hizi.”
“Ok kesho naomba ufanye jambo moja la msingi na
litakalotuwezesha kujua wapi tunaanzia, hapo Sinza Kijiweni
ama Sinza popote pale kuna mtu anaitwa Kindo, simjui kwa
sura wala sauti lakini ni huyu anajua kuhusu Ezekiel..”
“Ezekiel ni nani?” alinikatisha. Nikalazimika kumsimulia
upesi kwa ufupi sana juu ya hadithi ya shoga niliyemuona
Ubungo akanipa funguo na kisha nikaikuta maiti yake ikioza
kitandani Yombo Temeke.
Maelezo yangu yakamuacha Anitha katika kigugumizi lakini
akaahidi kushughulikia jambo hilo.
“Kwani huwezi kuja chuoni kesho.”
“Hapana sitakiwi kuonekana kwenye hadhara kubwa namna
hiyo ni hatari.”
“ila kweli, sawa Sam nitakupigia kwa lolote.”
“Hautanipigia wewe nitakupigia mimi Anitha. Simu
haitakuwa ikipatikana mara kwa mara.” Nilimaliza
mazungumzo na kisha kukata simu.
Hapo sasa niliweza kulala na amani kidogo moyo wangu
nikiuegemeza kwa Anitha ambaye niliamini anaweza
kunisaidia kwa lolote lile, lakini sikujitoa moja kwa moja
kwake. Nilikuwa nusu namuamini na nusu nikiishi kwa
tahadhari.
Baada ya kula chakula cha usiku majira ya saa tatu usiku
niliiwasha tena simu yangu na kisha nikambipu Anitha.
Upesi akanipigia.
Hakunipa nafasi ya kuzungumza na badala yake akachukua
usukani kusimulia.
ANITHA
SAM najua upo matatani sana, nisingeweza kungoja hata
kidogo hiyo kesho ifike ili nianze kumtafuta huyo mtu wa
kuitwa Kindo.
Sinza ni kubwa lakini kama una nia ya dhati ni mtaa mdogo
sana kuumaliza,. Niliondoka nyumbani nikimuaga baba
kuwa naenda chuoni, lakini sikuwa na safari hiyo, safari
yangu ikaishia mitaani. Halikuwa jambo jepesi kumpata mtu
usiyejua hata kazi yake, lakini nilifanya kwa ajili yako Sam.
Nilifanya nikijua kuwa wewe upo upande wa haki, na hakika
upo katika haki.
Mungu hamtupi mwenye nia na anayemtegemea, nilipopiga
hatua yangu na kuanza rasmi kumtafuta Kindo
nilimtanguliza Mungu, niliulizia kila kona na kila ofisi lakini
sikumpata Kindo. Wengine walidai kumfahamu lakini
hawakuonyesha ushirikiano kabisa, hadi ilipotimu saa kumi
na mbili jioni maeneo ya Sinza kijiweni nikiwa najiandaa
kupanda gari nirejee nyumbani pasipo na mafanikio
nikasikia jina kama hilo likiitwa. Nilikuwa nimebanwa hasa
lakini nguvu za kusukuma abiria wengine zilipatikana
nikafanikiwa kupenya na kushuka chini, nikamuuliza
mwanafunzi mmoja akaninyooshea kwa kidole huyo mtu wa
kuitwa Kindo.
Ni teja…teja aliyekubuhu, madawa ya kulevya yameweka
makazi katika mwili wake, sikuweza hata kusema naye
maana alikuwa akitiririkwa na udenda na alikuwa
ameuchapa usingizi. Nikapata kigugumizi kuamini kama
kweli huyu ndiye Kindo uliyeniagiza kumtafuta ama kuna
Kindo mwingine.
Swali hili nilitamani nije kukuuliza lakini ukadai kuwa
hujawahi kumwona Kindo na hata hujui sura yake ilivyo.
Kama ungekuwa unamfahamu walau ningekwambia haya
Sam. Kuwa kindo ni mweupe wa zamani lakini sasa
hajulikani rangi yake, ni mrefu wa wastani na kichwani hana
nywele.
Kwa sababu nisingeweza kusema na mtu asiyesema kwa
tahadhari kubwa nilijipiga picha nikiwa usawa wake na
katika hiyo picha ameonekana, kama unayo barua pepe
nitakutumia uweze kumwona teja huyu wa kuitwa Kindo.
Na hapo tutajua kama ndiye ama siye!!
Kesho nitaenda tena kumwona kama akiwa anaongea
nitamuuliza juu ya Ezekiel. Tumwombe Mungu atoe jibu
zuri, maa sura yake licha ya kumwagika kwa madawa
inatangaza chuki kali. Sijui anachukia nini Mungu wangu!!!
ANITHA akamaliza!!!
Nilibaki nimekaa hivyohivyo kitako katika kitanda cha futi
nne kwa sita, maelezo ya Anitha yalizidi kuzua utata. Japo
mwanga ulionekana lakini mwanga huu ulikuwa hafifu sana
walau kunipa uwezo wa kupiga hatua moja mbele.
Ni kweli nilikumbuka kuwa nilisikia jina kindo palepale
Sinza kijiweni, lakini katika ile karatasi paliandikwa kuwa ni
miezi tisa iliyopita.
Sasa kilitokea nini miezi tisa iliyopita. Je ni kweli huyu
Kindo anayetakiwa ama? Ama Anitha naye anataka
kunichezea kamchezo!!!
No no no!! nililipinga wazo la kumfikiria Anitha vibaya, ni
asubugi tu alitoka kuniokoa sasa iweje jioni anikane???
Hapana ilikuwa mapema sana kumwazia vibaya!!!
Nikarejesha mawazo yangu kwa Kindo!!
Kindo teja, kindo mwenye kipara Kindo asiyejitambua, kindo
wa miezi tisa iliyopita.
Kindo ambaye Anti Ezekieli alikuwa amemworodhesha
katika karatasi zile.
Hakuna picha wala neno la ziada!!!
Utata!!!!
 
SEHEMU YA SABA
Ni kweli nilikumbuka kuwa nilisikia jina kindo palepale
Sinza kijiweni, lakini katika ile karatasi paliandikwa kuwa ni
miezi tisa iliyopita.
Sasa kilitokea nini miezi tisa iliyopita. Je ni kweli huyu
Kindo anayetakiwa ama? Ama Anitha naye anataka
kunichezea kamchezo!!!
No no no!! nililipinga wazo la kumfikiria Anitha vibaya, ni
asubugi tu alitoka kuniokoa sasa iweje jioni anikane???
Hapana ilikuwa mapema sana kumwazia vibaya!!!
Nikarejesha mawazo yangu kwa Kindo!!
Kindo teja, kindo mwenye kipara Kindo asiyejitambua, kindo
wa miezi tisa iliyopita.
Kindo ambaye Anti Ezekieli alikuwa amemworodhesha
katika karatasi zile.
Hakuna picha wala neno la ziada!!!
Utata!!!!
**JIFUNZE: Katika maisha usipende kumfahamu mtu kwa
kuhadithiwa na fulani, ili umfahamu mtu vyema na tabia
zake basi akili yako ikupe majibu yenyewe kutokana na
vitendo vya huyo mtu. Usimuulize jirani yako ama usitumie
tetesi kumfahamu mtu. Je? Utajuaje kama hao
wanaokwambia wana chuki naye? Utajuaje kama ni marafiki
zake na sasa wanamsifia kwa lolote!!!
Epuka!! Na hii itakusaidia kujua kuishi na mwanadamu!!
ENDELEA!!!
ASUBUHI sana nilidamka, kitu cha kwanza nikapanga
mipango ya kuhamia nyumba nyingine ya kulala wageni.
Nilijiwekea tahadhari kabla ya hatari, ingewezekana kabisa
namba yangu ya simu kutumika katika kunisaka na hii
ingekuwa hatari sana kwangu. Isitoshe Anitha hakuwa
akijua lolote juu ya Ezekiel, hakumjua hata sura. Hivyo kama
ningekubali kukamatwa hata kama kweli alikuwa na nia ya
kunisaidia ndo basi tena mwisho wa jeuri yake.
Na nilivyoijua sheria ya Tanzania mwenye haki hana haki
tena akiwa nyuma ya vyuma vya mahabusu ama gereza.
Nani angenielewa na kunisikiliza nimweleze juu ya hadithi
za bunuasi kuhusu Ezekiel wa Ubungo na yule maiti wa
Temeke.
Hakuna sheria ambayo ingenilinda hata kidogo!! Huenda
hata Anitha naye angebadili misimamo yake juu ya jambo
hilo!!
Nilitambua kuwa sijaswaki baada ya kuzungumza kwa sauti
bila kujua na hapo nikatambua kuwa kinywa hakikuwa
katika usafi. Lakini nani angejali hali ile!!
Hakuna hata mmoja!! Nikaendelea kutembea nikiangalia
chini, mara mbele na wakati mwingine kushoto na kulia.
Sikuwa na amani!!!
Nikakatisha mitaa zaidi na zaidi na jua lilianza kuchomoza
nisijue wapi naelekea.
Umati wa watu ukanivuta katika eneo la wazi, nikajisogeza
kwa tahadhari nisijue ni nini nafuata huko.
Magazeti!!! Kundi lile lilikuwa likipepesa macho katika
vichwa vya magazeti.
Na mimi nikajiunga huku nikiwa makini kabisa nisiweze
kumtazama yeyote machoni, kofia yangu ya pama nayo
ilinifunika vyema.
“ALVIN ALILAWITIWA KABLA HAJAUWAWA!!” kichwa cha
habari katika gazeti mojawapo kilisomeka hivyo, pembeni
yake ilipambwa picha yangu ikisheheni maneno machache
“ANATAFUTWA”
Nikajikaza na kuendelea kutazama habari nyingine.
“MUUAJI ANASAKWA AUWAWE” pembeni yake kulikuwa na
picha ya kitanzi.
“MIAKA THELATHINI JELA INAMNGOJA SAMSON” kichwa
kingine cha habari.
“ALVIN AFA NA SIRI NZITO!!” hili lilikuwa gazeti la udaku
nikasonya.
“MANENO YA MWISHO YA ALVIN KABLA HAJAUWAWA.
ALIMUACHIA SAMSON UJUMBE MZITO.” Kichwa hiki cha
habari kikanivuta zaidi. Na hapo nikapata jibu langu huku
utatat ukizidi.
Kumbe aliyekufa anaitwa Alvin, sasa hili jina la Ezekiel
limetoka wapi? Nikajipekua na kutoa pesa kiasi na
kumpatia muuza magazeti, kisha nikaondoka nikiwa
nimeinama chini vilevile.
Mawazo lukuki yakinikabili, nilitarajia nitakuta habari juu ya
kuonekana kwangu maeneo ya Shekilango labda hata nguo
nilizokuwa nimevaa zingeweza kuandikwa pale. Ajabu
hakuna kitu kama hicho kilichoandikwa!!
Nikajikongoja hadi katika mgahawa mmoja, nikapata chain a
chapati mbili.
Baada ya hapo nikahama tena, safari hii nikajichimbia
maeneo ya Kimara Suka. Mbezi nikatoweka bila taarifa.
Majira ya saa sita nikaiwasha simu yangu!!! Ukaingia
ujumbe kutoka kwa Anitha, alikuwa anahitaji kuzungumza
name.
Nikambipu palepale!!
Baada ya dakika tano simu ikaingia!! Anitha alizungumza
kwa sauti yenye tumaini kiasi fulani.
Nikamwachia ukumbi Anitha akiwa msimuliaji name
msikilizaji.
ANITHA
KUTOKA saa kumi na moja alfajiri katika nyumba ya mzee
Matata si jambo jepesi hata kidogo, lakini yawezekana
ikiwa tu ukiwa jasiri. Nami niliuvaa ujasiri nikatoweka
nikidanganya kuwa kuna jambo la msingi la kufanya chuoni
asubuhi hiyo. Mzee wangu na shule nadhani unafahamu,
hakunioinga hata kidogo. Lakini hasira zake tangu usiku
uliopita zilikuwa bado zimemtawala, nadhani hakulala hata
kidogo maana tangu akaripie sebuleni usiku ule nilimkuta
hapo hapo. Baba ametamka kuwa anakuchukia sana huenda
kupita wanadamu wote duniani, eti kisa tu wewe ni mlawiti.
Dhambi kubwa kupita zote, analalamika kuwa umemnlawiti
kijana wa kuitwa jina la Alvin na ukaona hiyo haitoshi
ukamuua ili asikufichulie siri, aliyazungumza haya akiwa na
bastola yake ile ya tangu miaka ile. Akakulaani huku
akimlaumu mama kwa kushindwa kukufyatua ulipojileta
wewe mwenyewe nyumbani. Akatukanya sana nkuwa kwa
lolote lile tukiwasiliana nawe tumpe taarifa, hakika
amechukia mzee yule. Kila mmoja alimuunga mkono, dada
Jenipher akamtukana mama aliyekuzaa na mjomba Yakobo
naye akakilaani kizazi chako, mama akatoa ushauri kuwa
wakuendee kwa mganga ili wakufanye kichaa milele. Baba
akasema akikuona atakuua kwanza nd’o mengine yafuate.
Sasa nikajiuliza kuwa kishakuua ni kipi kinafuata zaidi yaw
ewe kuzikwa!!!
Niliumia moyoni lakini maneno yao hayakunifanya niwe
upande wao, nakufahamu zaidi ya wao wanavyokufahamu.
Kama ulikuwa mkweli kwangu ni vipi ufanye yote haya
nyuma yangu???
Nikaamua kuutafuta ukweli kama kweli upo…nikatoweka
alfajiri.
Sinza Kijiweni ilikuwa kimya!! Kama pangekuwa kijijini basi
lazima kuku wangekuwa wanawika lakini huku palikuwa
kimya, ni magari kadhaa tu yaliyokuwa yakipita na kupiga
kelele.
Nilinyata hadi nikalifikia eneo ambalo nilimkuta Kindo usiku
ule uliopita, nikaangaza huku na kule nikajikuta katika
ugumu. Huu nd’o ubaya wa jiji la Dar es salaam, watu wengi
hawana makazi ya kudumu, vijana wanasota na jua mchana
na bado usiku wanalala nje.
Nikashindwa kuelewa yupi ni Kindo na yupi si Kindo. Hofu
ya kubakwa ikaniandana iwapo vijana wale wataamka
pamoja na kutambua kuwa nilikuwa sina uelekeo maalum.
Nilijikabidhi kwa Mungu asubuhi ile kama nifanyavyo siku
zote hivyo ni yeye tu alikuwa tegemezi langu!!
Moshi mweupe hewani ukanivuta kutazama unatoka wapi,
nikasogea huku nikiwa tayari kwa hatari yoyote iwapo
itatokea nitimue mbio!!
Si unanijua tena mimi kwa riadha!!
Sura ya Kindo ilikuwa imara sasa. Haikuwa imemwagika
hovyo kama usiku ule, nikamsogelea huku nikihofia lolote
ambalo lingeweza kutokea. Sura yake ya kigaidi ilinitisha.
“Kaka…..” nilimwita mara moja na yeye akageuka.
Nikamsabahi kwa heshima zote naye akanijibu kwa upole.
Sikutegemea kabisa!! Nikakosa pa kuanzia akanikaribisha
katika gogo la mti nikaketi!!
“Naitwa Sarah” nilimlaghai jina ili kwa lolote lile la mbele
ushahidi usiwepo. Akatikisa kichwa akingoja nimuulize
zaidi, nikamuuliza iwapo yeye ndiye kindo akanijibu8 kwa
kirefu kuwa jina loake sahihi zaidi ni Kindole Emmanuel.
Mwenyeji wa Iringa!!
Nikastaajabu, hakufanania hata kidogo na maneno yake
ukifananisha na ugumu wa sura yake.
Nikamuuliza kuwa kama miezi tisa iliyopita aliwahi kumjua
Ezekiel, alijaribu kuvuta miezi nyuma lakini kabla ya kujibu
akaniuliza mimi ni nani. Nikakosa cha kujibu nikadanganya
kuwa ni rafiki yake Ezekiel na nimepotezana naye siku
nyingi lakini katika kumbumbukumbu zangu aliwahi
kuniambia ana ndugu ama jamaa aitwaye Kindo na ni
mwenyeji wa Sinza. Nikaendelkea kulaghai kuwa nina siku
chache sana jijini Dar es salaam na nimekuwa nikipatafuta
Sinza na nikimtafuta yeye.
Baada ya kunisikiliza kwa makini alionekana kustaajabu
mno, lakini alikana kabisa kumjua Ezekiel. Hakika uso wake
ulimaanisha alichokuwa anakisema.
Baadaye akanieleza kuwa miezi tisa iliyopita wala hakuwa
jinni Dar es salaam alikuwa zake huko Iringa. Akaniamini na
kunieleza kuwa hata yeye si mwenyeji sana jijini Dar es
salaam na maisha magumu nd’o yanamfanya alivyo!!
Nikamuuliza huko Iringa akumbuke kwa makini, akakataa
katakata kumjua Ezekiel.
Nilijaribu kukupigia simu labda walau uelezee muonekano
wa Ezekiel huenda anaweza kukumbuka lakini kama
ulivyopanga kutoniamini ulikuwa hupatikani hewani!!
Na asubuhi ikatukuta tukiwa katika mgahawa, Kindo si
katili kama nilivyodhani, Kindo si mkorofi hata kidogo!! Na
Kindo ni kama alikuwa anafahamika maana watu walitutania
sana walipotuona na yeye aliishia kucheka tu na wakati
mwingine wakirushiana matusi ya nguoni ambayo
hayakumwathiri Kindo.
“Wapiga debe wenzangu hao wakorofi sana…” aliniambia
Kindo na hapo nikaijua kazi inayomuweka mjini, nisiite kazi
bali kibarua kisichokuwa rasmi.
Kindo alinishukuru kwa ukarimu wangu!! Na baadaye
nikamuachia namba za simu iwapo atakumbuka lolote juu
ya Ezekiel. Nikampatia na kiasi cha pesa.
Nikaondoka na kwenda kituoni!!!
Hata kabla sijapanda gari nikasikia kilio kikuu kutoka
upande niliomuacha Kindo. Nikachungulia na kugundua
kuwa anayelia ni Kindo!!
Nikarejea upande ule kutazama kulikoni, alikuwa analia
akisema wamemuua kaka yangu, wamemuua kaka yangu!!
Sikuelewa ana maana gani bado. Hakutaka kuguswa na mtu
hata mimi hakutaka kunisikia.
Watu walibaki kuduwaa wasijue analia nini. Akakimbia na
kuvamia meza ya magazeti, akajipekua na kutoa pesa
niliyompa akanunua gazeti. Watu wakabaki kuduwaa
hakuomba chenji yake, sasa akawa amelikumbatia gazeti.
Na hata alipoliachia alikuwa akiililia picha ya mtu aitwaye
Alvin, ambaye amekufa ama ameuliwa na muuaji
unasadikika kuwa wewe Sam. Kindo analia akisema ni kaka
yake, kwa maana hiyo yawezekana Alvin ndo Ezekiel!!!
Nikaishiwa nguvu nikakaa chini. Na hilo nd’o jibu!!!
Kindo akiwa katika kuruka ruka huku na kule mara
wakatokea watu wawili waliojazia miili yao wakamchukua
na kuondoka kwenda naye wanapojua wenyewe!!!
Hakuna aliyejali, Kindo hakuwa na ndugu!! Nami nikaogopa
kujipeleka kimbelembele kwa sababu tayari alikuwa
amenikataa na mimi baada ya kuona habari ile katika
gazeti!!!
Majira ya saa tano asubuhi!! Nikapanda gari Sam na muda
huu naongea na wewe nipo chuoni mpendwa wangu!!
Sijui hata ni kipi kinafuata, labda nitaenda kuonana na Kindo
tena akishapoa nimweleze kuwa Alvin nd’o Ezekiel nimsikie
ataniambia nini japo ameonekana kuumia sana.
ANITHA AKAMALIZA………
UPANDE WANGU
Kijasho chembamaba kilikuwa kinanitoka, habari ile
ilinisisimua sana, ni kama mwanafunzi anayekaribia kulipata
jibu lakini mwisho analisahau tena, nd’o kilichotokea Kindo
alikuwa mtu sahihi wa kuweza kutupa mwanga juu ya Alvin
ama Ezekiel kama nilivyomtambua lakini mkanganyiko wa
majina ulituzuzua na sasa yule mtu sahihi akashindwa
kutueleza juu ya jambo tunalohitaji.
Nilijilaumu kwa kutokuwa hewani, labda kweli Anitha
alikuwa sawa kuweka hisia za mimi kutomwamini.
Nilifadhaika lakini ni kweli sikuwa nimejitoa kwa asilimia
mia kwake, na nisingeweza kufanyanhivyo kwa sababu.
Aumwae na nyoka akiguswa na ujani hushtuka!!!
Kama baba yake ananichukia vipi kuhusu yeye!!! Na
wahenga walisema damu ni nzito kuliko maji???
Majira ya saa kumi jioni nilikuwa katika pikipiki, sasa
nilijipanga kwa ajili ya kuonana na Kindo mimi mwenyewe,
maelekezo ya Anitha jinsia alivyokutana na kijana huyu
yalinisaidia na hatimaye nikajikuta eneo lile. Nikajiweka
kijiwe cha kahawa nikaanza kunywa kikombe kimoja baada
ya kingine. Wazee walikichangamsha kijiwe kwa hadithi zao
za uongo na kweli huku mimi nikiwa msikilizaji.
Laiti kama ningekuwa huru kama zamani basi kijiwe
kingepata wateja wengi sana siku hiyo kwani zile zilikuwa
hadithi nilizozipenda, hadithi za uongo na kweli kutoka kwa
wazee.
Nilichangia mada mara moja moja sana huku saa zote
nikijifanya kukolewa na utamu wa kashata!!
“Samahani mzee hivi bwana Kindo leo wapi?” nilimuuliza
mzee mmoja aliyevalia kibalaghashia. Aliangaza huku na
kule kisha akanieleza kuwa labda ameenda kwa daktari,
nikamchimba zaidi akanieleza kuwa daktari ni yule
anayewadunga madawa ya kulevya!!
Nikakubaliana naye!!!
Majira ya saa moja usiku kijiwe cha hadithi za sungura na
paka kikageuka kuwa cha hadithi ya kutatanisha.
Bwana mmoja akaketi na kunyamazisha wote kisha
akaelezea kuwa Kindo amekutwa ufukweni mwa bahari
akiwa amekufa!!!
Labda mimi ndiye nilishtuka zaidi, jina Kindo lilikuwa jina
nililofuata pale. Lakini kabla sijaiona hata sura yake
naambiwa kuwa amekutwa amekufa!!
Nikatahamaki!!
Lakini kabla sijakaa sawa mara nikashtushwa na kauli
iliyotolewa na mzee mwenye kibalaghashia ambaye awali
nilimuuliza juu ya Kindo.
“Huyu kijana ni mgeni hapa na amekuwa akimuulizia kindo
katika namna ya kipekee, kwanza usiku huu na amefunika
kichwa chake, macho pia yana mawani namna gani yakhee!!
Kwani huyo Kindo ulimtakia nini weye!!” aliwaka kwa sauti
ya juu, umati ukjnigeukia, wote wakawa kimya wakisubiri
niseme neno.
Sikutarajia shambulio hilo, nikabaki kutetemeka. Hali yangu
ya hofu ikawafanya wateja wa kahawa wavutike zaidi kujua
ni kwa nini nilimtaka Kindo!!
Wakaanza kunizongazonga, wengine walikuwa mateja na
wengine makondakta na wapiga debe, muuza kahawa
akaanza kukusanya vilivyo vyake. Hali ilikuwa tata!!
Mara mmoja akanikwapua kofia kichwani na mwingine
akanitoa mawani nyeusi usoni!!
Hawakuwa na utani wale watu!!
“Mlete kwnye mwanga huku…mlete huyoo, hawa ndo
tunawatafuta hawa hata Rama walimuua hivihivi….”
Alikoroma kijana mmoja. Wenzake wakatii wakaanza
kunighasi huku na kule!! Wakinivuta kuelekea kwenye
mwanga, yule mzee mwenye kibandiko alikuwa jirani na
mimi akinitukana sana huku akisisitiza kuwa najua
kinachoendelea.
Nilijaribu kujitetea kuwa hata sura ya Kindo siifahamu
lakini hakuna aliyeisikia sauti yangu!!!
Sam mimi nilikuwa nimepatikana!! Tukazidi kuuelekea
mwanga, na lazima ntungeufikia tu!!! Sura yangu ilikuwa
katika magazeti ya siku hiyo!!
Lazima watakuwa waliiona!! Isitoshe sakata alilonisimulia
Anitha la Sam kulilia picha katika gazeti. Basi wengi
watakuwa waliliangalia gazeti lile!
Gazeti lenye sura yangu!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom