Riwaya: Ant Ezekiel

Riwaya: Ant Ezekiel

SEHEMU YA NANE
“Mlete kwnye mwanga huku…mlete huyoo, hawa ndo
tunawatafuta hawa hata Rama walimuua hivihivi….”
Alikoroma kijana mmoja. Wenzake wakatii wakaanza
kunighasi huku na kule!! Wakinivuta kuelekea kwenye
mwanga, yule mzee mwenye kibandiko alikuwa jirani na
mimi akinitukana sana huku akisisitiza kuwa najua
kinachoendelea.
Nilijaribu kujitetea kuwa hata sura ya Kindo siifahamu
lakini hakuna aliyeisikia sauti yangu!!!
Sam mimi nilikuwa nimepatikana!! Tukazidi kuuelekea
mwanga, na lazima ntungeufikia tu!!! Sura yangu ilikuwa
katika magazeti ya siku hiyo!!
Lazima watakuwa waliiona!! Isitoshe sakata alilonisimulia
Anitha la Sam kulilia picha katika gazeti. Basi wengi
watakuwa waliliangalia gazeti lile!
Gazeti lenye sura yangu!!
**JIFUNZE: KATIKA maisha vikwazo ni sehemu ya mapito!!
Hakuna mapito nyoofu mpaka mwisho, jiandae kukabiliana
na makwazo maana hayo tuliumbiwa sisi wanadamu ili
kupimwa imani yetu!!!
ENDELEA
Lile kundi lilizidi kunighasi bila kunipa nafasi ya kunisikiliza.
Mwanzoni walisema wanaufuata mwanga ili wanitambue
vizuri lakini sasa waliupita ule mwanga na kukifuata
kichochoro walichokijua wao. Kuna lugha zao waliambiana
na sikuweza kuzikumbuka wala kuambulia chochote!!
Baada ya kukifikia kichochoro kile mara ghafla mimi na yule
mzee mwenye kibalaghashia tukajikuta tumewekwa
katikati. Harufu kali ya moshi wa bangi ilitawala eneo lile
na palikuwa kimya.
“Toa kila kitu ulichonacho bazazi wewe!!!” aliamrisha bwana
mmoja, nikashuhudia kisu kikubwa mkononi mwake!! Mzee
mwenye kibalaghashia akatumbua macho, hakutarajia kama
tukio linaweza kubadilika namna ile!! Yeye alitarajia labda
nikishatambuliwa basi atapongezwa lakini mambo
yaliharibika wale waliotuzunguka neno kifo cha Kindo
lilikuwa la kawaida sana kwao.
Wote tukajikuta tunatetemeka, lakini kwangu ilikuwa nafuu
zaidi kutekwa na wale watu ambao niliamini kuwa ni vibaka
tu wa kawaida kuliko kuingia katika mikono ya wale watu
wabaya ama serikali ambayo ilikuwa imehadaika na sasa
ikinisaka kama muuaji na mbakaji!!
Niliangusha simu yangu wakaikwapua!! Nikajipekua na
kutoka na kiasi cha pesa na hiki pia wakachukua. Wakatoa
vitisho kadha wa kadha
Yule mzee alikuwa na kanzu tu hakuwa na kitu cha ziada,
wakamweka kando!!
Si kwamba walimwachia la!!
Nilishangaa ghafla alikuwa hewani na mara akatua chini,
alikuwa amepigwa ngwala ya ghafla, yule mpigaji
akajikausha kana kwamba si yeye aliyetoka kufanya tukio
lile lililoipasua kanzu ya yule mzee na kukirusha
kibalaghashia chake kando!! Hawakumwambia lolote.
Wakanirudia mimi tena, hawakuwa na utani hata kidogo na
nyuso zao zilijawa chuki tupu!!
Kujifanya wananizongazonga waweze kunitambua mimi ni
nani hiyo ilikuwa hila tu hakuna lolote walilotaka zaidi ya
kuniibia \, na hilo walikuwa wamefanikiwa!!
Ajabu ni kwamba kuna watu walilishuhudia tukio hili lakini
hata kujihusisha kutusaidia hawakujisumbua, na ilikuwa heri
hawakujihusisha nasi maana wangeweza kutokea ambao
aidha wangeweza kunitambua ama wangeyafanya mambo
kuwa magumu zaidi!!
Hakika jiji la Dar es salaam lilikuwa limeoza na maovu kama
haya yalikuwa kama kitu cha kawaida mbele ya macho ya
watu!!
“Kindo umemfahamia wapi we -----?” mara aliniuliza yule
bwana aliyezungumza kama kiongozi na wenzake
kumsikiliza.
“Ni jamaa yangu tu….mimi ni mtu wa Iringa nd’o nilikuwa
namuulizia jamani” nilijitetea. Mara bwana mmoja akadakia
hoja.
“Na wewe ndo wahanga wa ridandansi ya Michigani ama?”
aliniuliza, akili ikafyatuka hilo neno Michigani halikuwa geni
hata kidogo masikioni mwangu.
“Hapana, ni ndugu tu jamani!!” niliendelea kujitetea.
Ile kusema neno Michigani basi kila mmoja akacheka kati ya
wale vibaka. Bila shaka halikuwa neno geni kwao. Ajabu ni
kwamba neno lile hata kwangu pia halikuwa geni kuna
mahali niliwahi kuliona kisha nikalipuuzia na sasa nalisikia
tena.
“Yaani kila mtu wa Iringa huwa anadanganya kuwa alikuwa
Michigani amefukuzwa kazi aisee sijui huko Michigani nd’o
kampuni pekee kubwa??….haya dakika moja potea hapa
urudi Michigani kwenu huko!!! Moja mbili…..” aliamuru na
hakuwa na utani, kabla hajafika tatu nikatimua mbio kali
huku nyuma nikimsikia yule mzee mwenye kibalaghashia
akilalamika kwa maumivu, bila shaka alikuwa akipokea
kipigo kingine kwa kutembea bila pesa.
Sikusimama maana nilikuwa nimeponea katika tundu la
sindano, nilikimbia bila kukoma hadi maeneo ya Tandale,
nikachepuka na kona kadhaa kabla sijairuhusu akili yangu
kufanya kazi tena.
Uzuri ni kwamba nilikuwa nimechukua tahadhari mapema
sana, pesa zangu niliziweka katika mafungu mbalimbali
kwenye nguo nilizokuwa nimevaa. Hivyo hata nilipowapa
wale wakora zile pesa na simu bado nilibakiwa na fedha
nyingine ambazo zilinitosha kufanya safari ya kurejea kule
nilipofikia kwa kutumia usafiri wa pikipiki tena!!!
Badala ya kusikitikia suala la kukaribia kukamatwa
nilitamani tufike upesi Kimara niweze kuwa huru na kisha
kujipanga tena upya kujitafutia haki yangu bila uhai wa
Kindo!!
Maeneo ya Tandale sokoni, kabla sijachukua pikipiki, kwa
tahadhari kubwa nilifanikiwa kununua kofia nyingine, na pia
nikavutika kununua fulana kubwa na suruali nyingine.
Ile kofia nikaivaa muda uleule na kisha kutoweka, nikiwa
kama mzuka aliyefufuka kutoka katika wafu nisiamini kama
na hatua ile nimepona pia.
Majira ya saa mbili nilikuwa chumbani!! Upesi nikachukua
bahasha yangu ambayo nilikuwa nimeificha chini ya godoro,
nikamwaga makaratasi yote chini na hapo nikaiona ile picha
ambayo jengo lake dogo limeandikwa Michigan. Ni hapa
nilipokuwa nikisumbua akili yangu kupatambua!!
Niliitazama kwa makini sana, na hapo nikaanza kuunganisha
matukio, nikayakumbuka mazungumzo baina yangu na
Anitha aliponambia kuwa Kindo ambaye anasadikika kuwa
marehemu tayari alikuwa mwenyeji wa Iringa, kama hii
haitoshi wale vibaka waliposikia kuwa mimi ni jamaa yake
Kindo mara moja wakadakia kuwa na mimi ni wa Michigan!!
Huko Michigan ni wapi?
Na je panahusika nini ni mauaji ya Ezekiel ambaye kwa jina
halisi ama vyovyote vile ni Alvin.
Kwa maana hiyo Kindo aliwahi kuwaambia vibaka hao kuwa
yeye alikuwa muajiriwa huko Michigan? Baadaye akapewa
ridandansi!!!
Hapa kuna tatizo lazima!! Kindo amekufa na siri kubwa
sana!!
Nikatamani sana kuzungumza na Anitha usiku huo lakini
tatizo sikuwa na simu tena wale mabazazi huenda
walishaiuza kwa bei ya kutupa tayari!!
Nikatoka nje na kumkabili muhudumu aliyekuwa mapokezi,
nilimkuta akiwa ametingwa katika kusikiliza muziki na
ilinilazimu kumuita mara tatu hata akanisikia, nikamsihi
aniazime simu yake kuna simu ya muhimu sana nahitaji
kupiga!!!
Akalalamika kuwa simu yake huwa haibadilishwi kadi,
nikamweleza kuwa sitabadili. Bado akalalamika mengi na
klusema simu yake haina muda wa maongezi, nikatoa
shilingi elfu tano mfukoni. Uzuri huduma ya vocha ilikuwa
pale, hapo akakosa ujanja na kufikia hatua ya kuniazima!!
Nikatoweka na ile simu na kuelekea chumbani kwangu!!
Nikajisifu kwa uwezo wangu mkubwa wa kukariri.
Nikaziandika namba za Anitha katika simu ile na kungojea
simu ile iiite.
Ikaanza kuita na baada ya dakika kadhaa ikapokelewa!!
Kama mimi nilivyotegea upande wa pili uanze kuzungumza
na upande wa pili nao ukangoja mimi nianze kuzungumza!!
Mtego!! Nikajiwazia huku nikiendelea kukaa kimya!!
“Halo!” hatimaye sauti kutoka upande wa pili ilinong’ona.
Alikuwa Anitha!!
Hapo nikapata ujasiri wa kujitambulisha upesiupesi!!
Anitha akasikika akikurupuka kwa fujo kutoka alipokuwa na
nikasikia vishindo na baada ya hapo aliniuliza kama
nilikuwa salama!! Nikajibu kuwa nipo salama kabisa,
akaniuliza tena na tena kama nina uhakika na usalama
wangu nami nikasisitiza kuwa hakuna baya lolote upande
wangu!!
“Kindo amekufa….” Aliniambia binti huyu kitu ambacho
nilikuwa nakitambua tayari.
“Nini kivipi?” nilimuuliza kana kwamba hakuna nijualo!!
Alinielezea kuwa na yeye hajui lolote lakini katika mapito
yake pale kuhakikisha kuwa anazungumza tena na Kindo
alipewa taarifa hiyo.
“Mbona unaulizia mara mbilimbili juu ya usalama wangu
lakini!!” nilimuuliza kutaka kujua.
ANITHA akachukua nafasi kusimulia!!
SAM naomba nikiri kuwa naipongeza nafsi yangu kwa
kuendelea kukuamini kila kukicha. Sikuwahi kukatishwa
tamaa na habari za kwenye magazeti. Kashfa na tuhuma
zote ulizozushiwa hazikuwahi kuniteteresha kamwe! Baada
ya kifo cha Kindo, nimeamini kuwa kuna watu wabaya wengi
wamelizunguka tukio hili na hakika u katika wakati mgumu
sana.
Sam najua hujipiganii peke yako na labda unaona haya
kunieleza kuwa unao uchungu sana kuwa hujui mkeo alipo
na usalama wa mtoto wako. Ni kweli ninao wivu kwa
sababu nakupenda lakini amini haya ninayokuambia. Sam
naumia sana ten asana, juu ya mama Eva na Eva
mwenyewe. Mama Eva ni mwanamke mwenzangu, hana
kosa alilowahi kunitendea zaidi tu ya kujikuta katika penzi
lako.
Eva ni mtoto mdogo hajui lolote kuhusu hisia zangu kwako!!
Hastahili kuchukiwa!! Na sijawahi kumchukia unalitambua
hilo.
Sam kwa hali ya amani ilivyo juu yako, kwa jinsi watu
wabaya wanavyoisaka roho yako. Nipo radhi niambie
unahitaji kitu gani kingine naweza kufanya kwa ajili yako
wewe, Eva na mama Eva. Niambie chochote hata kama ni
kigumu nami nitakujibu kuwa naweza ama kipo nje ya
uwezp wangu!!!” alinieleza kwa hisia kali huku akizungumza
kwa sauti ya chini, kila neno likawa na maana kwangu nami
nikajibu.
“Anitha, kama nilivyosema awali kuwa hata nikikushukuru
namna gani bado sitafikia kiwango unachostahili.
Anitha naomba niwe muwazi kuwa hakika baada ya usaliti
alioufanya mzee Matata ambaye ni baba yako imani yangu
kwa wanadamu imekuwa hafifu sana. Yaani namuogopa kila
mtu!!
Laiti kama ningekuwa sina familia nisingeogopa lolote lakini
Eva ndo ananiumiza zaidi huku mama yake akinipagawisha
kabisa, sijui alipo huenda hata wamemuua naye tutasikia
kama hivyo kwa Kindo!! Anitha nimeamua kitu kimoja,
nimeamua kujikabidhi kwako Anitha. Kujikabidhi kwa
asilimia zote mia moja.
Kama sitakuwa sahihi basi chozi la Eva na damu ya mama
Eva iwe juu yangu kwa upumbavu wangu!! Kilio cha Eva na
kinisulubu iwapo sitakuwa sahihi kukuamini wewe kama
mtu wa mwisho pekee ninayeamini upo upande wangu!!
Sina lolote la kufanya ikiwa sura yangu haitakikani mtaani
na sasa Tanzania nzima wanaijua sura na jina langu popote
pale nitakamatwa tu! Anitha narudia tena na samahani
kama nitakuwa nakukera, tambua kuwa mimi Sam sijaua
mtu wala kulawiti!! Iwapo baba yako ama familia kwa
ujumla zimekumezesha sumu na kuamua kunikamata mimi
sasa nipo radhi, lakini nikiwekewa kitanzi shingoni, neno
nitakalosema juu yako ni kwamba lawama za Eva na mama
yake ziwe juu yangu lakini damu yangu na uhai
nitakaoupoteza kwa hila na hujuma ya hali ya juu, vyote
vitakuwa juu yako Anitha. Namkabidhi Mungu uaminifu huu
wa mwisho mkubwa ninaoamua kuuleta kwako. Yeye pekee
ndiye ajuaye ni kiasi gani nipo upande wa haki na sijui lolote
kuhusu kuua. Na ni yeye huyuhuyu aliyeniambia kuwa kesho
nikutane na wewe ana kwa ana!!” nilimaliza huku
nikishindwa kuyazuia machozi yangu nilipomkumbuka mke
wangu asiyejulikana mahali alipo na Eva anayesadikika
kutunzwa na jeshi la polisi Tanzania.
Upande wa pili nilimsikia Anitha naye akililia kilio cha
kwikwi, na hata alipozungumza alitoa kauli fupi tu.
“Na kilaaniwe kizazi changu chote milele na milele iwapo
siku moja nitasimama na kutetea maovu…Sam tukutane
kesho saa tatu usiku. Utaniambia muda huo nije wapi??”
kisha akakata simu!!
Sikutaka kumpigia simu kwa sababu nilijua hataweza
kuzungumza tena, maneno yangu huenda yamemuumiza
moyoni ama yamemtia aibu kwa mpango aliokuwanao na
sasa anajutia kwa machozi!!
Nikamtumia ujumbe mfupi. Nikamuelezea wapi nitakuwepo,
sitakuwa na simu lakini nitafika kwa wakati!! Pia
nikamsisitiza asitumie namba ile tena!!
Nikamaliza nikaifuta namba yake katika simu ile na
kumrejeshea muhudumu, salio lililobaki mle lilimfanya
atokwe na tabasamu, meno yake ya njano yakaonekana.
Sikurudi kulala, nikaondoka na kujipatia mkate na soda
dukani, nikarejea chumbani kwangu kupooza njaa huku
nikitafakari Michigani ni kitu gani na kwanini Kindo ahusike
nayo na kisha Alvin.
Michigan Michigan!!!
Nililala nikiwaza hayo!!
SIKU iliyofuata kama ilivyoutaratibu wangu nilihama
nyumba ile na kuhamia kwingine kabisa maeneo ya Ubungo.
Baada ya kuwa nimepata supu ya maana nilijifungia ndani
mara nilale mara niamke huku nikitafakari mambo mengi
yasiyokuwa na ufumbuzi, kisha nikamtafakari Anitha na
uamuzi wangu wa kukutana naye!!
Roho ilinidunda sana na kujiona kuwa najikabidhi kwa
muuaji kirahisi, lakini ni kipi ningefanya iwapo hakuna
anayeniamini na ushahidi wangu wenyewe ulikuwa utata
mkubwa kuliko utata uliokuwepo. Picha na maandishi
yaliyoandikwa na msichana ama mvulana asiyejua kuandika
vizuri yangeisaidia nini mahakama zaidi ya kubambikiwa
kesi nyingine ya kudanganya mahakama.
Eva na mama yake hawa ndio waliniumiza zaidi!!
Hawakuwa na kosa na huenda wangekuwa wameaminishwa
kuwa mimi ni mtu mbaya, mwanangu Eva anaambiwa baba
yako ni gaidi,.
Nikazichanga karata na kisha nikaitupa kete moja tu kubwa
nay a mwisho kwa Anitha!! Kama ana mnapenzi ya kweli
ama anatumiwa!!
Nikasinzia tena!!
Majira ya saa mbili nilitoka nyumbani na kwenda eneo la
miadi ambalo nilimtumia Anitha katika ujumbe mfupi wa
maneno.
Niliwahi maksudi ili niweze kusoma mchezo kama
utakuwepo japo hiyo ilikuwa mbinu hafifu tu ya kujihami,
kama wamejipanga tayari nisingeweza kuchomoka tena!!
Saa mbili na nusu kwa mujibu wa saa iliyokuwa katika
mnara nilimuona Anitha akitembea kwa madaha kuelekea
katika eneo nililomwelekeza.
Baada ya kutingwa na mawazo siku kadhaa sasa
nilikumbuka kuwa kumbe Anitha ni msichana mrembo kiasi
kile. Nalivalia vazi refu jeusi lililozichora nyonga zake
vyema, vazi lile halikuishia kiunoni bali lilipanda hadi usawa
wa kifua chake na kuzistiri embe sindano ndogo
zilizong’ang’ania kukomalia pale kifuani na si mahali
pengine, mgongo ulikuwa wazi lakini si wazi kiasi cha
kuitwa uchi la! Ulifunikwa na nywele ndefu ambazo
alijitambia kila leo!!
Macho yake yalizibwa na miwani yenye mahadhi ya
kuvaliwa usiku, mkononi alibeba kipochi kilichofanana na
miwani.
Hakika aliwaka!!!
Niliwahi kuwa naye katika mahusiano lakini sasa alipendeza
zaidi!! Alichukua nafasi na kuagiza maji ya matunda!!
Akiwa anakunywa kinywaji kile hakuonyesha hofu yoyote
machoni mwake.
Nikatazama juu mbinguni na kusema na Mungu!!
“Wajua kuwa sikuua, wajua kuwa mimi ni mja wako!!
Nitazame baba huku ninapoelekea, kama ni sahihi nyanyua
mguu wangu sasa lakini kama si sahihi baba nitegue
nisiweze kuifikia meza ile” nilimaliza ile dua na kisha hatua
moja hadi nyingine hadi nikaifikia ile meza.
Nilikuwa nimevaa zile nguo nilizonunua Tandale usiku
uliopita!!
Anitha aligeuka na kunbitambua akasimama na
kunikumbatia.
Marashi yake yakamfanya azidi kuwa mrembo, joto lake
tulivu likanikumbusha mengi yaliyopita!!
Nikavuta kiti na kuketi mkabala naye sasa tukawa
tunatazamana. Alipotoa miwani uso wake ulikuwa
umechafuliwa na michirizi ya machozi.
Anitha alikuwa analia, na hapa akanyanyua mdomo na
kuniambia jambo ambalo sikuwahi kuliwaza.
“Sam umekonda hivi jamanii!!”
Nikashangaa!! Akasema tena, “Yaani umepauka kabisa si
wewe Sam. Pole sana.” Alinibembeleza, nikajisikia vibaya
badala ya kupata ahueni!!
Robo saa baadaye tukiwa tumeagiza vyakula, nilikuwa
nikimuelezea juu ya Michigan na utata niliokutana nao
nikiwa namtafuta Kindo.
“Kwa hiyo hukuniamini hata kidogo Sam ukaamua kwenda
mwenyewe!! Ni lini utaamini kuwa Anitha yu upande wako.”
Alilalamika, nikajifanya sikumsikia nikaendelea kumweleza
mambo kadha wa kadha!! Yote haya nilimsimulia nikiwa
sijaifungua bahasha mkononi mwangu!!
Ukafika wakati wa kuifungua bahasha, hapa akalazimika
kuja kuketi katika ubavu wangu ili nimwelekeze kitu kimoja
baada ya kingine ili atambue ni kitu gani namaanisha.
Picha moja baada ya nyingine, andishi moja baada ya
nyingine…
MARA tukakatishwa na sauti ya mwanamke, “Heloow!!”
tukadhani ni muhudumu wa ile sehemu tukapuuzia na
kuendelea na mambo yetu!!
Niliponyanyua macho kwa mbali niliona kitu kama ninacho
kifananisha na mzimu usiotakikana machoni kwangu!!
Lakini wakati naendelea kuduwaa mara mbele yetu akaketi
mwanamama akiwa anatabasamu. Tabasamu la kinafiki.
Nikamtambua upesi yeye na kisha nikapata jibu la yule
niliyemfananisha alikuwa ni nani!!
Mbele yangu alikuwa ni mama yake Anitha na yule mzee
aliyekuwa anakaribia kufika pale alikuwa ni mzee
MATATA…..baba yake mzazi Anitha…….
Bahasha yangu mezani, najilazimisha kufumbua macho
lakini hayafumbuki zaidi ili iwe ndoto!!
Nilikuwa maeneo ya Saveyi karibu na chuo kikuu cha Ardhi
na mbele yangu alikuwapo mama Anitha na huyu
anayemalizia hatua afike nilipokaa alikuwa ni mzee Matata.
Mapigo ya moyo badala ya kwenda kasi yakaanza kushuka
kwa fujo!!
Jasho halikutoka lakini mwili ukawa wa baridi sana. Ganzi
ikanishika.
NAKUFA!!!! Nikajiwazia…………..
 
SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA
Niliponyanyua macho kwa mbali niliona kitu kama ninacho
kifananisha na mzimu usiotakikana machoni kwangu!!
Lakini wakati naendelea kuduwaa mara mbele yetu akaketi
mwanamama akiwa anatabasamu. Tabasamu la kinafiki.
Nikamtambua upesi yeye na kisha nikapata jibu la yule
niliyemfananisha alikuwa ni nani!!
Mbele yangu alikuwa ni mama yake Anitha na yule mzee
aliyekuwa anakaribia kufika pale alikuwa ni mzee
MATATA…..baba yake mzazi Anitha…….
Bahasha yangu mezani, najilazimisha kufumbua macho
lakini hayafumbuki zaidi ili iwe ndoto!!
Nilikuwa maeneo ya Saveyi karibu na chuo kikuu cha Ardhi
na mbele yangu alikuwapo mama Anitha na huyu
anayemalizia hatua afike nilipokaa alikuwa ni mzee Matata.
Mapigo ya moyo badala ya kwenda kasi yakaanza kushuka
kwa fujo!!
Jasho halikutoka lakini mwili ukawa wa baridi sana. Ganzi
ikanishika.
NAKUFA!!!! Nikajiwazia…………..
***JIFUNZE!!! DUNIA inapokugeuka mwamini Mungu pekee,
yeye hadanganyi, yeye si mnafiki wala si msaliti!!
Ukimwambia baba tenda miujiza anasikia palepale!! Sema
naye kwa imani naye atatenda!!!
ENDELEA!!!
Mzee Matata hakuwa akikosea uelekeo alimaanisha kufika
katika meza ambayo nilikuwa nimeketi na Anitha. Usoni
alionyesha tabasamu lililojawa karaha tele, na alitembea
kama asiyetaka kufika upesi eneo lile lakini alikuwa makini.
Nikajikuta nipo nje ya ujasiri na suruali yangu ikajikuta
ikijitahidi kuumeza mkojo uliokuwa ukinitoka bila kuzuiliwa,
kwa sekunde kadhaa nikafanikiwa kuuona uso wa Anitha….
Ajabu!! Alikuwa anayo hofu kubwa kuliko mimi, jsho lilikuwa
likimtiririka na midomo ikimchezacheza.
Anaigiza!! Niliwaza huku nikiwa sijajua kipi cha kufanya,
nisingeweza kukurupuka na kukimbia bila kutambua iwapo
mzee Matata anayo silaha yoyote kwa wakati ule, maana
bunduki yake ndogo alikuwa akiimiliki kihalali na angeweza
kuitumia kunishambulia. Hata akiniua ataishia kupewa
pongezi kwa kumuua muuaji na mbakaji, asingelaumiwa na
mtu yeyote.
Nilibaki katika hali ileiloe ya kuinama nisijue wala kuamini
iwapo, Anitha amenisaliti ama naota!! Kama kweli alikuwa
amenisaliti nikajikuta lawama zangu nikizigeuzia kwa
Mungu!! Mbona nilimsihi sana kabla sijajikabidhi kwa binti
yule!!
“Si nilikwambia…..haya hii nd’o diskasheni…ooh Anitha
hawezi kulaghai hawezi sijui nini haya hapa ndo mpo katika
kudiskasi?” mama Anitha alihoji swali ambalo liliniduwaza.
Mwanga mwekundu wa taa haukunizuia mimi kuwatambua
wazazi hawa lakini ajabu wao waliuliza kitu kingine kama
vile hawanitambui!!!
Mzee Matata alishusha pumzi za nguvu sana, sikuwa
nimemtazama machoni bado moja kwa moja, niliendelea
kuinama huku kofia yangu ikinifunika.
“Mama!! Hivi mnataka kunichunga hadi lini?” alijibu Anitha
kisharishari!!
Nikazidi kupagawa.
Ina maana wote wawili wananiigizia Mungu wangu weee!!
“Johnson!! Johnson, nisamehe bure kwakweli halikuwa
dhumuni langu, naomba uniachie nafasi nizungumze nao
hawa ni wazazi wangu!! Samahani tena Johnson!!”
alinisisitiza Anitha, nikapagawa, inamaana yale mavazi
yangu niliyonunua Tandale na hilo kofia vimenibadilisha
kiasi kile?? Ilistaajabisha sana.
Sasa naitwa Johnson!! Nikashindwa kuelewa kama
nisimame ama nisisimame, Anitha akaugundua udhaifu ule
akanikanyaga mguu upesiupesi, bado sikuelewa nifanye
nini. Akaniinamia na kuninong’oneza.
“Baba haoni usiku ana ‘night blindness’ hajui lolote na
mama bado anajiuliza. Ondoka upesi ondoka tutawasiliana.”
Kwa kauli hiyo sasa nikatambua nini kinaendelea.
Nikasimama na kuondoka nikiwa na uoga mkubwa na
kichwa nikiwa nimekiinamisha. Bahasha yangu mkononi!!
Mapigo ya moyo yakiwa katika hali ya kufifia na miguu
ikitetemeka kwa fujo.
Anitha!!! Anitha steringi!! Ndo kitu nilichobahatika
kukitamka kwa midomo yangu baada ya kujikuta nipo peke
yangu mahali bahasha yangu mkononi na hakuna wa
kunighasi.
Suruali ilikuwa imelowana bado, sikuamini hata kidogo
kama tulikaa meza moja na mzee Matata na mkewe na sasa
nilikuwa nimeondoka tena.
Nikaikumbuka kauli ya mzee Matata tangu akiwa bosi
wangu aliponieleza kuwa Anitha ndo binti yake kipenzi,
hana la kusema juu yake na hataki baya lolote limtokee.
Naam!! Mtoto wa baba alikuwa ametumia nafasi kuniokoa!!
Nikazitazama mbingu na kumwomba msamaha Anitha kwa
lolote lile baya nililowahi kumuwazia!!
Anitha alikuwa upande wangu kwa asilimia mia!!
Sikupotezaq muda zaidi nikatokomea!! Si kuelekea katika
nyumba ya wageni niliyofikia bali kwingine kabisa ambapo
nilifahamu mimi na akili yangu!! Zile nguo nilizopewa na
Enock yule rafiki msaliti nikaamua kuachana nazo. Cha
muhimu kilikuwa mimi na bahasha yangu!!
*****
Majira ya saa nne usiku nilikuwa nikiusaka usingizi kwa
juhudi zote, suruali yangu nilikuwa nimeifua na kuinika chini
ya feni ili kufikia asubuhi iwe imekauka.
Niliwaza mengi na kisha kukumbuka kuwa pesa ilikuwa
inayoyoma hatimaye. Hili likanitia wasiwasi maana pasi na
pesa bila shaka njaa ingeniumbua na kujikuta naomba
msaada, msaada kutoka kwa mtu yeyote yule pasi na kujua
kama ni mtu hatari ama salama!!
Asubuhi kama nilivyopanga wakati usingizi unabisha hodi
nikamkumba muhudumu wa nyumba ile ya kulala, huyu
hakuniletea ugumu katika kuniazima simu yake.
Nilimwambia kuwa kuna mtu nataka kumbipu!!
Nilipopigiwa simu nikakimbilia chumbani kwangu na kisha
kwa tahadhari kubwa nikaipokea simu!!
“Nilijua tu ni wewe na hakika nilisubiri sana kuzungumza
nawe!!” Anitha kutoka upande wa pili alizungumza. Sauti
yake ilikuwa inaunguruma kiasi na nhakika hakuwa sawa na
siku nyingine. Kabla sijamuuliza lolote akaendelea.
ANITHA.
HUWA ni jambo gumu sana kuupina ama kuubatilisha usemi
wa damu nzito kuliko maji!! Lakini hubidi kuwa hivyo pale
upendo unapochukua nafasi!!
Tukio la jana ni kama ndoto na hata muda huu naamini ni
ndoto labda ni wewe wa kuibatilisha ndoto hii, ndoto ya
mwanamke kujikuta katika maamuzi ya kuachana na usemi
wa damu nzito na hatimaye kuubadili kuwa penzi zito
kuliko damu!!
Sijui nilitoa wapi ujasiri ule wa kujitetea mbele ya baba na
mama yangu!! Na wala sikutarajia ujio wao usiku ule tena
wakinifumania mimi na wewe. Ambaye wanakuita mtu
hatari.
Sam, nafsi yangu ilijawa na baridi, lile barafu la ubaridi
likazidi kuvimbiana na nikajihisi kukosa amani kwa zana
kuwa waweza kuniita msaliti!!! Naam!! Ni mwanadamu gani
awezaye kuamini eti mama alishika simu yangu nikiwa
nimeenda kuoga akausoma ujumbe uliokuwa umenitumia
kunielekeza mahali tulipotakiwa kukutana. Yule mama
akawa mjuaji zaidi akaangalia huduma za kipesa katika
namba hiyo na kugundua kuwa ulikuwa ukijiita Gabriel
Madaraka. Kwa hili naomba nikupongeze sana Sam, yaani
laiti kama ungekuwa umetumia namba ambayo umeisajili
kwa jina lako basi nadhani ule ujio wa wazazi wangu
usingekuwa wa kupooza namna ile.
Mama akamshirikisha baba yangu juu ya mimi kutaka
kukutana na mwanaume majira ya saa tatu usiku maeneo
yale tuliyokutana. Nadhani wajua ni jinsi gani baba yangu
ananipenda kwa dhati, hili kwako si jipya hata kidogo kuwa
hataki baya lolote linitokee, akasikia natarajia kukutana na
mwanaume ilhali nimewalaghai nyumbani kuwa naenda
katika majadiliano ya kimasomo na rafiki zangu. Wazazi
wakaitegea mida na hatimaye wakatufuma katika hali ile.
Najua kuwa usingepatikana muda wa mimi kusimulia haya
na unielewe iwapo wazazi wangu wangekugundua na
kukukamata, na jambo hili lingenifanya niwe adui yako
namba moja maisha yako yote!! Sikuwa tayari nikaamua
nkuwakosea heshima, nikakutetea na hatimaye ukaondoka.
Sam!! Nilibebwa mzega mzega nikaingizwa katika gari na
kuendeshwa moja kwa moja hadi nyumbani!!
Hakuna jambo baya kama kupingwa na wazazi wote wawili
katika jambo unalojaribu kulifanya, katika utetezi hakuwepo
aliyesimama upande wangu!! Nilipigwa sana na utu uzima
wangu huu, baba alinipiga kwa kutumia mkanda huku mama
akinipiga vibao na makofi!! Hasira za baba zilikuwa juu
zaidi, baada ya kunipiga sana hakutaka kulala nyumbani.
Akatoweka na mama naye akaondoka kwenda kumtafuta.
Nadhani waisikia sauti yangu ilivyo mbaya, hii ni kwa
sababu nina vidonda mdomoni, walinipiga sana Sam. Lakini
niliamua kubeba maumivu haya kwa ajili yako!! Nikateseka
lakini uwe na imani kuwa sijawahi kukukana hata siku moja!!
Kosa walilofanya wazazi wangu ni kujiridhisha kuwa Anitha
mimi sijakomaa kiakili, wakadhani siyajui mapenzi na sina
uamuzi wangu wangu wa mimi kama mimi!!!
Nilitarajia utanipigia simu Sam usiku ule niweze
kukushirikisha katika jambo nilililokuwa nimefikiria lakini
sikupokea simu yako na nililazimika kuchukua maamuzi ili
tu haki ipatikane, Sam mimi nasome sheria na haki za
binadamu. Lazima kuna kitu katika mlolongo huu, nami
nataka nitambue kuna nini hapa katikati, hii ni nchi yetu
Sam na sis indo vijana kama kuna uvundo wowote
unaendelea na vijana tunafumbia macho, amini umri na
elimu zetu hazitusaidii kitu chochote na ni watumwa wa
elimu ya mkoloni huku tukiwa vibaraka wa ukoloni
mamboleo. Maumivu hayakunizuia kukivamia chumba cha
wazazi wangu ambacho haikuwa mara ya kwanza kuingia.
Ile imani ya baba yangu kwangu na kuonyesha mapenzi
waziwazi sasa ulikuwa wakati muafaka wa kuitumia.
Nikafungua sanduku ambalo nilizijua namba zake za siri,
naam!! Nilichokitarajia nikakikuta!!
Unadhani ni kitu gani ki9nachokwamisha mkakati huu zaidi
ya pesa!! Unadhani kwa nini Eva na mama yake wapo
mahali usipopajua zaidi ya pesa? Sam Pesa haina mdomo
lakini ikipaza sauti basi itasikika dunia nzima na wanyonge
watatetemeka!!
Pesa inaficha maovu na pesa hii inatibua haya maovu!!
Pesa nyingi inaweza kuficha maovu milele lakini akili nyingi
na pesa kidogo hutibua mipango hii!! Sijielewi mimi lakini
natambua kuwa Sam wewe unao uwezo mkubwa sana wa
kufikiri, naam!! Kwa pesa hizi kidogo nilizochota naamini
harakati za kuirejesha amani, kutibua fumbo hili gumu na
kumrudisha mama Eva na Eva katika himaya yako basi zote
zitawezekana!!
Michigani, Kindo, Ezekiel, Alvin vyote hivi vitajulikana!!
Sam! Baada ya kuiba pesa hizo kutoka kwa wazazi
wasiofungamana nami!! Nilitoweka mlinzi akiwa amelala!!
Sasa nane usiku, kila kiungo kikiwa kinauma kutokana na
kipigo, macho yakikosa nuru kutokana na uchovu, bado
niliweza kuzurula mitaani.
Nakukumbusha kuwa Mungu ni muweza wa yote haogopi
usiku wala mchana maana vyote alivibuni yeye!!
Mungu alinisimamia na hadi muda huu unanipigia simu nipo
Royal Hotel Temeke chumba namba 18, Anitha huru katika
fikra na maamuzi huru!!! Simu yangu iliingoja simu yako tu
ili niweze kuizima na rasmi nakutambulishia namba yangu
mpya isiyojulikana na yeyote zaidi yako ni 07...675493.
nimeamua kuungana na wewe Sam, kama ni batili wazo hili
na niadhibiwe nikiwa hai. Na kama nikifa kabla ya kupewa
adhabu basi nifanyiwe alichofanyiwa yule dada katika
simulizi uliyoiandika na ikavuta maelfu ya watu..”NIKIFA
MAITI YANGU IPEWE ADHABU!!”
ANITHA AKAMALIZA!!!!
UPANDE WANGU
Nilibaki kuduwaa nisiamini nilichokisikia, sauti kakamavu
japo inayokoroma kutoka kwa Anitha ilibeba ujumbe mzito
sana. Harakati nilizokuwa nasisitiza kila siku katika makala
zangu, ule uzalendo uliopotea kwa vijana wengi na hali ya
kuthubutu sasa niliionja tena kwa Anitha. Na kubwa zaidi
yale mapenzi wanayodai kuwa yamelogwa na kuwa ya
kudanganyana sasa niliyashuhudia katika upande wa
mapenzi ya kweli.
Anitha alikuwa mwanaharakati!! Nilizungumza naye kwa
kina akanielekeza juu ya hiyo hoteli ilipo.
Sikupoteza muda nikaivaa ile nguo yangu ambayo siku
iliyopita ililowana mikojo ya kiutu uzima. Moja kwa moja
nikaenda Temeke kukutana na anitha.
Wakati huu sikumtilia mashaka tena!!
Nilifika hadi chumbani baada ya kuruhusiwa kuingia. Anitha
hakuwa akidanganya jambo lolote lile, uso wake mweupe
ulikuwa mwekundu, midomo ilivimba sana na yale macho
yaliyowahangaisha wanaume wengi sasa hayakuwa na
mvuto wowote. Alijaribu kutabasamu lakini akaishia njiani
ni kama alipatwa na maumivu kinywani. Nikajisikia huruma
nikamkaribia, nilimpooza kwa maneno ya hapa na pale na
kisha nikakiri mbele yake kuwa yeye alikuwa ‘steringi wa
kike’ katika filamu asiyehofia chochote.
“Anitha sasa vipi kuhusu shule….” Nilimuuliza, badala ya
kujibu akalazimisha tena tabasamu.
“Sam!! Tunasoma ili kupambanua mambo katika jamii
inayotuzunguka, na si kupata shahada ya makaratasi huku
tukishindwa kutatua matatizo katika jamii yetu. Huku
nilipoamua kuingia ni shule kubwa zaidi ya hiyo ya
makaratasi bila uwezo wa kuchanganua na kupambanua
mambo!!!
Unamfahamu Nelson Mandela?? Alifungwa akiwa na miaka
mingapi? Alifungwa gerezani miaka mingapi?? Je alipotoka
alitumia makaratasi ya shuleni kulipigania taifa lake
alilolipenda?? La!! Ile shule ya kunyanyaswa ilikuwa kubwa
kabisa katika maisha yake!! Ama labda nikuulize ni
wanafunzi wangapi wanaopata daraja la kwanza vyuoni na
nchi haiwatambui kwa lolote lile zaidi ya sifa wapatayo siku
ya matokeo?? Lakini ni nani awezaye kumsahau yule
mwanafunzi kijana kabisa kutoka chuo cha Havard Marekani
aliyebuni mtandao wa kijamii wenye nguvu kupita yote
duniani?? Nani wa kumsahau Mark Zuckerberg na facebook
yake.? Unadhani Mark alitumia makaratasi yake ya kufaulu!!
Tuutumie muda uliopo vyema ili tusijutie wakati ujao!!”
alijibu kwa kujiamini Anitha hadio akanishangaza, nikaamini
kwa kile alichokisema kuwa elimu ya darasani bila uwezo
wa kutatua tatizo ni buree!!
Tulizungumza mengi!! Majira ya saa kumi na mbili jioni
tukawa na maamuzi, nikaondoka na kwenda kukata tiketi
kwa ajiri ya safari ya kwenda Iringa. Kwa lengo moja tu
kuitambua Michigani ambayo hadi wakati huo hatukujua
kama ni hoteli, casino ama mgahawa!! Lakini tulitaka kuijua
Michigan.
Tuliamua iwe siku inayofuata ili kuokoa maisha ya Eva na
mama yake ambao lazima sumu za kwenye magazeti kuwa
mimi kibaka tena muuaji na mlawiti zilikuwa zimeathiri akili
yao kupindukia!!
Nilifanikiwa kupata tiketi mbili za kukaa katika siti moja.
Nikiwa nimeandika majina ya bandia!!
Tulilala kimya kila mmoja na tafakari yake, nilikuwa na
amani kuwa nipo na mtu sahihi kabisa katika harakati hizi
za kunirejeshea amani iliyotoweka na pia kunirejeshea
familia yangu!!!
Alfajiri tulikuwa tayari kwa safari ile, safari matata kabisa
kila mmoja akiwa mgeni katika mkoa wa Iringa!
Safari ya kwenda kutafuta kitu tusichokijua, lakini kitu
tulichoamini kuwa kitatuletea majibu ya maswali yetu
ambayo yalikuwa gizani nasi tukiwa gizani huku
tukilazimika kuyajibu ili utokee mwanga!!!
Badala ya kupata siti mbili zilizoungana kwa ajili yetu
tulijikuta tukiwekwa katika siti ya watu watatu!!
Hatukulalamika kwa sababu tulikuwa na shida ya kusafiri!!
Pembeni yetu alikuwepo msichana machachali ambaye
alizoeana na kila abiria kana kwamba ni ndugu yake!! Na
sisi tuliokuwanaye siti moja alitulazimisha hadi tukamzoea,
hadi kufikia Mikumi Morogoro ni kama alikuwa ndugu yetu
wa karibu!!
Hapo nikatumia nafasi ya mazoea hayo nikauliza swali.
“Hivi Michigani huwa ni Iringa ama Mbeya maana niliisikia
nikiwa Dar es salaam enzi hizo.” Swali lile lilimfanya acheke
na kisha kwa kutuonyesha ukomavu wake alitoa majibu
yake!!
“Yaani Michigani zimebakia picha tu, aisee paliteketea
moto mbona!! Miezi tisa iliyopita mbona ilikuwa
mshikemshike, sema uzuri hakuna mtu aliyekufa!! Kwa hiyo
Michigani imebakia stori tu hakuna kitu kama hicho kule
kama hukubahatika kupaona basi tena watafute akina sisi
malijendari wa miji tukuonyeshe picha!!” alijibu kwa kirefu
kisha akatoa cheko refu!!
Anitha akanibinya kuniondoa katika mshangao ule!! Lakini
na yeye alikuwa ameduwaa!!
Michigani iliteketea miezi tisa iliyopita, katika karatasi
lililoandikwa jina la kindo limendikwa miezi tisa iliyopita.
Kuna picha ya mahali panaitwa Michigani!!!
Mkasa ukaingia ugumu mwingine!!
Tunatafuta mahali ambapo pamebakia historia!!!!
Nikalegea kwa uchovu na kukata tamaa!!
 
Stori nzuri sana... naisubir kwa hamu.... unaileta mda gani tena Mzaramo?
 
SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA
Niliponyanyua macho kwa mbali niliona kitu kama ninacho
kifananisha na mzimu usiotakikana machoni kwangu!!
Lakini wakati naendelea kuduwaa mara mbele yetu akaketi
mwanamama akiwa anatabasamu. Tabasamu la kinafiki.
Nikamtambua upesi yeye na kisha nikapata jibu la yule
niliyemfananisha alikuwa ni nani!!
Mbele yangu alikuwa ni mama yake Anitha na yule mzee
aliyekuwa anakaribia kufika pale alikuwa ni mzee
MATATA…..baba yake mzazi Anitha…….
Bahasha yangu mezani, najilazimisha kufumbua macho
lakini hayafumbuki zaidi ili iwe ndoto!!
Nilikuwa maeneo ya Saveyi karibu na chuo kikuu cha Ardhi
na mbele yangu alikuwapo mama Anitha na huyu
anayemalizia hatua afike nilipokaa alikuwa ni mzee Matata.
Mapigo ya moyo badala ya kwenda kasi yakaanza kushuka
kwa fujo!!
Jasho halikutoka lakini mwili ukawa wa baridi sana. Ganzi
ikanishika.
NAKUFA!!!! Nikajiwazia…………..
***JIFUNZE!!! DUNIA inapokugeuka mwamini Mungu pekee,
yeye hadanganyi, yeye si mnafiki wala si msaliti!!
Ukimwambia baba tenda miujiza anasikia palepale!! Sema
naye kwa imani naye atatenda!!!
ENDELEA!!!
Mzee Matata hakuwa akikosea uelekeo alimaanisha kufika
katika meza ambayo nilikuwa nimeketi na Anitha. Usoni
alionyesha tabasamu lililojawa karaha tele, na alitembea
kama asiyetaka kufika upesi eneo lile lakini alikuwa makini.
Nikajikuta nipo nje ya ujasiri na suruali yangu ikajikuta
ikijitahidi kuumeza mkojo uliokuwa ukinitoka bila kuzuiliwa,
kwa sekunde kadhaa nikafanikiwa kuuona uso wa Anitha….
Ajabu!! Alikuwa anayo hofu kubwa kuliko mimi, jsho lilikuwa
likimtiririka na midomo ikimchezacheza.
Anaigiza!! Niliwaza huku nikiwa sijajua kipi cha kufanya,
nisingeweza kukurupuka na kukimbia bila kutambua iwapo
mzee Matata anayo silaha yoyote kwa wakati ule, maana
bunduki yake ndogo alikuwa akiimiliki kihalali na angeweza
kuitumia kunishambulia. Hata akiniua ataishia kupewa
pongezi kwa kumuua muuaji na mbakaji, asingelaumiwa na
mtu yeyote.
Nilibaki katika hali ileiloe ya kuinama nisijue wala kuamini
iwapo, Anitha amenisaliti ama naota!! Kama kweli alikuwa
amenisaliti nikajikuta lawama zangu nikizigeuzia kwa
Mungu!! Mbona nilimsihi sana kabla sijajikabidhi kwa binti
yule!!
“Si nilikwambia…..haya hii nd’o diskasheni…ooh Anitha
hawezi kulaghai hawezi sijui nini haya hapa ndo mpo katika
kudiskasi?” mama Anitha alihoji swali ambalo liliniduwaza.
Mwanga mwekundu wa taa haukunizuia mimi kuwatambua
wazazi hawa lakini ajabu wao waliuliza kitu kingine kama
vile hawanitambui!!!
Mzee Matata alishusha pumzi za nguvu sana, sikuwa
nimemtazama machoni bado moja kwa moja, niliendelea
kuinama huku kofia yangu ikinifunika.
“Mama!! Hivi mnataka kunichunga hadi lini?” alijibu Anitha
kisharishari!!
Nikazidi kupagawa.
Ina maana wote wawili wananiigizia Mungu wangu weee!!
“Johnson!! Johnson, nisamehe bure kwakweli halikuwa
dhumuni langu, naomba uniachie nafasi nizungumze nao
hawa ni wazazi wangu!! Samahani tena Johnson!!”
alinisisitiza Anitha, nikapagawa, inamaana yale mavazi
yangu niliyonunua Tandale na hilo kofia vimenibadilisha
kiasi kile?? Ilistaajabisha sana.
Sasa naitwa Johnson!! Nikashindwa kuelewa kama
nisimame ama nisisimame, Anitha akaugundua udhaifu ule
akanikanyaga mguu upesiupesi, bado sikuelewa nifanye
nini. Akaniinamia na kuninong’oneza.
“Baba haoni usiku ana ‘night blindness’ hajui lolote na
mama bado anajiuliza. Ondoka upesi ondoka tutawasiliana.”
Kwa kauli hiyo sasa nikatambua nini kinaendelea.
Nikasimama na kuondoka nikiwa na uoga mkubwa na
kichwa nikiwa nimekiinamisha. Bahasha yangu mkononi!!
Mapigo ya moyo yakiwa katika hali ya kufifia na miguu
ikitetemeka kwa fujo.
Anitha!!! Anitha steringi!! Ndo kitu nilichobahatika
kukitamka kwa midomo yangu baada ya kujikuta nipo peke
yangu mahali bahasha yangu mkononi na hakuna wa
kunighasi.
Suruali ilikuwa imelowana bado, sikuamini hata kidogo
kama tulikaa meza moja na mzee Matata na mkewe na sasa
nilikuwa nimeondoka tena.
Nikaikumbuka kauli ya mzee Matata tangu akiwa bosi
wangu aliponieleza kuwa Anitha ndo binti yake kipenzi,
hana la kusema juu yake na hataki baya lolote limtokee.
Naam!! Mtoto wa baba alikuwa ametumia nafasi kuniokoa!!
Nikazitazama mbingu na kumwomba msamaha Anitha kwa
lolote lile baya nililowahi kumuwazia!!
Anitha alikuwa upande wangu kwa asilimia mia!!
Sikupotezaq muda zaidi nikatokomea!! Si kuelekea katika
nyumba ya wageni niliyofikia bali kwingine kabisa ambapo
nilifahamu mimi na akili yangu!! Zile nguo nilizopewa na
Enock yule rafiki msaliti nikaamua kuachana nazo. Cha
muhimu kilikuwa mimi na bahasha yangu!!
*****
Majira ya saa nne usiku nilikuwa nikiusaka usingizi kwa
juhudi zote, suruali yangu nilikuwa nimeifua na kuinika chini
ya feni ili kufikia asubuhi iwe imekauka.
Niliwaza mengi na kisha kukumbuka kuwa pesa ilikuwa
inayoyoma hatimaye. Hili likanitia wasiwasi maana pasi na
pesa bila shaka njaa ingeniumbua na kujikuta naomba
msaada, msaada kutoka kwa mtu yeyote yule pasi na kujua
kama ni mtu hatari ama salama!!
Asubuhi kama nilivyopanga wakati usingizi unabisha hodi
nikamkumba muhudumu wa nyumba ile ya kulala, huyu
hakuniletea ugumu katika kuniazima simu yake.
Nilimwambia kuwa kuna mtu nataka kumbipu!!
Nilipopigiwa simu nikakimbilia chumbani kwangu na kisha
kwa tahadhari kubwa nikaipokea simu!!
“Nilijua tu ni wewe na hakika nilisubiri sana kuzungumza
nawe!!” Anitha kutoka upande wa pili alizungumza. Sauti
yake ilikuwa inaunguruma kiasi na nhakika hakuwa sawa na
siku nyingine. Kabla sijamuuliza lolote akaendelea.
ANITHA.
HUWA ni jambo gumu sana kuupina ama kuubatilisha usemi
wa damu nzito kuliko maji!! Lakini hubidi kuwa hivyo pale
upendo unapochukua nafasi!!
Tukio la jana ni kama ndoto na hata muda huu naamini ni
ndoto labda ni wewe wa kuibatilisha ndoto hii, ndoto ya
mwanamke kujikuta katika maamuzi ya kuachana na usemi
wa damu nzito na hatimaye kuubadili kuwa penzi zito
kuliko damu!!
Sijui nilitoa wapi ujasiri ule wa kujitetea mbele ya baba na
mama yangu!! Na wala sikutarajia ujio wao usiku ule tena
wakinifumania mimi na wewe. Ambaye wanakuita mtu
hatari.
Sam, nafsi yangu ilijawa na baridi, lile barafu la ubaridi
likazidi kuvimbiana na nikajihisi kukosa amani kwa zana
kuwa waweza kuniita msaliti!!! Naam!! Ni mwanadamu gani
awezaye kuamini eti mama alishika simu yangu nikiwa
nimeenda kuoga akausoma ujumbe uliokuwa umenitumia
kunielekeza mahali tulipotakiwa kukutana. Yule mama
akawa mjuaji zaidi akaangalia huduma za kipesa katika
namba hiyo na kugundua kuwa ulikuwa ukijiita Gabriel
Madaraka. Kwa hili naomba nikupongeze sana Sam, yaani
laiti kama ungekuwa umetumia namba ambayo umeisajili
kwa jina lako basi nadhani ule ujio wa wazazi wangu
usingekuwa wa kupooza namna ile.
Mama akamshirikisha baba yangu juu ya mimi kutaka
kukutana na mwanaume majira ya saa tatu usiku maeneo
yale tuliyokutana. Nadhani wajua ni jinsi gani baba yangu
ananipenda kwa dhati, hili kwako si jipya hata kidogo kuwa
hataki baya lolote linitokee, akasikia natarajia kukutana na
mwanaume ilhali nimewalaghai nyumbani kuwa naenda
katika majadiliano ya kimasomo na rafiki zangu. Wazazi
wakaitegea mida na hatimaye wakatufuma katika hali ile.
Najua kuwa usingepatikana muda wa mimi kusimulia haya
na unielewe iwapo wazazi wangu wangekugundua na
kukukamata, na jambo hili lingenifanya niwe adui yako
namba moja maisha yako yote!! Sikuwa tayari nikaamua
nkuwakosea heshima, nikakutetea na hatimaye ukaondoka.
Sam!! Nilibebwa mzega mzega nikaingizwa katika gari na
kuendeshwa moja kwa moja hadi nyumbani!!
Hakuna jambo baya kama kupingwa na wazazi wote wawili
katika jambo unalojaribu kulifanya, katika utetezi hakuwepo
aliyesimama upande wangu!! Nilipigwa sana na utu uzima
wangu huu, baba alinipiga kwa kutumia mkanda huku mama
akinipiga vibao na makofi!! Hasira za baba zilikuwa juu
zaidi, baada ya kunipiga sana hakutaka kulala nyumbani.
Akatoweka na mama naye akaondoka kwenda kumtafuta.
Nadhani waisikia sauti yangu ilivyo mbaya, hii ni kwa
sababu nina vidonda mdomoni, walinipiga sana Sam. Lakini
niliamua kubeba maumivu haya kwa ajili yako!! Nikateseka
lakini uwe na imani kuwa sijawahi kukukana hata siku moja!!
Kosa walilofanya wazazi wangu ni kujiridhisha kuwa Anitha
mimi sijakomaa kiakili, wakadhani siyajui mapenzi na sina
uamuzi wangu wangu wa mimi kama mimi!!!
Nilitarajia utanipigia simu Sam usiku ule niweze
kukushirikisha katika jambo nilililokuwa nimefikiria lakini
sikupokea simu yako na nililazimika kuchukua maamuzi ili
tu haki ipatikane, Sam mimi nasome sheria na haki za
binadamu. Lazima kuna kitu katika mlolongo huu, nami
nataka nitambue kuna nini hapa katikati, hii ni nchi yetu
Sam na sis indo vijana kama kuna uvundo wowote
unaendelea na vijana tunafumbia macho, amini umri na
elimu zetu hazitusaidii kitu chochote na ni watumwa wa
elimu ya mkoloni huku tukiwa vibaraka wa ukoloni
mamboleo. Maumivu hayakunizuia kukivamia chumba cha
wazazi wangu ambacho haikuwa mara ya kwanza kuingia.
Ile imani ya baba yangu kwangu na kuonyesha mapenzi
waziwazi sasa ulikuwa wakati muafaka wa kuitumia.
Nikafungua sanduku ambalo nilizijua namba zake za siri,
naam!! Nilichokitarajia nikakikuta!!
Unadhani ni kitu gani ki9nachokwamisha mkakati huu zaidi
ya pesa!! Unadhani kwa nini Eva na mama yake wapo
mahali usipopajua zaidi ya pesa? Sam Pesa haina mdomo
lakini ikipaza sauti basi itasikika dunia nzima na wanyonge
watatetemeka!!
Pesa inaficha maovu na pesa hii inatibua haya maovu!!
Pesa nyingi inaweza kuficha maovu milele lakini akili nyingi
na pesa kidogo hutibua mipango hii!! Sijielewi mimi lakini
natambua kuwa Sam wewe unao uwezo mkubwa sana wa
kufikiri, naam!! Kwa pesa hizi kidogo nilizochota naamini
harakati za kuirejesha amani, kutibua fumbo hili gumu na
kumrudisha mama Eva na Eva katika himaya yako basi zote
zitawezekana!!
Michigani, Kindo, Ezekiel, Alvin vyote hivi vitajulikana!!
Sam! Baada ya kuiba pesa hizo kutoka kwa wazazi
wasiofungamana nami!! Nilitoweka mlinzi akiwa amelala!!
Sasa nane usiku, kila kiungo kikiwa kinauma kutokana na
kipigo, macho yakikosa nuru kutokana na uchovu, bado
niliweza kuzurula mitaani.
Nakukumbusha kuwa Mungu ni muweza wa yote haogopi
usiku wala mchana maana vyote alivibuni yeye!!
Mungu alinisimamia na hadi muda huu unanipigia simu nipo
Royal Hotel Temeke chumba namba 18, Anitha huru katika
fikra na maamuzi huru!!! Simu yangu iliingoja simu yako tu
ili niweze kuizima na rasmi nakutambulishia namba yangu
mpya isiyojulikana na yeyote zaidi yako ni 07...675493.
nimeamua kuungana na wewe Sam, kama ni batili wazo hili
na niadhibiwe nikiwa hai. Na kama nikifa kabla ya kupewa
adhabu basi nifanyiwe alichofanyiwa yule dada katika
simulizi uliyoiandika na ikavuta maelfu ya watu..”NIKIFA
MAITI YANGU IPEWE ADHABU!!”
ANITHA AKAMALIZA!!!!
UPANDE WANGU
Nilibaki kuduwaa nisiamini nilichokisikia, sauti kakamavu
japo inayokoroma kutoka kwa Anitha ilibeba ujumbe mzito
sana. Harakati nilizokuwa nasisitiza kila siku katika makala
zangu, ule uzalendo uliopotea kwa vijana wengi na hali ya
kuthubutu sasa niliionja tena kwa Anitha. Na kubwa zaidi
yale mapenzi wanayodai kuwa yamelogwa na kuwa ya
kudanganyana sasa niliyashuhudia katika upande wa
mapenzi ya kweli.
Anitha alikuwa mwanaharakati!! Nilizungumza naye kwa
kina akanielekeza juu ya hiyo hoteli ilipo.
Sikupoteza muda nikaivaa ile nguo yangu ambayo siku
iliyopita ililowana mikojo ya kiutu uzima. Moja kwa moja
nikaenda Temeke kukutana na anitha.
Wakati huu sikumtilia mashaka tena!!
Nilifika hadi chumbani baada ya kuruhusiwa kuingia. Anitha
hakuwa akidanganya jambo lolote lile, uso wake mweupe
ulikuwa mwekundu, midomo ilivimba sana na yale macho
yaliyowahangaisha wanaume wengi sasa hayakuwa na
mvuto wowote. Alijaribu kutabasamu lakini akaishia njiani
ni kama alipatwa na maumivu kinywani. Nikajisikia huruma
nikamkaribia, nilimpooza kwa maneno ya hapa na pale na
kisha nikakiri mbele yake kuwa yeye alikuwa ‘steringi wa
kike’ katika filamu asiyehofia chochote.
“Anitha sasa vipi kuhusu shule….” Nilimuuliza, badala ya
kujibu akalazimisha tena tabasamu.
“Sam!! Tunasoma ili kupambanua mambo katika jamii
inayotuzunguka, na si kupata shahada ya makaratasi huku
tukishindwa kutatua matatizo katika jamii yetu. Huku
nilipoamua kuingia ni shule kubwa zaidi ya hiyo ya
makaratasi bila uwezo wa kuchanganua na kupambanua
mambo!!!
Unamfahamu Nelson Mandela?? Alifungwa akiwa na miaka
mingapi? Alifungwa gerezani miaka mingapi?? Je alipotoka
alitumia makaratasi ya shuleni kulipigania taifa lake
alilolipenda?? La!! Ile shule ya kunyanyaswa ilikuwa kubwa
kabisa katika maisha yake!! Ama labda nikuulize ni
wanafunzi wangapi wanaopata daraja la kwanza vyuoni na
nchi haiwatambui kwa lolote lile zaidi ya sifa wapatayo siku
ya matokeo?? Lakini ni nani awezaye kumsahau yule
mwanafunzi kijana kabisa kutoka chuo cha Havard Marekani
aliyebuni mtandao wa kijamii wenye nguvu kupita yote
duniani?? Nani wa kumsahau Mark Zuckerberg na facebook
yake.? Unadhani Mark alitumia makaratasi yake ya kufaulu!!
Tuutumie muda uliopo vyema ili tusijutie wakati ujao!!”
alijibu kwa kujiamini Anitha hadio akanishangaza, nikaamini
kwa kile alichokisema kuwa elimu ya darasani bila uwezo
wa kutatua tatizo ni buree!!
Tulizungumza mengi!! Majira ya saa kumi na mbili jioni
tukawa na maamuzi, nikaondoka na kwenda kukata tiketi
kwa ajiri ya safari ya kwenda Iringa. Kwa lengo moja tu
kuitambua Michigani ambayo hadi wakati huo hatukujua
kama ni hoteli, casino ama mgahawa!! Lakini tulitaka kuijua
Michigan.
Tuliamua iwe siku inayofuata ili kuokoa maisha ya Eva na
mama yake ambao lazima sumu za kwenye magazeti kuwa
mimi kibaka tena muuaji na mlawiti zilikuwa zimeathiri akili
yao kupindukia!!
Nilifanikiwa kupata tiketi mbili za kukaa katika siti moja.
Nikiwa nimeandika majina ya bandia!!
Tulilala kimya kila mmoja na tafakari yake, nilikuwa na
amani kuwa nipo na mtu sahihi kabisa katika harakati hizi
za kunirejeshea amani iliyotoweka na pia kunirejeshea
familia yangu!!!
Alfajiri tulikuwa tayari kwa safari ile, safari matata kabisa
kila mmoja akiwa mgeni katika mkoa wa Iringa!
Safari ya kwenda kutafuta kitu tusichokijua, lakini kitu
tulichoamini kuwa kitatuletea majibu ya maswali yetu
ambayo yalikuwa gizani nasi tukiwa gizani huku
tukilazimika kuyajibu ili utokee mwanga!!!
Badala ya kupata siti mbili zilizoungana kwa ajili yetu
tulijikuta tukiwekwa katika siti ya watu watatu!!
Hatukulalamika kwa sababu tulikuwa na shida ya kusafiri!!
Pembeni yetu alikuwepo msichana machachali ambaye
alizoeana na kila abiria kana kwamba ni ndugu yake!! Na
sisi tuliokuwanaye siti moja alitulazimisha hadi tukamzoea,
hadi kufikia Mikumi Morogoro ni kama alikuwa ndugu yetu
wa karibu!!
Hapo nikatumia nafasi ya mazoea hayo nikauliza swali.
“Hivi Michigani huwa ni Iringa ama Mbeya maana niliisikia
nikiwa Dar es salaam enzi hizo.” Swali lile lilimfanya acheke
na kisha kwa kutuonyesha ukomavu wake alitoa majibu
yake!!
“Yaani Michigani zimebakia picha tu, aisee paliteketea
moto mbona!! Miezi tisa iliyopita mbona ilikuwa
mshikemshike, sema uzuri hakuna mtu aliyekufa!! Kwa hiyo
Michigani imebakia stori tu hakuna kitu kama hicho kule
kama hukubahatika kupaona basi tena watafute akina sisi
malijendari wa miji tukuonyeshe picha!!” alijibu kwa kirefu
kisha akatoa cheko refu!!
Anitha akanibinya kuniondoa katika mshangao ule!! Lakini
na yeye alikuwa ameduwaa!!
Michigani iliteketea miezi tisa iliyopita, katika karatasi
lililoandikwa jina la kindo limendikwa miezi tisa iliyopita.
Kuna picha ya mahali panaitwa Michigani!!!
Mkasa ukaingia ugumu mwingine!!
Tunatafuta mahali ambapo pamebakia historia!!!!
Nikalegea kwa uchovu na kukata tamaa!!
 
SEHEMU YA KUMI
“Yaani Michigani zimebakia picha tu, aisee paliteketea
moto mbona!! Miezi tisa iliyopita mbona ilikuwa
mshikemshike, sema uzuri hakuna mtu aliyekufa!! Kwa hiyo
Michigani imebakia stori tu hakuna kitu kama hicho kule
kama hukubahatika kupaona basi tena watafute akina sisi
malijendari wa miji tukuonyeshe picha!!” alijibu kwa kirefu
kisha akatoa cheko refu!!
Anitha akanibinya kuniondoa katika mshangao ule!! Lakini
na yeye alikuwa ameduwaa!!
Michigani iliteketea miezi tisa iliyopita, katika karatasi
lililoandikwa jina la kindo limendikwa miezi tisa iliyopita.
Kuna picha ya mahali panaitwa Michigani!!!
Mkasa ukaingia ugumu mwingine!!
Tunatafuta mahali ambapo pamebakia historia!!!!
Nikalegea kwa uchovu na kukata tamaa!!
***JIFUNZE!!...UZALENDO ni hali ya kuwa tayari kupigania
kitu kwa manufaa ya wengi. Lakini Uzalendo huja hata
katika mazingira ya kawaida, je wewe ni mzalendo kwa
familia yako? Je una uzalendo kwa umpendaye ama ndo
akiwa katika ugumu unajiepusha naye!! Taifa lako ni kubwa
sana kulifanyia uzalendo, lakini vipi kuhusu jamii ndogo
inayokuzunguka, vipi kwa watu wema kwako???
ENDELEA
Safari iliendelea huku dada msema mengi akiwa anazidi
kutuburudisha kwa tuo. Mara alete simulizi hii mara ahamie
hii, Anitha alikuwa wa kwanza kuyachoka maongezi na
uchovu wa safari. Akasinzia!!
Kisha Yule dada naye baada ya porojo za muda mrefu na
yeye akasinzia!!
Binafsi sikuwa na hamu hata kidogo ya kulala, na macho
yalikuwa angavu kutazama hapa na pale ndani na nje ya
basi lile.
Ninakumbuka jina lake ni Super Feo!!
Tulipofika Mikumi basi lilisimama katika hoteli fulani,
kusimama huku kukamzindua tena yule dada msema sana.
Akaanza kusimulia juu ya hoteli ili kuonyesha kuwa anaijua
sana. Sote tulitelemka na kujipatia mahitaji yetu, kisha
tukarejea ndani ya basi tena kuendelea na safari ya masaa
kadhaa, tukaupita mlima Kitonga na hatimaye Iringa ikaanza
kunukia.
Nikamnong’oneza Anitha kuwa tusishukie Iringa bali
twende mbele kidogo aidha Mafinga ama Makambako
kabisa.
Aliniuliza kwa nini lakini sikutaka kumweleza kwa kirefu,
kichwani mwangu niliamua kuishi kwa hofu tena bila
kumwamini kiumbe aitwaye mwanadamu.
Dada msema mengi alikuwa ameahidi kuwa mwenyeji wetu
mjini Iringa na kama ikifaa atatuonyesha picha za Michigani
na eneo lenyewe.
Lilikuwa jambo ambalo tulikuwa tunalihitaji sana, lakini
hapakuwa na haja ya kuingia katika hatari usiyojua kama ni
hatari na kushindwa kujihadhari na mwishowe kuambulia
mabaya!!!
Tulipofika Iringa yule dada alijikuta akishuka yeye pekee
nasi tukiunganisha hadi Mafinga!!
Huko tukatelemka, bila kupumzika tukachukua gari ndogo
ikatusafirisha kurejea Iringa tena!!
Hatimaye majira ya saa kumi na mbili unusu jioni tulikuwa
Iringa mjini.
Hoteli inayokwenda kwa jina la MR ndo ilituhifadhi usiku ule
katika mji ule ambao una baridi haswa.
Ilikuwa hoteli yenye hadhi yake na tuliamua kujihifadhi
katika hoteli ya hadhi ile kwa sababu ilitulazima kwanza
kuupata usalama kabla ya kuendelea na jambo lolote lile.
Hakika tulikuwa salama!!! Lakini hatukulala kabla ya
kuamua jinsi ya kuianza safari yetu!!
Nilimweleza Anitha kuwa ule ulikuwa usiku wetu pekee wa
kuwa pamoja kabla hatujatengana na kisha kuwa tunaonana
mara moja moja iwapo inabidi!!
“Anitha, unajua fika kuwa mimi natangwaza magazetini
nikishushiwa kesi lukuki ambazo sihusiki nazo. Najua hata
wewe utatangazwa kupotea labda kutokana na kutoweka
nyumbani ghafla lakini taarifa zako haziwezi kuwa nzito
kama zangu. Hivyo kwa upande wako ukiamua kufanya
jambo moja tu la kuubadilisha mwonekano wako hakuna
ambaye atakuwa na shida na wewe. Na ninakwambia kuwa
inatulazimu kuwa mbalimbali ilimradi tu mkakati usije
kukomea njiani. Kesho nitakuwa nawe katika kuitazama
Michigan kwa jicho la tatu lakini baada ya hapo Anitha
utalazimika kuwa pekee nami kuwa mtu wa kupewa taarifa
na kutoa ushauri!!” nilimweleza kwa kirefu zaidi na
hakuonyesha kushtuka hata kidogo.
“Niliamua kuja huku kwa hiari yangu mwenyewe!!
Sikulazimishwa na litakalotokea huku ni juu yangu!! Usijali
Sam mimi nitasimama imara kukabiliana na lolote.” Hiyo
ilikuwa kauli kuu ya mwisho kabla kila mmoja hajapitiwa na
usingizi!!!
MKAKATI WA UKOMBOZI
MAJIRA ya saa nne asubuhi tulikuwa eneo ambalo
lilijulikana kama Michigan miezi kadhaa nyuma, sasa liliitwa
Semtema na katika eneo hilo kilikuwepo chuo kikuu cha
Tumaini.
Hapakufanania hata kidogo na hali ya hatari, kila mmoja
alikuwa na mambo yake eneo lile.
Semtema!! Tulilazimika kujaribu kuuliza kwanini paliitwa
hivyo, wenyeji wakadai kuwa kwa kihehe jina linaloanzia se
linamaanisha mwanamke, hivyo kama pangeitwa
Mwamtema, hii ingesimama badala ya mwanaume!!
Ilistaajabisha. Hiyo Michigan mbona haipo sasa. Wenyeji
wakakana kujua kuhusu Michigan na wengine wakasema
walisikia tu uvumi.
Yule dada msema mengi alitudanganya ama!!! Nilijiuliza
huku nikizidi kustaajabu.
Majira ya saa sita tuliamua kuzurura zaidi na kutafuta
chakula. Bila kujua wapi tunaelekea tulijikuta katika eneo
ambalo lilifahamika kwa jina la Isoka. Wenyeji hawakuwa na
haja ya kutueleza lolote mtaa huu ungeweza kuuita
uswahilini.
Kona hii bangi, mara gongo na kona kona nyingi bila
kukutana na mtu anayejali ya mwenzake!!
Tuliamua kutumia eneo lile ili kufaidika na ushushushu wa
watu wa uswahilini. Baada ya chakula ilikuwa zamu ya
Anitha. Akamuuliza mama muuza chakula juu ya Michigani.
Uzuri wa wahehe, wabena na wakinga ambao ndo wengi
katika mkoa wa Iringa, ni wakarimu sana na wanapenda
kuzungumza.
Huyu mama hapo tukawa tumemfikisha!!
Na yeye kama yule mama wa kwenye basi aliyetusimulia juu
ya Michigani huyu naye aliielezea kadri awezavyo. Hapo
sasa tukapata jibu kuwa huenda kule Semtema tulikuwa
tunapata majibu kutoka kwa wanachuo ambao wengi si
wenyeji wa Iringa na hawaujui mkoa ule.
Maelezo ya huyu mama yakaambatana na ucheshi kidogo.
Ni kweli alisisitiza kuwa Michigani haikuwepo tena Iringa,
lakini kicheko kilikuja alipomfananisha Masawe kama
mshamba!!
“Masawe nd’o nani tena?” Anitha alimuuliza.
“Yupo mchaga mmoja hivi ambaye amekimbia uchagani
huko si unajua walivyo wale kwa maduka!! Amefungua duka
huku eti akaliita Michigani, kiduka chenyewe kibovu!!
Sijaona wachaga wasiojua kufanya biashara kama Masawe
yaani!! Ukienda leo mara mafuta hakuna, kesho kiberiti
hakuna!! Hovyo kabisa nimemuhama. Michigani ilikuwa enzi
hizo, ye analeta leo khaaaa” Alijibu kwa sauti ya juu yule
mama na kuyapuuzia yote aliyokuwa anayasema kama
hayana maana!!
Tulimdadisi huku tukimuunga mkono kila alipotaka kucheka
nasi tulicheka!!
Tulipomaliza tukamlipa pesa yake na kuondoka.
“Mh!! Mama mcheshi yule.” Anitha alinisemesha. Badala ya
kumjibu nilimtazama na kuhisi mwenzangu hajang’amua
kitu fulani, kuwa yule mama ni zaidi ya ucheshi aliotupatia!!
Lipo neno la ziada!!
Michigani!! Michigani ya Masawe!! Huyu Masawe lazima tu
atakuwa anajua jambo kuhusiana na Michigani, huwezi tu
kuita Michigani bila kujua kwanini unaita.
Anitha akagutuka na kusawazika usoni katika namna ya
kustaajabu!!!
Tukapitia kibanda cha kutengeneza nywele.
Anitha akaingia mimi nikabaki nje kungoja!!
Alipotoka hakuna na nywele hata kidogo na hakutisha wala
kuchekesha kwa muonekano ule lakini alikuwa amebadilika
na asiyemjua asingeweza kuamini kuwa ni Anitha!!
Akiwa katika hali ile ile tulifanikiwa kukifikia kibanda cha
Michigani. Kilikuwa kibanda kidogo tena pa kichovu sana.
Tulikata tamaa huku tukijiaminisha kuwa maneno ya yule
mama ni kweli kabisa.
Katika ya wachaga waliochoka kimawazo huyu alikuwa
mmoja wao!!!
Anitha akanipa moyo kuwa tukae mahali na kungoja lakini
sikuwa nahitaji la ziada tayari nilikata tamaa. Masawe
anauza pipi kifua, ubuyu, na keki ndogondogo!! Wa nini sasa
huyu!!
Hana maana Anitha!! Nilimwambia!!
“Sasa unadhani Sam ni wapi tutampata huyo mwenye
maana?”
“Anitha ujue tunapigwa baridi saa mbili usiku hii, sikia
kwani ile pesa tuliyoiacha ndani ni shilingi ngapi? Na je una
pesa ya dharula tuachane hadi kesho tena nitakaponunua
simu nd’o tuwasiliane!!”
“Ni milioni nne ile….”
“Weee Anitha umemfilisi mzee Matata we mtoto.”
Hakujibu na badala yake tukakubaliana kuwasiliana siku
inayofuata!!
Nikamsindikiza hadi katika hoteli nyingine ya hadhi ya
kawaida nami nikarejea MR Hoteli huku matumaini yakianza
kufifia.
Matumaini ya kumrejesha Eva na mama yake katika himaya
yangu!!
Matumaini ya kuwaaminisha watanzania kuwa sikufanya
yote yali yaliyoandikwa gazetini.
****
Saa nne asubuhi tayari nilikuwa na simu, nikaandika namba
za simu za Anitha alizokuwa amenipatia!! Upesi akapokea.
“Sam!! Sam!! Mvumilivu hula mbivu!!” alianza hivyo na hapo
akaanza kutiririka.
ANITHA…….
“Kuwa wamoja haimaanishi hata mioyo yenu itaegemea
upande mmoja, iwapo itakuwa hivyo basi mmoja akianguka
nyote mnaanguka, mmoja akikata tamaa wote mnakata
tamaa.
Ningeweza kuwa kama wewe Sam, ulivyokata tamaa nami
nikate tamaa, lakini kama ulidhani kuwa nililala, mimi
sikuwa tayari kulala huku moyo wangu ukinisukuma
kufanya jambo fulani. Nilirejea kule uswahilini Isoka.
Nilirejea na kuitazama hiyo inayoitwa Michigani Sam,
nilikuwa makini sana kutazama huyu mchaga wa kuitwa
Masawe anafunga duka saa ngapi, anaishi wapi kama ikibidi
na muonekano wake maana jana alikuwa kwenye kidirisha
hatukumuona vizuri.
Sam. Kwa duka ama niite kiduka kama kile unaweza
kufuatwa na magari mawili!! Kwa hatari ipi iliyopo hadi iwe
hivyo, sijaiona sura yake kutokana na giza lakini sam.
Hapana mi nakataa yule Masawe yule…sijui lakini huenda
anajua juu ya Michigani. Ama la anazo biashara za magendo
anafanya na hicho kiduka ameweka kama gelesha tu!!”
alinieleza kwa hisia huku akiahidi kuwa analivalia njuga
suala hilo hadi ajue la ziada kuhusiana na kiduka kile.
Sikujua Anitha ataweza vipi kumchimba Masawe ambaye
anaonekana kujikita katika hiyo biashara yake ya duka!!
Nilitamani kumuuliza lakini nikaona huu ni ukatishaji tamaa.
Nikampa hongera kisha nikakata simu na kujipanga vyema
kitandani!!!
Bado nikiwa siamini kama kuna lolote linaweza kutokea
katika kile kibanda walichokiita Michigani.
Nikiwa nimekubaliana na Anitha kuwa mimi nitaweza kuwa
natoka mida ya usiku tu si vinginevyo kulingana na usala
wangu!! Basi niliendelea kuwasiliana naye mara kwa mara
kila palivyokuwa na tatizo lolote.
SAA NANE MCHANA. SIMU KUTOKA KWA ANITHA.
Wakati huu alizungumza kwa tahadhari kubwa sana. Sauti
yake ni kama ilikuwa inanong’oneza.
“Sam, nimefanikiwa kumfuatilia Masawe na gari ile
iliyomchukua usiku. Sam yule wa dukani si Masawe, Sam
niamini ninachokwambia, Masawe si yule wa dukani, kuna
mtu ameniambia kidogo juu ya uhusiano wao lakini
hatuwezi kuzungumza katika simu nitakueleza
nilichofanikiwa kujua juu ya Masawe. Sam kuna kitu
kinazunguka hapa hata wana Iringa hawakijui!! Nipo mitaa
ya huku wapi, sipajui ni wapi Sam lakini ndo huku anapokaa
Masawe mwenye lile banda wanaloliita Michigani.
Muonekano wake hauendani hata kidogo na kile
kiuchafu….kuna picha nimefanikiwa kuipiga japo
pamewekwa onyo kuhusu kupiga picha eneo hili.
Nimekutumia katika barua pepe!!!.......
(Mara anitha akanyamaza…nikamuita hakunijibu!!! Kama
sekunde kumi zikapita Anitha akaanza kuongea huku
akitetemeka.
“Sam….Sam..kuna wanaume wanne, yeah wanne wamevaa
suti nyeusi wawili nyuma yangu na wawili mbele
yangu….Sam wanakuja kwangu hawa…macho yao wameziba
kwa miwani…Sama nakamatwa….Sam Sam……Sam weeeee
nakamatwa mimi Sam!!.......”
Ghafla nikasikia Anitha akipiga kelele, na pale simu
ikakatika.
Nilipojaribu kupiga hakuwa akipatikana tena!!!
Maajabu haya!! Nilijaribu tena na tena kumpigia Anitha
lakini simu haikupatikana.
Mungu wangu weee!! Mtoto wa watu nitajibu nini kama si
kizaazaa kingine tena kikubwa zaidi.
Nilikaa, nikasimama, nikaingia bafuni na kutoka bila
kufanya lolote.
Wanaume wamevaa suti nyeusi mbele na nyuma
wakamzunguka!! Mungu wangu, sasa walijuaje kuwa
anawafuatilia.
Nilitoka haraka katika hoteli ile na mimi nikaizima simu
yangu kwa hofu ya kusomwa mtandao wa mahali
nilipokuwa!!
Moja kwa moja nikaingia mitaani, nikazama katika kibanda
kinachotoa huduma za Internet, upesi nikafungua barua
pepe yangu!!
Nikakuta kweli Anitha alituma picha.
Picha ikafunguka!!
Hamad!!! Ilikuwa picha ya mtoto fulani ambaye niliwahi
kumuona tena katika picha!!
Picha zilizokuwa katika fundo la makaratasi niliyochukua
kwa Ezekiel!!
Palepale nikajipekua na kutoka na ile picha.
Naam!! Ilikuwa yenyewe na ilifanana kwa kila kitu.
Kuna nini hapo Iringa? Iringa kubwa sijui hata ni wapi
alikuwepo Anitha hadi akafanikiwa kuchukua picha ile!!
Baada ya malipo nilikuwa kama nakaribia kupandwa na
wazimu!! Nikajilaumu kwa kumwacha Anitha peke yake
lakini kwa upande mwingine nikaona ni sawa kwa sababu
kama tungeambatana tungekamatwa wote na huo
ungekuwa wakati mbaya pengine kuliko yote katika maisha
yangu!!!
Nilijaribu kwa mara nyingine kuwasha simu!! Nikajaribu
kupiga simu ya Anitha lakini tatizo likawa lilelile. Nilipokata
nikakumbana na ujumbe katika simu yangu.
“UTAKUJA KUMCHUKUA MWENYEWE!!” ujumbe uleule
kama nilioachiwa wakati wakimchukua mama wa watoto
wangu!!
Mama Eva!!....
Ilistaajabisha sana, hawa watu walikuwa wametambaa kiasi
kikubwa hivyo????
Sasa nafanya nini? Hilo likawa swali ambalo sikuweza
kupata jibu mara moja!!!
Nikaumiza kichwa zaidi na kufikiria ni nani anaweza
kunisaidia.
Kwa mara ya kwanza tangu niingie katika kshkash hilo
nikakumbuka kumpigia simu. Mama Samson!!
Mama yangu mzazi!!!
Nilikuwa nimeegemea chini ya mti simu ikiwa inaita……..
Kwa mara ya kwanza haikupokelewa!!!
Nikapiga tena, safari hii ikapokelewa.
Nikasikia kelele nyingi sana zinazofanana na vilio.
Hatukuwa tukielewana, ikabidi mama akate simu.
Nikapiga tena, sasa alipokea na tulijitahidi kusikiana vyema.
“Nipigie baadaye nipo msibani!!!”
“Mama….” Nilimuita.
“Nani wewe mbona kama eeeh ni nani?” nilimsikia mama
akibabaika, ni kama alikuwa amenigundua lakini hakuweza
kusema moja kwa moja nami sikutaka kumhadaa.
“Sam hapa mama mwanao Sam.”
“Koma koma….ukome kuchezea akili yangu we mtoto…..ni
nyie mmemuua mnanitania sivyo!!!” mama alinistaajabisha
kwa majibu yake!!
“Mama mimi ni Sam mama, mama ni mimi.” Nilibaki
kusisitiza tu. Mama hakujibu kitu nikalazimika kufanya
jambo moja kuu la mwisho la kumsisitiza kuwa mimi ni Sam.
“Mama mimi ni Mwikwabe..” nikamtajia jina ambalo
alinitungia utotoni. Hapa nikamsikia mama akihema kwa
nguvu.
“Sam…..ni wewe mwanangu!! Mbona mnanichanganya, na
huyu wanayemleta kwenye jeneza ni nani sasa.” Alitokwa na
kauli ambayo ilinitoa machozi, mama alikuwa
amechanganyikiwa kweli na nilijua jinsi gani akili yake
imeghafirika.
“Mama sauti hii unayoisikia ni ya mtoto wako wa kumzaa,
nipo hai mama. Kama utaletewa mwili hakikisha
unautazama kwa makini mama utaamini kuwa nani ni
mwanao.” Nilijieleza.
“Sam si wanasema mwili hauna kichwa sijui kimefanyanini
huko na huku siwaelewi ujue, yaani Sam nimechanganyikiwa
mwanangu!! Mdogo wako amepoteza fahamu hadi leo, baba
yako ananiita mimi mchawi eti nimekutoa kafara Sam
wangu!! Kweli nilivyoteseka na wewe Sam miezi na miaka
leo hii nikutoa kafara Sam. Nilivyobangaiza pesa uende
shule na ukapata lazi bado nikutoa kafara. Kweli baba yako
ni wa kusema haya mbele ya watu kabisa ananitukana kiasi
hicho na watu wanaamini kuwa nimekuua. Sasa wameweka
kikao wananidai kichwa chako, eti kama sikitoa kichwa
chako basi wananikata changu!! Si uje Sam uniokoe mama
yako huku!! Ni wewe sam ujuaye mimi nina nafasi gani
kwako Sam. Kama kweli upo hai Sam nakuomba ufanye
jambo hili dogo kabisa kwangu!!! Njoo uwaumbue wazee
hawa wanaoniita mimi mwanga tena mchawi niliyeshindikan
a!!” mama alimaliza kuzungumza huku akijizuia kulia, mimi
kwa upande wangu sikuweza kujizuia, nilikuwa nalia. Sauti
ya mama iliniumiza, waliomwita mama yangu mchawi
waliniumiza zaidi nafsi.
Hadi mama yangu anakata simu nilikuwa katika mgagagiko
wa aina yako!!
Mpalanganyiko usio kifani.
Anitha amekamatwa na niliisikia sauti yake ikiomba huruma
yangu katika simu.
Mama yangu mzazi naye anazushiwa kuwa ameniua angali
nipo hai!! Nilijua ni hila za watu wale wabaya
kunifedhehesha na kuisababisha jamii nzima inilaani!!
Lakini kwanini sasa wamemgusa hadi mama yangu!!
Kwanini uchungu wangu nichangie na mke wangu,
mwanangu Eva, Anitha na sasa mama yangu mzazi.
Mwanamke mwenye thamani kwangu kuliko wanawake
wote!!!
 
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
Hadi mama yangu anakata simu nilikuwa katika mgagagiko
wa aina yako!!
Mpalanganyiko usio kifani.
Anitha amekamatwa na niliisikia sauti yake ikiomba huruma
yangu katika simu.
Mama yangu mzazi naye anazushiwa kuwa ameniua angali
nipo hai!! Nilijua ni hila za watu wale wabaya
kunifedhehesha na kuisababisha jamii nzima inilaani!!
Lakini kwanini sasa wamemgusa hadi mama yangu!!
Kwanini uchungu wangu nichangie na mke wangu,
mwanangu Eva, Anitha na sasa mama yangu mzazi.
Mwanamke mwenye thamani kwangu kuliko wanawake
wote!!!
**JIFUNZE!! Wakati wa malalamiko yako uyatoayo kila siku
na kujifanya wewe unaonewa kupita watu wote, kujifanya
kuwa ni wewe umetendwa kupita watu wote duniani. Wapo
wengine ambao kilio chao ni kikubwa zaidi na hawana amtu
wa kuwasikiliza kama ilivyo kwako wewe!! Hawana msaada
wowote na badala yake wanalia na nafsi zao!!
Wakati unajifikiria wewe kumbuka kumfikiria na jirani yako.
Huo nd’o UPENDO!!!
ENDELEA!!!!
KITENDO cha kujikuta namweka mama yangu mzazi na
Anitha katikia mzani mmoja ili nijue nini cha kufanya na nani
wa kuanzia kilinivuruga akili akili. Kuna mda nililazimika
kusema kwa sauti ilhali hakuna yeyote aliyekuwa
akinisikiliza. Nilihaha huku na kule katika mkoa ule wa
Iringa nab ado hali ilikuwa tete.
Sikuwa na ndugu, rafiki na hata jamaa wa karibu wa kuweza
kumshirikisha lolote lile. Niliketi chini ya ule mti na
pasipokutarajia nikapitiwa na usingizi. Bila shaka kutokana
na mawazo yaliyokuwa yanazidi badala ya kupungua.
Mimi naitwa marehemu!! Ni nani huyu anasimama nyuma ya
haya mambo yote? Niliwaza baada ya kurejewa tena na uhai
baada ya kifo cha usingizi!!
Mkononi nilikuwa na bahasha yangu ambayo thamani yake
ilizidi kushuka badala ya kuongezeka. Bahasha ambayo
badala ya kunipa tumaini iliishia kunipa dalili tu ya
matumaini kisha yakatoweka pasipo kutimia. Bahasha
ambayo sasa imenionyesha picha ya mtoto ambaye ameketi
na ni picha hiyohiyo kutoka katika barua pepe aliyonitumia
Anitha.
Anitha ambaye sasa sipo naye tena na sijui ni kitu gani
kimemsibu!!
Mbaya zaidi nimetumiwa ujumbe kuwa NITAMFUATA…sasa
namfuata wapi mimi eeh!!
Na huku mama anatishiwa kukatwa kichwa iwapo tu kichwa
change hakitaonekana!! Mimi ambaye nipo hai.
Washenzi wameamua kuigusa familia yangu ili nijitokeze
waniue!!! Ni hili nililitambua kichwani mwangu. Mbaya zaidi
sikuwa tayari kujitokeza kwa mtu yeyote yule kabla
sijajiweka salama.
Kilichonipa faraja ni maneno ya Anitha usiku ule tuliokutana
kwa mara ya kwanza tangu atoroke nyumbani kwao.
“Pesa ni kila kitu!!” nikafanya tabasamu na kisha
nikautazama ule mfuko wenye pesa zilizohifadhiwa katika
usalama wa hali ya juu!!
Asante sana Anitha!!! Sijui kama zisingekuwepo pesa hizi
ningekuwa katika mawazo gani mengine!! Nilijisemea. Na
hapo nikanyanyuka na kupiga hatua nyingi kuelekea popote
pale na sikuwa nikitambua majina ya mitaa mingi!!
Kufikia hapo nikaamini kuwa nilikuwa nahitaji kwa namna
yoyote ile mwenyeji wa mkoa huo aweze kuwa mwanga
wangu. Lakini kigumu zaidi nililazimika kupata mwenyeji
asiyenifahamu!!
Jambo gumu kabisa, utajuaje mtu hakufahamu!!!
Nikaghairi.
Maamuzi ya pili yakawa ‘jino kwa jino’.
Nikapanga safari ya kwenda Morogoro. Kwanza niwakabili
jino kwa jino hao watu wanaotishia amani ya mama yangu
halafu kitakachofuata hapo na lolote liwe lakini walau
nimpiganie mama yangu!!!
Kwa Anitha sikujua wapi naanzia hivyo huenda ni vyema
kupata moja kuliko kukosa yote, isitoshe Anitha alikuwa ni
askari aliye tayari kufia vitani akitetea haki!!
Nikalala bila kula chochote, asubuhi sana nikadamkia katika
stendi ya Iringa.
Baridi ilikuwa kali sana!! Na basi lilikuwa halijafika, hali ile
ya hewa ikanikumbusha jijini Dar es salaam, siku ambayo
nakutana na mauzauza ya Ezekiel wawili mmoja mzima na
mwingine maiti.
Kisha baada ya masaa kadhaa nakumbwa na kashfa ya
kulawiti hadi kuua!!
Uchachu ukanikumba mdomo baada ya kuwaza siku hiyo.
Nikatafuta sigara nikawasha na kuanza kupuliza kama siku
ile!!!
Nilipopiga funda nne, basi likawasili. Nikaionea huruma ile
sigara lakini nikalazimika kuizima kisha kuisagia chini!!
Nikaelekea garini!! Nikapata siti ya dirishani. Nilikuwa
sijielewi hata kidogo lakini nilijua naikaribia shari.
Kelele za vijana wauza maji, soda na vinywaji vingine
hazikunifurahisha bali kunibughuzi. Mara huyu apige
mayowe haya mwingine alalamike vile ilimradi tu bughudha.
“Pata Bajia, Sambusa za leoleo, sambusa za moto mtoto
anapoozewa, sambusa za nyama achana na zile za Singida
mwawekewa nyama ya punda, usisikie ya watu wahehe
wala mbwa…uzushi mtupu kula mwenyewe ujionee kisha
ukahadithie. Ukinunua moja nakupa na picha ya huyo
ng’ombe aliyechinjwa!! Usiwasikilize wazushi, niulize mimi
mama lao!!” hizi zilikuwa porojo nyingine tena, sauti hii
ilipangilia maneno hasa na ilikuwa ikirudia mara kwa mara
bila kukosea hata kidogo!! Abiria waliokuwa garini
wakajikuta wanacheka, lakini katika kucheka huko wengine
wakataka kununua kweli. Mimi nikajituliza huku
nikijilazimisha kusahau kama nimesikia porojo zile sikuwa
na hamu ya bajia wala sambusa za nyama ambazo yule
mama alipinga kabisa kuwa sio nyama ya mbwa!!!
Baada ya muda kidogo sauti ile ilihamia katika gari ndani!
Mama aliendelea kutuliwaza abiria na maneno yake.
Nikavutiwa kunyanyua kichwa nimtazame vyema
anafanania vipi huyu mama mwenye uwezo wa ajabu vile
wa kukariri.
Lahaula!! Sura haikuwa ngeni machoni mwangu!! Alikuwa ni
mama ama niite mwanamke ambaye siku kadhaa nyuma
tulisafiri naye wakati tunatoka jijini Dar es saalam, porojo
zake zikatufanya tuijue kiasi Michigani.
Sasa alikuwa katika basi letu!!
Nikataka kumpuuzia lakini imani ikanivuta kumuamini kiasi,
nikaisshusha vyema kofia yangu ikaniziba sura yangu. Na
mimi nikaomba huduma ya sambusa.
Akajongea nilipokuwa huku akiendelea kuhamasisha juu ya
sambusa zake.
“Anti samahani naweza kuuliza?” nilianza kujenga hoja.
“Wahehe, Wabena, Wakinga asili yetu ustaarabu na
ukarimu, ukitukera hatulipi kisasi siye twajinyonga tu!!
Niambie bila shida baba yangu!!” alinijibu huku akinifungia
sambusa tatu kama nilivyomwagiza.
“Hivi ni wewe tumesafiri wote majuzi kutoka Dar tuka….”
Kabla sijamalizia tayari alikwisha nitambua.
“Wa Michigani nyieeee ni wewe looh, yukwapi bibi yako
yule mbona ana wivu sana yule.” Alinieleza kwa sauti ya
chini nikasikia peke yangu.
“Hayupo leo mamangu kuna matatizo yamemkumba…”
“Alienda Michigani ama?” aliniuliza kwa sauti tulivu, sasa
hakuwa katika utani wowote ule. Uso wake ulionyesha
wasiwasi na ni kama kuna kitu hakupenda kiwe kama
anavyodhani. Hakutaka jibu langu liwe kweli.
“Hapana ni matatizo mengine tu, kwanini umewazia
Michigan?” nilihoji huku nikiuficha wasiwasi wangu.
“Mh…..afadhali kama sio huko maana….ehee we nawe tena
mbona unarudi mwenyewe Dar es salaam” alihoji na sasa
alikuwa anatabasamu.
“Hata sirudi Dar ujue, hivi tunaweza kuongea kidogo.”
Niliamua kutumia nafasi.
“Lakini bado dakika mbili gari linaondoka hapa.”
Alinitahadharisha. Nikamweleza haikuwa muhimu kusafiri
wakati sijazungumza naye.
Akakubaliana nami, tukatelemka chini huku akisifia
sambusa zake.
Mwanga ulikuwa umeanza kuonekana na giza likaipisha
nuru! Tukajiweka mbali na umati wa watu. Nikamweleza
shida yangu.
Nikamweleza juu ya Anitha na kupotea kwake katika namna
ya utata. Sikumuamini kiundani na kumweleza juu ya hatia
inayonikabili jijini dare s saalam juu ya mauaji. Nilimuacha
yeye awe msemaji mkuu.
“Kaka Sambusa zangu zitaniozea lakini ujue.”
Alinitahadharisha.
“Kwani kapu moja bei gani kwa ujumla.” Akanitajia bei,
nikamweleza kuwa nitamlipa mara mbili. Na kama
hakuamini vile nikajipekua na kutoka na kiasi alichotaja na
ziada yake.
Macho yakamtoka pima na bado hakuonekana kunitambua!!
Mazungumzo yakaanzia pale, yule mwanamke akanieleza
machache ayajuayo juu ya mkoa ule. Akapinga kabisa kuwa
Anitha amechukuliwa kishirikina. Akapinga kuwa mkoa ule
hauna mambo hayo ya kurogana.
“Tena basi bora angekuwa mwenyeji wa huku!! Yaani mgeni
hana hata siku nne!! Mi nakataa kwa kweli labda tu kuna
mwanaume amemuweka ndani wewe hujui.” Alinijibu
kiuhakika zaidi. Nikatamani kumweleza japo kwa ufupi
kuwa mimi ni nani lakini niliingiwa hofu.
Nikamuona kama anafikiria jambo kidogo na kasha akasema
kwa sauti ya chini kama anayejisemea mwenyewe.
“Auuu labda mambo ya Anti Ezekiel yameanza tena…lakini
hamna wala haiwezekani.”
Maneno yake yakanishtua, alikuwa ametaja jambo zito
katika sauti ndogo!!
Anti Ezekiel!! Jina hili lilihusiana na mkasa wangu moja kwa
moja. Nikakosa ustahimilivu nikahoji.
“Anti Ezekiel ndo nani kwani?”
“Jamaa aliyeleta uzushi huo na yeye ukimuuliza
anakwambia jibu hili moja tu UKIJUA NA WEWE
UNAPOTEA” alinijibu kwa utaratibu na hakutaka
kulizungumzia zaidi.
“Nani anayesema habari hizo kwani?’ sikutaka jambo hili
liishie juu ya juu. Nikambana.
“Simfahamu lakini wanasema ni kichaa mmoja hivi. Hakuna
atakaye kuamini kuhusu hilo. Si unajua maneno ya vichaa,
kwa jinsi nilivyosimuliwa ni kwamba watu walikuwa
wakipotea, waganga wa jadi wakishinda kupata majibu yeye
anasema ni upepo wa Anti Ezekiel. Mbona huu mwaka wa
nne unafika sasa tangu zivume hizi habari.” Alinieleza kwa
utulivu huku akiyatuliza macho yake usoni kwangu.
Maelezo yake yakazidi kunichanganya, sasa yule Ezekiel
nd’o anafanya nini sasa, mara amekufa mara akaonekana
Ubungo, sasa huku Iringa tena kuna Anti Ezekiel wao.
Upuuzi huu. Nilihisi kuchanganyikiwa.
“Kwani kaka, Anitha yeye kapoteaje ghafla hivyo!! Tatizo
lako ni moja tu wewe unanificha siri huku ukisahau kuwa
mficha uchi hazai. Na mficha jipu usaha utamuumbua….”
Alinipiga na maneno yale makali, nikajisikia aibu sana
maana alikuwa amesema kweli.
“Sio kama nakuficha mama…hapana nimechanganyikiwa
kabisa!!!”
“Unadhani suluhu n’do kukaa kimya kaka!!” alizidi kunibana.
Kabla sijasema lolote akachukua uwanja zaidi.
“Sam..” akaniita. Moyo ukapiga kwa nguvu kubwa!!
Amenijuaje jina langu huyu mwanamke ilhali siku ya safari
sikujitambulisha kwa lolote lile.
“Unajiuliza nimekujuaje?” alisema kilichokuwa katika akili
yangu!!
“Sam mdogo wangu! Ama kaka yangu vyovyote vile, katika
mawazo yako unadhani mimi ni mtu mbaya ama ninayeweza
kuhatarisha amani yako ambayo tayari ipo hatarini. Sam
mimi sipo hivyo, nd’o maana hata kwenye basi tulilopanda
nilikutambua kuwa unasakwa kwa udi na uvumba lakini je
nilisema neon lolote mie! Nilishakoma tabia ya kujifanya
najua mambo, biashara yangu ya bajia na sambusa
inanitosha sana.
Sihitaji kupata mamilioni kwa kumsukumiza kijana
mwenzangu katika moto. Baba yangu amefia jela kwa kosa
la kusingiziwa, nitajuaje kama na wewe wanakusingizia, ujue
polisi watu wa ajabu sana, wanapenda sana kusaidiwa
upelelezi lakini wewe sasa uwe na shida uwaombe msaada
nd’o utakoma na kiherehere chako. kama walishindwa
kuniruhusu tu kuongea na baba yangu!! Wakanitishia
kunifunga, niwapendee nini mimi sasa!!
Mzeewangu akahusishwa na wanaume wengine wanane eti
wamehusika kuteketeza Michigani?? Mimi nilikuwa
mfanyakazi pale ndani, Michigani haikuwa ya kuteketezwa
na watu masikini kama wale. Haya masikini ana haki,
Michigani ikateketea na baba naye akafungwa!! Nd’o mimi
unayeniona hapa sasa Iringa nd’o mama lao. Yaani sina
ndugu wala shoga, napiga kazi tu kupata mkate wangu wa
kila siku. Kama wewe usivyomwamini mtu kwa mkasa wako
huu na mimi simwamini mtu.
Nilipokuona nikakutambua, machoni hukufanania na mlawiti
na muuaji. Tena juzi niliposoma gazetini kuwa umekufa nd’o
nikajua kabisa kuwa kuna mpango hapa si bure!! Kama
kweli umekufa mbona upo hapa muda huu? “ sasa aliniuliza
na kasha kunitazama usoni.
Sikuwa na nguvu za kukimbia, ganzi ilishika mwili mzima.
Huyu mwanamke alikuwa ananijua vyema kuliko
nilivyodhani!! Na ilikuwa kama bahati tu hakuweza
kunichoma popote pale.
“Naiwa Jojina usiniite mama lao!!” akajitambulisha jina lake
hatimaye.
Nisingekuwa na lolote la kujitetea, nisingeweza kulaghai
tena. Jojina alikuwa ananitambua vyema!!
Nikajaribu kumwomba radhi, akanielewa huku akinisisitiza
ni vyema niishi kwa tahadhari kubwa.
“Sasa huyu Anitha, sina hata la kukusaidia lakini kama
maneno ya yule chizi yapo sahihi basi kile kitabia cha Anti
Ezekiel kinaweza kuwa kimeondoka naye.” Alinieleza huku
akijaribu kutabasamu.
“Chizi mwenyewe anayesema hivyo yupo wapi…..” nikaamua
kuuliza.
“Mh!! Kwa kweli ni miezi mingi sana imepita tangu
nimwone. Nitakudanganya nikikwambia kuwa yupo Iringa
hii. Kuna watu wanadai alionekana Dar es salaam, sasa sijui
kama ni kweli ama la!!” alinijibu baada ya kufikiria kwa
sekunde kadhaa.
“Na uliwahi kumtambua hata jina lake kwani?”
“Alikuwa na majina mengi sana mara wengine wamwite
mganga wa jadi mstaafu, wengine walimuita Zuzu…lakini
kuna waliodai kumfahamu na wakasema jina lake halisi ni
Kindole, wakamfupisha na kumwita Kindo!!!”
“Nini?” nilihamanika nisiamini kile ninachokisikia. Yaani
Kindo nimjuaye ama Kindo mwingine, Kindo alikuwa kichaa?
Mbona alikuwa timamu jijini Dar es salaam. Nilijiuliza katika
nafsi yangu!!
“Na kama ni kweli alikufa basi ndo yaleyale ya Anti Ezekiel
labda maana maneno huumba!!!” aligandamiza tena yule
mama na kuzidi kunichanganya!!!
 
ILIPOISHIA
Sikuwa na nguvu za kukimbia, ganzi ilishika mwili mzima.
Huyu mwanamke alikuwa ananijua vyema kuliko
nilivyodhani!! Na ilikuwa kama bahati tu hakuweza
kunichoma popote pale.
“Naiwa Jojina usiniite mama lao!!” akajitambulisha jina lake
hatimaye.
Nisingekuwa na lolote la kujitetea, nisingeweza kulaghai
tena. Jojina alikuwa ananitambua vyema!!
Nikajaribu kumwomba radhi, akanielewa huku akinisisitiza
ni vyema niishi kwa tahadhari kubwa.
“Sasa huyu Anitha, sina hata la kukusaidia lakini kama
maneno ya yule chizi yapo sahihi basi kile kitabia cha Anti
Ezekiel kinaweza kuwa kimeondoka naye.” Alinieleza huku
akijaribu kutabasamu.
“Chizi mwenyewe anayesema hivyo yupo wapi…..” nikaamua
kuuliza.
“Mh!! Kwa kweli ni miezi mingi sana imepita tangu
nimwone. Nitakudanganya nikikwambia kuwa yupo Iringa
hii. Kuna watu wanadai alionekana Dar es salaam, sasa sijui
kama ni kweli ama la!!” alinijibu baada ya kufikiria kwa
sekunde kadhaa.
“Na uliwahi kumtambua hata jina lake kwani?”
“Alikuwa na majina mengi sana mara wengine wamwite
mganga wa jadi mstaafu, wengine walimuita Zuzu…lakini
kuna waliodai kumfahamu na wakasema jina lake halisi ni
Kindole, wakamfupisha na kumwita Kindo!!!”
“Nini?” nilihamanika nisiamini kile ninachokisikia. Yaani
Kindo nimjuaye ama Kindo mwingine, Kindo alikuwa kichaa?
Mbona alikuwa timamu jijini Dar es salaam. Nilijiuliza katika
nafsi yangu!!
“Na kama ni kweli alikufa basi ndo yaleyale ya Anti Ezekiel
labda maana maneno huumba!!!” aligandamiza tena yule
mama na kuzidi kunichanganya!!!
**JIFUNZE!! SIRI ni siri iwapo ni ya kwako wewe na moyo
wako!! Usijidanganye kumshirikisha rafiki yako na kumwa
ENDELEA
Nilishangazwa na majibu ya Jojina yaani ni kama alikuwa
akijaribu kuniimbia mashairi ambayo yameunganika vyema
yakijali uzani wa vina na masivina lakini yakikosa mstari wa
mwisho kila mara.
Mara anieleze juu ya michigani, lakini mwishowe hiyo
Michigani yenyewe haipo tena.
Anazungumzia mkasa wa Anti Ezekiel ikiwa hamjui wala
hana uhakika juu ya kiumbe cha kuitwa jina hilo.
Huyohoyo anadai kuwa Kindo ambaye ana wazimu alikuwa
akisema sana juu ya Anti Ezekiel lakini mwishowe huyo
Kindo hayupo tena Iringa na mbaya zaidi hajulikani alipo
nan i tetesi tu kuwa alioneka Dar mara ya mwisho.
Kama kweli ni huyo kindo Aliyeonekana dar basi kwa namna
yoyote tunahangaisha vichwa kumzungumzia mtu
aliyeuwawa siku kadhaa nyuma baada ya kuchukuliwa na
watu wasiojulikana.
Hawa watu wasiojulikana nd’o hao hao waliomuua Ezekiel,
ndo haohao waliomchukua mke wangu na hawa hawa
wamenizushia kuwa nimekufa na wamemweka mama yangu
katika wakati mgumu kupindukia.
Hawa watu nd’o wanadai kuwa nitamfuata Anitha, na
nitamfuata mama Eva.
Hawa watu ni akina nani!!!
Swali hilo likanitia kati kati ya hasira na mtafaruku wa
kimawazo. Hawa watu walikuwa wamenizidi ujanja na tayari
walishacheza na akili ya watu wa kuaminika serikalini ili
nisiaminiwe popote pale!!
“Kwa hiyo dada Jojina….huyo Kindo wewe uliwahi kumuona
ama!!”
“Nd’o maanake, hapa Iringa nani ambaye hakumjua na
wazimu wake yule bwana. Zaidi lilikuwa skendo lake la
Michigan…….”
“Skendo la Michigani?? Kiaje skendo la Michigani, yaani
unanichanganya kweli dadangu hujui tu!!”
“Nakuchanganya na kipi tena, nakujibu kila unachouliza
kadri ya uwezo wangu!!....na ninajitahidi zaidi ili
ikiwezekana leo nyumba yangu iwe na mgeni.”
Akazungumza kwa madaha kisha akanitazama kwa jicho
fulani nikaelewa maana yake…sikutaka kuyakuza mambo
zaidi nikamuuliza kwa utulivu nini kilijiri huko Michigani.
“Wanaomfahamu huyo wa kuitwa Kindo wanadai kuwa
alichanganyikiwa baada tu ya kutoka Michigani.”
Akanitazama kisha aakaendelea, “Kindo alikuwa muajiriwa
huko Michigani, kilichomtoa huko hakijulikani lakini baada
tu ya kutoka huko siku kadhaa mbele Kindo ana wazimu!!
Lakini usiniulize maswali mengi maana mimi sijui lolote
nazisikia simulizi hizi nikiwa nauza bajia zangu na sambusa
za nyama.” Alinijibu kizembe, ni kama alikuwa amechoshwa
na maswali.
Majira ya mchahna tulikuwa tukitembea kwa tahadhari,
tukakipita chuo cha Tumaini na hapo akanieleza kuwa
mahali niliposimama ndipo Michigani.
Nilikata tamaa kwa sababu hapakuwa na sehemu ya
kuanzia, ni kama makumbusho tu ya kale ambayo
yamevunjwa na kusahaulika zamani sana. Hapakuwa na
ulinzi wala mtu yeyote aliyekuwa akijihangaisha na eneo
lile. Na hakuna aliyehangaika kutuuliza ni kitu gani tulikuwa
tunatafuta.
Sikuwa na la zaidi, nikaondoka na mama yule hadi nyumbani
kwake, huko nia ikiwa moja tu kujua zaidi kuhusu Michigani.
Tulipofika alinionyesha picha za Michigani hiyo ya zamani
ambayo iliteketea yote miezi mingi nyuma!!
Ilikuwa sehemu ya kuvutia, palikuwa na bwawa kubwa la
kuogelea, hoteli ya kifahari iliyoitwa Michigani na bustani
ya kisasa.
“Siku za sikukuu palikuwa panajaa sana hapa, sio unajua
mambo ya watoto na wazazi wao??” aliniambia wakati
tukiingalia picha ya Michigani.
“Ungeweza kuona maeneo mengi lakini si kila eneo
tuliruhusiwa kupiga picha kirahisi, hata hii yenyewe ni basi
tu niliipata kibahati. Watu wana mambo, visheria vya ajabu
ajabu kama nini!!!” alilalamika. Lakini akiona ufahari na
kisha kujisifu kuwa yeye ni mama wa mjini alifanikiwa
ajuavyo.
“Wewe uliipataje sasa.”
Kabla ya kujibu swali hili akacheka.
Kama nilivyokueleza awali juu yam zee wangu kuchukuliwa
na skendo hili la kuichoma Michigani jambo ambalo hata
naenda kaburini nitalikana kwa nguvu zote. Kweli
nilibahatika kuingia katika mahusiano na bwana mmoja mtu
mkubwa kidogo pale Michigani, basi nikawa nahudumiwa
kila kitu kwa bili yake, hakuwahi kunieleza kwa nini picha
hazipigwi hata zile za kumbukumbu!! Mzee wangu
akazinasa hizi habari, akaniweka kitako kunikanya kuwa
Michigani kuna mazingaombwe yanayofanana na ushirikina.
Kwani kila sikukuu ifikapo basi kuna watoto zaidi ya
watano wanapotea na wasionekane tena. Baba alisisitiza
kuwa anaifahamu vyema michigani kuwa watu wake si
wazuri, akanisihi nijiweke mbali nisije kupoteza mtoto
wangu kwa hila za wanadamu, mtoto huyo alikuwa akiitwa
Justin na nilimzaa bahati mbaya tuseme. Baba yake
alikimbia, maneno ya baba yakaja na ukweli ndani yake
lakini nilikuwa nimechelewa na wala sikutaka kuamini hata
kidogo kuwa mwanangu amepotea eti kisa Michigani, japo
alipotea siku ya sikukuu pia.
Tulizunguka kwa waganga wa kienyeji lakini hakuna hata
mmoja aliyesema ukweli wote walitulaghai. Baba alibaki
kusema kichinichini kuwa Michigani hiyo Michigani!!
Hakuwa na maelezo ya kutosha labda na yeye hakujua
vyema kama mimi nilivyobisha bila kujua neon lolote hadi
leo nipo ndotoni.
Nikiwa na mapenzi tele na Dulla huyo mtu mzito wa
Michigani nikafikia hatua ya kumweleza hisia za mzee
wangu juu ya mtoto wangu kupotea. Dulla akapinga na
kusema kuwa baba anazeeka vibaya. Name nikamuunga
mkono. Hiyo siku tulifurahi sana, akiwa kama mpenzi
akanitembeza maeneo kadha wa kadha akiahidi pia kuwa
atakuja nyumbani kujitambulisha kwa baba ili anioe moja
kwa moja!! Kwa kuhitimisha furaha yetu akanipa picha hii
inayoonyesha maeneo kadhaa ya Michigani.
Baada ya juma moja Michigani ikaungua moto!!!
Siku tatu baadaye baba yangu akaanza kusakwa,
akapatikana na alivyopotezwa……alivyopotezwa!!!! Basi tu
Mungu anajua” kufikia hapa Jojina akaanza kutokwa na
machozi, ilikuwa ni kumbukumbu mbaya sana kwake, lakini
ikiwa ni kumbukumbu yenye mafumbo makali ndani yake
bila yeye wala mimi kujua majibu!!
“Kwa nini sasa Dulla hakukusaidia katika kumsaidia mzee
wako asiende jela.” Nilimuuliza.
“Dulla…Dulla hakuonekana tena, masikini yaani wanadai
kuwa hakuna hata mtu mmoja aliyekufa lakini nina mashaka
kuwa huenda Dulla alikufa.”
“Kwanini una mashaka hayo sasa!!!”
“Kwa sababu sijawahi kumuona tena na kuna jamaa zake wa
karibu walinihakikishai kuwa Dulla alikufa. Na hapo
nikaamua kubadilika na kuwa mama lao. Kila biashara
nafanya.” Alimaliza kwa mbwembwe huku akilazimisha
tabasamu.
Maneno ya mama lao Jojina yalizidi kunivuruga, badala ya
mwanga likawa giza tena. Mkasa mmoja haujaisha
inaongezeka mikasa mingine lukuki.
Mtoto wa Jojina kupotea, kisha Michigani kuteketea, baba
yake Jojina kupotezwa katika uso wa dunia katika namna ya
kustaajabisha!!
Michigani ya kwenye picha haikuwepo tena duniani!!!
Kuna nini Michigani?
Swali halikupata jibu!!
“Dulla wangu jamani eeeh!!” alianza kulia chinichini huku
akiwa ameikumbatia picha fulani ambayo hakuwa
amenionyesha kabla. Nilimbembeleza taratibu, hadi
alipoitua ile picha kisha tukahamia katika mazungumzo ya
hapa na pale, akanichombeza name nikamchombeza lakini
hapakuwa na muda wa kuendelea mbele zaidi. Akasikika
muuza magazeti.
“Wacha wee hebu ngoja nikakwapua gazeti, halafu leo
kachelewesha huyo. Kuna hadithi nafuatilia magazetini,
nakuja Sam usiwe mpweke.” Alinisihi kisha akatoka nje.
Alipotoka nikaupangusa mdomo wangu, sikuwa nimefurahia
kumbusu mdomoni, lakini ilinilazimu kufanya vile maana
nilihitaji kujua mengi sana kutoka kwa mama lao. Nilikubali
kumbusu lakini moyoni nikijiapiza kuwa sitaendelea zaidi
japokuwa baridi la Iringa lilitia hamasa kuendelea zaidi.
Nikajiandaa kumkabili akirejea kwa maneno ya kumhadaa ili
niondoke pale kwake, nikaupanga uongo nao ukapangika.
Alipoingia badala ya kuniparamia pale kitandani,
akanitazama huku akistaajabu.
“Sam!!” aliniita, nikageuka kumtazama, hakuwa kimahaba
tena.
“Mkeo….mh!! mkeo anajua ulipo?” aliniuliza, nikaketi kitako
niweze kujua nini kinaendelea.
“Kwanini?” nilimuuliza kwa kiherehere nikitaka kujua
kulikoni.
“Si ndio huyu Edna ama …mama Eva si nd’o hivyo!!” alizidi
kunivuruga.
Uvumilivu ukanishinda nikasimama na kuangalia
anachokisoma.
Ilikuwa picha ya mke wangu Edna ama mama Eva kama
nilivyomzoea. Sura yake kama niijuavyo ilikuwa
inatabasamu!!!
Chini ya ile picha iliandikwa kitu ambacho nilitumia
sekunde nyingi kurudia kukisoma.
MAREHEMU EDNA KIMARO!!
Nguvu zikaniishia, nikajitahidi kujizuia lakini ikashindikana
na hapo nikaanza kuona giza ..
Kisha…..kisha …..nikaona kitu cha ajabu sana nikatami
kukitazama zaidi lakini sikuweza kiza kikazidi kutanda kisha
kimyaaa!!!!
Baadaye nilijikuta katika mikono ya uvuguvugu kiza kinene,
nikajigeuza huku na huku nikaisikia sauti ikikwaruzakwaru
za huku ikiliita jina langu!!
Nilijaribu kuvuta kumbukumbu zaidi kuwa ni wapi nipo.
“Sam!!” sauti iliita tena!! Sasa haikuwa ikikwaruza, ilikuwa
sauti ya mama lao. Name nilikuwa nimekumbatiwa vyema
na ule uvuguvugu ulitoka kwake.
Feni ilikuwa ikinipuliza!!
Mama lao akanyanyuka na kuwasha taa.
Akanieleza kuwa nilipoteza fahamu!! Kisha bila kunipa
nafasi ya kusema chochote akanisihi kuwa sitakiwi kuamini
kila ninachokiona wakati wa matatizo.
“Sam sidhani kama mkeo anaweza kulemazwa akili kiasi
hicho, yaani hapana kabisa..” alishindwa kuendelea
akanirushia gazeti.
Nikaisoma ile habari.
Eti mke wangu alikuwa katika msafara wa kusafirisha maiti
yangu kuelekea mjini Morogoro, walipofika chalinze
wakapata ajali mbaya ambapo maiti ilipotelea katika
korongo na mke wangu akiumia vibaya kabla ya kupoteza
uhai!!
Mimi ni mwandishi, nikamshangaa mwandishi mwenzangu
aliyelishwa sumu na watu wabaya hadi akafikia kuunda
makala ile mbovu inayoenda kupotosha akili za watanzania
wote.
Nilitamani walau kumfahamu jina lakini nikakuta makala ile
imeitwa MAKALA MAALUMU ikiwa imeandikwa na
MWANDISHI WETU
Upuuzi kabisa!!!
Picha ya mke wangu ikanifanya niingiwe hasira maradufu
nan i wapi pa kuzishusha hasira hizi.
Nikaamua kumpigia simu mama yangu mzazi ili nijue ni nini
kinatokea. Niliomba sana awe peke yake ili aweze
kuzungumza name vyema.
Hakika alikuwa peke yake!!
“Sam weee!! Sam mwanangu, nilipokuzaa sikukuzaa uende
kuyafanya haya wanayokuandikia. Najua kuwa wanajaribu
tu kukuchafua.
Nitakuwa upande wako!! Si nilikuzaa kwa upasuaji na fomu
ikasainiwa kufa ama kupona. Basi ni hivyo hivyo nipo nawe
katika kufa ama kupona.
Eti watu wa dar es saalam wanadai waliuaga mwili wako,
wafanyakazi wenzako waliuaga mwili wako. Tena
wananipigia simu kwa kasi kweli wakinipa pole juu ya kifo
chako.
Nasemaje Sam, watakukana wote lakini mimi nitakusimamia
hadi mwisho..” hapa mama akasita kisha akacheka kidogo!!
Na akamalizia na kauli moja ya kishujaa lakini kama
anayesanifu.
“Eti maiti imepoteaaaa, walijua tu kuwa mama nd’o pekee
awezaye kumtambua mwanaye hata asipokuwa na kichwa!!
Kama wamemkamata akili huyo Edna wako ni huyo huyo,
kama na baba yako ulevi wake unamsahaulisha magumu
tuliyopitia ni yeye si mimi (kisha Akatukana kwa kikabila
chetu)” nikajua kuwa mama amakasirika katika kiwango cha
mwisho!!! Haikuwa kawaida yake kutokwa na matusi.
Nilishusha pumzi zangu na kupata ahueni, kuwa mama
yangu habadilishwi mawazo hata kidogo.
Jojina alikuwa amejikita katika jiko la gesi akiandaa chai, na
nilipomaliza kuzungumza na mama na yeye alikuwa ameketi
kitandani akiwa na kikombe cha chai.
“Sam, umezungukwa na watu wabaya tena wenye nguvu
sana. Yaani mtu anaunda ajali kama hii maksudi anaharibu
gari, anachonga jeneza ilimradi tu kukuchafua na kuunda
ukweli usiokuwepo!! Wanadamu wabaya sana, na ili
ufanikiwe lazima haya mambo yaende hatua kwa hatua
vinginevyoo!!!!!” aliishia hapo akanipatia chai, nikachemsha
tumbo!!
Nikiwa katika kunywa chai na kumkumbuka mke wangu
kipenzi, nikakumbwa na kumbukumbu juu yay ale mazingira
ambayo alipotea!! Nilipokumbuka kule dar es salaam
nikakumbuka kuwa wakati naona giza kuna kitu
niliona….hakika kuna kitu nilikiona.
“Mama lao, kuna kitu nilikiona wakati nazimia kama
usemavyo…yaani kuna kitu niliona jamanii..” nilimweleza
huku nikikifinyafinya kichwa changu kutafuta
kumbukumbu.
Aliniambia kuwa huenda ni katika usingizi mzito tu wa
kuzimia lakini nilikana, kipo kitu cha msingi niliona
waziwazi!!!
Nikatoka kitandani na kumwomba Mama lao anisimamishe
sehemu niliyokuwa mara ya mwisho kabla ya kuzimia.
Akafanya vile huku akicheka kimadaha, kanga yake moja
maungoni.
Nilipokuwa pale nikamwomba anielekeze pia namna
ambavyo nilianguka!! Alifanya kila nilichotaka.
Nikaenda hadi chini na hapo nikajikuta nikionana na kitu cha
kustaajabisha na kutisha kwa wakati ule.
Japokuwa ilikuwa picha lakini ilitisha kuitazama,
niliisogelea huku nikitetemeka.
Nikaiona picha ile inayotabasamu kama ambayo
inanikebehi. Nikaishika huku nikitetemeka.
“Jojina huyu ni nani kwa jina?” nilimuuliza huku nikiwa
nimeipakata ile picha katika viganja vya mikono yangu!!
Badala ya kunijibu alicheka kidogo. Nikashangaa maana
picha ile ilinitisha mimi lakini yeye hakuiogopa.
“Jojina usicheke huyu ni nani huyu?”
“Anaitwa Dulla, nimwite hayati Dulla, mwanaume wangu
nimpendaye akafa kabla…”
Sikumwacha amalize nikayaingilia maongezi.
”Jojina huyu hajafa, huyu na mwenzake mzungu walimteka
mke wangu…niamini mama lao..huyu hajafa. Dulla si mtu
mzuri niamini sijamfananisha hata kidogo. Dulaa kama ni
kweli anaitwa hivyo, kwa jicho langu nilimwona akimchukua
mke wangu! Kuna kitu Mama lao..” sasa ikawa zamu yake
kuchanganyikiwa. Macho yalimtoka pima ……….
Tukabaki kutazamana.
 
safi sana mzaramo naomba weka sehem nyingine ya kulalia
 
SEHEMU YA KUMI NA TATU
SOTE tulitazamana bila shaka kila mmoja akiwaza lake juu
ya kinachoendelea.
“Kwa hiyo baba alikuwa anasema ukweli juu ya Michigani
eeh!!” alijisemea nami nikamuunga mkono kuwa kuna
uwezekano mkubwa sana kuwa mzee wake alikuwa sahihi
juu ya ubaya wa Michigani japo hakuwa anaweza kuielezea
vizuri.
“Mwanangu Justin jamani. Kwa hiyo wamemuua ama?”
aliniuliza kana kwamba mimi ni wakala wa hiyo Michigani
na ninajua kila kitu. Sikumjibu kitu akaendelea kuzungumza
na nafsi yake!!
Nilitumia fursa hiyo kumweleza juu ya mazungumzo baina
yangu na mama. Nikamweleza ukweli juu ya namna
alivyopotea anitha, na nikafikia hatua ya kumweleza hata
zile picha alizonitumia Anitha kabla hajakamatwa na yeyote
yule ambaye mimi simfahamu.
“Picha ya mtoto?? Picha ya mtoto kama huyo usemaye
ilikuwa inapatikana maeneo fulani ndani ya Michigani, sasa
ukiniambia kuwa Anitha alikamatwa ama alipotelea eneo
hilo nashindwa kukuelewa maana miezi tisa iliyopita
Michigan iliteketea” Jojina alinijibu baada ya kumweleza juu
ya picha katika barua pepe aliyonitumia Anitha kabla
hajakamatwa na watu waliovaa suti nyeusi!! Wawili nyuma
yake na wawili mbele yake!!
Majibu ya Jojina yakasababisha jambo tunalolifanya liwe
kama mchezo wa maigizo usiojulikana wapi unaanzia na
wapi unapoishia.
“Kwa hiyo hapa mjini hakuna tena sehemu kama hii!!”
“Haipo kwakweli ujue sambusa zangu napeleka kila kona ya
mji lazima ningekuwa nafahamu picha hiyo!!” alinijibu kwa
kujiamini.
Hayo yakawa mazungumzo yetu ya mwisho kabla kimya
hakijatanda na kila mmoja kusinzia!!
****
Asubuhi nilikuwa nimeamka na wazo kichwani!!
Nikamshirikisha Jojina akanielewa bila shaka naye akaunga
mkono!!! Kwa sasa na yeye alikuwa mhanga katika mambo
niliyokuwa napitia, Jojina aliamini kuwa ni kweli mtoto
wake naye alichukuliwa katika tetesi za Michigani na
mazingaombwe yake.
Akaamua kuungana rasmi na mimi huenda njia nitakayopitia
inaweza kuwa suluhu yake pia.
Lililomhamasisha zaidi ni suala la mimi kumuona Dulla
ambaye alikuwa mpenzi wake akiwa hai!! Wakati alidhani
kuwa ni marehemu.
Majira ya saa moja asubuhi tulikuwa ndani ya basi kuelekea
mjini Morogoro!! Tulitaka kuwashuhudia hao viumbe ambao
walikuwa wakingojewa nyumbani kwetu kwa ajili ya kuuleta
mwili wangu tayari kwa maziko, mwili ambao unasadikika
kutokuwepo tena na sasa walikuwa wakija na taarifa tu
rasmi kwa wazazi wangu!!
Nilikuwa nimejivika kofia kubwa kama kawaida kuificha
sura yangu!!
Majira ya mchana tulikuwa Morogoro tukipata chakula
katika mgahawa usiokuwa na mlundikano wa watu!! Baada
ya hapo kwa mwendo wa miguu tukaanza kupita mtaa
mmoja hadi mwingine tukipatafuta kwa hadhari kubwa
nyumbani kwetu nilipozaliwa. Hapakuwa mbali sana
kutokea stendi ya Msamvu, hivyo ilituchukua dakika chache
tu kuwasili katika eneo lile.
Tuliukuta umati mkubwa ukiwa pale nyumbani, nilisikitika
sana kuona kuwa wale watu wote wamelishwa sumu na
kuamini kuwa mimi nimekufa na huku nikihusika na mauaji
na pia nikihusika katika kulawiti.
Lakini huenda umati ule ulijazwa zaidi na tukio la msafara
wa kuleta maiti yangu nyumbani kupata ajali na kisha mtu
mwingine kufa huku jeneza likiingia katika korongo na maiti
kutoweka.
Nilifanikiwa kuwaona watu wawili ambao nilikuwa
nafahamiana nao. Wote walikuwa waandishi wa habari!!
Nilijisikia kwenda kuwasalimia lakini hofu ya kujizulia
mambo magumu zaidi ikanikwamisha.
Jojina alikuwa makini kabisa kuangaza huku na kule, nia ya
kuja naye pale ni kupata uhakika iwapo hiyo Michigani ni
kweli inahusika na mikasa yote tunayopitia na tuliyopitia
ama Michigani ni kitu kingine.
Iwapo atamuona mtu yeyote ambaye awali aliwahi
kumwona Michigani nilimsihi anijuze kwa wakati ile tujue
nini cha kufanya.
Namba yangu ya simu ilikuwa nyingine tena na
aliyeitambua alikuwa ni Jojina pekee. Tulipoufikia umati
tukatengana, kila mmoja akaenda upande wake huku
tukipeana ahadi kuwa baadaye tutakutana kwa ajili ya
kupeana taarifa juu ya nani kaona nini.
Zaidi ya wale waandishi wa habari kadha wa kadha watu
wengine niliofanikiwa kuwaona ni ndugu wa karibu, lakini
wao hawakunitambua!!
Nililiona kundi la watu likimuhoji mama yangu, aina ya
nywele zao ilinipa majibu mara moja kuwa wale ni askari.
Mama alikuwa anafanya viapo mara kwa mara, bila shaka
kuna swali walikuwa wanamuuliza na kila alivyojibu
wanadhani anadanganya.
Swali gani jingine kama si juu yangu??
“SAA MBILI USIKU, GIRAFFE HOTELI CHUMBA NAMBA 18
NITAACHA WAZI INGIA KWA TAHADHARI KABATINI”
Ulikuwa ujumbe kutoka kwa Jojina. Nikausoma na kuuelewa.
Hoteli ile ilikuwa inajulikana sana hivyo sikuhangaika,
nikajihesabia mida hadi ukafika huo wakati. Roho ilikuwa
inadunda na kuhisi kusalitiwa lakini kwa sababu niliamua
kumuamini Jojina nilipiga konde moyo.
Nikaanza kwa kuupenyeza umati hapa na pale hadi nikafika
mahali mama yangu ameketi peke yake chini ya mti akilia
kwa maumivu makubwa!!
Nilimgusa begani akageuka lakini sikuifunua kofia.
“Mama mimi Sam, usionyeshe dalili za kushtuka!!!”
nilimwambia kwa utulivu, lakini kama kawaida ya wanawake
nimemsihi atulie yeye akasimama wima.
“Mamaaa!!” nilimsihi, akabonyea tena chini.
“Usijishughulishe na mimi wakati huu tunapoongea.” Kweli
akatazama mbele.
Nikamweleza kwa ufupi sana juu ya wakati ambao ninapitia,
nikamwomba aniombee sana kwa Mungu!! Sikumjibu
maswali yake yote, lakini nikamweleza kuwa naenda kulala
na siku inayofuata nitamtafuta tuzungumze.
Nikampatia mkono wangu, akajikumbushia mazoea yake ya
miaka nenda rudi!!
Akaubusu!!
Nikaondoka.
Muhudumu alikuwa anakula wakati mimi naingia pale ndani,
akajiweka sawa aweze kunisikiliza. Nikaulizia vyumba
akanieleza kuwa vipo, nikamsihi anipatie chumba upesi,
akafanya hivyo.
Baada ya malipo nikapewa funguo wangu !!!
Badala ya kwenda chumbani kwangu, nikaenda chumba
namba 18. Kweli nikalikuta kabati kubwa kabisa.
Nikafungua na kuingia ndani yake.
Nikajipekua na kukuta dhana zangu kadhaa nilizonunua
kabla ya kuingia pale zikiwa sawa.
Kisu kidogo na nyembe kadhaa kwa ajili ya kujilinda!! Iwapo
litatokea lolote.
Likakatika saa la kwanza lakini la pili halikukatika mara
wakaingia wanaume wanne mle ndani. Kupitia kitundu
kidogo nikawa nawatazama, kabati lilikuwa limefungwa kwa
ndani na funguo nikiwanayo mimi.
“Huyu mwanamke kumbe aliacha wazi, yukwapi kwani?”
“Analewa huko nimemwacha!!” ilijibu sauti nene kutoka kwa
mtu mwenye kipara, sikuweza kuwaona vyema.
Waliketi na kuanza mazungumzo palepale.
Mwongeaji mkuu akiwa mwenye kipara!!
“Dulla eeh huu ujio wa ghafla ni kwako mshkaji wetu, na
ishu ni moja tu, wanawake Dulla angalia wasije
wakakuponza tena, huyu mwanamke huyu we unadai
anakufahamu sijui, angalia Dulla wasije majamaa wakakutoa
muhanga. Si unajua huyo ----- mwandishi amemvuruga
kabisa bosi sasa hivi na haoni hatari kuua. Sasa wewe
endekeza mambo ya wanawake halafu mwisho
wakuchomeshe jamaa akumalize. Usije ukasema
hatukukwambia, kama unaona tunaingilia uhuru wako Dulla
sawa lakini kama unajipenda acha hizi mambo.”
Alizungumza kwa sauti ya chini wenzake wawili wakawa
wanatikisa vichwa kukubaliana naye.
“Yaani ipo hivi sawa huyu mwanamke hatoki humu ndani,
nd’o mwisho wake sifanyi ujinga tena kama wakati ule wa
Michigani ya juu ile.” Aliposema kauli hii vicheko vikatawala
kisha maongezi ya hapa na pale. Kabla yule msemaji
hajaingiza maongezi mengine.
“Hivi huyu ----- wa kujiita mwandishi hajui kuwa atakufa
kifo kibaya sana akicheza. Yaani angezijua hasira za jamaa
dah bora hata ajinyonge kuliko kuingia mikononi mwa
bonge waiti.” Alisema kwa masikitiko bwana mwenye
kipara, kisha akainama na hapo nikaweza kumwona Dulla.
Alikuwa ni yuleyule mtekaji wa mke wangu.
“Mkewe anaipata suluba aisee hadi huruma. Halafu yule
msaidizi akajifanya kumtetea siku ile kaambulia vinao na
matusi, Bonge waiti ni habari nyingine jamani.” Dulla
alizungumza, na baada nya hapo ikasikika hodi mlangoni.
Sauti ya kilevi.
“Oya Malaya wako huyo, hakikisha unafanya
tulivyozungumza Dulla. Anakujua sana huyu demu.” Kipara
alimnong’oneza Dulla na maneno yale yakaonekana
kumuingia.
Mlango ukafunguliwa, wale mabwana watatu wakatoka nje
na ndani akabaki Dulla, kisha akaingia mama lao. Alikuwa
amelewa chakari kimtazamo, aliyumbayumba huku akiimba
nyimbo anazozijua yeye mwenyewe. Niliendelea kuyatazama
haya yanayoendelea huku nikijiuliza juu ya Michigani na
mkasa unaoendelea.
Bonge waiti!! Huyu ni nani katika mlolongo huu wa
kustaajabisha!!
Taa haikuzimwa na jicho langu likaendelea kushuhudia
mambo machafu kusimulia kati ya Dulla na Jojina. Lakini
nililazimika kutazama huku nikichukua tahadhari nisije
kugusa chochote kile ambacho kinaweza kutibua mipango
yetu.
Ni vyema kuwa niliendelea tu kutazama kinachoendelea,
maana ningeacha na kuona aibu huenda lingetokea baya na
kisha nikajutia muda wangu!!
“Jojina, ujue nakupenda sana.”
“We wala hunipendi na kama unanipenda mbona
ulinikimbia.” Alijibu Jojina kilevilevi.
Dulla akamtazama yule mwanamama jinsi anavyosinzia na
hapo nikamuona akichukua mto, akawa anasitasita lakini
hatimaye akaushusha na kuufunika uso wa Jojina kisha
akaukandamiza.
“Jojina lazima ufe ili niendelee kuishi kwa amani nisamehe…
nisamehe inanibidi tu kukuua kabla mimi sijauwawa.”
Alisema huku akiwa anauma meno yake.
Akili ikafanya kazi harakaharaka, mikono ikiwa inatetemeka
nikauzungusha funguo, na kisha kulikanyaga kabati kwa
nguvu. Dull hakujiandaa kuupokea mshtuko huo, akaacha
mara moja kile alichokuwa anafanya na sasa akawa
anatazamana moja kwa moja na mtu ambaye yeye binafsi
anaamini kuwa ni dhaifu na huenda alijinyonga tayari.
Mama lao alikuwa akihema kwa nguvu huku akikohoa bila
kikomo.
Sikumpa nafasi ya kuzubaa zaidi, nikajirusha na kumkaba
huku nikivuta picha ya mke wangu na mwanangu mpenzi.
“Wewe wewe!!” alianza kunisonta kwa kidole chake. Lakini
sikutishika nikajivuta nyuma na kumwangushia kichwa
kimoja, akatokwqa na yowe la uchungu, nikataka kumpiga
ngumi lakini akaniwahi akanikanyaga teke la tumboni.
Kisha zikafululiza ngumi mbili tatu, nikaanza kuona
mawenge!!
Lakini zile zikawa ngumi za mwisho. Ikajha ile sababu ya
muhimu kabisa niliyokuwa naingoja ya Jojina kuitwa mama
lao!!
Nikiwa chini nikamuoa akimnyanyua Dulla juu juu. Kisha
akamnasa vibao kama mtoto mdogo, na mkong’oto
uliofuata pale ni yeye pekee anaweza kusimulia maumivu
iwapo angepata nafasi ya kusimulia.
Lakini hakupata nafasi hiyo!!
“Justin yuko wapi?” aliuliza kwa jazba huku akiwa
amemuunganisha Dulla mikono yake vyema.
Mama lao alikuwa mama kweli!!
Dulla akaanza kujiumauma, mama Lao akamweka sawa
kisha akatuliza kisigino chake katika korodani za Dulla.
Yowe likamtoka na mimi nikasisimka.
“Unasema ama husemi wewe mpumbavu.” Alifoka mama
lao.
“Sijui alipo sijui chochote dear, mimi ni kibaraka tu
nisamehe…”
“Kwanza koma kuniita dear, wewe kibaraka wa nani?”
“Bonge…bonge waiti…..”
“Nd’o nani na yupo wapi na ni shughuli gani mnajihusisha
nayo?” alimbana swali.
Dulla badala ya kujibu akajitoa katika himaya ya Jojina na
kujaribu kujitetea huku na kule.
Jojina alikuwa macho haswa, mimi binafsi sikujua
nimekidondosha kile kisu muda gani lakini yeye alikikwapua
kutoka kilipokuwa, Dulla akajikuta akigumia kwa maumivu,
kisu kikiwa kimezamishwa mgongoni!!
“Hivi unajifanya umafia wangu umeusahau eeh!!” sasa
alizungumza huku akikizungusha kile kisu kama
akayechokonoa.
Mama lao alikuwa katili haswa!!
Dulla alikuwa anapiga kelele lakini zote ziliishia katika
kiganja cha mama lao. Alikuwa amemziba vyema.
Maumivu aliyokuwa akiyapata hata wewe unaweza tu
kuyakadiria!!
Mashuka yalikuwa yanazidi kuwa mekundu na mama lao
hakujali hayo. Sura yake ilikuwa imechafuka kwa ndita
zilizotangaza hasira.
“Justin mtoto wangu yupo wapi?” aliuliza tena kisha
akamwacha Dulla azungumze.
Lakini hakuzungumza na badala yake alianguka na kupoteza
fahamu!!!
“Bwege atatiharibnia akizinduka shenzi kabisa anazo picha
zangu niliwahi kumpa.” Alisema Jojina kisha akafanya
nisichotarajia.
Akazamisha kisu katika upande wa moyo wa Dulla.
“Kalale kwenye moto wa jehanamu muuaji mkubwa wewe.”
Alisema kwa hasira. Kisha akasimama kitandani akavua
nguo zake zote zilizolowana damu.
Akauendea mkoba wake akachukua nguo nyingine akavaa.
“Twen’zetu!!” alisema na hapo tukatoka nje.
Jojina akiyumba kama mlevi!!! Na hapo nikapata jibu kuwa
kumbe hakuwa amelewa bali alikuwa mtaalamu katika
kuigiza.
Nilimtazama kwa wasiwasiu mkubwa, sikujua kama
anaweza kuwa jasiri kiasi hiki mwanamama huyo.
Alimpataje Dulla? Na alimshawishi vipi hadi kumuamini
tena??
Hayo yalikuwa maswali niliyotarajia kumuuliza tukishafika
nje ama kwenda popote pale na kuwa huru!!!
“Sam, najua unajiuliza tunaanzia wapi eeh!! Usijali mpenzi
wangu, mimi naifahamu Iringa vyema. Na kama kweli kuna
kitu kibaya huko michigani nitajua tu!! Nakuhakikishia kuwa
kama mwanangu mimi Justin, mwanao, mkeo, na Anitha
wako salama basi watatoka salama. Hukuwahi kujua
kwanini naitwa mama lao, lakini utajua hatua kwa hatua…”
aliniambia huku akinibinyabinya kiganja cha mkono wangu
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE
Jojina akiyumba kama mlevi!!! Na hapo nikapata jibu kuwa
kumbe hakuwa amelewa bali alikuwa mtaalamu katika
kuigiza.
Nilimtazama kwa wasiwasiu mkubwa, sikujua kama
anaweza kuwa jasiri kiasi hiki mwanamama huyo.
Alimpataje Dulla? Na alimshawishi vipi hadi kumuamini
tena??
Hayo yalikuwa maswali niliyotarajia kumuuliza tukishafika
nje ama kwenda popote pale na kuwa huru!!!
“Sam, najua unajiuliza tunaanzia wapi eeh!! Usijali mpenzi
wangu, mimi naifahamu Iringa vyema. Na kama kweli kuna
kitu kibaya huko michigani nitajua tu!! Nakuhakikishia kuwa
kama mwanangu mimi Justin, mwanao, mkeo, na Anitha
wako salama basi watatoka salama. Hukuwahi kujua
kwanini naitwa mama lao, lakini utajua hatua kwa hatua…”
aliniambia huku akinibinyabinya kiganja cha mkono wangu
&**JIFUNZE: Hakuna mwanamke aliyehifadhi tumboni
mwake, Malaya, jambazi ama muuaji.. kwa miezi tisa kisha
akamzaa.
Mazingira nd’o huzaa tabia hizi, mwanadamu huongozwa na
mazingira na nyakati. Katika maisha yetu kuna nyakati
zinakuja na kutulazimisha kusema uongo ilimradi tu
kukomboa kitu flani, na zinakuja nyakati za hasira na chuki
na kutusukumia dhambini.
Ni kumwomba mungu tu atupe mioyo ya ujasiri sana!!!
Nilibaki katika mshangao kwa muda nikiendelea kujiuliza
yule mwanamke ni wa aina gani. Awali nilidhani kuwa ni
msema sana tu kutokana na haiba aliyoionyesha siku
tulivyosafiri naye kutokea jijini Dar es salaam, mara ya pili
tukakutana naye akiwa anauza sambusa na bajia, hapa
akazidi kunishangaza lakini ninazidi kumfahamu.
Sasa namtambua kama mama lao!!
Hakika alikuwa mama lao!!
“Mabwege wamelewa wale hawajui kama mwenzao kajifia
huko ndani shenzi kabisa!!!” Jojina alizungumza kama
anayesema mwenyewe, nikageuza shingo na kuwaona wale
jamaa waliovaa suti waliokuwa wakimsihi Dulla amuue
Jojina. Kulingana na mavazi aliyokuwa amevaa Jojina,
mavazi tofauti kabisa na yale aliyokuwa amevaa awali,
ilikuwa ngumu kwa mtu yeyote kuweza kumtambua. Kasoro
mimi tu!!
“Sam, umeyaokoa maisha yangu! Sikutarajia kama
ungeweza kushawishiwa na ujumbe ule mfupi niliokutumia
ukajileta kichwa kichwa katika chumba kile!! Vipi
tungekuwa tumepanga kukuua labda, ama vipi
ungegundulika kuwa upo ndani ya chumba kile!!
Umekuwa jasiri sana kujileta katika mdomo wa kifo bila
hofu. Na sit u kujileta katika mdomo wa kifo, bado ulikuwa
jasiri ulipoona yule bwana anataka kuniua hukuvumilia
ukatoka ndani ya maficho na kumkabili. Ni wanadamu
wachache sana wawezao kujihatarishia maisha yao kama
wewe ulivyofanya.” Jojina alikuwa akininong’oneza kwa
sauti ya chini huku akinivutia katika kifua chake. Tulikuwa
nyumba ya kulala wageni tayari.
Nilimjibu kizembezembe huku nikijifanya usingizi
umenitawala, nikambusu midomo yake kisha nikageukia
upande wa pili nikimwacha jojina akipitisha mikono yake
kutokea mgongoni mwangu na kisha kuiunganisha kwa
mbele!! Akanikumbatia.
****
ASUBUHI majira ya saa nne, tulikiachia chumba. Mama lao
akiwa amevaa kama alivyokuwa amevaa usiku uliopita huku
mimi nikiwa nimebadili na kuvaa kaptula na fulana kubwa,
kichwani nikiwa na kofia kama ilivyo kawaida tangu niingie
matatani.
Safari yetu ilikuwa ya kuvizia maeneo ya nyumbani kwetu ili
tuweze kujua ni kitu gani kinachoendelea, tulitambua fika
kuwa lazima taarifa juu ya kifo cha Dulla zilikuwa
zinafahamika kwa wenzake na kama kuna lolote litakuwa
limeendelea basi mwanzo wake ni pale msibani.
Tuukuta umati mkubwa tofauti na siku ya kwanza, jambo
hili halikuwa la kawaida hata kidogo, ni kweli msiba huu
ulikuwa na utata ndani yake lakini haukuwa utata wa
kuvuta umati mkubwa kiasi kile.
Tukajichanganya katika makundi kwa tahadhari kubwa!!
Jojina alikuwa wa kwanza kuchezwa machale, akiwa
amevalia wigi kichwani lililombadili sura yake alinivuta
katika kundi fulani kisha tukawapa migongo kama hatuna
habari nao.
“Hawa polisi walichofanya ni uonevu, haiwezekani mara
amekufa mara msafara umepata ajali, sasa wanasema sijui
kuna wadau wake mama yake anawajua??? Huu ushenzi
huu!! Mama ambaye hata Dar hajawahi kwenda anajua nini
sasa.” Alilalamika bwana mmoja, nikageuka kumtazama
sura ilikuwa ngeni.
“We! Bora tu unyamaze maana hii serikali yetu hii
ukionekana tu unatetea jambo basi. Chanzo eti jana pale
mazikoni mama amekataa kata kata kuwa mtoto wake ajafa
na siku ile usiku alipopiga mayowe kuwa ameisikia sauti ya
mwanaye. Hapo tu nd’o tatizo likaanzia siku aliyodai kuwa
amemsikia kesho yuake nadhani nd’o ikatokea ajali. Kwanini
serikali isikubane isitoshe huyu mwenyekiti wa mtaa ana
chuki binafsi na familia ya marehemu.” Alinong’ona kijana
mwingine na yeye sikuwa nikimfahamu. Maongezi yao
yakanipa mwanga kuwa mama yangu alikuwa matatani.
“Sam…jikaze usipaniki utaharibu!!” Jojina aliwahi kugundua
azma yangu maana kuna chembechembe za wazimu zilianza
kunipanda kichwani na kujisikia nikikabiliwa na mzimu wa
lolote na liwe. Ni heri Jojina aliniwahi kisha akanishika
mkono na kunitoa mahali hapo.
Mama yangu alikuwa kila kitu kwangu!! Almanusura
nimponyoke Jojina na kukimbia lakini ukakamavu wake
aliweza kunihimili, sikuweza kufanya lolote.
“Sam, unatakiwa utambue kitu kimoja. Tupo katika
mapambano ambayo hakuna ajuaye tunapambana. Hatuna
msaada na jeshi letu linazidi kuporomoka, ameondoka
Anitha, Mama Eva, Mzee Matata sijui, sasa ameondoka
mama, ukiiruhusu akili yako kujikita katika wazimu basi
ujue kuwa nitabaki peke yangu!! Siwezi kupambana peke
yangu Sam siwezi hata kidogo, wewe ukiharibu tu tambua
kuwa utajikuta umefungwa kamba wewe, Anitha, mama,
Eva, mama Eva na mimi pia halafu nani wa kumfungua
mwenzake, ama nd’o unataka kuanza kumlilia Mungu ilihali
amesema jisaidie nami nitakusaidia, unataka kujiingiza
katika janga maksudiu. Janga ambalo mwanga wake
tumeanza kuuona, tunatambua kuwa kuna Michigani,
tunajua kuhusu Anti Ezekiel kiasi fulani, tunalo la kusema
kuhusiana na kindo. Halafu wewe unataka kuharibu.
Sam kwa jinsi walivyokusaka kwa muda mrefu nadhani
unajua kuwa wakikukamata ……wakikukamata Sam. Si
umezikwa kiuongouongo, wale watakuzika kweli. Mbaya
zaidi Sam, hawa watu akina Bonge waiti wanaonekana
kukubalika samba serikalini kwa lolote lile
wanalodanganya. Sam unatakiwa kuwa imara, ni mimi na
wewe iwapo hatatokea mwingine wa kutuunga mkono
tunalo jukumu la kumwokoa mama, Eva, mama Eva, Justin
kama yupo hai mwanangu, Anitha na wengine wote wenye
haki.” Jojina alinieleza haya kwa hisia kali. Kila mstari wa
neno lake ulikuwa ni fimbo inayoumiza, aliusema ukweli
mtupu. Nikapepesa macho nisitazamane naye usoni lakini
yeye alizidi kunikazima macho ili maneno yaniingie.
Jojina!! Jojina alikuwa Anitha mwingine!!
“Nimekuelewa sana dada yangu!!” niliamua kukubali yaishe.
“Tunaondoka dakika hii kuelekea Iringa ama popote pale
lakini sasa hivi tunaondoka tukiwa na lengo moja tu
kuitafuta Michigani popote ilipo, kumtafuta Bonge waiti
kama kweli yupo, tunaondoka kwenda kuisaka amani!!!”
alizungumza katika namna ya kuamrisha sasa hakunitazama
machoni.
Nikatii!!
Tukaongozana mpaka stendi, bahati nzuri magari ya
kuanzia safari Morogoro kwenda Iringa yalikuwepo mengi
tu.
Tukaingia katika basi lililokuwa linakaribia kuondoka!!
Dakika kumi baadaye likaanza safari. Tulikuwa tumepata
siti mbili za mwisho nyuma kabisa!!
Hatukujali kuhusu hilo. Kama kawaida tukaandikisha majina
ya kughushi!!
Kimya kilitanda, hatukusemezana chochote kile. Kwa
takribani dakika thelathini, sijui Jojina alikuwa anafikiria
nini, lakini mimi nilikuwa nawaza juu ya Kusadikika iitwayo
Michigani, mahali palipovunjwa na kuteketezwa sasa
tunapatafuta, nikamuwaza pia Ezekiel wakati huu
nikimfananisha na mzimu wa ajabu uliojileta katika maisha
yangu!!
Ezekiel! Ezekiel asiyejulikana! Aidha yu hai ama amekufa.
Dakika chache baadaye gari likasimama na kuegesha
pembeni.
“Kuchimba dawa mapema hivi!!” hatimaye Jojina akatokwa
na neno la kwanza.
“Vibofu havifanani aisee.” Nikamjibu kiutani, akatabasamu.
Lile tabasamu halikudumu sana, akataka kusema neno lakini
akaishia kutanua tu mdomo na asiseme chochote.
Sikujua nini kimemsibu.
Baada ya sekunde kadhaa sikuwa na haja ya kuuliza tena
kulikoni!!
“Iwapo unajua kuwa umeandikisha jina lisilokuwa lako
katika tiketi yako, jisalimishe mapema kabla
haujapekuliwa!! Narudia tena, iwapo unajua umeandikisha
jina lisilokuwa lako katika tiketi uliyonayo tafadhali ndugu
jisalimishe mapema nje ya basi kabla upekuzi haujaanza!!”
sauti kali ya kiaskari iliamrisha.
Jojina alijisajiri kama Prisca na mimi nilijisajiri kama Rama.
Majina feki!! Mungu wangu!! Kuna nini tena?
Nilimtazama Jojina alikuwa akijaribu kujificha asionekane
kama anayeshangaa, lakini macho yangu yalipotua katika
kifua chake niliweza kushuhudia jinsi moyo wake
ulivyokuwa unadunda kwa kasi.
Sote tulikuwa tumepagawa, hasahasa mimi ambaye sura
yangu ilikuwa takribani katika magazeti yote nchini. Vipi
wakiniona hawa maaskari. Bila shaka nd’o safari ya jela na
kifo moja kwa moja.
“Sam, zama chini zama wajinga watakagua, ingia
nitakufukina na sketi yangu fanya fasta.” Jojina
alininong’oneza. Sikungoja zaidi maana kama ni hatari
tayari tulikuwa hatarini.
Nikazama chini wakati abiria wengine wakiwashangaa
askari waliokuwa wakitoa lile tangzo na wengine
wakijishughulisha katika kujisalimisha mbele.
Nikajibana na hatimaye Jojina akatanua miguu nikawa chini
ya himaya ya miguu yake miwili, joto kali likanitoa jasho
lakini bora joto, jinsi nilivyojibana chini ya viti vile niliumia
sana mgongo!! Miguu ya Jojina ilikuwa inatetemeka haswa.
Tulikuwa matatani!!
“Wanakagua tiketi Sam. Omba Mungu sana” Jojina aliinama
na kunong’ona nikamsikia lakini sikujibu, akazidi
kutetemeka.
Zikapita dakika kadhaa akanong’ona tena.
“Sam wanayo picha sijui ni picha ya nani, hawakagui tiketi
mafala hawa wanakagua sura Sam. Ni hatari Sam” Jojina
akazidi kunitia hofu.
Niliendekea kudumu katika hali ile bila kujitingisha wala
kukohoa. Hofu niliyokuwanayo katika mazingira haya
ilikuwa mara kumi ya hofu ya siku moja iliyopita nilipokuwa
kabatini nikiwasubiri akina Dulla, na hofu hii ilizidi ile hofu
ya kumuona Jojina akiua mtu.
Wakati naitafakari hali inayonikabiri nmara nikaisikia sauti
ya Jojina tena, safari hii ilizungumza kwa uoga zaidi.
“Sam…tumekwisha….mafala wana picha yangu aisee kumbe
wananitafuta mimi!! Jiweke safi Sali sala zako za mwisho,
wanatuua hawa!! Hawatuachi Sam”
Kauli hii haikuwa kavu, iliambatana na mkojo!!
Yule mwanamama jasiri alikuwa anajikojolea, ule mkojo wa
moto kutoka kwa Jojina ukatua vyema katika uso wangu!!
Nikataka kujitikisa lakini nikahofia kuharibu zaidi.
Hakika Jojina alikuwa ameogopa sana.
Na kama alivyosema kuwa tumekwisha ni kweli alimaanisha,
maana jasiri akifikia hatua ya kujikojolea basi ujue
amenyanyua mikono juu…
 
SEHEMU YA KUMI NA TANO
ILIPOISHIA
. . “Sam wanayo picha sijui ni picha ya nani, hawakagui
tiketi mafala hawa wanakagua sura Sam. Ni hatari Sam”
Jojina akazidi kunitia hofu.
. . Niliendekea kudumu katika hali ile bila kujitingisha wala
kukohoa. Hofu niliyokuwanayo katika mazingira haya
ilikuwa mara kumi ya hofu ya siku moja iliyopita nilipokuwa
kabatini nikiwasubiri akina Dulla, na hofu hii ilizidi ile hofu
ya kumuona Jojina akiua mtu.
. . Wakati naitafakari hali inayonikabiri nmara nikaisikia
sauti ya Jojina tena, safari hii ilizungumza kwa uoga zaidi.
. . “Sam…tumekwisha….mafala wana picha yangu aisee
kumbe wananitafuta mimi!! Jiweke safi Sali sala zako za
mwisho, wanatuua hawa!! Hawatuachi Sam”
. . Kauli hii haikuwa kavu, iliambatana na mkojo!!
. . Yule mwanamama jasiri alikuwa anajikojolea, ule mkojo
wa moto kutoka kwa Jojina ukatua vyema katika uso
wangu!! Nikataka kujitikisa lakini nikahofia kuharibu zaidi.
. . Hakika Jojina alikuwa ameogopa sana.
. . Na kama alivyosema kuwa tumekwisha ni kweli
alimaanisha, maana jasiri akifikia hatua ya kujikojolea basi
ujue amenyanyua mikono juu…
. . ***KUMBUKA!! MUNGU alitumia ubunifu wa hali ya juu
sana kuliko ubunifu wowote uliowahi kutokea popote pale,
kipindi anamuumba mwanadamu. Alimpa kila kitu, lakini
akamnyima uwezo wa kujua nini kitatokea katika sekunde
moja ijayo mbele yetu.
. . Kwa sababu hatujui lijalo, ni vyema kujiweka tayari kila
muda ikiwa hatujui siku wala saa!!!
. . ENDELEA
. . Sikukarahishwa na ile mikojo ya mama lao badala yake
fikra zangu ziligandiana maneno ya Jojina ambaye n’do
alikuwa shuhuda wa kila kinachoendelea.
. . Alikuwa amekiri kuwa hatuna ujanja na tumekamatika.
Niliisikia na kuiona vyema mikono yangu jinsi ilivyokuwa
ikitetemeka, nilijaribu kujiimarisha lakini sikuweza.
. . “Wewe kaza uso wako nitazame!!!” niliisikia sauti ya
askari ikiamrisha, Jojina akazidi kutetemeka, sasa hakuwa
akijikojolea tena, bila shaka mikojo ilijiishia katika kibofu!! .
.Mimi ndo nilikuwa kwenye mashaka zaidi.
. . Niliiona miguu ya yule askari ikiwa imesimama imara
mbele ya siti ya mwisho kabisa, bila shaka alikuwa
akiwakagua akina Jojina.
. . Niliusikia mkono wa Jojina ulishuka kwa kasi na kuanza
kunipapasa, alinishika sikio mara anishike kichwa!!
Nikajiuliza kulikoni na bado sikufanya jitihada za kumzuia
asinipapase. Sikujua anachokihitaji ni kipi. Mara akanishika
pua na hatimaye akapanda juu kidogo akainyofoa miwani
katika macho yangu.
. . Nilistaajabu nisijue kama hii ni hofu inasababisha ama ni
kipi kinamsibu mwanamama huyu!! Nilikuwa namwomba
Mungu afanye muujiza wowote ule na ile iwe ndoto. Tatizo
ni moja tu!
. . Mungu hapangiwi kazi!! Yeye huombwa tu. Nami
nikalazimika kuomba huku nikitarajia majibu ya haraka
haraka.
. . Hatimaye miguu ile ikageukia upande aliokuwa ameketi
Jojina. Hofu ikaongezeka maradufu.
. . “Kwani kuna nini hapa jamani!!!” nniliisikia sauti ya Jojina,
sikujua anamuuliza nani.,
. . “Tiketi yako ipo wapi mwanamke??” sauti kali ya kiaskari
ilijibu.
. . “Tiketi…tiketi yangu mimi….. Joshua, we Joshua….. mpe
kondakta tiketi yake.” Jojina alijibu nikabaki kuduwaa kule
chini nisijue nini kinaendelea baina yao.
. . Jojina aliendelea kusema maneno maneno, bila shaka
aliyajua mwenyewe mimi nikabaki katika fumbo!!!
. . Kimya kikatanda, nikamsikia yule askari akisonya na mara
akageuza na kuondoka zake. Nilistaajabishwa sana na
muujiza huo.
. . “Usitoke…vumilia huko huko!!!” alinong’ona Jojina, nami
nikajizi kujikaza. Gari likawashwa!! Safari ikaendelea na kile
kilichotokea kikabaki kuwa cha kutetwa ndani ya basi.
Baada ya dakika kadhaa Jojina aliniruhusu nitoke kule chini,
hii ni baada ya abiria kadhaa kuwa wameuchapa usingizi
wasijue kama nilitokea kule chini.
. . “Jojina umewalaghai kitu gani wewe mwanamke!!”
nilimuhoji kwa sauti ya chini.
Akaanza kwa tabasamu kisha akanieleza kitu kilichonifanya
niamini kuwa si lazima uende shule ndipo uwe na uwezo
mkubwa wa kimaamuzi kama wa mama lao.
. . “Yaani nilikuwa najua kuwa sitaweza kuchomoka hapa,
yaani kitu nilikuwa nimesahau ni kwamba Dulla huwa ana
picha zangu tena nyingi tu, na wale jamaa waliniona
nikiwanaye na mbaya zaidi aliwatambulisha kwangu. Hivyo
ule mzoga kwa namna yoyote ile lazima skendo za kuua
ziwe juu yangu. Sasa nikajibweteka kimawazo nikiaqmini ni
wewe wanakusaka. Alikuwa pale hivi siti ya nne nd’o
nikaiona picha, wacha nichachawe mtu mzima!! Yaani
nikajua tumekwisha. Aliponikaribia zaidi nikaamua kama ni
kufaacha nife kishujaa, ndo pale nikakupapasa nikakutoa
miwani yako harakaharaka nikaitundika katika uso wangu.
Aliponifikia nikaanza kujisemesha, jamaa akaniondoa
miwani, aisee kitu nilichofanya najua mwenyewe,
nikabenjua macho yangu, hii bolti nyeusi ikapotea ikabaki
hii nyeupe, hii michezo naijua sana tangu zamani, wakati
nabenjua nilikuwa napapasa huku na kule na mara
nimkamate mkono, mara nimshike kifua. Nadhani unajua
kilichotokea hapo, wasafiri bila kutumia aki;li wakaanza
kukoroma kuwa mimi sina uwezo wa kuona tena wakitumia
lile neno kali kabisa, kipofu!! Askari akaishiwa hamu,
akanirejeshea miwani yangu machoni, nikayaweka macho
yangu sawa na kumwona jinsi alivyokuwa na wasiwasi.
Lakini nadhani ile picha nikiwa na kipara na uhalisia huu
nikiwa na wigi umemwacha hoi. Kipofu mwenye wigi, wakati
picha ni mtu anayeona akiwa na kipara.
. . Akasonya na kuondoka zake!! Sam siamini hata kidogo
kama…….” Akasita kuzungumza, akaniegemea na
kunong’ona, “kuna ----- anatuchora….” Aliniambia na
kisha akanionya kuwa nisifanye jitihada zozote za kupepesa
macho.
. . “Pita upesai nenda kamwombe kondakta,,, mwambie
ninaumwa tumbo….pameharibika Sam hapa nenda haraka.”
Akanisihi, upesi nikasimama na kupita nikafanya hima na
kumfikia kondakta. Nikamsihi kama nilivyoelekezwa,
nikalalamika sana juu ya mgonjwa wangu asiyeweza kuona
anaumwa tumbo.
. . Kondakta akanielewa, nikarejea na kumchukua Jojina
katika namna ileile ya kumwongoza mimi mbele yeye
nyuma, akiigiza kuwa hana uwezo wa kuona. Wakati huu
niliweza kumtilia mashaka yule mtu ambaye Jojina alidai
kuwa hana nia nzuri, nilimwona akinong’ona na mwenzake.
Nikajifanya sijui lolote linaloendelea.
. . Tulipoufikia mlango mimi nikiwa mbele kama kawaida
mara tukasikia sauti kali ikiamrisha.
. . “Ninakutilia mashaka wewe mama usiyeweza kuona.
Simama hapo hapo ulipo!! Nayaongea haya kwa mamlaka
niliyopewa na jeshi la polisi Tanzania.” Niliskia miguu
ikiishiwa nguvu, nikaanza kutetemeka. Lakini haikuwa hivyo
kwa mama lao.
Ghafla akanisukuma nikatangulia nje.
. . “Saaaam poteaaaaa!!!” ndo neno pekee alilotoa, akatupa
miwani huko, akaikunja sketi yake. Akili ikafanya kazi
vyema sikulemaa, mwanamama anakimbia sijapata kuona,
kumbe ule unene ni gelesha tu.
Nikaanza kufuata nyuma, huku nyuma zikawa zinasikika
kelele za abiria. Yule askari sikuisikia sauti yake. Na niisikie
ili iweje tena.
. . Nikapenya kila alipopita Jojina, mimi nyuma.
. . “Simama la sivyo nafyatua risasi!!!” ilisikika sauti kwa
mbali, almanusura nisimame kama yasingekuwa maneno ya
Jojina.
. . “Sam usisimame hakuna kitu hapo Sam kimbia.”
Alinisisitiza pasipo kugeuka nyuma. Maneno yake yakanitia
wazimu wa kukimbia nikakazana zaidi. Hakika hatukujua ni
wapi tunakwenda!!
. . Taratibu nilianza kuchoka, na bado nilisikia vishindo kwa
nyuma. Jojina alikuwa ameniacha tayari na vile tulikuwa
tukipenya katika majani sikuweza kumwona kabisa. Hofu
ikaanza kutanda, dalili za kukata tamaa zikanikumba.
. . “Jojinaaa…..Jojinaaa..” nilianza kuita lakini sikujibiwa.
. . “Simama kimburu Kenge, shenzi kabisa simama.” Sauti
iliamrisha kwa nyuma. Nilikuwa nimechoka, nikasikia miguu
ikigongwa kwa nyuma, nikayumbayumba kisha kama mzigo
nikatua chini.
. . Meno yangu yakauma nyasi!!! Nikajitahidi kugeuka
nikakutana na mwanaume akiwa ameshikilia pingu. Alikuwa
anahema juu juu, ni yuleyule mwanaume ambaye
tulikuwanaye ndani ya gari. Alikuwa ananitazama kwa jicho
kali.
. . “Shetani mkubwa!!!” nikasikia sauti nyingine ikasikika
ikitokea katika majani!!! Mimi na yule mwanaume mwenye
pingu tukatahamaki, lakini hatukudumu sana mara yule
mwanaume akaaguka chini akijishika kichwa, nikaona jiwe
kubwa pembeni yake. Na hapo akatokea yule mama
aliyejikojolea ndani ya gari.
. . Jojina kwa mara nyingine!!!
. . “Mshenzi mkubwa wewe ukipona nenda kamweleze mkuu
wako wa kazi kuwa kuna watu wabaya anawafuga huko.”
Alikoroma mama lao. Lakini huyo mtu aliyepewa nafasi ya
kupona akataka kuleta ujanja, ambao Jojina aliutegemea
kumbe, akasimama na kurusha teke, mama lao akaingiza
mkono wake katika sketi yake, akatoka na jiwe jingine
kazuga kama analirusha yule askari akajificha kwa kutumia
mikono miwili huku akiruka kando.
. . Jojina akatabasamu wakati yule bwana anaitoa kinga
yake usoni, hapohapo akalivurumisha lile jiwe.
. . Nilibahatika kuona meno kadhaa yakitoka katika kinywa
cha yule bwana. Kufikia hapo mama lao hakuwa akizuilika.
. . “Auaye kwa upanga……” alisema huku akitua juu ya mwili
wa yule bwana anayevuja damu, “Atauwawa kwa upange
vilevile” akamalizia huku akiishika ile pingu na kuanza
kumcharaza nayo yule bwana usoni.
. . Kila alipoituliza paliumuka kisha damu!!
. . Akapiga kwenye taya, akapiga paji la uso!! Akapiga kila
kona!!!
. . Kisha mbio zikaendelea. Kidogo nilikuwa nimepumzika.
Nikaweza kukimbia zaidi, wakati huu tukiwa sambamba na
mama lao Jojina.
. . “Niliwahi kuwa mwanariadha shule!!” alisema bila
kunitazama.
. . Sikumjibu.
. . Hapakuwa na mtu anayetufuatilia kwa nyuma!!!
. . “Hivi unajua tunapoelekea lakini?” Jojina aliniuliza, hapo
tukajikuta tunapunguza mwendo taratibu huku kila mmoja
akikumbwa na kiwewe.
. . “Hata sijui ndugu ujanja wangu mimi Morogoro mjini tu
Msamvu, Kihonda basi!!” nilimjibu na hatimaye tulikuwa
tumesimama.
. . Jojina akajipekua na kutoka na simu yake katika koba lake
ambalo hakuwahi kulitua hata mara moja tangu tuliposhuka
garini na kuanza kutimua mbio.
. . “Simu imezima chaji aisee tungeweza hata kutumia
ramani ya simu kama ingeweza kufaa.” Akasonya kisha
akairudisha simu yake mkobani.
. . Tukaendelea kutembea kuelekea mbele bila kufahamu
kama ni salama ama hatari.
. . “HIFADHI YA TEMBO MIKUMI” Kibao kikatukaribisha
baada ya mwendo mrefu.
. . “Mungu wangu tupo mbugani Sam!! Mbugani Mikumi
hapa…” aliweweseka Jojina nami nikapagawa. Hapakuwa na
ngojangoja zaidi tukaanza kukimbia kuelekea uelekea
mwingine, tukapishana na makundi ya Swala, na kwa mbali
kabisa tukaiona barabara. Tukaukaza mwendo zaidi hadi
tulipoifikia ile barabara.
. . Ilikuwa barabara ya vumbi, na ilikuwa bahati yetu tena
tukaonana na wanadamu. Tukauliza na kupewa uelekeo wa
barabara ya kuelekea Iringa, tukakaza mwendo, miguu
yangu ilikuwa hoi sana lakini sikukubali kuonekana
lelemama.
. . “Sam hawa jamaa tunaopambana nao hawa
wananikumbusha hekaheka za Tunduma huko.” Jojina
akaanzisha maongezi, walau mwendo na maongezi
wapunguza uchovu.
. . “Tunduma? Harakati zipi tena huko.”
. . “Wakati ule wa uchunaji ngozi bwana!! Yaani kuna mdogo
wangu fulani hivi kidogo achunwe ngozi, mwanamama
nikaingia ‘front’ kutetea damu aisee, yaani mafunzo ya
mgambo niliyopitia yananibeba sana mara kwa mara.
Nikamjua jamaa anayewafahamu mabwana waliomteka
dogo, aisee akajifanya mbishimbishi, nilimpiga ngumi mbili
akalegea huko nikamkamata, nikamuwasha vibao ka’ vinne
hivi wacha apagawe!! Nikamzuga kama nampiga teke
akasema atanipeleka, nikamshika ile staili inaitwa
Tanganyika jeki, yaani nikamkamata suruali yake huku
nyuma nikamyanyua akawa anatembelea vidole. Moja kwa
moja hadi eneo la tukio, saa nane usiku hiyo mwanamke
barabarani. Nimeficha kisu huku kwenye pindo la sketi,
tumbili yeyote ajiweke mbele yangu nafyeka korodani zake
namtia uhanithi mimi!!, nikafika pale, nikatia mkwara na
jamaa akiwasihi, mbona walimtoa ndani, walikuwa nd’o
wanajiandaa na safari ya kwenda Zambia wakamchune
ngozi….nikaondoka naye mabwege wananishangaa tu!!
Chezea mama lao wewe!!!” alimaliza simulizi hii kwa
majigambo, nikamkodolea macho wakati huo tukiwa
barabarani tayari.
. . Kichwani nikakiri kuwa huyu Jojina alikuwa na mengi zaidi
ya nilivyomtambua.
. . Baada ya muda tukafanikiwa kuelewana bei na lori la
mbao lililokuwa linaelekea Mafinga, Jojina akawa siti ya
mbele mimi nikawa nyuma huku na vijana wengine.
. . Safari hii haikuwa na mushkeri wowote ule.
. . Tukafika Iringa mjini majira ya saa nne usiku!!
. . Tukatembea kwa miguu kuitafuta nyumba ya Jojina.
. . Tukaifikia nyumba vyema, lakini mazingira haya yalikuwa
tofauti kidogo!! Ni kama kuna aidha ukarabati ulikuwa
umefanyika ama la yale makazi kuna mtu aliongeza ama
kupunguza kitu.
. . Naam!! Tulipoufikia mlango palikuwa na kufuri!!
. . Nani amefunga sasa? Wakati sisi tulikuwa tukitumia
kitasa cha kawaida!!
. . Hatukungoja usiku ule upite, tukazunguka kwa nyuma na
kuifikia nyumba ya mmiliki wa nyumba zote pamoja na
chumba alichokuwa amepanga mama lao!!
. . Mwenye nyuma alikuwa hajalala, kuna mambo ya faragha
alikuwa anashughulika nayo na mkewe na bila shaka ujio
wetu ulimshtua sana!!!
. . “Kulikoni Jojina…” aliuliza kwa sauti tulivu.
. . “Mimi n’do niulize kulikoni kama ni kodi yako nilimaliza
mapema tu vipi tena kufuli jipya mlangoni kwangu!!”
. . Mwennye nyuma akaduwaa kabla hajauliza.
. . “Wewe mwanamama wewe mbona mnataka kunivuruga
sasa. Si wamekuja kaka zako hapa na dada zako wengine
kudai kuwa unahama wewe, tena wamekuja na simu yako
wewe kuwa haurudi tena hapa. Tena kizuri zaidi walikuja na
mwenyekiti wa mtaa na mjumbe, mimi nikawaruhusu
wakachukua mizigo yako kuwa wanakuletea huko ulipo,
sijui kwa mume wako wewe!! Mi hayo sijui na hapa
wakaacha vitu vichache tu!!!” alijibu kwa kujiamini baba
mwenye nyumba.
. . “Mungu wangu weeeee!! Bahasha!!!” ndicho kitu cha
kwanza kabisa kukumbuka kuwa tulikiacha ndani ya
chumba kila kabla ya kusafiri!!!
. . Jojina akalegea na kushuka chini.
. . Akakaa!!
. . Nikaungana naye katika fedheheko hili!!!
. . Bila kithibitisho kile ni wapi zaidi pa kujitetea?
. . Tumekwisha!!!!
. . Nilikiri kimoyomoyo!!!
 
SEHEMU YA KUMI NA SITA
. . Mwenye nyumba akaduwaa kabla hajauliza.
. . “Wewe mwanamama wewe mbona mnataka kunivuruga
sasa. Si wamekuja kaka zako hapa na dada zako wengine
kudai kuwa unahama wewe, tena wamekuja na simu yako
wewe kuwa haurudi tena hapa. Tena kizuri zaidi walikuja na
mwenyekiti wa mtaa na mjumbe, mimi nikawaruhusu
wakachukua mizigo yako kuwa wanakuletea huko ulipo,
sijui kwa mume wako wewe!! Mi hayo sijui na hapa
wakaacha vitu vichache tu!!!” alijibu kwa kujiamini baba
mwenye nyumba.
. . “Mungu wangu weeeee!! Bahasha!!!” ndicho kitu cha
kwanza kabisa kukumbuka kuwa tulikiacha ndani ya
chumba kila kabla ya kusafiri!!!
. . Jojina akalegea na kushuka chini.
. . Akakaa!!
. . Nikaungana naye katika fedheheko hili!!!
. . Bila kithibitisho kile ni wapi zaidi pa kujitetea?
. . Tumekwisha!!!!
. . Nilikiri kimoyomoyo!!!
. . . . ***
. . Mwenye nyumba alilazimika kutushangaa tu asijue nini
kinatusibu, ni kama tulikuwa tumechanganyikiwa vile. Mzee
yule akiwa na koti lake kubwa aliganda mlangoni
akitutazama.
. . “Mna nini kwani vijana wangu, eeh Jojina ni nini kwani?”
hatimaye aliuliza.
. . Jojina akamtazama kwa jicho linaloashiria kukata tamaa
akataka kusema neno lakini akaishia kufungua kinywa tu na
lisitoke neno lol.ote lile. Baridi ilikuwa kali na kiza kilikuwa
kimetanda. Nilitamani kumweleza mwenye nyumba juu ya
hofu yetu lakini nikahamisha na kuuliza swali.
. . “Kwani wamekuja lini hawa watu!!”
. . “Leo asubuhi tu!! Yaani hata majirani watakuwa
hawajasahau, yaani saa nne hivi walikuwa hapa. Mbona
wastaarabu sana ndugu zako wale mi sidhani kama
wanaweza kuwa wamekufanyia kitu kibaya!!”
. . “Ndugu zangu wapi mzee, umewahi kuona
nimekutambulisha ndugu yangu hata mmoja hapa tangu
mzee wangu yule marehemu, sina ndugu ni vibaka tu hao
hawana lolote…vibaka kabisa!!” alilalamika Jojina huku
akipigapiga mikono katika ardhi na miguu akiirusha huku na
kule. Alikuwa amevurugwa sana na jambo lile.
. . Nikamsogelea na kumnong’oneza, “Hapa si mahali sahihi
hata kidogo. Kama walikuja hapa asubuhi basi wanaweza
kurudi muda wowote ule nakwambia. Hawa si vibaka
watakuwa nd’o hao akina anti Ezekiel.”
. . Jojina akatumbua macho yake, huenda hakuwahi kuwaza
jambo kama lile. Akasimama wima. Wakati anasimama mzee
naye alikuwa ameuacha mlanngo na kupiga hatua zaidi
mbele.
. . “Sasa vibaka gani hao wa kuacha makochi, kabati na kila
kitu cha thamani na kuchukua sijui picha ganigani hizo
Jojina, kweli nd’o vibaka walivyo!!” alizungumza kwa sauti
ya chini katika namna ya kusihi.
. . Suala la vitu walivyoiba likazua mjadala upya na ni hapo
ambapo Jojina aliungana nami kuamini kuwa wale
hawakuwa vibaka bali ni watu wanaotutambua vyema na
kuna kitu walikuwa wanatafuta. Kipi zaidi ya picha za
Dulla!!!
. . La!! Si picha ya Dulla pekee na bahasha!! Bahasha yenye
picha na nakala nyingi ambazo bado ni fumbo.
. . Bahasha yenye ufunguo uliochakaa!!
Nikasimama wima baada ya kukumbuka vitu hivyo, na hapo
nikamuuliza yule baba mwenye nyumba.
. . “Na kitanda wameacha?”
. . “Hawajachukua kitu zaidi ya hizo picha na makaratasi
mengine!!” alinijibu huku akituona kama watu ambao tuna
wazimu vichwani mwetu.
. . Sisi hatukujali, na wakati huo Jojina naye alikuwa
amesimama. Akaomba chumba kifunguliwe, baba mwenye
nyumba akataka kugoma Jojina akamgeuzia jicho nkatika
namna ya kutangaza shari. Akaingia ndani na kurejea na
funguo.
. . Akatukabidhi tukaondoka kuelekea kule chumbani, ni
upande ule pia ilikuwepo stoo ambayo alidai kuwa baadhi
ya vitu vya Jojina vilihifadhiwa mle.
. . Jojina akaingia chumbani mimi nikazama stooni, kila
mmoja akitafuta bahasha nachochote kile kingine ambacho
kitaweza kutusaidia katika kufanikisha azma yetu ya
ukombozi.
. . Giza lilikuwa linatusumbua kuweza kuona vitu barabara,
lakini tulilazimika hivyohivyo. Nilivuta makochi huku na
kule, nikavuta vyombo na chochote ambacho nilihisi
kingeweza kunisaidia mbele ya safari.
. . Lile giza ambalo tulikuwa tunalichukia mara lilitoweka
ghafla, lakini si kwamba ulikuwa ni umeme umewaka la!
Hapakuwa na kibatari wala mshumaa na hata taa za kandili
hazikuwa jirani.
. . Nikautafakari ule mwanga!! Nikajivuta hadi dirishani na
kutazama miale yake inapoanzia.
. . Ama!! Zilikuwa ni taa za gari. Tena si gari moja, zilikuwa
gari mbili.
. . Nikajisogeza dirishani zaidi katika nondo niweze
kutambua zile gari usiku ule wa manane zinataka kitu gani
maeneo yale.
. . Nani angenieleza? Hakuwepo!!
. . Vinginevyo nitoke nje na kujisogeza eneo lile. Jambo
ambalo sikuwa tayari hata kidogo kulifanya.
. . Mara nikasikia kishindo nisijue kinatoka wapi. Mhanga wa
nyoka akigusana na ujani…….hiyo inajulikana. Nikaanza
kuingiwa hofu nisijue ni kitu gani nahofia.
. . Mara ghafla kiza cha awali lakini cha sasa kikiwa kinene
zaidi kwa sababu nilikuwa nimeathirika na ule mwanga.
. . Nikatamani sana ule mwanga ungeendelea kidogo maana
nilikuwa nimeona kitu cha rangi ya kaki. Ni kama bahasha
vile.
. . Nikajiundia matazamio ya wapi nilipokiona, mithili ya mtu
asiyeweza kuona nikaanza kupiga hatua moja baada ya
nyingi nikipapasa huku na kule huenda ile ingeweza kuwa
bahati kuu zaidi kupata kutokea.
. . Nikapapasa vibaya nikatengua vyombo kutoka katika
beseni, zaikazuka fujo!! Nikajikinga, bahati nzuri
sikudhurika, nikaendelea mbele, nikapapasa tena huku na
kule, wakati huu ikawa safari ya viti kuporomoka, katika
kujikinga na kuruka huku na kule nikaparamia kochi na
kuanguka chini. Viti kadhaa vikatua juu yangu.
. . Nikajikaza sikupiga mayowe, nikaanza kufanya jitihada za
kujinyofoa kutoka katika hali ile. Lakini haikuwa rahisi,
nikiwa nimesahau kabisa juu ya kishindo cha kwanza
nikasikia kishindo cha pili, mara cha tau na cha nne.
Vishindo vilikuwa vinajongea kuja katika chumba kile.
. . Mungu wangu!! Nikapagawa na kuanza kujinyofoa kwa
pupa. Hali hii haikusaidia.
. . Nikiwa bado katika sintofahamu, mara nikaona mwanga
mdogo kutokea dirishani, na ili kunidhibiti nisitokwe na
mayowe nikasikia sauti ya chini kabisa ikinong’ona.
. . “Wamekuja mabwege, wako wengi kweli wamembana
baba mwenye nyumba huko, tokea dirishani usirudi nyuma
wanaua wale.” Ilikuwa sauti ya Jojina.
. . “Joji…Jojina…nimebanwa na makochi nisaidie nipo huku
chini.” Nililia kwa uchungu uliochanganyika na uoga, na
mara nikakatisha kauli yangu, jicho langu liliiona bahasha
ile iliyonipelekea kubanwa na makochi yale.
. . “JItahidi u..” sikumwacha amalizie.
. . “Jojina bahasha hii hapa…..hii hapa Jojina.” Nilimsihi
wakati huo vishindo vikizidi kusogea na sauti ya baba
mwenye nyumba ikisikika ikilia.
. . Niliukaza mkono wangu nikajitahidi hatimaye nikaishika
ile bahasha. Nikaanza kuivuta mara nikawasikia wakiwa
wamefika.
. . Nikajikuta nachagua moja tu!!
Jojina aipate bahasha kama wataniua mimi yeye atausaka
ukweli. Nikatumia nguvu zangu za mwisho nikajinyanyua
kwa uchungu mkubwa viti vikaparanganyika, nikainyofoa
bahasha nikairusha dirishana, niliuona mkono wa Jojina
ukiidaka vyema, na hapo kochi kubwa likatua vyema usawa
wa paja langu na kunikandamiza vyema.
. . Hapa sikuweza kujizuia nikatokwa na yowe la uchungu!!
. . Mara miale mikali ikanimulika machoni, matusi makali
makali ya nguoni yakafuata baada ya hapo.
. . “Huyu ni nani ulisema hajaja mtu kimburu wewe!!” sauti
hii iliambatana na kilio kutoka kwa baba mwenye nyumba.
. . Ulikuwa msala wa aina yake!!
. . Tochi ziliwashwa na kuzimwa katika macho yangu hivyo
kunivuruga nisiweze kuona chochote kile.
. . “Kill him!!” nikaisikia sauti nyingine ikiamrisha kwa
ghadhabu. Nafsi yangu ikakubali kwa shingo upande kuwa
sikuwa na namna cha muhimu ni kumwombea Jojina aweze
kunitendea haki huku nyuma na hatimaye nizikwe kwa
heshima zote kama mpigania ukombozi.
. . Ukombozi nisioujua hadi nakufa!! Iliniuma sana.
. . Mara wale watu wakavamia mle ndani, wakaanza
kupangua vitu kwa harakaharaka, hata walipofanikiwa
kunifikia hakika nilikuwa hoi.
. . Lakini hawakujali, wakanikwapua na kunirusha nje.
. . “Samson… Samson!!!” niliisikia sauti ikiniita, nikajaribu
kutazama nikakutana nna mwanga wa tochi, sikumtambua
ni nani. Lakini alijawa na dharau wakati akilitaja jina langu.
Bila shaka alinijua vyema, nikiwa nahaha huku na kule mara
kiatu kikatua katika upande wa nyuma wa shingo yangu na
uso ukajivuta kwa nguvu kisha ukatua katika ardhi,
maumivu yakatambaa mwili mzima nikaishia tu kutoa
mguno wa maumivu. Nilipojilamba pembezoni mwa
midomo yangu nikaipata ladha ya chumvi, nilitambua kuwa
natokwa damu, lakini kabla sijatulia vyema nikasikia kiatu
kikiisambaza pua yangu!!
. . Naam!! Damu zikaanza kuchuruzika na maumivu makali
yakanifanya nilie kama mtoto!!
. . “Jack eeh hebu msake huyu Malaya lazima wapo wote
wajinga hawa” aliamrisha na pale wakatoweka wanaume
wawili, niliweza kuona miguu yao.” Nilianza kupatwa na
mashaka walipoondoka na kuelekea ule usawa ambao Jojina
alikuwa. Nikaendelea kuugulia maumivu pale chini. Sasa
nilikuwa nikilindwa na wanaume wawili. Hawakusema lolote
na mimi, bila shaka walingoja watuunganishe wote pamoja
na Jojina waweze kutuadhibu. Adhabu gani nyingine kama si
kuuwawa?
. . Ile hali ya kuamini kuwa baada ya muda mfupi nitakuwa
maiti iliniathiri sana, donge la hasira likanikaba na nikahisi
machungu ya kuonewa yakilidondosha chozi langu kutoka
katika maficho ya macho yangu.
. . Nauwawa kabla sijaonana na mke wangu na mbaya zaidi
kabla sijaonana na Anitha, sijaonana na Eva mwanangu
pekee.
. . Nikalegea na kuikumbatia ardhi nikiisihi iwapo ina uwezo
wowote kwa wakati ule na inisaidie niepukane na uonevu
ule.
. . Lakini ardhi haikunisikia vyema, ikazidi kuimeza damu
iliyokuwa ikinitoka puani. Mgongo ulikuwa unauma na kiuno
vilevile. Niligeuka kumtazama baba mwenye nyumba,
mwanga wa zile tochi ukanisaidia kumwona jinsi kinywa
chake kilivyosambaratishwa vibaya, taya ilikuwa imelegea
na kuangukia upande wa kushoto, udenda uliochanganyika
na na damu ulimiminika kutoka katika kinywa chake.
Sikumtazama mara mbili licha ya kuonekana kama
anayetaka kuniambia neno fulani.
. . Nilipougeuzia uso wangu upande mwingine nikakutana na
kivuli kikubwa chenye umbo kama la mnyama.
. . Mara kile kivuli kikapiga hatua kubwa mbili na kisha
kikapaa.
. . Kilipotua na jamaa mmoja kati ya wawili waliokuwa
wakitulinda akaanguka chini na hapo kile kivuli kikatangaza
uhai wake na ubabe uliopitiliza.
. . Kivuli kikabweka!!!
. . Lahaula!!! lilikuwa jibwa kubwa mithili wa yale majibwa
ya polisi!!!
. . Nikageuka kumtazama baba mwenye nyumba alikuwa
anajilazimisha kutabasamu. Nikastaajabu lakini nikahisi
kuwa lazima kuna jambo linaendelea na yeye analijua.
. . Na hapo nikamsikia akitokwa na sauti kwa kujilazimisha,
alijilazimisha kwa sababu kuu moja tu!!!
Sababu alitaka kujiokoa yeye na mimi pia.
. . “Simbaaa…..umaaa!!!!” alisema kisha akarudi chini na
kutulia tuli!!!
. . Ebwana eeh!! Hivi kumbe mbwa wana hatari kiasi hicho.
Yule bwanha aliyekuwa chini alijikuta akishambuliwa kwa
kasi ya ajabu, yule mbwa alikuwa anajua nini maana ya
kuuma!!
. . Dakika mbili zilitosha kumnyamazisha yule bwana.
. . Yule mwenzake aliyekuwa amesimama wima bado alianza
kuhaha akiitisha ile mbwa kwa mawe, lakini haikutetereka.
Alibahatika kuiponda kwa jiwe moja lakini kwa mara ya pili
ilikuwa kazi bure.
. . Jibwa likajirusha na kung’ata shingo!!! Jamaa akaanguka
chini, jibwa likaanza kumrarua kwa fujo.
. . Lilipohakikisha ametulia tuli likageuka na kutazamana
ana kwa ana na mimi!! Hofu ikaanza!!!
. . Macho ya jibwa lile yalikuwa yanang’ara haswa!!
. . Kauli ya kwamba ukilijua jina la mbwa basi hakutishi
niliduwaa haikufanya kazi, niliita jina la Simba lakini mbwa
yule alionekana kuwa mwenye hasira kali zaidi,
aliunguruma kisha akaendelea kunisogelea. Mapigo ya moyo
yakazidi kwenda kasi na amani ikatoweka tena.
. . Mara akaanza kubweka, nikafanya kosa kutishia kuwa
naweza kupambana naye kwa kumtisha kama namfukuza.
Jibwa likatanua kinywa na bila shaka alitaka kufanya
shambulizi!!!
. . Nikaamini kuwa ng’ombe wa masikini hazai ni usemi
sahihi kabisa. Nikakiona kifo tena mbele yangu. Nguvu nazo
zilikuwa zimeniishia.
. . **UJUMBE! Kukata tamaa nd’o asili ya mwanadamu,
hasahasa akishafanya jitihada zake binafsi pasi na
kumshirikisha mtu!! Lakini je? Kukata tamaa ni suluhu ya
kujikwamua kimaisha, ama kufanikiwa lolote lile?
. . Wanadamu wengi hushindwa kutimiza ndoto zao kwa
sababu ya pepo hili la kukata tamaa.
. . Ili ufanikiwe katika maisha ni lazima ulishinde pepo la
kukata tamaa lakini vinginevyo katika kila vita ulimwenguni
wewe utakuwa wa KUSHINDWA TU!!
Utashindwa vita ya kuupinga umasikini, utashindwa vita ya
kudharauliwa na mwisho kabisa utashindwa vita kuu ya
KUSHINDWA KUIONGOZA AKILI YAKO!!!
. . TAFAKARI!!
 
Stori nzuri sana. Asante endelea kutuburudisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom