RIWAYA : Angamizo

RIWAYA: ANGAMIZO
MWANDISHI: HALFANI SUDY
SIMU 0674 395733
WHATSAPP 0757 633010

SEHEMU YA TISA

ILIPOISHIA JANA...
Itakuwa ni kundi moja kama siyo muuaji mmoja. Lakini awe mtu kiwe kikundi nitahakikisha hafanyi mauaji mengine ya raia wema !" Alisema kwa uchungu mkubwa Daniel. Waliondoka pale Magereza wakiacha mwili wa marehemu Raiya ukipakiwa kwenye gari kupelekwa hospitali. Abdul alikuwa mwenye majonzi sana. Watu wawili waliojitolea kumsaidia kwa hali na mali walikuwa wamefariki kwa tofauti ya masaa machache sana. Ni mkosi gani huu ! Njiani alimuona Daniel Mwaseba akitabasamu. Akajua kuna kitu cha kakiona. Tena bila shaka cha hatari !
"Tunafuatwa" Alimsikia akisema kwa sauti ndogo.
"Ama zetu, ama zao ! "
Waliifuata njia iliyokuwa inaelekea Moshi mjini kutokea Arusha. Abdul roho inamdunda sana. Daniel alikuwa hana wasiwasi hata kidogo. Akiendelea na mluzi wake usioeleweka. Abdul aliangalia kwenye kioo cha pembeni naye aliona.
Gari tatu nyeusi aina ya Noah zilikuwa zinawafuata kwa kasi kubwa sana!.
Daniel alikuwa makini na usukani.
Alipofika Tengeru alikata kulia. Wakawa wanaelekea barabara ya vumbi iliyokuwa inaelekea katika Chuo cha Maendeleo ya jamii, Tengeru. Zilikuwa mbio kali sana kwenye barabara ya vumbi.
Jamaa walianza kurusha risasi!.
Daniel alikuwa dereva makini. Alihakikisha hawadhuriki na risasi zile. Na hawakudhurika!
Daniel aliingiza gari ndani ya Chuo cha Tengeru. Abdul hakutegemea kama ataiingiiza gari Chuoni kwa kasi ile. Yeye alidhani atakata kulia njia inayoelekwa chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela.
Haikuwa hivyo lakini.
Sasa Ilikuwa patashika ndani ya Chuo cha Tengeru. Walikuta wanachuo wengi wapo nje. Baada ya kufunga breki kali! Walishuka haraka haraka na kujichanganya na kundi la wanachuo waliokuwa wanaelekea kunywa chai mgahawani. Waliziona zile Noah tatu nazo zikifunga breki kali.
Vumbi lilitimka.
Baadhi ya wanafunzi wa kike wakipiga kelele za uwoga, wa kiume walikuwa wanashangilia. Bila kujua nini kinatokea . Walishuka jumla ya watu kumi na tano toka katika Noah zile tatu. Wote na bunduki mkononi. Abdul na Daniel walikuwa washaingia Mgahawani. Lakini waliona kila kilichokuwa kinafanyika kule nje karibu na geti ya kuingilia Chuoni. Wanafunzi walianza kukimbia hovyo. Jamaa moja alipiga risasi tatu hewani. Sasa lilikuwa vurumai. Wanafunzi walikimbia hovyo huku wakipiga kelele za taharuki. Wakajigawa wale majamaa. Watano walielekea madarasani. Wawili walienda maktaba. Watatu walienda uelekeo wa ofisi za walimu, na watatu wengine walielekea vimbwetani na wawili walikuwa wanaenda Mgahawani walipokuwa kina Daniel.
Daniel aliinuka pale kwenye meza akaenda kujificha nyuma ya mlango wa Mgahawa ule. Abdul alibaki palepale mezani pamoja na wale wanafunzi. Hali ya hofu ilitawala ndani ya Mgahawa.Wote waliwashuhudia watu wale wawili wakija Mgahawani na silaha zao mkononi. Wanafunzi walikuwa na hofu kubwa, walikuwa wanalia kimya kimya. Wale watu waliingia Mgahawani kwa umakini mkubwa sana. Abdul alikuwa anasubiri hatua atakayoichukua Daniel kule nyuma ya mlango. Alikuwa na imani nae sana.
Akaingia wa kwanza.
Akaingia wa pili.
Wote wakiwa na bunduki zao mkononi, aina ya SMG.
Ghafla yule jamaa mmoja alidondoka chini. Watu wote walistuka mule Mgahawani. Abdul akamwangalia Daniel kule nyuma ya mlango alikojificha. Aliiona mdomo wa bastola yake ukiwa unafuka moshi. Akajua bastola ya Daniel imetumika. Na ilikuwa imefungwa kiwambo cha kuzuia sauti. Na bila shaka risasi ilitua mgongoni kwa yule jamaa.
Yule jamaa mwengine alibabaika sana. Hakujua nini kimempata mwenzie. Mgahawa sasa ulikuwa kimya. Kila mtu alitulia kusubiri hatma ya roho yake.Yule jambazi mwengine aligeuka nyuma kuangalia kule mlangoni.
Alikutana nayo!.
Alipigwa risasi ya utosini. Damu chache ziliwarukia baadhi ya wanafunzi waliokuwa karibu naye. Nae alielekea kuzimu bila ya kuaga. Sasa Daniel alitoka kule mlangoni. Akazivuta zile maiti mbili na kwenda kuzificha nyuma ya mlango.
Hakuwa na wasiwasi kabisa.
Alikuwa kama anavuta magunia ya mkaa tu.
"Wanafunzi wote laleni chini haraka. Atakayejifanya mjuaji tu shauri yake !!" Daniel alisema huku na yeye akilala chini.
Baada ya kama dakika kumi sauti za mlango zilisikika tena. Aliingia jambazi aliyevaa sawa na wale wenzake. Suti nzuri nyeusi na shati jeupe ndani. Na bunduki iliyotayari kuuwa wakati wowote itakapoamrishwa. Huyu aliingia bila umakini wowote. Bila shaka alitegemea Uwepo wa wenzake mule ndani. Hivyo yeye hakuwa makini sana. " Chugaaa" alianza kuita. "Naam" Aliitikiwa. Daniel aliitikia ule wito huku akinyanyuka alipokuwa amelala. Jamaa aliashangaa sana. Akiwa Kwenye mshangao Daniel aliachia risasi iliyozama katika tumbo la yule jamaa. Alikufa na mshangao wake usoni ! Daniel aliivuta ile maiti tena na kwenda kuiweka nyuma ya mlango nayo. Ulikuwa ni mchezo hatari sana lakini Daniel aliucheza bila uwoga wowote. Kosa moja tu lingesababisha kifo. Wanafunzi wengi walikuwa wameshajikojolea pale sakafuni kwa uwoga. Abdul sasa kidogo alianza kuwa mzoefu. Mzoefu wa kuona maiti. Mzoefu wa kuona watu wakiuwawa. Alianza kuupenda pia mchezo wa kifo. Watu wote walikuwa wameikumbatia sakafu kasoro Daniel pekee. Alikuwa amesimama akiangalia kule nje. Simu moja ya wale marehemu ilikuwa inaita kule nyuma ya mlango. Daniel alienda kuipokea.
" Chuga hapa " Alisema, kisha alitulia kusikiliza.
"Yah, waje wawili "
Daniel alijitambulisha kuwa yeye ni Chuga. Na kuomba watu wawili waende mgahawani.
Hawakuchelewa.
Walikuja haraka sana. Wakati Daniel akiwa bado yupo kulekule nyuma ya mlango. Alikoenda kupokea simu. Wauaji waliingia ndani huku wakimwacha Daniel kule nyuma ya mlango. Hawakufikiria kabisa kama kuna hatari!
Abdul jicho lake lilikuwa linaangalia nyuma ya mlango, kwa Daniel kuona atafanya nini?.
Alimuona akijishika kiuno.
Alitoka na visu viwili.
Kimoja amekishika kwa mkono wa kulia na kingine mkono wa kushoto. Alivirusha vyote kwa mpigo na kwa nguvu visu vile kuelekea kwa wale majamaa. Vyote vilitua shingoni. Kila mmoja na chake. Walienda chini kama mizoga. Alimuona Daniel akitabasamu. Majambazi wanne sasa alikuwa kawamaliza kimya kimya mule Mgahawani .
Mara kundi la majambazi wote kumi na moja waliobaki kule nje lilikuwa linakuja Mgahawani wakiwa wanakimbia. Bila shaka walihisi kuna kitu cha hatari!
Sasa ilikuwa hatari zaidi.
Abdul nae alianza kutetemeka mwili mzima kwa hofu. Alimwangalia Daniel kule nyuma ya mlango, alimshangaa hakuwa na hofu kabisa mwanaume yule, alikuwa anatabasamu!. Kwa hakika Daniel hakuwa binadamu wa kawaida. Kila hatari inavyomkaribia yeye anazidi kuwa mtulivu na tabasamu lisiloisha usoni mwake. Wale jamaa waliingia ndani ya Mgahawa. Pale nyuma ya mlango sasa Daniel Alikuwa ameshika bastola mbili mkononi. Ndani ya nusu dakika watu wote kumi na moja walikuwa chini. Wote walikuwa wameuwawa na bastola ya Daniel Mwaseba!
Wanafunzi wote walisimama na kumpa mkono wa pongezi Daniel. Alikuwa shujaa kwao. Alikuwa shujaa zaidi kwa Abdul. Walimhusudu sana Daniel. Abdul alimhusudu zaidi Daniel. Walitoka eneo la Chuo huku Daniel akiwapigia simu Polisi waje kutoa maiti zile. Wao walielekea moja Kwa moja kituo cha Polisi Arusha...
ANAITWA DANIEL MWASEBA, TUKUTANE TENA KESHO KUMSOMA HUYU JAMAA.....
 
RIWAYA YA KIPELELEZI: ANGAMIZO
MWANDISHI: HALFANI SUDY
SIMU 0674 395733

SEHEMU YA KUMI

ILIPOISHIA JANA

Abdul nae alianza kutetemeka mwili mzima kwa hofu. Alimwangalia Daniel kule nyuma ya mlango, alimshangaa hakuwa na hofu kabisa mwanaume yule !. Kwa hakika Daniel hakuwa binadamu wa kawaida. Kila hatari inavyomkaribia yeye anazidi kuwa mtulivu na tabasamu lisiloisha usoni mwake. Wale jamaa waliingia ndani ya Mgahawa. Pale nyuma ya mlango sasa Daniel Alikuwa ameshika bastola mbili mkononi. Ndani ya nusu dakika watu wote kumi walikuwa chini. Wote walikuwa wameuwawa na Daniel ! Wanafunzi wote walisimama na kumpa mkono wa pongezi Daniel. Alikuwa shujaa kwao. Alikuwa shujaa zaidi kwa Abdul. Walimhusudu sana Daniel. Abdul alimhusudu zaidi Daniel ! Walitoka eneo la Chuo huku Daniel akiwapigia simu Polisi waje kutoa maiti zile. Wao walielekea moja Kwa moja kituo cha Polisi Arusha.
SASA ENDELEA
Katika nyumba moja iliyopo mtaa wa Mikocheni, jijini Dar es salaam. Kulikuwa na kikao. Kikao kilihusisha watu watano. Wanajeshi wanne wenye vyeo vikubwa jeshini na raia mmoja wa kawaida. Wanajeshi wale walikuwa wana vyeo vikubwa sana jeshini. Walikuwa wanajadili mpango wao walioupa jina la Angamizo. Lengo la awali la mpango huo ni kuwaangamiza watoto wote wa viongozi wa Tanzania. Ili kusafisha njia kwa Mpango wa Angamizo! Katika kikao kile mtu mmoja tu ndiye ambaye hakuwa mwanajeshi. Mumewe Raiya. Alikuwa anaitwa Salehe, yeye ndiye aliyesababisha siri za mpango huu zivuje Kwa mtu asiyehusika. Kwa bahati mbaya lakini, siri za mpango huu wa Angamizo zilimfikia mkewe, Raiya.
Ilikuwa siku ya ijumaa. Mumewe Raiya alichelewa kurudi nyumbani. Raiya alijisikia uchovu sana. Alichukua laptop ya mumewe ili apoteze mawazo . Kipindi hicho Raiya alikuwa na wakati ngumu sana katika maisha ya ndoa yake. Mumewe alikuwa bize sana. Vikao visivyoisha hadi saa tisa ya usiku. Kutokana na ubize huo Raiya akahisi anasalitiwa kwa kutopewa haki yake ya ndoa. Kumbe hakuwa anasalitiwa. Mumewe alikuwa bize na Mpango haramu, ulioitwa Angamizo!
Hakuwa anampa haki yake ya ndoa mkewe. Alibadilika kabisa. Muda mwingi alikaa peke yake kuipanga sawa mipango yake.
Siku moja hiyo akiwa anachezea laptop ya mumewe. Ndani ya laptop ya mumewe Raiya aliliona faili liliandikwa Siri. Akalifungua bila wasiwasi wowote. Ndani ya faili hilo ndimo alikutana na mambo yaliyomtisha sana. Mpango wa Angamizo ulipangwa utekelezwe baada ya miaka miwili. Ulikuwa Mpango hatari ulioratibiwa na watu hatari sana!
Siku alipoliona faili lile lenye siri toka Kwenye laptop ya mumewe kesho yake ndipo alipokutana na Abdul. Akiwa anatoka Bagamoyo kwa miguu, na kuanzisha uhusiano haramu. Ulikuwa uhusiano haramu lakini ulioleta faida kubwa kwa Taifa baadae.
Siku zilivyosonga mbele Salehe alihisi mabadiliko toka kwa mkewe. Akahisi huenda anatoka nje ya ndoa yao.
Anamsaliti!
Siku zote alikuwa anamlalamikia kuhusu suala la unyumba. Lakini Sasa alikuwa halalamiki tena. Akaanza kumchunguza. Na zaidi Raiya akaanza kumuogopa sana mumewe. Salehe akachunguza. Akagundua kila walichokuwa wanafanya na Abdul. Mbaya zaidi Salehe aligundua pia kuwa Raiya amegundua mpango wao wa Angamizo! Na akajua kwa vyovyote Raiya lazima atamsimulia mtu wake wa karibu. Ambaye ni Abdul! Sasa Salehe alianza kumfatilia Raiya kwa kila hatua aliyopiga. Siku Aliyomuaga kuwa anakwenda Arusha alimkubalia lakini hakumwacha peke yake. Alimfatilia!
Ndipo alipogundua kwa kina kila kitu kuhusu uhusiano wao na kuamua kuwaangamiza wote kwa sumu kali na hatari iitwayo Proxine!
Ndani ya kikao kile ilikuwa ni kutupiana lawama. Wanajeshi wote wanne walikuwa wanamtupia lawama Salehe. Kwa kuweka rehani Mpango wao hatari!. Salehe alijitetea sana.Lakini hakueleweka kabisa. Wakati wanaendelea na mazungumzo yao, simu ya Salehe iliita.
"Halo"
"Bon, Arusha"
"Nambie Bon"
'Mambo mabaya sana"
"Kuna nini tena ?"
"Tumepoteza wapiganaji kumi na tano leo"
"Unasema !!!"
"Ndio hivyo Salehe, kumi na tano wameuwawa "
"Sisi tumefanikiwa lakini !
"Hatujafanikiwa "
"Kwanini Bon..hadi sasa anapumua?"
"Ni msumbufu sana kaka"
"Inamaana ni Abdul ndiye aliyewauwa wapiganaji wetu kumi na tano"
"Ndio Abdul, ila yuko na mwenzie. Ni watu hatari sana"
"Nakuja na Avira na Avast kwa ndege ya jioni, kummaliza"
"Itakuwa poa kaka"
Hali ilikuwa tete ndani ya kundi hili lenye Mpango wa Angamizo.
Jioni ya siku ile Salehe akiongozana na Avast na Avira walikuwa wanaelekea jijini Arusha.Kwa kazi moja tu.
Kuhakikisha Abdul anauwawa!
Avast na Avira walikuwa wauaji hatari. Wauaji wanaojua aina zote za mauaji. Walikuwa makomandoo toka Nigeria walioletwa kwa ajili ya kuleta Angamizo nchini Tanzania. Ni hawa wauaji wanaotumia sumu hatari ya Proxine kuwaua watu kinyama. Asubuhi ya leo walikuwa Arusha kutekeleza kifo cha Raiya akiwa gerezani.Na sasa wanarudi tena Arusha kukatisha maisha ya Abdul. Hawakuwahi kushindwa wanapoamua kuuwa mtu. Walikuwa makini sana na kazi yao. Walitua jijini Arusha saa moja kamili usiku. Walipanga asubuhi ndio waanze kazi yao ya kumsaka Abdul. Hawakuwa na wasiwasi hata kidogo. Walikuwa na uhakika hata kama askari wote Arusha watakaa nje ya kituo cha Polisi alikokuwemo Abdul, waliamini lazima watamuuwa. Walikuwa na mbinu na hila zote za kijasusi.Waliamini watamuua tu!
Walijiamini.
Waliaminiwa pia!
Daniel Mwaseba alimwacha Abdul amemfungia katika chumba cha siri pale Polisi. Chumba kikichojulikana na baadhi tu ya Polisi. Kilikuwa chumba kinachotumiwa kwa nadra sana. Tena kwa sababu maalumu. Daniel alienda kufanya kazi. Aliyanasa maongezi ya Kwenye simu kati ya Bon na Salehe kutoka Kwa rafiki yake aliyekuwa anafanya kazi katika kampuni ya simu waliyotumia Bon na Salehe kuwasiliana. Alihisi kuna kitu kutoka kwa mumewe Raiya. Hivyo aliongea na rafiki yake anase na kurekodi simu zote za Salehe kwa kifaa kiitwacho telemax. Hivyo alisikia simu zote zilizoingia na kutoka katika simu ya Salehe. Ikiwemo simu aliyopiga Bon kwenda kwa Salehe. Na Daniel alikuwa anawasubiri wageni wake.
Daniel aliiona ndege waliyopanda Salehe, Avast na Avira ikitua pale uwanja wa ndege wa Arusha. Aliwaona watu wale watatu wakishuka kwa kujiamini sana. Macho ya Daniel yalikuwa makini sana na wale majamaa mawili, Avast na Avira. Macho yake yalimwambia hawakuwa watu wa kawaida! Aliwaona walivyoshuka kwenye ndege na kupanda kwenye gari aina ya Noah nyeusi. Sawa na zile alizofukuzana nazo asubuhi. Aliifuata nyuma Noah ile akiwa na pikipiki yake. Avast na Avira hawakuwa watu wa kawaida. Huwa wanaweka tahadhari kabla ya jambo halijatokea. Leo walivyoshuka tu kwenye gari walihisi watafuatwa. Walikuwa makini sana! Wakati Daniel akiwafata akina Avast na Avira kutoka uwanja wa ndege, kina Avast walikuwa makini sana na magari yaliyokuwa nyuma yao. Baadae kidogo waliitilia shaka pikipiki iliyokuwa inawafata nyuma. Wakawa wanasubiri muda muafaka wamtie mikononi mfuatiliaji. Wakawa wanaendesha gari taratibu wakiipigia hesabu ile pikipiki. Walikuwa na sumu yao hatari ya Proxine.Tayari kwa kuitumia muda wowote itakapobidi. Msafara uliwafikisha kwenye mzunguko wa Azimio la Arusha wakielekea stendi kuu Arusha.

DANIEL ANAWAFUATA WAKINA AVIRA, NAO WASHAGUNDUA KAMA WANAFUATWA, JE NINI KITATOKEA, SEHEMU YA KUMI NA MOJA NDIO YENYE MAJIBU....
 
  1. RIWAYA: ANGAMIZO

    ANAITWA DANIEL MWASEBA, TUKUTANE TENA KESHO KUMSOMA HUYU JAMAA....
 
  1. RIWAYA YA KIPELELEZI: ANGAMIZO
    MWANDISHI: HALFANI SUDY
    SIMU 0674 395733
    WHATSAPP 0757 633010

    SEHEMU YA KUMI

    ILIPOISHIA JANA

    Abdul nae alianza kutetemeka mwili mzima kwa hofu. Alimwangalia Daniel kule nyuma ya mlango, alimshangaa hakuwa na hofu kabisa mwanaume yule !. Kwa hakika Daniel hakuwa binadamu wa kawaida. Kila hatari inavyomkaribia yeye anazidi kuwa mtulivu na tabasamu lisiloisha usoni mwake. Wale jamaa waliingia ndani ya Mgahawa. Pale nyuma ya mlango sasa Daniel Alikuwa ameshika bastola mbili mkononi. Ndani ya nusu dakika watu wote kumi walikuwa chini. Wote walikuwa wameuwawa na Daniel ! Wanafunzi wote walisimama na kumpa mkono wa pongezi Daniel. Alikuwa shujaa kwao. Alikuwa shujaa zaidi kwa Abdul. Walimhusudu sana Daniel. Abdul alimhusudu zaidi Daniel ! Walitoka eneo la Chuo huku Daniel akiwapigia simu Polisi waje kutoa maiti zile. Wao walielekea moja Kwa moja kituo cha Polisi Arusha.
    SASA ENDELEA
    Katika nyumba moja iliyopo mtaa wa Mikocheni, jijini Dar es salaam. Kulikuwa na kikao. Kikao kilihusisha watu watano. Wanajeshi wanne wenye vyeo vikubwa jeshini na raia mmoja wa kawaida. Wanajeshi wale walikuwa wana vyeo vikubwa sana jeshini. Walikuwa wanajadili mpango wao walioupa jina la Angamizo. Lengo la awali la mpango huo ni kuwaangamiza watoto wote wa viongozi wa Tanzania. Ili kusafisha njia kwa Mpango wa Angamizo! Katika kikao kile mtu mmoja tu ndiye ambaye hakuwa mwanajeshi. Mumewe Raiya. Alikuwa anaitwa Salehe, yeye ndiye aliyesababisha siri za mpango huu zivuje Kwa mtu asiyehusika. Kwa bahati mbaya lakini, siri za mpango huu wa Angamizo zilimfikia mkewe, Raiya.
    Ilikuwa siku ya ijumaa. Mumewe Raiya alichelewa kurudi nyumbani. Raiya alijisikia uchovu sana. Alichukua laptop ya mumewe ili apoteze mawazo . Kipindi hicho Raiya alikuwa na wakati ngumu sana katika maisha ya ndoa yake. Mumewe alikuwa bize sana. Vikao visivyoisha hadi saa tisa ya usiku. Kutokana na ubize huo Raiya akahisi anasalitiwa kwa kutopewa haki yake ya ndoa. Kumbe hakuwa anasalitiwa. Mumewe alikuwa bize na Mpango haramu, ulioitwa Angamizo!
    Hakuwa anampa haki yake ya ndoa mkewe. Alibadilika kabisa. Muda mwingi alikaa peke yake kuipanga sawa mipango yake.
    Siku moja hiyo akiwa anachezea laptop ya mumewe. Ndani ya laptop ya mumewe Raiya aliliona faili liliandikwa Siri. Akalifungua bila wasiwasi wowote. Ndani ya faili hilo ndimo alikutana na mambo yaliyomtisha sana. Mpango wa Angamizo ulipangwa utekelezwe baada ya miaka miwili. Ulikuwa Mpango hatari ulioratibiwa na watu hatari sana!
    Siku alipoliona faili lile lenye siri toka Kwenye laptop ya mumewe kesho yake ndipo alipokutana na Abdul. Akiwa anatoka Bagamoyo kwa miguu, na kuanzisha uhusiano haramu. Ulikuwa uhusiano haramu lakini ulioleta faida kubwa kwa Taifa baadae.
    Siku zilivyosonga mbele Salehe alihisi mabadiliko toka kwa mkewe. Akahisi huenda anatoka nje ya ndoa yao.
    Anamsaliti!
    Siku zote alikuwa anamlalamikia kuhusu suala la unyumba. Lakini Sasa alikuwa halalamiki tena. Akaanza kumchunguza. Na zaidi Raiya akaanza kumuogopa sana mumewe. Salehe akachunguza. Akagundua kila walichokuwa wanafanya na Abdul. Mbaya zaidi Salehe aligundua pia kuwa Raiya amegundua mpango wao wa Angamizo! Na akajua kwa vyovyote Raiya lazima atamsimulia mtu wake wa karibu. Ambaye ni Abdul! Sasa Salehe alianza kumfatiliaRaiya kwa kila hatua aliyopiga. Siku Aliyomuaga kuwa anakwenda Arusha alimkubalia lakini hakumwacha peke yake. Alimfatilia!
    Ndipo alipogundua kwa kina kila kitu kuhusu uhusiano wao na kuamua kuwaangamiza wote kwa sumu kali na hatari iitwayo Proxine!
    Ndani ya kikao kile ilikuwa ni kutupiana lawama. Wanajeshi wote wanne walikuwa wanamtupia lawama Salehe. Kwa kuweka rehani Mpango wao hatari!. Salehe alijitetea sana.Lakini hakueleweka kabisa. Wakati wanaendelea na mazungumzo yao, simu ya Salehe iliita.
    "Halo"
    "Bon, Arusha"
    "Nambie Bon"
    'Mambo mabaya sana"
    "Kuna nini tena ?"
    "Tumepoteza wapiganaji kumi na tano leo"
    "Unasema !!!"
    "Ndio hivyo Salehe, kumi na tano wameuwawa "
    "Sisi tumefanikiwa lakini !
    "Hatujafanikiwa "
    "Kwanini Bon..hadi sasa anapumua?"
    "Ni msumbufu sana kaka"
    "Inamaana ni Abdul ndiye aliyewauwa wapiganaji wetu kumi na tano"
    "Ndio Abdul, ila yuko na mwenzie. Ni watu hatari sana"
    "Nakuja na Avira na Avast kwa ndege ya jioni, kummaliza"
    "Itakuwa poa kaka"
    Hali ilikuwa tete ndani ya kundi hili lenye Mpango wa Angamizo.
    Jioni ya siku ile Salehe akiongozana na Avast na Avira walikuwa wanaelekea jijini Arusha.Kwa kazi moja tu.
    Kuhakikisha Abdul anauwawa!
    Avast na Avira walikuwa wauaji hatari. Wauaji wanaojua aina zote za mauaji. Walikuwa makomandoo toka Nigeria walioletwa kwa ajili ya kuleta Angamizo nchini Tanzania. Ni hawa wauaji wanaotumia sumu hatari ya Proxine kuwaua watu kinyama. Asubuhi ya leo walikuwa Arusha kutekeleza kifo cha Raiya akiwa gerezani.Na sasa wanarudi tena Arusha kukatisha maisha ya Abdul. Hawakuwahi kushindwa wanapoamua kuuwa mtu. Walikuwa makini sana na kazi yao. Walitua jijini Arusha saa moja kamili usiku. Walipanga asubuhi ndio waanze kazi yao ya kumsaka Abdul. Hawakuwa na wasiwasi hata kidogo. Walikuwa na uhakika hata kama askari wote Arusha watakaa nje ya kituo cha Polisi alikokuwemo Abdul, waliamini lazima watamuuwa. Walikuwa na mbinu na hila zote za kijasusi.Waliamini watamuua tu!
    Walijiamini.
    Waliaminiwa pia!
    Daniel Mwaseba alimwacha Abdul amemfungia katika chumba cha siri pale Polisi. Chumba kikichojulikana na baadhi tu ya Polisi. Kilikuwa chumba kinachotumiwa kwa nadra sana. Tena kwa sababu maalumu. Daniel alienda kufanya kazi. Aliyanasa maongezi ya Kwenye simu kati ya Bon na Salehe kutoka Kwa rafiki yake aliyekuwa anafanya kazi katika kampuni ya simu waliyotumia Bon na Salehe kuwasiliana. Alihisi kuna kitu kutoka kwa mumewe Raiya. Hivyo aliongea na rafiki yake anase na kurekodi simu zote za Salehe kwa kifaa kiitwacho telemax. Hivyo alisikia simu zote zilizoingia na kutoka katika simu ya Salehe. Ikiwemo simu aliyopiga Bon kwenda kwa Salehe. Na Daniel alikuwa anawasubiri wageni wake.
    Daniel aliiona ndege waliyopanda Salehe, Avast na Avira ikitua pale uwanja wa ndege wa Arusha. Aliwaona watu wale watatu wakishuka kwa kujiamini sana. Macho ya Daniel yalikuwa makini sana na wale majamaa mawili, Avast na Avira. Macho yake yalimwambia hawakuwa watu wa kawaida! Aliwaona walivyoshuka kwenye ndege na kupanda kwenye gari aina ya Noah nyeusi. Sawa na zile alizofukuzana nazo asubuhi. Aliifuata nyuma Noah ile akiwa na pikipiki yake. Avast na Avira hawakuwa watu wa kawaida. Huwa wanaweka tahadhari kabla ya jambo halijatokea. Leo walivyoshuka tu kwenye gari walihisi watafuatwa. Walikuwa makini sana! Wakati Daniel akiwafata akina Avast na Avira kutoka uwanja wa ndege, kina Avast walikuwa makini sana na magari yaliyokuwa nyuma yao. Baadae kidogo waliitilia shaka pikipiki iliyokuwa inawafata nyuma. Wakawa wanasubiri muda muafaka wamtie mikononi mfuatiliaji. Wakawa wanaendesha gari taratibu wakiipigia hesabu ile pikipiki. Walikuwa na sumu yao hatari ya Proxine.Tayari kwa kuitumia muda wowote itakapobidi. Msafara uliwafikisha kwenye mzunguko wa Azimio la Arusha wakielekea stendi kuu Arusha.

    DANIEL ANAWAFUATA WAKINA AVIRA, NAO WASHAGUNDUA KAMA WANAFUATWA, JE NINI KITATOKEA, SEHEMU YA KUMI NA MOJA NDIO YENYE MAJIBU....

RIWAYA: ANGAMIZO
MWANDISHI: HALFANI SUDY
SIMU: 0674 395733
WHATSAPP 0757 633010

SEHEMU YA KUMI NA MOJA

ILIPOISHIA JANA
Alikufa kifo kinachofanana na cha Mayasa!. Alikufa kifo kinachofanana na cha Raiya ! . alikufa kifo kinachofanaa na cha afande John. Yule jamaa nae alivuka ngozi! Kumbe yule jamaa alishika ile dawa inayoitwa Proxine pale alipotaka kumsalimia Abdul kwa mkono. Na alivyokuwa anataka kutoa kitu mfukoni alikuwa anataka kutoa dawa nyingine ili ajipake dawa kuzuia madhara ya ile dawa. Lakini alichelewa. Daniel alikuwa anamzuia kwa pigo kila alipotaka kuitoa ile dawa hiyo. Alijua atakufa! Ndomana alianza kulia kabla.
Siku zote mshahara wa dhambi ni mauti!

ISOME YA LEO SASA....
Daniel alimsogelea taratibu na kuanza kumuuliza Abdul kwa upole.
"Kuna kitu wanahisi unacho. Wanataka kukuua ili kisitoke nje. N kitu gani hiko?"
"Mimi sina kitu kaka Daniel. Sijui hata to wananitakia nini ?"
"Kipo kitu Abdul"
"Kitu gani sasa kaka Daniel ?"
"Mayasa alishawahi kukupa kitu chochote enzi za uhai wake?"
"Amewahi kunipa vitu vingi lakini siyo vya kudumu"
"Raiya alikupa nini cha kudumu ?"
"Hamna zaidi ya hii simu "
"Hebu ilete" Akampa.
Daniel aliiangalia ile simu kwa makini. Aliigeuza nyuma. Aliifungua ile simu kule nyuma. Kule inakokaa betri ilidondoka chini karatasi ndogo. Abdul alishangaa sana. Hakuwa ameweka karatasi yoyote kwa kuwa hakuwahi kuifungua simu ile tangu alivyopewa na Raiya. Daniel akaisoma kwa sauti ndogo ile karatasi.
"Kwenye laptop ya mme wangu kuna faili la limeandikwa Siri. Linahusu mpango wa kuangamiza watoto wa viongozi wa nchi hii na mambo mengine mengi ya siri sana . Abdul jaribu kulifikisha suala hili kunapohusika ili kuliokoa Taifa hili "
Abdul alishangaa sana. Sasa alimhusudu sana Raiya. Alimuona ni mtu mwenye akili kuliko mtu yeyote duniani. Raiya kumbe alikufa na siri kubwa sana. Ambayo siri hiyo aliifikisha kwa Abdul kwa siri pia. Abdul alimhusudu zaidi Daniel. Aligundua kitu alichokaa nacho miaka miwili bila kutambua . Alikiri Daniel hakuwa mtu wa karne hii. Alikuwa na akili na uwezo wa ziada.
Daniel alitoka nje na kile kikaratasi. Baada ya dakika kumi na tano waliingia askari wawili kuutoa mwili wa yule jamaa. Daniel alitoka nje kwa nia moja tu. Kumtafuta mume wa Raiya popote alipo. Ilikuwa lazima ampate popote atakapokuwa!
Upande wa kina Avast ilikuwa ni patashika na taharuki kubwa. Ilikuwa yapata saa saba ya mchana sasa, Avira hajarudi. Ilikuwa ajabu. Avira hakuwahi kufanya kazi muda mrefu namna hii. Avira hufanya mambo kwa haraka na kwa uhakika. Hiyo ndio sifa kuu ya Avira. Alitekeleza kazi ya kumuua Raiya robo saa tu alivyoenda magereza. Leo masaa zaidi ya matano alikuwa hajarudi.
Walimsubiri.
Walimsubiri sana.
Hakurudi.
Na hajarudi mpaka leo!.
Daniel alivyotoka palepale moja kwa moja alienda kwa dada yake Raiya. Alienda na kumuulizia mtaa na namba ya nyumba akiyokaa Raiya huko Dar es salaam ilipo. Baada ya kuelekezwa Daniel aliweka 'booking' ya ndege ya kwenda Dar es salaam kesho yake asubuhi.
Aliipata.
Usiku ule ulikuwa mgumu sana kwa Avast na Salehe. Wakaanza kuhisi huenda Avira amekamatwa. Wakawa wanahofia endapo Avira atakuwa kakamatwa anaweza kutoa siri. Siri pekee ambayo hawakutaka itoke ilikuwa kwenye laptop, nyumbani kwa Salehe, Dar es salaam. Wakapanga kesho Avast aende Dar es salaam kuichukua ile laptop. Ili siri isifike mikononi kwa adui
 
RIWAYA: ANGAMIZO
MWANDISHI: HALFANI SUDY
SIMU 0674 395733
WHATSAPP 0757 633010

SEHEMU YA KUMI NA TATU

ILIPOISHIA JANA...
Avast anaenda Dar es salaam kesho kuifata laptop yenye siri nzito. Daniel anaenda Dar es salam kesho kuifata laptop hiyo hiyo yenye siri nzito! Wasakana! Watakutana Dar es salaam!

ENDELEA SASA...
Daniel Mwaseba ndiye alikuwa wa kwanza kufika nyumbani kwa Salehe Mikocheni. Hakupata shida sana kuingia ndani ya nyumba ya Salehe. Hakukuwa na ulinzi wowote kwenye nyumba ile. Aliruka ukuta na kuingia ndani. Aliitafuta laptop ndani ya chumba cha Daniel. Chumba hakikuwa na vitu vingi sana. Kulikuwa na kitanda kikubwa, meza ya kujirembea na kabati kubwa la nguo.
Robo saa ilitosha kukipata alichokuwa anakitafuta ndani ya nyumba ile kubwa. Aliikuta laptop ndani ya kabati la nguo chumbani katika chumba cha kulala cha Salehe. Aliiweka laptop yenye siri nzito kwenye begi na kuanza kutoka.
Hakutaka kuifungua akiwa mle ndani. Aliona ile siyo sehemu salama. Alipita sebuleni akafungua mlango wa sebule wa kutokea nje. Sasa akawa anatembea katika uwanja mpana kulielekea geti la nyumba ile. Alilikaribia kabisa geti. Zilibaki hatua kama tano ili Daniel atoke nje ya nyumba ile.
Ghafla! Geti lilianza kufunguka lenyewe! Aliingia mtu mrefu, mweusi, mkakamavu. Alikuwa ni Mnigeria. Kwa jina alikuwa anaitwa Avast! Pacha wa Avira aliyemuuwa kwa mateso makubwa jana, kule Arusha.
Sasa Daniel Alikuwa anatazamana macho kwa macho na Avast. Wote wakiwa Na bastola mkononi! Avast alikuwa anauangalia sana mfuko alioubeba Daniel. Akajua ndani ya mfuko ule kipo alichokifuata. Laptop yenye siri nzit !
"Wanaume wanaojiamini hawapambani kwa silaha. Tuweke silaha chini na tuoneshane ubabe" Avast aliongea kwa sauti yake mzito na ya kujiamini yenye lafudhi ya kinigeria. Aliongea kwa majigambo sana. Daniel alitii, kwa sababu nae alijiamini. Alitaka kumuonesha Avast jinsi Wanaume wa kweli wanavyopigana. Wote waliweka bastola chini. Sasa ulikuwa mpambano wa nguvu. Mshindi alitakiwa kuondoka na laptop ile yenye siri nzito!
Ndani ya sekunde thelathini walikuwa wanaangaliana tu . Kila mmoja akifikiria jinsi ya kumuingia mwenzie.
Avast ndiye alitangulia kushambulia. Avast aliruka juu na kumuelekezea Daniel mateke mawili ya nguvu kuelekea kifuani kwake. Daniel hakujiandaa vizuri . Mateke yale yalitua sawia kwenye kifua chake. Nguvu ya mateke yale yalimfanya Daniel adondoke chini. Huku mfuko wenye laptop nao ukidondoka chini!. Daniel alinyanyuka kivivu.
Avast alirusha teke la kulia lililokuwa linaenda mbavuni kwa Daniel. Alijaribu kulipangua lakini alizidiwa nguvu na uzito wa teke lile. Lilimpata kidogo Kwenye mbavu.
Aligumia kwa maumivu!
Avast alirusha ngumi na wakati uleule Daniel alirusha ngumi. Ngumi zile zilikutana katikati. Ila Daniel ndiye aliyepata madhara. Ngumi ya Avast ilikuwa na nguvu zaidi. Daniel aliumia mkono. Sasa Daniel akajua akitumia nguvu atapigwa. Yule jamaa alikuwa hatari sana. Sasa aliona ulikuwa wakati wa kutumia zaidi akili . Avast alirusha mateke mawili kwa mpigo. Kwa miguu miwili tofauti. Moja lilimpata Daniel kwenye mbavu ya kushoto na lengine mbavu ya kulia.
Daniel alidondoka chini kwa nguvu.
Alikuwa ameumia mbavu vibaya sana. Avast hakuwa mtu wa mchezo kabisa!
Avast alitoa kichupa kidogo cha dawa ya Proxine , akapaka kwenye kiganja chake na kumsogelea ili ampake Daniel pale chini alipokuwa amelala! Ile anataka kumgusa Daniel alijisogeza kwa nguvu na kwa haraka. Avast aligusa sakafu!
Daniel alinyanyuka sasa. Akawa makini zaidi. Akijua kosa moja tu linaondoka na maisha yake. Alisimama imara sasa. Avast nae alikuwa anataka kufanya haraka ili ile sumu ya Proxine isimdhuru mwenyewe. Ilikuwa na uwezo wa kukaa kiganjani kwa dakika kumi tu .Baada ya hapo ingemdhuru yeye mwenyewe. Daniel akajua hiyo ni nafasi pekee ya kumshinda Avast. Avast alirusha teke lililompata Daniel kwenye shingo. Teke lile lilimpeleka Daniel chini bila kutaka. Avast akawa anamsogelea tena ampake Proxine. Hakumgusa, alikutana na ngumi takatifu ya pua, damu zikaanza kumtoka. Avast hakujigusa pua. Kujigusa pua Ilikuwa inamaanisha kujivua ngozi. Kujiua mwenyewe kwa sumu kali ya Proxine! Wote walikuwa wamesimama, wanaangaliana kama majogoo. Avast alirusha kofi kwa kutumia ule mkono wake wa kulia wenye sumu ya Proxine . Daniel aliliona kofi lile. Alinesa kidogo likapita jumla. Daniel alipata nafasi. Kwa kutumia mkono wake wa kushoto alipiga ngumi ya nguvu kwenye mbavu za Avast. Avast aligumia kwa maumivu makali. Alitamani kujishika mbavu lakini hakuruhusiwa na Proxine.
Proxine sasa ikawa zuio kwake mwenyewe!
Sasa Avast mbavu zilikuwa zinamuuma huku damu zinachuruzika puani. Alikosa umakini, hakuweka kinga usoni. Daniel aliitumia vizuri hiyo nafasi. Alipiga ngumi mbili za haraka usoni kwa Avast. Avast Akawa anaona nyotanyota!
Avast aliyumba kutokana na uzito wa zile ngumi, lakini hakuanguka. Daniel alirusha teke kali lililompata Avast kwenye goti lake. Alienda chini taratibu. Kama Avira, Avast alikuwa analia naye. Alikiona kifo kwa mbali kikimsogelea. Proxine ilianza kuleta mrejesho.
Alijaribu kutoa dawa ya kuiondoa ile sumu ya Proxine, akaishika mkononi. Akitaka kufungua kile kichupa ili aondoe ile sumu hatari. Alichelewa, teke kali la Daniel liliupiga ule mkono ulioishika ile dawa. Chupa ilidondoka sakafuni na kuvunjika!
Avast sasa alilia kwa sauti kama mtoto mdogo. Alilia Kwa sauti kali! Daniel alikuwa anacheka kimoyomoyo.
Auwae kwa upanga siku zote huuwawa kwa upanga!
Daniel aliruka "double kick". Miguu yake yote miwili ilitua kwenye kifua cha Avast. Avast alitapika damu. Huku akiwa anatapika damu ngozi yake ilianza kuvuka taratibu.
Daniel hakusubiri. Alichukua lile begi lenye laptop na kutoka nalo nje akiwa anakimbia. Akitafuta hotel salama na kujifungia ndani peke yake.Tayari kuifungua ile laptop yenye siri nzito. Moyo wake ulikuwa unamwenda kasi alipoliona faili lililiandikwa Siri! Akabofyabofya kidogo.
Sasa akatulia na kuanza kulisoma.
Ghafla mlango ulifunguka kwa kasi! Ulikuwa umevunjwa kwa teke zito!. Waliingia wazee wawili wakiwa wamevaa suti nzuri nyeupe.
"Hatujaja kuua. Tumefata laptop tu!"

DANIEL ALIDHANI KUMUUA AVAST KAMALIZA KAZI, KAZI KUMBE BADO, JE DANIEL ATAJINASUA VIPI KATIKA MTEGO HUU MPYA, NJOO TENA KESHO HAPA TUSOME.
 
  1. RIWAYA YA KIPELELEZI: ANGAMIZO
    MWANDISHI: HALFANI SUDY
    SIMU 0674 395733
    WHATSAPP 0757 633010

    SEHEMU YA KUMI NA NNE

    Daniel hakusubiri.
    Alichukua lile begi lenye laptop na kutoka nalo nje akiwa anakimbia. Akitafuta hotel salama na kujifungia ndani peke yake.Tayari kuifungua ile laptop yenye siri nzito. Moyo wake ulikuwa unamwenda kasi alipoliona faili lililiandikwa Siri! Akabofyabofya kidogo.
    Sasa akatulia na kuanza kulisoma. Ghafla mlango ulifunguka kwa kasi! Ulikuwa umevunjwa kwa teke zito!.
    Waliingia wazee wawili wakiwa wamevaa suti nzuri nyeupe.
    "Hatujaja kuua. Tumefata laptop tu !" Mzee mmoja alisema.
    "Hamuwezi kuipata laptop mpaka mniuwe kwanza" Daniel nae alijibu. Wale wazee walicheka kwa sauti kwa pamoja.
    Walijiamini sana!
    Wazee wale walitoa bastola .Midomo miwili ya bastola ilikuwa inamuangalia Daniel! Hakuihofia. Yeye alitabasamu tu. Wale wazee wawili Walikuwa wamenuna hasa.Tabasamu lile la Daniel waliliona kama dhihaka toka kwa Daniel. Wakawa wanamsogelea taratibu pale kitandani alipokaa. Daniel aliacha kuwaangaalia. Akawa anaitazama ile laptop. Ikifanya alichoiagiza. Ilikubali! Kichwani alifikiria cha kufanya.
    Jamaa walimkaribia sasa. Zilibaki hatua kama tano wamfikie kabisa. walikuwa makini. Walikuwa wanamtambua Daniel. Walijua kosa moja tu lingewagharimu maisha yao yote!
    "Simama juu !" Mmoja aliamrisha. Daniel alisimama taratibu.
    "Mikono juu!" Yule yule wa mwanzo alitoa amri nyingine Daniel alinyoosha mikono yake juu.
    Yule aliyetoa amri alimsogelea huku yule mwengine akiwa amebaki palepale. Akimnyooshea bastola yake. Jamaa alimpekua Daniel harakaharaka. Alipata visu viwili na bastola moja. Hivyo viliwekwa sehemu ya kawaida. Silaha alizoweka sirini hakuzipata. Zilihitaji mtu anayejua kupekua hasa. Akaishika ile laptop. Bila kuitazama akaifunga. Wakawa wanarudi kinyumenyume sasa.
    "Naitwa kaspersky " yule aliyempekua Daniel alisema.
    "Naitwa Zwangendaba" Na yule aliyekuwa kimya muda wote alisema.
    Wakatokomea na laptop mbio!
    "Tutakutana tu " Daniel alisema kimoyomoyo, huku akitabasamu.
    Akatoka nje taratibu. Kwa utulivu mkubwa. Kama hajatizamwa na midomo miwili ya bastola dakika chache zilizopita. Alitembea kwa madaha. Kwa mwendo wa kujiamini. Huku akijiuliza kwanini wale jamaa walimwacha akipumua. Akawacheka ujinga. Hawakujua kuwa walifanya kosa la karne. Daniel Mwaseba alikuwa zaidi ya wanavyomfahamu!
    Akarandaranda mitaa ya Mikocheni bila uelekeo maalumu. Aliranda makusudi. Alikuwa anachunguza kama kuna mtu anamfatilia. Hakumwona mtu. Akaingia kwenye "internet cafe" moja. Akalipia masaa mawili. Akaifungua email yake.
    Alikuta akichokitaka.
    Daniel aliikuta email iliyotumwa muda mfupi uliopita. Aliwapongeza wamiliki wa hoteli ile aliyokuwa mwanzo kwa kuweka "wireless internet'. Aliikuta email aliyojitumia yeye mwenyewe muda mfupi uliopita alivyokuwa kule hotelini. Kabla ya wale jamaa hawajamvamia. Kichwa cha email kilisomeka "SIRI ". Daniel akatabasamu tena. Sasa alianza kuisoma. Alianza kuisoma ile email yenye siri nzito!
    "Hili ni Angamizo !.
    Macho yasiyohusika hayapaswi kabisa kuona maandishi haya...."
    Ghafla Daniel alihisi anapapaswa bega. Daniel aligeuka. Alikuwa anatazamana uso kwa uso na Zwangendaba!.
    " Sasa nimekuja kuichukua roho yako rafiki yangu, unajifanya mjanja? " Alimnong'oneza Kwa sauti ndogo iliyopenya vizuri katika sikio la kushoto la Daniel.
    Kwa mara ya kwanza mapigo ya moyo yalimpiga Daniel!. Hakutegemea kabisa watu wale kuwa mahali pale muda ule. Hakutegemea kabisa kukamatwa kirahisi namna ile. Alihisi Kutekenywa na kitu kigumu mbavuni.
    Akaelewa.
    Alikuwa ameguswa na bastola kwenye mbavu zake.
    "Simama juu" Zwangendaba alinong'ona tena.
    Daniel alisimama. Watu wote ndani ya 'internet cafe' hawakuelewa nini kinaendelea. Kila mtu alikuwa anatazamana na kompyuta yake. Daniel alikuwa anatekwa kimya kimya. Kaspersky naye aliingia ndani ya internet cafe. Akaisogelea ile kompyuta akiyoitumia Daniel. Akaifuta ile email ya siri. Akarudi nje wakapanda kwenye Noah yao nyeusi. Safari ya kwenda kusikojulikana iliaanza.
    Ndani ya gari ilikuwa kimya. Hakuna aliyeongea. Wale majamaa wawili walikuwa wanavuta bangi kwa fujo ndani ya gari. Gari yote ilitapakaa moshi wa bangi. Yalikuwa mateso kwa Daniel. Hakuwa mvutaji hata wa sigara. Lakini hakuruhusu hata kukohoa. Alijua kukohoa tu ataonekana dhaifu mbele ya watu wale.
    Safari isiyojulikana ilifika mwisho. Ilikuwa nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam. Kulikuwa na kibanda kidogo porini. Kibanda kilichojitenga na nyumba za watu. Walimuweka kwenye kibanda hicho. Daniel alishuhudia migongo ya Kerspersky na Zwangendaba ikitokomea. Daniel walimfungia peke yake kwenye kibanda hicho!
    Kilikuwa kibanda kidogo chenye mlango mmoja tu. Hakukuwa na madirisha wala sehemu yoyote ya kutolea au kuingiza hewa. Walimfungia kinje-nje. Alisikia muungurumo wa gari, jamaa walitoweka kwa kasi kwa gari yao. Bila shaka kwenda kumalizia mpango wao hatari wa Angamizo!.
    Hawakutaka kumuua Daniel. Nia yao Daniel ashuhudie Angamizo litakaloikumba Serikali yake. Walimuacha hai ili ateseke kwa kuona Angamizo hilo litakuwaje?

    DANIEL TUNDUNI, WALE MAJAMAA KWA MARA NYINGINE TENA WAMEIGUNDUA MBINU YA DANIEL...NJOO TENA KESHO KUUFAHIDI UHONDO HUU...MIMI TEAM ZWANGENDABA WEWE JE?

Back
Top Bottom