RIWAYA : Angamizo

RIWAYA : Angamizo

RIWAYA YA KIPELELEZI: ANGAMIZO
MWANDISHI: HALFANI SUDY
SIMU 0674 395733
WHATSAPP 0757 633010

SEHEMU YA KUMI NA TANO

Hakuwa mvutaji hata wa sigara. Lakini hakuruhusu hata kukohoa. Alijua kukohoa tu ataonekana dhaifu mbele ya watu wale. Safari isiyojulikana ilifika mwisho. Ilikuwa nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam. Kulikuwa na kibanda kidogo porini. Kibanda kilichojitenga na nyumba za watu. Walimuweka kwenye kibanda hicho.
Daniel alishuhudia migongo ya Kerspersky na Zwangendaba ikitokomea. Daniel walimfungia kwenye kibanda hicho! Kilikuwa kibanda kidogo chenye mlango mmoja tu. Hakukuwa na madirisha wala sehemu yoyote ya kutolea au kuingiza hewa. Walimfungia kinjenje. Alisikia muungurumo wa gari, jamaa walitoweka kwa kasi kwa gari yao. Kwenda kumalizia mpango wao hatari wa Angamizo!.
Hawakutaka kumuua Daniel. Nia yao Daniel ashuhudie Angamizo litakaloikumba Serikali yake. Walimuacha hai ili ateseke kwa kuona Angamizo hilo!
*****
Abdul aliendelea kukaa kule kwenye chumba cha siri cha Polisi Arusha. Alikuwa ameshachoka sasa. Alikuwa anautamani sana uhuru wake. Hakumuona Daniel ndani ya siku tatu. Alikuwa anatamani kumuona Daniel. Maana yeye ndio alikuwa tumaini lake pekee la kuurudisha Uhuru wake tena. Alianza kukonda kwa mawazo.
Upande wa jeshi la Polisi nao ulichanganyikiwa sana. Kutoonekana kwa Daniel kwa siku tatu bila mawasiliano yoyote lilikuwa jambo la kushangaza sana. Wakahisi huenda Daniel yuko katika matatizo makubwa. Walimtafuta kila sehemu waliyoifikiria bila mafanikio yoyote.
Ndani ya kibanda kile Daniel aliteseka sana. Kulikuwa na joto kali kupita kiasi. Ukijumlisha na njaa pamoja na kiu kikali alichokuwa nacho, yalikuwa mateso makubwa sana.
Alivyoachwa tu Daniel siku ileile alitafuta njia ya kujiokoa bila mafanikio. Mlango ulikuwa ni geti gumu la chuma. Ukuta wa tofali ulikuwa mrefu wa kunyooka juu, mgumu kuupanda. Kwa juu ziliezekwa bati za udongo. Ndani kulikuwa na giza kiasi cha kutotambua kwamba ilikuwa usiku au mchana. Hakukuwa na madirisha kabisa katika kibanda kile.
Dakika ya kwanza tu aliyowekwa Daniel alianza kutafuta namna ya kujiokoa, kutoka ndani ya chumba kile. Hadi leo, siku ya tatu hakuipata. Na wala hakuwa na dalili ya kuipata.
Alidhohofika sana kwa mawazo.
Alidhohofika sana kwa njaa. Sasa alikuwa amelala chini akiwa amekata tamaa. Alikuwa anakisubiri kifo!
Huku akisikitika siyo tu kwa kutozitimiza harakati alizozianzisha duniani. Hapana, alisikitika kwa kutofanikiwa angalau kujua watu wale walikuwa na siri gani wakiyoilinda namna ile. Alikuwa amelala chini huku akikoroma sasa.
Hakuwa na nguvu sasa.
Ndipo likamjia tumaini.
Akakumbuka kitu pekee kinachoweza kumuokoa mahali pale, ni Mungu. Daniel alipiga magoti kwa shida na kuanza kumuomba Mungu. Hakuwa mhudhuriaji kabisa wa nyumba za ibada. Lakini leo alikuwa amekwama kweli. Alimuomba Mungu kitu kimoja tu. Amuokoe katika mdomo wa mauti ili akaitetee nchi yake, akaitete Tanzania, akawatetee waTanzania. Atutetee mimi na wewe. Aliomba ndani ya nusu saa.
Hakikutokea kitu.
Sasa aliamua kulala akiwa amekosa matumaini kabisa. Daniel alimuona malaika mtoa roho akimsogelea!
Alikata mawasiliano na dunia.
Alilala usingizi wa kifo huku akikoroma !
*****
Ni siku ya nne leo mke wa mzee Washiro hakwenda kuchuuza samaki mtaani. Alikuwa anamhudumia mtu aliyemuokota mumewe, Mzee Washiro. Katika mizunguko yake ya kutafuta matunda ya mabungo porini ili akayauze sokoni Bagamoyo apate pesa ya nauli ili aende Arusha kumwangalia mwanae aliyekuwa mikononi mwa Polisi. Mzee Washiro alikutana na kitu cha ajabu.
Ni mwezi sasa tangu mwanae mpendwa, Abdul, alipompigia simu na kumueleza kuwa amepatwa na matatizo makuu huko Arusha. Mwanawe alikuwa amekamatwa Kwa kosa la kumuua mtoto wa makamu wa Raisi wa Zanzibar, Mayasa Ally.
Siku ya tatu baada ya kuacha kazi yake ya uvuvi ambayo aliona inamuingizia pesa pole pole aliamua kuingia msituni kutafuta matunda hayo ya porini na kwenda kuyauza sokoni Bagamoyo. Kidogo ilimpa matumaini biashara hiyo. Sasa alikuwa na akiba ya elfu kumi na tano ndani.
Lakini siku ya nne aliyoenda msituni kutafuta mabungo, hakurudi na mabungo. Alirudi na mwili wa mtu aliyepoteza fahamu!

JE MZEE WASHIRO KUMTOA WAPI HUYO MTU, NA ILIKUWAJE HADI AKAKUTANA NAE, TUKUTANE SEHEMU YA KUMI NA SITA...
 
RIWAYA: ANGAMIZO
MWANDISHI: HALFANI SUDY
SIMU: 0674 395733
WHATSAPP 0757 633010

SEHEMU YA KUMI NA MOJA

ILIPOISHIA JANA
Alikufa kifo kinachofanana na cha Mayasa!. Alikufa kifo kinachofanana na cha Raiya ! . alikufa kifo kinachofanaa na cha afande John. Yule jamaa nae alivuka ngozi! Kumbe yule jamaa alishika ile dawa inayoitwa Proxine pale alipotaka kumsalimia Abdul kwa mkono. Na alivyokuwa anataka kutoa kitu mfukoni alikuwa anataka kutoa dawa nyingine ili ajipake dawa kuzuia madhara ya ile dawa. Lakini alichelewa. Daniel alikuwa anamzuia kwa pigo kila alipotaka kuitoa ile dawa hiyo. Alijua atakufa! Ndomana alianza kulia kabla.
Siku zote mshahara wa dhambi ni mauti!

ISOME YA LEO SASA....
Daniel alimsogelea taratibu na kuanza kumuuliza Abdul kwa upole.
"Kuna kitu wanahisi unacho. Wanataka kukuua ili kisitoke nje. N kitu gani hiko?"
"Mimi sina kitu kaka Daniel. Sijui hata to wananitakia nini ?"
"Kipo kitu Abdul"
"Kitu gani sasa kaka Daniel ?"
"Mayasa alishawahi kukupa kitu chochote enzi za uhai wake?"
"Amewahi kunipa vitu vingi lakini siyo vya kudumu"
"Raiya alikupa nini cha kudumu ?"
"Hamna zaidi ya hii simu "
"Hebu ilete" Akampa.
Daniel aliiangalia ile simu kwa makini. Aliigeuza nyuma. Aliifungua ile simu kule nyuma. Kule inakokaa betri ilidondoka chini karatasi ndogo. Abdul alishangaa sana. Hakuwa ameweka karatasi yoyote kwa kuwa hakuwahi kuifungua simu ile tangu alivyopewa na Raiya. Daniel akaisoma kwa sauti ndogo ile karatasi.
"Kwenye laptop ya mme wangu kuna faili la limeandikwa Siri. Linahusu mpango wa kuangamiza watoto wa viongozi wa nchi hii na mambo mengine mengi ya siri sana . Abdul jaribu kulifikisha suala hili kunapohusika ili kuliokoa Taifa hili "
Abdul alishangaa sana. Sasa alimhusudu sana Raiya. Alimuona ni mtu mwenye akili kuliko mtu yeyote duniani. Raiya kumbe alikufa na siri kubwa sana. Ambayo siri hiyo aliifikisha kwa Abdul kwa siri pia. Abdul alimhusudu zaidi Daniel. Aligundua kitu alichokaa nacho miaka miwili bila kutambua . Alikiri Daniel hakuwa mtu wa karne hii. Alikuwa na akili na uwezo wa ziada.
Daniel alitoka nje na kile kikaratasi. Baada ya dakika kumi na tano waliingia askari wawili kuutoa mwili wa yule jamaa. Daniel alitoka nje kwa nia moja tu. Kumtafuta mume wa Raiya popote alipo. Ilikuwa lazima ampate popote atakapokuwa!
Upande wa kina Avast ilikuwa ni patashika na taharuki kubwa. Ilikuwa yapata saa saba ya mchana sasa, Avira hajarudi. Ilikuwa ajabu. Avira hakuwahi kufanya kazi muda mrefu namna hii. Avira hufanya mambo kwa haraka na kwa uhakika. Hiyo ndio sifa kuu ya Avira. Alitekeleza kazi ya kumuua Raiya robo saa tu alivyoenda magereza. Leo masaa zaidi ya matano alikuwa hajarudi.
Walimsubiri.
Walimsubiri sana.
Hakurudi.
Na hajarudi mpaka leo!.
Daniel alivyotoka palepale moja kwa moja alienda kwa dada yake Raiya. Alienda na kumuulizia mtaa na namba ya nyumba akiyokaa Raiya huko Dar es salaam ilipo. Baada ya kuelekezwa Daniel aliweka 'booking' ya ndege ya kwenda Dar es salaam kesho yake asubuhi.
Aliipata.
Usiku ule ulikuwa mgumu sana kwa Avast na Salehe. Wakaanza kuhisi huenda Avira amekamatwa. Wakawa wanahofia endapo Avira atakuwa kakamatwa anaweza kutoa siri. Siri pekee ambayo hawakutaka itoke ilikuwa kwenye laptop, nyumbani kwa Salehe, Dar es salaam. Wakapanga kesho Avast aende Dar es salaam kuichukua ile laptop. Ili siri isifike mikononi kwa adui
Duuh jmn
 
Back
Top Bottom