Mr RoundAbout
Member
- Oct 6, 2023
- 70
- 85
Ndugu wana bodi, nawasalimu na kuwatakia heri ya Sikukuu ya Noeli na Mwaka mpya 2024.
Ndugu za imenibidi niandike tu suala hili kwani ni zaidi ya mara 4 nimekutana na usumbufu sana katika ofisi za NIDA, Mimi mwenyewe nimehangaika sana kupata kitambulisho changu, yaani kifupi ofisi hii hawajitambui Nini wanachofanya. Iko hivi, Nina mdogo wangu ambaye anaishi South Africa, alizaliwa uingereza kipindi Mzee anafanya PhD kwani alikuwa mwalimu chuo kikuu Cha Dar es salaam, ana passport ya Tanzania hizi mpya aliichukulia ubalozi wa Afrika Kusini,, yaani ni raia wa Tanzania kabisa.
Sasa kaja kula Sikukuu nyumbani, akasema naye apate kitambulisho Cha Taifa maana ni haki yake. Tulienda ofisi mojawapo ya NIDA na fomu zetu zulizokamili. Tulipofika tukapokelewa kama kawaida na kupewa namba, tukaingia ofisi ya uhamiaji mdogo wangu akasainiwa fomu yake katika kipengele Cha Uraia na Afisa wa Uhamiaji baada ya kujiridhisha kuwa ni raia Kwa documents zote zipo. Baada ya hapo tukaambiwa tuende Kwa Maafisa wapiga picha wa NIDA, ndipo tukakutana na mambo ambayo yanashangaza, wakakataa kumpiga picha eti siyo.
Wakati watu wa Uhamiaji ndiyo wanaohusika na suala la uraia walikuwa wamesha mhudumia Kwa kuangalia nyaraka zake. Kimsingi inakera sana ofisi kama hii ya umma inakuwa na watumishi ambayo hawajitambui na hawajui nn Cha kufanya. Nilipokuwa pale nimeona wateja wengi tu wakijibiwa hovyo mpaka wengine kuamua kuondoka.
Nikahisi labda pengine ofisi hii imeshindwa kujisimamia ndiyo maana Mhe Rais, ameiunganisha na RITA, pengine Kwa ukubwa wa RITA itasaidia katika kuboresha huduma ya utoaji wa namba inayofanywa na NIDA.
Ndiyo hayo wanabodi, yaliyotukuta Watanzania wenzenu.