Ripoti ya Utetezi wa Bwawa la Stiegler - Ndiyo Hii? Nimeshindwa Kuisoma...

Mkuu Mzee Mwanakijiji, uzalendo ni pamoja na kuwa na blind faith, kuwa na imani isiotia shaka na matumaini na unaowaamini kwamba wanatupeleka mahala pema hata kama wanatupitisha njia iliyojaa mbigiri, hivyo huna haja kuiosoma na kuielewa muhimu ni kuisoma tuu na kuiamini na sii lazima kuielewa, kama tunavyo mwamini Mungu.
Ujamaa ni imani, aliyepo amekuja kuikamilisha na kuitimiliza ndoto ya Nyerere, tumuaminie na kumpatia kila ushirikiano ili ayaweze katika Yeye amtiaye nguvu.

Heri wewe umeisoma hukuielewa, mimi wala sihitaji kuisoma, nimeisha iamini bila kuisoma kwa kuwaaminia kwa sababu kuhusu Stigler niliisha sema kila kitu hapa
nilisema

Uzalendo wa kweli wa nchi yako ni pamoja na kusupport mipango kamambe
ya maendeleo ya nchi yako hata kama mipango hiyo itasababisha maumivu kwa walio wengi as long as itakuwa na faida kubwa kitaifa huko baadae.
P
 
Mzee Mwanakijiji huwa unawaamini sana wataalamu kutoka Ulaya kwa ripoti zao zilizopambwa?

Oh noooo.. siwaamini kabisa... nawasoma kwa umakini na nauliza kila assumption wanayotoa. Binafsi nilitarajia ripoti hii isiwe ye kisiasa kabisa; ingedeal na facts na facts tupu. Na pale inapotoa mahitimisho basi yatolewe kutokana na facts zilizopo. Siasa waachiwe wanasiasa. Binafsi kama mtu ambaye naunga mkono ujenzi wa bwawa hili hoja za umuhimu, ulazima na uharaka wa kujenga bwawa hili zinasimama peke yake bila kuhangaika na kujibu hoja za watalaamu wa "Ulaya". Unajua kuwa 2 + 2 ni 4. Haijalishi anayejumlisha ni Mchina, Mtumbatu, au Mdigo. Tunaweza kutofautiana kwenye mbili za "nini" na mbili za "nini" zinajumlishwa.
 
Hawa waandishi wana utaalam wowote wa Mazingira?
Nimejaribu kuangalia 'References' walizoweka nione kama wanayo maandishi yoyote katika eneo hilo, sioni hata mmoja wao ambaye maandishi yake yalishachapishwa katika eneo hilo, sikumwona hata mmoja.
LIcha ya hivyo, ningependa kujua competencies zao ni nini... kwa mfano, nimeona jina la Dkt. Kashililah.. ninadhania ni yule yule aliyekuwa Bungeni siyo? Hawa wataalamu wengine ni wabobezi wa maeneo gani ya kitaaluma?
 
Mr slowly ndo kandika. kila jambo awamu hii imekua politicized,,ni ujïnga mtupu
 
Mkuu Mzee wanavillage kutetea uongo na uzandiki ni kazi kubwa sana, lazima utaandika ugoro tu

"Siasa za mabunduki ni ushamba"
 
Hawa waandishi wana utaalam wowote wa Mazingira?
Nimejaribu kuangalia 'References' walizoweka nione kama wanayo maandishi yoyote katika eneo hilo, sioni hata mmoja wao ambaye maandishi yake yalishachapishwa katika eneo hilo, sikumwona hata mmoja.
Mkuu Kalamu, Tanzania ya sasa
hatuhitaji references za wataalamu wazungu katika ripoti zetu za kitaalamu, ripoti zetu sasa zinazingatia uzalendo, maadamu tumeamua kujenga mradi wa HEP wa Stigler, then ripoti zetu zitareflect our political wishes, nakumbuka kwenye hili tulikutana hapa na wote sisi mimi name wewe tulichangia page ya kwanza, ulianza wewe kuchangia post No. 5, nikaja mimi post No.8

Uzalendo wa kweli wa nchi yako ni pamoja na kusupport mipango kamambe
ya maendeleo ya nchi yako hata kama mipango hiyo itasababisha maumivu kwa walio wengi as long as itakuwa na faida kubwa kitaifa huko baadae.
P
 

Mipango kamambe haihitaji kuchezwa mdundiko, kujieleza yenyewe na wengi kama si wote wanaikubali. Kuna tofauti ya kuwa mfurukutwa na mfirigiswa
 
Ndugu hapo sio swala la ubora wa elimu tu! pia wataalam kutaka kumfurahisha mtawala maana aliepoa anataka kusikia anachopenda tu
 
"WATAALAMU" ndio wametufikisha hapa,Ndio hao walioingia mikataba ya KICHIFU MANGUNGO na kuliingiza taifa hasara ya matrilioni.....Naungana na wewe na mimi siisomi hiyo ripoti ya kitaalamu.
 
Sasa mkuu kama unasema hujaisoma yote then unaiponda na mbaya zaidi bila hata kutoa hoja za uchambuzi wa taarifa yenyewe! Lakini si shangai inasemekana watz ni wavivu wa kusoma sana vitu vya maana ila kwa udaku hawajambo. Acha siasa isome kwanza then njoo na hoja za kuipinga za kiuchambuzi siyo blabla tu mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…