Mradi wa Bwawa la Nyerere tulijilisha upepo au ndiyo mwendelezo wa siasa chafu za kibepari?

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,783
Wazungu husema hivi "Once is an accident, Twice is a Coincidence, but Thrice is a Pattern".

Hapa namaanisha nini, duniani kote ambako miradi ya namna hii yenye lengo la kuwakwamua wananchi kwenye lindi la umasikini lazima kuwepo na malalamiko.

Tena nimefuatilia kwa umakini na kufahamu kwamba malalamiko hayo ni lazima yafanane. Mbaya zaidi makundi ya wanaoleta haya malalamiko huwa ni ya watu wa aina ileile, tena huja na sababu zilezile.

Ukifuatilia kwa umakini, utatambua kwamba mfanano wa hawa watu ni mkubwa sana hadi utakubaliana na ule msemo wa kiingereza kwamba "History does not repeat itself, but people do repeat themselves".

Fanya utafiti wako binafsi, utakubaliana na nilichokiandika hapa.

Muda ni mchache, leo hii ntazungumzia nchi tatu ambazo ni Marekani, Ethiopia na Tanzania. Ambako kote katika nyakati tofauti kumekuwa na miradi mikubwa ya kuzalisha umeme wa maji ambao kwa mkono wa serikali, ambayo imelenga kuzalisha umeme wa gharama nafuu kwa wananchi huku miradi hiyo ikiendeshwa na serikali.

Hapa nazungumzia miradi ya The Tennessee valley Hydro-electric Power Projects (TVA), The Grand Ethiopian Rennaisance Dam (GERD) na Julius Nyerere Hydro- Power Project (JHPP).

Nimefuatilia kwa karibu nimeona kwenye hii miradi ya TVA, GERD na JNHPP ni lazima utakutana na majina kama WHITE-ELEPHANTS, DEBT-RIDDEN PROJECTS, UNSUSTAINABLE ENERGY SOURCE, ENVIROMENTAL HAZARDOUS, GOVERNMENT MONOPOLY, UNCOMPETITIVE SOEs na SOCIALIST EMBARKED PROJECT.

Mpaka sasa sijafahamu kwanini tokea kule Marekani, Ethiopia hadi Tanzania mambo yafanane hivi. Imetokea TVA (Once=An Accident), Imetokea GERD (Twice= A Coincidence) na Imetokea Tanzania (Thrice= A Pattern).

Pia sehemu nyinginezo yanaendelea kutoka tu, mpaka najiuliza nini hiki. Labda, huenda ni mawazo yangu hafifu tu, ambapo wazungu husema "A figment of your own imagination"

HEBU TUANGALIE MRADI WA UMEME CHINI YA TENNESSEE VALLEY AUTHORITY

Raisi Franklin Delano Roosevelt alianzisha The Tennessee Valley Authority (TVA) mwaka 1933 ili kuwezesha Marekani izalishe umeme wa bei ndogo ambao utasaidia majimbo kama saba ambayo yanazunguka lile eneo.

Lengo kubwa ni kusaidia kiuchumi ukanda ambao uliachwa nyumba kimandeleo, kutoa ajira kwa vijana na kusukuma uchumi wa viwanda eneo hilo.

Tokea mwaka 1933 mpaka sasa Marekani imefanikiwa kutengeneza mabwawa 50 ambayo yanasaidia kuzalisha umeme wa bei ndogo unaotumika kuendesha viwanda na uchumi wa majimbo karibia saba ya eneo ambalo bonde la Tennessee limepita.

Ila huwezi amini mpaka leo hii mwaka 2022, wanaharakati wa kimazingira wanapinga huu mradi kwa kusema unaleta madhara.

Wakati nasoma shule kuhusu huu mradi, tuliambiwa kwamba ulipigwa vita sana na makampuni binafsi ya umeme, wanasiasa, wanaharakati na wanasheria.

Ambapo walitumia mbinu mbalimbali kufanikisha hujuma dhidi ya huu mradi lakini hawakufanikiwa. Sababu kubwa ni kwamba raia wengi wa Marekani walikuwa ni watu wanaojielewa mno, siyo wajinga wanaopelekeshwa bila kufahamu linaloendelea (Dumbed-Down Citizenry) nchini kwao.

Upinzani haukishia kwenye uanzishwaji wa huu mradi mwaka 1933, mwaka 1936 mmoja wa wamiliki wa hisa kwenye kampuni binafsi la umeme THE ALABAMA POWER COMPANY aitwaye ASHWANDER alipeleka kesi mahakamani kuzuia serikali kuuza umeme kupitia The Tennessee Valley Authority (TVA) akisema kwamba serikali haitakiwi kabisa kuuza umeme hivyo kuna uvunjifu wa katiba ya Marekani.

Unaweza kutafuta kesi ya: Ashwander V Tennessee Valley Authority (1936)

Mahakama ya juu ya Marekani ilikataa na kusema uzalishaji huu wa umeme siyo wa faida tu, bali ulilenga kutoa huduma kwa kukuza uchumi wa eneo ambalo lilikuwa nyuma kimaendeleo na kuimarisha ulinzi wa nchi kwasababu viwanda vya silaha vilikuwepo eneo hilo.

Hivyo mabwanyeye wakapigwa chini na serikali inauza umeme kwa raia mpaka leo hii. Ikumbukwe inayofanya hivi ni serikali ya Kibeberu ya ulimwengu wa kwanza na siyo serikali ya Kijamaa ya ulimwengu wa tatu.

Wamarekani zaidi ya milioni 9 wanapata huduma ya umeme nafuu kutoka kwenye miradi 29 ya umeme wa maji kutoka Tennessee Valley Authority (TVA).

Kubwa zaidi ni kwamba huduma ya umeme kwenye majimbo hayo yanayopitiwa na bonde la Tennessee ni moja kati ya umeme wenye gharama nchini Marekani, kama siyo ndiyo wenye gharama nafuu zaidi kwenye nchi hiyo.

Kitakachoshangaza watu werevu ni kwamba PROPAGANDA CHAFU na UZANDIKI dhidi ya mradi huu hazijaisha tokea mwaka 1936. Raisi Dwight Eisenhower alishawahi kuutukana huu mradi kwa kuuita maneno kama "Ujamaa nyemelevu" (Creeping Socialism), ilhali mamilioni ya Wamarekani ni wanufaika.

Maneno kama haya hayatakiwi kabisa kutoka kwenye kinywa cha mkuu wa nchi mwenye lengo la kuwakwamua kiuchumi raia wa kawaida, kwasababu faida za mradi ni dhahiri kwa watu wote.

Lengo la Raisi Eisenhower lilikuwa siyo kupinga UJAMAA bali ni kubinafsisha (TVA), lakini akakumbana na upinzani mkubwa kutoka kwa wazalendo wa kimarekani na mwishowe akawa mpole.

Kilichomshangaza zaidi ni kwamba waliompinga ni wenzake kutoka REPUBLICAN PARTY ambao husifika kwa kuchukia UJAMAA hasa pale ambapo serikali yenyewe hufanya biashara. Nini kilipelekea Raisi na jopo la wataalamu wake kupingwa hivi ???

Sasa kubwa na baya zaidi dhidi ya mradi huu ni lile la mwaka 2013, ambapo Raisi Barrack Obama aliandaa muswada ili kubinafsisha The Tennessee Valley Authority (TVA) kwa watu binafsi.

Moja ya sababu kubwa ambayo Raisi Obama na washauri wake waliitoa ni kwamba mamlaka ya Tennessee Valley (TVA) ina madeni makubwa ambayo ni mzigo kwa serikali.

Walikuwa na hoja nzito sana maana ukweli ni kwamba mamlaka hiyo (TVA) ina madeni makubwa ambayo ni takribani dola za kimarekani bilioni 25.

Lakini hili halikuwa sababu ya kusema kwamba serikali ibinafsishe shirika hili la kiserikali na kuwaumiza raia wapatao milioni 9 kwa kupanda kwa gharama za umeme.

Sababu ya pili ambayo Raisi Obama na washauri wake waliitoa ili kufanikisha ubinafsishwaji wa The Tennessee Valley Authority (TVA) ni ile ambayo hata kwetu huku inatusumbua ya kutunza mazingira.

TVA mbali na miradi 29 ya umeme wa maji, imeongeza pia miradi 12 ya umeme wa makaa ya mawe, miradi 3 ya umeme wa nyuklia, miradi 15 ya umeme wa gesi na mradi 1 wa umeme wa upepo.

Inasemekana TVA inahitaji dola za kimarekani bilioni 25 ili kupunguza uchafuzi wa mazingira unaosababisha na huu mradi hasa kutoka kwenye vinu vya makaa ya mawe. Hivyo ili serikali isiingie kwenye hizi gharama zisizo za msingi, basi ni kheri ibinafsishe tu shirika hili.

Kuna nchi fulani hivi viongozi wake, wasomi na wafanyabiashara wanapenda kuzungumza kauli kama hizi za Raisi Barrack Obama na Dwight Eisenhower, bila shaka ndugu msomaji utakuwa unaifahamu.

Hivyo njia rahisi kwa Serikali ya Raisi Obama, kukwepa deni kubwa la TVA na gharama za marekebisho, wakaona ni bora wauze hii SOE (State Owned Enterprise).

Ila ukweli mchungu ni kwamba wangefanya hivyo ina maana gharama za umeme kwa wananchi wa Marekani zaidi ya milioni 9 ingepanda sana na wangeathiri biashara nyingi na maisha ya raia wa kawaida.

Mbali na madhaifu yake mengi, Marekani ni taifa ambalo raia wake wengi wanajielewa mno.

Wahafidhina wa chama cha REPUBLICAN hasa wawakilishi kutoka majimbo hayo, pamoja na watu binafsi walipinga kwa nguvu mswada ambao ungefanikisha ubinafsishwaji wa kiholela wa hii mamlaka ambayo lengo lake kuu ni kutoa huduma kwa raia na kuimarisha ulinzi wa nchi.

HEBU TURUDI NCHINI TANZANIA SASA, TUANGALIE TANESCO NA JNHPP

Bunge la Marekani lilichofanya ni kukataa mamalaka isiuzwe na kuiwekea ukomo wa deni, ambayo mamlaka haitakiwi kuvuka, ambapo ukomo ni dola za kimarekani bilioni 30.

Hivyo madeni hayapo tu kwenye shirika letu la TANESCO lakini hata TVA wana madeni tena yanakera. Sisemi haya kusema TANESCO inafanya vizuri, la hasha kuna mambo mengi ya ajabu yanafanyika.

Lakini naamini wakijipanga vizuri na kupunguza siasa tunaweza kufika sehemu nzuri sana. Mbona TVA wafananya vizuri na bado ni shirika la serikali ???

Jambo jingine ambalo nalisikia sana nchini Tanzania ni hilo la kusema umeme wa maji siyo endelev. Mimi siyo mtaalamu lakini naweza kufahamu wapi nadanganywa, kiukweli hili linanipa ukakasi mkubwa sana.

Mradi wa TVA umeanza mwaka 1933 na upo hadi leo hii, utasemaje kwamba umeme wa maji siyo endelevu jamani ???

Unaweza kumtukana Raisi Magufuli kwamba ni mjinga, lakini kumbuka huu mpango wa JNHPP umekuwepo tokea enzi za Mzee Nyerere, Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa, ina maana hawa wote na wataalamu wao walikuwa ni wajinga kabisa wasitambue kwamba Hydro-Electric Power is not sustainable source of energy ??? Aidha ni kweli sisi watanzania ni watu wajinga sana pamoja na viongozi wetu, AU kuna kitu kinachoendelea nyuma ya pazia sisi raia wa kawaida hatukioni.

Jambo kubwa zaidi la kujiuliza hapa: Ni kwamba kama mradi wa TVA ambao manufaa yake yanaonekana kwa mamilioni ya wananchi wa Marekani unapigwa vita kali hivi, tena hadi na viongozi wa serikali wakiwemo maraisi, sisi huku kwetu Tanzania tusipingwe kweli ???

Mwaka jana miezi ya mwishoni nilikuwa nafuatilia wanaharakati mitandaoni, nikasikia baadhi wakisema mamilioni ya miti yamekatwa na uharibifu mkubwa wa mazingira umefanyika kwenye mradi wa JNHPP ndiyo maana mvua zimegoma Tanzania.

Lakini, wengine wanasema kwamba JNHPP ni tembo mweupe (A White Elephant Project). Majibu ya Waziri Makamba, yamakuwa yakibadilika-badilika. Lakini naamini, ukweli tutaufahamu tu.

Wanaharakati wetu wangepinga huu mradi (JNHPP) peke yake sisi tungeelewa labda na binafsi ningesema hebu tujifanyie tathmini. Lakini hakuna mradi wowote mkubwa ambao umewahi kufanyika nchini Tanzania bila kupata upinzani mkubwa:

Uwe ni mradi wa msaada, uwekezaji au mkopo. Nasema hili kwa UJASIRI WOTE, kama upo naomba nitajiwe ili nijifunze.

Ukifuatilia kinachoendelea kwa wanasiasa wetu kuna sababu nyingi sana zinazoletwa ambazo hazina kichwa wala miguu.

Wengi wetu ni UJINGA, WOGA, BENDERA FUATA UPEPO lakini kubwa ni ULAJI TU wa watu wachache ambao wamevaa ngozi ya kutunza mazingira, kulinda katiba, matumizi ya mbinu za kisasa za kisayansi na kibiashara kuendesha sekta ya nishati nchini. Lakini ni hivi: UKWELI UKO KAMA MIMBA, HUWEZI KUUFICHA MILELE. Tutafamu tu...

NAMALIZIA NA ETHIOPIA, MRADI WA THE GRAND ETHIOPIAN RENNAISANCE DAM

Ingekuwa Tanzania ndiyo nchi pekee ndiyo inayopigwa vita kwa kuanzisha mradi kama huu ningesema, basi tujifanyie tathmini kidogo.

Ila hadi kule kwa ndugu zetu Ethiopia yametokea machafuko makubwa sana kupinga uanzishwaji wa The Grand Ethiopia Rennaisance Dam (GERD) ambalo litakuwa msaada mkubwa sana kwa mamilioni ya wahabeshi nchini humo.

Upinzani umekuwa mkubwa imefika kipindi kwamba Raisi wa Marekani Donald Trump akaweka bayana kabisa kwamba Misri inaweza kulipua bwana hilo" Egypt might blow up the dam".

WIKILEAKS wanasema kwamba, mradi huu ukimalika hautaisaidia Ethiopia peke yake kuzalisha umeme wa bei ndogo, bali utazalishwa umeme mwingi (Megawatts 5,250) ambao utauzwa hadi nchi jirani kama Sudan na serikali ya Sadani inafahamu hili vizuri kabisa.

Sasa ukifuatilia kwa umakini, kuna wanasiasa wakubwa ambao walisema wazi kwamba mradi wa GERD, hauna manufaa na ni tembo mweupe ( A WHITE ELEPHANT). Moja kati ya watu waliowahi kusema hivi ni Raisi Isaias Afwerki wa Eritrea.

Lakini mradi huu ukikamilika, umeme wa gharama nafuu utafika hadi nchini kwake. Watanzania tujiulize kitu hapa: Kama umeme wa maji siyo wa muda mrefu (Not Sustainable), hivi iweje serikali ya Uchina itupe zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 1, ambazo ni sawa na trilioni mbili za kitanzania au zaidi kwenye mradi ?

Asasi za kiraia (NGOs) nazo haziko nyuma katika kutuonesha madhara ya mradi huu wa GERD. NGO maarufu iitwayo INTERNATIONAL RIVERS kutoka California, nchini Marekani iliandaa ripoti kubwa kabisa kuonesha madhara ya mradi huo kwenye mazingira. Wakaenda mbali zaidi na kusema kwamba bwana hili linaweza kuchangia mabadiliko ya hali ya nchi.

Ikumbukwe hawa ndugu zetu wamezungumza sana juu ya miradi ya umeme wa maji nchini Tanzania na Ethiopia.

MWISHO KABISA: MAONI YA WANAZUONI KUHUSU SIASA ZA UMEME NA MABWAWA

Kama umefuatilia siasa za Afrika kwa muda mrefu, utatambua kwamba huu mchezo haujaanza na Tanzania wala Ethiopia. Prof Mike Muller ambaye ni mhandisi kutoka chuo cha Witswatersrand Afrika Kusini, amawahi kuandika na kusema siasa za kupinga miradi mikubwa ya umeme wa maji zilianza mapema nchini Misri kipindi cha Gamal Abdi Nasser ambapo alitaka kujenga bwawa la Aswan (ASWAH HIGH DAM) ambalo lingezalisha MegaWatts 2,100.

Prof Asit K. Biswas amtaalamu wa maji na mazingira, ambaye ndiye anaongoza kwa kufanyiwa rejea za kitaalamu linapokuja suala za mazingira na maji, akishirikiana na Prof Cecilia Tortajada waliandika chapisho ambalo limesema kwamba mradi wa BWAWA LA ASWAN una madhara makubwa kwenye mazingira.

Lakini ukweli ni kwamba wataalamu mradi huo ulipokamilika mwaka 1970, ulikidhi nusu ya mahitaji ya umeme nchini Misri.

Ikimbukwe kwamba siasa za ASWAN HIGH DAM ziliwahi kupelekea Misri ivamiwe kijeshi na Uingereza, Ufaransa na Israeli. Nasser alisema alitaifisha Mfereji wa Suez kwasababu maji yake ni muhimu kwa ujenzi wa bwawa la Aswan.

Nasser aliomba msaada kwa serikali ya Raisi Eisenhower ili kujenga bwana la Aswan, lakini Eisenhower aligoma.

Raisi Kennedy alikosoa sana haya maamuzi ya kuvuruga miradi ya Afrika akisema hivi "When we abruptly abandoned the Aswan Dam in Egypt, the Russians went ahead to finance it. While we starve the Development loan Fund, the Sino-Soviet bloc has already passed us in economic assistance to selected key areas" Hili ndilo lilitokea bwawa lilijengwa na Warusi.

Maajabu barani Afrika huwa hayaishi kabisa: Kinachotushangaza wengi wetu leo hii ni kwamba Misri ambao miaka ya nyumba walionewa katika kujengwa bwawa la Aswan (ASWAN HIGH DAM), leo hii wao nao wakishirikiana na mataifa makubwa nje, wanaharakati na asasi kubwa za kiraia, wanafanya hujuma kubwa sana dhidi ya mradi wa GERD nchini Ethiopia.

NB 1: Siasa kama hizi, zilionekana pia kule nchini GHANA kipindi cha marehemu Nkhrumah ambapo alikuwa anataka kujenga bwawa la AKASOMBO (The Akasombo Dam) ili kuzalisha umeme.

Uliundwa mtandao mkubwa sana wa watu ndani na nje ya nchi ili kumzuia. Muda ni mchache sana siwezi kuzungumza kilichotokea.

NB 2: Fanya utafiti wako kuhusu miradi mikubwa ya uzalishaji wa umeme kupitia maji (TVA, GERD, JNHPP) pia hata ASWAN HIGH DAM na AKASOMBO DAM utatambua kwamba siasa zake zinafanana.

Wahusika ni walewale, wakitumia mbinu zilezile, sema tu huja wakiwa wamevaa vingago (Masks) tofauti-tofati. Kiufupi hizi siasa zinachezwa sana kitaalamu na wengi wetu tunafuata upepo bila kufanya tafiti binafsi.

Mimi siyo mtaalamu sana wa haya mambo, hivyo naomba wale wajuvi wanisaidie zaidi kuelewa. Nitafurahi kurekebishwa na kuelekezwa pale ambapo nimepotoka na kutofahamu kinachoendelea.

CC: JokaKuu , Nguruvi3 , UmkhontoweSizwe , TUJITEGEMEE
 
Mkuu MALCOM LUMUMBA muda huu hata tukijadili ujinga wa Magufuli ni kupoteza muda, hata tujadili athari bado nikupoteza muda..labda for refreshment tu!

Swali langu! Huu mradi utakapokamilika na kukabidhiwa kwa Tanesco, je, watarecoop costs za investment ili wananchi wapungukiwe na mzigo wa kodi au ndio watakabidhiwa at zero cost.. wavujajasho tuendelee kumenyeka?
 
Tukipata umeme wa kuaminika na bei nzuri inatosha, cost za investment tutalipa tuu maana hata sasa kila kona ni tozo tuu na hakuna umeme wa maana
 
Mkuu MALCOM LUMUMBA muda huu hata tukijadili ujinga wa Magufuli ni kupoteza muda, hata tujadili athari bado nikupoteza muda..labda for refreshment tu!

Swali langu! Huu mradi utakapokamilika na kukabidhiwa kwa Tanesco, je, watarecoop costs za investment ili wananchi wapungukiwe na mzigo wa kodi au ndio watakabidhiwa at zero cost.. wavujajasho tuendelee kumenyeka?
Mkuu Paul Alex, umeniuliza swali la ndani ambalo binafsi ziwezi kulifahamu kabisa. Suala zima la Recuperation of investment costs au Zero-Cost ni suala la kisera ambalo nadhani serikali haijaliweka bayana. Hivyo sintalizungumzia kabisa.

Jambo ambalo binafsi nataka kulielewa hapa ni kwanini siasa nyingi inatumika kutaka kutuaminisha kwamba huu mradi hauna faida muhimu kwa Tanzania kama ilivyokadiriwa, ilhali sehemu nyingine duniani miradi kama hii imefanikiwa: Tatizo ni nini hapa?

Kumbuka: Huu mradi haukuanza na Rais Magufuli.
 
Umeandika vizuri sana kuonyesha kupingwa kwa miradi kama hii sio kitu cha ajabu na hakijaanza leo, tukomae tuu umeme uje mengine tutarekebisha, hope lile winch limefika na lile shimo bovu alilosema Makamba wamemaliza, ukiangalia vizuri tatizo kubwa la umeme Tanzania ni la kujitakia tuu na issue ni kubwa ni monopoly waliyopewa TANESCO, tumekuwa watumwa wa sheria zetu wenyewe
 
Umeandika mengi lakini umejichanganya sana.
Tafuta wataalamu wa haya masuala wakusaidie.
Kuna factors (moderating and mediating factors) nyingi umeziweka constant.
Umeme wa maji ni mzuri lakini si rafiki wa mazingira!
 
Kwenye aya za mwanzo kabisa za uzi wangu nimezungumzia GOVERNMENT MONOPOLY. Hebu naomba utueleweshe TANESCO's MONOPOLY inasababishaje tatizo la uhaba wa nishati ya umeme nchini na tutumiea mbinu ipi kulitatua tatizo.
 
Mkuu MALCOM LUMUMBA muda huu hata tukijadili ujinga wa Magufuli ni kupoteza muda, hata tujadili athari bado nikupoteza muda..labda for refreshment tu!

Swali langu! Huu mradi utakapokamilika na kukabidhiwa kwa Tanesco, je, watarecoop costs za investment ili wananchi wapungukiwe na mzigo wa kodi au ndio watakabidhiwa at zero cost.. wavujajasho tuendelee kumenyeka?

Miradi kama hii haipimwi kwa financial viability. Kuna vigezo zaidi ya hivyo. Angalia kwenye nyanja za kiuchumi na kijamii. Kuna internal rate of return kubwa sana for time infinity.

CC: MALCOM LUMUMBA
 
Umeandika mengi lakini umejichanganya sana.
Tafuta wataalamu wa haya masuala wakusaidie.
Kuna factors (moderating and mediating factors) nyingi umeziweka constant.
Umeme wa maji ni mzuri lakini si rafiki wa mazingira!
Mkuu, mimi siyo mtaalamu. Nachotaka kueleweshwa ni kwamba kwanini sehemu nyingine duniani kama Marekani na Misri madhara kwenye mazingira yasiwepo, lakini yawepo tu nchini Tanzania. Naomba unidadavulie zaidi nipate kufahamu.......
 
Hii ni Blog siyo library. Usitegemee watu wakae hapa saa nzima wanasoma thrd yako. Kwani shuleni hukufunzwa kuandika abstract? brevity? Kutuletea maelezo yote haya ni uzembe wako.
 
Mimi ni mmoja kati ya watu waliopinga huu ila sio kwasababu hauna faida!
Faida zipo ila;
1. Mradi huu haukua kwenye power master plan ya mpaka 2050. Kuna miradi ilikuwepo na ingeweza kugenerate hizo megawatts au zaidi. Hazikutolewa sababu za kuiacha hiyo miradi ambayo naona ingediversify risk.
2. Selous ilikuwa kwenye list ya world heritage sites, tungeweza kuendelea kufaidika na utalii na vivyo hivyo kuitumia kupata funds za kuboresha miradi iliyokuwa kwenye master plan, of which hii ingekuwa cheap means of financing kufikia same goals.
3. Kuna research zimefanyika kuonyesha environmental side effects za hiyo project ...na kama unavyojua research hujibiwa kwa research..ila hapa research zilijibiwa kwa siasa.

Ikikupendeza usiturudishe kwenye hii mijadala..
Mwache mwendazake apumzike kama alikuwa amepumzika!
Mkuu Paul Alex, umeniuliza swali la ndani ambalo binafsi ziwezi kulifahamu kabisa. Suala zima la Recuperation of investment costs au Zero-Cost ni suala la kisera ambalo nadhani serikali haijaliweka bayana. Hivyo sintalizungumzia kabisa.

Jambo ambalo binafsi nataka kulielewa hapa ni kwanini siasa nyingi inatumika kutaka kutuaminisha kwamba huu mradi hauna faida muhimu kwa tanzania kama ilivyokadiriwa, ilhali sehemu nyingine duniani miradi kama hii imefanikiwa: Tatizo ni nini hapa ???

Kumbuka: Huu mradi haukuanza na Raisi Magufuli.....
 
Mimi ni mmoja kati ya watu waliopinga huu ila sio kwasababu hauna faida!
Faida zipo ila;
1. Mradi huu haukua kwenye power master plan ya mpaka 2050. Kuna miradi ilikuwepo na ingeweza kugenerate hizo megawatts au zaidi. Hazikutolewa sababu za kuiacha hiyo miradi ambayo naona ingediversify risk.
2. Selous ilikuwa kwenye list ya world heritage sites, tungeweza kuendelea kufaidika na utalii na vivyo hivyo kuitumia kupata funds za kuboresha miradi iliyokuwa kwenye master plan, of which hii ingekuwa cheap means of financing kufikia same goals.
3. Kuna research zimefanyika kuonyesha environmental side effects za hiyo project ...na kama unavyojua research hujibiwa kwa research..ila hapa research zilijibiwa kwa siasa.

Ikikupendeza usiturudishe kwenye hii mijadala..
Mwache mwendazake apumzike kama alikuwa amepumzika!
Mtu kama wewe hujui maana ya mazingira. Nenda kasome taarifa ya Three gorges dam ya China. What is Selous? What is that useless master plan? Hiyo waliyojaza umeme wa solar? Miaka yote ya Tanesco ya Ngereja, Muhongo, etc. ulitegemea iandike master plan ya maana?
 
Mimi ni mmoja kati ya watu waliopinga huu ila sio kwasababu hauna faida!
Faida zipo ila;
1. Mradi huu haukua kwenye power master plan ya mpaka 2050. Kuna miradi ilikuwepo na ingeweza kugenerate hizo megawatts au zaidi. Hazikutolewa sababu za kuiacha hiyo miradi ambayo naona ingediversify risk.
2. Selous ilikuwa kwenye list ya world heritage sites, tungeweza kuendelea kufaidika na utalii na vivyo hivyo kuitumia kupata funds za kuboresha miradi iliyokuwa kwenye master plan, of which hii ingekuwa cheap means of financing kufikia same goals.
3. Kuna research zimefanyika kuonyesha environmental side effects za hiyo project ...na kama unavyojua research hujibiwa kwa research..ila hapa research zilijibiwa kwa siasa.

Ikikupendeza usiturudishe kwenye hii mijadala..
Mwache mwendazake apumzike kama alikuwa amepumzika!
Nashukuru mkuu, lakini naomba kujuzwa kidogo kuhusu hiyo Power-Master Plan 2050.

1. Iliandaliwa lini ?

2. Utekelezaji wake ulifikia wapi hadi kufika mwaka 2015 ?

3. Nchi inakusudia kupata Mega-Watts ngapi hadi kufika mwaka 2050 ?

4. Ni miradi mingapi mikubwa ambayo inge-diversify risk ambayo iliachwa kisa JHNPP ?

5. Serikali ya awamu ya sita bado ina mpango wa kuendelea na hiyo Power-Master Plan 2050 ?
 
Back
Top Bottom