Ripoti ya Utetezi wa Bwawa la Stiegler - Ndiyo Hii? Nimeshindwa Kuisoma...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Tumesikia na kusoma juu ya uzinduzi wa "ripoti ya wataalamu" wazalendo. Mimi binafsi naunga mkono ujenzi wa bwawa hili na nilikuwa miunngoni mwa watu waliofurahia sana kuwa hatimaye hili linafanyika... Lakini si kwa utetezi unaojaribiwa kwenye ripoti hii. Nimejaribu kusoma lakini sikufika mbali...

Ila inaitwa ni ya "wataalamu"... seriously... Ningekuwa na kaudikteta kadogo tu Ningeagiza watalaamu hawa wote waende Butimba angalau kwa mwezi mmoja... Kama wangeita ni "utetezi wa kisiasa".. nisingekuwa na matatizo nayo hii ripoti... lakini kuiita ni ya "kitaalamu".. basi neno "utaalamu" limepoteza maana...
 
Attachments

  • UTETEZIWASTIEGLERS.pdf
    3.9 MB · Views: 92
What do you expect when “wataalamu” were picked from garbage dumping area!?

Tumesikia na kusoma juu ya uzinduzi wa "ripoti ya wataalamu" wazalendo. Mimi binafsi naunga mkono ujenzi wa bwawa hili na nilikuwa miunngoni mwa watu waliofurahia sana kuwa hatimaye hili linafanyika... Lakini si kwa utetezi unaojaribiwa kwenye ripoti hii. Nimejaribu kusoma lakini sikufika mbali...

Ila inaitwa ni ya "wataalamu"... seriously... Ningekuwa na kaudikteta kadogo tu Ningeagiza watalaamu hawa wote waende Butimba angalau kwa mwezi mmoja... Kama wangeita ni "utetezi wa kisiasa".. nisingekuwa na matatizo nayo hii ripoti... lakini kuiita ni ya "kitaalamu".. basi neno "utaalamu" limepoteza maana...
 
Huu uchafu (ripoti) kwakweli unachekesha sana. Ni kama imeandikwa na wahuni kutokea jumuiya ya vijana ya CCM.

Wasomi wa PhD na wataalam hawaandiki hivi. Hii kamwe siyo ripoti ya kitaalam wala paper ya wasomi wa PhD.

Serikali ijitenge na hii ripoti. Kwa kuwa kama itachukuliwa na kufanywa ndiyo justification ya kuendelea na mradi tutaacha kumbukumbu mbaya kabisa kwenye nchi hii.

Hata hao wanaochambwa humo kwa vimaneno vya kwenye khanga, watatuona sisi wote ni vichaa.
 
Nina uhakika hawa jamaa wangemuomba hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDSM angeweza kuwaandikia karipoti kenye mwelekeo kidogo wa ripoti ya kisomi...
 
NI ya wataalamu kama ile ya Makinikia iliyoonesha, endapo Acacia wasingetuibia madini yetu, Tanzania ingekuwa ndie top gold producer duniani, na kuhitimisha tunawadai USD 190 Billion wakati Market Capitalization ya kampuni husika haifiki hata USD 5 Billion!!!

Serious note: Hivi kuna mtu anaweza kunifanyia mpango wa passport ya Kenya, manake hivi sasa najisikia aibu mimi kuingia nchi za watu na Passport za Tanzania! Haki ya Mungu hii sitanii! Kuna siku nimeshuka airport ya nchi fulani, lakini ghafla watu wakaanza kunitazama mara baada ya kutoka kwenye cube ya passport control. Yaani nahisi kama yule afisa aliwakonyeza watu kuwaambia "...mnamuona yule, jamaa ni Mtanzania, ile nchi inayoidai kampuni ya madini USD 190 Billion wakati mapato ya nchi yake kwa mwaka hayafiki hata USD 15 Billion"!

No wonder Jiwe hataki kwenda ughaibuni!
 
Ila inaitwa ni ya "wataalamu"... seriously... Ningekuwa na kaudikteta kadogo tu Ningeagiza watalaamu hawa wote waende Butimba angalau kwa mwezi mmoja... Kama wangeita ni "utetezi wa kisiasa".. nisingekuwa na matatizo nayo hii ripoti... lakini kuiita ni ya "kitaalamu".. basi neno "utaalamu" limepoteza maana...
Tunaposema elimu yetu imedidimia kiasi cha kutisha hatueleweki.

Lakini sasa inajionyesha kwamba sio katika elimu pekee ndiko tuliko kwisha. Chukua nyanja nyingine yoyote ile, michezo, siasa, utamaduni, n.k. ambako unaweza kusema tuna nafuu huko. Pengine kudhoofika katika haya nako kunaanzia kulekule kwenye elimu mbovu. Kwa sababu tunakosa misingi ya kuyafanya yote haya, misingi ambayo inatokana na elimu nzuri.

Vyuo vyetu vikuu na wasomi walioko huko. Hebu tafuta machapisho yanayotoka katika vyuo hivyo, hasa katika maeneo ya Sayansi, Uhandisi, na teknologia. Tafuta machapisho katika "journals" zinazotambulika duniani uhesabu ni ngapi zinatokana na wasomi wetu. Sokoine walikuwa wameinuka kidogo hapo siku za nyuma, siku hizi hata wao ni shida tupu!

Siasa inalipa sana Tanzania, na haya ndio matokeo yake. Kila jambo tunataka kulifanya liwe la kisiasa. Hata kucheza mpira wa miguu iwe ni siasa! Hata siasa yenyewe ndio hiyo tunaiua, kwa kuondoa ushindani wa mawazo huru.

Ripoti za Makinikia, Maprofesa wetu wanaweka pembeni ujuzi wao na kufanya mambo ya aibu kabisa, ili waonekane wao ni 'Wazalendo'.

Ni hapa mwisho mwisho wa ngwe ya Kikwete ndipo wale jamaa wa Taasisi ya Kikwete pale Muhimbili walijaribu kujitutumua kidogo kuonyesha wanachoweza kufanya kama wataalam. Kwingine kote, juhudi zipo katika kujiandaa kupata uteuzi wa kisiasa.

Kwa hiyo, ukiona ripoti za wataalam wetu zinazotia aibu na kukatisha tamaa kuzisoma, elewa hiyo ni sehemu ndogo sana inayoonyesha udhaifu wetu mkubwa katika nyanja nyingi.

Inatulazimu turudi katika misingi ya kuimarisha elimu yetu, na utendaji wetu. Tuache kuifanya siasa ndio iwe kila kitu kinachoendesha uhai wa taifa letu.

Sawa, ngoja nitoe sifa za kikorofi na kinafiki: Tanzania wakulima wetu wanazalisha mahindi kwa wingi kuliko wakati mwingine wowote.
Nani anaweza kusema mkulima wa leo ni tofauti sana na yule wa miaka ya Mwalimu Nyerere!
Natambua sana juhudi za "Kilimo Kwanza," lakini kweli kuna uendelevu hapo wa kujivunia?
 
Nini maana ya "report", tuanzie hapo?

Kwa uelewa wangu na elimu ndgo niliyonayo;

Report katika project ni kuwa unatoa taarifa ya maendeleo ya project inayoendelea au imekwisha fanyika.

Kwa project inayotegemea kuanza huwa inafanyiwa "feasibility study".

A feasibility study is an analysis that takes all of a project's relevant factors into account—including economic, environmental, technical, legal, and scheduling considerations—to ascertain the likelihood of completing the project successfully.

Yan hapa hakuna cha feasibility study. Ni brabra tu nyingi na vingereza vya shule ya secondary. In short hii ni kama tu maoni ya kundi fulani la watu wamepewa vipesa watunge uwongo wao kujustify ujenz.

Ila hii sio feasibility study ni riwaya ya maoni ya wanasiasa na si wanasayansi.
 
Huu uchafu (ripoti) kwakweli unachekesha sana. Ni kama imeandikwa na wahuni kutokea jumuiya ya vijana ya CCM.

Wasomi wa PhD na wataalam hawaandiki hivi. Hii kamwe siyo ripoti ya kitaalam wala paper ya wasomi wa PhD.

Serikali ijitenge na hii ripoti. Kwa kuwa kama itachukuliwa na kufanywa ndiyo justification ya kuendelea na mradi tutaacha kumbukumbu mbaya kabisa kwenye nchi hii.

Hata hao wanaochambwa humo kwa vimaneno vya kwenye khanga, watatuona sisi wote ni vichaa.
Hii nchi hii kwa hivi sasa hata wataalamu wetu wanafuata upepo.......

Na kwasababu wao wanajua kuwa qualification no 1 hapa nchini ya kuitwa mzalendo na kukumbukwa katika uteuzi, ni kufanya kile kitu kitakachomfurahisha Jiwe.

Matokeo yake ndiyo haya, kwa utaalamu kuwekwa pembeni na kubaki kuimba mapambio ya kumsifu na kumwabudu Jiwe!
 
Tatizo awamu hii ukifanya mambo kitaalam unaonekana sio mzalendo.

Yule Mama wa kituo cha utafiti alitenguliwa WHO wakampa kitengo.

Lakini hapa tatizo ni la hawa wataalam wetu kuamua kuacha utaalam na kufanya jambo kwa kufurahisha watawala.
Kubaki kwenye misingi ya kitaalam na kutokuwa na upande napo ni sifa ya utaalam.
 
Back
Top Bottom