Ripoti ya CAG: Mkataba wa Mlimani City na Chuo Kikuu cha UDSM ni wizi mtupu | Page 7 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti ya CAG: Mkataba wa Mlimani City na Chuo Kikuu cha UDSM ni wizi mtupu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Return Of Undertaker, Apr 17, 2017.

 1. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2017
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,776
  Likes Received: 11,057
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeanika madudu ya mkataba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwenye mradi wa Mlimani City.

  Madudu hayo yanaonyesha namna chuo hicho kinavyopoteza mamilioni ambako amependekeza mkataba huo ufanyiwe marekebisho.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni, ujenzi wa mradi wa Mlimani City ulianza Oktoba Mosi mwaka 2004, ukikadiriwa kukamilika Septemba Mosi mwaka 2016.

  Hata hivyo, CAG ameshauri yafanyike marekebisho katika baadhi ya vifungu vya mkataba huo.

  Ripoti hiyo inaonyesha kwamba moja ya sababu ya kukiukwa maeneo ya mkataba wa wabia hao wawili ni uzembe wa menejimenti ya chuo.

  Ripoti inasema: “Tulibaini kwamba mradi mdogo wa hoteli ya nyota tatu (ambayo ina vyumba 100 kikiwemo chumba cha mikutano kinachochukua watu 1,000) na uboreshaji wa bustani ya botania, ikiwa ni sehemu ya mradi wa Mlimani City, haujakamilika kwa kipindi cha miaka 10 tangu tarehe ya makubaliano ya kumaliza mradi.

  “Mtazamo wangu ni kuwa hakuna ufuatiliaji wa karibu, usimamizi na tathmini ya mkataba huo kwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  “Kwa sababu hiyo kuna uwezekano wa kushidwa kumalizia kazi iliyobaki kwa sababu ya ongezeko kubwa ya gharama ya kumalizia mradi tangu kipindi kilichopangwa kupita.

  “Menejimenti ya Chuo Kikuu inashauriwa kuuangalia upya mkataba iliouingia na Mlimani City Holding, kuharakisha umaliziaji wa miradi,” ilieleza ripoti hiyo ya CAG.

  Ripoti hiyo pia inaainisha ukiukwaji wa ulipaji wa ada ambayo mwekezaji anatakiwa kuitoa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa kifungu cha 1.1(j) cha mkataba pamoja na kifungu 10.1 cha hati ya ukodishaji wa uwanja, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinapaswa kipate asilimia 10 ya mapato ya kodi ghafi.

  “Kinyume na kufungu tajwa hapo juu, Mlimani Holding Limited (MHL), hufanya hesabu za gawio la kodi ya Chuo Kikuu kwa kuzingatia asilimia 10 ya mapato ya kodi baada ya kutoa gharama za uendeshaji badala ya kujumuisha gharama za uendeshaji.

  “Ukiukwaji huu unakifanya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa katika hatari ya kupoteza kiasi kikubwa cha mapato kutoka katika mradi wa Mlimani City,” inasema ripoti hiyo.

  CAG anaishauri menejimenti ya chuo hicho ifanye upya hesabu za gawio lake la asilimia 10 kutokana na mkataba na kuomba kulipwa na mpangaji kiasi kilichokuwa kimekosewa.

  Pia alishauri kuwasiliana na mpangaji na kufikiria kubadilisha mkataba kuweka vifungu ambavyo vitaruhusu idara ya ukaguzi ya ndani ya chuo kuangalia mapato na gharama za uendeshaji za mradi.

  Ripoti hiyo pia imeainisha udhaifu wa ufuatiliaji na usimamizi wa mapato kutoka kwa wapangaji wadogo kwenye mradi huo.

  Inasema kifungu cha 11.2(l) cha hati ya makubaliano, mpangaji (MHL) anapaswa kutopangisha mtu yeyote ambaye hajathibitishwa na Mpangishaji (Chuu Kikuu cha Dar es Salaam), ikiwa ni njia ya kudhibiti mapato yake.

  Kinyume na makubaliano ya hayo, ukaguzi wa CAG umebaini kwamba MHL amepangisha majengo kwa wapangaji wengine bila kupata kibali cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  “Kuna upungufu wa utekelezaji wa vipengele vya mkataba kwa upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hivyo kusababisha Chuo kushindwa kujua kwa usahihi mapato ya kodi kutoka kwa wapangaji wote.

  “Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam inashauriwa kutekeleza vifungu na vipengele vyote vya hati ya makubalian ya upangaji kikiwamo kifungu 11.2 (l) cha hati ya makubaliano ambacho kinakitaka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwathibitisha wapangaji wadogo wadogo,” anashauri CAG.

  Ripoti hiyo pia inaonyesha mapitio ya mkataba wa upangishaji wa ardhi kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mlimani Holding Limited yamegundua kwamba mkataba haumpi mmiliki wa ardhi haki ya kukagua kazi zinazofanywa na mpangaji.

  “Katika hali hii, mpangishaji, ambaye ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hawezi kujua endapo mpangaji, Mlimani Holding Limited, anakiuka mkataba katika uendeshaji au kuna baadhi ya wapangaji wa nyumba hawawekwi wazi na mpangaji huyu,” inasema ripoti.

  CAG anashauri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwasiliana na Mlimani Holding Limited kupata haki ya kukagua shughuli za miradi kwa manufaa ya pande zote mbili.

  Ripoti hiyo inasema pia kwamba mapitio ya mkataba yamegundua mkataba huo hauelezei hali halisi ya ugawanaji mali mkataba utakapoisha (miaka 50 au 85 kutokana na makubaliano ya pande mbili).

  “Hakuna makubaliano yoyote yanayoelezea mgawanyo wa mali na miondombinu itakayokuwapo wakati mkataba unaisha.

  “Kwa hali hii, kuna uwezekano wa kutokea mvutano wa sheria mwisho wa mkataba. Hali hii ikitokea, Chuo Kikuu kitakosa msaada wa sheria.

  “Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, unashauriwa kuingia katika mazungumzo na Mlimani Holding Limited kuweka vifungu vitakavyoonyesha haki ya kila upande wakati wa mkataba utakapoisha,” anaeleza CAG.

  Ripoti hiyo pia inasema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( kiliingia katika makubaliano na kampuni ya Ernest and Young kufanya ukaguzi maalumu kujua kiasi cha mapato ambacho kinaidai kampuni ya Mlimani Holding Limited katika kipindi cha Mei Mosi mwaka 2006 mpaka Juni 30 mwaka 2014 na kubaini kutolipwa dola za Marekani 57,607.

  “Wakati wa ukaguzi niligundua kuwa kiasi cha Dola za Marekani 309,458 kilitakiwa kipokelewe na Chuo kutoka MHL, lakini usuluhisho wa hesabu ulionyesha MHL ililipa Dola za Marekani 213,850 kupitia uhamisho wa benki kwa njia ya eletroniki na kubakisha Dola za Marekani 57,607.

  “Kuna ufuatiliaji duni kwa upande wa menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kukusanya deni hilo. Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inashauriwa kuongeza nguvu katika kufuatilia na kukusanya deni wanalolidai MHL,” inasema ripoti hiyo.
   
 2. Ngungenge

  Ngungenge JF-Expert Member

  #121
  Apr 19, 2017
  Joined: Jun 11, 2016
  Messages: 689
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 80
  Tatizo letu kama nchi ni viongoz, wako radhi watajirike wao na famili zao ila nchi ikafirisika. Hata baada ya haya madudu utaona kama kuna hatua zitakazo chukuliwa.
   
 3. c

  charles mususa JF-Expert Member

  #122
  Apr 19, 2017
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 231
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Na hapo ni kwa wasomi na mabingwa wa mikataba nchi hii duuh
   
 4. gwakipanga

  gwakipanga JF-Expert Member

  #123
  Apr 19, 2017
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 472
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Tukisema wabunge wetu, si wa ccm Wala wa vyama pinzani wapo kwa ajili ya masrahi yao, kuna watu wanatokwa na povu. Taarifa nyingi zinaanikwa na mkaguzi mkuu wa serikali kana kwamba kamati za bunge hazipo. Ila nawasifu wabunge wa vyama vya upinzani wanavyojua kucheza na ajili za wananchi, kwa kuwaminisha wapo kwa ajili yao. Bila ya kubadili mind set zetu taifa litaendelea kuwa shamba la Bibi, without uzalendo nothing we can do.
   
 5. marveljt

  marveljt JF-Expert Member

  #124
  Apr 19, 2017
  Joined: Jan 11, 2017
  Messages: 1,522
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Hivi Ripoti ya wizara ya miundo mbinu haijatoka?
   
 6. cosa nostra

  cosa nostra JF-Expert Member

  #125
  Apr 19, 2017
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,784
  Likes Received: 1,732
  Trophy Points: 280
  usimamizi hauhitaji kuumizwa kichwa panapokua na RUSHWA
   
 7. cosa nostra

  cosa nostra JF-Expert Member

  #126
  Apr 19, 2017
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,784
  Likes Received: 1,732
  Trophy Points: 280
  ugonile gwakipanga
   
 8. Hajto

  Hajto JF-Expert Member

  #127
  Apr 19, 2017
  Joined: Sep 30, 2013
  Messages: 1,803
  Likes Received: 815
  Trophy Points: 280
  Du,madudu mpaka kwa wasomi
   
 9. Wazo la kabwela

  Wazo la kabwela JF-Expert Member

  #128
  Apr 19, 2017
  Joined: Feb 13, 2013
  Messages: 1,335
  Likes Received: 610
  Trophy Points: 280
   
 10. Shebbydo

  Shebbydo JF-Expert Member

  #129
  Apr 19, 2017
  Joined: Feb 12, 2015
  Messages: 1,116
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  Hivi kumbe baadhi ya watu wanafikiri kuwa na theory kichwani kibao ndiyo kureflect reality? Hata kama ni Professor kama hujawahi kupractise huo utaalamu wako katika real world hujui kitu. Ingekuwa hivyo basi Prof. Lipumba angekuwa tajiri kuliko Dangote. Lipumba anaujua uchumi kwenye karatasi ila Dangote anaujua uchumi kwenye kwa vitendo, sasa sijui nani bora. Ukisoma Engineering, darasani unafundishwa na Prof. ama Phd. holder. Workshop unafundishwa na technician ambaye wakati mwingine hata Diploma hana. Hii formal education huwa siielewi wakati mwingine. Kwa hiyo msifikiri kuwepo maprof. UDSM ndo ukamilifu.
   
 11. H

  Hichilema JF-Expert Member

  #130
  Apr 19, 2017
  Joined: Sep 4, 2016
  Messages: 492
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 80
  Nacheka sana. Mambo mengne chuo kinaamuliwa. Watafanyaje kati wao ni waajiliwa?
   
 12. masatujr1985

  masatujr1985 JF-Expert Member

  #131
  Apr 19, 2017
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 1,946
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Chuo ambacho tungetegemea kiwe mstali wa mbele kukemea uozo kama huu, ndicho kinachoingia kwenye uozo chenyewe!!!

  Ule mradi ni moja ya miradi mibovu sana katika ujaribifu wa ardhi na mazingira. Vijengo kama uchafu alhali sehemu ya ardhi wanayotumia ingewezwa kutunzwa na kutumika kwa manufaa ya baadaye.

  Waliohusika na mkataba huo kwa kweli hawajawahi kunifurahisha katika hili.
   
 13. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #132
  Apr 19, 2017
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,957
  Likes Received: 1,403
  Trophy Points: 280
  Huyu Profesa Assad huyu.... sijui wale wazee wa.... Ooops kina msituseme hawajamuona!!!

  Profesa Assad Oyeee!! (sijaiona hii!!)
   
 14. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #133
  Apr 19, 2017
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,849
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  RIP Dr. Chungu....mtaalamu wa uwekezaji bandia na mwalimu wa somo la ujasiriamali. Ukweli kitu cha ajabu sana. Hakuna atakayeshinda akiamua kupambana nao
   
 15. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #134
  Apr 19, 2017
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,849
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Kuna Dr. mmoja alikwa Real Estate ya chuo...alikuwa mtu mjuaji kweli kweli....sishangai kusikia kuna matatizo maana yeye binafsi hakuwa sawasawa
   
 16. Poise

  Poise JF-Expert Member

  #135
  Apr 19, 2017
  Joined: May 31, 2016
  Messages: 7,492
  Likes Received: 7,436
  Trophy Points: 280
  Nakuambia, yaani hapo Tanzania robo Tatu (3/4) ya watanzania ni wezi katika ofisi zote siyo laudanum, msikitini wala serikali, sekta binafsi, hadi wengine katika familia zao wenyewe wanazihujumu yaani ni majanga aisee.
   
 17. Poise

  Poise JF-Expert Member

  #136
  Apr 19, 2017
  Joined: May 31, 2016
  Messages: 7,492
  Likes Received: 7,436
  Trophy Points: 280
  Rais, Dr. Magufuli , anastahiki pongezi nyingi Sana Kwa kumpatia huo uwezo wa kuleta repoti bila kuchakachuliwa na vipanga.

  Na hii kazi ya rais kupitia CAG, itupatie picha ya wazi jinsi nchi ilivyooza.

  Pia, CAG, Prof. Asaad , kweli amefanya kazi ambayo hakuna wa kuinua Kichwa tena.

  Maana, kila sekta ni wezi na matapeli,
   
 18. mpingo

  mpingo Member

  #137
  Apr 19, 2017
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 65
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  hahahahaha........hujua kuwa hao wanasoma ili wapate kazi.......na sio ili wafanye kazi zenye matokeo mazuri/maendeleo....wengi ni watu makaratasi mengi lakini si watendaji.....wanatafuta fulsa za kuhondomola tu.. sio kujenga nchi...
   
 19. Bome-e

  Bome-e JF-Expert Member

  #138
  Apr 19, 2017
  Joined: Jan 3, 2014
  Messages: 8,605
  Likes Received: 5,442
  Trophy Points: 280
  Na ile mv ifate kule kule jeshini
   
 20. mwanadome

  mwanadome JF-Expert Member

  #139
  Apr 19, 2017
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 2,289
  Likes Received: 1,868
  Trophy Points: 280
  Bahati nzuri ndo chuo kinachopigiwa chepuo na mkulu mwenyewe kua ndo bora.na mkulu kila anapofanya uteuzi jicho la kwanza ni UD,ikiwa wao wenyewe hawawezi jisimamia tutawaaminije huko wanako teuliwa?.

  Waziri wa katiba na sheria aibu yako hii,maana miaka kibao uko pale na sifa kemkem ukipewa kwa uhodari wako wa sheria.

  Sasa watipunguzie kelele za kuisifia UD
   
 21. mwanadome

  mwanadome JF-Expert Member

  #140
  Apr 19, 2017
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 2,289
  Likes Received: 1,868
  Trophy Points: 280
  Kwa uzembe huu,watashindwa kweli kutoa ka Phd ka kuungaungaa
   
Loading...