Ripoti ya CAG: Mkataba wa Mlimani City na Chuo Kikuu cha UDSM ni wizi mtupu | Page 8 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti ya CAG: Mkataba wa Mlimani City na Chuo Kikuu cha UDSM ni wizi mtupu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Return Of Undertaker, Apr 17, 2017.

 1. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2017
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,919
  Likes Received: 11,583
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeanika madudu ya mkataba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwenye mradi wa Mlimani City.

  Madudu hayo yanaonyesha namna chuo hicho kinavyopoteza mamilioni ambako amependekeza mkataba huo ufanyiwe marekebisho.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni, ujenzi wa mradi wa Mlimani City ulianza Oktoba Mosi mwaka 2004, ukikadiriwa kukamilika Septemba Mosi mwaka 2016.

  Hata hivyo, CAG ameshauri yafanyike marekebisho katika baadhi ya vifungu vya mkataba huo.

  Ripoti hiyo inaonyesha kwamba moja ya sababu ya kukiukwa maeneo ya mkataba wa wabia hao wawili ni uzembe wa menejimenti ya chuo.

  Ripoti inasema: “Tulibaini kwamba mradi mdogo wa hoteli ya nyota tatu (ambayo ina vyumba 100 kikiwemo chumba cha mikutano kinachochukua watu 1,000) na uboreshaji wa bustani ya botania, ikiwa ni sehemu ya mradi wa Mlimani City, haujakamilika kwa kipindi cha miaka 10 tangu tarehe ya makubaliano ya kumaliza mradi.

  “Mtazamo wangu ni kuwa hakuna ufuatiliaji wa karibu, usimamizi na tathmini ya mkataba huo kwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  “Kwa sababu hiyo kuna uwezekano wa kushidwa kumalizia kazi iliyobaki kwa sababu ya ongezeko kubwa ya gharama ya kumalizia mradi tangu kipindi kilichopangwa kupita.

  “Menejimenti ya Chuo Kikuu inashauriwa kuuangalia upya mkataba iliouingia na Mlimani City Holding, kuharakisha umaliziaji wa miradi,” ilieleza ripoti hiyo ya CAG.

  Ripoti hiyo pia inaainisha ukiukwaji wa ulipaji wa ada ambayo mwekezaji anatakiwa kuitoa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa kifungu cha 1.1(j) cha mkataba pamoja na kifungu 10.1 cha hati ya ukodishaji wa uwanja, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinapaswa kipate asilimia 10 ya mapato ya kodi ghafi.

  “Kinyume na kufungu tajwa hapo juu, Mlimani Holding Limited (MHL), hufanya hesabu za gawio la kodi ya Chuo Kikuu kwa kuzingatia asilimia 10 ya mapato ya kodi baada ya kutoa gharama za uendeshaji badala ya kujumuisha gharama za uendeshaji.

  “Ukiukwaji huu unakifanya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa katika hatari ya kupoteza kiasi kikubwa cha mapato kutoka katika mradi wa Mlimani City,” inasema ripoti hiyo.

  CAG anaishauri menejimenti ya chuo hicho ifanye upya hesabu za gawio lake la asilimia 10 kutokana na mkataba na kuomba kulipwa na mpangaji kiasi kilichokuwa kimekosewa.

  Pia alishauri kuwasiliana na mpangaji na kufikiria kubadilisha mkataba kuweka vifungu ambavyo vitaruhusu idara ya ukaguzi ya ndani ya chuo kuangalia mapato na gharama za uendeshaji za mradi.

  Ripoti hiyo pia imeainisha udhaifu wa ufuatiliaji na usimamizi wa mapato kutoka kwa wapangaji wadogo kwenye mradi huo.

  Inasema kifungu cha 11.2(l) cha hati ya makubaliano, mpangaji (MHL) anapaswa kutopangisha mtu yeyote ambaye hajathibitishwa na Mpangishaji (Chuu Kikuu cha Dar es Salaam), ikiwa ni njia ya kudhibiti mapato yake.

  Kinyume na makubaliano ya hayo, ukaguzi wa CAG umebaini kwamba MHL amepangisha majengo kwa wapangaji wengine bila kupata kibali cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  “Kuna upungufu wa utekelezaji wa vipengele vya mkataba kwa upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hivyo kusababisha Chuo kushindwa kujua kwa usahihi mapato ya kodi kutoka kwa wapangaji wote.

  “Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam inashauriwa kutekeleza vifungu na vipengele vyote vya hati ya makubalian ya upangaji kikiwamo kifungu 11.2 (l) cha hati ya makubaliano ambacho kinakitaka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwathibitisha wapangaji wadogo wadogo,” anashauri CAG.

  Ripoti hiyo pia inaonyesha mapitio ya mkataba wa upangishaji wa ardhi kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mlimani Holding Limited yamegundua kwamba mkataba haumpi mmiliki wa ardhi haki ya kukagua kazi zinazofanywa na mpangaji.

  “Katika hali hii, mpangishaji, ambaye ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hawezi kujua endapo mpangaji, Mlimani Holding Limited, anakiuka mkataba katika uendeshaji au kuna baadhi ya wapangaji wa nyumba hawawekwi wazi na mpangaji huyu,” inasema ripoti.

  CAG anashauri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwasiliana na Mlimani Holding Limited kupata haki ya kukagua shughuli za miradi kwa manufaa ya pande zote mbili.

  Ripoti hiyo inasema pia kwamba mapitio ya mkataba yamegundua mkataba huo hauelezei hali halisi ya ugawanaji mali mkataba utakapoisha (miaka 50 au 85 kutokana na makubaliano ya pande mbili).

  “Hakuna makubaliano yoyote yanayoelezea mgawanyo wa mali na miondombinu itakayokuwapo wakati mkataba unaisha.

  “Kwa hali hii, kuna uwezekano wa kutokea mvutano wa sheria mwisho wa mkataba. Hali hii ikitokea, Chuo Kikuu kitakosa msaada wa sheria.

  “Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, unashauriwa kuingia katika mazungumzo na Mlimani Holding Limited kuweka vifungu vitakavyoonyesha haki ya kila upande wakati wa mkataba utakapoisha,” anaeleza CAG.

  Ripoti hiyo pia inasema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( kiliingia katika makubaliano na kampuni ya Ernest and Young kufanya ukaguzi maalumu kujua kiasi cha mapato ambacho kinaidai kampuni ya Mlimani Holding Limited katika kipindi cha Mei Mosi mwaka 2006 mpaka Juni 30 mwaka 2014 na kubaini kutolipwa dola za Marekani 57,607.

  “Wakati wa ukaguzi niligundua kuwa kiasi cha Dola za Marekani 309,458 kilitakiwa kipokelewe na Chuo kutoka MHL, lakini usuluhisho wa hesabu ulionyesha MHL ililipa Dola za Marekani 213,850 kupitia uhamisho wa benki kwa njia ya eletroniki na kubakisha Dola za Marekani 57,607.

  “Kuna ufuatiliaji duni kwa upande wa menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kukusanya deni hilo. Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inashauriwa kuongeza nguvu katika kufuatilia na kukusanya deni wanalolidai MHL,” inasema ripoti hiyo.
   
 2. mwanadome

  mwanadome JF-Expert Member

  #141
  Apr 19, 2017
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 2,335
  Likes Received: 1,895
  Trophy Points: 280
  Mkuu,na wakitoka hapo wanaanza kupaza suuti za ufisadii.watuuache na vi digirii vyetu vya kampala international university
   
 3. mwanadome

  mwanadome JF-Expert Member

  #142
  Apr 19, 2017
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 2,335
  Likes Received: 1,895
  Trophy Points: 280
  Mkuu,watamtetea kua hakua na maamuzi,ukiuliza vipi kuhusu mv dar es salaam au nyumba za serikali au upotevu wa 252bln kwenye wizara aliyo kua akiiongoza,wataishia kusema hapa kazi tu.
   
 4. mwanadome

  mwanadome JF-Expert Member

  #143
  Apr 19, 2017
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 2,335
  Likes Received: 1,895
  Trophy Points: 280
   
 5. mwanadome

  mwanadome JF-Expert Member

  #144
  Apr 19, 2017
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 2,335
  Likes Received: 1,895
  Trophy Points: 280
  Mkuu,huko ni patakatifu pa watakatifu hapawezi kuguswaa.
   
 6. mwanadome

  mwanadome JF-Expert Member

  #145
  Apr 19, 2017
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 2,335
  Likes Received: 1,895
  Trophy Points: 280
  Cc vipanga wotee wa UD hongereni sanaaaa.
   
 7. kisu cha ngariba

  kisu cha ngariba JF-Expert Member

  #146
  Apr 19, 2017
  Joined: Jun 21, 2016
  Messages: 21,294
  Likes Received: 46,279
  Trophy Points: 280
  Ina maana pale UDSM hakuna wachumi,wahasibu na wanasheria? Kweli UDSM hii tunayoambiwa inatoa vipanga inaingia mikataba ya kijinga kiasi hiki?
   
 8. e

  eddy JF-Expert Member

  #147
  Apr 19, 2017
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 10,586
  Likes Received: 4,716
  Trophy Points: 280
  Hivi yule ndege anaekula ndege wenzie sianaitwa kipanga? Tunashangaa nini? Huyu kipanga mwewe cha mtoto, kuku akimwona ukiwa karibu nae anaweza ingia hata kwenye suruali kwa woga.
   
 9. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #148
  Apr 19, 2017
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 5,168
  Likes Received: 3,144
  Trophy Points: 280
  Nilishasema hawa wasome wetu wa masters au phd kwa kweli hata hatuwaelewi KWANINI HAWAWEZI SOMA MIKATABA?! AU WANAFANYA MAKUSUDI TU?! WAPUUZI SANA AISE..
   
 10. Rene Jr.

  Rene Jr. JF-Expert Member

  #149
  Apr 19, 2017
  Joined: Jan 31, 2014
  Messages: 3,317
  Likes Received: 901
  Trophy Points: 280
  Subiri kwanza, yaani 2006 mpaka 2014 hiyo dola laki tatu iliyokuwa ikidaiwa ni pango au? Inamaana ndiyo MGAO wa UDSM kwa miaka 6?!! Au kuna kitu sijakielewa? Maana kama ndivyo basi hiyo biashara ni kichaa, eneo loote hilo milioni hamsini kwa mwaka?!!
   
 11. Patriot

  Patriot JF-Expert Member

  #150
  Apr 19, 2017
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 2,341
  Likes Received: 1,258
  Trophy Points: 280
  Ushabiki wa kindugu mpaka lini?? Dau Dau utadhani naye mtume na dini yake. Rubbish. Mbona kuna watu walichunguzwa na majanga yao hayakuonekana mpaka baadaye ndo wamepigwa kumbo?

  Hiyo ardhi ilikuwa na bei hizo alizokuwa ananunulia kweli? Kweli ni yeye pekee aliyekuwa mtakatifu ktk ushetani wa awamu iliyopita? Huu ni ushabiki wa ndoa.
   
 12. L

  LJ Innocent Member

  #151
  Apr 20, 2017
  Joined: Oct 20, 2016
  Messages: 20
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 5
  Aisee yaani hii inafanyika in The Only place we thought there is hope... kama experts ndio hiv inasikitisha sana kufikiria sehemu nyingine
   
 13. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #152
  Apr 20, 2017
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,346
  Likes Received: 2,114
  Trophy Points: 280
  Kunahitaji kuwajengea uwezo watumishi wa umma kwenye nyanja ya usimamizi wa mikataba (contract management).
   
 14. N

  Nonda JF-Expert Member

  #153
  Apr 21, 2017
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,248
  Likes Received: 1,985
  Trophy Points: 280
  Unakumbuka Chenge ndiye alikuwa consultant wa kuwaonesha wapiga chenga vipi wazipige hizo chenga huku akiwekewa vijisenti vyake kule New Jersey?
  Huo ndio uzalendo wa watanzania. Uzalendo wa kushibisha tumbo.

  Link Chenge na vijisenti, Yuda na vijidinari – Raia Mwema

  Link2. Andrew chenge: Mnashangaa hivi vijisenti tu, ipo siku ukweli utajulikana
   
 15. wilson kaiser senior

  wilson kaiser senior Senior Member

  #154
  Apr 21, 2017
  Joined: Apr 4, 2017
  Messages: 188
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 80
  TANZANIA HAMNA WASOMI KAMA TAASISI YA KUTOA WASOMI IMEDHURUMIWA (INAINGIA MIKATABA YA KIJINGA) UTASEMA TANZANIA KUNA MA-PROFFESOR AU MA-DOCTOR (PHD) AU MASTEERS HOLDERS AU DEGREE HOLDERS?

  TANZANIA HAMNA WASOMI ILA KUNA WATU WANAO-JUA KUKALILI MASOMO...

  AIBU SANA
   
 16. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #155
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,722
  Likes Received: 2,436
  Trophy Points: 280
  Wapigaji haijalishi wamesoma wapi! Wizi ni tabia, wala haiendani na chuo husika.
   
 17. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #156
  Apr 21, 2017
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,441
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Kila mtu mwizi.jpg
   
 18. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #157
  Apr 21, 2017
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,441
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
   
 19. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #158
  Apr 21, 2017
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,441
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  JE TUNAKUMBUKA MANENO YA MKULU JUZI WAKATI ANAZINDUA HOSTEL YA UDSM ALIVYOSEMA KUHUSU VYUO VYA SERIKALI????

  NA HATA AKAPIGA MKWARA KWATCU WASIINGILIE UTEUZI WA WANAFUNZI ILI WANAFUNZI WACHAGUE WENYEWE PA KWENDA KWANI KWA IMANI YAKE NI KWAMBA HIVI VYA SERIKALI NI BORA KULIKO BINAFSI. NA KWAMBA IRAFIKIA WAKATI BINAFSI WATAKOSA WANAFUNZI WA KJJIUNGA!!!!!!!

  KUMBE HUKU ANASAHAU KUWA WOTE NI WIZI MTUPU......

  HIVI NAOMBA MNIKUMBUSHE MKUU WA UDSM NI NANI KWA SASA??????????


  SEMA USIKIKE...


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 20. Mwana

  Mwana JF-Expert Member

  #159
  Apr 21, 2017
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 4,953
  Likes Received: 1,339
  Trophy Points: 280
  Safi sana CAG. ila swali moja tu je taarifa hii pia ilikuwepo miaka mitano iliyopita? Hatua gani zilicgukuliwa as kama ingejulikana mapema hatua zingechukuliwa mapema ingesaidia zaidi kuliko kungoja miaia kumi!
   
 21. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #160
  Apr 21, 2017
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,613
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Loh! lawama kwenda kwa professor mmoja siyo suluhisho Mkuu, hao waliompokea je walishindwa kuuitisha na kuupitia upya mkataba huo? Walitakiwa du-draft Annex iwe sehemu ya mkataba. Badala yake wakasherehekea kwa kupiga kt mpaka leo. Huenda waliompokea hawajausoma huo mkataba mpaka leo. Mkataba wa taasisi kubwa na ya kisomi kama hiyo siyo koti la kuvalishwa mtu mmoja.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...