Ripoti ya CAG: Mkataba wa Mlimani City na Chuo Kikuu cha UDSM ni wizi mtupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti ya CAG: Mkataba wa Mlimani City na Chuo Kikuu cha UDSM ni wizi mtupu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Return Of Undertaker, Apr 17, 2017.

 1. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2017
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,912
  Likes Received: 11,562
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeanika madudu ya mkataba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwenye mradi wa Mlimani City.

  Madudu hayo yanaonyesha namna chuo hicho kinavyopoteza mamilioni ambako amependekeza mkataba huo ufanyiwe marekebisho.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni, ujenzi wa mradi wa Mlimani City ulianza Oktoba Mosi mwaka 2004, ukikadiriwa kukamilika Septemba Mosi mwaka 2016.

  Hata hivyo, CAG ameshauri yafanyike marekebisho katika baadhi ya vifungu vya mkataba huo.

  Ripoti hiyo inaonyesha kwamba moja ya sababu ya kukiukwa maeneo ya mkataba wa wabia hao wawili ni uzembe wa menejimenti ya chuo.

  Ripoti inasema: “Tulibaini kwamba mradi mdogo wa hoteli ya nyota tatu (ambayo ina vyumba 100 kikiwemo chumba cha mikutano kinachochukua watu 1,000) na uboreshaji wa bustani ya botania, ikiwa ni sehemu ya mradi wa Mlimani City, haujakamilika kwa kipindi cha miaka 10 tangu tarehe ya makubaliano ya kumaliza mradi.

  “Mtazamo wangu ni kuwa hakuna ufuatiliaji wa karibu, usimamizi na tathmini ya mkataba huo kwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  “Kwa sababu hiyo kuna uwezekano wa kushidwa kumalizia kazi iliyobaki kwa sababu ya ongezeko kubwa ya gharama ya kumalizia mradi tangu kipindi kilichopangwa kupita.

  “Menejimenti ya Chuo Kikuu inashauriwa kuuangalia upya mkataba iliouingia na Mlimani City Holding, kuharakisha umaliziaji wa miradi,” ilieleza ripoti hiyo ya CAG.

  Ripoti hiyo pia inaainisha ukiukwaji wa ulipaji wa ada ambayo mwekezaji anatakiwa kuitoa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa kifungu cha 1.1(j) cha mkataba pamoja na kifungu 10.1 cha hati ya ukodishaji wa uwanja, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinapaswa kipate asilimia 10 ya mapato ya kodi ghafi.

  “Kinyume na kufungu tajwa hapo juu, Mlimani Holding Limited (MHL), hufanya hesabu za gawio la kodi ya Chuo Kikuu kwa kuzingatia asilimia 10 ya mapato ya kodi baada ya kutoa gharama za uendeshaji badala ya kujumuisha gharama za uendeshaji.

  “Ukiukwaji huu unakifanya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa katika hatari ya kupoteza kiasi kikubwa cha mapato kutoka katika mradi wa Mlimani City,” inasema ripoti hiyo.

  CAG anaishauri menejimenti ya chuo hicho ifanye upya hesabu za gawio lake la asilimia 10 kutokana na mkataba na kuomba kulipwa na mpangaji kiasi kilichokuwa kimekosewa.

  Pia alishauri kuwasiliana na mpangaji na kufikiria kubadilisha mkataba kuweka vifungu ambavyo vitaruhusu idara ya ukaguzi ya ndani ya chuo kuangalia mapato na gharama za uendeshaji za mradi.

  Ripoti hiyo pia imeainisha udhaifu wa ufuatiliaji na usimamizi wa mapato kutoka kwa wapangaji wadogo kwenye mradi huo.

  Inasema kifungu cha 11.2(l) cha hati ya makubaliano, mpangaji (MHL) anapaswa kutopangisha mtu yeyote ambaye hajathibitishwa na Mpangishaji (Chuu Kikuu cha Dar es Salaam), ikiwa ni njia ya kudhibiti mapato yake.

  Kinyume na makubaliano ya hayo, ukaguzi wa CAG umebaini kwamba MHL amepangisha majengo kwa wapangaji wengine bila kupata kibali cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  “Kuna upungufu wa utekelezaji wa vipengele vya mkataba kwa upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hivyo kusababisha Chuo kushindwa kujua kwa usahihi mapato ya kodi kutoka kwa wapangaji wote.

  “Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam inashauriwa kutekeleza vifungu na vipengele vyote vya hati ya makubalian ya upangaji kikiwamo kifungu 11.2 (l) cha hati ya makubaliano ambacho kinakitaka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwathibitisha wapangaji wadogo wadogo,” anashauri CAG.

  Ripoti hiyo pia inaonyesha mapitio ya mkataba wa upangishaji wa ardhi kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mlimani Holding Limited yamegundua kwamba mkataba haumpi mmiliki wa ardhi haki ya kukagua kazi zinazofanywa na mpangaji.

  “Katika hali hii, mpangishaji, ambaye ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hawezi kujua endapo mpangaji, Mlimani Holding Limited, anakiuka mkataba katika uendeshaji au kuna baadhi ya wapangaji wa nyumba hawawekwi wazi na mpangaji huyu,” inasema ripoti.

  CAG anashauri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwasiliana na Mlimani Holding Limited kupata haki ya kukagua shughuli za miradi kwa manufaa ya pande zote mbili.

  Ripoti hiyo inasema pia kwamba mapitio ya mkataba yamegundua mkataba huo hauelezei hali halisi ya ugawanaji mali mkataba utakapoisha (miaka 50 au 85 kutokana na makubaliano ya pande mbili).

  “Hakuna makubaliano yoyote yanayoelezea mgawanyo wa mali na miondombinu itakayokuwapo wakati mkataba unaisha.

  “Kwa hali hii, kuna uwezekano wa kutokea mvutano wa sheria mwisho wa mkataba. Hali hii ikitokea, Chuo Kikuu kitakosa msaada wa sheria.

  “Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, unashauriwa kuingia katika mazungumzo na Mlimani Holding Limited kuweka vifungu vitakavyoonyesha haki ya kila upande wakati wa mkataba utakapoisha,” anaeleza CAG.

  Ripoti hiyo pia inasema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( kiliingia katika makubaliano na kampuni ya Ernest and Young kufanya ukaguzi maalumu kujua kiasi cha mapato ambacho kinaidai kampuni ya Mlimani Holding Limited katika kipindi cha Mei Mosi mwaka 2006 mpaka Juni 30 mwaka 2014 na kubaini kutolipwa dola za Marekani 57,607.

  “Wakati wa ukaguzi niligundua kuwa kiasi cha Dola za Marekani 309,458 kilitakiwa kipokelewe na Chuo kutoka MHL, lakini usuluhisho wa hesabu ulionyesha MHL ililipa Dola za Marekani 213,850 kupitia uhamisho wa benki kwa njia ya eletroniki na kubakisha Dola za Marekani 57,607.

  “Kuna ufuatiliaji duni kwa upande wa menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kukusanya deni hilo. Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inashauriwa kuongeza nguvu katika kufuatilia na kukusanya deni wanalolidai MHL,” inasema ripoti hiyo.
   
 2. e2n

  e2n JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2017
  Joined: Dec 24, 2015
  Messages: 552
  Likes Received: 662
  Trophy Points: 180
  Safi sana CAG kazi yako njema
   
 3. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2017
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,634
  Likes Received: 3,495
  Trophy Points: 280
  Siyo enzi za Magufuli!
   
 4. iparamasa

  iparamasa JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2017
  Joined: Nov 14, 2013
  Messages: 13,462
  Likes Received: 14,138
  Trophy Points: 280
  Kadri muda unavyoenda mkulu atakuwa anaishiwa pumzi,CAG kammwagia matatizo,kila akisoma,yote yako darini,lakini sijasikia wizara ya ujenzi na taasisi zake,hasa ile MV mzinga wa jeshi
   
 5. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2017
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,427
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  kazi nzuri sana CAG!ni aibu kubwa kwa chuo kikuu kilichobobea wataalam wa sheria na utawala kuingia mkataba mbovu kama huo na kutofanya ufuatiliaji wa uhakika na wa umakini.
   
 6. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2017
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,417
  Likes Received: 3,919
  Trophy Points: 280
  CAG amka ndugu yangu, sio kwamba kuna uzembe bali watu wanapiga pasenti zao hapo. Kwani haujui kuwa chimbuko la ufisadi hapa nchini ni Chuo Kikuu cha Dar. Hapo ndio ufisadi ulipozaliwa jamaa wanajiibia hadi wenyewe
   
 7. Sibonike

  Sibonike JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2017
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 10,856
  Likes Received: 5,689
  Trophy Points: 280
  Aliyajua yote hayo kabla ya kuwa CAG maana alikuwa Mfanyakazi wa UDSM

  Sasa nafasi yake inampa uwezo wa kujua hizo kasoro kwa undani

  Kama jamaa walitoa mlungula itakula kwao
   
 8. kirikou1

  kirikou1 JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2017
  Joined: Nov 8, 2016
  Messages: 3,323
  Likes Received: 4,031
  Trophy Points: 280
  Ndio pale wanasema sheria ilipozaliwa ndipo wanapigwa bila mfano,

  Nilitegemea Udsm kama taasisi komavu ya elimu ije na mikataba mujarabu zaidi ya ile ya singasinga kumbe nao bure kabisa.

  Tutabaki kuona miradi ya makerere kwa macho
   
 9. Keyboard Warrior

  Keyboard Warrior JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2017
  Joined: Aug 5, 2014
  Messages: 960
  Likes Received: 2,762
  Trophy Points: 180
  Further proof kuwa elimu ya Tz ni majanga.
  Pale school of law na udbs kuna wahadhiri/wataalamu "waliobobea" lakini bado chuo kimepigwa chenga ya mwili. We have a long way to go.
   
 10. Mavipunda

  Mavipunda JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2017
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 4,797
  Likes Received: 3,560
  Trophy Points: 280
  Si mambo ya ajabu kwa Chama cha Majizi
   
 11. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2017
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 23,145
  Likes Received: 14,360
  Trophy Points: 280
  Hili tuliwahi kuliongelea humu...kuhusu ujenzi wa 'magodown "badala ya uwekezaji wa kutoa ajira kwa wanachuo.
   
 12. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2017
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,172
  Likes Received: 620
  Trophy Points: 280
  Sehemu ambayo wanasheria wanaoitwa wasomi na wachumi wasomi mikataba inakuwa na loop holes za kizembe namna hii!!!

  Ila sishangai, kuna mtu atakuja kujazwa Kwenye Hizo loop holes aendelee kuchota.
  Maana wabongo ni maarufu Sana Kwa fursa za rushwa..
   
 13. SDG

  SDG JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2017
  Joined: Feb 28, 2017
  Messages: 7,307
  Likes Received: 7,533
  Trophy Points: 280
  CAG TENA
   
 14. Poise

  Poise JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2017
  Joined: May 31, 2016
  Messages: 7,492
  Likes Received: 7,440
  Trophy Points: 280
  Tanzania, rushwa na ubadilifu hadi mochwari!

  Maana kila siku humu waliosoma udsm hapo Tanzania, oooh oooh chuo bora mara Africa oooh the best in Tanzania University kumbe utapeli mtupu!

  Namhurumia Sana Rais, Dr. Magufuli maana madudu kila mahala!
   
 15. BILGERT

  BILGERT JF-Expert Member

  #15
  Apr 17, 2017
  Joined: Feb 27, 2015
  Messages: 2,015
  Likes Received: 1,617
  Trophy Points: 280
   
 16. Poise

  Poise JF-Expert Member

  #16
  Apr 17, 2017
  Joined: May 31, 2016
  Messages: 7,492
  Likes Received: 7,440
  Trophy Points: 280
  Actually, they knew what they did. It's a corrupted system from education to family level nothing else.
   
 17. misasa

  misasa JF-Expert Member

  #17
  Apr 17, 2017
  Joined: Feb 5, 2014
  Messages: 6,787
  Likes Received: 3,446
  Trophy Points: 280
  Si mlimshangilia akiingia bungeni?
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Apr 17, 2017
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,498
  Likes Received: 117,184
  Trophy Points: 280
  Eh! Hakuwemo Serikalini huyu!

   
 19. S

  Siku za ajabu JF-Expert Member

  #19
  Apr 17, 2017
  Joined: Dec 23, 2012
  Messages: 785
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  aliyasema haya utajengaje hostel nje ya eneo la chuo wkt lipo ajabu akianza kutumbua mtaanza kuongea anatumbua.
   
 20. Gut

  Gut JF-Expert Member

  #20
  Apr 17, 2017
  Joined: Jan 18, 2016
  Messages: 2,686
  Likes Received: 2,914
  Trophy Points: 280
  Siku nilipo sikia eti kile chuo wanasoma "vipanga" niliwahurumia sana vifaranga.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...