Ripoti ya CAG: Mkataba wa Mlimani City na Chuo Kikuu cha UDSM ni wizi mtupu

Aliyajua yote hayo kabla ya kuwa CAG maana alikuwa Mfanyakazi wa UDSM

Sasa nafasi yake inampa uwezo wa kujua hizo kasoro kwa undani

Kama jamaa walitoa mlungula itakula kwao
Kaka sasa ndo upime uwezo wetu sisi watanzania kufikiria uko wapi hawa ndo wasomi tuliowaamini tukawapa wadhifa wa kuendesha roho zetu sasa angalieni madudu wanayofanya alaf leo wanakuja kugundua ujinga na upumbavu waliofanya wanasema eti wanaibua makosa marekebisho inabidi yafanyike
 
Prof.Mukandala ni FISADI wa siku nyingi. Alifisadi sana pesa za Redet, pia kufisadi kwenye pesa za research kadhaa kabla ya kuwa VC na akajenga mahekalu kibao.
Na alipoteuliwa kiwa VC ikawa kama kumpa kichaa rungu. Ufisadi kwa kwenda mbele. Ikifanyika audit special atafungwa jela tu.
 
me sijui tunaenda wapi pamoja na umaarufu wa chuo, anyway tunazalisha tusichokitumia na tunatumia tusichozalisha
 
Loh! lawama kwenda kwa professor mmoja siyo suluhisho Mkuu, hao waliompokea je walishindwa kuuitisha na kuupitia upya mkataba huo? Walitakiwa du-draft Annex iwe sehemu ya mkataba. Badala yake wakasherehekea kwa kupiga kt mpaka leo. Huenda waliompokea hawajausoma huo mkataba mpaka leo. Mkataba wa taasisi kubwa na ya kisomi kama hiyo siyo koti la kuvalishwa mtu mmoja.
Too simplistic narrative. Unatakiwa kufahamu kuwa upande wa pili wa mkataba hawakuwa wajinga kupendekeza na kisha kusaini mkataba ywa aina hiyo. Walikuwa wanajua wanachokifanya. Mikataba ya namna hiyo huwa na stability clauses, ikiwa ni pamoja na kuweka vipengele vya kuzuia upande mmoja kufanya mabadiliko yoyote hadi uhai wa makataba au phase fulani. Kwa hiyo siyo simplistic kama unavyopendekeza kuwa upande mmoja ukitaka tu, kwa namna utakavyoona inafaa, unaandika vipengele vya nyongeza kurekebisha mkataba. la hasha.
 
Safi sana CAG. ila swali moja tu je taarifa hii pia ilikuwepo miaka mitano iliyopita? Hatua gani zilicgukuliwa as kama ingejulikana mapema hatua zingechukuliwa mapema ingesaidia zaidi kuliko kungoja miaia kumi!
Labda aulizwe Bwn. Ludovick Utto kwa nini hakukagua mahaesabu hayo.
 
Further proof kuwa elimu ya Tz ni majanga.
Pale school of law na udbs kuna wahadhiri/wataalamu "waliobobea" lakini bado chuo kimepigwa chenga ya mwili. We have a long way to go.
sijui ni uelewa wangu tatizo halipo katika mkataba, mkataba uko vizuri
tatizo ni management ndio imewashinda au wamefanya kusudi wanapiga hela hapo kiujanja maana haileti maana wasomi nao wamezidiwa
 
blood kenge kabisaaaaaaaa
yaani kila kitu kicho husu mikaba siku ya mwisho tunajikuta tumeingia 'cha kike'
sijui wanasheria wetu wapo hoii kitaluma au ni fisi maji?
 
4 years ndio anakuja kutuambia mambo ya Mlimani City?!?!?
What is wrong angefanya ukaguzi huo hata baada ya miaka 10 kupita? Sasa nadhani wewe ni kilaza. Unashindwa hata kusoma kuona ukaguzi huo uliofanyika ume-cover timeframe (fiscal years) gani. Nimekuambia CAG hufanya special audits kutokana na maagizo ya Rais au Bunge. Katika ukaguzi wa mwaka huu CAG amekabidhi ripoti 17, lakini huko nyuma alikuwa akifanya ukaguzi hesabu za Serikali Kuu, hesabu za LGAs na pengine 1 or 2 special audit (miradi ya maendeleo - mara nyingi kutokana na matakwa ya wafadhili). This time around CAG aliagizwa na Rais kukagua miradi ya maendeleo 15, ikiwa ni pamoja na UDSM (Mlimani City Development Project). Sasa utakuwa umeelewa kama ulikuwa na nia ya kuelewa.
 
Too simplistic narrative. Unatakiwa kufahamu kuwa upande wa pili wa mkataba hawakuwa wajinga kupendekeza na kisha kusaini mkataba ywa aina hiyo. Walikuwa wanajua wanachokifanya. Mikataba ya namna hiyo huwa na stability clauses, ikiwa ni pamoja na kuweka vipengele vya kuzuia upande mmoja kufanya mabadiliko yoyote hadi uhai wa makataba au phase fulani. Kwa hiyo siyo simplistic kama unavyopendekeza kuwa upande mmoja ukitaka tu, kwa namna utakavyoona inafaa, unaandika vipengele vya nyongeza kurekebisha mkataba. la hasha.


OK, I agree my comments could be simplistic but was that smart enough to agree to sign such an agreement? And are you sure that, that is how it reads or your are also being simplistic yourself? Come out clean and attach that clause here. Unfortunately I have no access to the agreement and that is what I would like to provoke exposing it to the public.
Common Sophist give us the contents to assure us you are also not simplistic!
 
OK, I agree my comments could be simplistic but was that smart enough to agree to sign such an agreement? And are you sure that, that is how it reads or your are also being simplistic yourself? Come out clean and attach that clause here. Unfortunately I have no access to the agreement and that is what I would like to provoke exposing it to the public.
Common Sophist give us the contents to assure us you are also not simplistic!
Ref. CAG report (UDSM/MLIMANI CITY Ltd)
 
Hizi report zimejaa kwenye kabati za magogoni
Hakuna jipya huyo CAG mbona report yake haisemi kuhusu ujenzi wa hostel zilizo chini ya ubora pale mlimani?
Mbona hasemi ununuzi wa ndege Mpya? Mbona report yake haisemi watu waliotumbuliwa lakini mishahara yao wameendelea kulipwa ni ujinga kujadili issue ys 2004 tukaacha ya 2016 mlimani city imekuwepo miaka kibao hata waliohusika katika mikataba wengine ndio wakuu wa idara furani na wengine ni makatibu wa wizara
 
Ref. CAG report (UDSM/MLIMANI CITY Ltd)

The Mlimani City Agreement itself ndio itakuwa suluhisho, siyo ripoti ya CAG.
Na kwa kuongezea tu angalia ushauri wa CAG, kuwa kuna haja ya kuuangalia mkataba upya na kufanya marekebisho. Do you mean even the CAG is being simplistic? Gosh!
 
Kazi nzuri kwa CAG, chuo kilichosifiwa ndio kwanza kinaongoza kwa mikataba ya uongo na kupigwa chenga, eti kuna school of law, kumbe blaa blaa, shame on u udsm.
UDSM ni chuo bora Afrika. Waliofanya Mikataba mibovu siyo Chuo ni personalities. Hata huko kwenye Vyuo vya Kata wezi lazima wapo. Usiwe mpumbavu wala lofa!!
 
Mdhibiti-na-Mkaguzi-Mkuu-wa-Hesabu-za-Serikali-300x190.jpg


RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeanika madudu ya mkataba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwenye mradi wa Mlimani City.

Madudu hayo yanaonyesha namna chuo hicho kinavyopoteza mamilioni ambako amependekeza mkataba huo ufanyiwe marekebisho.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni, ujenzi wa mradi wa Mlimani City ulianza Oktoba Mosi mwaka 2004, ukikadiriwa kukamilika Septemba Mosi mwaka 2016.

Hata hivyo, CAG ameshauri yafanyike marekebisho katika baadhi ya vifungu vya mkataba huo.

Ripoti hiyo inaonyesha kwamba moja ya sababu ya kukiukwa maeneo ya mkataba wa wabia hao wawili ni uzembe wa menejimenti ya chuo.

Ripoti inasema: “Tulibaini kwamba mradi mdogo wa hoteli ya nyota tatu (ambayo ina vyumba 100 kikiwemo chumba cha mikutano kinachochukua watu 1,000) na uboreshaji wa bustani ya botania, ikiwa ni sehemu ya mradi wa Mlimani City, haujakamilika kwa kipindi cha miaka 10 tangu tarehe ya makubaliano ya kumaliza mradi.

“Mtazamo wangu ni kuwa hakuna ufuatiliaji wa karibu, usimamizi na tathmini ya mkataba huo kwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Kwa sababu hiyo kuna uwezekano wa kushidwa kumalizia kazi iliyobaki kwa sababu ya ongezeko kubwa ya gharama ya kumalizia mradi tangu kipindi kilichopangwa kupita.

“Menejimenti ya Chuo Kikuu inashauriwa kuuangalia upya mkataba iliouingia na Mlimani City Holding, kuharakisha umaliziaji wa miradi,” ilieleza ripoti hiyo ya CAG.

Ripoti hiyo pia inaainisha ukiukwaji wa ulipaji wa ada ambayo mwekezaji anatakiwa kuitoa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa kifungu cha 1.1(j) cha mkataba pamoja na kifungu 10.1 cha hati ya ukodishaji wa uwanja, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinapaswa kipate asilimia 10 ya mapato ya kodi ghafi.

“Kinyume na kufungu tajwa hapo juu, Mlimani Holding Limited (MHL), hufanya hesabu za gawio la kodi ya Chuo Kikuu kwa kuzingatia asilimia 10 ya mapato ya kodi baada ya kutoa gharama za uendeshaji badala ya kujumuisha gharama za uendeshaji.

“Ukiukwaji huu unakifanya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa katika hatari ya kupoteza kiasi kikubwa cha mapato kutoka katika mradi wa Mlimani City,” inasema ripoti hiyo.

CAG anaishauri menejimenti ya chuo hicho ifanye upya hesabu za gawio lake la asilimia 10 kutokana na mkataba na kuomba kulipwa na mpangaji kiasi kilichokuwa kimekosewa.

Pia alishauri kuwasiliana na mpangaji na kufikiria kubadilisha mkataba kuweka vifungu ambavyo vitaruhusu idara ya ukaguzi ya ndani ya chuo kuangalia mapato na gharama za uendeshaji za mradi.

Ripoti hiyo pia imeainisha udhaifu wa ufuatiliaji na usimamizi wa mapato kutoka kwa wapangaji wadogo kwenye mradi huo.

Inasema kifungu cha 11.2(l) cha hati ya makubaliano, mpangaji (MHL) anapaswa kutopangisha mtu yeyote ambaye hajathibitishwa na Mpangishaji (Chuu Kikuu cha Dar es Salaam), ikiwa ni njia ya kudhibiti mapato yake.

Kinyume na makubaliano ya hayo, ukaguzi wa CAG umebaini kwamba MHL amepangisha majengo kwa wapangaji wengine bila kupata kibali cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Kuna upungufu wa utekelezaji wa vipengele vya mkataba kwa upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hivyo kusababisha Chuo kushindwa kujua kwa usahihi mapato ya kodi kutoka kwa wapangaji wote.

“Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam inashauriwa kutekeleza vifungu na vipengele vyote vya hati ya makubalian ya upangaji kikiwamo kifungu 11.2 (l) cha hati ya makubaliano ambacho kinakitaka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwathibitisha wapangaji wadogo wadogo,” anashauri CAG.

Ripoti hiyo pia inaonyesha mapitio ya mkataba wa upangishaji wa ardhi kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mlimani Holding Limited yamegundua kwamba mkataba haumpi mmiliki wa ardhi haki ya kukagua kazi zinazofanywa na mpangaji.

“Katika hali hii, mpangishaji, ambaye ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hawezi kujua endapo mpangaji, Mlimani Holding Limited, anakiuka mkataba katika uendeshaji au kuna baadhi ya wapangaji wa nyumba hawawekwi wazi na mpangaji huyu,” inasema ripoti.

CAG anashauri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwasiliana na Mlimani Holding Limited kupata haki ya kukagua shughuli za miradi kwa manufaa ya pande zote mbili.

Ripoti hiyo inasema pia kwamba mapitio ya mkataba yamegundua mkataba huo hauelezei hali halisi ya ugawanaji mali mkataba utakapoisha (miaka 50 au 85 kutokana na makubaliano ya pande mbili).

“Hakuna makubaliano yoyote yanayoelezea mgawanyo wa mali na miondombinu itakayokuwapo wakati mkataba unaisha.

“Kwa hali hii, kuna uwezekano wa kutokea mvutano wa sheria mwisho wa mkataba. Hali hii ikitokea, Chuo Kikuu kitakosa msaada wa sheria.

“Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, unashauriwa kuingia katika mazungumzo na Mlimani Holding Limited kuweka vifungu vitakavyoonyesha haki ya kila upande wakati wa mkataba utakapoisha,” anaeleza CAG.

Ripoti hiyo pia inasema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( kiliingia katika makubaliano na kampuni ya Ernest and Young kufanya ukaguzi maalumu kujua kiasi cha mapato ambacho kinaidai kampuni ya Mlimani Holding Limited katika kipindi cha Mei Mosi mwaka 2006 mpaka Juni 30 mwaka 2014 na kubaini kutolipwa dola za Marekani 57,607.

“Wakati wa ukaguzi niligundua kuwa kiasi cha Dola za Marekani 309,458 kilitakiwa kipokelewe na Chuo kutoka MHL, lakini usuluhisho wa hesabu ulionyesha MHL ililipa Dola za Marekani 213,850 kupitia uhamisho wa benki kwa njia ya eletroniki na kubakisha Dola za Marekani 57,607.

“Kuna ufuatiliaji duni kwa upande wa menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kukusanya deni hilo. Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inashauriwa kuongeza nguvu katika kufuatilia na kukusanya deni wanalolidai MHL,” inasema ripoti hiyo.
hii nchi kila mtu ana angalia tumbo lake.tusha zoea umaskini wetu.siku zote CAG katika madudu haya unakuwa wapi.
kama JPM unatusikiliza hii taasisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu hiweke kwenye ofisi ya raisi huweze kutatua kwa wakati.
 
What is wrong angefanya ukaguzi huo hata baada ya miaka 10 kupita? Sasa nadhani wewe ni kilaza. Unashindwa hata kusoma kuona ukaguzi huo uliofanyika ume-cover timeframe (fiscal years) gani. Nimekuambia CAG hufanya special audits kutokana na maagizo ya Rais au Bunge. Katika ukaguzi wa mwaka huu CAG amekabidhi ripoti 17, lakini huko nyuma alikuwa akifanya ukaguzi hesabu za Serikali Kuu, hesabu za LGAs na pengine 1 or 2 special audit (miradi ya maendeleo - mara nyingi kutokana na matakwa ya wafadhili). This time around CAG aliagizwa na Rais kukagua miradi ya maendeleo 15, ikiwa ni pamoja na UDSM (Mlimani City Development Project). Sasa utakuwa umeelewa kama ulikuwa na nia ya kuelewa.
Bravo Rais John Pombe Magufuli. This is only what I can say!
 
Back
Top Bottom