Ripoti: Uchumi unakua, umasikini unaongezeka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti: Uchumi unakua, umasikini unaongezeka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Sep 2, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  TANZANIA imetajwa kama nchi yenye uchumi unaokuwa kwa kasi barani Afrika. Katika taarifa yake ya hivi karibuni, “Tanzania na hadithi ya mabadiko Afrika,” Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limesema kuwa katika miongo miwili iliyopita, uchumi wa Tanzania umekuwa wa mafanikio. Mabadiliko ya uchumi huria na ya taasisi za umma yamesaidia kukuza pato la nchi kwa zaidi ya asilimia saba kwa mwaka, tangu mwaka 2000.


  Hata hivyo, taarifa hiyo haiendani kabisa na hali halisi ya maisha ya wananchi. Mafanikio yanayotajwa yameshindwa kuondoa umasikini kwa wananchi huku maendeleo yakielekezwa zaidi kwenye miji mikubwa kama Dar es Salaam.

  Ukuaji huo pia umekuwa chanzo cha kuongezeka kwa pengo kati ya masikini na matajiri, huku wananchi masikini wakiendelea kuwa masikini zaidi na matajiri kuendelea kutajirika. Tanzania pia imeshindwa kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umasikini (Mkukuta) na ikipitwa na nchi nyingine Afrika na Asia.

  Ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Policy Forum hivi karibuni, imetaja vipengele kadhaa ikionyesha kuwa ukuaji wa uchumi haujasaidia kupunguza umasikini.

  “Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), hauonyeshi kupungua kwa umasikini. Kati ya mwaka 2001 na 2007 sehemu ya watu masikini Tanzania ilipungua kidogo tu. Kupungua huko ni kudogo kiasi kwamba huwezi kusema kuwa umasikini umepungua au haukubadilika,” inasema taarifa hiyo.

  Inasema kwa kipindi cha miaka 16 kuanzia mwaka 1991 hadi 2007, umasikini umepungua kwa asilimia tano tu huku mabadiliko makubwa yakionekana Dar es Salaam wakati maeneo ya vijijini ukuaji wa uchumi ukiwa ni mdogo kiasi kwamba huwezi kuelezea kuwa umasikini umepungua.

  Kipengele cha pili kinaonyesha kuwa umasikini umeongezeka kuliko ilivyokuwa mwaka 2001. Inasema wakati kiwango cha watu masikini wanaotumia chini ya Sh500 kwa siku kikipungua, idadi ya watu wanaoishi chini ya umasikini imeongezeka hadi kufikia 1.3 milioni kwa mwaka 2001, hasa kutokana na ongezeko la idadi ya watu nchini.

  Umasikini unapimwaje?

  Ripoti hiyo inasema kwa Tanzania, watu wanahesabika kuwa masikini wakati matumizi yao yanapokuwa chini ya mstari wa umasikini. Matumizi hayo yanahusisha bidhaa zote zinazonunuliwa na zile zinazozalishwa na kutumiwa nyumbani.

  Bidhaa hizo ni kama vile, chakula, vifaa vya nyumbani, nguo, matunzo ya mtu binafsi, starehe, usafi, matumizi ya nyumbani, elimu, michango, mafuta na sabuni. Si matumizi yote yamehusishwa katika umasikini. Kwa mfano, afya, elimu na maji hayajahusishwa.

  “Mwaka 2001 kiwango cha umasikini kilikuwa ni Sh7,253 kwa mtu mmoja kwa siku 28. Kwa kuwa bei za bidhaa zimepanda kwa asilimia 93 tangu mwaka 2001 hadi 2007, kiwango cha umasikini ni Sh13,998, sawa na Sh500 kwa siku.”

  Kipengele cha cha tatu kinaonyesha kuwa, matajiri wanazidi kutajirika na masikini wanazidi kuwa masikini. Ripoti inasema kuwa siyo tu kwamba umasikini haukupungua tangu mwaka 2001, bali pia masikini wameendelea kuwa masikini.

  Kipengele cha nchi kinabainisha kuwa Tanzania haipo katika mwelekeo wa kufikia Malengo ya Milenia na Mkukuta. Iliridhia Malengo ya Milenia ambayo yanaitaka kupunguza umasikini kutoka mwaka 1990 hadi 2015 kwa asilimia 50.

  “Ni wazi kuwa hadi mwaka 2000/1, Tanzania ilikuwa nje ya mwelekeo kwa asilimia 5.9. Kati ya mwaka 2001 hadi 2007 hali ikaendelea kuwa mbaya hadi ilipofikia asilimia 7.6. Malengo ya Mkukuta ambayo ni kufikia Malengo ya Milenia hadi mwaka 2010, hayajafikiwa.”

  Kipengele cha tano kinaonyesha kuwa Tanzania inatembea wakati nchi nyingine zikikimbia. Inaonyesha kuwa utendaji wake ni hafifu kulinganisha na nchi nyingine zinazoendelea ambazo sasa zimejikwamua kiuchumi. Nchi hizo ni pamoja na Ghana na Uganda kwa Afrika. Nyingine ni Vietnam na India kwa Asia.

  “Wakati Tanzania imepunguza umasikini kwa asilimia 2.4 kati ya mwaka 1991 na 2007, imeshuka ukilinganisha na Uganda, Ghana na Vietnam mara 10. India nayo imefanikiwa kupunguza umasikini kwa asilimia saba katika kipindi kifupi.”

  Kipengele cha sita kinaonyesha kuwa nusu ya Watanzania hawapati chakula cha kutosha. Moja ya Malengo ya Milenia ni kuondoa njaa.
  Tangu mwaka 1991, Tanzania imetekeleza kwa sehemu ndogo malengo hayo kwa kupunguza utapiamlo kwa watoto.

  “Hata hivyo, takwimu zinaonyesha kuwa watoto wanne kati ya 10 wenye umri kati ya 0 hadi miezi 59, hawapati chakula cha kutosha.

  Inaonyesha pia kwamba mtoto mmoja kati ya watano huwa na uzito mdogo. Utapiamlo husabaisha matatizo ya ukuaji wa watoto kwa asilimia 56 na matatizo ya akili kwa watoto kwa asilimia 13 nchini.

  Inasema pia kwamba, asilimia 25 ya Watanzania hawapati lishe ya kutosha na wengi wao hufanya kazi nyepesi hasa za ofisini. Ni nusu tu ya idadi ya wananchi ambao hupata lishe ya kutosha kwa ajili ya kufanya kazi zao hasa za kutumia nguvu. Hata hivyo, inakisiwa kuwa kati ya watu wanaofanya kazi ngumu, wapo wasiopata lishe ya kutosha.

  Ripoti hiyo inabainisha madhara yatokanayo na ukosefu wa lishe ya kutosha kuwa ni ukosefu wa madini ya chuma na vitamini A na madini joto. Hali hiyo husababisha kuzorota kwa nguvu kazi ya Taifa.

  Kipengele cha saba kinabainisha kuwa watu wanamiliki rasilimali nyingi lakini haziwathaminishi. Ripoti inasema kuwa tangu mwaka 2001 umilikaji wa mali kama vile televisheni uliongezeka mara tatu wakati manunuzi ya vyandarua yaliongezeka mara mbili.

  Bidhaa nyingine kama vile, radio, baiskeli na simu za mikononi zimeongezeka kwa kasi. Mwaka 2007, robo ya Watanzania walikuwa wakimiliki simu za mkononi.

  Kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa, kuongezeka kwa manunuzi ya bidhaa kama hizo ni dalili ya kuboreka kwa hali za maisha ya watu igawaje, mabadiliko yake hayaridhishi.

  “Kulingana na kutobadilika kwa matumizi, thamani ya rasilimali zinazomilikiwa haijabadilika. Ukiondoa simu za mkononi, thamani ya bidhaa hupungua. Lakini simu hizo zinapoingizwa, thamani ya rasilimali zinazomilikiwa na wananchi huongezeka kwa asilimia tatu tu.”

  Kutokana na takwimu hizo, ripoti hiyo inabainisha kwamba, uboreshaji wa uchumi wa Tanzania umeshindwa kupunguza umasikini kwa watu wengi.

  “Watu wengi wanamiliki rasilimali, lakini inaonyesha kuwa Watanzania wengi wamekosa uwezo wa kujikimu kimaisha.
  Kwa hali hii ni vigumu kusema kuwa mabadiliko ya uchumi Tanzania yameleta mafanikio. Changamoto hizo zinapaswa kuwa agenda za kisera na kisiasa,” inasema ripoti hiyo.


  Chanzo. Ripoti: Uchumi unakua, umasikini unaongezeka
   
 2. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Mimi nafikiri kichwa cha taarifa hiyo ingekuwa "Uchumi unakua, wizi umeshamiri serikalini, umasikini unaongezeka"
   
 3. bosskilala

  bosskilala New Member

  #3
  Sep 26, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inanishangaza sana kuona jinsi Tanzania ilivyotawaliwa na Umaskini wakati tunamadini karibia aiza zota.

  Tani moja (1) ya MADINI YA ALMAS yanaweza kujenga Mkoa wa Shinyanga ukawa kama Cape town ya South Africa
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mkuu,

  Piga hodi kwanza kwenye jukwaa la Utambulisho.

  Lakini kimsingi una hoja kubwa!

  Napenda nikufahamishe kuwa rais wa chama tawala alikaririrwa akisema kwamba yeye mwenyewe hajui UMASIKINI WA WATANZANIA UNATOKANA NA NINI!...Kwahiyo ni ngumu sana kwake kufanya kitu, maana kwa kujua tatizo unaweza kulikwepa!

  Kwahiyo tutafute rais anayejua sababu ya umasikini wa nchi yetu, na mwenye uchungu juu ya hilo...
  Piga kura sahihi 31 Oct, na kwa kukupasha tu ni kwamba sisi watu makini tumeona kuwa Dr.sLAA ANAFAA KWA KAZI HIYO...
  STUKA..JIUNGE NASI!
   
 5. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa nikijiuliza

  Hivi Watanzania (hasa wa vijijini) wanaelewa maana ya cheo cha Rais?

  Hivi kweli ni nchi gani ambako mgombea wa Urais atasimama akaahidi elimu na matibabu bure na watu wakabeza?

  Hii nchi ina laana.

  Bora ningezaliwa mbwa ulaya kuliko kuzaliwa binadamu Tanzania.

  Nchi hii ina laana.

  Mafisadi (Lowasa, Rostam, Mramba, Kikwete, Chenge) wanakusanya umati wa watu kuwasikiliza na wanapigiwa makofi!!???

  Kwa nini?? Kwa nini Watanzania WAMELAANIWA???
   
 6. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Labda tujiulize ni raisi muongo kiasi gani atasimama katika dunia ya leo ya ubepari na mass consumption akadanganya kwamba atatoa elimu na matibabu bure? Nadhani umma ume-elimika kuliko rais anavyofikiri.

  Mwalimu alijaribu kutoa elimu na matibabu bure. Matokeo yake tukawa tunagawana penseli moja wanafunzi 3, tukawa tunakufa kwa kichocho kwa kukosa kuwalipa ma-bwana afya na kununua madawa, vifo vya wakati vya uzazi vikamaliza wajawazito na vichanga. Umri wa mtanzania kuishi ukawa miaka 48. Leo hii Dr Slaa anakuja kutonesha vidonda vya siasa ya ujamaa, anazani wananchi ni wapumbavu.
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ni ujinga na kulala usingizi kwa Watanzania, khalasss!!!
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280

  Hebu niambie............

  Enzi zenu za kugawana penseli kulikuwa vinu vingapi vya kuzalishia dhahabu? Tanzanite?

  Nchi ilikuwa na wasomi (Wahandisi, madokta, maprofesa) wangapi?

  Unaongea kama unakunya??
   
 9. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Acha hizo, haya maswali mepesi mepesi hayana tija. Machimbo ya mwadui yalianza lini? Ziwa victoria linalo ilisha samaki ulaya mzima kwani limeota leo? Ardhi yenye rutuba, mito, na madini yetu kwani vimekuja baada ya Nyerere? Jiulize ni ma-profesa wangapi waliikimbia Tz miaka ya 80, tena wengi wao wakaenda Botswana, Lesotho, na UK. Wewe unajuwa wasomi waliopo nje walioondoka wakati kwa ujamaa? Narudia, maswali yako ni ya kiwango cha darasa la mgombea mwenza!!

  Nirudie kusema kwamba Chadema inatudanganya kwamba itatoa elimu na afya bure!! Hata makanisa na misikiti kamwe hisingekuwapo paispo michango ya waumini. Chadema watuambie nchi italipiaje madawa ambayo hayazalishwi Tz, itaingizaje vifaa vya hospitali ambavyo havizalishwi nchini. Chadema watuambie kwanini nchi zilizoendelea mara dufu ya Tz hazifikirii kutoa elimu na afya bure? Au hazina mawazo ya Dr Slaa?
   
 10. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Mgonjwa wa Ukimwi;

  Hapo kwenye bold kidogo unaweza nifafanulia zaidi tofauti ya ubora wa huduma za Jamii kwa Wa TZ wakati wa Nyerere na wakati huu wa serikali hii ya JK ?

  Jibu langu tafadhali!
   
 11. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Malafyale, kwanza heshima zako. Pili, nashukuru kwamba wewe badala ya kuleta matusi wewe unataka tuongelee hoja. Kwa hili bro natoa salute. Tuje kwenye hoja sasa.

  Miongoni mwa failure za ujamaa wa Nyerere ni production inefficiencies ambazo zilisababishwa na jitihada zake za kuhakikisha equal distribution of goods and services. Wananchi wakawa wapata elimu, afya, na huduma nyingine za jamii bila kulipia, matokeo yake kadri idadi ya watu ilivyokuwa inaongezeka uwezo wa kuzalisha huduma ukadumaa. Kibaya zaidi, mchango wa wananchi katika kuhakikisha huduma zinapatikana in a sustainable manner na uwezo wa nchi kupanua tax base ili kuongeza uzalishaji ukapungua. Viwanda vikakosa vipuri, maligafi, na wasomi/waendeshaji viwanda walipoona wanalipwa mishahara ambayo ilikuwa fixed bila ku reflect productivity yao wakatimua mbio na waliobaki wakawa wanaiba kwa faida zao. Black market (ulanguzi) ikashamiri, wajanja wachache, wahindi in particular wakawa wanakula na vyombo vya dola na matokeo yake ufisadi ukatunga mimba. Hili lilipotokea kukawa na rationing ya huduma muhimu. Penseli moja wanagawana wanafuzi 3, sio kwa sababu wazazi hawakuwa na man power ambayo wangeitumia kupata ela bali uwezo wa nchi kuzalisha au kuingiza penseli kutoka China ulipungua due to production inefficiecies.

  Wakati huu penseli kugawana sio issue, na wala hili sitapoteza muda kuliongelea. Uwezo wa nchi kuingiza au kuzalisha penseli umeongezeka, na uwezo wa wananchi kujihusisha kwenye shughuli za kujipatia kipato nao umeongezeka. Tatizo lililopo ni unequal distribution katika huduma na katika investment, hii ndio challenge ya serikali yeyote itakayokuja, iwe ya Slaa au ya JK. Hili ni tatizo ambalo we can afford, but we can't afford production inefficiency ambayo italetwa endapo tutarudi kwenye ujamaa.
   
 12. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Salute YOU Mgonjwa wa Ukimwi:

  Lkn mkuu,Je kama tukiziba loopholes nyingi za uwizi wa mali asili zetu,tukibadili kutoka hivi vipaumbele vilivyoweka tuviweke vipya vitakavyo mnufaisha MTZ wa kawaida,tukidhibiti uadilifu wa hovyo wa baadhi viongozi wa serikali yetu na kurekebisha tax base yetu kwa nini ndoto ya Dr Slaa ya matibabu bure isiweze timia?

  Mosi;Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali Mzee Uttoh aliwahi kunukuriwa akisema kuwa asilimia 30 ya pesa zinazotengwa kwenye miradi ya maendeleo zinaibwa na wajanja wachache chini ya serikali ya JK;Asilimia 30 yote ya mwaka ni pesa nyingi sana na kama kungekuwa na mipango imara na pesa hiyo ingeokolewa tungekuwa wapi kwenye huduma za jamii wa wa TZ?Hapo sijaziweka hela zilizochotwa Meremeta,EPA,na kwingineko!

  Pili,kwenye vipaumbele vyetu;sioni mantiki ya kazi gani wanaifanya Wakuu wa Wilaya na benefits zao nyingi kuanzia mishahara minono hadi nyumba za bure na samani zake ndani,wakuu wa mikoa wana kazi zipi na mamia ya wabunge wa viti maalum wanamuwakilisha nani(hapo nampinga Dr Slaa kutolizungumzia hili la hawa wabunge maalum)?Ni pesa ngapi zingeokolewa na kuingizwa kwenye mambo ya maendeleo tukifuta vyeo hivi?Kwa nini tulinunua ndege ya Rais ya kifahari na rada ya bei ya juu ambapo wajanja wachache "wakatupiga" na kuita milion 1 ni tu senti ;kwa nini tunatenga bilion 30 kwa ajili ya maafisa wa serikali kunywa chai na sambusa wakiwa maofisini?Kwa nini kila mwaka Ikulu inatengewa mabilion ya pesa kutengenezwa?Tukirekebisha hii ya vipaumbele nahisi tunaweza piga hatua kwenye elimu na afya!

  Tatu;Serikali ya JK nahisi ni moja kati ya serikali korofi tulizowahi kuipata watz;Baadhi ya watendaji wake wanakosa uadilifu kabisa hasa kwenye suala la misamaha ya kodi.Kuna kesi ipo mahakamani siwezi kuizungumzia maana ipo mahakamani inamuhusu Waziri Mramba.Tax bracket wanayolipa wawekezaji hapa kwetu ni ndogo sana ukilinganisha kwa huduma kama hiyo wanayolipia wawekezaji hao hao kwenye nchi zingine kama vile Botswana;Tukirekebisha hili tutapiga sana hatua!

  Tukidhibiti mambo haya na mengineyo mengi yanayoikoseha TZ mapato hatuwezi kweli kumpa kila mtz maskini aspirini akienda hospitalini?Je hakuna nchi za mfano barani Afrika zinazotoa huduma za afya na matibabu bure kwa wananchi wake wanaohitaji at most?

  Mgonjwa wa Ukimwi,tuendelee kufundishana tafadhali!

  !
   
 13. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Mkuu Malafyale,
  Kwanza nikubali kwamba maswali yako yote yamekwenda shule. Na wala sitapenda nidanganye kwamba naweza kutoa majibu yatakayo kuwa clear kama "USIKU na MCHANA". Ujumbe wangu katika post hii ni kwamba risk ya kugawa huduma za jamii bure ni kubwa mara dufu ya faida zake na kwamba wanaoitakia mema Tz hawatathubutu kujaribu hili.

  Point zako kwamba tuzuie wizi, msamaha wa kodi, na kujaribu kupanga priorities ni point ambazo hazipingiki. Tukipunguza matumizi mabaya na ufisadi na kuhakikisha kwamba misamaha ya kodi haitolewi ovyo na kwa njia za rushwa tunaweza kuwa ela za kufanya mambo mengine muhimu, including education, health and the like. Hapa tupo pamoja. Sasa tatizo linakuja hapa, kupunguza wizi, matumizi mabaya, na kuthibiti misamaha ya kodi kuna affect DEMAND SIDE to the large extent. Mfano, baba mlevi na mfujaji anapoamua kuacha ulevi na ufujaji anachofanya ni kujiongezea "consumer surplus" kwa mantiki kwamba sasa anaweza kununua mambo bidhaa nyingine muhimu. Lakini kuacha kunywa na ufujaji hakuongezi mshahara UNLESS mahitaji ya ziada anayopata kwa kuacha pombe anayawekeza. Kwa mantiki hii hihi, Tz iki-sevu fedha za ufisadi ikawekeza itajiongezea pato, lakini ikizitumia katika kugawa elimu na afya bure itakuwa na matatizo ya aina mbili; (a) kwanza ugawaji huu hautakuwa sustainable kwa sababu ufisadi hautakuwa sustainable in a long-run (b) hadhi, ubora wa elimu na afya katika jamii vitapungua kutokana na matatizo ambayo wachumi wanaita "the bads of public goods" matokeo yake watu watakuwa wanapeleka watoto wao kwenye shule za kulipia Kenya na Uganda kama ilivyokuwa enzi za Mwalimu.

  Sasa tugeuze shilingi upande wa pili. Tukipunguza ufisadi na kuthibiti kodi tutakuwa na consumer surplus. Tukitoa elimu na afya ya kulipia inayowiana na uwezo wa wananchi tutakuwa tumepiga njiwa kadhaa kwa dongo moja. On one hand elimu na afya vitakuwa sustainable kwani mikopo ya wanafunzi itakuwa inakusanywa na kuwasomesha wengine, na riba ndogo itakayotozwa itasaidia sekta nyingine. On the other ubora wa huduma hizi utaongezeka mana public servants watakuwa motivated, wazazi wataona thamani ya fedha wanazolipia, matatizo ya "the bads of public goods" hayatakuwapo. In addition kila mtu anakuwa part katika shughuli za kiuchumi. Kutoa elimu na afya ya kulipia(au kuchangia) utaona kwamba kuna affect both SUPPLY na DEMAND in medium term. Ukiweka mizani katika pande hizi mbili utaona kwamba faida za elimu na afya ya kuchangia ni nyingi kuliko vinginevyo.

  Hii haina maana kwamba ufisadi usidhibitiwe au kusiwe na priority setting. Tunahitaji consumer surplus at the same time tunahitaji sustainability in production of goods and services.
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Nime kuwa niki soma vitabu kama "Rich Dad, Poor Dad" na "The Richest Man in Babylon" ambavyo ni vitabu vinavyo saidia sana katika uhuru wa kipesa wa mtu. Vina fundisha jinsi mtu anavyo weza kuwekeza pesa zake hata kama ana kipato kidogo mpaka kuwezi kufikia uhuru wa kipesa. Njia hizi hazi hitaji elimu kubwa wala pesa nyingi bali zina hitaji nia.

  Baada ya kusoma hivi vitabu nika gundua kitu. Tanzania tume zunguukwa na umasikini mkuwa. Haswa wakati huu wa uchaguzi watu wana tafuta viogozi au chama wanachoona kita waletea utajiri na mendeleo. Lakini je umasikini wetu una tokana na ufinyi wa elimu wa fedha wa watu wetu? Je wangapi wetu wana utaratibu wa kuji wekea akiba? Je wangapi wetu huwekeza pesa zetu? Wangapi wetu huishi chini ya kipato chetu?

  Nawa shauri watu wasome hivi vitabu na vingine vinavyo fundisha matumizi ya pesa na uwekezaji. Maendeleo hayata letwa na serikali au siasa. yata letwa na kila mmoja wetu kwa kujiendeleza. Ndugu zangu tusi tegemee miujiza. Nilisha wahi kuambiwa na mtu kwamba "Pesa humpeda yule anaye weza kuizalisha." Tuji funze njia rahisi za kuweka akiba na kuwekeza. Japo wote hatuta weza kuwa matajiri wakubwa lakini uhuru wa kipesa sote twaeza fikia.
   
 15. l

  liganga4 Member

  #15
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mgonjwa Ukimwi ni vizuri ukiwa mkweli. wakati wa mwalimu watu walikuwa wanatupa dawa wakipewa hospilini.mpaka ukaanzishwa utaratibu wa kumeza dawa chini ya uangalizi. Tulisafirishwa kutoka makwetu hadi mashuleni na serikali.
   
 16. M

  Malila JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Uwekaji akiba unasaidia sana mtu kuingia ktk uwekezaji kwa mtu anayetaka kuingia ktk mafanikio ya kifedha,hasa kwa sisi ambao tumeajiriwa. Rafiki yangu mmoja aliniambia yeye hutenga pato lake ktk mafungu matatu,hata kama ni dogo kiasi gani hujitahidi kutimiza lengo hilo. Fungu la kwanza ni matumizi, fungu la pili ni akiba ya familia yake na fungu la tatu ni uwekezaji ( ktk nini hakusema). Kwa watu wa dini ni vizuri kuongeza fungu la nne ambalo ni sadaka.

  Kwa hiyo huyu jamaa,hata akipata Tsh 10,000/ anaigawa hivyo ktk uwiano anaoujua yeye.
   
 17. a

  as me Member

  #17
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wengi wetu hatujui nini tunataka kufanya na ni vipi tutafanya kwahiyo tunashindwa kuweka mipango na tukiiweka haitekelezeki coz hatujui tunakoelekea.kinachotuharibu zaidi ni kupenda short cuts hamna anayependa kufuata utaratibu mwisho wa siku tunajikuta tunatumika tu, umasikini wetu utakoma iwapo tu tutaamua kubadili tabia zetu kifedha na mitazamo
   
 18. Erick_Otieno

  Erick_Otieno JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 28, 2010
  Messages: 630
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 180
  Kuweka akiba ni msingi mzuri sana wa kimafanikio katika maisha. Suala hili nafikiri linatanguliwa na malengo/ndoto/nia ya dhati ya mtu katika kupata uhuru wa pesa. Katika swali la msingi la Mwana falsafa kuhusu elimu ya uwekezaji, mimi nina imani kubwa sana kuwa huru kifedha kwa kuwekeza kwenye nyumba (real estate). Changamoto kubwa ninayokutana nayo ni namna ya mtu wa kipato cha chini nitakavyoweza kuanza katika huu uwekezaji. Je naweza kupata msaada kwenye hili?
   
 19. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tatizo Watanzania wengi wna changanya kati ya asset na liability. Watu wengi wana dhani nyumba ni asset bila kujua kwamba nyumba isiyo kuingizia kipato ni liability siyo asset. Ndiyo maana una wakuta watu wana miliki nyumba nyingi isiyo ingiza kipato chochote wakishani ni asset. Kwa hiyo mkuu ni muhimu kuelimishana na kupeana elimu ya jinsi ya kuinvest in real estate na kufanya nyumba asset.
   
 20. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Na short cuts ndiyo linalo tuponza wengi mkuu kwa sababu
  1. Ukiwa una tumia short cuts ni vigumu kupata maendeleo yoyote kwa hiyo mtu una fika umri fulani ndiyo unaanza kutambua sasa kwamba ume poteza muda ukiwaona wale walio kuwa waki wekeza pesa vizuri tokea mwanzo wakiwa na maendeleo.

  2. Mali za short cuts mara nyingi hazi dumu kwani kuwepo kwa hizo mali kuna tegemea na wewe kuendelea kubahatisha.
   
Loading...