Ripoti: Uchumi unakua, umasikini unaongezeka

Wakuu hii topic nadhani ni nyeti. Nakubaliana na kila kitu ambacho hawa wakuu kabla yangu walivyo changia. Kwa kuongezea, ili nchi kutengeneza uchumi wa kujitegemea lazima watu wamiliki ardhi au majengo.

Poor dad, rich dad na hichi kitabu kingine sijakisoma lakini mtungaji Robert Kobayashi anajua namna ya market financial instruments. Nimesoma Kobayashi nyingine inaitwa guide to investmetment which i would remend is to start with poor dad, rich dad, then Guide to Investment, then there is another one which my buddy will let me borrow. sisi wenyewe, basi hatunabudi tuingie biashara hii. Basi wakuu elimu ya uwekezaji hata nyumbani ipo tena wanayo sana. yani wakati nakua nilikua naambiwa maisha ya kesho mpaka unaona kama mwimbo. Mtu anaewekeza ni mtu ambae anatarajia maisha ya kesho. Nasababu ya kuingia uinteprenyua (ujasirimali) ni kutaka kesho tena upate rizki.

Hata elimu ya watu wazima bado ni elimu. Angalau kujua kubalance check book, wajasiri mali wengi hawana bank accounts. I used to be one myself. Max said something funny yesterady about picking up ones self from out of the ground. Men and women can not sell their products oversees simply they do not see the benefit of being inthe system.

Elimu nadhani kama tulivoambiwa ndio msing wa maendeleo, nadhani ni kweli
 
Sasa hivi wakuu nimeanza kusoma kitabu kinaitwa Africa's Greatest Entrepreneurs which also features Tanzania's very own Reginald Abraham Mengi. Hiki kitabu kimeandikwa na mwanamama mjasiriamaliaitwe MOky Makura ambae wengine wenu mtamfahamu kama host wa vipindi kama Carte Blanche na Living it on the Lifestyles's of Africa's wealthy elite au kwa wale mnaopenda tamthilia mtamtambuo toka kwenye kipindi cha Jacob's Cross cha South Africa. Kitabu hiki kinaelezea historia za kibiashara za wajasiriamali 16 wa Afrika. It is a good read. Nadhani vitabu ni good source of knowledge.

Ningependa kujua zaidi kuhusu real estate industry in Tanzania kwa sababu ni eneo ambalo nipo very interested in.
 
Mimi ni newcomer hapa JF, nimekuwa niikifuatilia kwa mda mrefu lakini nimeamua kujisajili ili tuweze kubadilishana mawazo na watanzania wenzangu wanaoitakia nchi yetu mema.

Kwa hali inavyodhihilika mpaka sasa umasikini wetu tunausababisha wenyewe kwa kushindwa kuwaadhibu viongozi wabovu ktk sanduku la kura,pia wengi wetu hatufanyi kazi tunishia vijiweni tu.Tatu bunge letu ndo la kulaumiwa maana kama liko pale kwa maslahi ya taifa kwa nini linawalinda viongozi ambao wako msitari wa mbele kuifirisi nchi yetu? Kwa nini hata wabunge wa ccm wasiwe mstari wa mbele kuunda katiba mpya?

Tujiulize maaana inawezekana kabisa kati ya wabunge wote walioko dodoma tuna asilimia 1 tu ambayo ina dhamila njema na nchi yetu wengine wamefuata posho na umaarufu.
 
Umaskini wa kutisha Tanzania
• Ripoti mpya ya UNDP yaanika kila kitu

na Tutindaga Mwakalonge
SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), limetoa ripoti yake ya hali ya maendeleo duniani inayoichambua Tanzania kuwa moja ya nchi zilizo nyuma sana kimaendeleo kwa kuwa na watu wengi wanaokabiliwa na umaskini.

Ripoti hiyo inayopima maendeleo ya nchi husika kwa kutazama maendeleo ya watu wake ilizinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam jana na kuitaja Tanzania kuwa nchi ya 148 kati ya nchi 169.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika kila Watanzania mia moja, 36 wanaishi katika hali mbaya sana ya umaskini, sawa na asilimia 36 ya watu wote, milioni 41.3.

Pia ripoti hiyo ya kimataifa imeonyesha kuwa katika kila Watanzania mia moja, 97 wanaishi kwenye umaskini wa kipato wa chini ya dola 2 za Marekani kwa siku, sawa na chini ya takriban sh 2,000 za Kitanzania kwa siku.

Aidha, ripoti hiyo iliyobeba kauli ya ‘Utajiri halisi wa mataifa', imeonyesha kuwa katika kila Watanzania mia moja, 89 wametajwa kuishi chini ya dola moja ya Marekani kwa siku.

"Kwa takwimu hizo, Watanzania wengi wako katika umaskini wa kutisha kwa sababu ya kuwa na uwezo duni wa kifedha wa kumudu maisha yao ya kila siku", alifafanua mtaalamu mmoja aliyehudhuria uzinduzi huo.

Hata hivyo, pamoja na takwimu hizo, Wizara ya Fedha na Uchumi, kupitia kwa Katibu wake, Ramadhani Khijjah, iliendelea kusifia mwenendo wa ukuaji wa uchumi nchini huku ikidai kuwa sekta za elimu na afya zimekuwa zikichochea ukuaji wa uchumi.
 
Ahsante kwa hii taarifa, vp unaweza kunipatia source ya hii taarifa katika mtandao wa computer, yaani inapatikana katika website address gani?
 
Ahsante kwa hii taarifa, vp unaweza kunipatia source ya hii taarifa katika mtandao wa computer, yaani inapatikana katika website address gani?
Nimeipata tu kwenye gazeti la Tanzania daima online. Ila nime google nikapata website ya UNDP Tanzania hii hapa hjaribu kuona kama wameweka maana mimi sijaipitia kuona yaliyomo kwenye website hiyo UNDP in Tanzania - Home
 
Hakuna la kushangaza hapo. Hizo figure CCM wameshazizoea, wao wanapima maendeleo kwa kuangalia idadi ya magari pale Dar. Hii nchi itakombolewa na wananchi na siwengine.

Kwa kifupi Tanzania ni masikini tangu 1961 na CCM wameshindwa kubadilisha matokeo, labda waje watu wengine. Miaka 15 iliyopita CCM na serikali yake wameongoza Tanzania bila kukerwa na mtu, wamejaribu kulipa Madeni, wakaja na sera ya kuendelea kukopa tena, na sasa 2015-2015 watakuja na sera mpya ambayo sijui ni ipi. Lakini bottom line ni kwamba CCM ndio mchawi wa maendeleo ya Tanzania. Mwaka 1981 takribani miaka ishirini tangu kushinda uhuru kwa tiger countries, ilikuwa wazi nchi hizo zilishaanza kukomesha umasikini.

Miaka 8 iliyopita raisi wa Brazil alichukua nchi ikiwa na million of poor people, leo Brazil ni nchi ambayo inatokomeza umasikini. Msituambie inachukua muda kuondoa umasikini, why Brazil wameweza? Haya ndio maswali ambayo Chadema inabidi iwaulize kina Anna Makinda, jee kwa nini Brazil waweze sisi tushindwe?
 
Kupinga tafiti ni sawa kwao kwani maendeleo kwao wameyaona ,wameweza kujenga nyumba mbilimbili(mahekalu) na mitaji kibao ktk miradi yao,
Wanasahau kua watanzania wenzao huku vijijini tunateseka hatuna maji, zahanati ,shule zimejengwa mbali na mlo wakila siku ukiwa ni shida sana. Hawa ndio wote wanao amini maendeleo yanaletwa na wawekezaji.
 
Hii ndio nashidwa kuelewa mtu ana Nyumba ya milioni 900 na gari la milioni 100 na kwenye account ana zaidi ya mamilioni, sasa mtu kweli anashidwa kusema mimi nitadhamini barabara sehemu flani, shule, hospitali au kitengo cha msaada sehemu flani...Umasikini hauwezi kuisha,Kisha utasikia anafanya biashara hii biashara ni biashara gani jamani?
 
Ni ukweli usiopingika kwamba umaskini wa watanzania ni mtaji wa kuendelea kutawaliwa na CCM. Kampeni za mwaka huu na miaka iliyopita zimeendelea kudhihirisha kwamba CCM haina nia ya dhati ya kuleta maendeleo katika nchi. Watanzania wengi tumekuwa tukinunuliwa na vijisenti ili hali tunaendelea kuangamiza taifa letu na kuwanufaisha watu wachache.

Kwa bahati mbaya zaidi watanzania wenge we are cheap politically na kwa sababu tunapenda fedha zinazopatikana kirahirahisi (easy money) tutaendelea kufanywa wajinga na kutumika kama mtaji kwa maslahi ya CCM na si watanzania wote. Imefika wakati tutambue kwamba pesa rahirahisi haziwezi kututoa kamwe kwenye matatizo na tuchukue maamuzi magumu ili kuzishinda nafsi zetu kwa ajili ya kuleta mabadiliko. Khanga, Kofia na T-shirts zitatatufikisha wapi? Tuwabane viongozi watuueleze misitu , madini, maziwa na bahari vinamanufaa gani kwa taifa letu kama havituondoi katika umaskini.

Shime tujadiliane kwa maslahi ya taifa.
 
na hasa kwa upande wa elimu ya uraia.
niliwahi kuwauliza wazee fulani huko mpwapwa kuhusu uchaguzi mwaka huu na majibu waliotoa ni kuhusu ubaguzi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa chama kuhusu mgawanyo wa sare za kampeni za ccm nikachoka!
 
INAASTAAJABISHA PAMOJA NA WATANZANIA KUWA KTK lindi la UMASKINI tuNATUMIA 18 % ya bajeti ya serikali 2trillion kupiga simu na sms!Jee ni dalili ya kukua uchumi au maendeleo? au kwa kuwa hatuna ajira kilichobaki ni matumizi mabovu ya mawasiliano au ni kutojielewa ni kiasi gani simu zinakula pesa zetu?source tcra
 
Wana JF
Hainingii akili tangu duniani iumbe bado wananchi wengi tanzania wanaishi ktk makazi duri (nyumba za tembe), hawana maji, umeme, vyoo, huduma za afya, na barabara?Je viongozi wetu wanajali? Je sisi tumekosa nani na tunahitaji nini ili tutoke hapa tulipo? mbona hali nzuri ni kwa viongozi tuu? Mimi naona kuna haja ya kuipindua serikali na watendaji wote wakuu serikali kama tunisia na Egypt. JK na CCM ni mzingo kwa taifa...ni maafa. Hawa jamaa ni matapeli. hawana dhamira ya kweli ya kulikomboa taifa hili. JK anajali mafisadi kuliko wananchi wengi waliompa madaraka. Pinda nanye siyo mtu wa action kama Lowassa.Ingawaje Lowassa naye ana matatizo yake lakini muda mfupi akiwa waziri mkuu, aliyoyasema aliyatenda.Jamani mpaka tunafika karne ya 21 wanafunzi wetu hawana madawati wanakaa chini wakati raslimali zote tunazo?!!Lazima kuna tatizo kubwa la uongozi??
 
Umetumwa. Wakati anafisadi fedha za maafa alipokuwa ofisi ya pm alikuwa anajenga au anabomoa?
 
watu wengi wanakufa kwa kukosa madawa, huduma za afya, na ajali. wengi hawana chakula wala maji. maji yanayopatikana haifai kwa afya ya binadamu. Je matatizo etu yote yanahitaji fedha za wafadhili? Je hatuna uwezo kabsa wa sisi kupunguza umaskini? Je hakuna njia mbadala ya kuchangua viongozi kwa mikataba kama Rwanda kama vile MaDC, RC, DEDs, directors, etc badala ya utaratibu wa sasa?Maskini wa tanzania wataendelea kuwangalia viongozi wao mpaka lini wakila na kusaza, na wakiwa kwenye VX? Je watanzania wao hawastahili maisha bora. yale maisha bora kwa kila mtanzania JK alihaidi yameishia wapi?
 
Mkubwa!!.. yaani kwako EL ni mwisho wa reli hadi umemuona kama kiongozi wa kutolea mfano???? Am I missing something here???!!!
 
wenye laana ni viongozi wetu au ni wananchi wake? Mbona sisi kila kitu ni ubabaishaji? sisi ni smart kwa jambo gani? Mbona tunadanganywa kiraisi sana. tuna abudu wageni na kuwatetemekea!. Jamani sisi tutaendelea tuu kulimbilia nchi zilizoendekea mpaka lini? sisi tumeshindwa yote kabsa?...
 
EL anasemekana ana mambo ya ufisadi. Pinda inawezekana kuwa clean lakini maneno mengi matendo kidogo saana. Labda tunahitaji mtu kama kina Lyatonga, Sokoine. Hali ni mbaya sana. Tunahitaji mtu anasema leo na matokeo yanaonekana leo leo au kesho asubuhi. Hatuhitaji tena viongozi wanaotoa ahadi. Jamani sisi tuu kila siku maskini maskini maskini..............mpaka lini....wakati wale matajiri wanapanda chati kila siku!!!.............tunahitaji kongamano la kitaifa kuzungumza matatizo ya hii nchi na utatuzi wa hayo matatizo
 
Wana JF
Hainingii akili tangu duniani iumbe bado wananchi wengi tanzania wanaishi ktk makazi duri (nyumba za tembe), hawana maji, umeme, vyoo, huduma za afya, na barabara?Je viongozi wetu wanajali? Je sisi tumekosa nani na tunahitaji nini ili tutoke hapa tulipo? mbona hali nzuri ni kwa viongozi tuu? Mimi naona kuna haja ya kuipindua serikali na watendaji wote wakuu serikali kama tunisia na Egypt. JK na CCM ni mzingo kwa taifa...ni maafa. Hawa jamaa ni matapeli. hawana dhamira ya kweli ya kulikomboa taifa hili. JK anajali mafisadi kuliko wananchi wengi waliompa madaraka. Pinda nanye siyo mtu wa action kama Lowassa.Ingawaje Lowassa naye ana matatizo yake lakini muda mfupi akiwa waziri mkuu, aliyoyasema aliyatenda.Jamani mpaka tunafika karne ya 21 wanafunzi wetu hawana madawati wanakaa chini wakati raslimali zote tunazo?!!Lazima kuna tatizo kubwa la uongozi??

Kongamano halitasaidia kitu kama mfumo wa kiuchumi na kiutawala duniani utabaki huu huu.We need to overhaul the worlds political and economic system.Makongamano mangapi yamekuwepo na hayajasaidia?
 
Back
Top Bottom