Ripota wa ITV Sam Mahela unaboa unaporipoti

Ripota wa ITV Sam Mahela unaboa unaporipoti

Mahela ndo staili yake katika kuripoti,,,,kila ripota anastaili yake rejea emmanuel buhohela,,spencer lameck joji maratu,,steven chuwa wakati huo....ni hayo tu.
 
Hizi avatar zenu hatari sana, kati ya wewe na MO11 nani mkubwa? Mtakua ndugu tu, mmefanana sana!

294185.jpg
216558.jpg
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] dah Jf burudani.
 
Taarifa ya habari itv naikubali sana kwa sababu wanajitahidi kutupatia taarifa kila kona ya nchi na kwa ufafanuzi mzuri kuliko vituo vingine hapa nchini.

Ila kuna ripota, sam mahela ananiboa sana anaporipoti... Mfano leo alikuwa anaripoti bomoa bomoa ya KIVULE MAGOLE kwa mbwembwe ni kama anafanya dhihaka kwa wahanga.

Sam angalia sehemu za kufanya mbwembwe bana......
Jamaa ana mikogo sana...
 
Waandishi habari bora nchi hii wapo wachache
Tido azam
Samadu startv
 
Mpaka sasa Sam Mahela anashikiria kijiti cha Ripota bora wa matukio , akifuatiwa na Spencer Lameck ..

Kama nimekosea ,wataje unaowaona maripota bora
 
Mimi ñimejikita Azam two

Tatizo hao Azam nao wana ubinafsi, hadi uwe na dishi lao ndo ungalie habari yao ndo maana inawatazamaji wachache tofauti na wenzao ITV ambao wapo ving'amuzi vyote hadi vi anntena vya tube light uwanja wa fisi
 
Umeniwahi saaan ayaan Sam kama toto shamba linaboa saaana though i was his fan lakin sasa hapana kubwazima li dag et????
 
nafikiri huwa analenga wajinga kama wewe. umewahi sikia watangazaji waBBC au CNN wakitangaza kwa sauti ya mzaha?
Bora ya mjinga akipata elimu huelimika kuliko wewe mpumbavu! akili ya mpuuzi ni majungu majungu kama yako,
MAISHA NI KAMA MKANDA KILA MTU ANA SIZE YAKE,
"HEBU TOKA HAPA (in Makonda'z voice)"
 
Yaani hayuko professional kabisa
But he is creative,iyo professionalism haimtofautishi mtu na kumpa uniqueness ambayo mtu mwingine hana, habari zenyewe ndo hizi hizi za hapa hapa mwacheni ajigambe atambe ndio muda wake huu
 
Taarifa ya habari itv naikubali sana kwa sababu wanajitahidi kutupatia taarifa kila kona ya nchi na kwa ufafanuzi mzuri kuliko vituo vingine hapa nchini.

Ila kuna ripota, sam mahela ananiboa sana anaporipoti... Mfano leo alikuwa anaripoti bomoa bomoa ya KIVULE MAGOLE kwa mbwembwe ni kama anafanya dhihaka kwa wahanga.

Sam angalia sehemu za kufanya mbwembwe bana......
Mimi niliona hilo nilijiuliza kwanini amemaliza kuripoti kwa mbwembwe vile na wakati ile ni taarifa ya huzuni sio taarifa ya burudani. Lakini hiyo ina akisi jinsi moyo wa mtu ulivyo, hata kama swala hilo halikumgusa moyoni mwake basi ajitahidi hata ku pretend. Yaani anajitambulisha huku analeta utani wakati watu wa kila aina hadi waliopatwa na hayo matatizo nao wanaangalia taarifa ya habari.
 
Geeeeoooorgeeeeeeee maraaaaaatooooooo wa aiiiii tiiiiii viiiiii.... Vipi huyo nae.. Unamuelewa
Hapa ndio shida tupu!
Mikogo imezidi, neno linavutwa make unasahau lilikoazia na neno gani, unabaki kusikiliza mvuto mreefu usioeleweka.
 
Back
Top Bottom