RIP emma.
Kumbe kuna vijana wa Mbeya Day na uzunguni humu...? Mmenikumbusha mbali sana.... enzi za mbwembwe za Mpesya, viboko vya Mwakamele na mama Sombrero..... na akina Mbawala..
Ratiba ya maakuli innakaribia kufikia tamati,
Ratiba inayofuata ni kuuaga mwili wa marehemu, halafu msafara wa kuelekea kanisani utaanza, baada ya ibada ya marehemu msafara utalekea makaburi ya segerea mwisho kwa maziko..
Ajali iliyoptwaa uhai wake ilitokana na kujaribu kumkwepa pedesterian aliyekuwa anakatiza barabara. Marehemu alikuwa anaingia barabara ya Sam Nujoma. Siku ambayo amefariki ndiyo siku ya kuzaliwa kwake. Alikuwa ameitanguliza familia yake kwa Mzee mwaikasu kwa sherehe ndogo ya birthday halafu yeye akapitia Mlimani City ATM....
Yule mtu mwingine aliyekuwa anagaagaa kwenye dimbwi la damu alikuwa amegongwa na gari iliyokuw2a inamkwepa marehemu baada ya kugongwa na RAV4... Kwa kweli hatujui hali yake ingawa taarifa za awali zinasema alivunjika miguu yote.
Marehemu baada ya kugongwa aliyumba mara kadhaa kabla ya kuanguka na pikipiki. helemet ilipasuka ikisababisha pia kupasuka kwa fuvu la kichwa chake hali iliyopelekea umauti wake sekunde chache baada ya ajali.
Marehemu nimemfahamu just two months ago kwa sababu alijitolea kuwa mshenga wa ndugu yake anayeoa kwenye familia ya mke wangu... Nilikutana naye kwenye msafara wa kupeleka mahari. Ni mcheshi sana na rafiki asiyebagua.
atakumbukwa the day alipoteremshwa pale round about ya sinza na mkwawa kuelekea kwa mama(vizib0), darajani utawala na kushuka kule down chabruma!! The real man from mbeya akajikuta anakabidhiwa mkulu jimmy by then chairman wa chabu akatupwa pale e6 uso kwa uso na miaka vallery luwi akisaidiwa na mzee francis mulungu na membi kileo na vijana fulani wa dodoma na morogoro, inafurahisha kuzikumbuka zama zile mpaka pale alipojiunga na jopo la wazee wa dojo kilemile na njagamba lawrence huku wakisaidiwa na kijana toka kigoma bitozi mtanashati wa kuuzoa kitwana, hahahaaaaaaaaaa!!! Imma akahamia seuta just to enjoy maisha ya msolopagaz akiwa karibu sana na kilemile na njagamba, he will always be bro,friend, binadamu. Jana nilifarijika sana kuona vijana wa lyandembela na pale sinza wakimuombeleza mtumishi wa mungu imma. Bwana alitoa na bwana ametoa, jina la bwana lihimidiwerip ema........ Nilikuwa naye ifunda
Dont tell me ni huyu aliyekuwa anafanya kazi TBL idara ya Packaging kama supervisor!, kama ndiye namjua, and he happened to be a friend!
Mungu mlaze mahala pema peponi!..