Ridhiwani Kikwete, thibitisha au kanusha

Ridhiwani Kikwete, thibitisha au kanusha

Guns don't kill people - people do.
GunsDontKillPeople.png
 
Tuwe waugwana watanzania, je hatuoni kuwa hayo ni maendeleo? je tulitaka hiyo nyumba ijengwe na wahindi au wamrekani kwa kutumia fedha zetu?

Tunasikia kila siku hakuna malazi dodoma hasa wakati wa bunge vyumba vyote vimejaa. Hatuoni kuwa kwa kufanya hivyo Ridhiwani kapunguza hilo tatizo kwa kiasi fulani? Upo uwezekano mkubwa hata baba yake huenda hajui kijana wake amepata wapi fedha hizo na upo uwezekano ni jitihada zake binafsi na kwa nafasi yake. Si kati kuwa kwa vile ni mtoto wa rais anakuwa na added advantage kiasi fulani. Sitarajii kuwa kuna watu wanafikiri kuwa kwa vile Ridhiwani ni Mtoto wa Rais basi asifanye jitihada zozote za kujitafutia mali au kuwekeza, hiyo itakuwa ni imani potofu kama ipo.

Ingekuma kama mtu akijitokeza na kusema Ridhiwani amemzulumu mtu fulani au amepokea fedha za rushwa mahali fulani hayo yana jadilika. Lakini kujadili kuwa amejenga ghorofa Dodoma mimi naona ni jambo la maendeleo na anahitaji kupongezwa.
 
ngowile, palasilote, asigwa, chilipamwao, mnambowa, ngoshwe, bangoo, kizamani, mmassi, mwanaharakatihuru, paty, kiumbo, ppm, ngano, na wengine weengi mnaochangia mada hii, nina jambo moja la kusema.

Tofauti ya ridhwani na sisi tusionacho ni moja, kwa nafasi yake ana uwezo wa kupata taarifa muhimu na miongozo ya jinsi ya kupata mitaji. Kwanza kwa kuwa mwanasheria na kutokana na uzoefu wake wa kushughulika na wateja, mara nyingi wanajua mbinu wanazotumia wateja wao katika kupata mitaji. Pili ni kwa baba yake kuwa raisi, hahitaji kusaidiwa na baba, kuwa mtoto inatosha. Hata wewe ungekuwa mtoto wa rais, tabia ya wa- tanzania wengi (ambayo tunatakiwa tuiache) ukiwa na nafasi kama hiyo ni kujikomba kwenda mbele. Wewe kama ni mkurugenzi wa beni, na ukaambiwa ridhwani anaomba apointment na wewe, unakurupuka na yeye anakuwa kipaumbele. Na utashare as much info as possible, just with expectation kuwa mtoto atanena jambozuri akiwa anakunywa chai nababa. So anapata access ya mikopo (kwa njia halali bila shaka) na hili ndilo ninaloamini.
Ni wape mfano mmoja wa wahindi wanavyofanya. Ghorofa au uwanja unauzwa, anakwenda kwa mhusika na kunegotiate nae, wakishakubaliana unajua tena manunuzo ya nyumba ni mlolongo, so ukaguzi ardhi, n.k. Wakati huo anakwenda bank kuzungumza nao anawaeleza kuwa anataka kununua gorofa na kufanyia biashara. Anatumia pesa kiasi kuandika mchanganuo mzuri wa biashara. Mradi unapita, na mabenki hayataki kuchelewesha mkopo wakijiridhisha kwa ajili ya ushindani. Basi bank wanamlipa yule mhindi na mwenye nyumba anakwenda bank anadeposit na transfer inafanyika na bank kuchukua hati zote za nyumba kama dhamana (normaly ni kama 80% ya gharama zote, ingawa kuna taratibu nyingi tu wengine hutoa 100% ambayo ina masharti tofauti) na mhindi anabaki na nyumba na anafanya biashara. So bank ikifanya evaluation wakakuta thamani ni kubwa kuliko bei unayonunulia, wao wanakupa hiyo cash, inayobaki ni mtaji! Sanasana atakuwa ametumia pesa kuandaa mradi. Mnaionaje hii?
ridhiwan before 2005 alikuwa mwanAfunzi udsm. Haya mafanikio yanayokuja kama mvua za el nino ni lazima hata mnaOmtetea hamwezi kuzuia fikra za mashaka juu YA kujipatia kwake mitaji kwa njia zisizo halali. HaiwezEKANI katika bingu hii hata kama yeye mwanasheria .anafanya biashara gani ya kuwa na uwezo kama mungu wa tanzania ambaye hajapata tokea . Watetezi uchwara nyie bila shaka MNAPATA mshiko wa kutosha kulinda maslahi yake ila mna akili ya kitoto sana nendeni shule kwanza inaonekana nyie mnafikiri hoja mnazotoa zina mshiko wla hazina mshiko hata kidogo. Hakuna muujiza .rz1 anauza hadi udc huyu ni dalali wa ikulu. IKULU KUNA BIASHARA GANI HATA UPAKIMBILIE. IKULU NI MZIGO,UKITOA PESA ILI KUINGIA IKULU UTAZIRUDISHAJE? HAYA NDIYO MASWALI MUHIMU YA R1 KUJIULIZA UKIONA WATU MABARABARANI UNAONA NI MZIGO WAKO HUO, UKIONA WATU WENYE NJAA NI WAKO. JE RZ1 ANAMSAIDIAJE BABAKE KUBEBA MZIGO. KWA SPEED ALIYO NAYO KUPOPOA MALI ZA NCHI. Ana nguvu kuliko vp, na hata pm. Serkali dhaifu sana hii tunasikitika tanzania inapita ktk wakati ikiwa dhalili namna hii. Watetezi mtakuwepo na mtamkana atakapokujanyongwa
 
Mkuu, zitoe tu hizo nyaraka, unasubiri nini??

Mi nipo Dom, jengo hili lipo kitaa gani?
 
Anamiki kama hizo mbili hapo dodoma, Pia Moro anayo Magorofa, Arusha pia. DAR LIVE PIA YAKE. Pia anamiliki Semi Trellar Kama 100, Anamiliki pia Kampuni ya kuchimba Visima vya Maji! Utajiri huo wote katoa Wapi wakati kamaliza chuo juzi tu, kama Sio Misamaa ya Kodi pia baba yake Jk lazima na yeye ana share Zake hapo.
 
acha wivu ulitaka na wewe uzaliwe na kikwete?

Ugonjwa wa akili mbaya, hasa pale mgonjwa huwa hajitambui kama anaumwa, na wala hapotezi hamu ya kula chakula, hata kama asizaliwe na kikwete, mali zote za kifisadi iko day wataeleza namna walivyopata, hii ni kwa sababu ili tulistore kuwa honesty (the quality, condition, or characteristic of being fair, truthful, and morally upright), sifa ambayo watanzania tumepoteza. hivyo itahitajika mafisadi wote kushughulikiwa na mihimili ya dola la kweli, ili iwe funzo kwa wengine, maana hali ya sasa imehalalisha ufisadi.
 
sawa bwana Ngowile, lkn si hiyo tu, kuna mlango wa nyuma na uharifu watoto wa wakubwa karibu wote wanafanya kupata utajiri. Kuna minong'ono kuwa Ridh kanunua magari ya mizigo 600 ambapo tayari vichwa vimekwisha ingia nchini-kilichobakia ni kutengenezea traillers. Hilo nalo vipi? kwa hali hii unadhani Mwkyembe anapopiga kelele ya kuboresha reli atafanikiwa kwa urahisi? biashara ya mtoto wa boss ife kwa sababu ya manufaa ya watanzania? Thubutu yako. Tazama pia tetesi kuhusu anna mkapa kumiliki convoy ya malori kwenda nje ya nchi, TUTAFIKA? Kwangu mimi haijalishi anawekeza nchini au nje, muhimu ni wizi tu. Hakuna wizi bora.
:flypig:
 
Anamiki kama hizo mbili hapo dodoma, Pia Moro anayo Magorofa, Arusha pia. DAR LIVE PIA YAKE. Pia anamiliki Semi Trellar Kama 100, Anamiliki pia Kampuni ya kuchimba Visima vya Maji! Utajiri huo wote katoa Wapi wakati kamaliza chuo juzi tu, kama Sio Misamaa ya Kodi pia baba yake Jk lazima na yeye ana share Zake hapo.

Una ushahidi gani kuwa mali zote hizo ni zake? kama ameandikisha majina ya watu wengine bure yake hiyo imekula kwake, baba mwanaasha mda ukifika wa kuachia mpini wa kisu, basi wale mlioandikishwa mtieni ndani hizo mali, kama huwa mnatoa sadaka msikitini au kanisani endeleeni na mzidishe zaidi, kwani utajiri wa bure mungu amewatelemshia
 
sio hii tu kaka,wana hotel ingine kubwa ipo tanga,ghorofa lingine kibaha na viwanja kibao hapa arusha.tunajua wametugeuza dili but one day we shall reclaim what is ours!
 
Tanzania bila ccm itakua Nchi ya Asali na Maziwa
Kuna jengo moja kubwa kali liko hapa Arusha sijui ni nani anaweza kuliweka hapa watu walione???? CCM NI JANGA LA KITAIFA WIZI KILA KONA HADI WATOTO NI WEZI!!!!

acha wivu ulitaka na wewe uzaliwe na kikwete?

Usikwepe mada na huja2mwa kumwongelea unless wewe ni Ridhiwani, ishu iliyopo ni kuthibitisha au kukanusha na si vinginevyo, acha ukibaraka mkuu
 
Tuwe waugwana watanzania, je hatuoni kuwa hayo ni maendeleo? je tulitaka hiyo nyumba ijengwe na wahindi au wamrekani kwa kutumia fedha zetu?

Tunasikia kila siku hakuna malazi dodoma hasa wakati wa bunge vyumba vyote vimejaa. Hatuoni kuwa kwa kufanya hivyo Ridhiwani kapunguza hilo tatizo kwa kiasi fulani? Upo uwezekano mkubwa hata baba yake huenda hajui kijana wake amepata wapi fedha hizo na upo uwezekano ni jitihada zake binafsi na kwa nafasi yake. Si kati kuwa kwa vile ni mtoto wa rais anakuwa na added advantage kiasi fulani. Sitarajii kuwa kuna watu wanafikiri kuwa kwa vile Ridhiwani ni Mtoto wa Rais basi asifanye jitihada zozote za kujitafutia mali au kuwekeza, hiyo itakuwa ni imani potofu kama ipo.

Ingekuma kama mtu akijitokeza na kusema Ridhiwani amemzulumu mtu fulani au amepokea fedha za rushwa mahali fulani hayo yana jadilika. Lakini kujadili kuwa amejenga ghorofa Dodoma mimi naona ni jambo la maendeleo na anahitaji kupongezwa.
Mku wewe unashabikia ufisadi unataka tuwe na taifa la wezi na mafisadi????? Hatutakubali hata Mungu wetu hatakubali nchi ikaliwe na wezi na mafisadi siku zao zinahesabika wataingia lupngo tuu na wewe pia utawafuata huko!!!!

TSN Supermarkets,KOBIL,malori ya mafuta kwa Davids MOSHA
 
Back
Top Bottom