View attachment 57923Ridhiwani kikwete naomba uthibitishe au ukanushe umiliki wako wa jengo hili ndani ya Dodoma.Nitatoa nyaraka baada ya kusikia kauli.Naomba kuwasilisha.
NGOWILE, palasilote, asigwa, chilipamwao, MNAMBOWA, ngoshwe, Bangoo, Kizamani, MMASSI, Mwanaharakatihuru, paty, kiumbo, PPM, ngano, na wengine weengi mnaochangia mada hii, nina jambo moja la kusema.
Tofauti ya Ridhwani na sisi tusionacho ni moja, kwa nafasi yake ana uwezo wa kupata taarifa muhimu na miongozo ya jinsi ya kupata mitaji. Kwanza kwa kuwa mwanasheria na kutokana na uzoefu wake wa kushughulika na wateja, mara nyingi wanajua mbinu wanazotumia wateja wao katika kupata mitaji. Pili ni kwa baba yake kuwa raisi, hahitaji kusaidiwa na baba, kuwa mtoto inatosha. Hata wewe ungekuwa mtoto wa Rais, tabia ya wa- Tanzania wengi (ambayo tunatakiwa tuiache) ukiwa na nafasi kama hiyo ni kujikomba kwenda mbele. Wewe kama ni Mkurugenzi wa beni, na ukaambiwa Ridhwani anaomba apointment na wewe, unakurupuka na yeye anakuwa kipaumbele. Na utashare as much info as possible, just with expectation kuwa mtoto atanena jambozuri akiwa anakunywa chai nababa. So anapata access ya Mikopo (kwa njia halali bila shaka) na hili ndilo ninaloamini.
Ni wape mfano mmoja wa wahindi wanavyofanya. Ghorofa au uwanja unauzwa, anakwenda kwa mhusika na kunegotiate nae, wakishakubaliana unajua tena manunuzo ya nyumba ni mlolongo, so ukaguzi Ardhi, n.k. wakati huo anakwenda bank kuzungumza nao anawaeleza kuwa anataka kununua gorofa na kufanyia biashara. Anatumia pesa kiasi kuandika mchanganuo mzuri wa biashara. Mradi unapita, na mabenki hayataki kuchelewesha mkopo wakijiridhisha kwa ajili ya ushindani. Basi bank wanamlipa yule mhindi na mwenye nyumba anakwenda bank anadeposit na transfer inafanyika na bank kuchukua hati zote za nyumba kama dhamana (normaly ni kama 80% ya gharama zote, ingawa kuna taratibu nyingi tu wengine hutoa 100% ambayo ina masharti tofauti) na Mhindi anabaki na nyumba na anafanya biashara. So Bank ikifanya evaluation wakakuta thamani ni kubwa kuliko bei unayonunulia, wao wanakupa hiyo cash, inayobaki ni mtaji! Sanasana atakuwa ametumia pesa kuandaa mradi. Mnaionaje hii?