Fanyeni juhudi mkatafute mbinu za kupata Mikopo n mitaji, madeni ya hawa watu ni makubwa ni nyinyi tu hamjui. Tembelea benki uliza taratibu, tembelea taasisi mbalimbali kama vile kituo cha uwekezaji nk. Kinachowashidna wengi ni ile pesa ya kuandaa logistics za mikopo mfano kuandaa mortgage, mikataba, na taratibu mbalimbali kuna ada fulani fulani huwa wengi unakuta hizo hela zinakuwa hazipo karibu. Mfano mkopo wa Milioni 100 wa kujenga unaweza kuhitaji logistic money kiasi kisichopungua milioni 5 mpaka kumi.
Ila pia usisahau kwa jina lake bila hata msaada wa Baba, anaweza kupewa michongo na madili na wafanya biashara wakubwa ili kulinda biashara zao. Kivipi? Afisa wa serikali akijua kuna mkono wa mtoto, hathubutu kukurupuka kuingilia au kuchunguza biashara hiyo kivile, na hii ni tabia tu wala si sheria. Na baba anaweza kuwa anajua. Hapo si lazima kuwe na ufisadi, lakini utamaduni wa serikali na maofisa wake ni cha mkubwa ni cha mkubwa. So baba anaweza kuwa anapewa taarifa aidha na mwanawe au watu wa usalama maana ni muhimu, lakini si kweli kuwa kila mali anayoweza kumiliki sasa sio halali.